Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110153 articles
Browse latest View live

MUFTI AWATAKA WAISLAMU KUOMBA NCHI IPATE MVUA IONDOKANE NA UKAME NA BAA LA NJAA

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

WAISLAM nchini wametakiwa kuomba nchi ipate mvua ili kuondokana na ukame na kuepusha baa la njaa.

Mwito huo umetolewa na Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Bin Zubeir Bin Ali wakati ukitolewa kwa niaba yake na Msemaji wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania, Sheikh Khamis Said Mataka wakati akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo.

"Taarifa mbalimbali zinaashiria nchi kukabiliwa na ukame kwa kukosa mvua za msimu zilizotarajiwa kutokana na hali hiyo Mufti anawaomba Masheikh, Maimamu na Waislamu wote kwa ujumla kuleta toba,kumuomba msamaha Mwenyezi Mungu ili 

aijaalie nchi yetu na nchi jirani zetu kupata mvua za kheri zitakazotusaidia kutuepushia ukame na madhara yake ikiwemo baa la njaa" alisema Sheikh Mataka.Katika hatua nyingine Mufti wa Tanzania amewateua Mwenyekiti wa Halmshauri Kuu Bakwata Taifa, Sheikh Khamis Said Mataka na Mkurugenzi wa Daa'wa na Tabligh Bakwata Makao Makuu Sheikh Hassan Said Chizenga kuwa wasemaji rasmi wa Baraza

Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata) uteuzi ambao umeaanza mara moja.Akizungumzia matumizi ya wadhifa wa Sheikh Mkuu alisema kumekuwa na matumizi yasiyosahihi kwa baadhi ya masheikh wa mikoa na wilaya kujiita masheikh wakuu wa maeneo hayo.

Alisema wadhifa wa Sheikh Mkuu ni Mufti pekee na si vinginevyo na akasisitiza kuwa masheikh wa mikoa na wilaya na mitaa wanakumbushwa kutumia nyadhifa zao kama ilivyoainishwa katika katika ya Bakwata.

Katika mkutano huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Bakwata Sheikh Suleiman Lolila alitumia fursa hiyo kutangaza rasmi kustaafu kutokana na kutumikia nafasi hiyo kwa muda mrefu na kuwa na umri mkubwa.Nafasi hiyo hivi sasa itashikiliwa kwa muda na Ustadhi Salm Ahmed.
Msemaji wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania, Sheikh Khamis Said Mataka (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kwa niaba ya Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Bin Zubeir Bin Ali, kuhusu waislamu kote nchini kuiombea nchi ipate mvua na iondokane na ukame na baa la njaa. Kulia ni Katibu Mkuu wa Bakwata aliyemaliza muda wake, Suleiman Lolila na kushoto ni Mshauri Mkuu wa Mufti, Sheikh Abubakar Ali.
Mshauri Mkuu wa Mufti, Sheikh Abubakar Ali (katikati), akizungumza katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Bakwata aliyemaliza muda wake, Suleiman Lolila (kushoto), akitangaza rasmi kustaafu wadhifa huo.
Mkurugenzi wa Daa'wa na Tabligh Bakwata Makao Makuu Sheikh Hassan Said Chizenga (wa pili kushoto), akiongoza dua maalumu katika mkutano huo.
Dua likifanyika.

RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI BARIADI MKOANI SIMIYU, AWEKA JIWE LA MSINGI HOSPITALI YA RUFAA YA SIMIYU PIA AFUNGUA BARABARA YA BARIADI-LAMADI (KM 71.8)

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati alipowasili Bariadi kwa ajili ya kuifungua rasmi barabara ya Bariadi-Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8. Wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati alipowasili Bariadi kwa ajili ya kuifungua rasmi barabara ya Bariadi-Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma za asili pamoja na kikundi cha Ngoma za asili Baseki cha Bariadi mkoani Simiyu mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kabla ya kufungua rasmi barabara hiyo la Bariadi-Lamadi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua moja ya nguzo katika ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na viongozi mbalimbali pamoja na madaktari na manesi mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu. PICHA NA IKULU

ASKARI MONUMENT GARDEN KUBORESHWA KUWA YA KISASA ZAIDI

$
0
0
Na Anthony John,Globu Jamii.

