Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1504 | 1505 | (Page 1506) | 1507 | 1508 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Rais wa Marekani, Barack Obama amewaaga Wamarekani na ulimwengu mzima kwa ujumla ikiwa ni mara ya mwisho akiwa kama rais, katika hotuba iliyojaa hisia kubwa aliyoitoa mjini Chicago na kuwataka Wamarekani kuunganisha nguvu katika kuleta mabadiliko. Rais huyo ametokwa na machozi wakati akimshukuru mke wake Michelle Obama kwa namna alivyotoa mchango mkubwa katika utawala wake.

  Akihitimisha utawala wake katika Ikulu ya Marekani, Obama amerejea katika mji ambao sasa ni nyumbani kwake wa Chicago ambako kampeni yake ya "ndio tunaweza" ilianzia hapo na leo akisema "ndio tumeweza".

  Akiorodhesha mafanikio ya utawala wake kuanzia mkataba wa nyukilia na Iran hadi huduma ya bima ya afya, sehemu kubwa ya hotuba yake iliegemea katika kuwatia moyo wafuasi wake waloshtushwa na ushindi wa Donald Trump pamoja na kutathmini mafanikio aliyoyapata katika uongozi wake na mtazamo wake kuhusu wapi Marekani inaelekea .
  Obama amewataka Wamarekani kuamka, kupigania demokrasia lakini akaonya kuwa ubaguzi wa rangi na kukosekana kwa usawa bado ni kitisho kwa demokrasia. "Sisi sote bila ya kujali vyama, ni lazima turudi katika ujenzi wa taasisi ya demokrasia", amesema Obama.

  "Hivyo sisi kama wananchi, lazima tuwe macho dhidi ya uchokozi wa nje, ni lazima tuilinde misingi yetu inayodhoofika inayotutambulisha sisi ni akina nani. Ndio maana katika kipindi cha miaka nane iliyopita nimefanya kazi ya kuweka mapambano dhidi ya ugaidi katika misingi ya kisheria.
  Ndio maana tumemaliza mateso, kufanya kazi kulifunga gereza la Guantanamo, na mageuzi ya sheria zetu zinazosimamia ufuatiliaji wa kulinda faragha na uhuru wa raia. Na ndio maana mimi nimekataa ubaguzi dhidi ya Waislamu Wamarekani", amenukuliwa rais huyo.

  Miongoni mwa mafanikio mengine anayojisifia Obama ni pamoja na kuimarishwa kwa uchumi, kuhalilisha ndoa za jinisia moja, kufunguliwa kwa mahusiano ya kidiplomasia na Cuba na maenedeleo mengine.

  Mke wake Michele Obama na makamu wa rais Joe Biden na mke wake Jill ambao rais amewaelezea kama "familia" wamehudhuria hafla hiyo.

  Obama akifuta machozi machoni mwake amemshukuru mke wake Michelle akimuita ni rafiki yake mkubwa, mtoto wake Malia aliyekuwa akibubujikwa na machozi pamoja na Sasha ambaye hakuwepo. Akielezea mchango wa mke wake, Obama anasema,  "Michelle Lavaughn Robinson, msichana kutoka upande wa kusini, kwa miaka zaidi ya 20 iliyopita, umekuwa sio tu mke wangu na mama wa watoto wangu lakini rafiki yangu mkubwa.

  Ulichukua jukumu ambalo hukuuliza na ukalifanya kuwa lako kwa neema , ujasiri, mipango na ucheshi mzuri. Uliifanya Ikulu kuwa sehemu ya kila mtu."

  Anasema Marekani imekua bora na yenye nguvu duniani tangu alipokula kiapo kuiongoza nchi hiyo miaka nane iliyopita. Donald Trump atakayeapishwa Januari 20 anatarajiwa kuondoa baadhi ya yaliyofikiwa na karibu kiasi ya watu elfu 18 waliohudhuria hafla hiyo mjini Chicago walimshangilia rais huyo wakisema "miaka minne zaidi" na Obama akasema hawezi kufanya hivyo.

  Obama katika hotuba yake ya mwisho ameepuka kumkosoa Trump moja kwa moja na kulaani mgawanyiko ambao umezikumba siasa za taifa hilo.Imeandikwa na Mtandao wa DW
  Michelle Obama akimliwaza binti yake Milia ambaye alijikuta akitokwa na machozi wakati akisikiliza hotuba ya baba yake Rais Barack Obama
  Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden naye alijikuta akishindwa kujizuia na kutokwa na machozi
   Rais wa Marekani, Barack Obama akikumbatiana na Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden baada ya kumaliza hotuba yake.
  Michelle Obama akimkumbatia mumewe rais Barack Obama baada ya kumaliza hotuba yake. 
  Rais wa Marekani Barack Obama akimkumbatia binti yake Milia baada ya kumaliza hotuba yake. 

