Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1486 | 1487 | (Page 1488) | 1489 | 1490 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Baadhi ya wasamalia wakiiangalia Gari aina ya Range Rover yenye namba za usajili T 777 CRK iliyopiga mweleka katika eneo la mataa ya St. Peter, Jijini Dar es salaam mapema leo asubuhi, kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, inaelezwa kuwa chanzo cha ajali ni mwendo kasi na Dereva wa gari hilo ambaye alionekana kuwa ni mtu aliyezidiwa na kilevi. watu wote waliokuwemo ndani ya gari hilo walitoka salama na majeraha kidogo sehemu ya mwili.
  Dereva na abirika wake wakitoka kwenye gari hiyo baada ya kupiga mweleka asubuhi ya leo, huku wakiendelea kufanya juhudi za kuwasiliana na ndugu na jamaa.
  Hivi ndivyo gari livyokuwa baada ya mzinga.


  0 0

  Katika ile hali ya kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2017, Timu ya Boko Beach Veterans (BBV) iliandaa mechi ya kirafiki baina ya BBV Basheka na BBV Kilimba mchezo uliopigwa katika uwanja wa BBV, Boko Jijini Dar es salaam. Mchezo huo ambao ulikuwa ni wa kuvutia sana kwa timu zote kucheza kwa kushambuliana kwa zamu, ulimalizika kwa timu ya BBV Basheka kuibuka na ushindi mnono wa bao 3-0 dhidi ya wapinzani wao, BBV Kilimba.
   Kikosi cha BBV Basheka.
   Kikosi cha BBV Kilimba.
  Mshambuliaji wa pembeni wa BBV Basheka, Juma Ndambile akijiandaa kuachia shuti kali kuelekea lango la wapinzani wao, BBV Kilimba, katika mchezo wa kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2017 uliopigwa katika uwanja wa BBV, Boko Jijini Dar es salaam jana.
  Kiungo mchezeshaji wa  BBV Kilimba, Tippo Athuman a.k.a Zizzou akiichambua vilivyo ngome ya BBV Basheka, katika mchezo wa kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2017 uliopigwa katika uwanja wa BBV, Boko Jijini Dar es salaam jana.
  Mshambuliji tegemeo wa BBV Kilimba, Messi akiondoka na mpira kuelekeza shambulizi langoni mwa wapinzani wao, katika mchezo wa kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2017 uliopigwa katika uwanja wa BBV, Boko Jijini Dar es salaam jana.


  0 0


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma mara baada ya kuwasili katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea katika katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera mara baada ya kuwasili na kupokewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma (katikati) pamoja na Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini wa kwanza (kulia).
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ibada ya mwaka mpya katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera mara baada ya Ibada.


  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge akiwa katika boti ya kisasa inayotumiwa na idara ya maliasili na uvuvi wilaya ya Nyasa kabla ya kuzunguka ziwa Nyasa kuangalia vivutio mbalimbali vya utalii katika wilaya ya Nyasa mkoani humo,kushoto ni mkuu wa wilaya ya Nyasa Esabila Chilumba.
  Naibu waziri wa elimu na mafunzo mhandisi Stella Manyanya kushoto akimsikiliza askofu wa kanisa la Anglikana Doyasisi ya Ruvuma Raphael Reuben Haule ndani ya boti la Mv Matema linalofanya safari zake kati ya kijiji cha Liuli na maeneo mengine ndani ya ziwa Nyasa,katikati mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge.
  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge katikati akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Tamasha la kuvitangaza vivuutio vya utalii katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma jana,kulia mkuu wa wilaya ya Mbinga Kosmas Nshenye,wa pili kulia mkuu wa wilaya ya Nyasa Esabila Chilumba na kushoto nmbunge wa jimbo la Nyasa Stella Manyanya.


  0 0

  MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) umefanikiwa kulipa vituoni madai yanayotokana na huduma za afya kwa wakati  zaidi ya bilioni 5.1 kwa mwaka wa fedha 2015/2016 sawa na asilimia 148.

