Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1494 | 1495 | (Page 1496) | 1497 | 1498 | .... | 3283 | newer

  0 0

   NA VICTOR  MASANGU, KIBITI
  LICHA ya  serikali ya awamu ya tano  kuongeza  juhudi za kuboresha sekta ya afya katika maeneo mbali mbali hapa nchini bado sehemu nyingine utoaji wa huduma hali bado ni tete kutokana na kukabiliwa na changamoto mbali mbali  ikiwemo ukosefu wa wauguzi,madaktari, madawa, magari ya kubebea wagonjwa,vitanda  pamoja na vifaa tiba hivyo kusababisha wagonjwa kupata shida kubwa pindi wanapokwenda kupatiwa matibabu.

  Changamoto hizo  ambazo zinadaiwa ni sugu na hazijafanyiwa utekelezaji wowote zimeweza kubainika baada ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Japo kufanya  ziara yake ya kikaz ya siku mbili kwa wananchi wa Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani  hususan katika maeneo ya wananchi wanaoishi katika maeneo ya Delta kwa ajili ya kukagua miradi  mbali mbali ya maendeleo pamoja na kubaini changamoto za muda mrefu zilizokuwa zinawakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.

  Naibu Wazari Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo wa kati kati akiwa kwenye boti katika ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Kibiti na viongozi wengine wa serikali,na wa kwanza kulia  kwake ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Khatibu Chaurembo kwa ajili ya safari ya kwenda kuwatembelea wananchi wa maeneo ya Delta kwa ajili ya kukagua miradi ya  mbali mbali maendeleo.(PICHA NA VICTOR MASANGU)  Taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Makete Veronica Kessy
  Image may contain: mountain, sky, outdoor and nature
  Na Edwin Moshi, Makete

  HERI YA MWAKA MPYA!
  Ndugu wananchi wa Makete na Watanzania wote kwa ujumla,wananchi wa kijiji cha Isapulano katika kata ya Isapulano hapa Wilayani Makete wamepatwa na maafa mnamo tarehe 02/01/2017.
  Maafa hayo yalisababishwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo,jumla ya nyumba 16 zenye jumla ya watu 37 ziliathirika kwa viwango tofauti.
  Katika tukio hilo waliumia watu wawili,wakapatiwa matibabu katika Zahanati ya Isapulano na kwa bahati nzuri wanaendelea vizuri,Aidha tunamshukuru Mungu hakuna mwananchi aliyefariki.
  Ndugu wananchi nyumba hizo zinahitaji vifaa vya ujenzi yaani matofali, saruji, mbao, misumari, mabati n.k, pia wananchi walioathirika wanahitaji kusaidiwa mahitaji ya kibinadamu kwa hiyo nawaomba wananchi na wadau wote wa ndani na nje ya Wilaya ya Makete tuguswe kwa namna moja ama nyingine kuchangia fedha au vitu ili kuwasaidia wananchi hao.
  Kwa sasa wananchi hao wamehifadhiwa na majirani na ndugu zao,Aidha wananchi wa kijiji hicho wameanza kujitolea kusaidia ujenzi huo.
  Ninawashukuru na kuwapongeza kwa jitihada hizo,nawasihi tuwaunge mkono kwa kutoa misaada ya hali na mali,michango ya fedha iingizwe kwenye Akaunti ifuatayo iliyopo NMB MAKETE.
  Jina la Akaunti:Kijiji cha Isapulano 
  Namba ya Akaunti:60410004408
  Na msaada wa vitu au vifaa uwasilishwe kwa Mtendaji wa kata ya Isapulano Bi.Tabu Mohamed mwenye namba 0745571046
  Ahsanteni sana 
  Ni mimi Veronica Kessy 
  Mkuu wa Wilaya ya Makete

