Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1513 | 1514 | (Page 1515) | 1516 | 1517 | .... | 3272 | newer

  0 0


  0 0

  Mkutano Mkuu wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) Mkoa wa kisoka wa Kinondoni utafanyika Februari 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam katika ukumbi utakaotangazwa baadaye.

  Mbali ya ajenda za Kawaida za kikatiba, Mkutano huo utaoongozwa na Mwenyekiti wake Eliutery Mholery utapanga tarehe ya uchaguzi ya Kamati mpya ya Utendaji baada ya iliyopo kumaliza muda wake.
  Pia Mkutano huo utazungumzia uanzishaji wa Chama cha Makocha cha Wilaya mpya ya Ubungo ambayo imemegwa kutoka Wilaya ya Kinondoni.

  Tayari Wilaya ya Ubungo imeshasajili na kufanya uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ubungo (UFA).
  Tunatoa mwito kwa makocha wote wa TAFCA Kinondoni kuhudhuria Mkutano huo muhimu kwa ustawi wao pamoja na mpira wa miguu kwa wilaya za Kinondoni na Ubungo.

  Boniface Wambura MGOYO
  Mjumbe Kamati ya Utendaji TAFCA Kinondoni

  0 0


  0 0

  Na MatukiodaimaBlog
  MKUU wa wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Abdallah ameanza jitihada za kuhamasisha wananchi wa wilaya hiyo kulima zao la Pareto kama zao la biashara. Akizungumza na wananchi wa Udekwa na Lulanzi leo, amesema kuwa Kampeni maalum ya kuhamasisha kilimo cha zao La Pareto zimeanza leo  kwa kupanda Pareto pia kuona vitalu vya miche ya pareto.Alisema kimsingi miche hiyo itatolewa bure kwa kila Mwananchi anayehitaji kulima zao hilo.
  Alisema pamoja na kupanda mazao mengine ya Chakula na biashara wasiache kupanda japo hekari moja ya zao La Pareto.
  Mkuu huyo alisema kuwa  zoezi La uhamasishaji upya wa zao La Pareto litafanyika katikati kata mbali mbali za Wilaya ya Kilolo. Kwani kati ya Wilaya ambazo zilikuwa zikilima zao La Pareto kwa mkoa wa Iringa Wilaya ya Kilolo ni moja ya wilaya ambazo zilikuwa zikilima zao hilo. Kuhusu soko aliwataka wakulima kuondoa hofu kwani soko kwa sasa ni uhakika

  "Nawaagiza mabwana shamba kutoka ofisini na kwenda kwa wananchi kuwapa Elimu juu ya kilimo cha Pareto", akisema na kuongeza kuwa zao La pareto limekubali sana Wilaya ya Kilolo kutokana na hali ya hewa ya ubaridi na kuwa zao hilo halihitaji mbolea. Aidha aliwataka wananchi hao kuanzisha vikundi vya kulima zao hilo japo mtu mmoja mmoja anaruhusiwa kulima. "Mimi mwenyewe nitatafuta eneo la kulima Pareto… ila sisemi muache kulima mahindi kwenye heka zako 10  tenga heka moja ya Pareto"
  Katika hatua nyingine amewataka wakulima kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kupanda mbegu za muda mfupi zaidi. Mtaalamu wa Kiwanda cha Pareto Mafinga Godfrey Mbeyela alisema kwa mbegu za Pareto zimeandaliwa na wanategemea wananchi zaidi ya 40 elfu kulima zao hilo. Alisema kwa wilaya ya Kilolo daraja La chini litanunuliwa kwa Tsh 2000 Kwa wakulima wa Pareto Kilolo.
  Alisema kuwa soko la Pareto liliyumba kutokana na mwekezaji aliyekuwepo ila sasa soko lipo La uhakika na kuwa pesa zitalipwa kijijini moja kwa moja.

  Alisema kuwa kuwa katika Wilaya nyingine kama Ludewa na Njombe  wanagombea kulima zao hilo. Hivyo aliwaomba viongozi   wa dini mbali mbali kutumia Nyumba za ibada kuhamasisha wananchi kulima zao hilo.

  Kwa  upande  wao  wananchi  wa Kilolo  wameeleza  kufurahishwa na utaratibu  huo  wa Kiwanda  kugawa  miche  bure na  kuwa  wapo tayari  kuanza  tena  kulima  zao  hilo ambalo awali  walikuwa  wakilima kwa  wingi  zaidi.
  Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo Mhe. Asia Abdallah  na  timu ya uhamasishaji wa kilimo  cha Pareto  wakitoka  kutazama  vitalu  vya miche ya  Pareto
  Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo  Mhe. Asia  Abdallah  akitazama  vitalu  vya  miche  ya  Pareto  miche ambayo inatolewa  bure kwa  wakulima
  Mtaalam  wa  kiwanda  cha  Pareto Mafinga Godfrey  Mbeyela  
  kulia  akishirikiana na  DC wa  Kilolo  Mhe. Asia Abdallah kupanda Pareto
  Mkuu  wa  wilaya ya Kilolo  mkoani  Iringa  Mhe. Asia Abdallah wa  tatu  kushoto  akishiriki  kupanda  miche  ya  Pareto  kwenye  shamba  la mtaalam  wa  Pareto Kilolo wakati wa  uzinduzi  wa kilimo  cha Pareto leo