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kulia) wakiagana na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na wake zake, Mama Zakia Biala (wapili kushoto) na Asha Bilal (watatu kulia) wakati walipowatembelea nyumbani kwao eneo la Mbweni, Zanzibar Januari 10, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (watatu kushoto) wakizungumza na Makamu wa Rais Mstafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na wake zake, Mama Zakia Biala (kushoto) na Mama Asha Bilal wakati walipowatembelea nyumbani kwao eneo la Mbweni, Zanzibar Januari 10, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Salmin Amour wakati alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Kilimani, Zanzibar Januari 10, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Salmin Amour wakati walipomtembelea nyumbani kwake eneo la Kilimani, Zanzibar Januari 10, 2017.


  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla akiagiza vyumba vya wafanyabiashara vilivyofungwa na halmashauri vifunguliwe mara moja,na kuwarejeshea Wafanyabiashara kwenye meza ya mazungumzo na kuiondoa kesi baraza la Ardhi , RC Makala pia ametoa siku saba kwa Mkurugenzi wa halmshauri hiyo amalize Mgogoro wa kodi kwa kukaa meza moja na wafanyabiashara.

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amefanya ziara katika mji wa Mbalizi kwa kutembelea kituo cha mabasi na soko la mbalizi na baadaye kufanya mkutano wa hadhara na wafanyabiashara na wananchi wa mji wa Mbalizi.

  RC Makala pia alipata wasaa wa kusikiliza kero mbalimbali za Wafanyabiashara na Wananchi kwa ujumla,kufuatia malalamiko na kero za wafanyabiashara hao,RC Makala amemuagiza Mkurugenzi na baraza la Madiwani kuhakikisha ndani ya siku saba mvutano wa kodi ya pango la vyumba sokoni hapo uwe umekwisha kwa kupatiwa ufumbuzi.

  Aidha RC Makala pia amesikitishwa kwa namna ambavyo Mgogoro huo umeachwa kwa muda mrefu bila kushughulikiwa na kusababisha mvutano mkubwa na kupelekea halmashauri kushtakiwa kwa baraza la Ardhi

  Rc Makala ameagiza uongozi wa halmashauri na Mamlaka ya mji Mdogo wa Mbalizi kusimamia usafi.Wananchi na wafanyabiashara wameshukuru na kupongeza uamuzi wa Mkuu wa Mkoa na wameahidi kuitoa kesi hiyo Mahakamani na kukaa katik meza ya mazungumzo na halmashauri kumaliza mvutano wa pango la Vibanda vya biashara.
  Baadhi ya wakazi na wafanyabishara wa soko la Mbalizi wakitoa kero zao kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alipo fanya ziara katika Stendi ya Mabasi na Soko la Mbalizi Mkoani Mbeya.
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara na wafanyabishara na wananchi wa Mji mdogo wa Mbalizi Mkoani Mbeya.HABARI PICHA NA MR PENGO-MMG MBEYA

  0 0

  Na. JOVINA BUJULU – MAELEZO

  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imefanikiwa kukamilisha mkakati wa kitaifa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza wa mwaka 2013-2020.

  Hayo yamesemwa jiji Dar es salaam na Mkurugenzi wa magonjwa yasiyoambukizwa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Profesa Ayoub Magimba.

  Profesa Magimba amesema kuwa mkakati huo ni muendelezo wa utekelezaji wa maazimio ya vikao vya 66 na 68 vya Umoja wa Mataifa vilivyofanyika mwaka 2015 na 2016 ambapo Tanzania iliridhia kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

   “Katika kuimarisha huduma za kinga kwa magonjwa hayo, Serikali inatoa elimu kwa wananchi na kuwahimiza kufanya mazoezi, kupunguza matumizi mabaya ya pombe na sigara na kuhamasisha upimaji wa afya angalau mara mbili kwa mwaka,” alisema Profesa Magimba. 

  Aliongeza kuwa mkakati huo  ambao umesambazwa nchi nzima kupitia kwa Waganga Wakuu wa Mikao yote unaainisha mikakati tofauti yenye malengo yanayoendana na malengo endelevu ya maendeleo ya melenia.

  “Serikali imeimarisha tiba katika vituo vyote vya kutolea huduma kwa kuhakikisha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na wataalamu, na kuimarisha huduma za Kibingwa za magonjwa ya moyo katika Taasisi za Bugando, KCMC, JKCI na ORCI,” Alisisitiza.

  Profesa Magimba aliyataja magonjwa yasiyoambukiza kuwa ni pamoja na Saratani, magonjwa ya Moyo, magonjwa sugu ya njia ya hewa, Selimundu, magonjwa ya akili, Figo, Kisukari na baadhi ya magonjwa ya macho.

  Akitolea mfano athari za magojnwa hayo, Profesa Magimba alisema kuwa utafiti uliofanywa katika ya mwaka 1994 – 2002 ulionyesha kuwa asilimia 18-24 ya vifo vilitokana na magonjwa yasiyoambukiza. 

  Shirika la Afya Duniani lilikadiria kuwa asilimia 20 ya vifo vyote vilivyotokea hapa nchini mwaka 2005 vilitokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

  Takwimu zinaonyesha kuwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni tatizo la kimataifa ikijumuisha nchi za Afrika na nchi zinazoendelea.  Magonjwa hayo yamesababisha vifo million 36 duniani sawa na asiliamia 63 kwa kipindi cha mwaka 2008.


