Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1502 | 1503 | (Page 1504) | 1505 | 1506 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akipokea kitabu kilichojikita katika Tafiti ya Kazi za Sanaa za Tanzania kutoka kwa Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Bi. Florence Tinguely Mattli alipomtembelea  Waziri huyo ofisini kwake leo.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akimsikiliza Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Bi. Florence Tinguely Mattli alipomtembelea ofisini kwake mapema leo.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Bi. Florence Tinguely Mattli alipofanya ziara ya kikazi ofisini kwake leo. Kulia ni Mkuu wa Mahusiano wa ubalozi wa Uswisi nchini Bi. Romana Tadeschi.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Bi. Florence Tinguely Mattli (hayupo pichani) alipotembelewa na Balozi  huyo ofisini kwake leo.

  0 0

  Na Benny Mwaipaja, WFM, Mwanza
  Wizara ya Fedha na Mipango yawataka wastaafu wanalipwa na Hazina ambao hawajahakikiwa katika mikoa ambayo zoezi hilo limeshafanyika na wanauwezo wa kufika katika maeneo ambayo zoezi hilo linaendelea , wajitokeze kwa wingi  kwa ajili ya kuhakikiwa.
  Wito huo umetolewa mkoani Mwanza na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Msaidizi, Bw. Stanislaus Mpembe wakati wa uzinduzi wa zoezi la Uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango katika Kanda ya Ziwa, mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu na Geita.
  Mpembe alisema kuwa zoezi hilo ni muhimu kwa wastaafu na Serikali kwa ujumla kwani limelenga kuiwezesha Wizara ya Fedha na Mipango kuhuisha taarifa za Wastaafu, kupata orodha sahihi ya wastaafu wanaolipwa na Wizara hiyo ili Serikali iweze kuwalipa wale wote wanaostahili.
  Alifafanua kuwa suala la uhakiki ni la lazima na kuwaomba wastaafu wajitokeze kwa wingi kwani baada ya zoezi hilo kumalizika nchi nzima wastaafu ambao hawatahakikiwa watafutwa katika mfumo wa malipo.
  “Naomba wastaafu wote wajitokeze katika Halmashauri zilizotangazwa, hata wasiokuwa na nyaraka wajitokeze wataelekezwa mahali wanapoweza kupata nyaraka zote muhimu” aliongeza Bw. Mpembe.
   Alisema kuwa wagonjwa na wasiojiweza wametengewa siku ya Ijumaa ambayo ni siku ya mwisho ya uhakiki, ambapo watakuja ndugu au jamaa zao watakaotoa taarifa sehemu walipo hususani waliopo hospitalini na sehemu ambazo zinaweza kufikika kwa karibu na wahakiki ili nao wahakikiwe.
  Naye Mstaafu John Msanja, pamoja na kuomba serikali iwafikirie kuwaongezea pensheni ili waweze kukabiliana na hali ngumu ya maisha inayowakabili, aliipongeza Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na waratibu kwa kuendesha  zoezi hilo kistaarabu pamoja na kutoa kipaumbele kwa wagonjwa  na wasiojiweza ambao waliweza kufika katika eneo hilo kwa lengo la kuhakikiwa.
  Alisema kuwa zoezi hilo linaonesha ni namna gani Serikali inawajali wazee waliolitumikia Taifa kwa muda mrefu kwa kuhakikisha ni namna gani wanapata stahili zao kwa wakati.
  Zoezi hili lilianza Oktoba, 2016 katika Mkoa wa Pwani na kuendelea katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kati na Kanda ya Kaskazini. Mpaka sasa wastaafu wa mikoa 13 ya Tanzania Bara wameshahakikiwa.
  Baada ya uhakiki kumalizika Kanda ya Ziwa, zoezi hili litaendelea katika mikoa ya Kigoma na Tabora.

  Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Msaidizi, Bw. Stancilaus Mpembe, akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mwanza wakati wa Uzinduzi wa zoezi la Uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango Kanda ya Ziwa.
  Baadhi ya wastaafu wakiwa wanahakikiwa na Wakaguzi wa ndani wa Serikali mkoani Mwanza katika uzinduzi wa zoezi la Uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa na Hazina, huku wengine (waliosimama kulia) wakiwa katika foleni.
  Picha ya pamoja ya Wakaguzi wa Ndani wakiendelea na zoezi la Uhakiki wa Wastaafu Wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango mkoani Mwanza, huku baadhi ya wastaafu wakiendelea kusubiri zamju zao katika viti.
  Baadhi ya wastaafu wakiwa wamepumzika wakisubiri zamu zao za kuhakikiwa wakati wa zoezi la Uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa na Hazina, utakao dumu hadi mwishoni mwa juma, jijini Mwanza.

  0 0

  Nteghenjwa Hosseah, Arusha

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameitaka Wizara ya Mifugo, Chakula na Ushirika kuacha kutoa vibali vya kusafirisha mahindi nje ya nchi kwa wafanyabiashara wa hapa nchini kwani Serikali Mkoani Arusha ilishapiga marufuku usafirishwaji wa mahindi hayo nje ili kulinda viwanda vya hapa nchini.

  Mhe. Gambo alisema hayo jana baada ya kutembelea maghala matatu ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula{NFRA} Kanda ya Arusha kujionea hali halisi ya uhifadhi wa mahindi katika maghala hayo na kuskiliza changamoto zake na kukuta tani 6,620 za mahindi zilizoko kwa sasa.

  Alisema serikali Mkoani Arusha ilishapiga marufuku uuzwaji wa mahindi nje ya nchi lakini kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekamatwa na vyombo vya ulizni na usalama wakiwa na vibali kutoka Wizarani vinavyowaruhusu kupeleka mahindi nchi jirani ya Kenya hali inayowafanya watendaji wa serikali kushindwa kufanya kazi kutokana na mkanganyiko huo.

  Mkuu huyo alisema uamuzi wa kupiga marufuku uuzwaji mahindi nje ulitolewa na serikali kuu na Mkoa ulisimamia hilo kwa lengo la kuvilinda viwanda vya hapa nchini kwa uzalishaji wa bidhaa hivyo na kunufaika na unga na pumba za mahindi tofauti na ilivyo sasa.

  Alisema kutokana na mkanganyiko huo aliwaomba watendaji wa Wizara kuacha kutoa vibali kwa wafanyabiashara kuuza mahindi nje ili kuwasaidia wenye viwanda vya nafaka kuuza unga na pumba nje wenye kiwango ili nao waweze kupata faida na nchi iweze kupata faida zaidi.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo (Pili kushoto) akiwasili katika Ofisi za Wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa Chakula Kanda ya Kaskazini zilizoko Mkoani Arusha kuangalia na kukagua hali ya uhifadhi wa Chakula.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kwanza kushoto) pamoja na Meneja wa NFRA Kanda ya Kaskazini Ndg.Abdillah Nyangasa wakitembelea maghala ya kuhifadhia Chakula wakati wa ziara yake katika Ofisi hizo.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kwanza kulia) akikagua taarifa za mazao yaliyohifadhiwa katika Magahala ya NFRA wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya Uhifadhi wa Chakula.
  Kutoka kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Ndg. Richard Kwitega akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo na Meneja wa NFRA Ndg. Abdillah Nyangasa wakati wa kikao na wafanyakazi wa NFRA Kanda ya Kasikazini.


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na Profesa Ibrahim Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria Chato mkoani Geita.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea barua yenye ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari uliowasilishwa na Profesa Ibrahim Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais huyo wa Nigeria, Chato mkoani Geita.
   Profesa Ibrahim Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari  akimshukuru Rais Dkt. John Magufuli mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Chato mkoani Geita.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mgeni wake Profesa Ibrahim Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Chato mkoani Geita.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Profesa Ibrahim Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Chato mkoani Geita. PICHA NA IKULU


  0 0


  0 0

  Frank Mvungi-Maelezo

  Serikali imewahakikishia Watanzania kuwa kuna utoshelevu wa dawa kwa asilimia 86 kinyume na taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya watu.Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo .

  Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa Bohari kuu ya Dawa (MSD) Bw. Laurean Rugambwa amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano imetenga bajeti yakutosha kukidhi mahitaji ya dawa hapa nchini ambapo kufikia machi 2017 upatikanaji wa Dawa utafikia asilimia 90.