  0 0

  Jeshi la Polisi Mkoani Geita limekanusha taarifa ya kukamatwa kwa Waziri mkuu mstaafu ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu Taifa ya chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mhe. Edward Lowassa.
  Kufutia taarifa ya kukamatwa kwa Mhe. Lowassa zilizosambaa mitandaoni, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo (pichani) alisema kwamba walimzuia kwa sababu za kiusalama na kwamba walilenga katika suala la ulinzi wa jamii na usalama wa wao wenyewe na si vinginevyo.
  “Kwa Kiswahili kizuri ni kwamba tulikuwa tumemzuia...Hatukuwa tumemkata. Tulikuwa tumezuia ule msafara wake kwa ujumla. Nyuma ya kumzuia kwake lilikuwa ni suala la usalama na ulinzi kwa ujumla na si vinginevyo”, alisema Mwabulambo.

  0 0

  NA VICTOR MASANGU, KIBITI

  UONGOZI wa halmashauri mpya ya Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani imeanza kutekeleza maagizo yaliyotolewa Naibu waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo ya kuhakikisha wanaboresha sekta ya afya hususan katika maeneo ya Delta kwa kununua vifaa tiba, madawa, pamoja na vitanda maalumu kwa ajili ya kujifungulia wakinamama wajawazito.

  Akizungumza na waandishi wa habari  katika mahojiano maalumu kuhusina na utekelezaji wa maagizo hayo ya naibu Waziri Mkurugenzi mtendaji wa  halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Alvera Ndabagoyo alisema kuwa kwa sasa tayari wameshaanza kununua vifaa mbali mbali katika zahanati  ili kuweza kuboresha huduma kwa wagonjwa wanaokwenda kupatiwa matibabu.

  Alvera alisema kwamba hapo awali katika sekta ya afya hasa kwa upande wa wananchi waliokuwa wanaishi  maeneo ya visiwani (Delta) walikuwa wanakabiliwa na changamoto  ya upatikanaji wa huduma ya afya kwa kipindi kirefu kutoka na sehemu zenyewe ufikaji wake kuwa ni  mgumu kutokana na kutumia usafiri wa majini.

  “ Ni kweli hivi karibuni Naibu Waziri ofisi ya Rais Seleman Jafo alifanya katika Wilaya yetu mpya ya Kibiti, na kuweza kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo na kujionea changamoto zinazowakabii wananchi,hivyo alituagiza sisi kama watendaji tujipange na kuweza kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu changamoto hizo,hasa katika sekta ya afya na kimsingi tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kununua mambo muhimu ambayo yanahitajika kwa wananchi wetu,”alisema Mkurugenzi huyo.

  Alibainisha kuwa licha ya Wilaya hiyo ya Kibiti kuwa ni mpya lakini uongozi wa halmashauri hiyo wameshaanza kuweka mikakati kabambe kwa ajili ya kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi wao katika maeneo mbali mbai ikiwemo  sekta ya afya, elimu, miundombinu pamoja na maji  ili kuweza kuwasogezea huduma kwa ukaribu.

  Pia Mkurugenzi huyo alisema moja ya jitihada ambazo wamekwisha zifanya ni pamoja na kupeleka nishati ya umeme wa Solar power katika zahanati ya Salale,kupeleka kitanda maalumu kwa ajii ya kujifungulia kinamama wajawazito katika zahanati ya Mchinga ikiwa sambamba na kupeleka Solar Power nyingine katika zahanati ya Mfisini.

  Kadhalika alisema nia na madhumuni yao makubwa ni kuhakikisha wanatekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Naibu waziri hasa kwa kuwaangalia zaidi wananchi wa maeneo ya vijijini na wale wanaoshi sehemu za Delta katika kuwafikishia huduma mabli mbali wanazostahili.


  HIVI karibuni Naibu Waziri ofisi ya Rais Seleman Jafo alifanya ziara yake ya kikazi katika Wilaya mpya ya Kibiti na ambapo aliweza kubaini kuwepo kwa changamoto mbali mbali katika sekta ya afya, elimu, maji, miundombinu, usafiri, hivyo aliagiza uongozi wa halmashauri hiyo kuweza kuzitatua haraka iwezekanavyo  ili kuweza kuwapa fursa wananchi waweze kufanya shughuli za maendeleo bila ya kuwa na vikwazo.

