Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1509 | 1510 | (Page 1511) | 1512 | 1513 | .... | 3284 | newer

  0 0
  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA NISHATI NA MADINI

     TAARIFA YA UFAFANUZI KUHUSU KIKAO CHA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MHE. PROF. SOSPETER MUHONGO (MB.) NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA KILICHOFANYIKA TAREHE 28.09.2016


  Wizara ya Nishati na Madini inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu kikao cha Waziri wa Nishati na Madini na Ujumbe wa Benki ya Dunia kilichofanyika tarehe 28.09.2016 kikihusishwa na kupandishwa kwa bei ya umeme kama ilivyoripotiwa na magazeti ya Mwananchi ya tarehe 12.01.2017 lenye kichwa cha habari “Prof. Muhongo alivyoshiriki kupandisha bei ya umeme” na la tarehe 13.01.2017 lenye kichwa cha habari “Prof. Muhongo awekwa mtu kati”.


  Wizara inapenda kuutaarifu Umma kuwa, imekuwa ikifanya vikao na wadau mbalimbali wakiwemo Taasisi za Umma, Binafsi na Washirika wa Maendeleo yakiwemo Mashirika ya Kifedha ya Kimataifa. Lengo la vikao hivyo ni pamoja na kuhamasisha uwekezaji katika Sekta za Nishati na Madini nchini.


  Aidha, tarehe 28/9/2016 Wizara ilifanya kikao na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia ikiwa ni mwendelezo wa vikao vya majadiliano kuhusu upatikanaji wa mkopo wa Dola za Marekani Milioni 200 kwa ajili ya kuboresha uendeshaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO). Kikao hicho pia kilihudhuriwa na taasisi nyingine zikiwemo Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA).


  Katika kikao hicho masuala yaliyojadiliwa yalikuwa ni;


  1.  Upatikanaji wa umeme wa kutosha, uhakika na  bei nafuu kwa ajili ya kuchochea shughuli za maendeleo ya kukuza uchumi wa nchi ikiwemo viwanda, biashara, kilimo na huduma za jamii;

  2.  Kuongeza ufanisi wa utendaji wa Shirika la Umeme (TANESCO); na

  3.  Kupunguza deni la TANESCO.


  Katika kulipunguza deni la TANESCO ambalo linakaribia Shilingi Bilioni 800 (takriban Dola za Marekani Milioni 363) na kuboresha shughuli za utendaji za TANESCO, Benki ya Dunia ilijadiliana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Madini ili kupata mkopo wa Dola za Marekani Milioni 200. Hivyo, katika kikao hicho, hakukuwa na makubaliano ya kupandisha bei ya Umeme kama ilivyoripotiwa na gazeti hilo.


  Vile vile, tunaomba kuutaarifu Umma kwamba Wizara ya Nishati na Madini kwa niaba ya Serikali inafanya majadiliano na Benki ya Maendeleo ya Africa (AfDB), Umoja wa Ulaya (EU), JICA (Japan), na Mashirika mengine ya fedha kwa lengo la kutafuta fedha za kuboresha Sekta ya Nishati.


  Imetolewa na;

    
  WIZARA YA NISHATI NA MADINI


  13.01.2017


  0 0


  0 0


  0 0

  “BINGWA WA MABADILIKO” au “CHAMPION FOR CHANGE” ni kauli mbio iliyoanzishwa kwenye shindano lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya wanawake (UN-WOMEN) lenye lengo wa kuwapata vijana watakaoweza kushirikiana na serikali za nchi zao kuwainua wanawake kiuchumi.
  Maombi zaidi ya 4000 kutoka kona zote za dunia yalitumwa kwa shirika hilo na ni vijana 170 tu ndio waliobahatika kuchaguliwa wakiwemo vijana watano kutoka Tanzania.
  Vijana hao waliofanikiwa kuchaguliwa kuwa mabalozi wa “CHAMPION FOR CHANGE” ni Agnes Mgongo, Doris Mollel, Hassan Mohamed Toziri, Catherine Ruge pamoja na Sadick Lungendo.
  Mabalozi hawa watashirikiana na serikali kwa kwa hamasa na mafunzo mbalimbali ili  kuwainua na kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi. 
  Hivyo basi wadau wote kwenye njanja tofauti tofauti wanaombwa kuwaunga mkono mabalozi hawa kwa kushiriki kwenye midahalo au mahojiano kwa kupitia kwenye mtandao mkubwa kijamii ulioanzishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya wanawake (UN-WOMEN) unaoitwa “JOIN THE MOVEMENT” kwa kufuatisha kiunganishi (link) hapa chini kujisajili na kuanzisha mijadala yako.

  https://www.empowerwomen.org/en/join-the-movement

  0 0
  0 0

  Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (CAF) limetoa nafasi ya mwisho kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Jamhuri ya Congo (FECOFOOT) kumpeleka mchezaji Langa Lesse Bercy (pichani) jijini Libreville, Gabon kwa ajili ya kipimo kipya cha MRI ili kutambua umri wake.

