Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110129 articles
Browse latest View live

MKURUGENZI TAASISI YA ILTC YA JIJINI MWANZA AOMBA SERIKALI KUZISAIDIA TAASISI BINAFSI ZA ELIMU

$
0
0
Na George Binagi-GB Pazzo
Taasisi ya lugha ya International Language Traing Centre iliyopo Isamilo Jijini Mwanza, imeiomba serikali kuzisaidia taasisi binafsi za kelimu nchini ili kutimiza vyema wajibu wake.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Mwalimu Charles Mombeki (pichani), ameyasema hayo wakati akizungumza na Lake Fm ya Mwanza na kuomgeza kwamba ikiwa serikali itafanya hiyo, itazisaidia taasisi hizo kutekeleza vyema wajibu wa kutoa elimu bora kwa wananchi.
Amesema si vyema serikali kuzifungia taasisi binafsi za kielimu ikiwemo shule na vyuo pindi zinapokabiriwa na changamoto za kielimu badala yake inaweza kuzisaidia katika kuondokana na changamoto hizo.
Taasisi ya International Language Training Centre inajihusisha na uendelezaji wa lugha mbalimbali ikiwemo lugha za asili, Kiswahili, kiingereza, kifaransa na nyinginezo.
Bonyeza hapa kusoma zaidi

HABARI KUTOKA TELEVISHENI LEO

NEWS ALERT:WATU KUMI WATIWA MBARONI KWA KUMCHAPA VIBOKO MWANAMAMA RORYA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMTEMBELEA MAMA FATMA KARUME

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mjane wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mpinduzi ya Zanzibar, Mama  Fatma Karume wakati alipomtembelea nyumbani kwake  eneo la    Maisara Zanzibar Januari 10, 2017.    (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakizungumza na mjane wa Rais wa kwanza wa serikali ya  Mapinduzi ya Zanzibar, Mama Fatma Karume  (katikati wakati walipomtembelea nyumbani kwake eneo la Maisara mjini Zanzibar Januari 10, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na mjane wa Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi   ya  Zanzibar, Mama Fatma Karume wakati alipomtembelea nyumbani kwake, eneo la  Maisara, Zanzibar, Januari 10, 2017.
  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa  akisalimiana na  Mjane wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mama Fatma Karume wakati yeye na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa walipomtembelea nyumbani kwake   ENEO LA  Maisara Zanzibar  Januari 10, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary  wakiongozana na Mjane wa Rais wa Kwanza wa  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mama Fatma Karume  kutoka  ndani  wakati walipomtembelea  mama huyo nyumbani kwake eneo la Maisara mjini Zanzibara, Januari 10, 2017. 

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS DKT. MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KUZAMA WATU 12 BAHARINI TANGA

POLISI YAPIGA MARUFUKU 'TINTED' KWENYE KIOO CHA MBELE CHA GARI

SERIKALI YA AWAMU YA TANO IMEZAMILIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI NCHINI - MABULA

$
0
0
Na Ofisa habari Mufindi

Naibu Waziri  Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula amesema serikali ya awamu ya tano imedhamilia kwa dhati kupunguza kwa asilimia kubwa kama si kuondosha kabisa kero ya migogoro ya ardhi nchini ili kuondokana na malumbano yanayozikabiri jamii nyingi hapa nchini.

Mh. Mabula ameyasema hayo mjini Mafinga wakati wa ziara ya kikazi aliyofanya wilayuani humo akiwa na lengo la kukagua  masuala mbalimbali yaliyo chini ya wizara yake sanjari na kusikiliza kero za wananchi zinazohusiana na migogoro ya ardhi.

Amesema kwa muda mrefu jamii nyingi hapa nchini zimekuwa katika migogoro ya kugombea ardhi, jambo ambalo linachochea mafarakano miongoni mwa wananchi, hivyo serikali  imejizatiti kuhakikisha inapunguza au kuondosha kabisa migogoro iliyopo na akatoa rai kwa wakurugenzi wa halmshauri kuhakikisha wanasimamia vema masuala ya ardhi ili kuzuia kuibuka kwa migogoro mipya.