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo kushoto akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Kibiti Ally Ungando wakati alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwa sambamba na kubaini changamoto mbali mbali zinazowakabili.
  Naibu Waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo kulia akizungumza na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Alvera Ndabagoyo wakati alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kukagua shughuli za kimaendeleo pamoja na kubaini changamoto zinazowakabili wananchi(PICHA NA VICTOR MASANGU)

  0 0

   Pichani kati ni kile kilichokuwa kiota maarufu cha maraha katikati ya jiji la Dar,kilichojulikana kwa jina la  Billicanas Club,tayari kwa asilimia kubwa kimeishabomolewa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),kama uonavyo pichani,baada ya kunaswa na Camera ya Globu ya Jamii.
  Shirika  la Nyumba la Taifa (NHC) linaendelea kwa kasi kubomoa jengo la iliyokuwa Klabu Bilicanas.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akiongoza kikao cha wadau wa kutafuta suluhu ya mgogoro wa matumizi ya ardhi katika Pori Tengefu la Loliondo uliofanyika Kijiji cha Wasso ukiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyotoa katika ziara yake hivi karibuni mkoani humo.
  Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro ambaye ni Naibu Waziri wa Kilimo,Ufugaji na maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha akizungumza katika mkutano huo ,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa,Lekule Michael Laizer.
  Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akipokea nyalaka kutoka kwa Mkazi wa Kijiji cha Wasso, Tina Timan zilizowahi kutumika kutafuta suluhu ya mgogoro huo ambao eneo la Kilometa za mraba 1, 500 lilitengwa kwaajili ya kuruhusu shughuli za uhifadhi ya wanyapori jambo linalopingwa na wenyeji.
  Afisa Ardhi wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro,Kasema Samawa akifafanua namna wilaya hiyo ilivyopanga matumizi bora ya ardhi.
  Diwani wa Viti Maalumu katika halmashari ya wilaya ya Ngorongoro,Kijoolu Kakeya akizungumza kwenye kikao kilichowakusanya wadau wote kujadili namna ya kupata suluhu ya mgogoro wa Pori Tengefu la Loliondo mkoa wa Arusha.  0 0


  Wanawake wanaoshiriki katika mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) unaoendeshwa na Kampuni ya AFREXA International Ltd, wametakiwa kufahamu haki mbalimbali za binadamu zinamwongoza mwanadamu kushiriki vyema katika shughuli za kimaendeleo.

  Akizungumza Jijini DSM, wakati wa semina ya siku moja ya wanawake kuelekea katika mafunzo ya kuendesha vyombo vya moto vya biashara, mwanasheria kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) WIGAYI KISSANDU amesema ni muhimu kwa wanawake kufahamu haki hizo kwa kuwa zinatoa mwongozo kufikia malengo.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) MARTIN GABONE amesema semina hiyo ni moja ya hatua za mwanzo za mafunzo ya udereva kwa wanawake kwa ajili ya kuendesha vyombo vya moto vya biashara na kusisitiza wanawa wajibu wa kuhakikisha wanawake hao wanaingia rasmi katika sekta ya usafirishaji kwa kuajiriwa au kujiajiri.

  Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) hadi sasa umesajili zaidi ya wanawake 200 kutoka maeneo mbalimbali nchini, ili waweze kuwapatia bure mafunzo ya udereva wa vyombo vya moto vya biashara ambapo baada ya mafunzo hayo watatafutiwa ajira na wengine watawezeshwa ili waweze kujiajiri.

  Martin Gabone-Mkurugenzi Mkuu Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) akifungua semina ya mafunzo ya haki za wanawake wanaoshiriki katika mradi huo iliyofanyika mwishoni mkwa wiki Kinondoni jijini Dar es salaam.
  WIGAYI KISSANDU-Mwanasheria Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) akitoa mafunzo katika semina hiyo.
  Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo.

  0 0

  Unafahamu kwamba ni rahisi kufikia malengo yako ya kujiwekea akiba ukiwa na “NMB Bonus Account au Business Savings Account” ambayo inakupa faida hadi 13%*? 

  Mfano, ukiwa na lengo la kujiwekea akiba ya shilingi 500,000 kwa mwaka 2017 inabidi uweke kiasi cha shilingi 42,000 tu kwa mwezi na ukiwa na nidhamu ya kuhakikisha kwamba kiwango hakipungui kiasi ulichojiwekea basi utakuwa umechagua njia sahihi kuelekea kutimiza ndoto zako. 

  Jambo la msingi ni kuhakikisha unakuwa na akaunti ambayo haiingiliani na matumizi yako ya kila siku, hii ni hatua muhimu katika kutimiza malengo binafsi uliyojiwekea ama ya kibiashara.
  NMB inatambua umuhimu wa kujijengea nidhamu ya kuweka akiba na kuwaletea wateja wake bidhaa zitakazowasaidia kuweka akiba na pia kuhakikisha wanakuza na kupata maendeleo binafsi na ya kibiashara. ‘Bonus Account’ na ‘Business Savings Account’ ni akaunti maalum kwa ajili ya wateja wanaotaka kutimiza malengo yao binafsi au ya kibiashara. 

  Labda ungependa kuweka akiba kwa ajili ya kulipia ada ya mwanao mwakani, kununua nyumba miaka minne ijayo au kuanzisha biashara miaka siku za usoni, ukiwa na akaunti hizi utakuwa umepata njia sahihi ya kufikia malengo yako. 