  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku kushoto akimkabidhi rangi Ustadhi wa Madrasat Ikhilaswi ,Ibrahim Hassani Mtaa wa Mwarongo Kata ya Marungu kwa ajili ujenzi wa msikiti huo
   Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akisoma risala ya Madrasat Ikhilaswi mara baada ya kukabidhiwa baada ya kwenda kuwatembelea na kukabidhi msaada wa makopo ya rangi kwa ajili ya ujenzi unaoendelea.
  Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akuzungumza na wanafunzi wa Madrasat Ikhilaswi wakati alipotembelea kuona changamoto wanazokabiliana nazo ikiwa ni ziara yake lakini pia aliwakabidhi makopo ya rangi
  Hili ni Jengo la Madrasat Ikhilaswi lililopo mtaa wa Mwarongo Kata ya Marungu Jijini Tanga muonekano wake.habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0


  0 0

  Kama wewe ni mpenzi wa filamu ya kihindi basi sura ya Mwigizaji huyu mashuhuri nchini India Om Puri, ambaye pia aliigiza kwenye filamu zilizovuma sana nchini Uingereza si ngeni machoni mwako, Mwigizaji huyu amefariki dunia leo Januari 6 akiwa na umri wa miaka 66.

  Om Puri aliigiza kwenye filamu ya ucheshi ya East is East nchini Uingereza ambayo ilisimulia kuhusu maisha ya mhamiaji kutoka Pakistan aliyekuwa akizoea maisha ya kaskazini mwa England.

  Taarifa zinasema mwigizaji huyo alifariki baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo nyumbani kwake huko Mumbai nchini India.

  Om Puri alijulikana sana kwa ustadi na uigizaji wake katika filamu za Kihindi miaka ya 1980.

  Aidha, aliigiza kwenye filamu za Kiingereza, zikiwemo Mahatma Gandhi ya Richard Attenborough.

  Aliigiza pia katika filamu za Pakistan na Hollywood.
  Mwaka 2004, alitunukiwa nishani ya staha ya OBE kwa mchango wake katika tasnia ya filamu Uingereza.

  Puri, alizaliwa 1950 jimbo la Haryana, kaskazini mwa India.

  Filamu yake ya kwanza kuigiza ilikuwa ya Ghashiram Kotwal mwaka 1976.
  nchini India, anafahamika kwa filamu maarufu za Ardh Satya, Sadgati, Paar na filamu ya ucheshi ya Jaane Bhi Do Yaaro.

  0 0

  Madaktari nchini Kenya wameigomea nyongeza ya mishahara na posho iliyopendekezwa na serikali yao, ikiwa ni katika juhudi za kujaribu kumaliza mgomo wa madaktari na wahudumu wa afya ambao umedumu kwa takribani mwezi mmoja sasa.

  Mgomo huo ambao kwa sasa umelemaza huduma za matibabu katika hospitali na zahanati za umma nchini Kenya, umekuwa ukiishinikiza serikali kuwalipa mishahara itakayokidhi mahitaji ya madaktari na wauguzi hao.

  Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta alikutana na wawakilishi wa chama cha taifa cha madaktari hao mapemna Jumanne wiki hii na kupendekeza nyongeza ya mshahara na marupurupu ya madaktarii kwa angalau $560 (£450).

  Hilo lingesababisha madaktari wanaoanza kazi kulipwa takriban $2,000 kila mwezi.
  Viongozi wa chama hicho, ambao walikuwa wameahidi kutangaza msimamo leo, walisema pendekezo la serikali linawafaa madaktari lakini kuna baadhi ya mambo ya kuwafaa wananchi ambayo yameachwa nje.

  Madaktari wanaitaka serikali kutekeleza makubaliano ya mishahara na marupurupu yaliyotiwa saini mwaka 2013.

  Kwenye makubaliano hayo, serikali iliahidi kuongeza idadi ya madaktari, kuongeza pesa za utafiti wa kimatibabu, dawa na vifaa na mitambo katika hospitali za umma.

  0 0

  Jitihada za Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan za kuiingiza Tanzania katika mpango mkubwa wa Biashara kwenye bara la Asia, Mashariki ya kati,Ulaya na Afrika umefanikiwa baada ya Tanzania kuchaguliwa kuwa miongoni mwa nchi Saba kuingizwa katika mpango unaojulikana kama China One Belt, One Road Stratergy.

