Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1485 | 1486 | (Page 1487) | 1488 | 1489 | .... | 3284 | newer

  0 0

  UONGOZI wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga (SPC),na baadhi ya waandishi wa habari wilayani Kahama,wamekutana na mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu ili kupata muafaka wa tatizo la kukamatwa na kufikishwa mahakamani mwandishi wa habari wa kujitegemea Paul Kayanda.

  Kikao hicho cha usuluhishi kilichofanyika leo Jumamosi Desemba 31,2016 katika ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo,kimehudhuriwa pia na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Kahama.

  Kayanda alikamatwa jana Desemba 30,2016 na kufikishwa mahakamani kwa agizo la Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akimtuhumu kuandika habari za kumdhalilisha na kuzisambaza kwenye barua pepe mbalimbali za vyombo vya habari.
  Katika kikao ,Uongozi wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ,ulimuomba mkuu wa wilaya Nkurlu kutaka kufahamu kilichomsukuma kuchukua maamuzi hayo,na nini ushauri wake juu ya suala hilo lakini pia kumsikiliza mwandishi Paul Kayanda.

  Baada ya kusikiliza pande zote mbili, kikao kilibaini kuwepo kwa mapungufu katika habari iliyoandikwa na Kayanda kuhusu habari ya laptop mbili zilizoibiwa nyumbani kwa mkuu huyo wa wilaya.
  Mkuu huyo wa wilaya alikiri kuwepo kwa tukio la wizi nyumbani kwake lakini mwandishi huyo aliandika habari kwa kuingilia uhuru binafsi wa kiongozi huyo akielezea watu wanaoingia na kutoka nyumbani kwake lakini maisha anayoishi na kijana wake.
  Kwa kuangalia maslahi mapana ya umma kutokana na kutegemeana katika kusukuma maendeleo ya jamii baina ya uongozi wa serikali na waandishi wa habari, kikao kimemtaka Kayanda kumwomba radhi mkuu huyo wa wilaya kwa kuingilia uhuru wake binafsi na kuuhusisha na habari ya wizi wa laptop badala ya kujikita kwenye tukio la wizi wa laptop pekee.
  Kikao pia kimebaini kuwa pamoja na mapungufu ya mwandishi, ni ukweli ulio wazi kuwa mkuu huyo wa wilaya aliibiwa kompyuta mpakato (lap top) mbili nyumbani kwake na kuagiza vijana watatu wakamatwe kwa mahojiano polisi akiwemo mmoja anayeishi nyumbani kwake japo ameelezea kuwa hakujua walishikiliwa kwa siku ngapi.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii Kilombero

  Ujenzi Wa Daraja la mto kilombero ni moja ya vitu vinavyotajwa na vilivyopo katika vinywa Vya wakazi wa eneo hili kukuza uchumi wa Wilaya ya Malinyi na Ulanga.

  Ujenzi Wa daraja hilo ambao umekamilika kwa asilimia 80 unatarajiwa kuongeza  matumaini makubwa kwa wakazi wa Wilaya hizi mbili, ambazo kwa kiasi kikubwa hutegemea biashara ya mchele Kama ndio uti wa mgongo wa mapato.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Chalinze wa Malinyi, Marcelin Ndimbwa amesema daraja hilo litafungua Biashara upya kwa kasi kutokana maeneo hayo kufikiwa na vyombo vya usafiri kwa saa 24 .

  Amesema Wilaya hizi mbili zilikuwa zinadumaa kutokana na kutofikika kwa urahisi ,lakini kwa muonekano huo kila mmoja ana matumaini na serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

  Mmoja wa wakazi wa Ifakara Said Lumisha amesema kila mfanyabiashara ana imani na serikali ya awamu ya tano,kwani kila mmoja anahitaji kusafirisha Mchele mwingi, ila wanashindwa kutokana na tatizo la miundo mbinu ikiwemo kivuko.

  Ametaja kuwa mzigo wa kupakiwa kwenye Lori,unapakiwa nusunusu kutokana na kivuko kutokuwa na uwezo mkubwa, lakini siku chache maroli makubwa yataweza kufika mpaka Ulanga na Malinyi kwa urahisi na zaidi.