  0 0

  Benki ya KCB Tanzania yatoa mafunzo kwa ajili ya wanawake wajasiriamali inayoitwa 2JIAJIRI. Programu hii inalenga kumkomboa mwanamke mjasiriamali kutoka katika matatizo yanayosababisha biashara yake ishindwe kuendelea. Programu hii itaongeza ajira nchini kwa wanawake na hivyo biashara zao zitapanuka na kuwa na uwezo wa kuajiri wengine. 

  Mafunzo haya yataendeshwa na wataalamu kutoka Tanzania Entrepreneurship and Competitiveness Center -TECC waliobobea katika masuala ya kijasiriamali, kifedha na ushindani wa biashara

  “Mpango huu ni endelevu na tumepanga kufundisha wajasiriamali 315 nchi nzima. Leo tunafundisha wajasiriamali 100 katika makundi mawili tofauti. Mafunzo haya ni bure kabisa, KCB Bank itagharimia gharama zote. Tunachokihitaji kutoka kwao ni mahudhurio ya siku zote tatu na usikivu wa hali ya juu.” Alisema Godfrey Ndalahwa, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB.

  Bw. Ndalahwa aliendelea kwa kusema kuwa mafunzo hayo yatafanyika mikoa yote ambako benki ya KCB ina matawi, Dar Es salaam, Mwanza, Morogoro, Arusha, Moshi na pia Zanzibar. Na tunalenga wanawake wajasiriamali wadogo na wa kati ambao tayari wanaendesha biashara lakini wanataka kuziimarisha zaidi. 

  Lengo ni kuwawezesha kudhibiti vipengele vya uzalishaji na mgawanyo wa mapato na faida {control over factors of production and distribution of income and benefits) lakini zaidi ni kuwawezesha kuyatawala maisha yao kiuchumi na kijamii. 

  “Matatizo tunayotarajia kutatua kutoka kwa wanawake wajasiriamali ni elimu ya kifedha, kufikia huduma za kifedha, Ukosefu wa dhamana, kutokujua vizuri masuala ya kisheria, uelewa finyu wa sera za serikali na kiuchumi, njia hafifu za kuendesha biashara endelevu, ukosefu wa mtaji na utaalamu wa kuanzisha biashara kubwa” alisema.

  Mkurugenzi aliongeza kwamba baada ya mafunzo hayo benki itawapatia wanawake wajasiriamali hao maafisa watatu watakaotembelea bishara zao na hii ni kwa wale tu ambao watahudhuria mafunzo ya siku tatu yote na kuonyesha nia ya kubadilika/kuendelea kibiashara). Maafisa hao watakua ni afisa fedha, afisa sheria na afisa masoko.

  Alimaliza kwa kuwaambia wanawake wajasiriamali “JIULIZE KWANINI uhangaike wakati benki ya KCB tupo!”
  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Tanzania Godfrey Ndalahwa akizungumza na baadhi ya wanawake waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na benki hyo mkoani Dar es salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Tanzania Godfrey Ndalahwa, akiongea na wanawake wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na benki hyo mkoani Dar es salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Tanzania Godfrey Ndalahwa, akiongea na wanawake wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na benki hyo mkoani Dar es salaam. 
  Baadhi ya wanawake wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yalitolewa na Benki ya KCB mkoani Dar es salaam. 

  0 0

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,SACP,Wilbroad Mutafungwa (kushoto mwenye fimbo) akizungumza jambo wakati akikagua maenedeleo ya ujenzi wa kituo cha Polisi cha Kimanganoni Uru wilaya ya Moshi. 
  Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro akikagua ujenzi wa kituo cha polisi kinachojengwa kwa nguvu za wananchi eneo la Uru Kimanganoni kati. Kushoto ni askari mstaafu,mkazi eneo hilo Philipo mushi akimpokea Mutafungwa .Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  Na Judith Mhina – MAELEZO
  “Wakati umefika wa kujenga makumbusho ya Taifa ya Mapinduzi ya Zanzibar, ili kizazi cha sasa na kijacho waweze kujifunza na kuipitia historia muhimu kwa Watanzania na wageni kutoka nje. 

  Hayo ni maneno ya msingi ambayo yamesemwa na Dkt Mohammed Seif Khatibu wakati wa mahojianno yake na Idara ya Habari MAELEZO mapema mwishoni mwa wiki. 

  Dkt Khatib alisisitiza “Ni vema kuonesha katika picha, maandishi na sura halisi za historia ya Zanzibar kabla yaani wakati wa Waajemi, Wareno, Waarabu, Waingereza na sasa Serikali ya Mapinduzi”. 

  Dhamira ya makumbusho hayo, Dkt. Khatib amesema “Vijana wengi ukiwaambia nchi hii kulikuwa na unyanyasaji wa Waafrika hawakubali maana hawajui historia, waelezwe kwa nini tuko huru, kuna wasioitakia mema Zanzibar wanapotosha historia hiyo”.