  “ Serikali imetenga bilioni 250 katika bajeti ya mwaka huu na Kila mwezi Serikali inatoa zaidi ya bilioni 20 ajili ya ununuzi wa dawa hali iliyosaidia kuondoa tataizo la dawa hapa nchini kwa sasa”

  Akifafanua Rugambwa amesema kwa sasa fedha sio tatizo kwa Bohari ya dawa kutokana na hatua za makusudi zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata huduma bora za afya ikiwemo upatikanaji wa dawa.

  Moja ya mikakati iliyochukuliwa na Serikali katika kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa ni kuboresha matumizi ya mfumo wa msimbo pau (Barcode) hali itakayosaidia kuongeza ufanisi katika upokeaji,utunzaji na usambazaji wa dawa na vifaa tiba.

  Mikakati mingine ni kuanziasha mpango wa huduma maalum kwa wateja wakubwa ambao ni Hosipitali ya Taifa Muhimbili,MOI, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Hospitai ya Bugando,Hosipitali ya Kibongoto,Hospitali ya Mirembe,Hospitali ya Amani, Hospitali ya Temeke, Mwanenyemala,Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya,KCMC, Hosipitali ya Benjamin Mkapa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

  Pia kununua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji na kuanzisha mchakoto wa ujenzi wa viwanda vya kuzalisha dawa na vifaa tiba nchini ili kupunguza gharama.

  Katika kipindi cha mwaka 2016 MSD imefungua maduka ya dawa sehemu mbalimbali nchini lengo likiwa ni kuwezesha Hospitali ambazo ndio wateja wakubwa wa MSD,Maduka ambayo mpaka sasa yameshafunguliwa ni pamoja na lile lililopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,Sekou Toure Mwanza,Hospitali ya rufaa Mbeya,Mount Meru Hospitali ,Chato Halmashauri ya Mji wa Geita na Ruangwa Mkoani Lindi.
  Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa ya kuimarika kwa upatikanaji wa dawa nchini. Kulia ni Ofisa Mwandamizi wa Idara Habari Maelezo, Zamaradi Kawawa.

  0 0

  Frank Mvungi- MAELEZO

  Watanzania wameaswa kupunguza unywaji wa pombe ili waweze kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda na kulifikisha taifa kwenye uchumi wa kati ifikapo 2020.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Msaidizi Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Prof. Ayoub Maghimba amesema kuwa ni vyema watu wakapunguza unywaji wa Pombe ili kutumia muda mwingi katika uzalishaji na kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

  “Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni pamoja na Saratani,magonjwa ya moyo,magonjwa sugu ya njia ya hewa,seli mundu,magonjwa ya akili na dawa za kulevya,magonjwa ya figo,kisukari,ajali, na magonjwa ya macho yasiyo ya kuambukiza” Alisisitiza Prof. Maghimba.
  Akifafanua Prof. Maghimba alisema kuwa utafiti uliofanyika ulionyesha asilimia 15.9 ya wananchi wanavuta sigara, asilimia 29.3 wanakunywa pombe, asilimia 97.2 wanakula mbogamboga na matunda chini ya mara tano kwa siku hali inayowaweka katika hatari ya kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

  Alisema kuwa unywaji wa pombe uliokithiri unasababisha magonjwa kama saratani ambayo inachangia vifo na wastani wa wagonjwa 109 hugundulika na saratani kila siku hapa nchini.

  “Magonjwa yasiyo ya kuambukiza au magonjwa sugu ni magonjwa ambayo mtu akiyapata hawezi kuambukiza wengine na ataishi nayo hadi siku ya kufa.” Alisisitiza Prof.Maghimba.

  Magonjwa haya yamekuwa yakiongezeka duniani kote, hasa kwenye nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara,Tanzania ikiwemo. Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanachangia asilimia 27 ya vifo vyote duniani.


  0 0

  Ajali ya Jahazi ambayo ilitokea usiku wa kuamkia leo iliyosababisha vifo vya abiria 12 na wengine 25 kujeruhi kwenye tukio hilo.

