Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

HAPPY NEW YEAR FROM TANZANIA BLOGGERS NETWORK


MAGAZETI YA LEO JUMATAU JAN 2

WALEMAVU WA KIJIJI CHA LULANZI WAMLILIA MBUNGE RITTA KABATI

0
0

Na Fredy Mgunda,Iringa

FAMILIA ya watu watano wenye ulemavu wa viungo wamemuomba mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rita Kabati kuendelea kuilea familia hiyo kama familia
yake.

Akizungumza na blog hii mmoja wa wanafamilia hiyo,Elias Mpogole ambaye ni mlemavu alisema kuwa mbunge huyo amekuwa akiwasaidia toka siku ya kwanza walipokutana naye katika kijiji hicho cha Lulanzi.

“Zamani tulikuwa tunaishi kwenye nyumba ambayo inavuja haina dilisha wala mlango pia tulikuwa tunalala chini lakini mbunge Kabati katusaidia nyumba nzuri kama mnavyoiona waandishi,katuletea magodoro,mashuka,blanket na sasa ameanza kutujenga choo cha kisasa na ameshawalipa mafundi pesa zote ndio maana tunaomba anendelee kuwa na sisi.”Alisema Mpogole

Mpogole alishukuru msaada waliopatiwa na kuwataka wadau wengine waweze kujitokeza zaidi kuwasaidia kuwapatia vyakula na radio za kuwezakusikiliza nyimbo za dini.

Kwa upenda wake mbunge wa viti maalum mkoa waIringa(CCM) Rita Kabati ametoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo ukarabati wanyumba kwa familia yenye watoto walemavu wanne wa kijiji cha Lulanzi kilichoko kata ya Mtitu wilayani Kilolo mkoa wa Iringa. 

Mbunge wa viti maalum mkoa waIringa(CCM) Rita Kabati akiongea na familia ya watu watano wenye ulemavu wa viungo alipowatembea katika kijiji cha Lulanzi kata ya Mtitu wilayani Kilolo mkoa wa Iringa wakati wa kuwasaidia msaada kukarabati nyumba yao pamoja na kuwapa vitu vingine vya kimsaada
Leah mwamoto mtoto wa mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto naye alishuhudia maisha magumu wanaoishi familia ya watu watano wenye
ulemavu wa viungo alipowatembea katika kijiji cha Lulanzi kata ya Mtitu wilayani Kilolo mkoa wa Iringa na hapo aliposimama ndio choo kinachotumiwa na familia hiyo kwa sasa huku wakisubili ujenzi wa choo kipya kinachoendelea kujengwa kwa hisani ya mbunge Ritta kabati
Hivi ni baadhi ya vifaa vilivyoletwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rita Kabati kwa ajili ya kuwasidia familia ya watu watano wenye ulemavu wa viungo alipowatembea katika kijiji cha Lulanzi kata ya Mtitu wilayani Kilolo mkoa wa Iringa.

39 wauawa wakikaribisha mwaka mpya Uturuki

0
0
 WATU takriban  39 wakiwemo wageni 15 wanahofiwa kuuawa katika shambulio lililotokea katika moja ya klabu ya burudani mjini Istanbul Uturuki usiku wa kuamkia mwaka mpya 2017.

Kwa mujibu wa waziri wa maswala ya ndani nchi hiyo, Süleyman Soylu alisema Mtu aliyekuwa amejihami kwa bunduki aliwafyatulia risasi watu waliokuwa wakijiburudisha katika mkahawa huo wa Reina majira ya saa saba usiku wakati ambapo watu walikuwa wakisherehekea kuingia kwa mwaka mpya.
Idanaiwa kuwa Mtu huyo aliingia katika klabu hiyo akijifanya kikaragosi kilichovaa mavazi ya Santa Claus na punde alianza kuwafyatulia risasi kiholela waliokuwepo ndani ya klabu hiyo ya burudani, hali iliyopelekea Baadhi yao kujirusha baharini kuepuka msusuru wa risasi zilizokuwa zinafyatulia na mtu huyo.Polisi mmoja ni miongoni mwa waliofariki.

Huku waliojeruhiwa wakikimbizwa hospitali, maafisa wa usalama wanaendelea kufanya upekuzi katika eneo hilo lakini muhusika wa shambilo hilo hajakamatwa bado.

Waziri wa mazingira nchini Burundi auwawa kwa kupigwa risasi

0
0
Waziri wa mazingira katika Serikali ya Burundi, Emmanuel Niyonkuru, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi mjini Bujumbura saa chache tu baada ya kuingia mwaka mpya.

