Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

DC BUHIGWE KANALI GAGUTI AWATAKA WAKUU WA SHULE KUTUNZA MADAWATI WANAYOPEWA NA KUKOMESHA UTORO WA WANAFUNZI WILAYANI HUMO

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel- Globu ya Jamii ,Kigoma,

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marco Gaguti amewataka Wakuu wa Shule Wilayani humo pamoja na Wazazi kuhakikisha wanatunza madawati waliyo kabidhiwa pamoja na kukomesha utoro wa Wananafunzi. Aidha, aliwataka Kuhakikisha ufaulu wa Wanafunzi unaongezeka kutoka asilimia 74.3 kufikia asilimia 84% kutokana na Miundombinu ya kufundishia kuboreshwa ikiwa ni pamoja na kutatua suala la upungufu wa madawati.

Rai hiyo aliitoa jana wakati akikabidhi madawati 1600 kwa wakuu wa Shule 50 zilizokuwa na upungufu wa madawati katika Shule ya Msingi Buhigwe ambapo aliwaomba kuhakikisha wanayalinda madawati hayo yasiharibiwe pamoja na kuhakikishi wanafunzi wote wanahudhuria Shuleni kwasababu changamoto kubwa iliyokuwa ikichangia elimu kushuka ni pamoja na wanafunzi kukaa chini na utoro wa wanafunzi suala ambalo limetafutiwa ufumbuzi.

Gaguti alisema pamoja na kero hiyo ya ukosefu wa madawati kutatuliwa, Serikali imejipanga kila mwanafunzi kupata elimu bora na inayo stahili; hivyo ni jukumu la wazazi kwa kushirikiana na walimu kuhakikisha wanafunzi wanapata malezi mazuri na kuwahimiza watoto kuhudhuria shuleni ilikuweza kusoma kwa juhudi na waweze kufaulu.

Aidha Kanali Gaguti aliwataka wakuu wa shule kuweka malengo ya kupandisha ufaulu ili wilaya iweze kujipima kutoka asilimia 74.33% mwaka jana na kupanda hadi kufikia asilimia 84.3% ikiwa ndio njia sahihi ya kutathimini kama jitihada za Serikali zimefanikiwa na malengo yamefikiwa.

"Niwashukuru Wadau wote walio jitokeza kuchangia madawati katika Wilaya yetu, na Wananchi kwa kufanikisha jukumu hili. Mwitikio wenu ni ishara ya uzalendo kwa Nchi yenu na kutambua dhana ya maendeleo ya kweli ni lazima Wananchi washirikishwe. Aidha,dhana na mawazo ya Serikali kufanya kila kitu imepitwa na wakati hivyo nimefurahishwa sana na Wananchi wa Buhigwe kujitoa katika suala hili",alisema Gaguti.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Anosta Nyamoga alisema wakati zoezi la utengenezaji wa madawati linaanza uhitaji ulikuwa ni madawati 18896 na madawati yaliyo kuwepo ni 7908, awamu ya kwanza yalipatikana madawati 9156 upungufu ukawa madawati 1832 siku chache zilizo pita Wilaya imekamilisha zoezi hill kwa asilimia 100% na yamekabidhiwa katika shule 88 za Wilaya hiyo.

Nyamoga aliwapongeza Wananchi pamoja na Mkuu wa Wilaya kwa juhudi alizo zifanya za kuwashawishi watu na taasisi mbalimbali kichangia madawati kwa kiasi kikubwa na kuhakikisha hadi sasa tatizo hilo linatatuliwa na kukamilika kwa Wakati na Wanfunzi wetu wataendelea kupata elimu nzuri .

Akisoma Risala kwa niaba ya Wakuu wa Shule Kaimu Afisa elimu Wilaya ya Buhigwe Issa Kambi alisema katika kuunga mkono juhudi za serikali walijitahidi kuwahimiza Wananchi kuchangia madawati ambapo Wananchi walichangia madawati 430 kwa vijiji vyote na mengine kutolewa na serikali pamoja na wadau wengine na kukamilisha idadi ya madawati iliyo hitajika.

Alisema watahakikisha Miondombinu ya serikali inalindwa kwa kuweka sheria kali kwa watakao sababisha uharibifu na kuhakikisha wanafunzi wote wanahudhuria ili kupunguza utoro na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wote.
 Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marco Gaguti  akikabidhi madawati 1600 kwa wakuu wa Shule 50 zilizokuwa na upungufu wa madawati katika Shule ya Msingi Buhigwe
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marco Gaguti  akikabidhi madawati 1600 kwa wakuu wa Shule 50 zilizokuwa na upungufu wa madawati katika Shule ya Msingi Buhigwe.

 Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marco Gaguti  akizungumza na baadhi ya waalimu hao kabla ya kuwakabidhi madawati 1600 kwa wakuu wa Shule 50 zilizokuwa na upungufu wa madawati katika Shule ya Msingi Buhigwe.

Rais wa Ivory Coast afikiana muafaka na Wanajeshi waasi nchini humo

$
0
0
Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara  amesema makubaliano yamefikiwa Jumamosi (07.01.2017) kumaliza uasi wa jeshi wa siku mbili ambao ulirejesha hali ya wasi wasi wa usalama katika taifa hilo linaloongoza kwa zao la kakao duniani .