  Jahazi hilo lenye namba za usajili Z5512 MV Burudani maarufu kama Sayari lilikuwa likitokea eneo la Bandari Bubu ya Sahare kuelekea Visiwani Pemba ambapo lilipofika eneo la Jambe chombo hicho kilipigwa na dhoruba kali na hivyo kumshinda nahodha wake Badru Saidi na kuzama

  Akizungumza na MTANDAO huu,Mbunge Mussa alisema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za ajali hiyo na kuwataka ndugu na jamaa kuwa na uvumilifu na kuhaidi kuwa nao bega kwa bega.

  Licha ya hivyo lakini pia mbunge huyo alikabidhi sanda 12 kwa ajili ya maziko ambayo yanatarajiwa kufanyika leo na kesho kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.Ajali hiyo ambayo ilitokea usiku wa kuamia leo kwenye eneo la kisiwa cha Jambe kandokando ya bandari ya Tanga imeacha simamanzi kubwa kwa wakazi wa mji huu na viunga vyake.

  Alisema kuwa yeye kama mbunge wa Jimbo la Tanga yupo nao bega kwa bega na kuwaombea mwenyezi mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.“Ajali sio jambo ambalo tunalipanga bali ni mipango ya mwenyezi mungu lakini pia nivitake vyombo vya usafiri majini kuhakikisha havipakii mizigo mingi zaidi ya uwezo wao kwani hali hiyo inaweza kusababisha ajali “Alisema.

  Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Benedict Wakulyamba alithibitisha kutokea tukio hilo na kueleza hivi sasa vyombo vya ulinzi na usalama wapo kwenye mchakato wa kutafuta watu wengine kwenye bahari ya hindi.

  Alisema kati ya miili hiyo iliyopatikana mpaka sasa wanaume watano na wanawake 7 wameweza kuokolewa katika tukio hilo.Aidha alisema mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana hivyo wanashirikiana na vyombo vyengine ili kubaini ingawa kwa mujibu wa mashuhuda chanzo chake kinatokana na chombo hicho kupigwa na wimbi eneo la nyuma na kukosa mwelekeo na kuzama baharini.

  Kwa upande wake,Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo,Dkt Goodluck Mbwilo alithibitisha kupokea maiti 12 pamoja na majeruhi 25.Alisema kati ya majeruhi hao 18 ni watu wazima huko watoto wadogo wakiwa ni saba ambao waliweza kupewa huduma ya kwanza na kuendelea na matibabu mengine.
  MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku ametoa pole kwa ndugu na jamaa waliopoteza ndugu zao kwenye ajali ya kuzama kwa Jahazi kwenye kisiwa cha Jambe kandokando ya Bahari ya Hindi jijini Tanga na kuwataka kuwa na moyo wa uvumilifu katika kipindi hiki kigumu.


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati ) alipokuwa akitoa hutuba yake ya Ufunguzi wa Tamasha la Tatu (3) la Biashara Zanzibar  katika viwanja vya Maisara wilaya ya Mjini Unguja leo ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe, Amina Salum Ali , na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko Bakari Hassan Bakari (kushoto), 
  Baadhi ya Watendaji na wageni mbali mbali waliohudhuria katika sherehe za Ufunguzi wa maonesho ya Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa kitoa hutuba yake ya ufunguzi katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja leo baada kufungua rasmi maonesho hayo  ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

  Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe, Amina Salum Ali ,(kulia) alipo
  kuwa akimkaribisha  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ( katikati )  kufungua Tamasha la Tatu (3) la Biashara Zanzibar  katika viwanja vya Maisara wilaya ya Mjini Unguja leo ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Wafanyakazi kutoka Taasisi za Serikali na Binafsi waliohudhuria katika Ufunguzi wa maonesho ya Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa kitoa hutuba yake ya ufunguzi katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja leo baada kufungua rasmi maonesho hayo 
  ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Wafanyakazi kutoka Taasisi za Serikali na Binafsi waliohudhuria katika Ufunguzi wa maonesho ya Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa kitoa hutuba yake ya ufunguzi katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja leo baada kufungua rasmi maonesho hayo ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,.
  Kikundi cha wasanii wa ngoma ya kibati wakiburudisha kwa Viongozi na Wananchi wakati wa Ufunguzi wa maonesho ya Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar lililofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja leo,ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Dhow Financial Prof Mohamed Warsame akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji wa Umma (PIC) juu ya uwekezaji katika mashirika ya Umaa.
  Waheshimiwa Wabunge ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji wa Umma (PIC) wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya uwekezaji katika mashirika ya Umma.
  Msajili wa Hazina Dkt Oswald Mashindano akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji wa Umma (PIC) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wabunge hao juu ya uwekezaji katika mashirika ya umaa. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Albert Obama.Mafunzo hayo ya siku mbili yamefanyika Jijini Dar es Salaam.
  (Picha na Ofisi ya Bunge)