  Malipo hayo yamesaidia huduma kuboreshwa kwenye vituo mbalimbali ikiwemo watoa huduma kuhamasika na uelewa juu ya mfuko huo .

  Hayo yalisemwa hivi karibuni na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga(NHIF) Ally Mwakababu (Pichani )wakati akitoa taarifa ya utendaji wa mfuko huo kwa waandishi wa habari mkoani hapa.

  Ambapo alisema kwenye kipindi cha mwaka 2014/2015 walilipa kiasi cha zaidi ya bilioni 3.5 hali inaonyesha ongezeko kwa mwaka huu.

  Alisema pamoja na malipo kuongezeka lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo huduma za afya vijijini imekuwa kikwazo sanjari na upatikanaji wa dawa vituoni.

  Aidha alisema lakini pia kuongezeka kwa magonjwa yakiwemo ya ukimwi ikiwemo upungufu wa watumishi katika sekta ya afya.

   “Lakini changamoto nyengine ni ugonjwa wa ukimwi kwa wanachama ni chanzo cha magonjwa nyemelezi na lakini pia halmashauri hazijachangamkia mikopo ,vifaa tiba,ukarabati na dawa kwenye vituo vyao “Alisema.

  Aidha alisema katika kuhakikisha uhai wa mfuko huo unakuwa endelevu mfuko huo uliamua kufanya ukaguzi kwenye vituo vinavyoashiria wizi na udanyanifu.

  “Katika kipindi hicho mfuko umefanikiwa kuokoa kiasi cha zaidi ya milioni 83.6 kutokana na ukaguzi maalumu 29 zilifanyika kwenye vituo 22 kutokana na kuona vinaashiria vya hujuma au uadanyanyifu wa huduma kwa wanachama wa Bima ya Afya “Alisema.

   “Kaguzi hizo zilifanyika kwenye vituo vya serikali 10 sawa asilimia 45,vituo vya madhehebu ya dini 8 sawa na asilimia 36 na vituo vya watu binafsi 4 sawa na asilimia 19 “Alisema.
  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tangaraha

  0 0


  Naibu Spika wa Bunge, Dk.Tulia Akson, akipeperusha bendera ya Taifa wakati wa mkesha mkubwa wa kitaifa wa dua maalumu uliofanyika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam jana. Dk.Akson alimwakilisha Rais Dk.John Magufuli kwenye mkesha huo ambaye alikuwa mgeni rasmi.
  Na Dotto Mwaibale

  NAIBU Spika wa Bunge Dk. Tulia Akson amesema Tanzania mpya na yenye matokeo chanya kwa mwaka 2017 inawezekana hivyo akamataka kila mmoja wetu kufanyakazi kwa bidii ili kuliletea taifa maendeleo.

  Dk.Akson aliyasema hayo kwa niaba ya Rais Dk.John Magufuli wakati akihutubia kwenye mkesha mkubwa wa kitaifa wa dua maalumu uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana.

  "Tanzania mpya na nchi mpya yenye matokeo chanya kwa mwaka 2017 inawezekana" alisema Akson.  Akson alimwakilisha Rais Dk.John Magufuli alikuwa mgeni rasmi kwenye mkesha huo mkubwa ulioandaliwa na makanisa mbalimbali ya kiroho.

  Akinukuu baadhi ya maneno kutoka katika kitabu cha biblia cha Nyakati mungu ataiponya nchi iwapo kila mtu atamuita kwa jina lake na kujinyenyekesha na kuomba na kuziacha njia mbaya.


  "Tukimuita mungu kwa jina lake na kujinyenyekesha kwa kuacha kutenda mambo mabaya mungu ataiponya nchi yetu" alisema Akson.

  Mratibi wa mkesha huo Askofu Godfrey Malesi alisema hivi sasa kila Januari Mosi mikoa 17 hapa nchini imekuwa ikifanya mkesha huo ikiwepo na Zanzibar kwa ajili ya kuwaombea viongozi wa nchi na taifa kwa ujumla.