Kampuni inayojishughulisha na Uhifadhi wa Mazingira na Usafishaji ya Green WastePro Ltd imesema kuwa, wamejitolea kuiboresha Askari Monument Garden kuwa ya mfano na ya kisasa katika Jiji la Dar es salaam.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja Mwendeshaji wa Kampuni hiyo,Abdallah Mbena leo wakati akizungumza na Globu ya Jamii,amesema wamejitolea kutengeneza Garden hiyo ili kuunga mkono kampeni mbali mbali za Usafi zinazo ongozwa na Rais Magufuli pamoja na Mkuu wa Mkoa.

"Baada ya kuona kampeni mbali mbali za Usafi zinaendelea tukaona njia rahisi ya kuunga mkono kampeni hizo ni kujitolea kuiboresha Askari Monument Garden kuwa ya kisasa katika jiji la Dar es salaam kwa kuunga mkono Serikali ya awamu ya tano," amesema Mbena

Pia Mbena amesema mpaka itakapofika Mwezi wa tatu marekebisho hayo yatakuwa yamesha kamilika na tutakuwa tayari kuzindua.

Amesema kuwa "Watu wenge wamekuwa wakijiuliza maswali kwa nini pamezungushiwa uzio katika Sanamu la Askari Monument Garden lakini ni Kwa sababu tunataka kuiweka kuwa ya kisasa zaidi."
 Maneja Mwendeshaji wa Kampuni ya Green Weste Pro Ltd,Abdallah Mbena akizungumza na Globu ya Jamii Juu ya Uboreshaji wa Monument Garden Leo hii Jijini Dar es salaam.
Picha ya ndani ya ukarabati unavyoendelea wa Askari Monument Garden.

KAMATI YA BUNGE YA PIC YATEMBELEA EPZA

$
0
0
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda wa Uwekezaji (EPZA) Bw.  Lamau Mpolo akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakati Kamati hiyo ilipotembelea eneo hilo mapema leo.
   Mkurugenzi wa Raslimali Watu wa Kiwanda cha Tanzania Tooku Garments kilichopo eneo la EPZA Bw.  Bakanga Paul akizungumza mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakati Kamati hiyo ilipotembelea Kiwanda hicho.
 Mwanasheria  wa Kiwanda cha Tanzania Tooku Garments Bw  Ibrahim Gamba (kushoto) kilichopo eneo la EPZA akimuelezea Mwenyekiti wa Kamati ya ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji wa Umma (PIC) Mhe Albert Obama akimuelezea jinsi uzalishaji wa nguo unavyofanyika Kiwandani hapo wakati Kamati hiyo ilipotembelea Kiwanda hicho.
   Wajumbe wa  Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji wa Umma (PIC) wakiangalia shughuli za uzalishaji nguo zinafofanyika Kiwandani hapo.
  Msajili wa Hazina (kulia) Dkt Oswald Mashidano pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) Mhe Albert Obama (katikati) wakiangalia jinsi shughuli za ushonaji nguo zinavyofanyika Kiwandani hapo.(Picha na Ofisi ya Bunge).

SERIKALI WILAYANI HANDENI YAPIGA MARUFUKU UUZAJI HOLELA WA MKAA

$
0
0
Serikali wilayani Handeni imepiga marufuku uuzaji holela wa mkaa ili kudhibiti matumizi mabaya ya rasilimali za misitu NA kuwataka wananchi kutumia vituo rasmi kuuza na kununua mkaa. 

Marufuku hiyo ilitolewa na Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe alipokuwa akizindua vituo maalumu vilivyotengwa kwaajili ya kuuzia mkaa (mkaa centre) vinavyotarajiwa kuwa mazingira rafiki kwa vijana wanojihusisha na biashara za mikaa wilayani hapa. 