   Wasiliana na NMB leo kupitia namba 0800 002 002 utimize matarajio yako kupitia NMB Bonus Account na NMB Business Savings Account.

  0 0
  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani, (aliyesimama), akizungumza na Wakazi wa Rufiji wakati wa ziara ya kukagua Mradi wa Umeme Vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijiji (REA) katika wilaya hiyo.

  Na Zuena Msuya, Pwani

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amesema Wilaya za Mkuranga, Rufiji pamoja na Kibiti mkoani Pwani zitaunganishwa katika Gridi ya Taifa wakati wa kuanza kwa Awamu ya Tatu ya utekelezaji wa Mradi Umeme Vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO).

  Dkt. Kalemani alisema hayo wakati wa ziara yake ya siku moja ya kukagua maendeleo na utekelezaji Mradi wa Umeme Vijiji katika  Wilaya hizo pamoja na kuzungumza na wananchi.

  Alifafanua kuwa ni lazima Wilaya hizo zikaungwanishwa katika Gridi ya Taifa ili waweze kupata umeme mwingi, wa kutosha na wa uhakika ili kuongeza kasi na ufanisi katika shughuli za wananchi za kujipatia maendeleo.
  Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega,( kulia)akimueleza jambo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani( kushoto) wakati wa ziara ya kukagua miradi ya umeme vijijini wilayani Mkuranga katika kijiji cha Njopeka.

  dkt. kalemani aliweka wazi kuwa wakati wa kutekeleza awamu ya tatu ya mradi wa rea, tanesco itajenga kituo kikubwa cha kupokea na kupoza  umeme katika Wilaya ya Mkuranga ili kusambaza katika Wilaya hizo. 

  " Umeme unaopatikana hapa Mkuranga , Kibiti na Rufiji kwa sasa hautoshelezi mahitaji ya watumiaji,ni mdogo sana na unakatika mara kwa mara,kwa kuwa shughuli za kiuchumi zimeongezeka, sasa suluhu ya tatizo hili ni kuunganisha Wilaya hizi katika Gridi ya Taifa mara tu baada ya REA, Awamu ya Tatu kuanza", alisema Dkt. Kalemani. 

  Aidha alitumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi kuwa huduma ya umeme kwa sasa ni jambo la lazima kwa kila mtanzania ili kurahisisha maendeleo, hivyo ni vyema kila mmoja ajiunganishe na huduma hiyo kupitia  Mradi wa REA ambao huduma hiyo hupatikana kwa bei nafuu na Serikali imeugharamia kwa asilimia mia moja kwa ajili wananchi wa vijijini.
  Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Mohamed Mchengerwa, akizungumza na wakazi wa rufiji (hawapo pichani)wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani ya kukagua miradi ya umeme vijijini wilayani Rufiji.

  Katika hatua nyingine, aliwagiza wakandarasi wote wanaotekeleza Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili, katika Mkoa wa Pwani,kuwasha umeme katika vijiji vyote ambavyo vimepitiwa na kuunganishwa na mradi wa huo ifikapo mwishoni mwa mwezi huu wa Januari kabla ya kuaza kwa Awamu ya Tatu ya Mradi huo.


  0 0

  Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (kulia) akielekea katika Gati namba moja la Bandari ya Tanga kuangalia shughuli mbalimbali zinazoendelea bandarini hapo. Penmbeni yake ni Mhandisi wa Bandari hiyo Bw. Saleh Sapi.

  Na Adili Mhina, Tanga.
  Mamlaka ya Bandari nchini imeshauriwa kuangalia taratibu za kurasimisha bandari bubu ili kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali pamoja na kuhakikisha bidhaa zinazopitishwa katika maeneo hayo zinakubalika kisheria. 

  Ushauri huo umetolewa hivi karibuni na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati  timu ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango ilipofanya ziara katika Bandari ya Tanga kwa lengo la kufanya ufuatiliaji na tahmnini ya shughuli zinazotekelezwa bandarini hapo. 

  Mwanri alieleza umuhimu wa kurasimisha bandari bubu baada ya kupata taarifa kuwa katika Mkoa wa Tanga pekee kuna bandari bubu takriban 42 ambazo zinaendesha shughuli mbalimbali bila  ya usimamizi wa Mamlaka ya Bandari. 
  Mhandisi wa Bandari ya Tanga Bw. Saleh Sapi (mwenye t-shirt) akitoa maelezo kwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (koti jekundu) juu ya kina cha maji katika bandari hiyo. Upande wa kulia ni Bw. Jordan Matonya na Bi Anna Kimwela, wachumi kutoka Tume ya Mipango. Upande wa kushoto (mwenye miwani ya jua) ni Afisa Mipango Mwandamizi wa Bandari ya Tanga, Bibi Moshi Mtambalike.