Aidha, amemtaka Mkurugenzi mtendaji wa Mji wa Mafinga kuhakikisha anarasimisha makazi ya wakazi wa kata ya Kinyanambo iliyopo mjini Mafinga kwa  kuhakikisha kuwa makazi yao yanapimwa na wanapatiwa hati ili wamiliki  maeneo yao kisheria ili waishi kwa kujiamini katika maeneo yao lakini pia waweze kuzitumia hati hizo kama dhamana katika taasisi za kifedha. 
  Mh. naibu waziri akiwa Angelina Mabura akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri  William mara baada ya kukagua mfumo unaohifadhi takwimu za wamiliki wa ardhi Wilayani Mufindi
 Naibu Waziri Mhe. Angelina Mabura akikagua mfumo wa  kielektroniki  wa wamiliki wa ardhi katika  ofisi za ardhi wilayani Mufindi.
 Naibu Waziri Mhe. Mabula akiongea na wananchi katika ukumbi wa CCM mjini Mafinga kabla hajaanza kusikiliza kero zao.
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri Mabula kabla hawajaanza kumweleza kero zao,

SIMBA YATINGA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI KWA KUIFUNGA YANGA 4-2 KWA MATUTA

$
0
0
Na Bin Zubeiry
SIMBA SC imefanikiwa kwenda fainali ya Kombe la Mapinduzi, baada ya kuwatoa watani wa jadi, Yanga kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Amaan, Zanzibar. 
 Penalti za Simba zilifungwa na Nahodha Jonas Mkude, kipa Daniel Agyei, Muzamil Yassin na beki Mkongo Janvier Besala Bokungu, wakati kipa wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’ aliokoa mkwaju wa beki Mzimbabwe Method Mwanjali. 
Waliofunga penalti za Yanga ni Simon Msuva na kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko wakati kipa Mghana wa Simba, Daniel Agyei aliokoa penalti za Dida na Mwinyi Hajji Mngwali.


Introducing Wimbo Kutoka Kwa Sallii Teknik "umejengwa juu ya nini"

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 10.01.2017

SIMBA YAIFUATA AZAM FAINALI, YAING'OA YANGA KWA MATUTA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, 
Globu ya Jamii, Unguja


NI AZAM VS SIMBA, klabu ya Simba imeendeleza ubabe kwa watani wao wa jadi Yanga baada ya kuwaondoa kwenye hatua ya nusu ya kombe la mapinduzi kwa mikwaju ya penati 4-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Penalti za Simba zilifungwa na Nahodha Jonas Mkude, kipa Daniel Agyei, Muzamil Yassin na beki Mkongo Janvier Besala Bokungu, wakati kipa wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’ aliokoa mkwaju wa beki Mzimbabwe Method Mwanjali na kwa upande wa Yanga waliofunga penalti ni Simon Msuva na kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko wakati kipa Mghana wa Simba, Daniel Agyei aliokoa penalti za Dida na Mwinyi Hajji Mngwali.

Dakika 90 za mchezo huo zilianza kwa kasi kwa kila upande kutaka kuliona lango la mwenzake lakini umakini wa golikipa Daniel Aggey aliweza kudaka mpira uliopigwa na Haruna Niyonzima katika dakika ya nane na dakika ya 16, kiungo Mohammed Ibrahim alijaribu kwa kupiga shuti kali lililodakwa na kipa wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’.

Kwa ujumla timu zote zilishambuliana kwa zamu, lakini Yanga ndiyo waliomiliki mpira zaidi wakicheza kwenye eneo lao na kuvusha upande wa pili kwa mipira mirefu, hivyo kuwafanya viungo wa Simba muda mwingi wawe wazurulaji katikati ya Uwanja.

Kikosi cha Simba SC kilikuwa; ⁠⁠Daniel Agyei, Janvier Bokungu, MOhammed Hussein 'Tshabalala', Abdi Banda, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya/Jamal Mnyate dk72, James Kotei, Juma Luizio/Pastory Athanas dk77, Muzamil Yassin na Mohamed Ibrahim/Laudit Mavugo dk85.
Yanga SC; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondan, Saidi Juma ‘Makapu’, Simoni Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Haruna Niyonzima na Deusi Kaseke/Emmanuel Martin dk63
Wachezaji wa Yanga wakijipanga kwa ajili ya kona.
Mshambuliaji wa Simba Mohamed Ibrahim akigangwa baada ya kuumia wakati wa mchezo wa nusu fainali ya kombe la Mapinduzi leo Usiku katika uwanja wa Amani, SAimba wakifanikiwa kuingia hatua ya fainali baada ya kushinda kwa penati 4-3.
Maohamed Ibrahim akimtoka beki wa Yanga wakati mchezo wa nusu fainali ya kombe la Mapinduzi leo Usiku katika uwanja wa Amani, SAimba wakifanikiwa kuingia hatua ya fainali baada ya kushinda kwa penati 4-3
Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo akijaribu kumtoka beki wa Yanga Haji Mwinyi kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la Mapinduzi leo Usiku katika uwanja wa Amani, SAimba wakifanikiwa kuingia hatua ya fainali baada ya kushinda kwa penati 4-3

Steve nyerere aibuka na East African Stand up comedy kupitia TBC one

Busara itumike katika matumizi ya maji ya bonde la Eyasi - RC GAmbo

$
0
0
Na Nteghenjwa Hosseah, Arusha

Serikali Mkoani Arusha imesema busara ilipaswa kutumika zaidi katika Utekelezaji wa Agizo la Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa alilotoa wakati wa ziara yake Wilayani Karatu katika Bonde la Eyasi kuhusu kusogezwa kwa Mashine za kuvuta maji Umbali wa Mita 500 kutoka chanzo cha Maji.