Polisi nchini wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa kusema amepigwa risasi alipokuwa akielekea nyumbani kwake eneo la Rohero.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, ameapa kuchukua hatua kali za kisheria kwa atakayepatikana na hatia ya kuhusika katika mauaji hayo.

Mamia ya watu , wakiwemo maafisa wa ngazi za juu katika jeshi wameuawa tangu Rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu 2015, hatua ambayo wapinzani wanasema ni kinyume na sheria.

Lakini hii ni mara ya kwanza kwa waziri wa serikali kuuawa.
Kwa miezi kadhaa taifa hilo limekuwa tulivu.CHANZO:BBC SWAHILI

MATUKIO MAKUBWA YA MUZIKI WA DANSI NCHINI KWA MWAKA 2016

0
0
BENDI MPYA
•Tarehe 26-Feb-2016, bendi mpya ya BMM ilizinduliwa rasmi katika ukumbi wa Mzalendo Pub. Bendi hiyo, pamoja na wanamuziki wengine, inaundwa na Mule Mule FBI (Rais wa bendi) na Totoo Ze Bingwa. Bendi pia inamjumuisha mpiga solo mahiri Losso Mukenga, ambaye pia ni mpiga solo wa Ally Kiba. Hata hivyo bendi hii ilidumu kwa muda mchache sana.

•Tarehe 08-Apr-2016 (Ijumaa), bendi mpya ya Sky Melodies chini ya uongozi wa Nicco Millimo, ilitambulishwa ndani ya Club la Aziz Classic, Dodoma.

•May-2016, bendi mpya ya Ivory Band ilianzishwa. Bendi hii kwa asilimia kubwa imeanzishwa na wanamuziki waliotokea bendi ya Double M Plus baada ya kutokea mtafaruku. Wanamuziki hawa ni kama Dogo Rama, Saleh Kupaza, Jojo Jumanne, Rashid Sumuni na kadhalika.

•Nov-2016, bendi ya Original Dar Musica ilianzishwa chini ya mwanamuziki Jaddo Field Force. Hii ni baada ya mwanamuziki Jaddo Field Force kuenguliwa (au kujiengua) katika bendi ya Dar Musica.

•Tarehe 24-Dec-2016 (Jumamosi), bendi mpya inayoitwa DSS Band (Dar-es-Salaam Super Sound) “Wazee wa Kujilipua” yazinduliwa rasmi katika ukumbi wa Family Bar, Tabata Mbuyuni. Bendi hiyo inamilikiwa na wanamuziki Ferguson na Rogart Hegga “Caterpillar”.

BOFYA HAPA KUONA MATUKIO ZAIDI

WATANZANIA SAIDIENI JAMII YA WATU WASIOJIWEZA - Dkt. Geordavie

0
0

 Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie akiombea  bajeti mbalimbali  za waumini walizoziletwa kwa ajili ya kutolewa neno la unabii hiii leo

Na Woinde Shizza,Arusha.

Watanzania nchini wametakiwa kusaidia Jamii ya watu wasiojiweza ikiwemo walemavu,watoto yatima pamoja na wazee ili waweze kupata mahitaji yao na kuondokana na umasikini uliokithiri.

Hayo yameelezwa na Baadhi ya Wananchi waishio katika kata ya Kisongo mkoani Arusha ambapo walisema kuwa jamii ya wahitaji imekua ikiishi katika mazingira magumu hivyo ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha kuwa anawasaidia jamii hiyo.
"Katika jamii kuna watu wengi wakiwemo watoto wanatoto na watu wasio jiweza ambao wanakaa katika mazingira magumu mno  hivyo ni wajibu wetu sisi kuwasiaidia wale ambao awajiwezi ,mtu ukiwa na uwezao kidogo unatakiwa ujijengee tabia ya kuwasiaida hawa wasio jiweza"alisema Sekela Tondolo

Mkazi mwingine wa kata ya  Kisongo Wiliam James Alisema kuwa  jamii ya wasiojiweza imekua ikisahaulika mara kwa mara hivyo ni jukumu la kila Mwananchi kuhakikisha kuwa anafanya kitu kwa ajili ya jamii yake kitakacholeta mchango ambao ni chanya na kuwawezesha kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo kimaisha.

