Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1484 | 1485 | (Page 1486) | 1487 | 1488 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Wajumbe wa Kamati ya Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini wameagizwa kuhakikisha wanakagua utekelezaji wa miradi ya kilimo ya vikundi vilivyokabidhiwa vifaa kutoka kwenye mfuko huo ili kujiridhisha.

  Agizo hilo limetolewa hivi karibuni na Mbunge wa Jimbo hilo, Profesa Sospeter Muhongo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati husika wakati wa mkutano wa hadhara wa kuainisha matumizi ya fedha za Mfuko wa Jimbo kwa Awamu ya Pili uliofanyika katika kijiji cha Tegeruka, Musoma Vijijini.

  Ilielezwa kwamba Awamu ya kwanza ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya Mfuko wa Jimbo hilo ni shilingi milioni 70,820,000 ambazo zilitumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo shilingi milioni 20,000,000 kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Murangi.

  Fedha zingine ni milioni 27,500,000 ambazo zilitumika kwa ajili ya kurekebisha nyumba na madarasa yaliyokuwa yameezuliwa na upepo kwa shule mbili za msingi, milioni 22,500,000 ilitumika kununulia mashine za umwagiliaji, mbegu za mbogamboga na matunda pamoja na dawa za kilimo na shilingi 820,000 zilitengwa kwa ajili ya kuwezesha ufuatiliaji.

  Profesa Muhongo alisema ni jukumu la Kamati husika kuhakikisha fedha imetumika kwa matumizi yaliyokubaliwa na aliagiza vikundi vyenye miradi ya kilimo ambayo haijaanza vinyang’anywe vifaa vilivyokabidhiwa na vipewe vikundi vingine vyenye vyenye nia dhabiti ya kuendeleza kilomo.

  “Tembeleeni hivi vikundi, mkikuta havijaanza kutumia vifaa tulivyowapatia mvinyanga’anye na vifaa hivyo vigawiwe kwenye vikundi vyenye nia ya dhati,” aliagiza Profesa Muhongo.Akizungumzia Awamu ya Pili ya Mfuko wa Jimbo, Profesa Muhongo alisema Mfuko wa Jimbo umepokea kiasi cha shilingi milioni 38,479,000 ambazo alisema Kamati husika kwa kushirikiana na wananchi pamoja na madiwani wamependekeza zitumike kwa ajili ya kuboresha kilimo.

  Alisema shilingi milioni 16,000,000 zitatumika kwa ajili ya kununulia mbegu za kisasa za mihogo za mkombozi kiasi cha vipando 532,000 ambazo zitagawiwa kwenye Kata 21 kwa ajili ya vijiji 68, na shilingi milioni 21,900,000 itatumika kununulia mashine 21 za kukamulia alizeti. 

  Aliongeza kuwa hapo awali alisambaza mbegu za alizeti za majaribio kiasi cha kilo 4000 ambazo alisema zimeonesha mafanikio na hivyo aliongeza mbegu zilizoboreshwa kutoka Arusha kiasi cha kilo 5000 ambazo pia zilisambazwa.

  Alisema ili kujiongezea kipato kutokana na kilimo cha alizeti, wameamua badala ya kuuza mbegu, wakulima hao watauza mafuta na ndiyo sababu ya kutenga kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya mashine hizo ambazo alizielezea kuwa ni za kuzungusha kwa mikono na hazihitaji mafuta wala umeme.