  Kumbe kwa kuweka makumbusho na usahihi wa historia ya nyuma kabla, wakati, baada ya Mapinduzi na yanayotokea sasa, hayo yote yakiwa katika makumbusho yatakuwa msingi wa historia ya Zanzibar hatua ambayo itasaidia kuwekwa wazi mambo yaliyowahi kutokea, hivyo sio rahisi kwa mtu yoyote ambaye ana agenda ya kupotosha umma kufanya hivyo.

  Lakini kwa sasa ni kweli kabisa mtu yoyote anaweza akasema vyovyote atakavyo kwa kuwa hawajui historia na wala hawana mahali pa kurejea historia ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

  “Watu walitoka Kongo, Malawi, Kigoma na Tabora wakibebeshwa pembe za Ndovu na kusafiri kwa mguu,  wakifuata njia ya reli ya kati, mpaka Bagamoyo na  kusafirishwa na boti mpaka Unguja na kuwekwa sokoni kuuzwa kama samaki katika soko la watumwa. Huu ndio ukweli” alisema Dkt Khatib.

  Tuchukulie mfano wa jirani zetu Rwanda walikubwa na mauaji yakimbari mwaka 1994, kwa kutambua kuwa hicho siyo kitu kizuri kutokea tena hapa duniani wameona waweke makumbusho ya kitaifa. Inahuzunisha lakini ndio ukweli, unapoona yale mafuvu ya vichwa yalivyopangwa huwezi kuamini kama hiyo ni hali halisi iliyotokea hapa duniani. 

  Kwa Wanyarwanda na watu wengine duniani, makumbusho kimbari ni sehemu ya Utalii ikizingatia msemo wa waswahili wanasema kuona ni kuamini.

  Siyo hiyo, tu hata kule Namibia kuna jumba la makumbusho la mauaji yaliyofanywa na wajerumani kwa kabila la Waherero waliuwawa katika vita ya kwanza ya dunia. Takribani Waherero nusu ya milioni waliuwawa na hivi karibuni Waherero wa Namibia walikuwa wanaomba fidia kwa Serikali ya Ujerumani, ingawa Ujerumani wameomba msamaha kwa mauaji hayo ya kimbari.

  Uingereza ni nchi inayoongoza duniani kwa kuweka kumbukumbu zake katika makumbusho za Kifalme, Kimataifa, Kitaifa, Vita, Silaha, Bahari, Mtu Binafsi, Jiji au Mji husika. Uingereza ina zaidi ya makumbusho 55 ambayo yanafahamika duniani.  

  Mfano  “British Museum London, Natural History Museum London, National Gallery London, Science Museum London, Victoria and Albert Museum, National Maritime Museum, Museum of London City, National Portrait Gallery, National Army Museum,  Sir Johns Soanes Museum, Wallace Collection London, National War Museum nk”

  Hivyo, tuunge mkono wazo hilo na tushirikiane wote kama Watanzania kuhakikisha kituo hicho cha makumbusho kinajengwa na kuhifadhi kila kinachohitajika ili kukamilisha historia husika. 

  Kujengwa kwa kituo cha makumbusho Zanzibar kitasaidia kuingizia fedha kama sehemu ya Utalii wa historia ambapo mtu anayehitaji kuijua historia hiyo atapata kila kitu mahala pamoja bila kusumbuka.  Mungu ibariki Tanzania “MAPINDUZI DAIMA”.


  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Nyamikoma Wilayani Busega wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Simiyu kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Kisesa mkoani Mwanza wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Simiyu kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Magu mkoani Mwanza wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Simiyu kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi.
  . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli mara baada ya kushuka kwenye kivuko cha Mv Misungwi wakati akitokea Chato mkoani Geita. PICHA NA IKULU

  0 0

   Uoto wa asili wa aina mbalimbali unavyoonekana wakati unapoanza safari ya kuelekea kituo cha Kibo ukitokea kituo cha Horombo. 
   Mawe yenye michoro mithili ya mistari ya Pundamilia yanaonekana katika eneo lijulikanalo kama Zebra Rocks. 
   Kwa mbali ni muonekano wa vibanda viwili maalumu kwa ajili ya kujisaidia ambavyo viko njiani wakati unaelekea Kibo Hut ,eneo hili linajulikana kama Last woter Point ni eneo la mwisho linaloonekana kuwa na maji. 

   Ndege wakubwa aina ya Kunguru mwenye baka jeupe shingoni wanaonekana katika maeneo haya wakisubiri mabaki ya chakula kutoka kwa wageni wanaopanda Mlima Kilimanjaro. 


  0 0
 • 01/11/17--03:55: BEI YA MADAFU LEO


 • 0 0


  Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Yusuph Singo Omari

  0 0

   Na  Lilian Lundo - MAELEZO

  Mamlaka ya Elimu Tanzania Tanzania (TEA) imetiliana saini na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mkataba wa ujenzi wa uzio katika hosteli za Mwalimu J.K. Nyerere Kampasi ya Mlimani.

  Mradi huo umedhaminiwa na TEA kupitia Mfuko wa Elimu (Education Fund) utakaogharimu jumla ya shilingi 496,646,868 hadi kukamika kwa ujenzi huo.