  "Mungu amekuwa akijibu maombi yetu tangu tuanze kuomba kupitia mkesha huu tulipoanza jijini Dar es Salaam mwaka 1997" alisema Malesi.

  Alisema tangu wakati huo wamekuwa wakiiombea nchi iwe na amani na kuondokana na ufisadi na kumpata Rais atakayeifanya Tanzania iwe mpya ambapo amepatikana Rais Dk.John Magufuli ambaye ameifanya nchi kuwa na muelekeo mpya. Alisema lengo lao ni kuhakikisha mkesha huo unafanyika katika mikoa yote na kila eneo la nchi yetu.

  Mkesha huo uliopambwa na nyimbo kutoka kwaya ya Mass ya Sinza jijini Dar es Salaam na Brass Band ya Polisi ulihudhuriwa na viongozi wa dini kutoka nchi za jirani za Rwanda na Burundi ambao walipata fursa ya kuzungumzia umuhimu wa nchi kuwa na amani.


  Naibu Spika wa Bunge, Dk.Tulia Akson (katikati), Mratibu wa mkesha huo Askofu Godfrey Malesi na Askofu Damas Kenasi (kulia), wakishiriki kuomba katika mkesha huo.
  Waimbaji wa Kwaya ya Mass ya Sinza jijini Dar es Salaam wakiimba nyimbo za kumsifu mungu.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Papa Francis
  Mwinjilisti wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mtaa wa Kivule, Ukonga Dar es Salaam Michael Mgaya (wa pili kushoto) akiwa na wazee wa kanisa hilo baada ya kumalizika kwa ibada. 


  Picha na habari na 
  Richard Mwaikenda

  KIONGOZI Kanisa la Katoliki Duniani, Papa Francis amekubali mwaliko wa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 500 ya kuasisiwa kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Duniani.
  Taarifa hiyo imetangazwa leo wakati wa Ibada ya Jumapili ya kuukaribisha mwaka mpya katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Mtaa wa Kivule Ukonga, Dar es Salaam.
  Maadhimisho hayo yatafanyika hivi karibuni eneo ambapo kanisa hilo liliasisiwa nchini Ujerumani ambapo kutakuwa na shamrashamra za kila aina zitakazoshuhudiwa na wageni kutoka nchi mbalimbali.
  Kwa hapa nchini maadhimisho hayo yatafanyika katika Chuo cha Dini cha Makumira, mkoani Arusha, ambapo mnara wa kumbukumbu utajengwa. Kanisa hilo liliasisiwa mwaka 1557.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera amesema watendaji wa Vijiji ambao sio waadilifu kutokana na kupokea rusha kutoka kwa wafugaji kwa lengo la kuwapa makazi katika vijiji , ndiyo chanzo cha migogoro hiyo katika ya wakulima na wafugaji. Kwa undani wa habari hii bonyeza hii video.Habari na RUVUMA TV.


  0 0


  0 0


  0 0

   Usiku wa December 31,  2016 kuamkia leo mwaka mpya January 1, 2017 wanamitindo mbalimbali walikutana na kusherekea kwa pamoja Usiku wa Khanga yaani “Khanga Party”. Tukio hili kama lilivyokuwa limetaarifiwa awali limefanyika Regency  Park Hotel Mikocheni jijini Dar es salaam . Mitindo mbalimbali ya vazi la Khanga kutoka kwa wanamitindo ilioneshwa kwenye stage na kuzikonga nyoyo  za wahudhuriaji  usiku huo.
  Hafla hii iliandaliwa na Mama wa Mtindo maarufu Asya Idarous Khamsin, ambapo mbali na burudani zilizo kuwepo pia kulikuwa na Red Carpet yenye sifa kubwa ya kuwakutanisha mastaa na mashabiki wao kuweza kupiga picha za pamoja kwa ajili ya kumbukumbu. Tunawatakia mwendelezo mwema na wenye baraka wadau na wanamitindo wote wa Tanzania. (Cheers 2017)
   Mama wa Mtindo Asya Idarous Khamsin akiwa katika red carpet na baadhi ya waalikwa kwenye hafla hiyo
   Mama wa Mtindo Asya Idarous Khamsin akiwa katika red carpet na baadhi ya waalikwa kwenye hafla hiyo
  Mamodo kwenye catwalk.