  “Hizi nilitoa fedha yangu na sio katika mfuko wa jimbo; na kukitokea mapungufu nifahamisheni nijazilizie,” alisema.Akizungumzia utaratibu wa mashine hizo, alisema kila Kata itakabidhiwa mashine yake na kwamba zitafungwa kwenye ofisi za kata chini ya usimamizi wa Afisa kilimo.
  Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza jambo wakati wa mkutano wa kujadili matumizi ya fedha za Mfuko wa Jimbo. Kushoto ni wajumbe wa Kamati ya Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini.
  Baadhi ya wananchi wa Kata ya Tegeruka, Musoma Vijijini waliohudhuria mkutano wa kujadili matumizi ya fedha za Mfuko wa Jimbo hilo.
  Katibu wa Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini na Afisa Mipango wa Wilaya ya Musoma, Mukama Rugina (aliyesimama) akizungumza wakati wa mkutano wa kujadili matumizi ya fedha za mfuko huo.
  Diwani wa Kata ya Tegeruka, Benjamin Maheke (aliyesimama) akizungumza wakati wa mkutano wa kujadili matumizi ya fedha za mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Malinyi

  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi,Marcelin Ndimbwa amemwandikia mwenyekiti wa Halmalmashauri Mh. Nasoro Liguguda na baraza lake, kubadilisha matumizi kiasi cha fedha shilingi milioni 100 alizotengewa kwa ajili ya ununuzi  wa gari ya mkurugenzi na kuzielekeza katika ujenzi wa Zahanati tatu.

  Akizungumza na globu ya jamii ofisini kwake mapema leo asubuhi Ndimbwa amesema kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na mahitaji ya huduma za afya katika Wilaya hiyo kuliko yeye kununuliwa gari ya kifahari huku wananchi wakiwa wanateseka.

  “nimemwandikia mwenyekiti wa Halmashauri barua juu ya kubadili matumizi ya fedha hizo kwani nimeona wazi kuwa mahitaji ya Zahanati katika wilaya yangu ni makubwa kuliko hiyo gari kwani Malinyi inahitajika kuwa na zahanati 33 lakini mpaka sasa zipo zahanati tisa tu jambo ambalo linawafanya watu kutembea umbali mrefu kufata huduma za afya”amesema Ndimbwa.

  Amesema kuwa ujenzi wa Zahanati hizo unaanza mara moja katika vijiji vilivyo ainishwa na tayari wananchi walishaanza kukusanya nguvu kwa kujitolea Mchanga ,Mawe na Matofali.

  Ameweka wazi kuwa pindi ujenzi huo utakapoanza hautasimama, kwani kutokana na fedha hizo na nguvu ya wananchi iliyopo kila kitu kitakamilika kwa muda muafaka na wananchi watapata huduma kama ilivyo katika matarajio yao.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, Nasoro Liguguda amesema kuwa ameridhia uamuzi huo kutokana na sera ya serikali na ilani ya chama cha mapinduzi kuitaka kila kata kuwa na kituo cha afya na kila kijiji kuwa na zahanati moja kama mkurugenzi ameona gari sio ya muhimu na zahanati ndio ya msingi sisi tunashukuru.

  Amesema kuwa wanampongeza Mkurugenzi kwa uamuzi huo kwani ni viongozi wachache wenye kariba kama yake ya kufikiria wananchi kwanza kuliko yeye, kwani angekuwa mwanasiasa ningeona kawaida lakini yeye ni mtendaji lakini bado amekuwa na uchungu na watu wa malinyi kuliko mtu mwingine yoyote hivyo sisi tunamuombea awe na moyo huohuo na aishi muda mrefu katika wilaya yetu.

  0 0  Bw. Venanti Kagombora wa Bunju Dar es Salaam anasikitika kutangaza kifo cha baba yake mzazi Omulangira Cornel Kagombora, kilichotokea leo katika Hospitali ya Serikali ya Mkoa, mjini Bukoba. 

  Habari ziwafikie watoto wake Verdiana Kagombora na Prosper Kagombora wa TEXAS Marekani, mkwe wa marehemu Bw. Justin Lambert wa Dar es Salaam na Father Mushuga wa Ibalaizibu Bukoba. Mazishi yafanyika Jumapili, tarehe 1 Januari, 2017 nyumbani kwake Katika kijiji cha Bulembo kitongoji cha Katoma Kamachumu, Kagera.