  Nchi nyingine ambazo zimechanguliwa kuingizwa kwenye mpango huo ni Malaysia,Sri lanka, Nepal, Bangladesh,Pakistan na Thailand.

  Baada ya Tanzania kuingizwa rasmi katika mpango huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye pia Mjumbe katika jopo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kumuwezesha mwanamke kiuchumi akiwakilisha nchi za ukanda wa Kusini na Mashariki mwa Afrika amekutana na Watendaji kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF),Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Biashara (TCCIA) na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kuwaeleza kuhusu muhimu wa Tanzania kuingizwa kwenye mpango huo.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania imepata uanachama wa mpango huo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mfanyabiashara wa Madini na Vito kutoka China Dkt Helen Lau kuhusu manufaa ya mpango huo na Makamu wa Rais alimwomba Mfanyabiashara huyo kuisaidia Tanzania kuingia kwenye mpango huo China One Belt, One Road Stratergy jambo ambalo limefanikiwa.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa Mwezi Septemba mwaka 2016 ulifanyika mkutano Guangdong nchini China kujadili maombi ya kujiunga na mpango huo ambapo Makamu wa Rais alimwomba Dkt Helen kuiwakilisha Tanzania katika kuwasilisha maombi na kwa bahati nzuri ombi la Tanzania lilikubaliwa na kupata uanachama katika mpango huo mkubwa wa China One Belt, One Road.

  Makamu wa Rais amesema kuwa moja ya fursa zinazotolewa na Serikali ya China katika mpango huo ni kila nchi Mwanachama kupewa vyumba vya ofisi katika jengo linaloitwa 21st Century Maritime Silk Road Expo bila kulipa kodi ya pango kwa miaka Mitatu na baadhi ya vyumba vya jengo hilo vitatumiwa na nchi husika kuonyesha na kutangaza bidhaa zao.

  Kufutia Tanzania kuingizwa kwenye mpango, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewaagiza watendaji wa sekta binafsi alikutana nao ikulu jijini Dar es Salaam wajipange na kuweka mikakati ya namna ya kunufaika na mpango huo haraka iwezekanavyo.

  Amesisitiza kuwa mpango huo wa China One Belt, One Road Stratergy uliobuniwa na serikali ya China kwa dhamira ya kuzikutanisha Jumuiya za Wafanyabiashara za Mashariki mwa bara Asia, Mashariki ya kati, Ulaya na Afrika kwa ajili ya kubadilishana mawazo,kuonesha njia na kupeana ushauri wa jinsi ya kukuza biashara kati ya nchi wanachama wa mpango huo kwa lengo la kuiwezesha sekta ya biashara kuchangia nyema kwenye uchumi wa mataifa yao. 

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania baada ya kuingia kwenye mpango huo itanufaika na fedha za mfuko kwa ajili ya maendeleo ya miundombinu ambazo zinatolewa kwa nchi zilizojiunga na mpango huo.

  Kwa upande wake, Mweyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania Godfrey Simbeye na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar Taufik Turki wamemuahidi Makamu wa Rais kuwa watatumia fursa hiyo ipasavyo ili kukuza biashara kati ya Tanzaniana Nchi wanachama wa mpango huo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wenyeviti wa TPSF,CTi,TCCIA na ZNCCIA juu ya mpango wa kibiashara unaojulikana kama China One Belt, One Road ulio asisiwa na serikali ya China na unajumuisha bara la Asia, Mashariki ya Kati,Ulaya na Afrika, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Wenyeviti wa TPSF,CTi,TCCIA na ZNCCIA juu ya mpango wa kibiashara unaojulikana kama China One Belt, One Road ulio asisiwa na serikali ya China na unajumuisha bara la Asia, Mashariki ya Kati,Ulaya na Afrika.

  0 0

   LakeFmHabari.

  Baadhi ya akina mama waliojifungulia katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure, wameishukuru serikali pamoja na wadau wengine wa afya kwa kuendelea kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo.

  Akina mama hao wameyasema hayo jana baada ya mbunge wa viti maalumu kupitia Chama cha Mapinduzi mkoani Mwanza, kukabidhi msaada wa vitanda, magodoro, mashuka na vyandarua katika hospitali hiyo.