Mh Gondwe alisema "ni marufuku kuanzia sasa mtu yeyote kuuza mikaa kwenye maeneo ambayo sio vituo rasmi, mkaaa utauzwa na kununuliwa kwenye vituo vilivyopangwa atakayekiuka hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake”. Aliongeza kuwa lengo kuu la kuweka vituo vya kuuzia mkaa ni kudhibiti matumizi mabaya ya rasilimali za misitu; Kulingana na sera ya ukusanyaji mapato,kwa kutumia vituo hivi serikali itaweza kupata mapato yake ambayo hapo awali kulikua na utoroshaji na ukwepaji wa kulipa kodi kwa wavunaji na wauzaji wa mikaa.

Mkuu wa wilaya aliwataka wavunaji wa mkaa kuunda vikundi ambavyo vitawatambulisha na kusaidia kuwa na umoja utakaopelekea kupata vibali halali vya uvunaji wa mazao ya misitu. Alisema kuwa utaratibu huo utasaidia kuwepo kwa uvunaji endelevu ambao utahusisha kupanda miti na kuvuna tofauti na ilivyokuwa awali watu wanavuna miti bila kupanda miti mingine ili kufidia ile iliyovunwa hali itakayoiepusha Handeni kuwa jangwa na kuharibu vyanzo vya maji.

Aliwaeleza wananchi kuwa vituo hivyo vitasaidia kuwa na bei elekezi ambayo itawanufaisha wafanyabiashara wote tofauti na awali ambapo kulikua na ushindani mkubwa uliopelekea wengine kujaza lumbesa ili kupata wateja kwa haraka. 
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe na wataalamu wakipata maelekezo mafupi juu ya moja ya kituo cha kuuzia mkaa cha Manga.

Mkurugenzi akionesha baadhi ya vibakuli vilivyokamatwa ambavyo vilitengenezwa na mti aina ya mkarambati tayari kwa kusafirisha kuelekea nchini Kenya kwa mauzo.
Meneja wa wakala wa Misitu Tanzania wa Wilaya ya Handeni akizungumza na wafanyabiashara wa mazao ya misitu ya Mkaa wakati wa Uzinduzi.
Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji Bw. William Makufwe na Meneja wa wakala wa Misitu wa Wilaya Bw. Elias Mwaijere wakitoka kuzindua kituo cha wauza mkaa cha Manga
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe akizungumza na wafanyabiashara wa mkaa wakati wa Uzinduzi . 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe akizungumza na wafanyabiashara wa Mkaa.

Alda sadango,Afisa habari 
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.

TEA Yatoa Milioni 496 Kujenga Uzio wa Hosteli Mpya za UDSM.

$
0
0
Na Lilian Lundo – MAELEZO

Mamlaka ya Elimu Tanzania Tanzania (TEA) imetiliana saini na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mkataba wa ujenzi wa uzio katika hosteli za Mwalimu J.K. Nyerere Kampasi ya Mlimani.

Mradi huo umedhaminiwa na TEA kupitia Mfuko wa Elimu (Education Fund) utakaogharimu jumla ya shilingi 496,646,868 hadi kukamika kwa ujenzi huo.

Mkataba huo umesainiwa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Graceana Shirima na Makamu Mkuu wa Chuo cha UDSM Profesa Rwekaza Mukandala wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Alisema kuwa utekelezaji mradi huo unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 12 ijayo.Kwa upande wake Prof. Mukandala aliwashukuru TEA kwa msaada huo na kuongeza kuwa ujenzi wa uzio hizo ni suluhisho kubwa kwa wanafunzi watakaoishi katika eneo la kampasi hiyo.

Alisema kuwa uzio utasaidia kuimarisha usalama wa wanachuo na mali zao kutokana na kuwepo eneo ambalo lina mzunguko mkubwa wa watu unaotokana na stendi ya mabasi ya simu 2000 , maduka ya Mlimani City pamoja na viwanja hivyo kutumika kama njia ya mkato na vijiwe kwa watu wasio na kazi.