Rais Ouattara  alisema hayo  wakati  wa mkutano wa baraza la mawaziri siku  ya jumamosi jioni. Hapo  mapema , waziri wake  wa  ulinzi Alain-Richard Donwahi , aliongoza  ujumbe  wa majadiliano  pamoja  na  wanajeshi  hao  wanaolalamika  katika  mji wa  pili  kwa  ukubwa  nchini  humo, Bouake, ambako uasi  ulianzia Ijumaa  asubuhi  na  kushuhudia  wanajeshi  wakifyatua  risasi hewani.
Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara
Lakini  katika  ishara  za  mapema  kwamba  si  kila  mwanajeshi alikuwa  akishiriki  uasi  huo, waasi  mjini  Bouake walianza  kufyatua tena bunduki  zao  za  Kalashnikov  pamoja  na  silaha  nyingine baada  ya  tangazo  la  Ouattara, na  kusababisha  Donwahi kukamatwa  na  kuwekwa  katika  nyumba  ya  afisa  wa  mji  huo pamoja  na  ujumbe  wake  na  waandishi  habari.
Kundi  hilo hatimaye liliweza  kuondoka  kabla  ya  saa  kumi  jioni, alisema  mmoja  wa  mateka , Aboubakar Al Syddick, mwandishi wa habari  wa  gazeti la  mjini  Abidjan  la   L'Intelligent. Wizara  ya  ulinzi baadaye  ilitoa  taarifa  ikikaja  kwamba  Donwahi  alikamatwa kinyume  na  matakwa  yake, ikisema  alikuwa  tu  akiendelea kufanya  majadiliano.

Katika  tangazo  lake , Rais Ouattara  alisema  yuko  tayari  kutilia maanani  madai  ya  wanajeshi  hao wanaodai  fedha  zaidi  na mazingira  mazuri  katika  maeneo  wanayoishi  pamoja  na  kazini, lakini  alikosoa  mbinu  walizotumia  za  uasi.
"Nataka  kusema  kwamba  njia  hii  ya  kudai  si  sahihi. Kwa  kweli , inachafua  taswira  ya  nchi  yetu  baada  ya  juhudi  zetu  zote za maendeleo  ya  kiuchumi  na  kujijengea  nafasi  ya  kidiplomasia," alisema.

Rais Ouattara  aliingia  madarakani  mwaka  2011  baada  ya  mzozo  wa baada  ya  uchaguzi  ambao  ulisababisha  zaidi  ya  watu  3,000 kuuwawa.
Mzozo  huo  ulizushwa  na  kukataa  kwa  rais  wa  zamani  wa  nchi hiyo Laurent Gbagbo  kukubali  kushindwa   na  kujiuzulu. Machafuko hayo  yalifikisha  kilele  cha  mzozo  uliokuwa  ukitokota  wa  zaidi  ya muongo  mmoja  ambao  ulianza  kwa  mapinduzi  ya  kwanza  nchini humo  mwaka  1999.

Mzozo  huo sio  mwisho wa  matatizo
Rais huyo mpya  anakabiliwa  na  changamoto  nyingi  katika  kujaribu kujenga  jeshi la  pamoja. Wadadisi  wa  masuala  ya  kisiasa walitabiri  serikali  itatoa  fedha  ili  kuzima  mzozo  wa  wiki  hii, kama ilivyofanya  wakati  wanajeshi  walipofanya  uasi  kama  huo mwaka 2014.

Maelezo  kuhusiana  na  makubaliano  hayo  hayakupatikana  mara moja. Licha  ya  juhudi  hizo  za  serikali  kupata  suluhisho  la haraka, tukio  hilo  linaelekeza  katika  matatizo  yanayoendelea kuwapo  katika  nchi ya Ivory Coast  inayojitoa  kutoka  katika  matatizo, amesema Cynthia Ohayon, mchambuzi  wa  masuala  ya  kisiasa  wa Afrika  magharibi  kwa  ajili  ya  kundi  la  kimataifa  linaloangalia mizozo.

"Hii  ni tukio  jingine  linalokumbusha  kwamba  masuala  ambayo bado  yapo ambayo  yalisababisha  mzozo bado  hayajatatuliwa," amesema. "Baadhi  ya  watu  wanasahau  na  wanafikiri  kwamba kila  kitu kinakwenda  vizuri  nchini  Cote d'Ivoire. Nafikiri  hali  hii inapaswa  kupunguzwa."

Imeandikwa na Mtandao wa DW

WIMBO WA PEMBETULE WA KINYAKYUSA UNAENDELEA KUKONGA NYOYO ZA WANAMBEYA

$
0
0
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mbeya wakiserebuka kwa staili ya aina yake kama ionavyo pichani wakati wimbo wa kinyakyusa ufahamikao kwa jina la "Pembetule" Ukiwa na maana ya Kucheza, Wimbo huo unaendelea kubamba maeneo mbali mbali ya Jiji na nje ya Jiji la Mbeya haswa kwenye Sherehe Mbalimbali.
Huu ndio uchezaji wa Wimbo huo lazima uwe na nguo ya ziada baada ya kumaliza kuucheza maana inaweza kuisha upande mmoja.
Mwana kaka akiendelea kupembetulika yaani kucheza Wimbo huo.
Pembetuleee.....Pembetuleeee..........Peembetuleeeee.