  Wamesema hivi sasa huduma za afya hususani kwa mama na mtoto zimeboreshwa katika hospitali hiyo ikilinganishwa na kipindi kilichopita ambapo wameomba maboresho zaidi yaendelelee ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.

  Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonard Subi amesema huduma za afya zinaendelea kuboreshwa katika halmashauri mbalimbali mkoani Mwanza huku msisitizo ukiwa ni kuwahamasisha akina mama kujifungulia kwenye vituo vya afya.

  Mbunge wa viti maalumu kupitia Chama cha Mapinduzi mkoani Mwanza, Kemirembe Lwota kwa kushirikiana na taasisi ya Mo Dewji amesaidia upatikanaji wa mashuka 100 pamoja na vitanda 20 vilivyoambana na magodoro pamoja na vyandarua.
  Kutoka kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, mbunge viti maalumu CCM Mkoani Mwanza, Mkuu wa Mo Dewji Foundation, Mwenyekiti wa UWT mkoani Mwanza pamoja na wadau wengine, wakiwa kwenye wodi ya akina mama hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, kujionea hali ya wodi hiyo.

  0 0

   Mkuu wa wilaya ya Mbulu, Chelestino Mofuga  akizungumza na wananchi wa kijiji cha Gidmadoy baada ya kusikiliza mgogoro wa mapato na matumizi uliodumu tangu 2014 hadi 2016. Mkuu wa wilaya aliagiza kukamatwa mtendaji wa kijiji ambaye alihamishwa kinyume cha utaratibu kukimbia madeni na kumweka ndani masaa 48.

   Pia mkurugenzi aliagizwa kukagua taarifa ndani ya siku saba na kuleta taarifa kwa wananchi. Pia mkurugenzi aliagizwa kutuma watalaam wa ardhi kukagua maeneo yaliyopimwa na kulalamikiwa na wananchi. Wananchi walikiri hawajawahi kutembelewa na Mkuu wa wilaya au kiongozi wa wilaya tangu kuanzishwa kwa kijiji hicho kwake
  Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mkuu wa wilaya Mbulu


  0 0


  Na Adili Mhina, Dar.

  Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango imefanya ziara katika Mradi wa ujenzi wa Barabara za juu (Flyovers) unaoendelea katika makutano ya barabara za Nyerere/Mandela Jijini Dar es salaam na kuelezwa kuwa utekelezaji wake umefikia asilimia 19.2.

  Ziara hiyo iliyofanyika hivi karibuni kwa lengo la kuangalia maendeleo ya mradi huo ilitoa fursa kwa Bw. Kiyokazu Tsuji, Mhandisi Mkazi kutoka Kampuni ya ujenzi ya Sumitomo Mitsui ambayo ndiyo inayotekeleza ujenzi huo kueleza maendeleo ya ujenzi kwa wataalam kutoka Tume ya Mipango. 

  Mhandisi huyo alieleza kuwa malengo ya awali yalielekeza kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Novemba 2016, utekelezaji uwe umefikia asilimia 21.2 lakini lengo hilo halikufikiwa kutokana na moja ya mashine kupata hitilafu na kulazimika kuagiza wataalam kutoka nje ya nchi kuja kuifanyia matengenezo. 

  Hata hivyo Mkandarasi huyo alieleza kuwa tayari wamejipanga vizuri katika kuhakikisha wanafidia muda uliopotea wakati mashine hiyo ilipokuwa haifanyi kazi ili ujenzi wa barabara hizo ukamilike ndani ya muda uliopangwa. 

  Nao walaalam kutoka Tume ya Mipango walieleza kuwa Serikali na Wananchi kwa ujumla wanatarajia kuwa ujenzi huo utakamilika kwa muda uliopangwa hivyo Mkandarasi huyo ana wajibu wa kufanya kila linalowezekana ili mradi huo ukamilike kwa wakati. 

