Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1507 | 1508 | (Page 1509) | 1510 | 1511 | .... | 3283 | newer

  0 0


  Kocha  msaidizi wa Simba Jackson Mayanja

  Kueleka mchezo wa fainali wa kombe la Mapinduzi baina ya Azam na Simba makocha wa pande zote mbili wameanza kutambiana kila mmoja akijinadi kuwa ana uwezo wa kumfunga mwenzake ndani ya dakiika 90.
  Fainali hiyo inayofanyika kesho kwenye uwan ja wa Amani inawakutanisha timu hizo zilizofanikiwa kuingia hatua hiyo Azam wakiwatoa Jang'ombe Taifa kwa goli 1-0, Simba wakiwatoa Yanga kwa mikwaju ya penati 4-2.
  Kocha  msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amejigamba kwa kusema kuwa mechi kati yao na Azam ni mechi ya fainali na ina utofauti mkubwa sana na mchezo uliopita wa watani wao wa jadi na walifanikiwa kuwaondoa kwa mikwaju ya penati.
  Ameweka wazi kuwa mechi hiyo itarajiwa kuwa ni moja ya mchezo wa kukata na shoka kwani silaha zoet zipo kamili na zinajiandaa kikamilifu kabisa. 
  “Maandalizi yapo vizuri kabisa, tuna majeruhi wawili ambao ni Blagnon pamoja na Mohamed Ibrahim kwani hatuna uhakika kama anaweza kucheza ila  wengine wote wako vizuri,”
  Kocha wa muda wa Azam Idd Cheche amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kupambana na anataka kuhakikisha analichukua kombe la Mapinduzi kwani timu nzima inajiamini na watashuka dimbani kupambana. 
  Pia amesifu safu yake ya ushambuliaji kutokuruhus goli hata moja mpaka wanaingia  hatua ya fainali ya Mapinduzi Cup 2017.Cheche amejigamba kuwa anaifahamu vizuri Simba toka anacheza na pia amecheza nazo nikiwa mchezaji na sasa hivi ni mwalimu najua najua jinsi ya kuzikamata.
  Azam imelichukua kombe la Mapinduzi mara mbili (2012 na 2015) tangu ilipoanza kushiriki michuano hiyo wakati Simba tangu 2007 wamelibeba mara tatu (2008, 2011 na 2015)
  0 0


  0 0
  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  KIKOSI cha Usalama Barabarani kimesema hakitaacha kuwachukulia hatua madereva watakaokiuka sheria za usalama barabaani ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali barabarani.

  Hayo yamesemwa  leo na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishina wa Polisi (DCP), Mohamed Mpinga wakati akifungua semina ya madereva iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani  RSA iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

  Mpinga amesema ajali zinapoteza watanzania pamoja na wengine kuwaacha na ulemavu wa kudumu na taifa kukosa nguvu kazi ya kujenga uchumi.

  Amesema madereva wa mabasi ndio wanachangia sehemu kubwa ya ajali ambazo nyingi zinatokana na makosa ya kibinamu hivyo kupitia kampeni ya Abiria Paza Sauti ilete matokeo ya kupunguza ajali.

  Nae Mwenyekiti wa RSA, John Seka amesema semina ya madereva ni mwendelezo wa kampeni ya abiria paza sauti yenye tija kuwaongezea maarifa wanapokuwa katika kazi ya udereva.

  Amesema RSA imedhamiria kutoa elimu ya usalama barabarani kwa kushirikiana na jeshi la polisi katika kuhakikisha ajali zinapungua nchini  na kuwa Tanzania bila ajali inawezekana.

  Kwa Upande wa Meneja wa Usalama Barabarani  na Mazingira wa Sumatra, Geoffrey Silanda amesema wamefunga vidhibiti mwendo kwa mabasi 100 ya kanda ya ziwa kutokana na ukanda huo kuwa na ajali nyingi.