  0 0

   Mkuu wa wilaya ya Songea Pololeti   Mgema akionyesha moja ya sehemu ambayo moto bado unawaka .
   Hiyo ndiyo hali halisi ya ofisi jinsi ilivyoungua kwa ndani
   Nyaraka za serikali ya kijiji cha Mtyangimbole zikiwa zimeteketea kwa moto na kubaki majivu tu.
   Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya madaba Shafii Mpenda wa kwanza kushoto akiwa anafatilia jambo katika mkutano wa wanakijiji ambao ulifanyika baada ya kumaliza kuzima moto
  Mkuu wa wilaya ya Songea Pololeti   Mgemaakizungumza na wakazi wa kijiji cha Mtyangimbole  baada ya zoezi la kuzima moto kumalizika. Kwa undani wa habari hii angalia hiyo video. (Habari na RUVUMA TV)

  0 0

  NA HAMZA TEMBA -WMU.

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani amesema hakuna mamlaka nyingine ya Serikali chini ya ofisi ya waziri mkuu yenye mamlaka ya kutoa tamko au ufafanuzi kuhusiana na Faru John kwa sasa kwakua jambo hilo bado lipo kwenye uchunguzi.

  Amesema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika tarafa ya Loliondo, Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku mbili wialayani humo kwa ajili ya kufuatilia changamoto za uhifadhi pamoja na utekelezaji wa maagizo wa Waziri Mkuu aliyoyatoa hivi karibuni akiwa ziarani mkoani Arusha.

  Amesema miongoni mwa maagizo aliyoyatoa Waziri Mkuu katika ziara hiyo ni kuwasilishwa kwa taarifa ya inayoelezea utaratibu uliotumika kumuhamisha Faru John kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Sasakwa Black Rhino Sanctuary iliyoko kwenye Hifadhi ya Grumeti pamoja na kuwasilishwa kwa pembe zake ambapo baadae aliunda tume ya kuthibitisha ukweli wa taarifa hiyo.
  .
  "Ripoti hii ya uchunguzi ni mali ya Waziri Mkuu atakayeweza kutoa ripoti hii nje kwa ajili ya matumizi  ya kila mmoja wetu ni Waziri Mkuu, kwa maana ya mamlaka, kwa hiyo hakuna mamlaka nyingine yeyote ya Serikali chini ya Waziri Mkuu yenye uhalali wa kutoa tamko au ufafanuzi wa jambo hili, mpaka pale Waziri Mkuu atakapokamilisha kusoma ripoti kwa kina kwa kutumia wataalam wake, kufanya vipimo kama ambavyo tunasikia amevipeleka kwa mkemia mkuu wa Serikali, pamoja na udadavuzi wa ripoti.

  "Kwa kipindi hiki nnapozungumza, zaidi ya kwamba tunasubiri maagizo au maelekezo au muelekeo sasa juu ya jambo hili kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, hakuna jambo jingine ambalo Wizara inaweza kufanya wala kusema kuhusiana na suala la Faru John, hatuna mamlaka hiyo", amesema.
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akizungumza katika kikao cha wadau wanaohusika na mgogoro wa pori tengefu la Loliondo alichokiitisha katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, katika tarafa ya Loliondo wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha jana. Kupitia kikao hicho aliunda kamati maalum ya kutatua mgogoro wa muda mrefu wa pori tengefu la Loliondo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mfaume Taka.
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akizungumza katika kikao hicho.

  Baadhi ya wadau wanaohusika na mgogoro wa pori tengefu la Loliondo wakiwa kwenye mkutano huo.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Humphrey Shao , Globu ya Jamii Morogoro

  MKUU wa mkoa wa Morogoro Dkt.Kebwe Stevene Kebwe amesema mkoa huo kwa sasa una ziada ya chakula cha tani Milioni 1 na laki 3 katika akiba iliyotokana na uzalishaji wa mwaka 2015/2016.

