Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1506 | 1507 | (Page 1508) | 1509 | 1510 | .... | 3348 | newer

  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  MGOMBEA wa Udiwani wa Kata ya Kijichi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Tausi Milanzi amesema kuwa wananchi wamchague ili aweze kufanya kazi ya maendeleo ya Kijichi.
  Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Kampeni, Tausi amesema  yuko tayari kuwatumikia wananchi na sio jambo lingine hivyo anahitaji kura ndio itakayomuwezesha  kuwapa maendeleo.
  Amesema vijana ndio wenye maamuzi hivyo watumie fursa ya kupiga kura ili aweze kushirikiana na vijana hao katika maendeleo.
  Tausi amesema kuwa yeye ni mwanamke mwenye uchungu wa maendeleo hivyo anaomba kura ndio aweze kutimiza malengo hayo.
  Naye  Mbunge wa Mkuranga,na Katibu  Msaidizi  wa Kamati ya Wabunge wa  Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Ulega amesema wananchi wa kijichi wamchague Tausi kwa ajili ya maendeleo.
   Mgombea  wa Udiwani wa Kata ya Kijichi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Tausi Milanzi akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Sayari wakati wa kuomba kura leo.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
   Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam,Afidu Luambano akizungumza na wakazi  wa Kijichi wakati mkutano wa hadhara  wa  kuomba kura ya Mgombea wa Udiwani wa Kata ya Kijichi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Tausi Milanzi leo katika mkutano wa hadhara wa kuomba kura.
   Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza wakati wa akimnadi Mgombea wa Udiwani wa Kata ya Kijichi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Tausi Milanzi leo katika mkutano wa hadhara wa kuomba kura.
   Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akiwa ,amemshika mkono Mgombea wa Udiwani wa Kata ya Kijichi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Tausi Milanzi leo katika mkutano wa hadhara wa kuomba kura.
   
   Mbunge wa Mbagala, Issa Mangungu akizungumza na wakazi  wa Kijichi wakati mkutano wa hadhara  wa  kuomba kura ya Mgombea wa Udiwani wa Kata ya Kijichi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Tausi Milanzi leo katika mkutano wa hadhara wa kuomba kura.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Kahama Bw. Fadhili Nkurlu ametoa siku saba kwa wafanyabiashara waliouziana majengo ya hoteli kubwa na nyumba mjini Kahama kufikisha mikataba yao ya mauziano ofisini kwake ndani ya siku saba ili kutoa nafasi kwa TRA kuifanyia ukaguzi ambapo amedai kuwa sehemu ya biashara hizo zimekuwa zikifanyika kimya kimya hali ambayo imekua ikiikosesha serikali mapato.

  0 0


  0 0


  Mjadala umeshika kasi mitaani, mitandaoni na kila mahali baada ya Mahakama ya wilaya ya Kilombero kumhukumu kutumikia kifungo cha miezi sita jela bila faini Mbunge Wa jimbo la Kilombero Mhe. Peter Lijualikali (30) kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki katika maeneo ya ukumbi Wa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.

  Mbunge huyo, akiwa mshtakiwa namba moja pamoja na mwenzie Stephano Mgata (35) walitenda kosa hilo Machi 1, 2016 saa 4 asubuhi Kwenye kikao cha Baraza la Madiwani katika eneo la Kibaoni ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro.  Imesemwa kuwa kwa pamoja walifanya fujo kinyume na kifungu namba 89 kifungu kidogo cha kwanza B, cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002, ambapo washtakiwa walikana mashtaka na hivyo kufanya kesi kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili na upande wa mashtaka ukathibitisha bila kuacha shaka.


  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan ameibuka na kukata kiu ya wananchi ya kutaka kujua endapo kama baada ya hukumu hiyo Mhe. Lijualikali ataendelea kuwa mbunge.

  Akihojiwa na TBC One wakati wa taarifa ya habari ya saa mbili usiku huu Bw. Kailima ameweka bayana kwamba mbunge huyo ataendelea na wadhifa wake kwa kuwa sheria inasema ili kupoteza kiti ni lazima uwe umepewa adhabu ya kifungo cha ZAIDI ya miezi sita jela.