  CAF limetaka FECOFOOT kumpeleka mchezaji huyo huko Libreville, Gabon ndani ya siku 10 zijazo kuanzia jana Januari 12, 2017.CAF limepata kumwita mchezaji huyo mara mbili mwaka jana, na FECOFOOT imeshindwa kumpeleka kwa sababu mbalimbali wanazozijua FECOFOOT.
  Kwa mujibu wa kanuni za mashindano ya kimataifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, vijana waliohitajika kucheza ni wale wenye umri wa chini ya miaka 17.

  Langa Lesse Bercy, amelalamikiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwamba amezidi umri hivyo kuhitajika kumpeleka kwani hakustahili kucheza hatua ya kufuzu kwa michuano hiyo ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana.
  Fainali za vijana zinatarajiwa kufanyika katika nchi nyingine itakayotangazwa hapo baadaye baada ya Madagascar kuondolewa kuandaa fainali hizo baada ya kubainika kutokamilisha baadhi ya taratibu.
  0 0


  0 0


  Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kilichofanyika kwenye ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi.
  Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati)akiongoza kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kilichofanyika kwenye ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi, kushoto ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na kulia ni Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
  iWaziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akielezea masuala mbali mbali ambayo yamejadiliwa na Mawaziri wa Tanzania Bara pamoja Visiwani
  Baadhi wa Mawaziri kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia kwa makini kikao hicho ambacho changamoto mabli mbali zinazohusu Muungano.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Meneja wa Afya, Usalama na Mazingira  Kazini, Bw. Gilbert Lameck akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa bomba la majitaka na mvua katika barabara ya Azikiwe jijini Dar es Salaam, akieleza kuwa mradi huo unatarajia ifikapo kukamilika Juni mwaka huu.
   Mafundi wakiendelea na ujenzi bomba hilo ambapo sehemu ya maunganio ya Askari Moment jijini Dar es Salaam.
   Muonekano wa ujenzi wabomba la majitaka na mvua katika barabara ya Azikiwe jijini  Dar es Salaam.
  Mafundi wakiendelea na kazi Askari Moment jijini Dar es Salaam. 
  Picha na Emmanuel Massaka,Glob ya Jamii

  0 0

  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Annastanzia Wambura, jana akizungumza kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo, Mhe.Nape Nnauye, kwenye mchezo wa hisani kati ya timu za UMISETA wilaya za Nyamagana na Ilemela mkoani Mwanza, uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.


  Na Binagi Media Group

  Mhe.Wambura, alisema Serikali haijayafuta mashindano ya UMITASHUMITA na UMISETA na kwamba imejipanga vyema ili kuiendeleza michezo hiyo mwaka huu 2017 kwa kuondoa dosari zote zilizojitokeza hapo awali na kusababisha kuahirishwa mwaka jana.

  Lengo la mchezo huo ilikuwa ni kumuenzi aliyekuwa mchezaji wa timu ya soka ya vijana chini ya miaka 20 ya Mbao Fc inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Isamail Khalifan Mrisho ambaye Disemba 04 mwaka jana, alifariki dunia akiwa uwanjani kwenye mchezo baina ya na timu yake na Kagera Sugar huku kiingilio kilichopatikana kwenye mchezo huo kikiwasilishwa kwa familia ya mchezaji huyo.

  Mchezo huo uliandaliwa na taasisi ya soka nchini iliyomlea mchezaji huyo ya The Football House kwa ushirikiano wa karibu na taasisi ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Mama Angelina Mabula iitwayo Angeline Foundation.