  Kebwe amesema hayo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa globu ya jamii juu ya mafanikio ya uzalishaji wa chakula katika mkoa huo, ambao una sifa ya kuwa na udongo wenye rutuba na hali ya hewa nzuri.

  “Katika kipindi cha uzalishaji cha mwaka 2015/2016 tumefanikiwa kuzalisha jumla ya tani milioni 1 na laki 8 na huku mahitaji yakiwa ni tani laki tano katika mkoa wetu,hivyo uzalishaji huo umetufanya tuwe na zida kubwa ya  kufikia Milioni 1 na laki 3 tukiwa tunafunga mwaka wa 2016’’amesema Kebwe.

  Ameongeza kuwa katika mwaka huu uzalishaji wa mazao ya shabni uko vizuri, hali inayoashiria hakutakuwa na njaa katika mkoa huo na badala yake ziada ya chakula kinachopatikana hapa kitaweza kulisha mikoa ya jirani.

  Ametaja kuwa licha ya kuwa na mafanikio makubwa katika kilimo cha mashambani,bado kumekuwa na changamoto kubwa ya ongezeko la mifugo katika mkoa huo kulinganisha na eneo ambalo lililopo na mahitaji yanayohitajika kutokana na hesabu za kitaalamu.

  Amesema kuwa serikali yake ya mkoa imejipanga kuhakikisha kuwa inatoa elimu kwa wafugaji kupunguza mifugo mingi na kuwa na mifugo yenye tija ambayo italeta faida kiuchumi kwa muda mfupi hili kupunguza migogoro ya malisho baina ya wakulima na wafugaji.

  0 0
 • 12/31/16--02:39: Article 13


 • 0 0


  Na Lucas Mboje
  KAIMU Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa (pichani) amewaasa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza  nchini kuzingatia  kuwa utendaji wao wa kazi za kila siku uende sambamba na kasi ya Serikali ya Awamu ya tano ili kuleta ufanisi unaotarajiwa.
  KAIMU Kamishna Jenerali, Dkt. Malewa ameyasema hayo jana wakati wa Baraza la Kufunga Mwaka 2016 na kuukaribisha Mwaka 2017 lililowahusisha baadhi ya Maafisa na Askari kutoka Ofisi ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga, Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani pamoja na Magereza ya Mkoa wa Dar es Salaam.

  0 0

  Uongozi wa Coastal Union kutoka mkoani Tanga inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, unawataka wapenzi wake waliopo Dar es Salaam kesho (Jumapili Januari 1, 2017) kufika uwanja wa Karume zilipo ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ili kushuhudia timu mpya na yenye uwezo wa hali ya juu. 
  Kwa mujibu wa Meneja wa timu Hilal Said, vijana wa sasa ni wapya nah ii ni mechi ya pili tangu mzunguko wa pili uanze. Hivyo usajili mpya umeonyesha mwanga na vijana wanapiga soka la uhakika. 
  “Naweza kusema sisi hatustahili kucheza na timu za ligi daraja la kwanza. Hata ligi kuu hakuna timu ya kutufunga kwani kwa  sasa tumekua level nyingine kabisa. Inafika wakati hata tukifanya mechi za majaribio tunaona kama tunazionea timu tunazocheza nazo.
   “Hivyo nawaomba wapenzi wa soka si lazima wawe wa Coastal Union tu bali mpenzi yeyote anayependa kuona soka la uhakika aje Karume kesho Jumapili. Tunafungua mwaka kwa kuichapa Kimondo mabao yasiyo na idadi,” alisema Hilal. 
  Coastal Union inayoshika nafasi ya tano katika kundi B kwa sasa ina point sita huku Kimondo FC kutoka beya ikishika mkia kwenye kundi hili. Mchezo uliopita Coastal Union ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya Polisi Morogoro katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro huku mashabiki wa soka mkoani humo wakisifia kiwango kikubwa kilichoonyeshwa na wachezaji wa Coastal Union. 
  Katibu wa Coastal Union, Thabit Abuu, aliweka wazi kuwa kwa sasa timu yoyote itakayoingia katika anga zao watarajie kichapo kwani wanataka kuhakikisha mechozote sita zilizobaki wanashinda ili kujiweka katika nafasi nzuri. 
  “Tunataka turudi ligi kuu.. Hakuna namna nyingine zaidi ya kuendeleza kichapo popote pale iwe nyumbani au ugenini, kwa sababu timu ya ushindani tunayo na uwezo tunao, hatuna sababu ya kuwa wanyonge,” alisema. 
  Wachezaji wa Coastal Union wameshawasili jijini Dar es Salaam tangu Ijumaa ambapo wamefichwa katika kambi maalumu kwenye moja ya fukwe za Bahari ya Hindi tayari kwa mechi ya Jumapili.