  "Ibara ya 67(2)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza mambo yanayotoa sifa ya kuwa Mbunge kutoka  madarakani ni kifungo cha zaidi ya miezi sita jela. Huyu bwana kafungwa miezi sita kwa hiyo bado hajapoteza sifa za kuendelea kuwa mbunge akiwa gerezani na baada ya kumaliza kifungo chake", alisema Bw. Kailima.


  0 0


  0 0

  Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Mhe. Cosato Chumi akikabidhi mashuka kwenye moja ya Zahanati ilikuwa na upungufu wa mashuka katika kata ya Isalavanu wakati wa ziara yake ya kukagua na kugundua changamoto za zahanati za jimbo la Mafinga mjini

   Mbunge wa jimbo la mafinga mjini  Mhe. Cosato Chumi kushoto akiwa na katibu wake pamoja na mfanyakazi wa zahanati matanana wakati wa ziara yake
   Mbunge wa jimbo la mafinga mjini  Mhe. Cosato Chumi akiwasalimia wananchi wa kata ya Isalavanu wakati wa ziara yake
  Mbunge wa Mafinga mjini akitandika moja ya shuka kati ya mashuka aliyoyagawa katika zahanati mbalimbali katika jimbo lake. Mashuka hayo yametolewa na mfuko wa bima ya afya NHIF.

  0 0

  Na Profesa Mbele

  Wiki iliyopita nimepata zawadi ya picha kutoka Ramble Pictures, kampuni ya kutengeneza filamu. Kampuni hiyo, ambayo ilianzishwa na mmoja wa wanafunzi wangu, Jimmy Gildea, na marafiki zake, ndiyo iliyotengeneza filamu ya Papa's Shadow, inayohusu maisha na safari za mwandishi maarufu Ernest Hemingway Afrika Mashariki, pamoja na maandishi yake kuhusu Afrika Mashariki. Sehemu kubwa ya filamu hiyo ni mazungumzo baina ya Mzee Patrick Hemingway na mimi, kuhusu masuala hayo.
  Picha niliyopewa inaitangaza filamu ya Papa's Shadow. Inamwonesha Ernest Hemingway, Patrick Hemingway na mimi, Kuna pia Mlima Kilimanjaro na nchi tambarare chini ya mlima, na pia ndege ikiwa angani. Hiyo picha ya mlima na mazingira yake, pamoja na ndege, inakumshia hadithi maarufu ya Hemingway, "The Snows of Kilimanjaro."

                                                                Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0


   Na Nteghenjwa Hoseah, Karatu 
  MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Theresia Mahongo kuhakikisha fedha za walimu wa shule za sekondari na msingi zilizokatwa na halmashauri ya wilaya hiyo kwaajili ya vitambulisho vya kazi zinarudishwa. 
   Mhe. Gambo alitoa agizo hilo jana wilayani Karatu wakati alipokuwa akizungumza na walimu hao kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Karatu Boys ili kujua changamoto wanazokutana nazo na jinsi ya kuzitatua ikiwemo madeni ya likizo, upandaji wa madaraja. 
   Alihoji ni kwanini walimu hao wakatwe Sh. 6000 kwa ajili ya kutengenezewa vitambulisho vya kazi wakati ni haki yao kama watumishi na waajiriwa wa halmashauri hiyo na ni haki yao kupata vitambulisho vya kazi bure; Mwajiri anao wajibu wa kumtengenezea kila mtumishi Kitambulisho cha kazi.  Alimwagiza DC Mahongo kuhakikisha anafuatilia na kumchukulia hatua watumishi wa halmashauri hiyo waliowakata walimu hao wa msingi na sekondari kiasi hicho cha fedha kwa ajili kuwachukulia hatua. 
    Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (aliyesimama) akifungua Kikao cha walimu alichokiitisha ili kuskiliza changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi wakati wa ziara yake Wilayani Karatu.
   Walimu wa shule za msingi na Sekondari wanaofanya kazi katika Halmashauri ya Karatu wakifuatilia kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati wa ziara ya kikazi.