TEA tayari imefadhili miradi mbalimbali Chuo Kikuu cha UDSM ikiwemio ujenzi wa vyumba vya mihadhara, ununuzu wa vitabu vya kiada, vifaa kwa ajili ya wanafunzi kwenye mahitaji maalum, ufadhili wa kozi za “Pre Entry” kwa wanafunzi wa like katika masomo ya sayansi, ununuzi wa mitambo na vifaa vya Tehama.
Makamu Mkuu wa Chuo cha UDSM Prof. Rwekaza Mukandala na Kaimu Mkurugenzi Mkuu TEA Graceana Shirima wakisaini mkataba huo.

Makamu Mkuu wa Chuo cha UDSM Prof. Rwekaza Mukandala na Kaimu Mkurugenzi Mkuu TEA Graceana Shirima wakibadilishana mkataba huo mara baada ya kuusaini. Kulia ni Kaimu Meneja Miradi ya Elimu TEA, Anne Mlimuka.


Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Sylivia Lupembe akitoa utambulisho wa viongozi kutoka TEA na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa uzio wa hosteli mpya za Mwalimu J. K. Nyerere Kampasi ya Mlimani unaodhaminiwa na TEA ambao utakaogharimu shilingi Mil. 496. Kutoka kushoto ni Kaimu Mwanasheria wa UDSM Dkt. Saudin Mwakaje, Makamu Mkuu wa Chuo cha UDSM Prof. Rwekaza Mukandala, Kaimu Mkurugenzi Mkuu TEA Graceana Shirima na Kaimu Meneja Miradi ya Elimu TEA Anne Mlimuka.

Uongozi wa TEA na UDSM wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini mkataba wa ujenzi wa uzio wa hosteli za Mwalimu J. K. Nyerere zinazojengwa kandokando ya barabara ya Sam Nujoma, Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu NHIF azitaka hospitali zote nchini kutoa huduma bora kwa Wanachama wake

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernard Konga akiongozana na baadhi ya wakurugenzi wa Mfuko na uongozi wa Hospitali ya Kairuki walipotembelea maeneo mbalimbali ya hospitalini hapo kuangalia huduma zinazotolewa kwa wanachama wa Mfuko. Pichani akimjulia hali mwanachama wa Mfuko aliyelazwa hospitalini hapo.

Na Grace Michael

KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Bernard Konga amezitaka Hospitali zote nchini zinazohudumia wanachama wake kuhakikisha zinatoa huduma bora na zinazostahili kwa wanachama ikizingatiwa ukweli kwamba wamekwishazilipia huduma hizo kabla ya kuugua.

Aidha amewahakikishia wanachama wa Mfuko kwamba, Mfuko umejipanga kuwahudumia na kutatua kero wanazokabiliana nazo wakati wa kupata huduma ili wajivunie huduma walizolipia.

Bw. Konga amesema hayo wakati alipofanya ziara ya kujionea namna wanachama wa Mfuko wanavyohudumiwa katika Hospitali ya Kairuki mjini Dar es Salaam ambapo mbali na kuona huduma pia alipata fursa ya kuzungumza na wanachama waliofika hospitalini hapo kupata huduma.
Bw. Konga akiwasikiliza wanachama wa Mfuko waliokuwa wakipata huduma za matibabu hospitalini hapo.

Akizungumza na wanachama katika Hospitali ya Kairuki, Bw. Konga alisema kuwa ameamua kuanza ziara ya kutembelea hospitali zote ili kukutana na wanachama, kusikiliza kero zao pamoja na kuzungumza na watoa huduma kwa lengo la kutatua matatizo yaliyopo na kujenga uhusiano bora.

“Nimeamua kuanza rasmi ziara hizi za kikazi kuwaona moja kwa moja wanachama wanahudumiwa ili nizungumze nao na kupata maoni kutoka kwao…wanachama kwangu ndio kipaumbele cha kwanza kwa kuwa ndio wametupa dhamana ya kuwahudumia na kukaa na fedha zao hivyo binafsi sitakubali kuona mwanachama akipata huduma hafifu”. Alisema Bw. Konga.