  Mkataba huo umesainiwa leo  Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Graceana Shirima na Makamu Mkuu wa Chuo cha UDSM Profesa Rwekaza Mukandala wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

  Alisema kuwa utekelezaji mradi huo unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 12 ijayo.Kwa upande wake Prof. Mukandala aliwashukuru TEA kwa msaada huo na kuongeza kuwa ujenzi wa uzio hizo ni suluhisho kubwa kwa wanafunzi watakaoishi katika eneo la kampasi hiyo.

  Alisema kuwa uzio utasaidia kuimarisha usalama wa wanachuo na mali zao kutokana na kuwepo eneo ambalo lina mzunguko mkubwa wa watu unaotokana na stendi ya mabasi ya simu 2000 , maduka ya Mlimani City pamoja na viwanja hivyo kutumika kama njia ya mkato na vijiwe kwa watu wasio na kazi.

  TEA tayari imefadhili miradi mbalimbali Chuo Kikuu cha UDSM ikiwemio ujenzi wa vyumba vya mihadhara, ununuzu wa vitabu vya kiada, vifaa kwa ajili ya wanafunzi kwenye mahitaji maalum, ufadhili wa kozi za "Pre Entry" kwa wanafunzi wa like katika masomo ya sayansi, ununuzi wa mitambo na vifaa vya Tehama

  0 0

   Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi wa shule maalumu ya msingi ya Mundindi wilayani Ludewa Mkoani Njombe, Yohana Mwaifuge(katikati) akipokea moja ya msaada toka kwa Meneja wa Vodacom Tanzania wa Mkoa huo, Benedict Kitogwa aliyekabidhi msaada huo jana  kwa niaba ya Vodacom Tanzania Foundation.Msaada huo wenye thamani ya shilingi Milioni 15/- ni Vyakula,Sabuni, Magodoro pamoja na mablanketi.
   Meneja wa Vodacom Tanzania Mkoa wa Njombe, Benedict Kitogwa(kushoto) akimsalimia mtoto mwenye ulemavu wa macho wa shule maalumu ya Mundindi wilayani Ludewa Mkoani humo, Robert Lwaizala wakati alipotembelea shule hiyo jana  kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali wenye thamani ya shilingi Milioni 15/- kwa niaba ya Vodacom Tanzania Foundation.
  Baadhi ya watoto wanaosoma katika  shule maalumu ya Mundindi wilayani Ludewa Mkoani Njombe, wakila chakula cha mchana na Meneja wa Vodacom Tanzania wa mkoa huo, Benedict Kitogwa(katikati)baada ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali jana kwa niaba ya Vodacom Tanzania Foundation wenye thamani ya shilingi Milioni 15/- kama vile Vyakula, Sabuni, Magodoro pamoja na mablanketi.


  0 0

  NA VICTOR MASANGU, MAFIA  

  WAKATI serikali ya awamu ya tano ikiwa ni mpango wa kuhakiisha inajenga zahanati katika kila kijiji katika nchi nzima wananchi katika baadhi ya maeneo mengine wanakabiliwa na  changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa vifaa tiba, madawa, wauguzi, madaktari  pamoja na huduma ya upatikanaji wa mashine ya X-Ray  hali inayopelekea  wagonjwa kushindwa kupatiwa matibabu kwa wakati unaotakiwa.

  Changamoto hizo zimebainika baada ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo wakati wa ziara yake ya kikazi  katika Wilaya ya Mafia iliyopo Mkoani Pwani  kwa ajili ya kuweza kukagua shughuli mbali mbali za miradi ya  kimaendeleo ikiwa pamoja na   kuweza kubaini changamoto  na matatizo yanayokakabili wananchi.

  Naibu Waziri Jafo mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku moja ameweza kuzungumza na watumishi na kusema kwamba amesikitishwa sana na hali  inayowakabili wananchi wa Mafia hususan katika sekta ya afya kwani kwa sasa  wapo katika wakati mgumu kutoka na na kukosa huduma ya mashine ya X-Ray kwa kipindi cha miezi sita sasa hivyo kuwalazimu baadhi ya wagonjwa kwenda kupatiwa matibabu Jijini Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa boti au ndege.

  “Kwa kweli mimi kama kiongozi wenu hili jambo la wananchi wa Wilaya ya Mafia kutokuwa na huduma ya X-Ray sio sahii kabisa hata kidogo yani wataalamu ndani ya miezi mitatu mmeshindwa kulitafutia ufumbuzi wakati wananchi wanaendelea kupata tabu na ukizingatia mtu akiumwa wakati yupo huku mafia inakuwa ni vigumu sana kumsafirisha kwenda Dar es Salaam kutibiwa, na ukizingatia gharama yenyewe ni kubwa”alisema Jafo kwa masikitiko.
  Jafo alisema kwamba kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo ya ukosefu wa  huduma ya X-ray aliahidi kulishughulikia kwa hali na mali ili  kuweza kuwasaidia wananchi wa Mafia waweze kupatiwa matibabu yanayostaili na sio kupata tabu wakati serikali yao ipo kwa ajili ya kuweza kuzitatua changamoto walizonazo.