  Hadi dakika 90 zinatamatika, timu ya kombaini ya Nyamagana iliibuka mshindi kwa ushindi wa mabo2-1. Mabao ya Nyamagana yalifungwa na Rajesh Kotecha na Kuzaifa Mdabiru huku Ilemela wakipata bao la kufutia machozi baada ya mchezaji wa Nyamagana Jefta John kujifunga.
  Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Dkt.Leonald Masele, alisema wilaya yake imejipanga kuhakikisha inaendeleza mchezo wa soka ambapo imeanzisha timu kwa kila soko la machinga wilayani humo hatua ambayo itasaidia kuukuza mchezo huo.
  Mkurugenzi wa taasisi ya The Football House, Mbaki Mutahaba, alisema taasisi hiyo itaendelea kumuenzi mchezaji wake Ismail Khalifan Mrisho huku akiwasisitiza vijana kutumia vyema vipaji walivyonavyo kama ilivyokuwa kwa Mrisho ambaye ameacha alama ya soka nyuma yake baada ya umauti kumkuta.
  Kaka wa marehemu Ismail Khalifan Mrisho, aitwaye Athman Kitwana, akitoa salamu za shukurani kwa niaba ya familia kwa namna ambavyo wadau mbalimbali walivyojitoa kumwendeleza kipaji chake, kusaidia kwenye msiba wake na namna wanavyoendelea kumuenzi baada ya umauti.
  Wazazi wa marehemu Ismail Khalifan Mrisho, kushoto ni Rehema Mfaume (mama) na kulia ni Khalifan Mrisho (baba). 


  0 0

  Na Woinde Shizza, Arusha

  HALMASHAURI ya jiji la Arusha imeifungia kwa muda usiojulikana shule ya msingi Hazina Mision iliyopo kata ya Baraa, baada ya uongozi wa shule hiyo kushutumiwa kwa makosa mbali mbali ikiwemo kuwatelekeza watumishi wake pamoja na mindombinu kuwa chini ya viwango vinavyohitajika katika uandikishaji wamafunzi wa shule hiyo.

  Hatua hiyo ya kufungiwa kwa shule hiyo imekuja baada ya siku chache zilizopita wamiliki wa shule hiyo kulalamikiwa kuwanyanyasa na kushindwa kuwalipa mishahara watumishi na walimu wa shule hiyo na hivyo kutakiwa kufanya marekebisho na kuwalipa stahiki watumishi lakini wakakaidi kufanya maagizo hayo kwa muda waliopewa.
  Akitoa agizo hilo katika viwanja vya shule hiyo, kaimu afisa elimu shule za msingi katika jiji la Arusha, Eunice Elibariki alisema kuwa wameamua kusimamisha huduma ya utoaji elimu kutokana na shule hiyo kushindwa kufanya marekebisho waliyotakiwa kuyafanya shuleni hapo.

  Alisema kuwa awali kabla hatua hiyo haijafikiwa walipata taarifa kuwa uongozi wa shule hiyo inawanyanyasa walimu kwa kuwanyima mishahara yao, kutokuwa na mindombinu kuachilia viwango pamoja na kuwepo uchafuzi wa mazingira na ndipo uongozi ukapewa muda wa kufanya marekebisho hayo pamoja na kimaliza migogoro ya kimaslahi lakini walikaidi kutoa ushirikiano hali iliyopelekea halmashauri hiyo kuchukua hatua ya kusimamisha utoaji huduma.

  "Kwa kuwa uongozi wa shule hii mlishindwa kufanya marekebisho mliyoagizwa ikiwa ni pamoja na kishindwa kumaliza migogoro ya walimu kuanzia sasa nasimamisha huduma za masomo hadi hapo mtakapoweza kuiweka shule yenu katika mazingira yanayohitajika kwani lazima shule iwe na viwango na sifa zinavyohitajika sio tu kuendesha kiholela "alisema Eunice

  Wananchi wa eneo hilo akiwemo Diwani wa kata ya baraa, Elifasi Ndetika akizungumzia uamuzi wa kufungiwa kwa shule hiyo alisema kuwa ni halali kabisa kwani walikuwa na malumbano ya muda mrefu baina ya uongozi na walimu lakini walishindwa kumaliza wenyewe huku akidai kuwa mazingira yalikuwa hayadhirishi na hivyo kupitia usimamishaji huo unaweza kupelekea marekebisho yakawepo.

  0 0

  The US Secretary of State - the Rt Hon John Kerry in between managing global flashpoints such as Syria, Iran, and Israel, has met with 14 year old Girl Education Advocate, Zuriel Oduwole at the US State Department in Washington DC.

  He commended Zuriel for what he called her 'clarity of purpose' in her fight for Girls Education in Africa through her Dream Up, Speak Up, Stand Up project. He also pointed out her other secondary initiatives such as her film making class for unemployed youths in Africa. 

  Zuriel has now taught a film making class to more than 305 youths across 4 African countries - including Namibia, Kenya, Mauritius and Nigeria. The secretary was very impressed that a student from her first film class workshop in February 2016 - Namibian Girl Anna Kalola, produced her first documentary just 9 months later, in November 2016 in Windhoek.