Alisema kuwa kitendo cha kutoka na kusikiliza wanachama kitasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma lakini pia kukutana uso kwa uso na wananchi ambao Mfuko unawahudumia.
Wakiendelea kupata maelezo ya huduma hospitalini hapo.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

TANZIA


RAIS DK. SHEIN AFANYA UZINDUZI WA SKULI YA SEKONDARI KWARARA 2

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa  Balozi wa Korea Kusini Bw.Song Geumyoung wakati wa sherehe za uzinduzi wa Skuli ya Sekondari ya Kwarara na Kituo cha Elimu ya Habari,uliofanyika leo Skulini hapo, Ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambapo ujenzi wake umejengwa kwa Ushirikiano  wa Serikali na Shirika la Kimataifa la Maendeleo kutoka Korea (KOICA)
Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa Hutuba yake katika sherehe za uzinduzi wa Skuli ya Sekondari ya Kwarara na Kituo cha Elimu ya Habari, aliyoizindua rasmi  leo ,Ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar,ujenzi wa Skuli hiyo umejengwa kwa ushirikiano wa  Serikali ya Mapinduzi na Ushirikiano  wa Serikali ya Mapinduzi na Shirika la Kimataifa la Maendeleo kutoka Korea (KOICA). (Picha  na Ikulu).
 Chumba cha Kompyuta katika Skuli ya Sekondari ya Kwarara iliyozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ambayo imejengwa na  Ushirikiano  wa Serikali ya Mapinduzi na Shirika la Kimataifa la Maendeleo kutoka Korea (KOICA), Ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar
  Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia)  akifuatana na   Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof.Joyce Lazaro Ndalichako (katikati) na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali (kulia) wakati alipotembea katika madarasa mbali mbali ya  Skuli ya Sekondari ya Kwarara na Kituo cha Elimu ya Habari ,iliyoizindua rasmi leo, iliyojengwa kwa Ushirikiano  wa Serikali ya Mapinduzi na Shirika la Kimataifa la Maendeleo kutoka Korea (KOICA), Ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipanda mti aina ya muembe baada ya kuizindua Skuli ya Sekondari ya Kwarara na Kituo cha Elimu ya Habari,aliyoizindua rasmi  leo, Ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar, ujenzi wa Skuli hiyo umefadhiliwa na Serikali ya Mapinduzi na Ushirikiano  wa Serikali ya Mapinduzi na Shirika la Kimataifa la Maendeleo kutoka Korea (KOICA)

mwanafunzi wa kidato cha kwanza awasili shuleni kwa chopa

$
0
0
Shughuli za masomo zilisimama kwa muda shule ya Nyeri High School nchini Kenya Jumatano asubuhi wakati mwanafunzi aliyeripoti kuanza elimu ya kidato cha kwanza alipotua kwa chopa.

Kijana Kevin Muriuki, aliyepasi katika shule ya msingi ya Karichen alipelekwa shuleni hapo kwa njiamya anga na chama cha veterani wa kikosi cha anga cha Kenya (Kenya Air Force Veterans Association).



Muriuki, anayetoka kwenye familia inayoishi kwenye mazingira magumu, ana ndoto ya kuwa rubani wa ndege na maveterani hao wakaona wamwonjeshe kwa kumpeleka shuleni kwa chopa. 

 Kijana Kevin Muriuki na chopa iliyompeleka shuleni Nyeri
 Kijana Kevin Muriuki na wazazi wake wakielekea kwenye chopa
 Kijana Kevin Muriuki akiaga 
Kijana Kevin Muriuki haamini bahati yake

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi azindua Kituo cha Zimamoto na Uokozi cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametahadharisha kwamba uzembe wa aina yoyote  unaoweza kufanywa  na Kikosi cha Zimamoto na Uokozi wakati inapotokea dharura kwa bahati mbaya unaweza kukimbiza huduma za ndege za Kimataifa zinazotumia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar.
Alisema  umuhimu wa Kikosi hicho kuwepo katika maeneo ya Viwanja vya ndege hata Bandarini kwa ajili ya kutoa huduma za uokozi wa masuala ya dharura ni muhimi na mkubwa kwa Uchumi wa Taifa hili.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa Kituo cha Zimamoto na Uokozi cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964.