Katika Agizo lake Mhe. Waziri Mkuu aliagiza kusogezwa kwa mashine za za kuvuta maji kutoka chanzo cha maji cha bonde la Eyasi ambapo akati mchakato wa utekelezaji ukiendelea baadhi ya wakazi wa eneo hilo walizichoma moto mashine hizo ambazo kwa wakati huo zilikuwa zimesogezwa umbali wa mita 60 ambazo zinaruhusiwa kisheria.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akiwa katika ziara ya Kikazi Wilayani Karatu amesema kutokana na umuhimu wa bonde la Eyasi katika uzalishaji wa Chakula haikuwa busara kwa wananchikuchoma mashine hizo bila kujali mazao ambayo tayari yameshaoteshwa katika eneo hilo na gharama zilizotumika kununua mashine hizo.

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akizungumza na walimu wa wilaya ya Karatu katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi wilayani humo.

 Katika Kikao kingine Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho  Gambo (aliyesimama mbele) akizungumza na wazee wa Karatu pamoja na viongozi wa dini.

 Mtaalamu wa Halmashauri ya Karatu(kwanza kulia) akiwaandikisha  Wananchi wa Kijiji cha Oldeani waliojiunga na Mfuko wa afya ya Jamii wakati wa Mkutano wa hadhara na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kwanza kulia) akichangia Fedha kwa ajili ya wazee 10 kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii.  

Balozi wa Cuba nchini Tanzania aagwa baada ya kumaliza muda wake

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisoma hotuba wakati wa hafla fupi ya kumuaga Balozi wa Cuba Nchini Tanzani Mhe. Jorge Luis Lopes Tormo iliyofanyika katika Hoteli ya Southern Sun Jijini Dar Salaam
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara Bi. Mindi Kasiga akiongea katika hafla hiyo
Toka kulia ni; Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Comrade Abdulahaman Kinana, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Balozi wa Cuba Nchini anayemaliza muda wake Mhe. Jorge Luis Lopes Tormo, Mkurugenzi wa Idara ya Marekani na Ulaya Balozi Joseph Sokoine, na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa Bw.Mlingi E. Mkucha wakifurahia jambo katika hafla hiyo
Balozi wa Cuba Nchini anayemaliza muda wake Mhe. Jorge Luis Lopes Tormo akiongea katika hafla hiyo
Picha ya pamoja

Makala ya sheria: JE, MPANGAJI ANAWEZA KUPANGISHA?

$
0
0
Sheria  Na  4  sura  ya  113 Sheria  ya Ardhi  ndiyo  sheria  inayotawala  habari  nzima ya  upangaji  na  upangishaji. Mpangaji  ni  mpangaji  anajulikana  lakini  swali  ni  kama  baada  ya  kupangishwa  na  yeye  anaweza  kupangisha. Hata  hivyo  kabla  ya  hilo  tutizame  vipengele  muhimu  vinavyotakiwa  kuwa  katika mkataba  wa  upangaji.


Ni  muhimu  kuangalia  vipengele  hivi  kwasababu  suala  la uwezo  wa mpangaji  naye  kupangisha  ni  moja  kati  ya  migogoro   kati  ya  wenye  nyumba  na  wapangaji  ambayo  husababishwa  na  mikataba   isiyoshiba  kwa vipengele  muhimu. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AKUTANA NA UJUMBE WA KOICA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)  akisalimiana na Makamo wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Korea  KOICA Bw.Wooyong Chung   akiwa na ujumbe aliofuatana nao walipofika Ikulu Mjini  Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa  akizungumza na  Ujumbe wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Korea  KOICA unaoongozwa na Makamo wa Rais wa Shirika hilo Bw.Wooyong Chung (wa pili kulia) mara  walipofika Ikulu Mjini Zanzibar. Picha na IKULU