Mheshimiwa Nabii Mkuu Dkt. Geordavie  wa Huduma ya Ngurumo ya Upako  katika ibada ya makusanyo ya vitu na fedha kwa ajili ya kuwasaidia wahitaji alisema kuwa taasisi za dini hazina budi kujikita katika kuwasaidia wahitaji na wasiojiweza ili kuwa na taifa imara na endelevu.
"Ni wajibu wa taasisi za kidini  ,makampuni mbalimbali , hata watu binafsi ambao wanauwezo kuweza kusaidia watu hawa wenye mahitaji na walae wasio jiweza ili nao wajisikie vyema na kuona nao  ni sehemu ya watu kama wengine "alisema  Dkt. Geordavie

Huduma hiyo inautaratibu endelevu wa kila mwaka wa kupeleka mahitaji kwa wato wasiojiweza pamoja na kuwawezesha kiuchumi kaya zilizoathiriwa na umasikini kwa kiasi kikubwa.

WAKAZI WA KASULU WAMWOMBA RAIS DKT MAGUFULI KUTATUA MGOGORO MIGOGORO YA MIPAKA KATI YA WANANCHI NA HIFADHI YA MISITU YA KAGERANKANDA

0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

CHAMA Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kasulu Kimemuomba Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli kuitimiza ahadi yake ya kuwasaidia Wananchi wa Wilaya ya Kasulu ya Kutatua Migogoro ya Mipaka inayo endelea baina ya Wananchi na eneo la hifadhi ya Misitu ya kagerankanda kama alivyo wahahidi Wananchi hao Wakati wa Kampeni kutatua kero hiyo endapo watakichagua Chama hicho.

Akizungumza na gazeti hili katibu mwenezi wa Wilaya ya Kasulu Masoud Kitowe alisema wakati wa kampeni Rais aliwaomba Wananchi hao wakichague Chama cha mapinduzi na kuwaahidi endapo watakichagua chama hicho atahakikisha anatatua mgogoro huo na kuongeza mipaka Kwa Wananchi hao waweze kulima,na Wananchi walikichagua chama hicho mpaka sasa ahadi hiyo haijatekelezwa.

Alisema CCM Wilaya ya Kasulu wanapata shida kuwajibu Wananchi dhidi ya mgoholo unaoendelea katika poli la Kagerankanda Wananchi wanao kutwa Wakilima katika poli hilo wanapigwa na kunyanganywa vifaa vyao kwa madai kuwa hawaruhusiwi kulima katika poli hilo ilihali maeneo ya kulimia katika Wilaya hiyo ni Machache na Wananchi wengi wanategemea kulima Mahindi katika poli hilo.

Kitowe alisema mpaka sasa Dawa zimeshafika katika Wilaya ya Kasulu iliwatu wa TFS waliopewa Dhamana ya kulinda msitu huo wamejipanga kumwagia Tindikari mahindi na Maharage yaliyo pandwa katika poli hilo hali inayoweza kupelekea Wilaya ya Kasulu na wilaya zingine za Mkoa wa Kigoma kukabiliwa na Njaa kwakuwa mazao yanayo limwa katika Msitu huo yanahudumia zaidi ya Wilaya nne za Mkoa wa Kigoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAGAZETI YA LEO JUMATAU JANUARI 2, 2017

RC KIGOMA,BRIGEDIA JENERALI MSTAAFU EMANUEL MAGANGA AWATAKA WANANCHI KUTOKUDAI FIDIA MARA MBILI

0
0

Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

MKUU wa Mkoa wa Kigoma , Brigedia Jenerali msaafu Emanuel Maganga amewataka Wananchi wa Mkoa wa Kigoma kuacha tabia ya kudai fidia mara mbili katika maeneo yao yanayo chukuliwa kwaajili ya kufanyiwa uwekezaji wa viwanda na uchumi hali inayopelekea Mkoa huo kushindwa kuendelea kwasababu ya Baadhi ya watu wanaong'ang'ania maeneo kwa kudai walipwe fidia ya ziada.

Rai hiyo aliitoa jana wakati akitoa salamu za Mwaka mpya kwa Wananchi wa Mkoa huo katika kanisa la Kiinjili la kiruthel Tanzania KKKT ushirika wa Kigoma alisema Mkoa wa kigoma kwa mwaka 2017 tumeandaa kubolesha Uchumi kwa kuanzisha viwanda vingi na kutenga maeneo kwaajili ya Shughuli za kiuchumi jambo ambalo litasaidia mkoa huu kufunguka kiuchumi.

Maganga alisema kumekuwa na tabia ya Wananchi wengi wa Mkoa wa huu kudai fidia mara mbili unakuta eneo moja wanakuja watu zaidi ya wawili kudai fidia ya sehemu moja hali inayo pelekea Serikali kushindwa kufikia malengo yake kwakuwa fedha inayotengwa kwaajili ya suala la kuwekeza kwenye uchumi inaishia kuwalipa watu fidia tumeyaona hayo wakati wa kulipa fidia kwa eneo tunalo tarajia kujenga Bandari ya Nchi kavu.