  0 0

   Mhandisi Felchesmi Mramba


  0 0

  Na Lulu Mussa

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amefanyia ziara ya kikazi ya kukagua hatua za ujenzi katika miradi inayofadhiliwa na Ofisi yake.

  Akiwa katika Wilaya ya Ilala, Waziri Makamba ametembelea ujenzi wa Mfereji wa kupitishia maji taka katika eneo la Ilala Bungoni na kuongea na wananchi wa eneo hilo.

  Waziri Makamba ameugiza uongozi wa Dezo  Civil Constractors Co. Ltd kuhakikisha ujenzi wa Miundombinu ya maji taka katika Manispaa za Ilala na Temeke unakamilika kwa muda uliopangwa na kwa ubora wa hali ya juu kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo katika mkataba.

  “Nataka mradi huu uwe wa mfano kwa ubora na viwango vya hali ya juu, ikiwa ni jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi, kwa kuweka mfumo mzuri wa kukusanya maji taka na kuyaelekeza sehemu stahiki” Makamba alisisitiza.

  Aidha, Waziri Makamba amewataka wakazi wanaozuka eneo hilo kuacha mara moja utupaji wa taka maji na taka ngumu katika mfereji huo unaojengwa, na kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Palela Msongela kutoa adhabu kali kwa yeyote atakayekiuka agizo hilo.

  “Kwa kupitia kamati za Mazingira za vitongoji na sheria ndogo ndogo mlizojiwekea hakikisheni kuwa hifadhi ya mazingira inazingatiwa kwa mstakabali wa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo.”

  Pia, Waziri Makamba amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha Wakandarasi wanaopewa kazi za ukusanyaji wa taka, wanakuwa na vifaa na uwezo wa kutosha kwa kuhakikisha taka zote zinazolewa kwa wakati ili kuepuka mrundikano wa taka katika makazi ya watu.

  “Natoa wito pia kwa vijana wa maeneo haya kuunda vikundi vidogo vya kuzoa taka ili kuwa chanzo cha ajira kwenu.” Makamba alisisitiza.

  Waziri Makamba ameliagiza Baraza la Taifa La Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira -  NEMC kutembelea eneo hilo la Ilala Bungoni na kutoa maelekezo kwa Gereji bubu  zinazokiuka hifadhi na usimamizi wa Mazingira kwa kufanya shughuli zao pembezoni mwa mfereji unaojengwa.


  Ujenzi wa Ukuta wa (Obama/Ocean Road na Kigamboni) na Miundombinu ya maji taka katika Manispaa za Ilala na Temeke unatekelezwa chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia  Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi na  unafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira (UNEP). Aidha, Kampuni ya Dezo Civil Contractors ndio inafanya kazi ya ujenzi huu na kazi zinatarajiwa kukamilika mwezi Julai 2017.

  Waziri Makamba katika ziara yake hii leo ametembelea Ilala Bungoni, Mtoni kwa Azizi Ali, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Kutembelea eneo la Ujenzi wa Ukuta Barabara ya Obama.

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiongea na Diwani wa Kata ya  Buguruni Mhe.  Adam Fugame (katikati) wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa mfereji wa maji taka katika eneo la Ilala Bungoni jijini Dar es salaam

   Sehemu ya Mfereji wa Maji taka unaojengwa eneo la Ilala Bungoni chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia  Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi na  unafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira (UNEP).

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiongea na Wananchi wakazi wa Ilala Bungoni, mara baada ya kukagua ujenzi wa mrefeji wa maji taka 
  Mwakilishi wa UNOPS Bw Bernard Omondi akifanunua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba katika eneo la Temeke - Mtoni kwa Azizi Ali ambapo kazi ya kusafisha na kujenga mfumo wa maji taka inaendelea. 


   Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora ( wa tatu kutoka kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba mara baada ya ziara ya kukagua hatua za ujenzi kwa miradi inayosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.  Kulia ni Bw. Kanizio Manyika Afisa Mazingira Mkuu na Msimamizi wa Mradi na Bw. Richard Muyungi Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira.  0 0   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kabyaile Misenyi Mkoani Kagera. Wengine katika picha ni Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage, Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Vija Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama pamoja na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako wakiwa wameshika utepe huo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi  mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Kituo cha Afya cha Kabyaile Misenyi Mkoani Kagera.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maeneo ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.

  Moja ya majengo katika mradi huo wa kituo cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera. PICHA NA IKULU.

  0 0

  Matukio 12 yaliyotikisa Tanzania mwaka 2016  na kuchukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi. Kwa undani wa matukio hayo Bonyeza Video hii.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Funguo za Gari aina Mpya ya Noah  Mkuu wa Mkoa Mstaafu Mhe, Abdalla Mwinyi Khamis iliyotolewa na Ofisi ya  Mkoa Mjini Magharibi jana katika sherehe za Kumpongeza kwa Utumishi uliotukuka  katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,hafla iliyofanyika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipena mkono na Mkuu wa Mkoa Mstaafu Mhe, Abdalla Mwinyi Khamis kama ishara ya kumkabidhi  Gari aina Mpya ya Noah iliyotolewa na Ofisi ya  Mkoa Mjini Magharibi  katika sherehe za Kumpongeza Mstaafu huyo kwa Utumishi wake katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,hafla iliyofanyika  jana katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud (kulia) wakiwa na  Mkuu wa Mkoa Mstaafu Mhe, Abdalla Mwinyi Khamis katika sherehe za Kumpongeza Mstaafu huyo na kumzawadia zawadi mbali mbali ikiwemo Gari aina ya Noah yenye thamani Millioni kumi na Mbili ,katika hafla iliyofanyika  jana katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja. 
   Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mjini Magharibi Mhe, Abdalla Mwinyi Khamis akipokea Taarifa ya pongezi zake kwa ushirikiano uliotukuka kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mjini Marina Joel Thomas baada ya kuisoma jana wakati wa sherehe maalum ya kumpongeza na kumzawadia,iliyofanywa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja,(katikati)Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo
  Mwimbaji wa Kikundi cha Zanzibar One Marium Juma akiimba wimbo wa "Nadekezwa" wakati wa sherehe ya kumpongeza Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mjini Magharibi Mhe, Abdalla Mwinyi Khamis zilizofanyika jana katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja,liyofanywa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi chini ya usimamizi wa Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud,Picha na IKULU

  0 0

  Katika picha hii ya kutoka maktaba inamuonesha Rais Dkt John Pombe Magufuli akimsalimia Mama Jitto Ram mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara wakati wa kampeni katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. 
  Mama Jitto Ram amefariki dunia mjini Morogoro baada ya kuugua ugonjwa wa moyo. Mama Jitto Ram alikuwa mbunge wa viti maalum CCM. Alikuwa mkufunzi wa manesi Muhimbili. Alikuwa mtetezi wa haki za WAVIU/PLHIV. Alikuwa mwana harakati wa kutokomeza unyanyapaa dhidi ya WAVIU/PLHIV. Khitma ya arobaini ya Mama Jitto itafanyika nyumbani kwa mwanae Morogoro, January 28,  2017 Insha Allah. Inna lillahi wa inna ilaihi raajiun. Amen