  Mwanri alieleza kuwa kwa sasa Serikali haiwezi kuendelea kufumbia macho suala hilo kwani licha ya Serikali kupoteza mapato yake wapo baadhi ya watu wanaotumia njia hizo nyakati za usiku kuendesha shughuli zinazoenda kinyume na kisheria na taratibu za nchi, hivyo kuchochea uhalifu.

  “Kuna umuhimu mkubwa kuangalia shughuli zinazoendelea katika bandari bubu kwa kuwa wakati mwingine wafanya biashara wanaopaswa kulipa kodi wanatumia maeneo hayo kupitisha bidhaa bila kulipa kodi na wengine wanatumia bandari bubu kuendesha biashara haramu. Ni lazima kuanza kufanya utaratibu wa kurasimisha bandari hizo ili kuharakisha maendeleo ya nchi yetu,” alisema Mwanri.

  Pamoja na hayo, Mwari alitembelea maeneo ya Bandari ya Tanga na kushuhudia shughuli mbalimbali zikiendelea ikiwa ni pamoja na ujenzi wa gati namba 2 ikiwa ni moja ya malengo katika kuimarisha huduma za upakiaji na upakuaji wa mizigo bandarini hapo. 
  Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akikagua ukarabati wa boti katika Bandari ya Tanga.


  0 0

  Mkurugenzi wa Ufundi wa Soka la vijana TFF, Kim Paulsen akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu ya vijana U-17 wakati wa ufunguzi wa kliniki ya Airtel Rising Stars katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam jana.

  Kliniki ya Soka ya Airtel Rising Stars imeanza leo kwenye Uwanja wa Karume kwa kuwakutanisha wavulana 40 na huku ya wasichana ikifanyika kwenye uwanja wa JK Park zamani kidongo chekundu.

  Akizungumza wakati wa kliniki hiyo, Kocha Mkuu wa Timu ya Serengeti Boys, Bakari Shime alisema, ‘kwanza tutakuwa tukiangalia ufundi binafsi wa mchezaji’. Hii ni mara ya kwanza kukutana na wachezaji hawa na kuangalia vitu binfasi ambavyo mchezaji anatakiwa kuwa navyo hii itatusaidia kujua ni sehemu ipi ya kutilia mkazo.

   Juhudi binafsi za Mchezaji, Ufundi na stamina (ukakamavu) ni vitu muhimu kwa mchezaji kuwa navyo katika kiliniki hii, hiyo ndio sababu leo kwa siku ya kwanza wachezaji tumewapa nafasi ya kuchezea mpira ili kuangalia vitu hivyo,’ alisema Shime.
  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa kliniki ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam jana.

  Lakini pia tutapata nafasi ya kuingalia timu yetu ye Serengeti Boys kama ina mapungufu yoyote na kama kutakuwa na wachezaji wenye umri mkubwa basi hauwaruhusiwa  kuendelea kuchezea timu ya vijana.

   Hapa ndipo tutapa fursa ya wachezaji wa kuweza kuziba nafasi zilizoachwa wazi katika timu hiyo,  Kwa wiki hii yote tutakuwa na kazi ya kushirikiana na Makocha wengine  kuikamilisha zoezi hili, aliongeza Shime.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Maendeleo ya Soka la vijana TF,  Ayoub Nyenzi alisema, ‘klikini ya Airtel Rising Stars inatoa fursa pana kwa vijana chipukizi kuonyesha uwezo wao mbele ya makocha wenye uzoefu wa mpira wa miguu nchini’. 
  Katibu Mkuu TFF, Selestine Mwesigwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa kliniki ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam jana.
  Hii ni nafasi adhimu kwa  vijana wetu kuendelea kuonyesha uwezo wao na kuzidi kuendeleza vipaji vyao. Sio lazima wachezaji wote hawa hawawezi kuchanguliwa kuchezea timu ya vijana ya Serengeti Boys, lakini kuna klabu zetu ambazo zinaitahitaji wachezaji kwenye timu zao za vijana. Hii ndio nafasi kwao kujitokeza na kuangalia wachezaji wenye uwezo wa kuchezea timu zao,  Ayoub aliyasema hayo jana.

  Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya alisema, ‘kufanyika kwa kliniki ya Airtel Rising Stars kunahitimisha awamu ya sita ya michuano ya Airtel Rising Stars’  ambayo ilifanyika kwa Mikoa tisa nchini kwa mafanikio makubwa sana. 
  ‘Nachukua fursa hii kuwashukuru TFF pamoja na wadau wote wa mpira wa miguu nchini ambao tumeshirikiana kwenye 2016 Airtel Rising Stars. Michuano hii lifanyika kwa mafanikio makubwa sana na leo tunapaonza kliniki hii inayojumuisha wachezaji bora naomba tuendelea tushirikiana kwa pamoja ili vijana wetu waweze kutimiza ndoto zao za kuwa wachezaji bora katika maisha yao’ alisema Mallya

