Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

Profesa Mwandosya akagua upanuzi wa chanzo cha maji ruvu chini leo

$
0
0
  Waziri wa Nchi katika ofisi ya Rais asiye na wizara maalum Profesa Mark James Mwandosya akikagua  mradi wa MCC wa upanuzi wa chanzo cha maji Ruvu chini. Picha ya chini anapata maelezo kutoka kwa Eng. Kasiga wa DAWAS.Mradi huo wa Mellinium Challenge Corporation kutoka Marekani utagharimu milioni 36 9 dola za kimarekani.


MWANRI AZITAKA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KUSIMAMIA VIZURI FEDHA ZA MIRADI YA SERIKALI

$
0
0

Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akipima kwa tape maalum urefu wa moja ya barabara zilizojengwa na Manispaa ya Sumbawanga katika Mji huo kuhakikisha kama barabara hiyo imejengwa kwa vipimo vilivyoanishwa kwenye mpango wa ujenzi huo (BOQ). Naibu Waziri huyo alitumia fursa hiyo kuziasa halmashauri zote nchini kusimamia vyema fedha za Serikali katika miradi kuhakikisha inafanana na thamani ya fedha zilizotumika, alilazimika kusema hayo baada ya kubaini mapungufu mbalimbali katika mradi huo wa barabara na miradi mingine aliyofanikiwa kuitembelea Mkoani Rukwa.

Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akikagua barabara za lami zilizo chini ya Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga zilizojengwa hivi karibuni. Katika ukaguzi huo alibaini mapungufu mbalimbali katika ujenzi huo na kuagiza Halmashauri hiyo kuhakikisha mapungufu hayo yanaondolewa. Aliitaka pia halmshauri hiyo kusimamia vyema kazi za Serikali kuepusha minong'ono inayotoka kwa wananchi juu ya utendaji mbovu wa baadhi ya watendaji Serikalini.

Mhe. Agrey Mwanri akiweka jiwe la msingi kiwanda cha unga cha Malangali kinachomilikiwa na muwekezaji wa ndani mapema hivi leo. Kwa sasa Mkoa wa Rukwa una viwanda vitatu vya unga vinavyomiliwa na wawekezaji wa ndani.  

Naibu wa Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Agrey Mwanri akikagua kiwanda cha unga cha Malangali Mjini Sumbawanga leo alipotembelea kiwandani hapo kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi.

Mhe. Mwanri akizungumza na wakazi wa Mji wa Sumbawanga katika Stendi kuu ya mabasi ya Mjini hapo ambapo alipokea kero mbalimbali ikiwepo ubovu wa miundombinu ya umeme na barabara katika stendi hiyo. Aliuagiza uongozi wa Manispaa ya Sumbawanga kufanya Mkutano wa hadhara na wananchi hao kuskiliza kero zao zote pamoja na kuzitaftia ufumbuzi na kumpelekea taarifa ya utekelezaji.

Katika hali isiyotegemewa msafara wa Mhe. Mwanri ulipowasili katika kijiji cha Mlanda katika Manispaa ya Sumbawanga kwa ajili ya Mkutano wa hadhara ulikuta msiba ambapo walishiriki na kutoa ubani ambapo Mhe. Mwanri alitoa laki moja na alfu mbili na aliyekuwa Mbunge wa Sumbawanga Mjini CCM ambaye pia ni Mjumbe wa halmashauri kuu Taifa ya CCM (NEC) kupitia Mkoa wa Rukwa Aeshi Hillal alikabidhi shilingi alfu hamsini. (Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

Article 10

UZINDUZI WA MRADI WA "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA" ZANZIBAR

$
0
0
 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwapungia Mkono Vijana waliopita mbele ya Jukwaa la Uwanja wa Amaan Studiuam,akipokea maandamano ya vijana katika sherehe za  uzinduzi wa Mradi wa  "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA", ikiwa ni shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) ni Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na MIchezo Said Ali Mbarouk
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitia saini Mpira katika uzinduzi wa Mradi wa  "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA",mradi ambao utawapatia vijana wa Zanzibar Mipira Ishirini Elfu ,(20,000) katika vikundi mbali mbali na kupelekea kuongezeka kwa vipaji vya Soka nchini,katika sherehe za kuadhimisha miaka 49 ya mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
 Watoto wakibeba mabango yenye ujumbe tofauti unaosisitiza kulindwa haki zao,wakipita kwa maandamano mbele ya Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika sherehe za  uzinduzi wa Mradi wa  "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA", zilizofanyika katika Uwanja wa Amaan Studiuam,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea kitabu kutoka kwa Nasra Sheikh Mohamed,wa Skuli ya Mwembeshauri Mjini Unguja,kitabu  chenye Agenda ya Watoto kuhusu usisitizaji kwa Serikali na Jamii kushirikiana katika kuwapatia haki zao za Msingi bila unyanyasaji. katika uzinduzi wa Mradi wa  "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA",katika uwanja wa Amaan Studium ikiwa ni shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi zawadi Mwakilishi wa Shirika la UNICEF Paulo Edwards, katika sherehe za uzinduzi wa Mradi wa ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA" ,katika   Uwanja wa Amaan Studium, ikiwa ni shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar.[

RESI ZA NGARAWA ZAFANYIKA ZANZIBAR IKIWA NI SHAMRA SHAMRA ZA MIAKA 49 YA MAPINDUZI.