  1.     Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo akiongea na walimu wa Shule za Msingi na Sekondari katika Wilaya ya Karatu. 

  0 0

  Wizara ya Nishati na Madini kupitia Mradi wa Kuwajengea Uwezo  Wataalam wa Nishati na Tasnia ya Uziduaji  (CADESE: Capacity  Development  in the Energy Sector  and Extractive Industries), inatarajia kuanzisha mfumo wa uhifadhi data  kwa ajili ya nishati  jadidifu  ujulikanao kama  Tanzania  Renewable Energy Management  Information System (TREMIS)  utakaowezesha wawekezaji ndani na nje ya nchi  kubaini fursa za uwekezaji zilizopo katika  sekta ya nishati jadidifu.
  Hayo yameelezwa na  Msimamizi wa Mradi wa Kuwajengea Uwezo  Wataalam wa Nishati na Tasnia ya Uziduaji  (CADESE), Paul Kiwele katika ziara ya maandalizi ya mfumo huo jana, Kahama mkoani Shinyanga.
   Mtaalam kutoka Sehemu ya Nishati Jadidifu- Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Stephan Kashushura (kushoto) akizungumza na mtaalam  kutoka kampuni ya vifaa vya umeme jua ya Mobisol, Devis Mtete (kulia) mjini Kahama mkoani Shinyanga tarehe 11 Januari, 2017

   Mtaalam kutoka Sehemu ya Nishati Jadidifu- Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Stephan Kashushura (kushoto) akizungumza na mtaalam  kutoka kampuni ya vifaa vya umeme jua ya Mobisol, Devis Mtete (kulia) mjini Kahama mkoani Shinyanga tarehe 11 Januari, 2017

  Mtaalam kutoka kampuni ya vifaa vya umeme jua ya Zola, Omary Raymond (katikati) akielezea shughuli za kampuni yake kwa Mtaalam kutoka Sehemu ya Nishati Jadidifu- Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Stephan Kashushura (kulia). Kushoto ni Msimamizi wa Mradi wa Kuwajengea Uwezo  Wataalam wa Nishati na Tasnia ya Uziduaji  (CADESE) chini ya  Wizara ya Nishati na Madini, Paul Kiwele. 

  0 0


  0 0

   Tanzania Portland Cement Company Ltd, the market leader in the country’s cement industry, has announced the launch of  ‘Twiga Jenga “ a new cement product to the market ’. 

  Twiga Cement Commercial Director Mr. Simon Delens has said that the product specifically addresses the needs for masonry activities such as plastering, external and internal wall repair, laying tiles and production of mortar for brick and blocklaying. Also Mr. Delens states that "this new brand is the result of almost one year of careful research and development by our business development section together with cement technical experts." 

  The introduction of Twiga Jenga  is completing the wide product range of the company and will provide the appropriate product for specific applications. Masons will finally have a suitable cement product for their need at an affordable price. Twiga Jenga will be sold 600 TZS/bag lower than the current cheapest cement available in the company’s portifolio making cement even more accessible for Tanzanians.Twiga cement is continuosly innovating and conducting reseach to come up with better product to satisfy our customer needs. 

  Mr. Delens concluded by reminding customers that this product is mainly made for finishing and masonry activities and that this cement is not recommended for block making and concrete production. Twiga cement customers are encouraged to continue using Twiga Cement brand for other applications.