  0 0

  MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) umefanikiwa kulipa vituoni madai yanayotokana na huduma za afya kwa wakati  zaidi ya bilioni 5.1 kwa mwaka wa fedha 2015/2016 sawa na asilimia 148.
  Malipo hayo yamesaidia huduma kuboreshwa kwenye vituo mbalimbali ikiwemo watoa huduma kuhamasika na uelewa juu ya mfuko huo .
  Hayo yalisemwa hivi karibuni na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga(NHIF) Ally Mwakababu (Pichani )wakati akitoa taarifa ya utendaji wa mfuko huo kwa waandishi wa habari mkoani hapa.
  Ambapo alisema kwenye kipindi cha mwaka 2014/2015 walilipa kiasi cha zaidi ya bilioni 3.5 hali inaonyesha ongezeko kwa mwaka huu.
  Alisema pamoja na malipo kuongezeka lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo huduma za afya vijijini imekuwa kikwazo sanjari na upatikanaji wa dawa vituoni.
  Aidha alisema lakini pia kuongezeka kwa magonjwa yakiwemo ya ukimwi ikiwemo upungufu wa watumishi katika sekta ya afya.
   “Lakini changamoto nyengine ni ugonjwa wa ukimwi kwa wanachama ni chanzo cha magonjwa nyemelezi na lakini pia halmashauri hazijachangamkia mikopo ,vifaa tiba,ukarabati na dawa kwenye vituo vyao “Alisema.
  Aidha alisema katika kuhakikisha uhai wa mfuko huo unakuwa endelevu mfuko huo uliamua kufanya ukaguzi kwenye vituo vinavyoashiria wizi na udanyanifu.
  “Katika kipindi hicho mfuko umefanikiwa kuokoa kiasi cha zaidi ya milioni 83.6 kutokana na ukaguzi maalumu 29 zilifanyika kwenye vituo 22 kutokana na kuona vinaashiria vya hujuma au uadanyanyifu wa huduma kwa wanachama wa Bima ya Afya “Alisema.
   “Kaguzi hizo zilifanyika kwenye vituo vya serikali 10 sawa asilimia 45,vituo vya madhehebu ya dini 8 sawa na asilimia 36 na vituo vya watu binafsi 4 sawa na asilimia 19 “Alisema.
  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tangaraha

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
  Wananchi wa Mkuranga wameibua sakata la kuibiwa kwa dawa za serikali katika hospitali yao na kutaka majibu katika mkutano wa mbunge wa jimbo la mkuranga, Abdallah Ulega. 
  Wananchi hao walisema wizi wa dawa za serikali unawakera kutokana kila wanapokwenda hospitali hiyo wanaambiwa wakanunue dawa huku wakitoa sh.10000 na dawa hawapati. 
  Akizungumza na wananchi wa Mkuranga Mbunge wa Jimbo hilo, Abdallah Ulega amesema suala la kuibiwa kwa dawa haliwezi kuvumilika kutokana na wananchi wanakwenda hospitali na kuambiwa dawa wakanunue nje. 
  Amesema hakuna sababu wananchi kutoa sh.10000 wakati dawa au vipimo hawapati huku na maneno yasiyostahili wakipewa. Amesema kuna umuhimu wa fedha wanayoitoa kuungani Huduma ya Afya ya Jamii (CHF). 
  Ulega amesema kuwa katika ziara ya vijiji 90 licha wananchi wamekuwa wakihoji upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya na kusema wanawajibu kama baraza la madiwani kuangalia thamani fedha hiyo na huduma wanayoipata kutokana mazingira wanayoipata fedha hiyo ni magumu. Akuzungumzia suala hilo, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Gilberto Sanga amesema mtu aliyekamatwa na dawa haitakiwi kufanyiwa uchunguzi na kumtaka Mkurugenzi wa Wilaya hiyo suala hilo kushughulikia mara moja
   Mbunge wa Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa vijiji vya mkuranga katika  mkutano   hadhara alioutisha kwa ajili ya kupata taarifa ya maendeleo.
    Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Hassan Sanga  akizungumza katika mkutano wa hadhara uliotishwa na mbunge wa jimbo la Mkuranga. 03.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga Msham Munde  akizungumza katika mkutano wa vijiji vya vya Mkuranga. 
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga,  Juma Abeid akizungumza juhudi mbalimbali za. Halmashauri hiyo katika mkutano wa hadhara uliotishwa na mbunge wa jimbo hilo. 
   Sehemu ya wananchi wa Mkuranga waliofika katika mkutano wa hadhara uliotishwa na  mbunge wa Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega. 
  Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

older | 1 | .... | 1486 | 1487 | (Page 1488) | 1489 | 1490 | .... | 3284 | newer