  Amesema wataendelea kufanga mabasi yote vidhibiti mwendo ikiwa nia ya kupunguza ajali ambazo zimekuwa zikipoteza watanzania wengi na wengine kuachwa na uemavu wa kudumu.
  Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishina wa Jeshi Polisi (DCP), Mohamed Mpinga akizungumza na madereva wa mabasi yaendayo mkoani wakati akifungua semina ya madereva iliyoandaliwa Mabalozi wa Usalama Barabarani RSA iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa RSA, John Seka akizungumza katika semina ya madereva walioiandaa kwa ajili ya kuwaongezea maarifa wanakuwa safarini iliyofanyka leo jijini Dar es Salaam.
  Meneja wa Usalama Barabarani na Mazingira wa Sumatra, Geoffrey Silanda akizungumza katika semina ya madereva wa mabasi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishina wa Jeshi Polisi (DCP), Mohamed Mpinga akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa RSA, pamoja na madereva.

  0 0

   ZANZIBAR imeadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu huku ikiwa imepiga hatua mbalimbali za kimaendeleo na utoaji wa huduma bora za kijamii.

  Hayo yamebainishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein wakati akihutubia wananchi katika sherehe za maadhimisho ya Mapinduzi leo katika uwanja wa Amani, Unguja, Zanzibar.

  Dkt. Sein amesema kuwa siku ya Mapinduzi ni muhimu sana katika historia ya Zanzibar kwani ndiyo siku ambayo Wazanzibar walipokuwa huru katika nchi yao na kuweza kufanya shughuli mbalimbali za kujiletea maaendeleo.
  “Tukiwa tunasherehekea miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ni vyema tukajivunia maendeleo yaliyopatikana na yanayoendelea kupatikana.”Alisema Dkt. Shein.

  Akitaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana tangu Mapinduzi Matukufu yatokee tarehe 12 Januari 1961, Dkt. Shein amesema kuwa mafanikio makubwa yamepatikana katika sekta za elimu kwa kuwa na ongezeko la shule kutoka shule 752 mwaka 2015 hadi kufikia 843 mwaka 2016.

  Ongezeko hilo limeenda sambamba na ongezeko la udahili wa wananfunzi ambapo umeongezeka kutoka wanafunzi 384,000 hadi kufikia 424,000 mwaka 2016.

  Katika sekta ya afya kumekuwa na mafanikio ya kuongezeka kwa vituo vya afya kwa asilimia 13.4 ambapo mwaka 2015 kulikuwa na Vituo vya Afya 134 hadi kufikia sasa jumla ya Vituo 152 vimepatikana.

  Mafanikio mengine ni pamoja na upatikanaji wa ajira 2658 zilizotokana na miradi mbalimbali iliyozindulia katika kipindi hiki cha maadhimisho ya siku ya Mapinduzi, kukua kwa Sekta ya Utalii kwa ongezeko la watalii kwa asilimia 13 huku ikichangia pato la taifa kwa asilimia 27.

  Huduma za kijamii zimezidi kuboreshwa huku upatikanaji wa maji safi na salama umeendelea kutatuliwa ambapo miradi ya maji imeekuwa ikitekelezwa ikiwemo kuchimba visima vipya 9 na kuvifanyia ukarabati visima vya zamani.

  Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd amesema kuwa Mapinduzi haya yamekuwa chachu ya kuleta maendeleo kwa kuwa yamewaweka Wazanzibar kuwa huru katika kutekeleza shughuli zao za kujiletea maendeleo.


  Zanzibar imeadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar huku ikiwa imepiga hatua kubwa za kimaendeleo ambapo katika shamra shamra za maadhimisho haya jumla ya miradi 32 ya maendeleo imezinduliwa huku mingine 16 ikiwekwa jiwe la msingi tayari kwa utekelezaji wake, hayo yote ni matunda yatokanayo na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambayo baadaye yalizaa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiwasalimia wananchi walijitokeza katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiimba wimbo wa Taifa katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akikagua gwaride katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na viongozi wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.


  0 0

  Wakati timu pinzani ‘derby’ za JKT Ruvu na Ruvu Shooting zikitarajiwa kuchuana kesho Ijumaa Januari 13, 2017 kwenye Uwanja wa Mabatini, ulioko Mlandizi mkoani Pwani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Bodi ya Ligi Kuu, imetangaza tarehe rasmi za michezo mitatu ambayo awali haikupangiwa tarehe katika ratiba.

  Mbali ya ‘derby’ ya JKT Ruvu na Ruvu Shooting, Jumamosi Januari 14, 2017 kutakuwa na mchezo mwingine wa upinzani kati ya Stand United na Mwadui FC – zote za Shinyanga na zitapambana kwenye Uwanja wa CCM Kambarage.