  0 0

  Mbunge Jimbo la Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa Mwanambaya, Luzando, Mipeko na Mlamleni juu ya kumuomba Rais Dkt. John Pombe Magufuli kufuta hatimiliki ya shamba lenye hekari 2472 linalodaiwa kumilikiwa na wawekezaji wenye asili ya Kiasia baada ya wawekezaji hao kushindwa kuliendeleza kwa muda mrefu na badala yake wapewe wananchi.
  Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filberto Hassan Sanga (wa pili kutoka kushoto) na ujumbe wake wakiwasili katika mkutano uliofanyika leo mkoani Pwani.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga, Msham Munde akizungumza na wananchi wa Mwanambaya, Luzando, Mipeko na Mlamleni katika mkutano uliofanyika leo mkoani Pwani.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga, Juma Abeid akizungumza na wananchi wa Mwanambaya, Luzando, Mipeko na Mlamleni katika mkutano uliofanyika leo mkoani Pwani.
  Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Salum Ally Papen akifafanua jambo kwenye mkutano uliofanyika leo mkoani Pwani. 

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Rombo Agnes Hokororo akiangalia namna pombe ya kienyeji inavyoandaliwa baada ya kukamata kiwanda bubu cha kutengenezea pombe bila ya kufuata taratibu.
  Mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza pombe ya kienyeji  aliyefahamik kwa jina moja la Carlos akitoa maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Rombo Agnes Hokororo namna wanavyoandaa pombe hiyo.
  Nyumba ambayo imekuwa iktumika kutengenezea Pombeza kienyeji kulipokutwa mitambo wa kutegeneza pamoja na pombe iliyokuwa katika maandalizi.
  Mkuu wa wilaya ya Rombo Mhe. Agnes Hokororo akimwaga pombe ya kienyeji iliyokuwa ikiandaliwa katika moja ya kiwanda bubu kilichokutwa katika kijiji cha Useri wilayani humo.
  Katibu tawala wa wilaya ya Rombo Bw. Abubakar Asenga akimwaga pombe hiyo mara baada ya kufanya operesheni ya kushtukiza katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Rombo. Picha zaidi BOFYA HAPA  0 0

  NAHODHA wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’, amewatakia mashabiki wa timu hiyo kheri ya mwaka mpya ‘2017’ unaoanza leo saa 6.00 usiku huu huku akiwashukuru kwa sapoti yao waliyoionyesha mwaka huu.

  Bocco ametoa kauli hivi karibuni mara baada ya kumalizika kwa mchezo uliopita wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) dhidi ya Tanzania Prisons walioifunga bao 1-0, huku akifanikiwa kutupia bao hilo pekee lililorudisha morali ndani kikosi hicho baada ya kutofanya vizuri kwenye mechi mbili za ufunguzi wa mzunguko wa pili walipocheza ugenini na African Lyon (0-0) na Majimaji (1-1).