"Serikali ya Mkoa wa Kigoma kwa mwaka uliopita tumejitahidi sana kubolesha huduma za Kijami ikiwa ni pamoja na elimu ambayo imetuletea matokeo mazuri kwa mwaka uliopita Mkoa wa Kigoma umeshika nafasi ya kwanza kitaifa na umeongoza kwa asilimia 94% kwa mwaka huu kipaumbele chetu ni kuhakikisha tunakuza uchumi wa Mkoa wetu,"alisema Maganga.

Alisema kuanzia sasa utaandaliwa utaratibu utakao saidia kujua ninani anastahili kulipwa fidia na kila eneo moja atalipwa Mtu mmoja watu wasitumie Fulsa ya uwekezaji wa Serikali kama njia ya kutajilika na kupatia mitaji tutajitahidi kufanya kazi hii kwa ufanisi ilikuhakikisha malengo tuliyo yaweka kwa mwaka huu yanakamilika.

Aidha Maganga amewaomba Wananchi kufanya kazi kwa bidii na kuwaahidi huduma zote zitakazo tolewa na Serikali yake zitakuwa nzuri na zenye lengo la kuwasaidia wananchi wenye kipato cha chini iliwaweze kuinuka na kufikia uchumi wa kati kwa kubolesha miundombini mbalimbali ya kijamii itakayo fungua Fulsa za maendeleo ya Mkoa huo.

Aliwaomba wafanya biashara kusafilisha bidhaa mbalimbali kupeleka nje ya Mkoa wa Kigoma kwa kutumia barabara zilizo jengwa vizuri kwa mwaka huu ilikuhakikisha Uchumi wa Mkoa wa Kigoma unakuwa kwa kasi na kwa kiwango cha juu.

Nae Mchungaji wa Ushirika wa kanisa la Kiinjili la Kiruthali Mkoa wa Kigoma Emanuel Mtoi aliiomba serikali kuwahurumia Wanachi kwa kuwaboleshea huduma za kufanyia biashara na kuwawekea miundombinu mizuri ya kuwawezesha kufanya biashara bila kubuguziwa.

Alisema Mwaka huu wananchi wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuweka malengo na mikakati itakayo wasaidia kujikwamua kiuchumi na kuacha kuilaumu serikali kwamba imebana hela na kushindwa kufanya kazi iliwapate fedha.

SERIKALI KULIPA DENI LA WALIOTHIRIKA NA WANYAMAPORI - MHANDISI MAKANI

0
0
NA HAMZA TEMBA - WMU

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema italipa madeni yote ya miaka ya nyuma ya vifuta jasho na vifuta machozi ambayo inadaiwa na wananchi waliokubwa na vitendo vya uharibifu wa wanyamapori nchini kabla ya bunge lijalo la bajeti, madeni hayo ni yale ambayo yameshaifikia wizara hiyo na kuhakikiwa. 

Akizungumza jana na uongozi wa wilaya ya Bunda wakati wa kuhitimisha ziara yake ya siku moja ya kufuatilia changamoto za uhifadhi wilayani humo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani amesema uamuzi huo wa Serikali utaondoa kilio cha muda mrefu cha wananchi ambao wamepata madhara mbalimbali ya wanyamapori ikiwemo vifo, majeruhi, kuliwa mazao na kuharibiwa mashamba yao. 


"Serikali ya awamu ya tano imeshakamilisha takwimu za madai, yale yote tunayodaiwa huko nyuma, yaliyoifikia Wizara yakafanyiwa uhakiki na nimesema kwenye uhakiki huo ndani ya kipindi cha miaka kumi, kwa wilaya zaidi kidogo ya 80 ambazo ndizo zina changamoto hizi kwa kiwango kikuu, deni jumla ni shilingi 2,081,532,700 (bil. 2.9)", amesema. 


Amesema wilaya ambazo zimeathirika zaidi na vitendo hivyo na ambazo madai yao ni makubwa zaidi ya Wilaya zingine ni Serengeti na Bunda ambazo ziko mkoani Mara na zinapakana na Hifadhi ya taifa ya Serengeti, Ziwa Victoria, Pori la Akiba Grumeti na Ikorongo. "Serengeti ndiyo inayoongooza kwa madai hayo, shilingi milioni 408,547,600 alafu Bunda shilingi milioni 265,969,750",. 

Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akikagua moja ya shamba la mahindi lililoharibiwa na tembo katika kijiji cha Kunzugu, wilaya ya Bunda Mkoani Mara jana  wakati wa ziara yake ya kuangalia changamoto za uhifadhi mkoani humo. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili. 

Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kunzugu, wilaya ya Bunda, mkoani Mara jana alipotembelea moja ya shamba la mahindi lilioharibiwa na tembo wakati wa ziara yake ya kuangalia changamoto za uhifadhi mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Wanadiplomasia wa Urusi waliotimuliwa Marekani waondoka

0
0
Vyombo vya habari vya Urusi vimeripoti kuwa wanadiplomasia 35 wa Urusi waliotimuliwa na rais Barack Obama kutoka Marekani wameondoka wakiandamana na familia zao.

Urusi ilituma ndege maalum ya kuwarudisha nyumbani.

Wanadiplomasia hao waliamuriwa kuondoka Marekani baada ya Urusi kushtumiwa kuwa ilijaribu kuingilia uchaguzi wa hivi majuzi wa Marekani kwa njia ya udukuzi wa mitandaoni.

Vyombo vya kijasusi vya Marekani vinadai kuwa utawala wa Urusi ndio ulioamuru kudukuliwa kwa hasa tovuti ya chama cha Democratic ili kuvuruga kapeni za bi Clinton na kumsaidia Donald Trump ambae sasa ndiye rais mteule.CHANZO: BBC SWAHILI

BEI YA MADAFU LEO

WAZIRI MKUU AMJULIA HALI MAJIMAREFU KAIRUKI HOSPITALI

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani ambaye amelazwa katika hospitali ya Kairuki, Mikocheni jijini Dar es salaam akitibiwa Januari 2, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mhe. Steven Ngonyani (Profesa Majimarefu) aliyelazwa katika Hospitali ya Kairuki akipatiwa matibabu.
Akiwa hospitalini hapo leo (Jumatatu, Januari 2, 2017), Waziri Mkuu amesema amefurahi baada ya kumkuta Mbunge huyo anaendelea vizuri na kwamba afya yake inaridhisha.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumtakia afya njema Mhe. Ngonyani. Amesema anaamini hivi karibuni atapona na kuruhusiwa kutoka hospitali.
Kwa upande wake Mbunge huyo ambaye amelazwa katika hospitali ya Kairuki iliyoko Mikocheni jijini  Dar es Salaam, amemshukuru Waziri Mkuu kwa kwenda kumjulia hali.

Pia amesema anaendelea vizuri na anatarajia kwenda nchini India kwa matibabu zaidi mara taratibu zitakapokamilika.

 IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
JUMATATU, JANUARI 2, 2017.

TTCL Kudhamini Mashindano Ya Soka la Ufweni

0
0

Na. Lilian Lundo – MAELEZO

Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imedhamini mashindano ya Soka la ufukweni kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu vilivyopo Jijini Dar es Salaam yanayotarajiwa kufanyika katika fukwe za Coco Januari 07 mwaka huu.

Afisa Mkuu wa Mauzo kutoka Kampuni hiyo Peter Ngota ameyasema hayo leo, Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya udhamini huo.

Aliendelea kwa kusema kuwa, mashindano hayo yanawalenga wanafunzi wa Vyuo Vikuu vilivyopo Jijini Dar es Salaam ambao ni wadau wakubwa wa Kampuni ya TTCL kupitia huduma ambazo wanazitoa kama vile vifurushi vya intanenti, dakika pamoja na ujumbe mfupi.

“Tumeamua kudhamini mashindano hayo kwa wanafunzi hao kutokana na umuhimu wa michezo kwao katika kuwajengea amani, furaha na afya njema ambavyo vitawawezesha kufanya vizuri katika masomo yao na hata kuwa wabunifu katika maeneo wanayosomea na kupelekea nchi kufikia uchumi wa kati,” alifafanua Ngota.

Kwa upande wake kocha Mkuu wa mashindano hayo John Mwansasu ameishukuru Kampuni ya TTCL kwa kudhamini mashindano hayo ambayo bado hayajapata umaarufu mkubwa hapa nchini.

Aidha amesema kuwa, ili kuwapa uzoefu washiriki wa mashindano hayo, kutakuwepo na wachezaji ambao walichezea timu za Simba na Yanga ambao pia watacheza kutokana na timu ambazo walikuwa wakichezea.

Vilevile Mwansasu amesema kuwa, wataendelea kushirikiana na Kampuni ya TTCL ili kusambaza mchezo huo katika mikoa yote ya Tanzania.

Vyuo vilivyothibitisha ushiriki wa mashindano hayo mpaka sasa ni Chuo cha Biashara (CBE), Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Chuo Kikuu Huria (OUT), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) pamoja na Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT). Mashindano hayo hayatakuuwa na kiingilio na yataanza saa 3:00 asubuhi.