  Kadhalika siku hiyo ya Jumamosi Januari 14, 2017 Kagera Sugar itakuwa mwenyeji wa Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba katika mchezo mwingine wa VPL.

  Jumapili Januari 15, 2017 kutakuwa na mchezo mmoja tu wa Ligi Kuu ya Vodacom ambako Mbao itakuwa mwenyeji wa African Lyon ya Mwanza katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

  Kadhalika Jumatatu Januari 16, 2017 kutakuwa na mchezo mmoja tu ambako Tanzania Prisons itakuwa mgeni wa Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

  Michezo mitatu ambayo haikupangiwa tarehe hapo awali kwa alama ya TBA ikiwa na maana ya kutajwa baadaye (To Be Announced), tayari Bodi ya Ligi – chombo cha Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF), kinachosimamia na kuendesha ligi, imepanga tarahe.

  Tarehe hizo ni Januari 17, 2017 – siku ya Jumanne kutakuwa na mchezo mmoja kati ya Majimaji itakayowaalika mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Young Africans ya Dar es Salaam katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.

  Kadhalika mechi nyingine ziliopangiwa tarehe na muda ni kati ya Mtibwa Sugar itakayocheza na Simba, Jumatano Januari 18, 2017 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati Azam itakuwa mwenyeji wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Mbagala jijini Dar es Salaam.

  Mchezo huu wa Azam na Mbeya City utaanza saa 1.00 usiku wakati michezo yote tajwa hapo juu itaanza saa 10.00 jioni lengo likiwa ni kutoa nafasi kwa mashabiki kushuhudia mechi nyingi kupitia Kituo cha Televisheni cha Azam - Wadhamini wenza wa ligi hiyo.

  Ligi hiyo ambayo pia inabarikiwa na Benki ya Diamond Trust (DTB), Mdhamini Mkuu ni Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom iliyokuza ubora wa huduma zake hapa nchini katika mawasiliano ya kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maneno na intaneti yenye kasi.

  0 0

  Kamera yetu ilipo kuwa ikiangazia maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya leo ilijikuta ikikuibulia Taswira mbalimbali za Mvua iliyopiga kwa kitambo kuanzia asubuhi ya leo mpaka saa nane mchana na kuweka hali ya usawa kwa wanambeya hasa kwa wafanyabiashara mbalimbali jijini hapo. pichani ni chombo cha usafiri aina ya Bajaji kikiwa kimetumbukia kwenye dimbwi la Maji maeneo ya Shule ya Sekondari Sinde jijini Mbeya.
  Hapa ni ndani ya uzio wa Soko kuu la kimataifa la Mwanjelwa eneo la wafanyabishara ndogo ndogo maarufu kwa jina la Wamachinga wakiwa wamejiweka sawa kwa kujiongeza kufunika bidhaa zao zisiathiliwe na Mvua.
  Hapo kila mtu na Mwamvuli wake mitaa ya Ilemi jijini Mbeya.
  Hivi ndivyo mambo yalivyo noga leo Jijini Mbeya.
  PICHA ZOTE NA MR.PENGO WA MMG MBEYA.

  0 0

  Na: Frank Shija - MAELEZO.

  Rais wa Jmamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Shinyanga kumfutia usajili mwekezaji wa Kiwanda cha Nyama, Kampuni ya Triple S na badala yake watafute mwekezaji mwingine.

  Agizo hilo limetolewa leo Mjini Shinyanga wakati akiwahutubia wananchi wa mji wa huo ambapo yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi iliyoambatana na sherehe ya kuadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

  “Futeni usajili wa mradi wa Triple S, haiwezekani mwekezaji hakashindwa kuendesha kiwanda kwa zaidi ya miaka 10 sasa afu tuendelee kumkumbatia, tafuteni mwekezaji mwingine, mkishindwa semeni Serikali iweke hela, ili uzalishaji uendelee,” alisisitiza Rais Magufuli.

  Aliongeza kuwa mwekezaji huyo amekuwa mbabaishaji kwani tangu kipindi yeye (Rais Magufuli) alipokuwa Waziri wa Uvuvi na Mifugo alimfahamu na alimpa maelekezo cha kusikitisha hakuna jambo aliloendeleza ikiwemo kuanza kwa uzalishaji.