  Zuriel who is Fluent in English and Mandarin, asked Secretary Kerry what his most difficult challenge was in the last four years as Secretary of State. In one word, he replied 'Syria'. He explained the difficulty was because of the various proxies and complexities of dealing with many factions with varying interests in the country.

  This is a true moment of honor for your country, as no Nigerian, African, or US individual, who is not associated with a foreign government at the highest level, has ever been scheduled to meet formally on a one-on-one basis with a current US Secretary of State.

  You have all encouraged her to soar, and so she is doing just that !!!
  Secretary of State John Kerry Welcomes Zuriel to State Department
  Zuriel Listens to Secretary of State John Kerry
  Zuriel Talking To Secretary of State John Kerry.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza (katikati) akiwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) wakiongoza mazoezi kwa wanawake watumishi na wasio watumishi pamoja na baadhi ya wanaume leo katika uwanja wa Samora mazoezi ambayo yataendelea kila jumamosi mjini hapa Picha zote na MatukiodaimaBlog

  Baadhi ya askari wanawake walioshiriki mazoezi leo uwanja wa Samora Iringa.


  0 0

  MICHUANO ya Kombe la mataifa ya Afrika, maarufu kama Afcon, inatarajiwa kuanza rasmi kuwaniwa na timu 16 za bara hilo, leo Jumamosi (14.01.2017) ambapo wenyeji wa mashindano Gabon wanafungua dimba kwa kupambana na Guinea Bissau.

   Wenyeji  wa  mashindano Gabon  wanapaswa  kujiweka  imara kiakili  wakati  watakapopambana  na  wapinzani  hao  ambao hawafahamiki  sana  katika  soka  la  Afrika, Guinea  Bissau  wakati wanawania  kuanza  vizuri  kampeni  yao  katika fainali  za  kombe hilo  zitakapofunguliwa  rasmi  kwa  michezo  miwili leo Jumamosi(14.01.2017).

  Kombe  la  mataifa  ya  Afrika  linaelekea  kuzowea  kufanyika  nchini Gabon , likirejea  katika  taifa  hilo  ambalo  lilikuwa  koloni  la zamani  la  Ufaransa   katika  pwani  ya  magharibi  ya  Afrika  kwa mara  ya  pili  katika  mashindano  manne  yaliyopita. Gabon  ilifanya kazi  nzuri  kuwa  wenyeji  wenza  pamoja  na  Guinea  ya  Ikweta mwaka  2012  na   mwaka  huu  inafanya  kazi  hiyo  peke  yake baada  ya  Libya  inayokumbwa  na  vita  kuamua  kujitoa  kuwa mwenyeji  wa  mashindano  hayo.
  Wapinzani  hao  wa  Gabon  Guinea  Bissau  wanawania kuendeleza mafanikio  yao  waliyoyapata  katika  michezo  ya mchujo. Guinea  Bissau  ni  moja  kati  ya  nchi  masikini  sana barani  Afrika   na  matayarisho  yao  wamekumbwa  na  matatizo  ya fedha, ikiwa  ni  pamoja  na  mgomo  wa  wachezaji  wiki  iliyopita.

  Burkina  Faso  na  Cameroon  zinapambana  katika  mchezo  wa  pili wa  kundi  A  katika  uwanja  unaoweza  kuingiza  mashabiki 40,000 wa  Stade de I'Amitie, mjini  Libreville, timu  zote  zikiwa  na matumaini  ya  kushinda  na  kujiweka  katika  nafasi  nzuri  ya kutinga  katika  nusu  fainali.
  "Iwapo tutashinda  mchezo  huu tayari  tutakuwa  na  asilimia  50  ya kuingia  katika  robo  fainali," amesema  kocha  wa  Cameroon Hugo Broos. Michezo  ya  leo  Jumamosi  inazindua  wiki  tatu  za  heka heka  za  mapambano  ya  kuwania  kombe  la  mataifa  ya  Afrika kuamua  nani atakuwa  bingwa  mpya  wa  bara  la  Afrika  katika fainali  itakayofanyika  mjini  Libreville  hapo  Februari  5.
  Ghana  imewahi  kukaribia  kupata  mafanikio  baada  ya  kuonesha mchezo  mzuri   katika  fainali  tano  za  kombe  hilo  la  Afrika  lakini imeshindwa  kulinyakua  kila  mara,  hali  inayotoa changamoto kubwa  na  pia  motisha  kwa  kikosi  hicho  cha  Black Stars  wakati wakiwania  tena  kulinyakua  kombe  hilo  mara  hii.

  ikosi  kipya  cha Tembo  wa  Cote d'Ivoire  kinajitayarisha  kutetea ubingwa  wao  wa  kombe  la  Afrika , wakichochewa  na  matokeo mazuri  na  kiwango  cha  juu  cha  timu  yao  kutoka  kwa  mchezaji mpya  Wilfried Zaha.