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  MAAFISA Maendeleo ya Jamii nchini wametakiwa kuacha kutumia muda mwingi kukaa maofisini na badala yake kutembelea jamii inayowazunguka ili kubaini fursa zitakazoleta mabadiliko ya haraka katika jamii.

  Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Sihaba Nkinga wakati wa mahojiano Maalum ya kipindi cha TUNATEKELEZA kinachoratibiwa na Idara ya Habari (MAELEZO) na kurushwa hewani na Shirika la Utangazaji Nchini (TBC).

  Bi. Sihaba amesema kuwa Serikali imefanya juhudi kubwa ya kuanzisha Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya kuzalisha maafisa wengi wa kada hiyo watakaotumika kuisaidia Serikali katika kuibua fursa mbalimbali zilizopo kwenye jamii ambazo zitasaidia kuleta maendeleo ya nchi.

  “Afisa Maendeleo ya Jamii ni chachu ya maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla kwani wao ndio wana jukumu la kubaini fursa na kuwaongoza wananchi katika kutumia fursa hizo,” alisema Bi. Sihaba.

  Ameongeza kuwa jukumu kubwa la maafisa maendeleo ni kuwahamasisha, kuwashirikisha na kuwajengea uwezo wanajamii kutumia rasilimali walizonazo kujiletea maendeleo yatakayopelekea kukua kwa uchumi wa nchi.

  Aidha, Bi. Sihaba amewataka wananchi kuacha dhana potofu ya kuitegemea Serikali na badala yake washirikiane na Serikali kuleta maendeleo kwa kufanya kazi kwa bidii kwa kutumia rasilimali zinazowazunguka katika maeneo wanayoishi.

  Akiongelea kuhusu makazi ya wazee, Bi. Sihaba amesema kuwa kwa sasa kuna vituo 17 nchi nzima vyenye jumla ya wazee 460 wanaopatiwa huduma mbalimbali zikiwemo za malazi, mavazi na chakula.

  “Tunatoa rai kwa vijana kufanya kazi kwa bidii ili waweze kujitegemea na sio kwenda kukaa kwenye nyumba za wazee ili wapatiwe huduma, makazi ya wazee ni kwa ajili ya wazee wasiojiweza tu,” alimalizia Bi. Sihaba.

  0 0


  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi  0 0


  Na Woinde Shizza,Arusha

  Chama cha soka Mkoa wa Arusha (ARFA) kimefanikiwa kupata uongozi mpya baada ya uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika mwishoni mwa wiki Wilayani Monduli ambao watakaa madarakani kwa miaka minne.

  Katika uchaguzi huo uliokuwa unawaniwa nafasi kumi, ulionekana mgumu kwa nafasi mbili pekee ile ya Mwenyekiti pamoja na nafasi ya Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF,ambapo wagombea walikua wawili wawili.

  Waliofanikiwa kupita katika uchaguzi huo kwa nafasi ya mwenyekiti ni Peter Temu aliyemshinda Omary Walii kwa kura 13 kwa 6, Katibu mkuu Zakayo Mjema aliyepata kura 18, katibu msaidizi akipitaNassoro Mwarizo.

  Nafasi ya Mweka hazina ikienda kwa Omary Nyambuka, Huku nafasi ya Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF Issa Hamisi alimshinda Athumani Mhando kwa kura 13 kwa 8, na nafasi ya kamati tendaji ya ARFA ikienda kwa Soud Abdy.

  Washiriki ambao ni wajumbe wa vyama vya soka kutoka Mkoani hapa waliojitokeza ni kutoka Arusha Mjini, Monduli, Arumeru, Karatu, Longido, FRAT ambao walifanya jumla ya wajumbe 19 waliopiga kura.