  0 0

  MKUU wa wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa (pichani) ametoa jukumu kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo,Yohana Sintoo la kuamua hatma ya watumishi wake watano wanaotajwa katika tuhuma za ubadhilifu wa fedha wakati wa zoezi la utengenezaji wa madawati.
   Akiwa ndio mamlaka ya nidhamu kwa watumishi wa halmashauri hiyo,Mkurugenzi Sintoo ndiye mwenye maamuzi ya kuwasimamisha kazi watumishi hao baada ya tume iliyoundwa na mkuu wa wilaya hiyo, Byakanwa kumaliza kazi yake ya uchunguzi dhidi ya watumishi hao na kubaini mapungufu kadhaa.
   Akihitimisha taarifa yake wakati wa kikao na watumishi wa halmashauri hiyo,Byakanwa aliagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya watumishi hao akiwemo aliyekuwa kaimu Mkurugenzi, Mhandisi Kweka.
   “Mamlaka ya nidhamu ya watumishi wa  Halmashauri ni mkurugenzi pamoja na baraza la madiwani. Lakini mwajiri ni ofisi ya katibu tawala mkoa. Ofisi hizi mbili ndizo zinazoweza kukaa na kuchukua hatua za kuzuia matukio au vitendo kama hivyo.”alisema Byakanwa.
   “Niishauri ofisi ya Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro pamoja na ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai  ambayo ndio mamlaka ya nidhamu kwa watumishi hao kupima kuhusu hatua za kuchukua dhidi ya watumishi hawa”aliongeza Byakanwa.
   Mkuu huyo wa wilaya alisema tuhuma zinazowakabili watumishi hao ,majina yao tumeyahifadhi kwa sasa ni pamoja na kupitisha barua ya malipo bila kujiridhisha kama kuna mkataba wa kutengeneza madawati na kufanya malipo ya fremu za madawati badala ya madawati.

   Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Gelasius Byakanwa akionesha sehemu ya nyaraka ambazo zinazoonesha namna baadhi ya watumishi walivyoshiriki kufanya ubadhilifu wa fedha za madawati.

   Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe Gelasius Byakanwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai kuhusu ubadhilifu uliofanyika wakati wa zoezi la utengenezaji wa madawati.Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo  Bw. Yohana Sintoo.

   Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai wakiwa katika kikao hicho.

  Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Bw. Yohana Sintoo akizungungunza wakati wa kikao hicho.


  0 0

  Mwana anga wa Marekani Gene Cernan, aliyekuwa binadamu wa mwisho kutembea kwenye Mwezi, amefariki dunia akiwa na miaka 82.

  Shirika la anga za juu la Marekani Nasa limesema limehuzunishwa sana kumpoteza mwana anga huyo mstaafu. Cernan alikuwa mmoja wa watu watatu pekee waliowahi kwenda Mwezini mara tatu na ndiye binadamu aliyeukanyaga Mwezi mara ya mwisho kabisa, mwaka 1972.

  Maneno yake ya mwisho aliyoyasema kabla ya kuondoka kwenye Mwezi yalikuwa: "Tunaondoka jinsi tulivyokuja na Mungu akitujalia, tutarejea na amani na matumaini kwa binadamu wote."
  Alikuwa kamanda wa chombo cha anga za juu cha Apollo 17 wakati huo.

  Ni watu 12 pekee waliowahi kutembea kwenye Mwezi, na kati yao ni sita pekee ambao bado wako hai.
  Mwana anga wa Marekani Gene Cernan
  Kupitia taarifa iliyotolewa, familia ya Cernan imesema alifariki dunia Jumatatu baada ya kupata matatizo ya kiafya. Hawakutoa maelezo zaidi.

  Kabla ya kufanya safari ya Apollo 17, Cernan alikuwa amesafiri anga za juu mara mbili awali - mwaka 1966 na 1969.
  Alistaafu mwaka 1976 na akaingilia biashara ya kibinafsi. Alikuwa mara kwa mara akichangia katika runinga kuhusu masuala mbalimbali.

  Cernan pia aliandaa makala ya video kuhusu maisha yake.

  Alizaliwa 14 Machi 1934 mjini Chicago, na jina lake kamili ni Eugene Andrew Cernan.
  Ameacha mjane Jan Nanna Cernan, bintiye na binti wawili wa kambo pamoja na wajukuu wanane.
  Kifo chake kilitokea wiki chache baada ya mwana anga mwingine wa Nasa John Glenn kufariki dunia. 

  0 0

  Na: Lukelo Mshaura, Njombe.

  Halmashauri ya Wilaya ya Njombe imesaini mkataba wenye thamani ya zaidi milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa mradi mkubwa wa umwagiliaji katika kijiji cha Itipingi kilichopo Kata ya Ingongolo Wilayani Njombe,

  Mradi huo unafadhiliwa na Shirika la JAICA kutoka nchini Japani ambao utekelezaji wake unaanza januari mwaka huu, utajengwa na mkandalasi Engineering Plus kutoka Dar es Salaama na utatekelezwa kwa kipindi cha miezi nane huku ukisimamiwa kwa pamoja baina ya wataalamu wa umwagiliaji kutoka kanda ya Mbeya na wa Halmashauri ya Njombe. 