  Pictured below is the Managing director of TPCC (Twiga Cement ) Mr. Alfonso Velez (center) announcing the introduction of the new Twiga Jenga cement product mainly produced for masonry activities such as plastering, laying tiles and brick/block laying  at Twiga cement headquarters at  Tegeta in Dar es salam.  Mkurugenzi mkuu wa Twiga Cement Bw.  Alfonso Velez wa tatu kutoka kulia akiongea wakati wa uzinduzi wa  saruji mpya ya "Twiga Jenga " iliyotengenezwa mahususi kwa ajili ya mafundi uashi kwa matumizi ya kupiga lipu, kuwekea malumalu na kwa ajili ya matumizi madogo madogo ya kujengea. Uzinduzi huu umefanyika mapema jana Kiwandfani kwao Wazo Hill Tegeta, jijini  Dar es salaam.
  Timu ya masoko ya Twiga Cement ikiongozwa na Mkurugenzi mkuu ndugu Alfonso Velez wa tatu kutoka kulia wakizindua saruji mpya ya "Twiga Jenga " iliyotengenezwa mahususi kwa ajili ya mafundi uashi kwa matumizi ya kupiga lipu,bkuwekea malumalu na kwa ajili ya matumizi madogo madogo ya kujengea. Uzinduzi huu umefanyika mapema jana Kiwandani kwao Wazo Hill  Tegeta, jijini  Dar es salaam.

  0 0


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Melinne saccos kuhakikisha wanakuwa wawazi na kutoa taarifa za hesabu za umoja huo kila wakati ili wanachama waweze kuwa na takwimu sahihi. 
  Alitoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Januari 11, 2017) wakati akizindua saccos hiyo yenye mtaji wa zaidi ya sh. bilioni moja kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinguzi Matukufu ya Zanzibar. 
  Waziri Mkuu alisema viongozi hao wanatakiwa kuwa wawazi kwa wanachama wenzao jambo ambalo litawajengea uaminifu hivyo kuwezesha umoja huo kudumu na kufikia malengo yaliyokusudiwa. 
  Alisema vyama vingi vya ushirika nchini vimekufa kutokana na viongozi wake kutokuwa waaminifu hivyo Serikali hatokubali kuona suala hilo linatokea katika umoja huo kwani litakwamisha maendeleo. 
  Aidha, Waziri Mkuu aliwapongeza wananchi hao kwa kuanzisha saccos hiyo kwani wameweza kutimiza ndoto ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume ya kuondokana na umasikini, dhuluma na unyonge.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,  Mama Asha Seif Idd kabla ya kufungua ukumbi wa SACCOS ya Melinne  mjini Zanzibar ikiwa ni moja ya shughuli za sherehe ya Mapinduzi ya Zanzibar 
   Waziri  Kassim Majaliwa , viongozi mbalimbali wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakimsikiliza  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd wakati  alipozungumza  baada ya Waziri Mkuu kufungua SACCOS ya Melinne mjini Zanzibar
   Baadhi ya wananchama wa SACCOS ya Melinne ya Zanzibar wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kufungua ukumbi wa SACCOS hiyo 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kufungua SACCOS ya Melinne mjini Zanzibar ikiwa ni moja ya shamrashamra  za sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar januari 11, 2017.   Kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd
   Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanachama wa SACCOS ya Melinne ya Zanzibar baada ya kufungua ukumbi wao Januari 11, 2017. Kulia kwake ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd. Habari kamili BOFYA HAPA

  0 0
  0 0

  NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amewaagiza Wakuu wa wilaya nchini kuhakikisha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu wanakwenda kuanza shule huku akiwasisitiza wazazi watakaoshindwa kuwapeleka shule watoto hao wachukuliwe hatua za kisheria.

  Jafo ametoa agizo hilo leo alipofanya ziara ya kukagua miundombinu mbalimbali katika shule za msingi, Chadulu, Chang’ombe A na B, Manispaa ya Dodoma.

  Katika ziara yake ya kukagua maagizo aliyoyatoa kwenye shule hizo kuhusu masuala ya miundombinu, Jafo amesema  “Sisi kama serikali hatutaki mtoto akose elimu hasa katika kipindi hichi ambacho serikali imeamua kuelekeza nguvu za kutosha kwenye elimu kwa ajili ya watanzania.”
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( OR-TAMISEMI) Seleman Jafo akipokea taarifa za maendeleo ya ujenzi wa madarasa shule ya msingi Chang’ombe ‘’A ‘’kutoka kwa Afisa mteule daraja la -I- ambaye ni Fundi mkuu kutoka (JKT) Aluleyani Mapunda wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa madarasa shule ya msingi hiyo unaofanywa katika kata ya Chang’ombe mjini Dodoma.