Balozi Seif alisema  Serikali imekuwa ikichukuwa jitihada mbali mbali za kukiimarisha Kikosi hicho cha Zimamoto ili kiende sambamba  na Teknalojia  ya kisasa pamoja na kufikia  kutoa huduma zenye viwango vya  Kimataifa.
Alisema Idara ya  Zimamoto na uokozi  ni nyenzo muhimu katika Taifa lolote Duniani, hivyo ni vyema kwa watendaji wa Taasisi hiyo   wakaandaliwa utaratibu muwafaka wa kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara  ndani na nje ya nchi.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua gari jipya la zimamoto baada ya  kuzindua rasmi Jengo la Kituo cha kikosi cha zimamoto na uokozi cha uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Gari jipya la Kikosi cha zimamoto na Uokozi likiwa ni moja  miongoni mwa magari Manne yaliyonunuliwa na Serikali Kuu kwa ajili ya Kikosi cha zimamoto na Uokozi Zanzibar.
 Kamishna wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar Kamishna Ali Abdulla Malimus akitoa Taarifa ya ujenzi wa Kituo cha Zimamoto cha Uwanja wa Ndege wa Zanzibar.
 Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ  Bibi Radhia Rashid Haroub akizungumza kwenye uzinduzi wa Jengo la Kituo cha Zimamoto na Uokozi cha Uwanja wa Ndege wa Zanzibar.
Balozi Seif Ali Iddi  kati kati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Mawaziri wa SMZ, Viongozi wa  Taasisi zinazosimamiz sekta ya mawasiliano pamoja  na Maafisa wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi mara baada ya uzinduzi wa jengo la Kikosi cha Zimamoto Uwanja wa Ndege wa Zanzibar. Picha na – OMPR – ZNZ.

TEASER JOTO LA ASUBUHI ALHAMISI JANUARY 12, 2017

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LEO TAREHE 11.01.2017

MAJALIWA AZINDUA BARABARA YA MWANAKWEREKWE HADI FUONI- ZANZIBAR

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watendaji wa Serikali wahakikishe wanawasimamia vizuri wakandarasi wanaojenga miradi mbalimbali nchini ikiwemo ya barabara ili viwango vyake vifalingane na thamani halisi ya fedha zinazotolewa.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Januari 11, 2017) wakati akizundua mradi wa ujenzi wa barabara ya Kwerekwe/Fuoni yenye urefu wa kilomita 4.01 iliyogharimu sh. bilioni 10.07 zilizotolewa na Mfuko wa Barabara. Ujenzi huo ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015.

Waziri Mkuu amezindua barabara hiyo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Amesema Serikali inatumia fedha nyingi katika miradi ya ujenzi wa barabara hivyo watendaji wake hawana budi kuhakikisha miradi hiyo inalingana na thamani halisi ya kiwango cha fedha kinachotolewa.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka watendaji hao kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kulinda na kuhifadhi miundombinu hiyo na kuwachukulia hatua wote watakaobainika kufanya uharibifu ikiwemo uchomaji wa matairi katikati ya barabara.

Pia amewataka wananchi kutojenga majengo ya kudumu katika hifadhi ya barabara ili kuepusha usumbufu pale Serikali inapotaka kuyatumia maeneo hayo. “Lazima wananchi wazingatie sheria ya hifadhi ya barabara,”

“Serikali imedhamiria kuboresha mawasiliano kwa kujenga barabara zetu kwa kiwango cha lami. Hatatutakubali kuona mtu anaharibu miundombinu hii tunayoijenga kwa gharama kubwa ikiharibiwa. Lazima tuilinde ili iweze kutunufaisha wote,” amesema.