  “Kwanza tunawashukuru mashabiki wetu kwa uvumilivu waliouonyesha, kwa sapoti waliotupa katika kipindi chote kigumu tulichopitia, kama wachezaji na timu kwa ujumla tunawaomba waendelee kuwa na moyo huo huo na pia tunawatakia kheri ya mwaka mpya (2017) na wamalize mwaka huu vizuri, tuendelee kuwa pamoja ili kuisaidia timu yetu iweze kufanya vizuri,” alisema Bocco wakati akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz

  Bocco ambaye ameipatia mafanikio makubwa Azam FC kwa mabao yake muhimu tokea timu hiyo ikiwa madaraja ya chini hadi kupanda Ligi Kuu mwaka 2008, aliendelea kusema kuwa wamepitia changamoto nyingi sana kwa mwaka huu unaoisha huku akidai kuwa wamejifunza kupitia hayo na wanachoangalia kwa mwaka mpya ni kuipeleka mbele zaidi timu hiyo ili kufikia mafanikio. Kusoma zaidi BOFYA HAPA
  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Iringa  Mhe. Richard Kasesela amewaomba radhi wale wote aliokwaluzana nao mwaka 2016 kwa njia moja au nyingine akisisitiza kwamba yeye ni binadamu si malaika hivyo hajakamilika.

  Mhe. Kasesela ameongezea na kusema kuwa katika kuhakikisha mambo yanakwenda sawa lazima mtapishana lugha na watu ndipo mambo yaende sawa, pia amewataka wana Iringa kusherekea mwaka mpya kwa njia ya amani na tulivu kwa undani wa habari hii angalia hiyo video.


  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza walimu wanaishi mbali na shule wakati shule zao zina majengo wahame mara moja na warudi kuishi kwenye nyumba za shule. 
  Amesema haifai kuacha walimu waishi mbali na maeneo ya shule kwani hali hiyo inachangia uchelewaji kazini na inapunguza muda wa kuwasimamia wanafunzi au kuwasaidia jioni pale wanapohitajika kufanya hivyo.

  Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Chingumbwa, kata ya Mbekenyera, wilayani Ruangwa jana mchana (Ijumaa, Desemba 30, 2016) kwenye mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi kijijini hapo. 
  “Nimeambiwa kuwa walimu wako wachache kwa sababu hapa shuleni hakuna nyumba za kuishi walimu. Mbona wanakaa Mbekenyera? Watawezaje kuwahi kazini asubuhi wakati hawana magari? Mvua ikinyesha watafikaje shuleni? Kuanzia leo, walimu wote warudi mara moja na waje kupanga hapa kijijini kwa sababu nyumba zipo,” amesisitiza.


  0 0

   Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea cheti maalum cha kutambua mchango wake katika kukijenga na kukiimarisha Chama cha Mapinduzi wilayani Ruangwa kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi, Ali Mtopa katika mkutano wa hadahara aliouhutubia mjini Ruangwa Desemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Cheti Maalum  cha kutambua mchango wake katika kukijenga na kukiimarisha Chama cha Mapinduzi wilayani Ruangwa alichokabidhiwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Lindi, Ali Topa   (kulia) katika mkutano wa hadhara aliouutubia mjini Ruangwa Desemba 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM wa wilaya ya Ruangwam Issa Njinjo.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni sita kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Pacco GEMS Limited, Bw. Mahendra Bardiya katika harambee  ya kuchangia ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari wilayani Ruangwa ambapo jumla ya shilingi milioni 138.26 zilichangwa. Harambee hiyo ilifanyika sambamba na  mkutano wa hadhara uliohutubia wa Waziri Mkuu mjini Ruangwa, Desemba 30, 2016.
  Wananchi wa Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara mjini Ruangwa, Desemba 30, 2016. 

  0 0

  Na Dotto Mwaibale

  ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Angilikana Tanzania, Dk Valentino Mokiwa amesema migogoro ya kisiasa inayoibuka hivi sasa inaweza kuhatarisha hali ya amani nchini.