Ziara ya kikazi ya Naibu Waziri Dkt.Mabula mkoani Iringa

$
0
0
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akikagua mfumo wa kielektroniki wa ukadiriaji na ulipaji kodi ya ardhi  Wilayani Kilolo mkoani Iringa mara baada ya kuwasili wilayani humo mapema wiki hii kufuatilia utendaji wa sekta ya ardhi. Dkt. Mabula pia alikagua kumbukumbu za majalada za ulipaji kodi.Anayetoa maelezo ya ufanyaji kazi wa mfumo huo ni Afisa Ardhi wa Halmashairi ya Wilaya hiyo Bw. Elinaza Kiswaga.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akisalimiana na wajumbe wa Baraza la Kata ya Mtitu Wilayani Kilolo mkoani Iringa mara baada ya kuwasili wilayani humo kufuatilia utendaji wa sekta ya ardhi. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Juma Abdallah.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Kata ya Mtitu Wilayani Kilolo mkoani Iringa Bibi Veronica Salangeni ambaye amemaliza muda wake.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akikagua mfumo wa kielektroniki wa ukadiriaji na ulipaji kodi ya ardhi  katika Wilaya ya Iringa Mjini mkoani Iringa alipotembelea kufuatilia utendaji wa sekta ya ardhi. Anayetoa maelezo ya ufanyaji kazi wa mfumo huo ni Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bw. Shadrack Haule. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Bw. Richard Kasesela.

UWANJA WA NDEGE WA MWANZA KUKAMILIKA NOVEMBA.

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka Mkandarasi anayejenga na kukarabati uwanja wa ndege wa Mwanza Beijing Construction Engineering Group (BCEG), kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ifikapo Novemba mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa mnara wa kuongozea ndege, jengo la kuhifadhia mizigo, eneo la kuegeshea ndege na jengo la umeme litakalotoa huduma katika uwanja huo, Profesa Mbarawa amesema tayari Serikali imeshamlipa mkandarasi huyo kiasi cha shilingi bilioni saba kwa ajili ya ujenzi huo.

“Sisi tumeshamlipa pesa yake yote na hivyo tunachotaka kwake ni kukakamilisha kazi yetu kwa wakati ili kuupa hadhi inayostahili uwanja wa ndege wa Mwanza amboa ni kiungo muhimu katika kanda ya Ziwa”, Amesema Profesa Mbarawa.

Prof. Mbarawa amemuagiza Meneja wa uwanja wa ndege wa Mwanza Bi .Easter Madale kuhakikisha vikwazo vyote vinavyomkabili mkandarasi vinaondolewa ili kumuwezesha kufanya kazi kubwa kabla ya kipindi cha mvua za masika zinazotarajiwa kuanza mwezi machi.

Kwa upande wake Mhandisi Lili Ang aneyesimamia ujenzi huo kutoka kampuni ya BCEG amemhakikishia Prof. Mbarawa kuwa baada ya kupokea malipo wamejipanga kukamilisha kazi hiyo kwa wakati na viwango ili waweze kupata fursa nyingine za ujenzi hapa nchini.

Naye Meneja wa Uwanja wa ndege wa Mwanza Bi .Easter Madale ameyataka mashirika ya ndege kuongeza safari za ndege kwenye uwanja wa Mwanza kwa kuwa sasa utakuwa na hadhi ya kimataifa na kusisitiza umuhimu wa wawekezaji wa hoteli, vituo vya mafuta na maduka makubwa kuwekeza karibu na uwanja huo ambao ndio lango la uchumi wa kanda ya ziwa.

Katika hatua nyingine Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano ameelekea mkoani Simiyu kuanza ziara ya siku mbili mkoani humo amabapo pamoja na mambo mengine anatarajiwa kushiriki katika ufunguzi wa barabara ya Bariadi- Lamadi iliyojengwa kwa kiwango cha lami.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawssiliano.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mhandisi Lili-Ang kutoka kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) inayakarabati na kujenga uwanja wa ndege wa Mwanza.
Mhandisi Mshauri anayesimamia ukarabati na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa Mnara wa jengo la kuongozea ndege alipokagua ujenzi wa uwanja huo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa viongozi wa uwanja wa ndege wa Mwanza namna ya kushirikiana na Mkandarasi Beijing Construction Engineering Group (BCEG)   anayekarabati na kujenga uwanja huo.
Muonekano wa jengo jipya la kuongozea ndege linalojengwa na kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) katika uwanja wa ndege wa Mwanza.

KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS PROF. FAUSTIN KAMUZORA ATEMBELEA NEMC

$
0
0

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora akisalimiana na baadhi ya Wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) mara baada ya kutemebelea Ofisi za Taasisi hiyo zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. NEMC ni Taasisi iliyopo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais.
Katibu Mkuu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (kulia) akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Bw. Bonaventure Baya (Kushoto) mara baada ya kuetembelea Ofisi za Baraza hilo zilizopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni sehemu ya wajumbe wa Menejimenti katika Ofisi hiyo.
Katibu Mkuu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Bw. Bonaventure Baya na Bi. Magdalena Mtenga Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais.

Picha zote na SIGLINDA CHIPUNGAUPI

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JANUARI 11, 2017

Viewing all 110129 articles
Browse latest View live




Latest Images