$
0
0
 Naibu Waziri wa Ardhi,Makazi,Maji na Nishati Haji Mwadini Makame akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza katika mshindano hayo Nahodha Fundi Abuubakar kutoka Bumbwini.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. PICHA NA MAKAME MSHENGA-MAELEZO ZANZIBAR.
 Ngarawa mbili za mbele zikichuana vikali katika mashindano yalio fanyika huko forodha mchanga ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
 Ngarawa zikianza mashindano mara tu ilipopulizwa firimbi ya kuanza mashindano hayo huko forodha mchanga ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. 
 Naibu Waziri wa Ardhi,Makazi,Maji na Nishati Haji Mwadini Makame akipuliza filimbi kuonyesha ishara ya kuanza kwa mashindano hayo.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
 Wananchi wakishangiria jinsi mpambano ulivyokuwa mkali huko forodha mchanga ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Ngarawa zikianza mashindano mara tu ilipopulizwa firimbi ya kuanza mashindano hayo huko forodha mchanga ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Super Sunday Football

$
0
0
Join us for an exciting Super Sunday BPL Classic – Clash of the Titans!!!! It’s Manchester United vs Liverpool & Arsenal vs Manchester City both matches live on HD, Sunday @ East 24 Bar, Arcade House, Mikocheni. 
Be there for a true live experience + free bottles of Bubbly for the winning teams… Dress Preference: Football T-shirts Please!!! 
Event by Shaffih Dauda & Sports Extra

ngoma azipendazo ankal - enzi hizo

$
0
0
Enzi hizo wengi walicheza chacha kila mara ngoma ya Carlos Santana ya Black Magic Woman ilipopigwa

ngoma azipendazo ankal - kizazi kipya

$
0
0
Ngoma ya injili ya 'Kiatu Kivue' cha Bibie Annastazia Mukabwa akimshirikisha Rose Muhando si mchezo... Sikiliza ujumbe huo!

viwanja vinauzwa.

$
0
0
Viwanja vinauzwa,vimepimwa na vina hati,vipo eneo la Viwanda Mwanambaya Mkuranga barabarani na vimezingatia hifadhi ya barabara,vimepakana na kiwanda cha Cement,kiwanda cha Gypsum na Yad ya Scania used,Heka 4 bei yake ni sh mil.700,zipo heka 28 nyuma ya hicho mil 700,zipo heka 4 zinapakana na ukuta wa kiwanda cha Cement Mil.600.

Zipo heka 6 hazijapimwa zipo barabarani  eneo hilo hilo mil 500. Mwandenga  zipo heka 67 Mil. 700,Zipo nyumba eneo la Gerezani  kariakoo Mil. 700 kwa Mil.900,Round about ya Kariakoo bilioni 1 na 200 milioni.Kariakoo stendi ya Kawe ni bilioni 1 na 200 mil. Ipo beach gezaulole Kigamboni Mil.600,pia vipo viwannja vya Mil.10 na vilivyopimwa kwa mil 25 Gezaulole-Kigamboni.

Kwa mawasiliano piga namba 0652020343

Article 3

Mdau wa Lindi ameremeta na Mai waifu wake

$
0
0
Mdau Shaban Leo wa Halmashauri ya wilaya ya Lindi akifurahia baada ya kufunga pingu za maisha na mai waifu wake Pendo Kuboga wa manispaa ya Lindi pia. Ndoa ilifungwa katika kanisa la Waadventista wasabato Mtaa wa Lindi na Tafrija ya kuwapongeza ilifanyika katika Ukumbi wa Kanisa la Mt Andrea Kaggwa.Picha na Abdulaziz Video.
Maharusi na Wapambe wao wakiwa kwenye nyuso za furaha.
Maharusi wakipewa Baraka ya Ndoa toka kwa Mchungaji.

MCHUNGAJI DANIEL NA HOYCE MBOWE WANAWAALIKA KWENYE IBADA YA PILI YA KISWAHILI ITAKAYONYIKA BONN: UJERUMANI

$
0
0
Mchungaji Daniel na Hoyce Mbowe, wanapenda kuwakaribisha wote wanaoongea Kiswahili hapa Ujerumani na marafiki wengine katika ibada ya pili ya Kiswahili itakayofanyika Jumapili hii tarehe 13.01.2013 .