  Ametaja uwepo Wa daraja hilo kuwa utafungua njia ya basi kwenda Songea kupitia Malinyi kwani njia ni fupi kuliko kuzunguka Iringa,Anataja kuwa watu Wa mikoa ya kusini wakihitaji kwenda Dodoma hawatakuwa na haja ya kupitia Dar es salaam kwani daraja hili likikamilika mambo mengi ya kimaendeleo yatafunguka,


  Muonekano wa daraja la Kilombero kwa mbali ambalo inaelezwa kwa asilimia 80 limekwishakamilika


  Sehemu ya ujenzi wa daraja hilo muhimu ukiendelea

  0 0
  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni sita kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Pacco GEMS Limited, Bw. Mahendra Bardiya katika harambee  ya kuchangia ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari wilayani Ruangwa ambapo jumla ya shilingi milioni 138.26 zilichangwa. Harambee hiyo ilifanyika sambamba na  mkutano wa hadhara uliohutubia wa Waziri Mkuu mjini Ruangwa, Desemba 30, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni sita kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Pacco GEMS Limited, Bw. Mahendra Bardiya katika harambee  ya kuchangia ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari wilayani Ruangwa ambapo jumla ya shilingi milioni 138.26 zilichangwa. Harambee hiyo ilifanyika sambamba na  mkutano wa hadhara uliohutubia wa Waziri Mkuu mjini Ruangwa, Desemba 30, 2016.
   Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea cheti maalum cha kutambua mchango wake katika kukijenga na kukiimarisha Chama cha Mapinduzi wilayani Ruangwa kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi, Ali Mtopa katika mkutano wa hadahara aliouhutubia mjini Ruangwa Desemba 30, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Cheti Maalum  cha kutambua mchango wake katika kukijenga na kukiimarisha Chama cha Mapinduzi wilayani Ruangwa alichokabidhiwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Lindi, Ali Topa   (kulia) katika mkutano wa hadhara aliouutubia mjini Ruangwa Desemba 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM wa wilaya ya Ruangwam Issa Njinjo
  Wananchi wa Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara mjini Ruangwa, Desemba 30, 2016. (Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Zubery Muhombeji amewataka wanaruvuma kusherekea sherehe za kuupokea mwaka katika hali ya amani na utulivu kwa undani zaidi wa habari hii msikilize kupitia video hii


  0 0

   Baadhi ya wahitimu wa Shahada ya Uzamili ya Habari na Mahusiano ya Umma iliyotolewa hivi karibuni  na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT) kwenye viwanja vya Raila Odinga mkoani Mwanza.
  Wahitimu wa Shahada ya Uzamili ya Habari na Mahusiano ya Umma kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT) wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mahafali ya 18 hivi karibuni, kuanzia kulian ni Martin Kayera, Bahati Mollel na Nicodemas Inkoko. 
   Wakiwa kwenye picha ya pamoja wahitimu wa Shahada ya Uzamili ya Habari na Mahusiano ya Umma iliyotolewa hivi karibuni katika mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), kuanzia kushoto ni Concilia Niyibitanga, Bahati Mollel, Jackline Issack na Latifa Abdallah.
  Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bahati Mollel (kulia) akiwa na wahitimu wenzake Benedict Luvanda, Theresia Mendoza, Debora Ngalijo na Mariam Lusewa wa Shahada ya Uzamili ya Habari na Mahusiano ya Umma ya SAUT hivi karibuni.

  0 0

  Mwakilishi wa Kimweri Promotion Nchini Tanzania Yuyuph Mnyeto kushoto akimkabidhi vifaa vya ndondi kwa kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' baada ya kupokelewa na kukabidhiwa kwa wadau mbalimbali nchini vifaa hivyo vimetolewa na Bondia Mtanzania anayefanya shughuli zake nchini Australia, Omari Kimkweri.