  Akizungumzia sababu ya kufanya maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar katika upande huu wa Bara Rais Magufuli amesema kuwa Tanzania ni moja, na kuongeza kuwa chimbuko halisi la uwepo wa Taifa la Tanzania ni Mapinduzi ya Zanzibara mabapo miezi michache tu baada ya kufanyika kwa mapinduzi hayo Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuzaliwa kwa Taifa la Tanzania.

  Kwa upande wake Waziri wa TAMISEMI na Kazi maalumu kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Haji Omari Heri amesema wao kama Wazanzibar wamefarijika sana kwa kitendo cha Serikali ya Awamu ya Tano kuamua kushiriki maadhimisho ya Mapinduzi Matukufu kwa kusherehekea katika upande wa Bara kitu ambacho akijawahi kufanyika kabla.

  Aliongeza kuwa ujio wake umetokana na ukweli kwamba Tanzania ni nchi moja hivyo Rais Magufuli alivyoeleza nia yake ya kuadhimisha Maapinduzi huku Bara, Rais Dkt. Shein alimteua aje kumwakilisha na kueleza kuwa maefarijika sana na kusema Tanzania ni yetu sote na tutaendelea kuwa wamoja.

  Rais Dkt. Magufuli yuko ziarani Mkoani Shinyanga ambapo kesho anatarajiwa kufungua viwanda kadhaa vilivyopo mkoani hapo, baadhi ya viwanda hivyo ni pamoja na Kiwanda cha Vinywaji Baridi (maji) cha Jambo, Kiwanda cha Mafuta na vingene. 

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuwasalimia wananchi wa Shinyanga waliofika katika uwanja wa mpira wa Kambarage katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar mkoani humo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kuwahutubia wakazi wa Shinyanga katika kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Kambarage mkoani humo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Shinyanga katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Kambarage mkoani humo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Kwaya ya KKKT Shinyanga mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.


  PICHA NA IKULU

  0 0


  0 0
  0 0
 • 01/13/17--12:30: SHINDANO


 • 0 0

  TAARIFA KWA UMMA Dar es Salaam Januari 13, 2017- Kampuni ya Bia ya Serengeti inapenda kuwataarifu wateja wake na umma na kwa ujumla kuwa kuna video isiyo na maadili inaiyosambazwa katika mtandao ya kijamii ikionesha msanii akiigiza na kuimba wimbo wenye mahadhi ya taarabu mbele ya bango lenye nembo ya bia Serengeti Premiur Lager. 
   
  Tunapenda kuweka bayana kuwa onesho la msanii huyo halikuidhinishwa wala kudhaminiwa na SBL Pia msanii huyo sio sehemu na hajawahi kuwa mmoja wa mawakala wetu wanaotoa huduma za kutangaza bidhaa zetu.
   
   Video hiyo ambayo haizingatii maadili ya sanaa inatoa picha mbaya jambo ambalo ni kinyume na sera ya SBL ya kuzingatia maadili mema katika shughuli za kutangaza bidhaa zake. Aidha ikumbukwe kwamba SBL imekuwa mstari wa mbele katika kulinda na kusimamia maadili katika shughuli zake za kijamii ikiwa ni pamoja na kuhamasisha unywaji wa pombe kistaarabu.
   
   Tunauhakikishia umma na wateja wetu kuwa SBL inafanya shughuli zake za kijamii kwa kuangalia mambo yenye tija kwa jamii na sio vinginevyo. Tunapenda kuwashukuru sana wateja wetu na umma kwa ujumla kwa kuendelea kushirikiana nasi.
   
   Imetolewa na Mkurungezi wa Mahusiano 
  Serengeti Breweries Limited.

  0 0

  Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa wa Chama cha Wananchi
  (CUF), Mhandisi Shaban Kaswaka (kushoto), akimtambulisha kwa
   wananchi Mgombea Udiwani kupitia chama hicho
  Kata ya Kijichi, Abdallah Shamas katika mkutano wa
  kampeni uliofanyika eneo la Mwanamtoti
  Temeke jijini Dar es Salaam jana.
  Na Dotto Mwaibale

  MGOMBEA  Udiwani  Kata ya Kijichi kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Abdallah Khalid Shamas amewataka wananchi na wagombea wenzake kuacha siasa za chuki na chafu ili kuiletea maendeleo kata hiyo na taifa kwa ujumla.