  Ameongeza “Kwa mzazi ambaye mtoto wake atabainika hajaenda shule na kupewa kazi zingine kama kuendesha bodaboda hatua za kisheria zichukuliwe mara moja,”.

   Pamoja na hayo, Jafo amekemea tabia ya wazazi kutotilia mkazo masuala ya elimu na kuwakabidhi watoto wao kuendesha bodaboda kama ajira yao badala ya kuwapeleka shule na kuwataka kuhakikisha wanawanunulia mahitaji yote ya shule.

  Aidha amesema serikali haitarajii kuna vijana waliochaguliwa wakishawishiwa na wazazi kufanya vibaya kwenye mitihani kutokana na elimu kuwa ni bure.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Selemani Jafo akitoka kukagua ujenzi wa choo cha walimu katika shule ya msingi Chang’ombe ‘B’ wakati wa ziara yake aliyoifanya katika kata ya Chang’ombe.

  Akizungumzia kuhusu watoto walioandikishwa kuanza kusoma elimu ya awali na msingi, Jafo amesema kumekuwepo na mwitikio mkubwa katika suala la uandikishaji watoto hao na linatokana na uwepo wa elimu bure.

  Hata hivyo, amesema shule nyingi idadi ya wanafunzi imeongezeka zaidi na kwa serikali ni faraja kuona watanzania wengi sasa wanapata elimu huku akiwataka wazazi wahakikishe watoto walioandikishwa wanahudhuria shule ipasavyo  na wakurugenzi kuendelea kuweka mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia.

  Kadhalika, Jafo ameridhishwa na ukarabati wa miundombinu mbalimbali kwenye shule hizo huku akiwaahidi walimu kuwa serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kufundishia ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na mwanafunzi George John wa darasa la saba ambaye ni mlemavu na kutoa agizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi,kuhakikisha mradi wa ujenzi wa vyoo vya wanafunzi Shule ya Msingi Chang’ombe A unazingatia miundombinu rafiki kwa ajili ya watu wa ulemavu wakati wa ziara yake aliyoifanya katika kata ya Chang’ombe.

  Naye, Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi, amesema kwasasa Manispaa hiyo inaendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja ujenzi wa shule za msingi na sekondari na kuongeza madarasa kwenye baadhi ya shule ili kukabiliana na ongezeko la wanafunzi hasa wanaohamia Dodoma.

   Kwa upande wake, Ofisa Elimu wa Manispaa hiyo, Scholastika Kapinga, amesema hadi sasa watoto zaidi ya 8,000 wameandikishwa kwenye manispaa hiyo kuanza kusoma elimu ya awali na msingi.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Selemani Jafo akipokea maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi juu ya ukamilifu wa ujenzi wa choo cha walimu shule ya msingi Chang’ombe ‘B’ pia uendelevu wa ujenzi wa vyoo vya wanafunzi katika ziara yake aliyoifanya katika kata ya Chang’ombe.

  0 0
  0 0

  Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya wakishiriki zoezi la usafi katika kituo cha Afya kiwanja Mpaka jijini Mbeya ikiwa ni sehemu ya kusherekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya wakishiriki zoezi la usafi katika kituo cha Afya kiwanja Mpaka jijini Mbeya ikiwa ni sehemu ya kusherekea miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo pia wakabidhi vifaa vya usafi katika kituo hicho cha Afya .

  Zoezi la usafi likiendelea


  Zoezi la Usafi likiendelea........

  Wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya katika picha ya pamoja mara baada ya kushiriki zoezi la usafi katika kituo cha Afya kiwanja Mpaka jijini Mbeya ikiwa sehemu ya kusherekea sherehe za Miaka 53 ya  mapinduzi Zanzibar. Picha zaidi BOFYA HAPA
  0 0

  Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
  MBUNGE wa jimbo la Bagamoyo,dk.Shukuru Kawambwa ameelekeza nguvu zake katika ujenzi wa madarasa katika shule mbalimbali jimboni humo ambapo amechangia zaidi ya mifuko 1,000 ya saruji.
  Aidha ametoa zaidi ya sh.mil.10 kuchangia vikundi viwili vya ujasiriamali kwenye kila kata kwa ajili ya kukopeshana ambapo kati ya vikundi hivyo vimewezeshwa sh.mil.1 hadi mil.1.5.
  Hayo aliyasema ,kijiji cha Mwavi,Mkenge na Fukayose wakati wa ziara yake inayolenga kupeleka mrejesho kwa wananchi kuhusiana na hatua anazozichukua kufuatilia kero zao zinazowakabili.
  Dk.Kawambwa alisema jimbo hilo lina jumla ya kata 11 na kila kata ameichangia kati ya mifuko 100-150 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa .
  Alieleza kuwa amehakikisha mfuko wake wa jimbo unaunga mkono juhudi za wananchi kwenye ujenzi huo na kuwezesha wajasiriamali.
  Mbunge huyo alisema,ameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona bado shule nyingi zinapambana na changamoto ya uhaba wa madarasa na vikundi kukosa mitaji.
  Hata hivyo,dk.Kawambwa aliahidi kutoa matofali 1,000 katika kitongoji cha Kalimeni na kwa kijiji cha Kitopeni ameshawapa ardhi yenye heka 6 na fedha kwa ajili ya kujenga shule na tayari wameanza .
  “Nimeona suala la madawati limemalizika vizuri kwa ushirikiano wa wadau,halmashauri na ofisi ya wilaya ya Bagamoyo,tumevuka kwa hili lakini tatizo ni majengo “
  “Nitaelekeza nguvu zangu katika ujenzi huu kulingana na uwezo uliopo pamoja na kusupport akina mama na vijana kwenye vikundi vyao”alisema dk.Kawambwa.
  Aliiomba jamii washirikiane kwa pamoja kwenye ujenzi wa madarasa ili kufanikisha lengo lao la kuondokana na upungufu wa madarasa.
  MBUNGE wa jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa akizungumza na wanachama wa vikundi vya ujasiriamali vya jipe moyo na kiroho safi,vilivyopo Mwavi kata ya Fukayose,wakati wa ziara yake aliyoianza jimboni hapo.
   
   MBUNGE wa jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa akizungumza na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mkenge kata ya Fukayose,wakati wa ziara yake aliyoianza jimboni.

  0 0

   
  BBC Focus on Africa television and radio, along with the BBC Swahili TV programme, Dira ya Dunia, will hit the road together in January to broadcast live from Uganda for a week from 23rd to 27th January. This will be the first time the programmes will come together to broadcast from the continent, which will feature special guests and studio audiences on TV, radio and online.
   
  Focus on Africa is the flagship news and current affairs programme for Africa, broadcast every weekday on BBC World News television and BBC World Service radio. The show is presented by some of the biggest names in African journalism, including Peter OkwocheSophie Ikenye and Paul Bakibinga, as well as Salim Kikeke and Dayo Yusuf from Dira ya Dunia.

  “There is so much to explore and discuss in Africa at the moment, that we felt it was the right time for the shows to collaborate and bring something fresh to our audience of 111 million people in Africa,” says Sophie Ikenye. “We’re giving Focus on Africa and Dira ya Dunia a different dimension by coming live from Kampala and featuring voices from the region. It promises to be a fascinating week in one of the world’s most vibrant cities.”

  Throughout the week, exclusive stories from BBC correspondents in Malawi, Algeria, the Democratic Republic of Congo and Sierra Leone will be featured on the programmes, showcasing the breadth and depth of the BBC’s coverage across the continent, and holding those in positions of responsibility to account.