KINGA DHIDI YA UGONJWA WA PEPO PUNDA IPO-SERIKALI

MAHAKAMA YATOA MAELEKEZO KWA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI KUFANYA MAREKEBISHO MOJA YA KIFUNGU CHA SHERIA YA MITANDAO

0
0
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa kupinga sheria ya mtandao iliyotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015 ili kulinda maslahi ya Taifa ya kupambana na kutoa mwelekeo wa kukabiliana na makosa ya mtandao.

Hukumu hiyo ya kihistoria ilitolewa na jopo la majaji watatu, Prof. John Ruhangisa, Winfrida Korosso na Lugano Mwandambo mara baada kuona hoja zilizowalishwa na wakili wa kujitegemea Jebra Kambole kuwa hazina msingi.

Hata hivyo, mahakama hiyo imetoa maelekezo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kufanya marekebisho kwenye kifungu kimoja kati ya 18 vya sheria hiyo vilivyokuwa vikilalamikiwa kwa vile kifungu hicho kinakiuka haki ya msingi ya mwananchi ya kusikilizwa.

Pamoja na kutoa maelekezo hayo, mahakama imeona vifungu vingine ndani ya sheria hiyo havikuwa na mapungufu yoyote ya kikatiba kama ilivyokuwa inadaiwa na mwombaji (Kambole).

Katika malalamiko yake, Kambole alidai kuwa Sheria ya mtandao ilikuwa na baadhi ya maneno ambayo hayakutafasiriwa ambavyo kwa namna moja au nyingine vingeweza kuchambuliwa vibaya na vyombo vya usalama na hivyo kumwonea mwananchi.

Hata hiyo, jopo la majaji hao waliona hoja hizo hazina mashiko mara baada ya kupitia kwa kina vifungu vya Sheria husika na kuona kuwa vifungu hivyo lalamikiwa vinaainisha kosa ambalo linaweza kutendeka na kutoa adhabu inayotakiwa.

Majaji hao wamebainisha kuwa vifungu namba 4, 5, 6, 7, 8, 9, 14, 19, 21 na 22 vya sheria ya mtandao vilivyolalamikiwa vinaenda sambamba na Ibara ya 17 (2) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hivyo haviwezi kwenda kinyume na katiba.

Kwa mujibu wa jopo hilo, mwananchi anayonafasi ya kupinga maamuzi yanayotolewa na kiongozi kwa kupeleka maombi ya mapitio (judicial review) mahakama kuu kama itabainika kuwa alienda kinyume na madaraka yake aliyopewa kisheria.

Mara baada ya kufikia uamuzi kuwa vifungu hivyo vya sheria ya mtandao havikinzani na Ibara ya 17 (2), 20 (5) na 30 (2) vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, majaji hao walikataa wito wa mlalamikaji wa kuviona vifungu hivyo vinakiuka katiba.

Kambole katika maombi yake alilalamikia pia vifungu namba 38 na 50 vya sheria ya mtandao kwamba vinakiuka Ibara ya 13 ya Katiba juu ya mwananchi kuwa na haki ya kusikilizwa.

Mlalamikaji huyo alidai kuwa kifungu namba 38 kinatoa uhuru kwa mamlaka kupeleka maombi mahakamani ambayo yanaweza kusikilizwa kupitia upande mmoja bila upande wa pili katika maombi hayo kuhusishwa.

Hata hivyo, majaji hao walibainisha kuwa kifungu hicho kinahusiana na maswala ya kufanya upekuzi, kukamata, kukusanya na kuweka wazi takwimu kwa lengo la upelelezi. Katika mazingira hayo, majaji waliona kuwa malalamiko yaliyotolewa hayakuwa na msingi wowote kwa vile maswala ya upelelezi hayatoi ukomo katika kutatua haki ya mwananchi.

Suala la Usafi wa Mazingira kuwa liwe utamaduni wa kudumu

0
0

Na Is-haka Omar, Zanzibar.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewataka wananchi, wanachama, viongozi na watumishi wa Chama na Jumuiya zake kufanya suala la Usafi wa Mazingira kuwa utamaduni wa kudumu ili kuenzi Mapinduzi ya mwaka 1964 kwa vitendo.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai wakati akifanya usafi wa Mazingira kupitia Tawi la CCM la Afisi Kuu Zanzibar Kisiwa Ndui lililopo katika maeneo ya Ofisi hiyo, Mjini hapa.

Alifafanua kwamba suala la usafi wa mazingira nchini lifanyike kwa ushirikiano wa wananchi wote bila ya kujali tofauti zao za kidini, kisiasa na kikabila kwani panapotokea athari mbaya zinazotokana na uchafu zinawakumba jamii nzima.