Muda wa Ibada: Saa saba mchana (13:00 hours) hadi saa tisa mchana ( 15:00 hours).

Mahali: Evangelischen Friedenskirchengemeinde Bonn

Anuani: Franz-Bücheler-Straße 10
53129 Bonn

Ibada hii ya Kiswahili itakuwa ikifanyika kila Jumapili ya pili ya kila mwezi, ibada ya Kwanza ilifanyika tarehe 9 mwezi uliopita na kuhudhuriwa na watu wengi.

Mawasiliano: dmbowe@hotmail.com or hoycembowe@hotmail.com
Wote mnakaribishwa: Karibuni tumwabudu na tumsifu Mungu wetu.

TASWIRA MBALI MBALI ZA MH. KANDEGE ALIPOPANDA MLIMA KILIMANJARO

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Kalambo,Mh. Josephat Kandege akiwa katika kilele cha Gilmans alipopanda Mlima Kilimanjaro mwishoni mwa mwaka jana,Mh Kandege ndiye mbunge pekee aliyefanikiwa kufika katika kilele hicho kati ya wabunge saba waliopanda mlima Kilimanjaro.
Mbunge wa Jimbo la Kalambo,Mh. Josephat Kandege akiwa na wapandaji wengine ambao kwa pamoja walifanikiwa kufika katika kituo hicho cha Gilmans mmoja wapo akiwa ni Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.
Mbunge wa Jimbo la Kalambo,Mh. Josephat Kandege akiwa katika kilele cha Gilmans alipopanda Mlima Kilimanjaro mwishoni mwa mwaka jana,Mh Kandege ndiye mbunge pekee aliyefanikiwa kufika katika kilele hicho kati ya wabunge saba waliopanda mlima Kilimanjaro.
Safari ya Mlimani ikiendelea.
Ukiwa juu ya mlima Kilimanjaro hivi ndivyo maeneo mbalimbali ya mlima yanavyoonekana. Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

MH. AMOS MAKALLA AKABIDHI VIFAA MBALI MBALI JIMBONI KWAKE MVOMERO

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( kati kati kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Kijiji cha Matale, Kata ya Mvomero akiwemo Muunguzi wa Zahanati ya Kijiji, Margreth Ngole na Diwani wa Kata ya Mvomero, Seleman Miraji ( wa kwanza kulia) juzi ( Jan 10) baada ya kukabidhi vitanda viwili na magodoro kwa matumizi ya wagonjwa kwenye Zahanati hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Kikundi cha Sungusungu Kijiji cha Ndole, Kata ya Kinda, Lucas Henry , vifaa vya aina mbalimbali vya ulinzi kwa ajili ya Askari wa Sungusungu ‘Polisi Jamii’ wa Kijiji hicho kwa lengo la kuimalisha ulinzi ndani ya Kata hiyo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kinda, katika Kata ya Kinda, Wilaya ya Mvomero, Garusi Manyaku ( kushoto) akipeana mkono na Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ( kulia) ikiwa ni ishara ya kupokea madawati 25 yaliyotolewa na Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo walipofanya ziara juzi ( Jan 10),kwenye Kata hiyo,( kati kati ) ni Kaimu Ofisa Elimu Salum Masalanga na nyuma ni baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo akiwa ameketi katika dawati pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kinda, iliyopo katika Kata hiyo baada ya kuukabidhi uongozi wa Shule madawati 25 aliyoyatoa masaada kwa lengo la kupunguza tatizo hilo wakati alipofanya ziara juzi ( Jan 10) kwenye Kata hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( kati kati kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Kijiji cha Matale, Kata ya Mvomero akiwemo Muunguzi wa Zahanati ya Kijiji, Margreth Ngole na Diwani wa Kata ya Mvomero, Seleman Miraji ( wa kwanza kulia) juzi ( Jan 10) baada ya kukabidhi vitanda viwili na magodoro kwa matumizi ya wagonjwa kwenye Zahanati hiyo.