  Wataalamu hao pia walimshauri Mkandarasi huyo kuwa ni vyema akawapeleka nje wataalam wanaoziendesha mashine hizo ili waweze kupata ujuzi na uwezo wa kutengeneza mitambo pale inapohitajika badala ya kusubiri watu kutoka nje kuja kufanya kazi hiyo. 

  Walieleza kuwa kuwepo kwa wataalam wa ndani wenye uwezo wa kutatua hitilafu zinazojitokeza katika mitambo itasaidia kupunguza gharama na kuokoa muda ili kufanya mradi uende bila kusimama.

  Ujenzi huo unaotekelezwa kwa miezi 35 kauanzia Disemba 1, 2015 hadi Oktoba 31, 2018 unalenga kupunguza tatizo la msongamano wa magari na kuboresha huduma za usafiri katika Jiji la Dar es Salaam.
   Mhandisi Mkazi kutoka Kampuni ya ujenzi ya Sumitomo Mitsui, Bw.Kiyokazu Tsuji (wa kwanza kulia) akionesha hatua zilizofikiwa katika mradi wa ujenzi wa Barabara za juu (Flyovers) eneo la Tazara Jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni kiongozi wa timu ya ukaguzi wa Miradi kutoka Tume ya Mipango, Mhandisi Omari Athuman.
    Kiongozi wa timu ya ukaguzi wa Miradi kutoka Tume ya Mipango, Mhandisi Omari Athuman (mwenye shati ya mikono mifupi) akitoa ushauri kwa wahandari wanaotekeleza mradi wa ujenzi wa bararabara za juu jijini Dar es Salaam.
    Shughuli za ujenzi wa barabara za juu (Flyovers) zikiendelea katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.
      Mhandisi Omari Athuman (kulia) akiongea na Ofisa Mshauri wa masuala ya usalama kazini,  Bw. Richard Barwan wakati wa ziara ya Timu ya Mipango katika mradi wa ujenzi wa Barabara za juu eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.  

    Shughuli za ujenzi wa barabara za juu (Flyovers) zikiendelea katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.

  0 0

  *Wagharimu sh. bilioni 1.092, unahudumia wakazi 5,300

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua mradi wa maji safi na tenki lenye uwezo wa kuhifadhi lita 200,000 ambao utahudumia vijiji viwili vya Mkongotema na Magingo katika kata ya Mkongotema, wilayani Songea, mkoani Ruvuma.

  Akisoma taarifa ya mradi huo kwa Waziri Mkuu jana (Alhamisi, Januari 5, 2017), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba, Bw. Shafi Mpenda alisema mradi huo ulioanza kujengwa mwaka 2013, umegharimu sh. bilioni 1.09.

  “Hadi kukamilika kwake, mradi huu umegharimu sh. 1,092,439,812 ambapo kati ya hizo sh. 1,069,647,312 zimetolewa na Serikali kuu na sh. 22,792,500 zimechangwa na wananchi,” alisema.

  Bw. Mpenda alisema mpaka sasa kaya 915 zenye watu 5,300 zinahudumiwa na mradi huo wenye vituo 57 vya kutolea huduma za maji kwa jamii. Alisema lengo lao ni kufikisha vituo 71 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

  Akifafanua zaidi, Bw. Mpenda alisema kukamilika kwa mradi huo kumesaidia kuwapunguzia wananchi gharama za kununua maji ambapo pipa moja liligharimu sh. 3,000. “Pia kutasaidia kupunguza adha ya kufuata maji umbali mrefu; kupunguza magonjwa yanayotokana na mlipuko na kuwapa wananchi muda wa kutosha kufanya shughuli nyingine za maendeleo,” alisema.

  Akizungumza na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa mradi huo, Waziri Mkuu aliwapongeza wakazi hao kuwa kukubali kuchangia ujenzi wa mradi huo kwani katika baadhi ya maeneo miradi kama hiyo imekwama kukamilika kwa sababu wananchi waligomea kuchangia.

  Aliwataka wakazi wa vijiji hivyo wasiharibu mazingira na watunze vyanzo vya maji ili mradi huo uweze kuwa endelevu. “Mradi huu ni lazima tuutunze kwani hali ya hewa imebadilika sana hivi sasa, sababu ni sisi wenyewe wananchi ambao tumekata miti sana ili kupanua maeneo ya kilimo.”