  Huku nafasi ya wajumbe watatu wa kamati tendaji iliyopata mtu mmoja na mwakilishi wa vilabu ambazo hazajajazwa utafayika uchaguzi mdogo baada ya siku 90 kupita alisema katibu wa kamati ya Uchaguzi Seleimani Kirua

  Katibu mkuu mpya wa ARFA Zakayo mjema akiongea na gazeti hili alisema wameingia madarani huku kukiwa na deni kubwa la kuitendea haki Arusha ili kuweza kurudisha timu ligi kuu.

  " Kwanza nashukuru nimechuguliwa kwa idadi kubwaya kura na hii ni dhahiri wajumbe wameniamini na nitahikisha tunashirikiana kwa pamoja na wilaya zetu katika kuhakikisha soka la mkoa huu linarejea kama ilivyokuwa zamani,"alisema Mjema.

  Mwenyekiti mpya Peter Temu aliwasihi wadau wa soka wawe na matumaini kuwa mpira utarejea kulingana na safu mpya yenye morali ya wa kusaidia na kuendeleza mpira.
  Mwenyekiti mpya wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Arusha (ARFA) Peter Temu 

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar sherehe zilizofanyika leo huko katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe Amina Salum Ali.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ( wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Najma Hussein (katikati) alipotembelea banda la maonesho ya Biashara la Bakhresa Group Companies mara baada ya kufungua Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar leo katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Ndg.Mohamed Suleiman wa Kiwanda cha Uchapaji cha Serikali wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Biashara mbali mbali alipofungua Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar leo katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja leo ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa kituo cha tiba,ushauri nasaha na Utafiti wa magonjwa Sugu na Ukimwi Dr.John A.Kidua (kulia) wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Biashara mbali mbali alipofungua Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja leo ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe Amina Salum Ali.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akisalimiana na Wajasiriamali kutoka Mkoa wa Mwanza,ambao wanafanya bishara ya mikoba na dawa asilia wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Biashara mbali mbali alipofungua Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja leo ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe, Amina Salum Ali,[Picha na Ikulu.] 10/01/2017.


  0 0

   Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora akisalimiana na baadhi ya Wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) mara baada ya kutemebelea Ofisi za Taasisi hiyo zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.  NEMC ni Taasisi iliyopo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais.
   Katibu Mkuu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (kulia) akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira  Bw. Bonaventure Baya (Kushoto) mara baada ya kuetembelea Ofisi za Baraza hilo zilizopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni sehemu ya wajumbe wa Menejimenti katika Ofisi hiyo.

  Katibu Mkuu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).  Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira  Bw. Bonaventure Baya na Bi. Magdalena Mtenga Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais. 
  Picha zote na SIGLINDA CHIPUNGAUPI

  0 0
 • 01/10/17--09:35: VOTE FOE MO DEWJI
 • Who will it be? This is the question agitating the mind of millions of Africans and friends of Africa, as the African Leadership magazine UK, prepares to announce the 2016 African Leadership Magazine Person of the Year, from a shortlist of 8 distinguished Africans that made the final list for this edition.Voting Ends on the 16th of January 2016
  Businessman Mohamed Dewji 'Mo' has been nominated for the African Leadership Person of the Year. Visit the following site to cast your vote:


  0 0


  0 0

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mhandisi Lili-Ang kutoka kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) inayokarabati na kujenga uwanja wa ndege wa Mwanza.

   Mhandisi Mshauri anayesimamia ukarabati na ujenzi wa  uwanja wa ndege wa Mwanza akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa Mnara wa jengo la kuongozea ndege alipokagua ujenzi wa uwanja huo.

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa viongozi wa uwanja wa ndege wa Mwanza namna ya kushirikiana na Mkandarasi Beijing Construction Engineering Group (BCEG)  anayekarabati na kujenga uwanja huo. 

  Muonekano wa jengo jipya la kuongozea ndege linalojengwa na kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) katika uwanja wa ndege wa Mwanza. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. 

  0 0

  Na Rose Msoka, Zanzibar
  Wananchi wa Zanzibar leo wamejitokeza kwa wingi kwenye sherehe za uzinduzi wa maonesho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar, yanayoendelea kwenye viwanja vya Maisara mjini Zanzibar.