  Dk. Mokiwa ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam leo wakati akiwaongoza waumini wa  kanisa hilo Archidikonari ya Kinondoni kutoa misaada ya vifaa tiba na kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala.

  "Migogoro ya kisiasa ambayo imeanza kuzuka hivi sasa inaweza kuhatarisha amani ya nchi ni vizuri viongozi wanaovutana wakutana na kuweka mambo sawa" alisema Mokiwa.

  Alisema migogoro ya kisiasa inayoendelea inaweza kusababisha kutoweka kwa amani hivyo ni jukumu la viongozi husika kuliangalia jambo hilo kwa karibu na kulitafutia ufumbuzi.

  Alisema nchi yetu inahitaji amani na utulivu na kuondokana na matukio ya kuogopesha akitolea mfano miili ya watu saba iliyokutwa ndani ya viroba vilivyotupwa mto Ruvu Bagamoyo mkoani Pwani.Alisema matukio kama hayo yanaweza kuwafanya wananchi kukimbia nchi yao kwa hofu hivyo inatakiwa kila mmoja wetu kuwa na hofu ya mungu.
   Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dk.Valentino Mokiwa (katikati), akiwaongoza waumini wa kanisa hilo Archidikonari ya Kinondoni kufanya usafi katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala Dar es Salaam leo asubuhi wakati kanisa hilo lilipotoa msaada wa vitanda na magodoro katika hospitali hiyo vyote vikiwa na thamani ya sh.milioni 12.
   Waumini wa kanisa hilo wakiendelea na kufanya usafi.
  Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk.Valentino Mokiwa (kulia), akipanda mti nje ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, wakati alipowaongoza waumini wa kanisa hilo  kutoa msaada wa magodoro na vitanda vya wagonjwa pamoja na kufanya usafi wa mazingira Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto anayemsaidia kupanda mti ni Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk.Daniel Nkungu na wengine ni waumini wa kanisa hilo. 
   Askofu Dk. Valentino Mokiwa akimkabidhi moja ya kitanda kati ya 15,  Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Daniel Nkungu.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifanya mazoezi ya viungo kwenye viwanja vya makazi yake jijini Dar es salaam ikiwa sehemu ya kuendeleza kampeni yaKitaifa ya kudhibiti Magonjwa yasiyo ya kuambukiza  aliyoizindua tarehe 17 Desemba, 2016 katika viwanja vya Leaders Club.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi na Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa Oyster bay Ndugu Zefrin Lubuva ikiwa sehemu ya kuendeleza kampeni yaKitaifa ya kudhibiti Magonjwa yasiyo ya kuambukiza  aliyoizindua tarehe 17 Desemba, 2016 katika viwanja vya Leaders Club.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi na Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa Oyster bay Ndugu Zefrin Lubuva pamoja na wasaidizi wake ikiwa sehemu ya kuendeleza kampeni yaKitaifa ya kudhibiti Magonjwa yasiyo ya kuambukiza  aliyoizindua tarehe 17 Desemba, 2016 katika viwanja vya Leaders Club.

  0 0

  Na Frank Mvungi (MAELEZO) 

  Serikali imesema hakuna uhaba wa dawa ya usingizi katika Hospitali ya Rufaa Bombo Mkoani Tanga kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kuwa hali hiyo inachochea kuzorota kwa huduma za upasuaji.

  Akifafanua suala hilo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt. Asha Mahita amesema kuwa taarifa kuwa huduma za upasuaji katika hosipitali hiyo zimesimama si za kweli na ukweli ni kwamba huduma zinaendelea kama kawaida.“Huduma za upasuaji katika Hosipitali yetu zinaendelea kama kawaida na hakuna tatizo kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari” Alisisitiza Dkt. Mahita.