  Shamas alitoa ombi hilo wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika eneo la Mwanamtoti Kijichi Dar es Salaam jana wakati akijinadi kwa wapiga kura.

  "Siasa  chafu za chuki na  zinazowatenganisha wananchi kutokana na itikadi za vyama vyao hazifai na haziwezi kuleta maendeleo katika kata hiyo na taifa kwa ujumla" alisema Shamas.

  Alisema siasa chafu zilizokuwepo katika eneo hilo la Mwanamtoti zilifikia hatua ya kugawana makaburi jambo ambalo lilikuwa ni hatari katika kushirikiana.

  Akizungumzia baadhi ya vipaumbele vyake iwapo atachaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo alisema cha kwanza ni kuhakikisha eneo la Mwanamtoti wanapata shule ya msingi ambayo itawasaidia watoto wa eneo hilo kutotembea umbali mrefu wa kwenda shuleni.

  Alitaja kipaumbele chake cha pili ni kuhakikisha eneo hilo linapata zahanati pamoja na kukaa na wataalamu wa taasisi za fedha kuona namna ya kuanzisha Saccos au chombo cha fedha ili kuweza kutoa fursa kwa wananchi wa kata hiyo kukopa na kufanikisha maendeleo yao.

  Mgombea huyo amewaomba wananchi wa eneo hilo Januari 22, mwaka huu wamchague ili awatumikie baada ya kata hiyo kukosa maendeleo kwa zaidi ya miaka 20.

  Uchaguzi huo mdogo wa ngazi ya udiwani unafanyika katika kata hiyo kufuatia aliyekuwa diwani kufariki dunia mapema mwaka jana na nafasi hiyo kuwa wazi.
   Mgombea Udiwani kupitia chama cha CUF wa Kata ya Kijichi, Abdallah Khalid Shamas akihutubia katika mkutano huo.
   Wafuasi wa CUF wakimkaribisha mgombea udiwani wa Kata ya Kijichi wakati alipokuwa amewasili kwenye mkutano wake wa kampeni.

  0 0

  “BINGWA WA MABADILIKO” au “CHAMPION FOR CHANGE” ni kauli mbio iliyoanzishwa kwenye shindano lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya wanawake (UN-WOMEN) lenye lengo wa kuwapata vijana watakaoweza kushirikiana na serikali za nchi zao kuwainua wanawake kiuchumi.

  Maombi zaidi ya 4000 kutoka kona zote za dunia yalitumwa kwa shirika hilo na ni vijana 170 tu ndio waliobahatika kuchaguliwa wakiwemo vijana watano kutoka Tanzania.

  Vijana hao waliofanikiwa kuchaguliwa kuwa mabalozi wa “CHAMPION FOR CHANGE” ni Agnes Mgongo, Doris Mollel, Hassani Tozir, Catherine Ruge pamoja na Sadick Lungendo.

  Mabalozi hawa watashirikiana na serikali kwa kwa hamasa na mafunzo mbalimbali ili  kuwainua na kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi. 

  Hivyo basi wadau wote kwenye njanja tofauti tofauti wanaombwa kuwaunga mkono mabalozi hawa kwa kushiriki kwenye midahalo au mahojiano kwa kupitia kwenye mtandao mkubwa kijamii ulioanzishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya wanawake (UN-WOMEN) unaoitwa “JOIN THE MOVEMENT” kwa kufuatisha kiunganishi (link) hapa chini kujisajili na kuanzisha mijadala yako.


  https://www.empowerwomen.org/en/join-the-movement

  0 0

  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), usiku wa kuamkia leo umenusurika kuteketa kwa moto uliozuka ghafla na kusababisha taharuki kwa wasafiri na watumiaji wa uwanja huo, hali iliyolazimu kusimamishwa kwa shughuli zote uwanjani hapo.

  Vikosi vya Zimamoto vilifika eneo la tukio kwa wakati na kuanza kukabiliana na moto huo ambao walifanikiwa kuuzima.