MKOA WA ARUSHA KUKOMESHA MIGOGORO YA ARDHI

$
0
0

Serikali mkoani Arusha imejipanga ndani ya kipindi cha miaka miwili iwe imekomesha migogoro ya ardhi sanjari na mivutano ya mikapa ya kiutawala kati ya wilaya moja na nyingine.

Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo alisema hayo kwenye kikao cha Ardhi,Kilimo,Mifugo na Mazingira kilichowaleta pamoja wakuu wa wilaya,Wakurugenzi na Wenyeviti wa halmashauri pamoja na maafisa wengine kujadili kwa kina mbinu za kumaliza migogoro hiyo.

Alisema baada ya uhakiki wa mipaka na ushauri kutolewa eneo husika lipo Kijiji au wilaya fulani kiongozi au mwananchi atakayehamasisha uvunjifu wa amani atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Awali Mpima Ardhi mkoa wa Arusha,Hamdoun Mansoor akiwasilisha taarifa ya sekta ya ardhi alisema imekua ikitoa maelekezo ya kusimamia uendelezaji katika maeneo ya vijiji na miji kwa kuzingatia sheri ya ardhi namba 5 ya ardhi ya vijiji na 4 ya mwaka 1999 kanuni na taratibu zake.

Alisema changamoto inayoikabili sekta yake ni ujenzi holela unaofanyika kwa kasi kubwa katika maeneo ambayo kisheria yametangazwa kuwa maeneo ya Mpango,ambayo hayaruhusiwi kuendelezwa bila kupata kibali kutoka kwenye mamlaka husika.

"Serikali hujikuta ikilipa fidia zisizo za lazima wakati wa kuendeleza miundombinu mbalimbali na inapotaka kupeleka huduma nyingine za kijamii kwenye maeneo hayo,"alisema Manssor.

Aliyataja maeneo ya umma yanayopaswa kuhifadhiwa kuwa ni pamoja hifadhi za misitu,maeneo oevu,maeneo yenye vilima,vyanzo vya maji,mabonde na kingo za mito.

Manssor alisema uwezo mdogo wa halmashauri kulipa fidia umefanya maendeo mengi kutopangwa na kupimwa na hivyo kuruhusu ukuaji wa kasi wa makazi holela katika maeneo mengi ya mkoa na wilaya zake.

Migogoro ya mipaka ngazi ya mkoa ni katika vijiji vya Ngabobo, Olkung'wado, Leguruki, Ngejusosia, Miririnyi wilayani Arumeru mkoa wa Arusha na Kijiji cha Lekirimuni wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro ambayo inasababishwa na tofauti ya matangazo ya serikali namba 135 la mwaka 1954.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akizungumza kwenye kikao cha kutatua migogoro ya Ardhi mkoani humo. 

TANZIA

$
0
0
Familia ya marehemu Julius Dunstan Mganga wa 21 Ali Hassan Mwinyi Road (Old Bagamoyo Rd)
Dar es salaam, wanasikitika kutangaza kifo cha mama yao mpendwa Flora Agnes Mganga kilichotokea tarehe 7 Januari 2017 katika hospital ya Muhimbili, Dar es Salaam.

Mazishi yatafanyika siku ya jumanne Tarehe 10 Januari,2017 kama ifuatavyo:

5.00 - 7.00 Mchana heshima za mwisho nyumba kwa marehemu 21 Ali Hassan Mwinyi Road,Dar es salaam
8.00 - 9.30 Misa St. Peters church Oysterbay
10.00 Mazishi makaburi ya Kinondoni

Raha ya milele umpe eeh Bwana na Mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa amani,AMINA




Ma Dj wa ‘Sauzi’ Waufagilia muziki wa bongo

$
0
0
 Ma DJ’ maarufu Afrika Kusini Siyabonga Sibeko ‘DJ Capital’ na  Lutendo Kungoane ‘Dj Sliqe’  wakizungumza na waanadishi wa habari hawapo pichani, Dar es Salaam jana kuhusiana na ziara yao ya wiki moja nchini katika kujifunza vitu tofauti vya kimuziki.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


Ma DJ’ maarufu Afrika Kusini Siyabonga Sibeko ‘DJ Capital’ na Lutendo Kungoane ‘Dj Sliqe’ wamesema  kwa sasa muziki wa Tanzania upo vizuri na utafika mbali kama wasanii watajituma zaidi na kuweza kuufikisha kimataifa.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari jana katika hoteli ya New Africa Jijini  Dar es Salaam, ma DJ hao kutoka  redio na  vituo vya luninga nchini Afrika Kusini walisema kwa sasa Tanzania imepiga hatua kubwa kimuziki katika hatua  

“Kwa sasa huwezi kuzungumzia nchi zinazofanya vizuri kwa kiwango cha juu kimuziki Afrika bila kuitaja Tanzanja,”alisema Dj Capital na kuongeza “Afrika Kusini, Nigeria, Ghana, Tanzania na Kenya hizo ndizo nchi za Afrika zinazofanya vizuri katika muziki wa kisasa,”alisema. 

“Tumekuja hapa kujigunza na kukutana na wasnaii kwa sababu sisi pia ni watayarishaji wa muziki,”alisema Capital. 