  Akifafanua zaidi Dkt. Mahita alisema kuna mgonjwa mmoja tu ambaye upasuaji wake ulisogezwa mbele kutokana na sababu za kitabibu na si kwa sababu ya kukosekana kwa dawa ya usingizi.
  Aliongeza kuwa sababu zinazoweza kusababisha kuahirishwa kwa upasuaji wa mgonjwa aliye kwenye ratiba ni pamoja na uwepo wa wagonjwa wengi wa dharura hali inayoweza kuchangia nguvu kubwa kuelekezwa katika kuhudumia wagonjwa hao wakiwemo wahanga wa ajali.

  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekuwa ikichukua hatua mbalimbali katika kuwahudumia wananchi na kuhakikisha kuna dawa za kutosha na vifaa tiba katika hospitali na vituo vya kutolea huduma hapa nchini.

  0 0

  Na Dotto Mwaibale

  SERIKALI ya Mtaa wa Maruzuku katika Kata ya Mnyamani Buguruni Manispaa ya Ilala kupitia Chama cha Wananchi (CUF), imetoa sare za shule kwa watoto 200 wanakaoanza darasa la kwanza mwezi Januari ili kuleta msukumo wa masomo katika mtaa huo.

  Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa mtaa huo, Jabiri Sanze alisema wanaziunga mkono jitihada za Rais Dk.John Magufuli za kuhakikisha kila mwanafunzi anapata elimu bure na katika mazingira bora.

  "Tumeamua kutoa msaada huu mdogo kwa watoto 200 waliopo katika mtaa wetu ili kutoa hamasa kwa wazazi na walezi kwani kipindi hiki cha mwezi Januari kinachangamoto kubwa na mahitaji mengi ya shule kwa wanafunzi" alisema Sanze.

  Sanze alitaja msaada huo kuwa ni mashati ya shule, madaftari na penseli za kuandikia ambapo aliwaomba wazazi wasaidie eneo la sketi, kaputura, viatu na mabegi.Alisema watoto walionufaika na msaada huo ni wavulana 86 na wasichana 114 wote kutoka katika mtaa wa Maruzuku.

  Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mnyamani Jafari Mrisho aliupengeza uongozi wa mtaa huo kwa mpango huo wa kuwasaidia watoto hao wanaotarajia kuanza darasa la kwanza na akawaomba wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kusaidia ili kuwafikia watoto wote wa mitaa mitatu ya kata hiyo ambayo ni Mji Mpya, Mbarouk na Mnyamani.

  Mjumbe wa mtaa huo Haroub Mussa aliwataka wazazi wa watoto waliopata msaada huo kutunza sare hizo na kuwa serikali ya mtaa itaendelea kushirikiana na wananchi na kuhakikisha watoto wote wanaopaswa kuanza darasa la kwanza wanakwenda shuleni.
  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Maruzuku katika Kata ya Mnyamani Buguruni Manispaa ya Ilala, kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Jabiri Sanze (kulia), akimkabidhi sare za shule mtoto, Hamad Ali Dar es Salaamleo, ambaye ataanza darasa la kwanza mwezi huu. Serikali ya mtaa huo imetoa sare za shule, daftari na penseli kwa  watoto 200 watakaoanza darasa la kwanza mwaka huu wa 2017. Katikati ni mama wa mtoto huyo, Farida Rashid.
  Mtoto Issa Athumani akipokea msaada huo. Katikati mama yake Halima Issa.
  Mtoto Asnat Mashaka akipokea msaada huo. Nyuma yake ni mama yake, Arat Hamisi

  Watoto na wazazi wao wakisubiri msaada huo.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa salamu za mwaka mpya wa 2017 kwa Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla,   ambapo Dkt Shein ameuombea 2017 kuwa mwaka wa mafanikio na amani katika salamu hizo alizotoa alipokuwa akifanya mahojiano na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Bi. Imane O.Duwe leo katika  ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo. Picha na IKULU


older | 1 | .... | 1484 | 1485 | (Page 1486) | 1487 | 1488 | .... | 3282 | newer