  Akizungumza baada ya tukio hiho, Kamanda wa Polisi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Kamishna Msaidizi (SACP), Martin Otieno amesema kuwa wamefanikiwa kuudhibiti moto huo na kwamba uchunguzi wa kina juu ya chanzo cha moto huo na hasara iliyosababisha, unaendelea kufanyika na kwamba tayari shughuli zote za uwanjani hapo zimerejea na zinaendelea kama kawaida.

  Aidha Meneja wa Uwanja huo amewatoa hofu Watanzania na wasafiri wote wanaotumia Uwanja huo, kwa kuwaeleza kuwa hali imekuwa shwari uwanjani hapo na huku akikiri  kutokea kwa moto huo unaodaiwakuwa ulizuka kuanzia majira ya saa 6 hadi saa 7 usiku wa kuamkia leo.

  Ambapo ameeleza kuwa shughuli zote za usafirishaji zimehamishiwa uwanja wa zamani (Terminal One) na kule zinaendelea kama kawaida huku wakiweka sawa maeneo yalioathirika na moto. 


  “Madhara kidogo yametokea kwenye jengo la kuhifadhia mizigo pekee, hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa kutokana na moto, mashine zote zipo salama na sasa shughuli zote za usafirishaji tumezihamishia kule uwanja wa zamani (Terminal One) zinaendelea kama kawaida”. Amesema Meneja huyo.
  Kwa mbali kule ni sehemu ya moto huo ulipoekuwa ukiendelea kuwaka.
  Giza lilitawala katika eneo lote la jengo la Uwanja wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

  0 0

  Mhe Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Athony Peter Mavunde wa tatu kushoto akionyeshwa na kupata maelekezo juu ya ufugaji wa Samaki na Msimamizi wa Kituo cha Maendeleo ya Vijana SASANDA Ndg Martin kambisi wa Pili kushoto.

  Mhe Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Athony Peter Mavunde akizungumza na Vijana wajasilia mali wakulima na wafugaji wanaopata Mafunzo juu ya kilimo bora na Ufugaji wa kisasa katika Kituo cha maendeleo ya Vijana SASANDA kilichopo Wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe.

  Mhe Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Athony Peter Mavunde akikagua duka la dawa baridi Moja kati ya Mradi wa Vijana wa kikundi cha MELANAKO kilichopata Mkopo wa shiling Milion Saba toka Wizarani.

  Mhe Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Athony Peter Mavunde akitazama bidhaa za ujasiliamali Asali pamoja na Dawa ya Kusafishia chooni vinavyo zalishwa na kikundi cha Vijana wajasilia mali MELANAKO kilichopo wilayani Mbozi mkoani Songwe.

  Mhe Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Athony Peter Mavunde akikagua Mradi wa Ufugaji wa Ng’ombe wa kisasa alipotembelea Kituo cha maendeleo ya Vijana SASANDA chenye vikundi vya vijana 12 vyenye jumla ya Vijana 200 wanaojifunza shughuli mbali mbali za kilimo na Ufugaji wa kisasa.
   


  0 0
 • 01/13/17--01:23: Article 4


 • 0 0

  Maonesho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yameendelea leo kwenye viwanja vya Maisara – Zanzibar, ambapo wananchi wameendelea kumiminika kwa wingi kwenye banda la maonesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kusajiliwa, kuchukua vitambulisho vyao na kupata elimu kuhusu umuhimu na faida za Vitambulisho vya Taifa.

  Miongozi mwa wageni waliotembelea banda hilo ni Mhe. Mwinyiusi A. Hassan, Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “A”, Dr. Hamed Rashid Hikmany; Mkuu wa chuo Kikuu cha Abdulrahman Al-Sumait Memorial, ambao wamepongeza kazi nzuri inayofanywa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa na kupendekeza Vitambulisho vya Taifa kuanza kutumika katika shughuli mbalimbali ili kupunguza utitiri wa vitambulisho.

  “Tuimarishe utendaji na tufanye kazi kwa malengo na kwa kufanikisha utendaji kwa kuendelea kuwa karibu zaidi na Serikali za Wilaya, Shehia na wananchi” alisisitiza Mkuu wa Wilaya.