  “Changamoto inayotupata hivi sasa ni kwama tumebakia kuwa na eneo kubwa la kilimo lakini mazao yanayopatikana ni kidogo. Mtazamo wetu katika Serikali hivi sasa ni kulima kwenye eneo dogo lakini mavuno yawe mengi,” alisema.

  “Mtu asilime chochote karibu na chanzo hiki ili tuweze kukitunza chanzo chetu. Na wenyeviti wa Serikali za vijiji vyote viwili, wekeni utaratibu wa wananchi kwenda kupanda miti ili eneo hili libaki kuwa na unyevunyevu kwa muda mrefu,” alisisitiza.

  “Sera ya Serikali ni kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata maji katika umbali usiozidi mita 400, na hili tutaweza kulitimiza kama tu mtatunza vyanzo vya maji vilivyopo,” alisema.

  Alitumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wa vijiji hivyo watunze akiba ya chakula walichonachi kwa sababu hali ya hewa imebadilika na hakuna anayejua mvua itaanza kunyesha lini. “Hatujui mvua itakuja lini na kwa kiasi gani; mara zitakapoanza kunyesha kila mmoja katika familia ahakikishe analima mazao mbadala kama kunde, maharage na mihogo ambayo yanastahimili ukame,” alisema.

  Waziri Mkuu pia alikagua utoaji huduma kwenye kituo cha afya cha madaba na ujenzi wa kituo cha kupozea umeme cha Madaba.


  IMETOLEWA NA
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  IJUMAA, JANUARI 6, 2017.

  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimjulia hali Sophia Mgeni ambaye ametoka kujifungua mtoto wa kike, Waziri mkuu alitembelea Zahanati ya Madaba iliyopo wilaya ya Songea ili kuwasikiliza wagonjwa katika zahanati hiyo Waziri mkuu yupo Mkoani Ruvuma kwa ziara ya kukagua shughuli za maendeleo 
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wauguzi wa zahanati ya Madaba huku akiwataka waendelee na moyo waliokuwa nao wa kuwapenda wagonjwa na kuwahudumia, kwani serekali inatambua mchango wao wanaoutoa kwa taifa
  Waziri Mkuu Kassim  Majaliwa akiwahutubia wananchi wa madaba waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza,Waziri Mkuu alitumia nafasi hiyo kuwaelezaa  Wananchi hao juhudi za serekali za kuwasaidia katika sekta mbali mbali ikiwemo Huduma ya bima ya afya.  Waziri mkuu yupo mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi.Picha na Chris Mfinanga

  0 0


  0 0

  *Wasomi wamshukia, wamtaka aache siasa

  WADAU mbalimbali wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwa muwazi kwa wananchi wake wakati wanapohitaji misaada mbalimbali wakati wa majanga.

  Wametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizi kueleza kauli ya hivi karibuni ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye amekaririwa akidai kuwa kauli za Rais mkoani Kagera ni za hatari.

  Wamesema kuwa baadhi ya Watanzania wamezoea kupewa ahadi ambazo kwa wakati mwingine ni vigumu kutekelezeka na sasa watu kama Mbowe bado wako kwenye mtazamo huo.Wameongeza kuwa Rais Magufuli amekuwa siku zote mkweli, jambo ambalo baadhi ya watu wasiopenda ukweli wanapotosha kauli zake kwa kutaka kuwachonganisha wananchi na Rais wao ambaye amekusudia kuwaletea wananchi maendeleo.

  Rais Magufuli akiwa Kagera hivi karibuni alisisitizia msimamo ambao si mpya, umekuwa msimamo wake na wa Serikali tangu yalipotokea maafa ya tetemeko la ardhi mkoani humo kwamba Serikali itasaidia lakini haitaweza kumjengea nyumba kila mtu.“Baadhi ya wanasiasa na viongozi wamekuwa wakitoa kauli zenye kupotosha na kubeza hotuba ya Rais Magufuli mkoani Kagera jambo ambalo sio zuri na sio ukomavu wa kiasa” walisema.

  Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cvha Dar es Salaam, Dkt Bashiru Ally amesema kuwa katika mfumo wa siasa huru kuna kutofautiana mitazamo kati ya wananchi ,Serikali na viongozi wa siasa lakini ni wazi kuwa Rais alisimama katika msimamo wa Serikali yake na uwezo wa kutekeleza ahadi zake.

  Alisema kuwa Rais Magufuli alikuwa na maana nzuri ya kukabiliana na majanga nchini inategemea uwezo wa nchi na mshikamano wa wananchi na huo ni ukweli ambao wengi hawakupenda kuusikia.

  Dkt. Bashiru Ally alisema kuwa kwa janga la Kagera kulikuwepo mshikamano wa Serikali katika ngazi zote, wananchi na wadau mbalimbali walishiriki kwa namna moja ama nyingine kukabiliana na janga hilo.

  “Wito wangu ni kuwataka wanasisa kujifunza kutokana na majanga badala ya kutoa kauli tatanishi na zenye kubomoa mshikamano wa wananchi, bali wanatakiwa kukosoa bila kubeza, kupotosha kwa namna ni ya kungwana,” alisema Dkt Bashiru

  Kwa upande wake Dkt. Benson Bana kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema kuwa watu wanatafsiri vibaya maneno ya Mhe. Rais aliyoyaongea Mkoani Kagera hivi juzi.“Mheshimiwa ameongea ukweli kwa sababu ni sahihi kuwasaidia watu wengi kwa pamoja kuliko kumsaidia mtu mmoja mmoja,” alisema.
  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akiwaangalia wafanyakazi wa Shirika la ZSTC wakitoa uchafu katika Karafuu zinazotayarishwa kwa mauzo  ambazo huingizwa  katika chupa na kuwekewa alama maalum kwa ajili ya mauzo  wakati alipotembelea kazi hizo leo katika  uzinduzi Awamu ya kwanza ya Branding  ya Karafuu ya Zanzibar,ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(wa pili kushoto) Mkurugenzi Mwendeshaji Dkt.Said Seif Mzee
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akipata maelezo kwa Asmahani Abdulkadir alipotembelea Karafuu zinazotiwa katika chupa kuwekewa alama maalum kwa ajili ya mauzo  wakati alipowasili Saateni Mjini Unguja kuzindua Awamu ya kwanza ya Branding  ya Karafuu ya Zanzibar  leo,ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) Mkurugenzi Mwendeshaji Dkt.Said Seif Mzee.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Viongozi,Wafanyakazi na Wananchi  katika hafla ya Uzinduzi wa Awamu ya kwanza ya Branding  ya Karafuu ya Zanzibar huko Saateni Mjini Unguja leo,ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe,Amina Salum Ali
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(kulia) akinyanyua Nembo ya KARAFUU kama ishara ya Uzinduzi wa  Awamu ya kwanza ya Branding  ya Karafuu ya Zanzibar,uliofanyika leo  huko Saateni Mjini Unguja,ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya  miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe,Amina Salum Ali,(kushoto) Mwenyekiti wa Bodi ya ZSTC Maalim Kassim Suleiman.  

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi akiwasilisha mada iliyohusu mapendekezo ya mkakati wa pamoja wa kudhibiti uvuvi haramu wa kutumia mabomu, katika mkutano wa Makatibu wakuu na wadau wa sekata ya mazingira ulohusu mkakati wa kudhibiti uvuvi haramu wa kutumia mabomu.
  Kushoto Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Profesa Faustin Kamuzora akizungumza katika kikao cha Makatibu wakuu na wadau wa sekta husika za masuala ya mazingira, katika mkutano ulohusu mkakati wa kudhibiti uvuvi haramu wa kutumia mabomu. Mkutano huo wa ndani ulifanyika katika ukumbi wa mkutano wa Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam. (Picha na Evelyn Mkokoi). Sehemu ya washiriki katika mkutano wa Makatibu Wakuu wa Wizara na wadau wa  sekta husika za masuala ya mazingira uliohusuhusu mkakati wa kudhibiti uvuvi haramu wa kutumia mabomu.