  Bondia Selemani Kidunda kushoto kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' na Mwakilishi wa Kimweri Promotion Nchini Tanzania Yuyuph Mnyeto kushoto wakiwa katika picha wa pamoja baada ya kukabidhi vifaa vilivyotoka kwa bondia Omari Kimweri anayefanya shughuli zake nchini Australia, Omari Kimkweri.
  Picha na Superboxing news

  0 0

  Shamra shamra za Maadhimisho ya kusherehekea kutimia Miaka 53 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar  ya kwaka 1964  yaliyowakomboa Wakwezi na Wakulima kutokana na madhila ya Wakoloni yameanza rasmi  hapa Nchini kwa shughuli za usafi wa mazingira katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Unguja na Pemba.
  Usafi huo uuliowajumuisha wananchi wa rika zote  wakiongozwa na Viongozi wao wa Wadi,  Majimbo, Wilaya pamoja na Mikoa umefanyika mapema asubuhi kwa kuweka mazingira safi katika baadhi ya sehemu zikiwemo Bara  bara Kuu.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar  alijumuika pamoja na Wananchi hao katika usafi huo hapo Mtoni Kidatu  Wilaya ya Magharibi “A”.
   Baadhi ya Wananchi wakishiriki usafi wa mazingira  hapo Mtoni Kidatu pamoja na meneo mengine Nchini ikiwa ni kuanza rasmi kwa maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar  ya Mwaka 1964 kutimia Miaka 53.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwaongoza Viongozi pamoja  na Wananchi katika usafi wa Mazingira hapo Mtoni Kidatu ikiwa ni uzinduzi wa Sherehe za Mapinduzi kutimia Miaka 53. Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mheshimiwa Ayoub Mohamed Mahmoud.
   Balozi Seif akijumuika pamoja na Wananchi katika usafishaji wa Bara bara ya Mkapa hapo Mtoni Kidatu ili ziwe katika mazingira mazuri kwa wanaozitumia wakiwemo wageni wanaotembelea Zanzibar. Sambamba na  Balozi Seif  kulia yake ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mheshimiwa Ayoub Mohamed Mahmoud.
  Balozi Seif akionyesha mfano wa umuhimu wa kutunza mazingira kwa kufanya usafi katika zoezi la uzinduzi wa sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 kutimia miaka 53 hapo Mtoni Kidatu.
   Picha na – OMPR – ZNZ. Taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0  0 0  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Bw. Ashraf Ramadhani, mlemavu kutoka Bukoba mkoani Kagera, aliyemtembelea kijijini kwake Chato mkoani Geita ambapo alikaa na kuongea naye masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na changamoto za kimaisha anazokumbana nazo.


  0 0
 • 12/31/16--11:49: Bwawa la maini oye!
 •  Goli la alfajiri la kicha la Georginio Wijnialdum  dhidi ya Manchester City leo limemaliza ubishi kwamba Bwawa la Maini sio nguvu ya soda katika ligi kuu ya Uingereza kufuatia ushindi wake wa bao 1-0 katika uwanja wa nyumbani wa Anfield katika mkesha wa mwaka mpya.


  0 0

  Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU Ughaibuni yenye makao yake nchini Ujerumani inawatakia wadau wote popote mlipo heri ya mwaka mpya 2017.
  Inawaombea amani,upendo na mshikamano muda wote.

  Happy New Year  2017!

  0 0  0 0

  Siku ya Alhamis tarehe 29/12 Bw. Wasia Maya kutoka mjini Houston , Texas aliamua kuachana na kambi ya makapera na kufunga ndoa na Bi. Laila Martin. Harusi hiyo ilifanyika nyumbani kwa Bw. Wasia na kuhudhuriwa na Watanzania wengi waishio katika jiji la Houston na miji ya jirani. Ijumaa ya tarehe 30/12 kulifanyika Nikka Dinner katika ukumbi wa Pakwan uliopo kwenye makutano ya barabara za HW6 na Beechnut . 
  Pata picha za Harusi na Nikka Dinner hapa chini.
  Bw. Wasia na Bi. Laila siku ya ndoa yao
  Maharusi wakiwa na sura za furaha 
   Hakika harusi ilipende
  Ndugu, jamaa, marafiki wa maharusi na maharusi.