  Akizungumza wakati wa utiaji saini wa mkataba huo uliohudhuriwa na meneja uendeshaji wa kampuni ya Engineering Plus, wawakilishi wa kikundi cha umwagiliaji skimu ya Itipingi, wataalamu kutoka ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe , Bi Monica PZ Kwiluhya, amewataka wakandalasi kutekeleza mradi huu kwa wakati na ubora unakubalika.

  “Kawaida mimi huwa siongezi muda wa kutekeleza mradi kwa kuwa pesa tayari ipo hivyo hakuna visingizio, siko tayari kuona mradi unacheleweshwa pasipokuwa na sababu za msingi maana pesa hizi ni za wafadhili na mradi ukicheleweshwa zinatakiwa zirudi” alisema Kwiluhya. 

  Amewataka wakandalasi kushirikiana na wananchi kwa kazi zile ambazo zinaweza kufanywa na wananchi pamoja na kujiepusha na vitendo vitakavyopelekea kukosa ushirikiano kutoka kwa wananchi ambao ndio wamiliki wa mradi..

  Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe Bw. Valentino Hongoli amewataka wakandalasi kufanya kazi kwa mujibu wa makubaliano yaMkataba kwa kuzingatia tarehe ya kuanza utekelezaji na tarehe ya kumaliza.

  “Naomba mfanye kazi kwa kuzingatia thamani ya fedha na kwa viwango vinavyokubalika ili kuweza kutoa mtokeo chanya kwa wananchi” alisema Hongoli.

  Kusainiwa kwa mkataba huu kunatoa matumaini kwa wananchi wa Itipingi ambapo awali walikuwa wakitumia mifereji katika kufanya kilimo cha uzalishaji wa mazao mbalimbali ikiwemo chakula na mboga mboga.

  Mradi ukikamilika unatarajia kuwanufaisha zaidi ya wakazi 1500 ambao watakuwa wakilima mazao ikiwemo, mahindi, nyanya, vitunguu pamoja na mboga mboga. Mradi huu umekuja wakati muafaka ambapo Halmashauri iko katika hatua za mwisho kukamilisha kituo cha kuzuia upotevu wa mazao ya mboga mboga na matunda ili kuyaongeza thamani ambacho kimejengwa kwa ufadhili wa shirika la MIVARAF mjini Njombe.

  Sambamba na hilo mradi huu ukikamilika utasaidia kuinua kipato cha wakulima, kuongeza lishe kwa jamii pamoja na kuiongezea Halmashauri Mapato.


  Lukelo Mshaura
  Afisa Habari 
  Halmashauri ya Wilaya ya Njombe.


  0 0

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

  Serikali imesitisha waraka wa muongozo uliotolewa kuhusu matumizi ya mihuri kwa wenyeviti wa Mitaa na vijiji mpaka pale itakaposhirikiana na kukubaliana namna bora ya kuendesha masuala ya kuhudumia wananchi.

  Akizungumza na baadhi ya wenyeviti wa mtaa, Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene amewataka wenyeviti wa mitaa nchini kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo.

  Mhe.Simbachawene alisema kuwa nia ya kusitisha waraka huo ni kuweka utendaji mzuri baina ya Serikali na watendaji wake wa chini.

  “Utaratibu uliopo uendelee mpaka pale Serikali itakapotoa utaratibu mwingine wa matumizi mbalimbali ya mihuri hiyo baada ya kujadiliwa na kushirikiana vya kutosha” alifafanua Waziri Simbachawene.

  Mhe.Simbachawene alisema kuwa kuna baadhi ya wenyeviti wa mitaa wamekuwa wakitumia vibaya mihuri hiyo na kupelekea migongano na migogoro ya ardhi katika vijiji na mitaa ikiwemo maeneo ya Ununio, Temeke.

  Mbali na hayo alisema kuwa katika Tangazo la Serikali namba 3 lililotolewa 5 Septemba, 1994 limeeleza baadhi ya vitendea kazi vya mwenyekiti wa mtaa ni bendera yenye nembo ya Halmashauri, daftari ya kutunza kumbukumbu na rejista ya makazi.

  Alisema kuwa mamlaka ya mwenyekiti haitokani na mihuri, bali utendaji uliopo ndani ya mtaa au kijiji husika, hivyo mamlaka ya mwenyekiti ipo pale pale na haibemwi na muhuri bali muhuri huonesha nguvu ya ofisi baada ya kuwashirikisha watendaji tofauti ndani ya kijiji katika kutoa maamuzi.

   “Mhuri si mali ya mwenyekiti binafsi, hivyo kwa yeyote atakayekiuka matumizi ya mihuri hiyo Sheria itachukua mkondo wake” alisisitiza Mhe. Simbachawene.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Temeke Bakiri Makele, ameahidi kushirikiana na Serikali kwa kutumia mihuri hiyo kwa kufuata Sheria na taraibu zilizopo.

  Naye Katibu wa Wenyeviti hao, Marium Machicha alimshukuru Waziri mwenye dhamana kwa kauli aliyoitoa baada ya kuliona tatizo hilo na kuahidi kulifanyia kazi.