  Aidha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Dr. Andrew W. Massawe naye amejumuika na wananchi wa Zanzibar kwa kutembelea na kukagua shughuli zinazofanyika kwenye banda la NIDA Maisara- Zanzibar na kushiriki kuzungumza na kujibu hoja za wananchi wa Zanzibar walio kuwepo kwenye banda la NIDA kupata huduma. Wananchi hao wameonyesha kufarijika na utendaji wa Mkurugenzi huyo na kuelekeza furaha yao kwa jinsi alivyojitoa na kushirikiana na wafanyakazi wake katika kujibu hoja mbalimbali za wananchi.

  Akizungumza wakati akijibu hoja za wananchi, Bwana Masssawe amepongeza wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye banda la NIDA kupata huduma na ufafanuzi kuhusu Vitambulisho vya Taifa; na kuipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi kwa jumla kwa kutimiza miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  “NIDA tunaahidi kuendelea kuwa karibu zaidi na wananchi kwa kuendelea kutoa huduma nzuri zaidi kwa wananchi; lengo letu tuhakikishe kila Raia mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea anapata kitambulisho chake, pamoja na kuwasajili Wageni, Wakimbizi wenye sifa za kuishi nchini kama sheria ya Usajili na Utambuzi wa watu inavyoelekeza” Amesisitiza

  Maonesho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yalianza tarehe 07 Januari na yatamalizika Jumamosi tarehe 14 Januari 2017 viwanja vya Maisara Zanzibar, NIDA ikiwa miongoni mwa taasisi zinazoshiriki kwa kutoa huduma za Utambulisho kwa wananchi na usawaji wa Vitambulisho kwa wananchi ambao wamekamilisha taratibu za usajili.  Mhe. Mwinyiusi A. Hassan, Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “A” akiweka saini  kwenye kitabu cha wageni alipotembelea banda la Mamlaka ya Vitambulisho  vya Taifa NIDA kwenye Maonesho ya 53 ya Sherehe za Mapinduzi Zanzibar viwanja vya Miasara Zanzibar.

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA, Ndg. Andrew W. Massawe akisaliana na Ndg. Aboubakar Mikidadi Othuman mwananchi aliyetembelea banda la NIDA kupata huduma ya Usajili.

  Ndg. Abdulaziz Juma Mtumwa (kushoto) Afisa Msajili Msaidizi – NIDA akimsajili Ndg. Aboubakar Mikidadi Othuman kupata kitambulisho cha Taifa baada ya kupokea maelezo ya kina toka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA.

  Dr. Hamed Rashid Hikmany; Mkuu wa chuo Kikuu cha Abdulrahman Al-Sumait Memorial akiweka saini kitabu cha wageni alipotembelea banda la maonesho la Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa Zanzibar
  Mmoja wa wananchi akipata maelezo ya kina kuhusu muonekano mpya wa Kitambulisho cha Taifa alipofika kutembelea banda la NIDA Maisara – Zanzibar.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA Ndg. Andrew W. Massawe akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi kwenye banda la Mamlaka ya Vitambulisho NIDA- Maisara Zanzibar.

  0 0

  Kikao cha kujadili changamoto za Muungano kinafanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la wawakilishi Kikwajuni Unguja. Kikao hiki cha ngazi ya Mawaziri kinajumuisha Mawaziri kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ). Kikao hicho ni utangulizi wa Kikao cha Makamu wa Rais kitakachofanyika mchana wa leo.
  Kikao cha kujadili changamoto za Muungano kinafanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la wawakilishi Kikwajuni Unguja. Kikao hiki cha ngazi ya Mawaziri kinajumuisha Mawaziri kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ). Kikao hicho ni utangulizi wa Kikao cha Makamu wa Rais kitakachofanyika mchana wa leo.
  Katika Picha Sehemu wa viongozi wa Serikali ya (SMZ) katika kikao cha ngazi ya Mawaziri kinachojadili changamoto cha Muungano Mjini Zanzibar Leo.
  Katika Picha Sehemu ya Viongozi wa SMT katika kikao cha ngazi ya Mawaziri kinachojadili changamoto cha Muungano Mjini Zanzibar Leo.(Picha na Evelyn Mkokoi na Lulu Mussa wa OMR).

older | 1 | .... | 1507 | 1508 | (Page 1509) | 1510 | 1511 | .... | 3283 | newer