  Maonesho hayo yamezinduliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa  Dr. Ali Mohamed Shein, ambaye pamoja na mambo mengine amesisitiza Taasisi za Serikali na binafsi kutumia vema fursa ya maonesho kujitangaza na kuonyesha shughuli wanazofanya kwa wananchi.

  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ni miongoni mwa Taasisi zinazoshiriki maonesho hayo ambapo pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa Vitambulisho, inaendesha zoezi la kusajili wananchi ambao bado hawajasajiliwa, kugawa vitambulisho vya Taifa kwa wananchi waliokamilisha taratibu za usajili, pamoja na kuonesha mfumo salama (tovuti) inayotumika kusoma taarifa za mtu zilizoko kwenye mfumo kwa njia ya mtandao. Njia hiyo itawezesha wadau mbalimbali kutumia mfumo huo kuhakiki taarifa za mwananchi mwenye kitambulisho kabla ya kumpatia huduma.

  Banda la NIDA limekuwa moja ya mabanda ya kuvutia, ambapo wananchi wengi  wamekuwa wakitembelea shughuli mbalimbali zinazoendelea kwenye viwanja hivyo na kuonekana kuridhishwa na huduma zinazotolewa na NIDA.

  Maonesho ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yameanza tangu Jumamosi tarehe 07 Januari 2017 yakihusisha Taasisi mbalimbali za Serikali zikiwemo Taasisi za Muungano, mashirika na Taasisi binafsi na yanatarajiwa kumaliza Jumamosi tarehe 14/01/2017.

   Wafanyakazi  wa NIDA wakiwa katika picha ya pamoja katika Banda lao la  maonyesho katika viwanja vya maonyesho vya Biashara vya Maisara Zanzibar  tayari kuhudumia wananchi watakaohudhuria.
   ) Ofisa wa NIDA  Ng Abdulaziz Juma Mtumwa akimkabidhi Dada Lidia Adminic Kaguo Kitambulisho chake katika Banda la Maonyesho wakati maonesho ya sherehe za Mapinduzi Zanzibar yakiendelea kwenye  viwanja vya  Maisara
   
   Kaimu Meneja  wa kitengo cha Operesheni Zanzibar Ndg. Abdallah O. Mmanga akitoa elimu juu ya matumizi ya Vitambulisho Vya Taifa kwa wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Maonyesho vya Maisara Zanzibar
   
   Bi.  Shau Mwalim Haji akimsajili mwananchi aliejitokeza katika maonyesho ya Biashara ya Maisara.
  Wananchi wakijisajili kwenye kitabu cha wageni walipofika kutembelea banda la Maonesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) viwanja vya Maisara Zanzibar.

  0 0


  Na George Binagi @BMG
  Jimmy Gospo (pichani) ni mwanamziki mpya kwenye muziki wa injili nchini Tanzania. Kabla ya mwaka 2014 alikuwa akifanya muziki wa Bongo Fleva, akiwakilisha mkoa wa Geita na Kanda ya Ziwa kwa ujumla.
  Baada ya mwaka 2014, Jimmy Gospo aliamua kugeuza uelekeo na kuanza kuimba nyimbo za injili kwenye matamasha mbalimbali ya injili hususani Kanda ya Ziwa. Baada ya hapo alianza kurekodi albamu yake ambayo hadi sasa jina liko kampuni.
  Mwaka huu 2017 ameanza kuachia rasmi baadhi ya nyimbo zilizo kwenye albamu hiyo. Ameanza na wimbo uitwao "Nakujua Bwana" ambao hakika ni wimbo bora kusikiliza na hata mafundisho yake.
  "Ni nyimbo nzuri kwa watu wengi hasa wale ambao tunatamani kuisikia faraja ya Bwana ikitenda na sisi. Niwakaribisheni watanzania wote tuisikilize Ninakujua Bwana, ni nyimbo nzuri na natumaini utaifurahia na kuipenda". Amesisitiza Jimmy.
  Mwimbaji wa muziki wa injili, Jimmy Gospo (kulia), akizungumza na George Binagi-GB Pazzo wa BMG (kushoto), kuhusiana na ujio wake kwenye muziki huo, baada ya kuachana na muziki wa kidunia. 

older | 1 | .... | 1502 | 1503 | (Page 1504) | 1505 | 1506 | .... | 3272 | newer