Kwa upande wake DJ Sliqe’ alisema kwamba anavutiwa zaidi na wasanii wawili wa Tanzania kwa sasa, ambao ni Diamond Platnumz na Vanessa Mdee na  huku akisisitiza kuwa kuna  wasanii wengi wa Tanzania wanaofanya vizuri kwa sasa, lakini kwa  upande wake anawapenda zaidi hao wawili.

Wawili hao, wote ni Ma DJ wa kituo cha Redio cha Touch Central cha Johannesburg, Afrika Kusini wakati DJ Capital pia anafanya kipindi cha Club 808 cha Televisheni ya ETV nchini humo na wamekuja nchini kwa ziara ya wiki moja kujifunza zaidi kuhusu muziki wa Tanzania, pia ni Ma DJ wa kumbi za disko nchin kwao. 

WAZIRI MKUU AAGIZA MAAFISA WANNE WAKAMATWE

$
0
0
*Ni kwa tuhuma za uzembe na upotevu korosho zaidi ya tani 2,000
* Wapelekwa Masasi chini ya ulinzi wakajibu tuhuma zinazowakabili

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Zuberi Mwombeji awakamate maafisa wanne na kuhakikisha wanapelekwa Masasi chini ya ulinzi ili wajibu tuhuma za upotevu wa tani 2, 138 za korosho.

Maafisa hao ni Kaimu Meneja Mkuu Chama Kikuu cha Ushirika cha Masasi (MAMCU), Bw. Kelvin Rajab na Meneja Tawi wa MAMCU, Bw. Lawrence Njozi. Wengine ni wakurugenzi wa kampuni ya YURAP ya Masasi inayohusika na uhifadhi wa mazao kwenye maghala, Bw. Yusuph Namkukula na Bw. Ramadhani Namakweto.

Waziri Mkuu alifikia uamuzi huo kwenye kikao alichokiitisha Songea mjini jana jioni (Jumamosi, Januari 7, 2017) baina ya watendaji kutoka Bodi ya Korosho Tanzania, MAMCU, wamiliki wa ghala la BUCO – Masasi na kikundi cha wakulima sita waliowawakilisha wenzao kutoka vyama vya msingi (AMCOS) za wilaya za Mtwara na Masasi.

Katika kikao hicho, Waziri Mkuu alitaka apatiwe maelezo ya kina ni wapi zilipo hizo tani 2,138 za korosho wakati taarifa waliyompatia viongozi hao jana inaonyesha kuwa waliuza korosho zote na hakuna hata kilo moja ambayo haijanunuliwa katika mnada wa tano uliofanyika Novemba 10, mwaka jana.

Kaimu Meneja Mkuu wa MAMCU, Bw. Kelvin Rajab alikiri mbele ya Waziri Mkuu kwamba korosho zote ziliuzwa na zilishalipwa an wanunuzi wa mnda wa tano lakini akadai hakupewa taarifa ya kukosekana kwa kiasi hicho cha korosho. Naye mmiliki wa ghala la BUCO, Bw. Ramadhan Namakweto alikiri kupokelewa kwa korosho hizo ghalani kwake lakini akashindwa kutoa maelezo ni kwa nini hazionekani zilipo.

“Tangu mnada wa tano, mmekwishafanya minada mingine mitano hadi kufikia mnada wa 10. Kama kweli hizo korosho zipo ghalani, ni kwa nini korosho za hawa wakulima hazijatolewa ghalani na kuuzwa katika minada iliyofuata huku taarifa yenu ya fedha kuwa mlishazipokea na kuziuza?” alihoji Waziri Mkuu bila kupata majibu ya kueleweka.

Tuhuma zinazowakabili maafisa hao wanne ni kuwalipa kilo pungufu ya zile zilizowasilishwa ghalani, wakulima wa korosho katika wilaya ya Masasi na kutowapa maelezo yoyote juu ya upungufu huo. Mfano ni kufanya makato ya unyaufu kwa wakulima wa chama cha msingi CHAMALI kinyume na maagizo ya Serikali.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimuhoji Kaimu Meneja mkuu wa chama kikuu cha ushirika Masasi Mtwara (MAMCU) Bwana Kelvin Rajabu kuhusiana na upotevu wa koroshozaidi ya tani 2000 Waziri mkuu alifanya kikao na Bodi ya korosho pamoja na baadhi ya wanaushirika Mamcu kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano Ikulu ndogo Mkoani Ruvuma
Kamanda wa polisi mkoani Ruvuma Zuberi Mwombeji akiwatarifu Maofisa wa Mamcu na Yurap wako chini ya ulinzi wa polisi kuhusiana na upotevu wa korosho tani 2000 kulia mwenye kaunda suti Kaimu meneja mamcu Bwana Kelvin Rajabu anayefuatia Mkurugenzi wa YURAP inayojishughulisha nauhifadhi korosho katika Ghala la BUCO Masasi Bwana Yusuf Namkula anayefuatia Mkurugenzi mwenzake Bwana Ramadhan Nama na Meneja tawi la Mamcu Bwana Lawrence Njozi
Watuhumiwa wakipelekwa kupanda gari la polisi kwa ajili yakuwapeleka rumande
Kaimu Meneja wa Mamcu bwana Kelvin Rajabu akipanda gari la polisi tayari kwakwenda rumande.Picha na Chris Mfinanga .