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua barabara ya Mwanakwerekwe hadi Fuoni yenye urefu wa kilomita 4.1 iliyopo Zanzibar Januari 11, 2017.  Kushoto ni  Waziri wa  Ujenzi,  Mawasiliano na  Usafirishaji, Ali Karume . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kuzindua barabara yenye urefu wa kilomita 4.1  ya kutoka Mwanakwerekwe hadi Fuoni Zanzibar ikiwa ni moja ya shughuli za sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar, Januari 11, 2017.  Katikati ni Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa rais wa Zanzibar, Mohammed Abood na Kulia ni  Mkuu wa mkoa waMjini Magharibi, Mohammed Mahmoud. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akiwapungia wananchi wa Zanzibar wakati  alipowasili kwenye eneo la  Barabara ya Mwanankwerekwe  hadi Fuoni kufungua barabara hiyo yenye urefu wa Kilomita 4.1 Januari 11, 2017. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, , Mawasiliano na Usafirishaji, Ali Karume. (Picha na  Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Baadhi ya wananchi wa Zanzibar wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kuzindua barabara ya Mwanakwerekwe hadi Fuoni yenye urefu wa Kilomita 4.1 ilyopo Zanzibar Januari 11, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika dua iliyosomwa baada ya kuzindua barabara ya Mwanakwerekwe hadi Fuoni yenye urefu wa Kilomita 4.1 iliyopo Zanzibar Januari 17, 2017.Wengine pichani kutoka kushoto ni Spika wa Baraza la Wawakilishi,   Zubri Ali Maulid, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mohammed Mahmoud na kulia ni Waziri wa Ujenzi, Mawsiliano na  Usafirishaji, Ali Karume. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

SOMA ZAIDI HAPA

TTCL YAZINDUA RASMI HUDUMA YA 4G ZANZIBAR

$
0
0

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti w Baraza la Mapinduzi Issa Haji Gavu akiwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Waziri Waziri Kindamba wakinyanyua mabango ya matangazo kuashiria kuzinduliwa kwa  huduma ya 4G  ya Kmpuni hiyo  Zanzibar (kushoto)  Mkuu wa Kanda ya Zanzibar Franscis Mabula.
 Afisa wa kutengeneza bidhaa wa TTCL Rashid Maggid  akimueleza Waziri Gavu namna ya huduma ya 4G inavyofanyakazi kwa urahisi na kwa haraka wakati wa sherehe za uzinduzi wa huduma hiyo iliyofanyika makao Makuu  ya TTCL Zanzibar, Kijangwani.
 Waandishi wa Habari wakifanya mahojiano na Waziri Gavu na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL (hawapo pichani) baada ya uzinduzi wa huduma ya 4G Zanzibar.
 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Waziri Waziri Kindamba akijibu maswali ya waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya 4G uliofanyika Ofisi Kuu Kijangwani.
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa TTCL na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Gavu baada ya uzinduzi wa huduma ya 4G Zanzibar. Picha na Makame Mshenga.
Kwa taarifa zaidi BOFYA HAPA

waendesha bodaboda na abiria wasiovaa helmet Dar es salaam wakamatwa, wapewa elimu

$
0
0

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam Kamishina Msaidizi Wa Polisi Awadhi J. Haji, akimwelekeza mwendesha bodaboda namna sahihi ya kuvaa kofia ngumu.Hiyo in baada ya kuwapa elimu waendesha bodaboda na abiria ambao walikamatwa kwa kosa la kutovaa kofia ngumu (helmet) katika operesheni kali na endelevu inayoendelea jijini Dar es salaam ya kuwakamata bodaboda na abiria wasiovaa helment na wanaopakiwa abiria zaidi ya mmoja (mishikaki)  ili kuwanusuru na vifo au ulemavu wa kudumu pindi wanapopata ajali.