Wateja 70 waibuka washindi kwenye droo kubwa ya Promosheni ya Patapata na Nokia Ushinde

$
0
0
Msimamizi wa michezo ya kubahatisha Tanzania,Bw.Mrisho Millao akishuhudia Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bw.Kelvin Twissa akiongea na mmoja wa washindi Bw.Fidel Ngowi mkazi wa sinza jijini kupitia simu ya mezani,wakati wa kuchezesha droo kubwa ya mwisho ya promosheni ya PATAPATA na Nokia iliyokuwa ikiendeshwa na Vodacom pamoja na Nokia, msimu wa sikukuu, Jumla ya washindi 70 wamepatikana kupitia droo hiyo,anaeshuhudia kulia ni Meneja Masoko wa Nokia Bi.Ellen Lupilli.
Meneja wa Idara ya vifaa vya mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bw.Elihuruma Ngowi(kushoto)akimpigia simu mmoja wa washindi kati ya 70 walioibuka kidedea wakati wa droo kubwa ya mwisho ya promosheni ya PATAPATA na Nokia iliyokuwa ikiendeshwa na Vodacom pamoja na Nokia, msimu wa sikukuu, Jumla ya washindi 70 wamepatikana kupitia droo hiyo,kulia ni Msimamizi wa michezo ya kubahatisha Tanzania,Bw.Mrisho Millao, na katikati ni Meneja Masoko wa Nokia Bi.Ellen Lupilli.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bw.Kelvin Twissa akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani,wakati wa kuchezesha droo kubwa ya mwisho ya promosheni ya PATAPATA na Nokia iliyokuwa ikiendeshwa na Vodacom pamoja na Nokia, msimu wa sikukuu, Jumla ya washindi 70 wamepatikana kupitia droo hiyo,kushoto Msimamizi wa michezo ya kubahatisha Tanzania,Bw.Mrisho Millao na kulia ni Meneja Masoko wa Nokia Bi.Ellen Lupilli.

Rais wa Madagascar awasili kuhudhuria mkutano wa SADC-TROIKA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), (kushoto) akisalimiana na Mhe. Andry Rajoelina, Rais wa Madagascar mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Januari, 2013. Mhe. Rais Rajoelina yupo nchini  kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano unaoendelea wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC-TROIKA).
Mhe. Rais Rajoelina akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili.
Mhe. Rais Rajoelina akiwa amefuatana na Mhe. Membe mara baada ya kupokelewa.
Mhe. Rais Rajoelina akipita katikati ya Gwaride  lililoandaliwa kwa heshima yake huku akisindikizwa na Mhe. Membe
Mhe. Rais Rajoelina akiwa na Mhe. Membe wakifurahia burudani ya ngoma za utamaduni zilizokuwepo Uwanjani hapo mara baada ya kuwasili.

aongoza kikao cha Asasi ya Siasa,Ulinzi na Usalama cha SADC Rais Adry Rajoelina wa Madagascar ahudhuria

$
0
0
Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa,Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo kusini Mwa Afika SADC Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na na Rais wa Madagascar Andry Rajolina(kulia),Rais Wa Namibia Hifikepunye Pohamba(kushoto) na Rais wa Msumbiji  Armando Guebuza Ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi wakati wa kikao cha Kamati hicho leo. Picha na Freddy Maro wa Ikulu

RATIBA ZA KAMATI ZA BUNGE JANUARI, 2013

$
0
0
Ofisi ya Bunge inapenda kuwataarifu Wanahabari wote kuwa Vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge vitaanza kukutana hapa jijini Dar es Salaam siku ya Jumatatu 14 Januari 2013, kabla ya Mkutano wa 10 wa Bunge unaotarajiwa kuanza Mjini Dodoma siku ya Jumanne Januari 29, 2013. 

Kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, Kamati hizi hukutana angalau majuma mawili kabla ya Vikao vya Bunge, ili kupitia Taarifa mbalimbali za utekelezaji wa Shughuli za Serikali na Taasisi na Idara zake, ikiwa ni pamoja na kupitia miswada inayotarajiwa kuletwa Bungeni. 

Aidha baadhi ya Kamati zitajihusisha na kufanya Ziara za Ukaguzi katika Sehemu mbalimbali nchini kwa mujibu wa Kanuni ya 114 (1- 5) kama Ratiba inavyojionesha katika kiambatanisho BOFYA HAPA

MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO CHA PILI, 2012

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Mtihani wa Taifa wa Elimu ya Sekondari Kidato cha Pili ulifanyika nchini kote kuanzia tarehe 05/11/2012 na kumalizika tarehe 16/11/2012. 
Mwaka 2012 kulikuwa na jumla ya vituo 4,304 vilivyosajili watahiniwa, ikiwa ni ongezeko la vituo 117(2.79 %) ikilinganishwa na ile ya mwaka 2011. 

YALIYOJIRI WAKATI WA UZINDUZI WA DARAJA LA MBUTU, IGUNGA

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa darala la Mbutu wilayani Igunga katika mkoa wa Tabora Januari 7, 2013. Kukamilika kwa ujenzi wa daraja hili mnamo Novemba mwaka huu kutakuwa ukombozi mkubwa kwa wananchi wa eneo hilo na mikoa ya jirani
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images