MLIMANI CITY YAKABIDHI ZAWADI YA GARI KWA MSHINDI WA DROO YA KRISMAS NA MWAKA MPYA

$
0
0
 KATIKA kusherehekea msimu wa sikukuu za Krismas na Mwaka mpya, uongozi wa Jengo la biashara la Mlimani City kwa kushirikiana na wafanyabiashara waliopo ndani yake, waliandaa promosheni maalum kwa wateja waliofika kununua bidhaa mbalimbali kwenye maduka yaliyomo ndani ya Jengo hilo, ambapo droo yake imechezeshwa leo na mshindi wake ameondoka na gari mpya aina ya Renault Kwid yenye thamani ya Dola za marekani elfu nane miatano (8,500). Pichani ni Mgeni rasmi katika hafla hiyo, ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka aliemuwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru, akichanganya vikaratasi wakati wa droo ya kumtafuta mshindi wa gari mpya aina ta Renault Kwid, iliyofanyika mchana wa leo ndani ya Mlimani city, Jijini Dar es salaam. Mshindi wa Gari hilo ametambulika kwa jina la Julius Lyanga aliefanya manunuzi katika duka la Game.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka akipokea mfano wa funguo ya gari aina ya Renault Kwid kwa niaba ya mshindi, kutoka kwa Meneja Mkuu wa Jengo la Biashara la Mlimani City, Pastory Mrosso.
Sehemu ya wadau walioshiriki na gari iliyoshindaniwa.
"Huyu ndie mshindi wetu leo"

WAZIRI MKUU AAGIZA MAAFISA WANNE WAKAMATWE

$
0
0
*Ni kwa tuhuma za uzembe na upotevu korosho zaidi ya tani 2,000


* Wapelekwa Masasi chini ya ulinzi wakajibu tuhuma zinazowakabili

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Zuberi Mwombeji awakamate maafisa wanne na kuhakikisha wanapelekwa Masasi chini ya ulinzi ili wajibu tuhuma za upotevu wa tani 2, 138 za korosho.

Maafisa hao ni Kaimu Meneja Mkuu Chama Kikuu cha Ushirika cha Masasi (MAMCU), Bw. Kelvin Rajab na Meneja Tawi wa MAMCU, Bw. Lawrence Njozi. Wengine ni wakurugenzi wa kampuni ya YURAP ya Masasi inayohusika na uhifadhi wa mazao kwenye maghala, Bw. Yusuph Namkukula na Bw. Ramadhani Namakweto. 

Waziri Mkuu alifikia uamuzi huo kwenye kikao alichokiitisha Songea mjini jana jioni (Jumamosi, Januari 7, 2017) baina ya watendaji kutoka Bodi ya Korosho Tanzania, MAMCU, wamiliki wa ghala la BUCO - Masasi na kikundi cha wakulima sita waliowawakilisha wenzao kutoka vyama vya msingi (AMCOS) za wilaya za Mtwara na Masasi.

Katika kikao hicho, Waziri Mkuu alitaka apatiwe maelezo ya kina ni wapi zilipo hizo tani 2,138 za korosho wakati taarifa waliyompatia viongozi hao jana inaonyesha kuwa waliuza korosho zote na hakuna hata kilo moja ambayo haijanunuliwa katika mnada wa tano uliofanyika Novemba 10, mwaka jana.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

JAMBO LEO WALIVYOUPOKEA MWAKA MPYA 2017

$
0
0
 Wafanyakazi wa Gazeti la Jambo Leo linalochapishwa na Kampuni ya Quality Media Group Limited wakiwa na furaha wakati wa hafla ya kuukaribisha Mwaka Mpya 2017 kwenye Ukumbi wa Ground Zero, Kurasini Dar es Salaam juzi.
 Wakigongeana ikiwa ni ishara ya kutakiana heri ya Mwaka Mpya wa 2017
 Wakicheza kwa furaha muziki uliokuwa ukiporomoshwa wakati wa hafla hiyo
 Mwenyekiti wa Kamati ya hafla hiyo ambaye ni Mpiga Picha Mkuu wa gazeti hilo, Richard Mwaikenda akimtambulisha Mkurugenzi wa Gound Zero Lounge, Juma Pinto kwa madereva wa Kampuni Mama ya Quality Group Limited (QGL), Salumu (kushoto) na Ramadhan.

DC Kahama Awaonya Wanasiasa Kufanya Kampeni za Kistaarabu.

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Kahama Bw. Fadhili Nkurlu, amewaonya wanasiasa wanaotumia lugha za vitjsho, kashfa na uchochezi kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa diwani kuacha mara moja tabia hiyo.

Nkurlu aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara na kuongeza kuwa hatua kali sana zitachukuliwa kwa mwanasiasa wa chama chochote atakayesikika akitoa lugha za uchochezi au kashfa kwa viongozi wa serikali.

" kumezuka tabia ya wanasiasa kuwakashfu viongozi wa serikali. Sasa nasema hivi Mimi ndiye mkuu wa wilaya hii na ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya. Sitamvumilia mtu yeyote anayetumia jukwaa la kampeni kutoa lugha zenye viashiria vya uvunjifu wa amani na kuwakashfu viongozi".