  Kwa upande wake  Mganga mkuu wa Wilaya ya Mafia Joseph Mzimbe amekiri kuwepo kwa tatizo hilo la kutokuwa kwa huduma ya X-Ray na kudai kwa sasa wagonjwa wengine pindi wanapohitaji huduma hiyo wanashindwa kufanyiwa vipimo kutoka na gharama ya usafiri kutoka Mafia hadi kupelekwa katika hospitali zilizopo  Dar es Salaam ni kubwa

  Naye mmoja wa wananchi aliyejitambulisha kwa jina la Hamisi Mshilazi  akizungumza kwa niaba ya wenzake,amesema kuwa mashine hiyo ya X-ray  kwa upande ni tatizo sugu kutokana na kuharibika mara kwa mara hivyo kuzolotesha utoaji wa huduma kwa wagonjwa na kubainisha gharama ya usafiri  wa boti na ndege ni kubwa hivyo wanajikuta  baadhi yao wenye kipato cha chini wanashindwa  kwenda  kupelekwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi katika hospitali ya Taifa ya  Muhimbili.

  Riziki Mngwari  yeye ni Mbunge wa viti maalumu ambaye anaiwakilisha Wilaya ya Mafia Mkoa wa Pwani kupitia  (CUF) ambaye alikuwepo katika ziara hiyo hakusita kutoka kilio chake kwa serikali ya awamu ya tano katika kuwaboreshea huduma ya afya  wananchi eneo hilo kwani wanateseka sana katika kupatiwa matibabu yanayostahili.

  WANANCHI wa Wilayani ya Mafia Mkoa  Pwani  kwa sasa hawana  huduma yoyote ya mashine ya X-ray hivyo kuwalazimu baadhi ya wagonjwa kutumia gharama kubwa kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu zaidi katika hopsitali zilizipo Jijini Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa ndege au kwa boti ambayo kutokana na gharama yake kuwa ni kubwa wanashindwa kuimudu hivyo kunahitajika juhudi za makusudi kutoka serikalini ili kuweza kuboresha sekta ya afya.
   Naibu Waziri ofisi ya Rais Tamisemi Seleman Jafo akiwasili katika uwanja wa ndege wa Mafia Mkoani Pwani kwa ajii ya ziara yake ya kikazi kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo na kuweza kubaini changamoto za wananchi zinazowakabili.
    Naibu Waziri Ofisi ya Rais Seleman Jafo akisaliamina na baadhi ya viongozi na watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Mafia Mkoani Pwani mara baada ya kuwasali kwa ajili ya kuendelea na ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo
  Naibu Waziri akizungumza na baadhi ya watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Mafia wakiwemo walimu wa sekondari  hawapo pichani wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo Wilayani humo,(PICHA NA VICTOR MASANGU)

  0 0
 • 01/11/17--05:41: TANZIA
 • 0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.


  WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amesema wanatarajia kufanya mapitio ya sheria zinazohusu sekta ya sanaa na burudani nchini ili kutoa fursa kwa taasisi binafsi kuwekeza zaidi.

  Katika kufanya mapitio hayo wataangalia jinsi ya kufanyia kazi sheria mbovu zinazokandamiza sekta ya sanaa na burudani nchini na kuziondoa kabisa ili kuleta manufaa kwa wasanii na wadau wanaohusika na sanaa.

  Nape ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua rasmi urushwaji wa matangazo ya Kombe la mataifa Afrika (AFCON) pamoja na kumkabidhi bendera kwa msanii wa Bongofleva Nasib Abdul(Diamond Platnum) anayekwenda kutumbuiza katika ufunguzi wa mashindano hayo yatakayofanyika Januari 14 nchini Gabon.

  Amesema wasanii na watu wengine kwenye sanaa wamekuwa wakifanya kazi kwa juhudi kubwa licha ya kutofaidika na kazi wanazozifanya na hatimaye wakijikuta wakiwa chini kadri siku zinavyozidi kwenda mbele.

  Amesema serikali imedhamiria kushughulikia masuala yote yanayofanya wasanii na wadau wngine kuwa wanyonge kutokana na uwepo wa sheria hizo.

  ‘Natambua Kampuni ya Multichoice kupitia king’amuzi chake cha DStv katika kuhakikisha wanakuza na kuendeleza masuala ya michezo na burudani nchini, na sisi kuonesha tunaunga mkono jitihada zao tutapitia sheria zote ambazo zimekuwa ni kikwazo kwenye ukuzaji tasnia ya sanaa hapa nchini’ amesema Nape.

  Nape alimpongeza Diamond Platnum kwa kupata nafasi ya kwenda kutumbuiza katika mashindano hayo na kudai kuwa kitendo hicho kinaipa faraja Tanzania licha ya kuwa hawajapeleka timu katika mashindano hayo makubwa barani Afrika.

  Nae Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Salum Salum amesema watanzania wataweza kujioneamashindano hayo Mubashara kutoka nchini Gabon kupitia king’amuzi chao cha DStv kwenye kifurushi cha bei ya chini cha Shilingi 19,975 pekee.