  0 0


  0 0

  0 0

  Na: Frank Shija – MAELEZO

  CHAMA cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina Saccos kimepanga kujenga kitega uchumi cha kisasa kupitia mradi wa njedengwa katika Mkoa wa Dodoma ili kuendana na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhamishia makao makuu ya shughuli za Serikali mjini humo.

  Hayo yamebainishwa na leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Eligius Mwankenja wakati wa mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama hicho, na kuongeza kuwa mradi huo katika hatua ya utafiti wa kiuchumi na fedha.Mwankenja amesema kuwa wapo katika hatua za awali za kuanza utekelezaji wa mradi huo ambao zabuni yake inatarajiwa kutangazwa mwezi wa Aprili 2017.

  “Mradi wa Njedengwa upo mbioni kuanza tunategemea utakuwa chachu ya maendeleo ya Chama chetu kwa kutuingizia kipato kutokana na shuguli zitakazokuwa zikifanyika kupitia mradi huo”. Alisema Mwankenja.

  Aliongeza kuwa kupitia mradi huo wanatarajia kujenga hoteli ya kisasa, kumbi za kufanyia mikutano, majengo la Ofisi, , Viwanja vya Michezo na bwawa maalum la kuogelea.

  Mpaka sasa tayari upembuzi yakinifu wa hali ya eneo hilo imekwishafanyika ambapo mradi huo utajengwa kwa ubia baina ya mwekezaji kupitia utaratibu wa Jenga, Endesha na Hamisha (Build, Operate and Transfer - BOT) ambapo mwekezaji atagharamia ujenzi wote na kuendesha kwa muda ambao utakualiwa ndani ya mkataba.

  Palimo na mafanikio hakukosi kuwa na chamagamoto, Mwenyekiti wa Bodi ya Hazina Saccos anasema kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo kwa sasa ni ufinyi wa ofisi ukizingatia kwamba idadi ya wananchama imeendelea kuongezeka toka wanachama 100 mwaka 1972 wakati Hazina Saccos ilipoanzishwa hadi kufikia zaidi ya 5000 mwaka huu.

  Changamoto hii inasababisha pia kuongezeka kwa mahitaji ya wanachama wanaohitaji kupatiwa mikopo, hivyo inakilazimu chama kubuni njia mbada za kukuza na kuongeza mtaji ili kukabiliana na hali hiyo.

  Mradi wa Njedengwa ni mradi wa uwekezaji wa Hazina Saccos katika kuhakikisha wanawekaza ili kukuza mtaji wa Chama chao kwa lengo la kuhakikisha kinawahudumia wanachama wake wote i kulingana na mahitaji yao kwa wakati.
   Kamishina wa Sera kutoka Wizara ya Fedha, Mipango na Uchumi Bw. Augustine K. Ollal akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tatu wa Wakilishi wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Haznina (Hazina Saccos) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chama hicho Bw. Eligius A. Mwankenja.

   Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Tatu wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Haznina (Hazina Saccos) wakifuatilia Mkutano Mkuu wa Tatu wa Chama hicho kilichofanyika leo katika ukumbi wa Wizara ya Fedha leo jijini Dar es Salaam.

  Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tatu wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Haznina (Hazina Saccos) Bw. Eligius A. Mwankenja (wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Hazina Saccos leo jijini Dar es Salaam. Watatu kutoka kushoto mstari wa mbele ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw.  Eligius A. Mwankenja.

  Picha na: MAELEZO.

  0 0
 • 01/01/17--00:15: usafi wa mazingira Lindi
 •  Wakaazi wa mji wa Lindi wakifanya usafi wa mazingira katika mitaa na barabara  zinazozunguka hospitali ya mkoa huo Desemba 31, 2016. Walifanya hivyo kuitikia agizo la  Rais John Pombe Mgufuli la kuwataka Watanzania kutumia muda wa asubuhi kila Jumamosi kufanya usafi wa mazingira. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0

older | 1 | .... | 1485 | 1486 | (Page 1487) | 1488 | 1489 | .... | 3284 | newer