Nkurlu amewataka wanasiasa kunadi sera zao na namna wanavyoweza kuwasaidia wananchi badala ya kujikita kwenye uchochezi na kashfa kwa viongozi huku wengine wakitishia amani. Pia amewataka kufuata mwongozo na maadili ya uchaguzi. "kura hukomesha mashindano. Ni heri kunadi sera zako ili upate kura nyingi. Kukashfu kiongozi hakutakusaidia lolote badala yake unatafuta ugomvi wa makusudi na serikali. Fanyeni kampeni za kistarabu"

Hivi karibuni akihutubia kwenye uzinduzi wa kampeni hizo, mmoja wa viongozi wa chama kimoja cha upinzani alinukuliwa akisema kwamba ataleta malori 10 ya vijana toka Tarime ili kufanya fujo endapo chama chake hakitashinda kwenye uchaguzi mdogo wa diwani kata ya Isagehe wilayani hapa utakaofanyika tarehe 23 mwezi huu.

Uchaguzi huu mdogo unafanyika baada ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo kufariki dunia.

MAALIM YAHYA HUSSEIN AMTABIRIA MAKUBWA RAIS MAGUFULI NA CCM

$
0
0
Na  Humphrey Shao , Globu ya Jamii

Mtabiri na mnajimu maarufu Tanzania, Malim Hassan Yahya Hussein ametabiri makubwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais John Pombe Magufuli huku akitaja moja ya chama  cha upinzani kufa.

Yahya amesema kuwa anatabiri Chama cha Mapinduzi kushika hatamu katika chaguzi mbalimbali za mwaka huu huku moja ya chama kikuu cha upinzani kufa na viongozi waliotoka chama tawala kurudi huku viongozi wa dini na kisiasa kukumbwa na kashfa za ngono na ulevi.

“natabiri Rais John Pombe Magufuli kupata nishani ya juu ya Dunia kutoka kwa rais wa moja ya mataifa makubwa kutokana na uongozi wake” amesema Malim Yahya.

Aidha ametabiri kuwa katika kipindi cha mwaka 2017 viongozi kadhaa wa mataifa mbalimbali duniani watatoa matamshi ya ajabu yatakayowashangaza raia na wananchi wa nchi zao kiasi cha kusababisha kuanguka au kuuwawa kwa viongozi hao.

Pia amesema kuwa katika utabiri mwingine kuwa kutakuwepo kwa ajali nyingi zitakazo wakuta wanasiasa watawala na viongozi wa dini.

Alimaliza kwa kutoa ushauri kuwa vifo na maafa vinaweza visitokee iwapo watu wataacha rabsha na uharaka wa kufanya mambo kama nyota ya mwaka 2017 inavyosema.

DKT. SHEIN AZINDUA SOKO LA MATUNDA NA OFISI YA BARAZA LA MJI WETE PEMBA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa Soko la Matunda na Ofisi ya Baraza la Mji la Wete katika Shamara shamra za Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar,(kulia) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe.Omar Khamis Othman (wa pili kushoto).
Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Nd,Radhiya Rashid wakati alipolitembelea Soko la Matunda Wete Mjini Mkoa wa Kaskazini Pemba baada ya kulizindua rasmi leo katika Shamara shamra za Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwapungia mkono Wananchi wa Wilaya ya Wete leo baada ya kulizindua rasmi Soko la Matunda na Ofisi ta Baraza la Mji Wete Mkoa wa Kaskazini ikiwa ni katika Shamara shamra za Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar,(katikati) Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Nd,Radhiya Rashid.

GURU PLANE YAANDAA SEMA YA MAFUNZO YA KAZI KWA VITENDO KWA WAHITIMU WA VYUO VIKUU.

$
0
0

Na Antony John ,Globu ya Jamii

TASISI inayoshughulika na uandaaji wa Semina na Makongamano ya Mafunzo ya kazi kwa vitendo ya Guru Plane, imeandaa Semina ya kuwajengea uwezo vijana walio hitimu vyuo vikuu pamoja na vyuo mbalimbali ilikuepukana na tatizola ajira nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mkurugenzi mtendaji wa tasisi hiyo Nickosn Magezi amesema Vijana wengi ukumbwa na kizingiti cha changamoto ya uzoefu wa kazi wanapoingia katika soko la ajira.

Magezi amesema utafiti unaonyesha vijana wengi wanao hitimu vyuo vikuu na vyuo vingine Nchini wanakumbana na changamoto za kutopata ajira kutokana sababu ambazo zimekuwa zikitumiwa na waajiri wengini ni suala la wahitimu kukosa uzoefu wa kazi.

“ Semina hii itakuwana lengo la kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi na kuwapatia uzoefu wahitimu wa vyuo mbalimbali kwa mafunzo ya vitendo hilo ndio lengo kubwa ya semina yetu” amesema Magezi.

Sanjari na hayo ameongeza kuwa semina ya mafunzo ya kazi kwa vitendo imeweza kutatua changamoto za ukosefu wa ajira hasa pale taasisi na makampuni zinapokuwa zimehakikishiwa uzoefu wa kazi unaoendana na soko la ajira.
Mkurugenzi wa guru plane Nickosn Magezi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo

YANGA VS SIMBA " KARIAKOO DERBY' YAHAMIA UWANJA WA AMANI, KUKUTANA NUSU FAINALI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Baada ya ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Jang'ombe Boys zilizofungwa na mrundi Laudit Mavugo, timu ya Simba sasa itaumana na watani zao wa jadi Yanga katika mchezo wa nusu fainali wa kombe la Mapinduzi unaotarajiwa kuwa Jumanne.