  Amesema kampuni hiyo itagharamia tiketi za watu sita kutoka kundi la WCB ili kufanikisha adhma ya msanii Diamond Platnum kufanya shoo yenye uwezo wa kuijulisha dunia kuwa Tanzania inavipaji vingi vya uimbaji mziki licha ya kutopewa sifa katika baadhi ya maeneo mengine.

  Aidha Salum amesema mashindano yatakuwa yakionyeshwa mubashara(Live) ili kuweza kutoa fursa ya watanania na kujikita zaidi kwenye michezo ili na wao wapate nafasi ya kushiriki mashindano hayo katika kipindi cha miaka ijayo.
  Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi bendera kwa msanii wa Bongofleva Nasib Abdul(Diamond Platnum) anayekwenda kutumbuiza katika ufunguzi wa mashindano hayo yatakayofanyika Januari 14 nchini Gabon iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
  Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye, akimkabidhi bendera msanii wa Bongofleva Nasib Abdul(Diamond Platnum) anayekwenda kutumbuiza katika ufunguzi wa mashindano yatakayofanyika Januari 14 nchini Gabon iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Salum Salum akizungumza wakati hafla ya kumkabidhi bendera msanii wa Bongofleva Nasib Abdul(Diamond Platnum)anayekwenda kutumbuiza katika ufunguzi wa mashindano yatakayofanyika Januari 14 nchini Gabon iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Msanii wa Bongofleva Nasib Abdul(Diamond Platnum) anayekwenda kutumbuiza katika ufunguzi wa mashindano yatakayofanyika Januari 14 nchini Gabon akizungumza na waandishi habari juu ya safari hiyo leo jijini Dar es Salaam.
  Balozi DSTV, Joti akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi bendera msanii wa Bongofleva Nasib Abdul(Diamond Platnum) anayekwenda kutumbuiza katika ufunguzi wa mashindano yatakayofanyika Januari 14 nchini Gabon iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Ofisa habari Mufindi.

  Naibu Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh. Angelina Mabula, amesema serikali ya awamu ya tano imedhamilia kwa dhati kupunguza kwa asilimia kubwa kama si kuondosha kabisa kero ya migogoro ya ardhi nchini ili kuondokana malumbano yanayozikabili jamii nyingi hapa nchini.

  Mh. Mabula ameyasema hayo mjini Mafinga wakati wa ziara ya kikazi aliyofanya Wilayani Mufindi akiwa na lengo la kukagua masuala mbalimbali yaliyo chini ya wizara yake sanjari na kusikiliza kero za wananchi zinazohusiana na migogoro ya ardhi.

  Amesema kwa muda mrefu jamii nyingi hapa nchini zimekuwa katika migogoro ya kugombea ardhi, jambo ambalo linachochea mafarakano miongoni mwa wananchi hivyo serikali ya awamu ya tano imejidhatiti kuhakikisha inapunguza au kuondosha kabisa migogoro iliyopo na akatoa rai kwa wakurugenzi wa halmshauri kuhakikisha wanasimamia vema masuala ya ardhi ili kuzuia kuibuka kwa migogoro mipya.

  Aidha, amemtaka Mkurugenzi mtendaji wa Mji wa Mafinga kuhakikisha anarasimisha makazi ya wakazi wa kata ya Kinyanambo iliyopo mjini Mafinga kwa kuhakikisha kuwa makazi yao yanapimwa na wanapatiwa hati ili wamiliki maeneo yao kisheria jambo ambalo litawafanya waishi kwa kujiamini katika maeneo yao lakini pia waweze kuzitumia hati hizo kama dhamana katika taasisi za kifedha.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akiongea na wananchi katika ukumbi wa CCM mjini Mafinga kabla hajaanza kusikiliza kero zao.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akikagua mfumo wa kielektroniki wa wamiliki wa ardhi alipotembelea ofisi za ardhi Wilayani Mufindi.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William mara baada ya kukagua mfumo unaohifadhi takwimu za wamiliki wa ardhi Wilayani Mufindi.

  0 0

  #LakeFm Habari
  Wakazi wanaoishi maeneo ya mijini nchini wamehimizwa kujikita kwenye kilimo cha mbogamboga kwa kutumia masalia ya makopo na mifuko ya aina mbalimbali ili kuondokana na uchafunzi wa mazingira.

  Mwanamama Victoria Buzare ambaye ni mjasiriamali kutoka Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza, ameyasema hayo wakati akizungumza na Lake Fm huku akiongeza kwamba kilimo hicho pia kinawaepusha wanajamii na athari za kutumia mbogamboga zenye kemikali.

  Amesema kilimo hicho kinagharimu mtaji kidogo hadi shilingi 5,000 ambazo mkulima anaweza kulima aina tatu za mbogamboga ikiwemo sukumawiki, nyanya chungu, biringanya na nyinginezo.