  Serikali ilitoa Muongozo huo wa namna wa matumizi ya mihuri kwa wenyeviti wa mitaa na vijiji kwa sababu ya matumizi mabaya ya mihuri kwa baadhi ya wenyeviti wa mtaa na vijiji nchini.

  0 0

  Katika kuendeleza juhudi za kupunguza na kutokomeza majanga ya moto yanayoikabili jamii, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeendelea na zoezi la utoaji elimu juu ya Kinga na Tahadhari dhidi ya Majanga ya Moto Nchini.

  Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linajukumu kubwa la kutoa huduma kwa jamii katika Nyanja mbalimbali zikiwemo Kuokoa maisha ya watu na mali zao, Kuzima moto, Kutoa elimu ya kinga na tahadhari ya majanga moto, Kufanya ukaguzi wa tahadhari na kinga ya  moto, Kusoma ramani za majengo na kutoa ushauri, Kutoa huduma ya kwanza katika majanga na ajali barabarani, Kutoa mafunzo ya kukabiliana na majanga ya moto, Kufanya uchunguzi kwenye majanga ya moto na Kutoa huduma za kibinadamu.

  Huduma ya Zimamoto inatolewa bure na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji hivyo basi tunawaasa wananchi kutumia namba ya dharura 114 mara tu wapatwapo na majanga ili kurahisisha uokoaji wa Maisha na Mali kwa haraka.  Kwa kuzingatia majukumu hayo Askari wa kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya wamewapatia elimu ya kukabiliana na majanga ya moto Watumishi wa banki ya Access tawi la Mkoa wa mbeya.
   Sajini Simon Sadala wa kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya (Mbele) akitoa elimu ya Kinga na Tahadhari dhidi ya majanga ya moto katika taasisi ya kifedha(Access Bank) tawi la Mbeya.

   Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa mbeya wakiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa benki ya Access tawi la mbeya mara baada ya kumaliza kupata mafunzo hayo mapema leo asubuhi (Picha na Jeshi la Zimamoto)

  0 0


  Na Raymond Mushumbusi WHUSM.

  Serikali imeahidi kuendelea kushirikiana na vyombo vya habari nchini katika kutoa habari kwa ajili ya kuhabarisha umma kuhusiana na mambo mbalimbali yahusuyo Serikali katika kutekeleza majukumu yake.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipotembelea na kujionea utendaji kazi wa Kampuni ya IPP Media kwenye vituo vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv pamoja na Sahara Media kwa tawi la Dar es Salaam.

  Katika ziara hiyo Mhe. Nape Moses Nnauye amehaidi kuendeleza ushirikiano baina ya Serikali na vyombo vya habari katika utoaji wa habari ambazo ni muhimu kwa wananchi kujua zikiwemo hatua ambalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kutekeleza majukumu yake katika kuwaletea wananchi maendeleo.

  “Niseme kwa kipindi cha nyuma kumekuwa na urasimu wa utoaji wa taarifa muhimu kutoka kwetu kuja kwenu vyombo vya habari lakini niwahakikishe kuwa sasa Serikali imefungua milango kwenu na tuendelee kushirikiana katika kuhabarisha umma wa watanzania” Alisistizia Mhe. Nnauye.

  Kawa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abass amevihakikishia vyombo vya habari nchini ushirikiano mzuri katika kupata habari za Serikali kutoka katika vitengo vyote vya Mawasiliano Serikalini.

  Dkt Abass ameeleza kuwa kwa sasa wako katika mpango wa kuboresha vitengo vya Mawasiliano serikali ili kuboresha upatikanaji wa habari zinazohusu Serikali.

  “Niwahakikishieni ndugu zangu wanahabari kuwa suala la upatikanaji wa habari kutoka Serikali litakuwa si la kusumbuana tena na tunatengeneza mfumo katika vitengo vyote vya Mawasilaino Serikalini ili iwe rahisi kupata taarifa kutoka kwetu” alisisitiza Dkt Abass.
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na uongozi na  baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya IPP Media yenye vituo vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv alipotembelea na kujionea utendaji kazi wa vituo hivyo Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abass(kushoto) akifafanua jambo kwa uongozi na wafanyakazi wa IPP Media upande wa Televisheni wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  alipotembelea Kampuni ya IPP Media kwenye vituo vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza mara baada ya kuwasili katika kampuni ya IPP media kwa ajili ziara yake ya kujionea utendaji kazi wa vituo vilivyo chini ya Kampuni hiyo Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.
    Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiangalia studio ya kutangazia habari katika kituo cha Televisheni cha ITV alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wa vituo vilivyo chini ya IPP Media Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.
    Mkuu wa Sahara Media kwa upande wa Dar es Salaam Bw. Cyprian Musiba akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipotembelea Sahara Media kwa upande wa Dar es Salaam kujionea utendaji wake wa kazi Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.

older | 1 | .... | 1513 | 1514 | (Page 1515) | 1516 | 1517 | .... | 3272 | newer