Ni katika kipindi cha kwanza dakika ya 11, Mavugo anawainua mashabiki wa Simba baada ya kuipatia goli la kwanza na la kuongoza.

Mpaka inafika mapumziko Simba walienda kifua mbele kwa goli 1-0, na katika kipindi cha pili Simba waliingia kwa kasi na katika dk  54 ni  mavugo  Tena  anaiandikia  simba  bao  la  pili  baada  ya kufanya  juhudi  binafsi  Kwa  kuwatoka  mabeki  wa Jangombe  boys  na  kuachia  shuti  lililomshinda  kipa                 
                                       
 Dk ya 70 Jang'ombe walikosa bao la wazi baada ya shuti la Hafidh Bariki Juma kupanguliwa na kipa wa Simba ikamkuta Khamis Mussa Makame ambaye shuti lake lilitoka nje.  

Mpaka kufikia dakia 90 Simba wanatoka na ushindi wa goli 2-0 wakishika nafasi ya kwanza kwenye kundi A wakiwa na alama 10 na watakutana na Yanga kwenye mchezo wa nusu fainali.,
                      
 Jopo  la makocha  wa  timu  zote  mbili  limemchagua  laudit  mavugo  kuwa  man  of the mech  katika  mchezo  wa  leo.
 Kikosi cha Jang'ombe Boys kilichopambana leo na Simba katika mchezo wa hatua ya makundi uliomalizika kwa nSimba kupata ushindi wa goli 2-0.
Kikosi cha Simba Boys kilichopambana leo na Jang'ombe Boys katika mchezo wa hatua ya makundi uliomalizika kwa Simba kupata ushindi wa goli 2-0.
 Shiza Kichuya akipambana na beki wa Jang'ombe Boys katika mchezo  wa hatua ya makundi uliomalizika kwa Simba kupata ushindi wa goli 2-0.
Jamali Mnyate akiwatoka mabeki wa Jang'ombe Boys wakati wa  mchezo  wa hatua ya makundi uliomalizika kwa Simba kupata ushindi wa goli 2-0.


WAZIRI MKUU MJALIWA " AKIBA YA CHAKULA ILIYOPO NCHINI IENDELEE KUDHIBITIWA"

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, KASSIM MAJALIWA meagiza akiba ya chakula iliyopo nchini iendelee kudhibitiwa ili kuepukanana hatari ambayo i naweza kujitokeza kutona na maeneo mengi nchini hajaanza kupata mvua.Undani wa habari hii angalia hiyo hapo chini Video.Habari na www.ruvumatv.com.

DC WA BUHIGWE,KANALI GAGUTI AANDAA UTARATIBU WA KUPANDA MITI ZAIDI YA MILIONI MOJA KUPAMBANA NA TATIZO LA NYUMBA KUEZULIWA PAA

$
0
0

Na Rhoda Ezekiel-Globu ya Jamii Kigoma

MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marko Gaguti amewataka Wananchi Wa Wilaya ya Buhigwe kuzingatia kanuni za ujenzi kwa kujenga Nyumba zenye ubora na kupanda miti katika Nyumba zao ili kuepukana na majanga yatokanayo na Upepo mkali pamoja na Mvua kubwa zinazo endelea kunyesha na kusababisha madhara makubwa .

Akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Mnyegera ambapo upepo mkali ulitokea huko na kusababisha nyumba tisa kuezuliwa na kusababisha uharibifu wenye thamani ya Shilingi milioni 13 wakati akitembelea kuangalia uharibifu huo, Gaguti alisema nyumba nyingi zilizoezuliwa hazijajengwa kwa kuzingatia kanuni za ujenzi.

Gaguti alisema ili kuhakikisha tatizo hilo linakwisha Wilaya imeandaa utaratibu wa kupanda miti milioni moja na laki moja kwa Wilaya nzima na wananchi wote wanatakiwa kuzingatia utaratibu huo,Viongozi wa vijiji wanatakiwa kuzingatia zoezi hilo kila nyumba kupanda miti ya kutosha ili kuepukana na madhara ya kuharibikiwa Nyumba.

Aidha Gaguti aliwaomba viongozi wa kijiji kuwasaidia wote waliopatwa na majanga hayo kwa kipindi hiki ambacho serikali inatafuta namna ya kuwasaidia ili waweze kupata mahali pa kuzihifadhi familia zao.

"Poleni sana kwa majanga yaliyo wapata nimetembelea kote ambapo kimbunga kimeezua nyumba lakini hakuna majanga yaliyo tokea ya watu kupoteza maisha wala uharibifu wa mazao ni jambo la kumshukuru mungu kunabaadhi ya Bati zinaweza kutumika nahisi tasmini iliyofanyika inaweza kupungua, niwaombe tupande miti ilikujikinga na tatizo hili wakati tunasikitika kwa tukio lililojitokeza na niwaombe viongozi nione jitihada zenu kwa kuwasaidia sisi tutawasaidia kama Wilaya baada ya kuona juhudi zenu za kusaidiana",alisema Gaguti.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mnyegera Alfonce Ntatie alisema tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 6 Januari, ambapo kulitokea upepo mkubwa ambao ulieezua nyumba tisa na Kusababisha uharibifu wa shilingi milioni 13 ambapo Mpaka sasa juhudi za kuwasaidia wathilika wa tukio hilo zinaendelea kufanyika na Wananchi wanaendelea kuwachangia wenzao. 