Alisema usafi wa mazingira ni miongoni mwa mambo muhimu yaliyokuwa yakisisitizwa na waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, kwa lengo la kuweka mazingira katika hali ya usafi na haiba nzuri kwa kuepusha jamii na maradhi ya miripuko.

Alisema Chama Cha Mapinduzi Pamoja na kufanya kazi za kisaiasa bado kina jukumu la kuhamasisha wafuasi wa chama hicho na wananchi kwa ujumla kuendeleza tabia ya kufanya usafi wa mara kwa mara katika maeneo wanayoishi.

“ Nakuombeni viongozi, wanachama, na watumishi pamoja na wananchi kwa ujumla suala la usafi lianzie katika mioyo yetu hadi katika mazingira tunayoishi, ili kuweka nchi yetu katika muonekano na haiba ya kuvutia wakati wote.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai pamoja na maafisa wengine wa chama na jumuiya zake wakifanya usafi wa mazingira kwa kufyeka majani katika uwanja uliopo katika Afisi kuu ya CCM kisiwandui Zanzibar.
Kaimu Mkuu wa Utawala Afisi Kuu ya CCM Zanzibar, Said Omar Mwenemzi akifanya usafi katika maeneo ya Afisi hiyo.
Mwenyekiti wa Tawi la CCM Afisi Kuu Zanzibar ambaye pia ni Msaidi Katibu wa Idara ya Oganazasheni ya Afisi Kuu CCM Zanzibar, Nadra Juma Mohamed akifyeka majani katika uwanja wa ofisi hiyo.

WAZIRI MKUU AKEMEA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

0
0
Aonya wanaokata miti ovyo, asisitiza utunzaji wa vyanzo vya maji

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaonya wakazi wa Ruangwa wanaokata miti kwenye misitu waache kufanya hivyo mara moja ili kuokoa ardhi chepechepe waliyokuwa nayo.

Amesema ukataji miti huo unafanywa zaidi na watu wanaoanzisha mashamba ya ufuta na wapo walioamua kulima karibu na vyanzo vya maji hali iliyosababisha maji yakauke kwenye maeneo mengi.

“Zamani kuna maeneo ulikuwa haupiti hadi ukunje suruali, na kama una gari napo pia ilikuwa ni taabu kupita kwenye maeneo hayo. Lakini sasa hivi, hakuna tena maeneo hayo ndiyo maana kila unakopita unakuta akinamama wanatembea mwendo mrefu na ndoo huku vijana wakibeba madumu kwenye baiskeli nao wakitafuta maji,” alisema Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Ruangwa.

Ametoa onyo hilo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na wakazi wa vijiji mbalimbali vya  wilaya hiyo ambao walifika Ruangwa mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya CCM kusikiliza taarifa ya mambo aliyoyafanya jimboni humo katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

“Kilimo cha ufuta kimekuwa balaa, sasa hivi hakuna maji sababu ya ukataji miti ovyo. Mfano mzuri ni mto Mbwemkuru ambao ulikuwa ukitiririsha maji mwaka mzima, angalia sasa hivi, umegeuka kuwa mto wa msimu na chanzo ni ukataji wa miti,” alisisitiza.

“Tusipobadilika na kuacha hiyo tabia tutamlaumu mbunge na Serikali kuwa hawaleti maji wakati sisi wenyewe tumechangia hali hiyo kwa kuharibu vyanzo vya maji,” alionya na kuongeza kuwa amelazimika kutafuta mashine ya kuchimba maji ili kupunguza tatizo la maji.

Alisema mapema mwaka huu, wataalamu wataanza kufanya utafiti ili kubaini maji yako umbali gani kwenda ardhini kabla ya kuanza kuchimba visima hivyo. “Ikibidi tutaaza na visima vifupi na vya kati ili maji yapatikane haraka,” alisema.

Akielezea mipango ya mwaka huu kwenye sekta ya afya, Waziri Mkuu aliwaeleza wakazi wa jimbo hilo kwamba anatamani kuona kila kijiji kinakuwa na zahanati ili kupunguza umbali wa upatikanaji wa huduma za afya kwa wakazi wa vijijini.

“Kila nilikopita vijijini nimewahamasisha wananchi waanze kufyatua mafotali ili ujenzi wa boma ya zahanati uanze. Na mimi nimeahidi kuchangia mabati kwa kila zahanati, na kuna baadhi ya maeneo nimechangia hata mabati ya nyumba ya mganga na muuguzi,” alisema.