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI BARABARA YA BARIADI-LAMADI KM 71.8 BARIADI MKOANI SIMIYU

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 11 Januari, 2017 ameanza ziara ya siku mbili mkoani Simiyu kwa kuwataka wananchi wa mkoa huo na Tanzania kwa ujumla kuwapuuza  watu wanaoendesha siasa alizozitaja kupitwa na wakati kwa kutumia baadhi ya vyombo vya habari kutangaza kuwa Tanzania inakabiliwa na njaa badala ya kuwahamasisha wananchi kufanya kazi
Dakta Magufuli amesema hayo wakati akizungumza na wananchi katika uwanja wa Shule ya Msingi Somanda mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika  Hospitali ya Mkoa wa Simiyu na kufungua barabara ya Lamadi hadi Bariadi yenye urefu wa kilomita 71.8 iliyogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 90.
Amesema kumekuwepo na baadhi ya wanasiasa na wafanyabiasha ambao wamekuwa wakiwahamisisha wananchi na kutumia baadhi ya vyombo vya habari kutangaza baa la njaa wakati wanasiasa hao hao ndio waliopitisha Bungeni kutaka nchi iuze chakula nje ya nchi na sasa hao hao wanatangaza baa la njaa.
'' Baadhi ya wanasisa walizungumza Bungeni kutaka wananchi waruhusiwe kuuza chakula nje ya nchikwa kuwa kuna chakula cha kutosha leo hii hao hao wanatumia baadhi ya vyombo vya habari kutanga baa la njaa'' . KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe  na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka pamoja na Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa kuashiria ufunguzi wa barabara ya Barabara ya Bariadi-Lamadi yenye kilometa 71.8.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi yenye kilometa 71.8 wengine katika picha ni  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Luhaga Mpina, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, Mwenyekiti wa CCM Simiyu Titus Kamani na Mbunge wa Bariadi Andrew Chenge.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Bariadi kabla ya kufungua rasmi barabara ya Bariadi-Lamadi, katika mkoa wa Simiyu.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Bariadi mara baada ya kumaliza kufungua barabara ya Bariadi-Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8.

 PICHA NA IKULU

MISS UNIVERSE TANZANIA 2016 AONDOKA LEO KWA MASHINDANO

$
0
0
Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2017 Jihan Dimachk ameondoka leo alfajiri na ndege ya Oman Air kuelekea Manilla nchini Philipines kwa ajili ya kushiriki Mashindano ya Miss Universe. 
Jihan Dimachk aliyetwaa taji la Miss Universe Tanzania mapema mwezi Novemba mwaka jana anaenda kuiwakilisha Tanzania akiungana na wenzake kutoka nchi mbalimbali Ulimwenguni kuwania taji hilo. 
 Jihan Dimachk ameondoka akiwa amejiandaa vyema ikiwemo kisaikolojia, kimazoezi na kimavazi akishirikiana na wataalam mbalimbali kutoka hapa nchini. 
 Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications  ambaye pia ndio Mkurugenzi na Muandaaji mkuu wa Kitaifa wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai amewashukuru wadau mbalimbali kwa kujitoa na kushiriki katika kuhakikisha mrembo wetu anatayarishwa vyema. 
 Mrembo wa Miss Universe akikabidhiwa bendera ya Taifa na Bi.Joyce Hagu akimwakilisha mkurugenzi wa kitengo cha sanaa.
 
 Miss Univere Tanzania Jihan Dimachk akiwa na Miss Universe Kenya Marry Esther Were uwanja wa ndege wa JK Nyerere wakati wakisubiri ndege kwa ajili ya kuanza safari.(katikati yao ni matron/mlezi wa Miss Universe Tanzania Happy Kimbe akiwatakia baraka za mwisho na ushindi mwema.)
Washiriki wa shindano la Miss Universe Tanzania wakimtakia kila la kheri kinara wao katika mwendelezo wa mshindano haya.

HABARI KUTOKA TELEVISHENI LEO

Obama's Farewell Address to the American People

Viewing all 110153 articles
Browse latest View live




Latest Images