  0 0

  Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu, Mhe. Harold Reginald Nsekela akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake leo.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela (wa pili kulia) alipomtembelea Waziri huyo ofisini kwake leo.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akimsikiliza Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela (hayupo pichani) alipotembelewa na Kamishna huyo ofisini kwake leo.


  0 0

  SERIKALI kupitia Wizarya afya , maendele ya jamii , Jinsia Wazee na Watoto imetenga bilioni 251 ili kuimarisha upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya na zahanati zote nchini.
  Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara Ya Afya, Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee Na Watoto Dokta Mpoki wakati wa mahojiano katika kipindi cha Tunatekeleza kinachoendeshwa na kituo cha matangazo TBC1 jijini Dar es salaam.
  “Kutokana na taarifa zinazozagaa juu ya upungufu wa dawa katika zahanati hapa nchini ,taarifa hizo si za kweli napenda kuwatoa hofu wananchi na bajeti yetu ya mwaka huu ni shilingi Bil. 251 kwa ajili ya dawa tu” alisema Dkt. Ulisubisya. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, KASSIM MAJALIWA katika ziara yake ya Siku ya Pili mkoani Ruvuma ametembelea na kukagua eneo litakalojengwa mtambo wa kupoozea umeme wa Gridi ya Taifa kutoka Makambako mkoani Njombe kwenda Songea mkoani Ruvuma . Habari kamili hii hapa video yake.Ruvuma Tv


  0 0

  Na Stella Kalinga, Simiyu
  Serikali  Mkoani  Simiyu imedhamiria kwa mwaka 2017 kutatua na kuondoa migogoro yote  ya  ardhi ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara kwa wananchi wa mkoa huo.
  Akitoa ufafanuzi wa namna ya  kutatua kero hiyo wakati wa mkutano wake na wananchi wa jimbo la  Meatu ,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka alisema kuwa amechoshwa kusikia na kuona migogoro ya ardhi  inayojitokeza ndani ya mkoa wake, hivyo mwaka 2017 ndio utakuwa mwisho wa kero hizo.
  Mtaka amesema kuwa kamwe hawezi kukubali kuona migogoro  hiyo inaendelea hivyo wananchi na watendaji wa idara ya ardhi wanapaswa kila mmoja ajue utaratibu sahihi wa utoaji na ununuaji wa ardhi ili kuepusha sintofahamu zinazojitokeza.
  “ mwaka huu  wa 2017 ni mwaka ambao mimi mkuu wa Mkoa wa Simiyu nimeamua kusimamia, kusikiliza na kutatua kero zote za ardhi… Nataka ndani ya kipindi hichi ifikie mahali migogoro ya ardhi kwa mkoa wa Simiyu inakuwa sio kipaumbele chetu… alisema Mtaka.
   Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka (kushoto) akiwa na Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Simiyu kupitia CCM, Mhe. Leah Komanya wakizungumza na wananchi wa Wilaya ya Meatu katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kituo cha Mabasi cha Mjini Mwanhuzi kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wilayani humo.
   Ndg. Ngodongo Maganga mkazi wa kijiji cha Cambala wilayani Meatu akimweleza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) kero yake ya kuporwa eneo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kituo cha Mabasi cha Mjini Mwanhuzi kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wilayani humo.
   Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilonga, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Meatu, Fabian Manoza, Mbunge Viti Maalum, Mhe. Leah Komanya, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini wakimkabidhi mabati Bibi Yunge Masanja yaliyotolewa na Mhe.Mbunge Komanya ili kumsaidia katika ujenzi wa nyumba yake.
   Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Simiyu, Mhe. Leaah Komanya wakizungumza na Bibi Yunge Masanja mara baada ya kumkabidhi mabati yaliyotolewa na Mbunge huyo kwa lengo la kumsaidia kujenga nyumba.

older | 1 | .... | 1494 | 1495 | (Page 1496) | 1497 | 1498 | .... | 3283 | newer