  Buzare amewashauri wanafamilia wote wanaoishi mijini kuhakikisha wanakuwa na bustani za makopo na mifuko kwani ni salama kwa matumizi ya chakula na pia rahisi kusimamia ikizingatiwa ndoo moja ya maji kwa siku inatosheleza mahitaji yake.
  Kwa maoni na ushauri ama swali, wasiliana na Victoria Buzare (pichani) kwa nambari za simu 0754 21 85 55.


  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimwa Samia Suluhu Hassan ameuagiza uongozi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) uchangamkie fursa za uwekezaji wa ujenzi wa nyumba za makazi Tanzania Bara hasa kwenye Makao Makuu ya nchi Dodoma hatua ambayo itauwezesha mfuko huo kuongeza maradufu mtaji wake kwa uuzaji wa nyumba hizo.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati anaweka jiwe la msingi katika mradi mkubwa wa ujenzi wa nyumba 252 za makazi katika eneo la MBWENI kisiwani Unguja ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Makamu wa Rais amesema kutokana na kazi kubwa na nzuri inayofanywa na mfuko huo wa ZSSF hasa ujenzi wa nyumba za makazi ya wananchi ni muhimu kwa mfuko huo kuangalia namna bora ya kwenda kuwekeza katika mikoa mbalimbali ya Tanzania bara kutokana maeneo mengi kuwa na mahitaji makubwa ya nyumba za makazi.

  Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema ujenzi wa nyumba za makazi Tanzania Zanzibar ulitokana na fikra na ahadi za hayati mzee Karume kupitia ASP wakati wa haraka za kudai uhuru za kuhakikisha wananchi wanapata makazi bora ya kuishi katika kisiwa cha Pemba na Unguja kutokana na idadi kubwa ya wananchi katika kipindi hicho kuishi katika mazingira yasiyoridhisha.

  “Miradi yote hii ni katika kuenzi utekelezaji wa kauli ya Mapinduzi Daima yanayotaka kuleta maendeleo yanayoonekana kwa wananchi kila uchao hususani kipindi hiki tunapotimiza miaka 53 ya Mapinduzi yetu ya Matukufu ya Zanzibar”

  Makamu wa Rais pia amewahimiza wananchi wote wachangamkie fursa za kununua na kumiliki nyumba kwa bei nafuu na zenye miundombinu ya kisasa na huduma zote za kijamii ikiwemo viwanja vya michezo.

  Kuhusu umiliki wa nyumba kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameziagiza Wizara zinazoshughulika na masuala ya ardhi Tanzania Bara na Zanzibar kutoa ufafanuzi au tafsiri sahihi ya sheria zinazoongoza masuala ya ardhi na umiliki wa nyumba ili kuondoa sintofahamu iliyopo kuhusu wana diaspora kumiliki nyumba.

  Amesisitiza kuwa Serikali zote mbili zimekuwa zikisisitiza wana diaspora kuchangia maendeleo ya nchi na kutumia fursa mbalimbali zilizoko nyumbani ikiwemo kununua nyumba zinazojengwa na mifuko na mashirika mbalimbali hivyo ni muhimu kwa wizara zinazoshughulikia masuala ya ardhi kutoa maelekezo haraka ili kuondoa sintofahamu iliyopo kwa sasa kuhusu wana diaspora kulimiki nyumba kwa ajili ya makazi.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema ni muda muafaka sasa hivi kwa mifuko hiyo kuwekeza katika sekta ya viwanda hasa kwenye miradi yenye tija kwani viwanda vitatoa fursa kwa vijana wengi kuajiriwa na kuongeza kipato na kuongeza huduma za kijamii na kupunguza umaskini kwa wananchi.

  Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipngo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Khalid Salum Mohamed amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa Serikali hiyo inaendelea kumuezi Mzee Karume kwa vitendo kwa kujenga nyumba za makazi na kukarabati nyumba zilizopo ili kuhakikisha wananchi katika Kisiwa cha Pemba na Unguja wanapata makazi bora ya kuishi.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba 252 za makazi zinazojengwa na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) zilizopo Mbweni, Zanzibar ikiwa moja ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia mara tu alipoweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba 252 za makazi zinazojengwa na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) zilizopo Mbweni, Zanzibar ikiwa moja ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi.


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiwa ndani ya moja ya nyumba hizo 252 mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba hizo za Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) zilizopo Mbweni, Zanzibar ikiwa moja ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiangalia ramani ya ujenzi wa nyumba 252 za makazi zinazojengwa  na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) zilizopo Mbweni, Zanzibar ikiwa moja ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi.

  Pichani ni Nyumba za makazi zinazojengwa na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) zitakazokuwa na nyumba 252, Viwanja vya Michezo kwa Watoto,Sehemu ya kuogelea na Ukumbi mkubwa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akfurahia jambo na wanafunzi waliojitokeza kushuhudia uwekaji wa  jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba 252 za makazi zinazojengwa na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) zilizopo Mbweni, Zanzibar ikiwa moja ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi.


  0 0

  Rais Dkt. John Pombe Magufuli.


older | 1 | .... | 1504 | 1505 | (Page 1506) | 1507 | 1508 | .... | 3348 | newer