  The shows will also feature some of Uganda’s biggest and best in the entertainment and sports world. There will be live performances from musicians, dance troupes and comedians, as well as special reports from our reporters in Gabon for the Cup of Nations, where we’ll join Ugandan fans for the Cranes’ final group match against Mali.

  Watch Focus on Africa on BBC World News TV at 1730 GMT, Monday to Friday, and listen on BBC World Service radio at 1500, 1700 and 1900 GMT, Monday to Friday. You can also stay up to date with the week’s stories on the Africa Live page on www.bbc.com/africa and on BBCSwahili.com, and by searching #BBCFOA on Facebook, Instagram and Twitter. On social media, @BBCAfrica and @BBCSwahili will also share extras, including behind-the-scenes footage and interviews.


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
  HISTORIA ya watumwa na kuanza kwa dini ya kikristo visiwani Zanzibar yawa kivutio kikubwa sana kwa watalii kutoka nchi mbalimbali kwa kufika katika Kanisa la The Cathedral Church of Christ lilijengwa na Bishop Edward Sterre kufahamu undani wakuja kwa dini hiyo kwneye visiwa hivyo.

  Kanisa hilo limejengwa lilipokuwa Soko la watumwa lilijojengwa mwisho wa karne ya 19 pakitumika kama eneo la kuhifadhi watumwa wanaotolewa maeneo mbalimbali na Zanzibar ikiwa ndio kitivo cha biashara hiyo na Bishop Edward Sterre akaamua kuwanunua watumwa hao kwa lengo la kukomesha biashara ya utumwa na wakati wa ujenzi wa jengo la kanisa  watumwa walitumika kujenga na ikiwa ni kama  kuwakomboa na kisha baadae kuwabatiza na kuwa wakristo.

  Kwa sasa kanisa hilo linaweza kupokea wageni kutoka mataifa mbalimbali  wanaoenda kufahamu historia ya watumwa na kuanza kwa dini ya kikristo pia kuna huweza kufika 1000 kwa siku kulingana na kipindi kilichopo.

  Katika chumba kimoja cha watumwa walikaa takribani 75 yaani watoto 25 na wakubwa 50 na waliweza kukaa humo kwa kipindi kisichopungua siku mbili hadi tatu na wengine walikufa kutokana na kukosa hewa pamoja na kutokupewa chakula, mbali na hilo pia walifariki kwa magonjwa ya mlipuko kwani walikuwa wakilala juu ya kibaraza lakini kwa chini wakawa wanatumia kama sehemu ya haja ndogo na kubwa wakisubiri maji yajae baharini ili yaingie na kusafisha.

  Picha za maeneo ya kanisa hilo liliopo eneo la Darajani Mkunazini Visiwani Zanzibar.
  The Cathedral Church ambapo kabla ya kuwa kanisa lilitumika kama soko la watumwa visiwani humo wakiletwa kutoka sehemu tofauti kwa ajili ya biashara hiyo.
   Muonekano wa nje wa The Cathedral Church of Christ lilijengwa na Bishop Edward Sterre lililojengwa karne ya ya 19 kwa lengo la kukomesha biashara ya utumwa.

   Kanisa la Thed Cathedral Church of Christ katika muonekano wake wa ndani.
  Wageni mbalimbali wakiwa wametembelea kanisa hilo na kufahamu historia ya watumwa iliyokuwa imeshamiri visiwani Zanzibar na kuanza kwa dini ya kikristo.
   Kinanda cha kwanza kutumika katika kanisa hilo na kinapatikana katika nchi kadhaa barani Afrika ikiwamo Visiwa vya Zanzibar.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3) katika Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka watatu kutoka kulia Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa wakwanza kulia pamoja na viongozi wengine.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengiene  akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa mradi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3).
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo ya mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3) kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS  Mhandisi Cristianus Ako kabla ya kuweka jiwe la msingi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Maswa kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3), mkoani Simiyu.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka mara baada ya kuwasili Wilayani Maswa. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1506 | 1507 | (Page 1508) | 1509 | 1510 | .... | 3348 | newer