  Mshambuliaji  huyo  wa  timu  ya  Crystal Palace  anamatumaini  ya kuweka  alama  yake  katika  mashindano  hayo  ambayo yanajumuisha  wachezaji  kadhaa  wanaocheza  soka  katika mataifa  ya  Ulaya  kama  Riyad Mahhrez  wa  Algeria , Pierre -Emerick Aubameyang  wa  Gabon  na  Sadio  Mane  wa  Senegal.

  Zaha  ni mchezaji  muhimu  aliyeongezwa   katika  kikosi  hicho  kwa kuwa  nyota  wengi  wa  zamani  kama  ndugu wawili  Toure , Kolo na  yaya  wamejiuzulu  na  mshambuliaji  nyota  wa  pembeni Gervinho  ni  majeruhi.

  Zaha  aliyezaliwa  mjini  Abidjan  ameshawishiwa  kushiriki  katika kombe  la  mataifa  ya  Afrika  na  uwezekano  wa  mafanikio  katika kombe  hilo  na  kombe  la  dunia baada  ya  kushiriki  katika michezo  miwili  ya  kirafiki  katika  timu  ya  nchi  anakoishi  hivi sasa  England.Imeandikwa na Mtandao wa DW.

  0 0


  0 0

  Joseph akimvisha pete ya ndoa mke wake Mariam.
  Mariam akimvisha pete ya ndoa mume wake Joseph.
  Jose akimkumbatia mke wake baada ya kuvalishana pete za ndoa.
  Josephna Mariam wakioneesha pete zao za ndoa.

  0 0  0 0

   Mkaguzi wa Magari wa Jeshi Polisi , Ibrahim Samwix akikagua basi la leo yenye namba za T 735 DFX usajili katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
   Mkaguzi wa magari wa Polisi Sajeti , Elisante Bulla akikagua basi la kampuni ya Imo yenye namba za usajili T 773 CVX ambapo alibaini kukosa mikanda na kuirudisha ndani ya kituo cha mabasi Ubungo leo jijini Dar es Salaam.
  Mkaguzi wa magari wa Polisi Sajeti , Elisante Bulla akikagua basi la kampuni ya Islam na kubaini kukosa langi katika mgongo wa basi hilo na kung’o namba za usajili ili wakapake rangi katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo leo jijini Dar es Salaam. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akipokea msaada wa mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa Skuli ya ngambwa uzi kutoka kwa Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Ndg. Waziri Barnabas, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja Dunga.
  Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said (mwenye koti) akipokea msaada wa mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa Skuli ya msingi Ngambwa uzi kutoka kwa Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Ndg. Waziri Barnabas, mwenye tai kulia Afisa Elimu wa Wilaya ya Kati Unguja Ndg. Makame Haji na kushoto kwa Mwakilishi Sheha wa Ngambwa Ndg. Amour Ali Mussa na Mratibu wa Shughuli za Serikali SMZ  Wilaya ya Kati Unguja Ndg. Khamis Foum. hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika ukumbi wa Ofisi Kilimo Gunga Wilaya ya Kati Unguja.

  Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Wilaya ya Kati Unguja akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni kumi kutoka kwa Kaimu Meneja wa Benk ya NMB Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa Skuli ya Msingi Ngambwa kisiwa cha Uzi Wilaya ya Kati Unguja na kutowa shukrani kwa msaada wao huo kutowa kwa ajili ya jamii kuwapatia watoto wao majengo ya skuli katika eneo lao. Benk ya NMB itejenga jengo la Skuli hiyo katika Kijiji cha Ngambwe Uzi.

  Kaimu Meneja wa Benk ya NMB Waziri Barnabas akizungumza na Uongozi wa Wilaya ya kati Unguja kuhusuana na kuguswa kwa hali ya kijiji hicho cha ngambwa watoto kupata elimu yao ya msingi masafa marefu na makazi yao. kushoto Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Wilaya ya Kati Ungja. 
   Afisa Elimu Wilaya ya Kati Unguja Ndg. Makame Haji, akitowa shukrani kwa uongozi wa Benk ya NMB kwa msaada wao huo kuwakumbuka Wakazi wa Ngambwa kuwapatia msaada kwa ajili ya kumalizia jengo la Skuli yao ya Msingi. ilioazwa msingi na wananchi wa kijiji hicho. 

older | 1 | .... | 1509 | 1510 | (Page 1511) | 1512 | 1513 | .... | 3284 | newer