Alisema mwaka uliopita, alifanikiwa kukamilisha ujenzi wa wodi ya akinababa, ya akinamama na kukarabati wodi ya magonjwa mchanganyiko katika hospitali ya wilaya ambapo fedha taslimu milioni 100 zilitumika. Pia aliwezesha kufunga umeme wa jua kwenye zahanati zote zinazotoa huduma za afya ndani ya jimbo na kazi hiyo itaendelea kwa awamu ya pili.

“Pia niliweza kulipia kaya 10 zisizokuwa na uwezo kwa kila kijiji ili zijiunge na mfuko wa afya ya Jamii (CHF) kwa gharama za shilingi milioni 9. Jumla ya vijiji 92 vimefikiwa. Ninawasihi wana-Ruangwa kila mmoja ajiunge na mfuko huu ili muweze kupatiwa huduma za afya bila matatizo,” aliongeza.

Akielezea kuhusu sekta ya elimu, Waziri Mkuu alisema ameweza kufadhili ujenzi wa matundu ya vyoo 70 Katika shule za msingi saba ambapo kila shule imejengewa matundu 10 (manne wavulana, manne wasichana na mawili kwa walimu) ambapo jumla ya sh. milioni 63 zimetumika. Alisema kazi hiyo itaendelea awamu ya pili.

“Zaidi ya hayo, nimefanikisha ufungaji wa umeme jua kwenye shule za sekondari nne za Chunyu, Makanjiro, Narungombe na Nambilanje. Katika awamu ya kwanza tumekamilisha kuweka umemejua kwenye sekondari za tarafa ya Mandawa, na tarafa ya Ruangwa imefikiwa nusu tu. Katika awamu ya pili, tutamalizia tarafa ya Ruangwa na kukamilisha tarafa nzima ya Mnacho,” alisema.


IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATATU, JANUARI 2, 2017.

MTOTO ADAIWA KUMUUWA BABA YAKE MZAZI KISHA KUCHIMBA SHIMO LA KUTAKA KUMZIKIA,SONGEA

0
0
Na Amon Mtega .

JESHI la polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Patrick Malindisa [29 makazi wa mtaa wa Namanyigu kata ya Mshangano Manispaa ya Songea mkoani humo kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi Atanasi Malindisa [70] kwa kumpiga na kitu chenye ncha butu kichwani na kidevuni upande wa kushoto kisha kufanya jaribio la kuchimba shimo kwenye nyumba hiyo kwa malengo ya kumzikia baba huyo.

Akizungumza na Ruvuma TV katika eneo la tukio mmoja wa wanafamilia ambaye ni mdogo wa marehemu Piusi Malindisa alisema kuwa wao walipata taarifa ya kifo cha ndugu yao Januari Mosi mwaka huu majira ya 1.30 kutoka kwa mtoto wa marehemu Patrck Malindisa .

Piusi alisema kuwa mtoto huyo ambaye alikuwa akiishi kwenye nyumba hiyo na marehemu huyo alitoa taarifa kwa wanandugu kuwa baba yake amefariki kwa homa ya tumbo na ndugu walipofika kabla ya kuingia chumbani alikokuwa akilala marehemu waliamua kuuita uongozi wa mtaa ambao uliingia na kubaini kuwa Atanasi Malindisa ameuwawa kwa kupigwa na kitu kichwani na kidevuni.

Alisema kuwa baada ya kubaini hilo walitoa taarifa polisi kisha mwili huo ulichukuliwa na kwenda kuuhifadhi Hospital ya mkoa Ruvuma [HOMSO] kwa uchunguzi huku jeshi la polisi likimshikilia mtoto wa marehemu kwa mahojiano zaidi.

Alifafanu kuwa polisi wakiwa bado kwenye nyumba hiyo walibaini kuwa kwenye moja ya chumba ambacho hakijaezekwa kulichimbwa shimo linaloendana na vipimo vya marehemu ambalo lilihisiwa kuwa alitaka amfukie humo ili watu wasijue kwa kuwa kwenye nyumba hiyo walikuwa wakiishi wawili.

“Uchimbaji wa shimo hilo lenye mithiri ya kaburi lilimshinda kisha akamua kulifukia na kuchukua hatua ya kuja kutoa taarifa kwetu wanandugu kuwa baba yake amefariki kwa homa ya tumbo ambayo inadaiwa alikuwa akilia nalo kumbe sivyo bali kapigwa na kitu kichwani”alisema Ndugu wa marehemu.
 Mwenye tishert ya damu ya mzee ni Pius Malindisa ambaye ni mdogo wake marehemu.Nyumbani kwa kwa marehemu ATANAS PATRICK watu wakiwa wamejitokeza kwa ajili ya kwenda kumstili. 


Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images