kwa upande wao Baadhi ya Wananchi walio haribiwa nyumba zao na upepo mkari walisema Mpaka sasa wanalazimika kulala nje na familia zao suala ambalo linawapa wakati mgumu hasa ukuzingatia wakati huu ni wakqti wa Mvua.zinaendelea kunyesha na zikinyesha wanalazimika kunyeshewa na watoto wao.
 Moja ya nyumba iliyoezuliwa paa kama ionekanavyo pichani.
  MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marko Gaguti akiratibu tukio la kuezuliwa paa baadhi ya nyumba za wakazi wa kijiji cha Mnyegera wilayani Buhingwe kufuatia upepo mkali uliotokea wilayani humo na kupelekea nyumba tisa kuezuliwa paa zake. 
 MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marko Gaguti akiwapa pole Wananchi wa kijiji cha Mnyegera wilayani Buhingwe kufuatia upepo mkali uliotokea na kusababisha nyumba tisa kuezuliwa na kusababisha uharibifu wenye thamani ya Shilingi milioni 13.
MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marko Gaguti akiwa pamoja na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mnyegera wilayani Buhingwe waliothiriwa na  
upepo mkali uliotokea na kusababisha nyumba tisa kuezuliwa mapaa.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 9, 2017

MKUU WA MKOA WA RUKWA ATOA AMRI KUHUSU KUPOKEA, KUINGIZA, KUIHAMISHA, KUSAFIRISHA NA KUPITISHA MIFUGO NDANI YA MKOA WA RUKWA

$
0
0
Mkuu wa mko wa Rukwa kamishna Mstaafu Zelote Stephen amewaagiza wakuu wa Wilaya kutokubali kupokea mifugo kutoka katika wilaya nyingine bila ya mifugo hiyo kuipa kibali maalum cha kuhamia katika wilaya zao.

Ameyasema hayo katika amri halali namba 1/2017 kuhusu kupokea, kuingiza, kuihamisha, kusafirisha na kupitisha mifugo ndani ya mkoa wa rukwa kwa mamlaka aliyopewa na kifungu cha 7 cha sheria Nambari 19 ya mwaka 1997 ya Tawala za Mikoa Sura Namba 97 mapitio ya mwaka 2002, kwa lengo la kusimamia na kutekeleza maagizo ya waraka wa Rais Na. 1 wa mwaka 2002 unaokataza kabisa usafirihaji kiholela wa mifugo.

“Mifugo isihamishwe kutoka katika Kijiji, Wilaya ama Mkoa kabla ya kupata kibali cha Kijiji, Wilaya ama Mkoa inakopelekwa. Hivyo Kijiji, Wilaya na Mkoa itatoa kwanza idhini ya kupokea mifugo hiyo ndipo kibali cha kusafirisha mifugo kitolewe,” Zelote Stephen alisema.

Zelote Stephen alisisitiza kuwa Vijiji, Wilaya na Mkoa usitoe vibali vya kupokea mifugo kabla ya kujiridhisha kwamba wanayo maeneo ya kutosha ya malisho ya mifugo, yaliyopimwa na kuthibitishwa na wataalamu kama yanafaa kwa malisho na maji ya kutosha na majosho ya kuoshea mifugo.

Vile vile Mkuu wa Mkoa aliwaagiga maafisa mifugo kuanzia ngazi ya Kijiji, Wilaya na Mkoa kusisimamia na kuhakikisha hakuna mifugo inayosafirishwa kutoka Kijiji, Wilaya na Mkoa kwenda Mkoa mwingine au kuingia katika Kijiji, Wilaya au Mkoa bila ya kupimwa na kuchanjwa chanjo lengo likiwa ni kuthibiti uenezaji wa magonjwa ya mifugo nchini.

“Kabla ya kutoa vibali vya kusafirisha mifugo, madaktari wa mifugo wa Wilaya ama wawakilishi wao wahakikishe kwamba mifugo inaogeshwa na kuchanjwa dawa za kuzuia magonjwa husika kabla ya kuiruhusu mifugo hiyo kusafirishwa ili kuzuia uenezaji wa magonjwa ya mifugo,” Zelote Stephen alifafanua.

Aidha Mkuu wa Mkoa amewatahadharisha maafisa mifugo ambao sio waaminifu wanaotumia njia ya kuingiza mifugo kwenye wilaya kwa njia ya biashara za minada na matokeo yake mifugo hiyo kubaki eneo husika bila ya kufuata taratibu zozote.

Amri hii itafanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia tarehe 9 January, 2017 hadi tarehe 31 Desemba, 2017.

MKUU WA WILAYA ASIYEFATA MAELEKEZO YA MKUU WA MKOA ATAKUWA ANATAFUTA NAFASI YA KUACHA U DC

$
0
0

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, KASSIM MAJALIWA amewataka wa kuu wa wilaya kufuata maelekezo ya mkuu wa mkoa ,na kwa yule ambaye ataenda kinyume na maelekezo ya mkuu wa mkoa atakuwa anajitafutia nafasi ya kuondoka. Kwa undani wa habari hii angalia video yake. Habari na www.ruvumatv.com

Viewing all 110025 articles
Browse latest View live


Latest Images