Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1483 | 1484 | (Page 1485) | 1486 | 1487 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.  Baada ya ushindi wa jana wa goli 1-0 dhidi ya  Tanzania Prisons, kikosi cha Azam kwa sasa kinaondoka kwenda visiwani Zanzibar kujiandaa na mivhuano ya Mapinnduzi inayotarajiwa Desemba 31 huku benchi jipya la ufundi likijizatiti kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.

  Katika mchezo huo wa ligi kuu ulikuwa ni wa mwisho kwa Azam  kabla ya kuukaribisha mwaka mpya ‘2017’,  na bao pekee la ushindi likiwekwa kimiani na nahodha John Bocco ‘Adebayor’, katika dakika ya 40 baada ya kupokea pasi safi ya Joseph Mahundi na kuwahadaa mabeki wa Prisons kisha kupiga shuti la kiufundi lililojaa kimiani.

  Azam FC iliingia kwenye mchezo huo ikiwa na sura mpya kwenye benchi la ufundi lililosimamiwa na makocha wa timu yake ya vijana, Idd Nassor Cheche na Idd Abubakar na hii ni kufuatia kuwasitishia mikabata wakufunzi kutoka Hispania wakiongozwa na Kocha Mkuu, Zeben Hernandez na h

  uo ni ushindi wa kwanza wa Azam FC kwenye mechi za mzunguko wa pili wa ligi baada ya kuanza vibaya kwa kutoka sare mechi mbili mfululizo dhidi ya African Lyon (0-0) na Majimaji (1-1).


  Kocha Iddy Nassor Cheche amesema kuwa, kwa sasa anachokiangalia ni kuweza kuisaidia timu yake kuweza kufanya vizuri kwenye kombe la Mapinduzi na si vinginevyo na zaidi ana imani na kikosi che kwani kinaweza kufanya vizuri ya mchezo wao dhidi ya Prison.

  Azam FC kwa sasa inaelekea kwenye changamoto nyingine ya kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambapo itaanza kufungua dimba Jumatatu ijayo kwa kucheza na Zimamoto saa 10.15 jioni ndani ya Uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar wakipangwa katika kundi moja na mabingwa watetezi wa ligi kuu Yanga huku mechi yao ikitarajiwa kuwa Januari 06.

  Kiungo wa Azam Fc Joseph Mahundi akijaribu kumtoka beki wa Prison katika mchezo uliofanyika jana usiku kwenye  Uwanja wa Azam Complex Chamazi

  0 0

  Msajili wa Hazina Dk.Oswald Mashindano akikabidhiana na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya AICC Balozi Dk.Ladislaus Komba mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa mkakati wa mwaka kati ya Taasisi za Serikali na Zisizo za Serikali kupitia msajili wa Hazina.
  Msajili wa Hazina Dk.Oswald Mashindano akizungumza jambo na baadhi ya wajumbe kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam(UDSM)na Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Kitropiki Tanzania.(TPRI) wakati wa hafla ya makabidhiano ya makubaliano ya utekelezaji wa mkakati wa mwaka kati ya Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali kupitia msajili wa hazina.
  Msajili wa Hazina Dk.Oswald Mashindano akikabidhiana na mwakilishi kutoka Mfuko wa Umoja wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa mkakati wa mwaka kati ya Taasisi za Serikali na Serikali kupitia msajili wahazina .Nyuma ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Umoja wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania Bw.James Washima.
  Wajumbe mbalimbali kutoka Bodi yaWakurugenzi ya AICC na Mfuko wa Umoja wa Dhamana ya Uwekezaji  Tanzania wakimskiliza Msajili wa Hazina Dk.Oswald Mashindano (hayupo pichani) wakati wa makubaliano ya utekelezaji wa mkakati wa mwaka kati ya Taasisi za Serikali na Serikali kupitia msajili wa hazina.
  MsajiliwaHazinaDk.Oswald Mashindano akikabidhiana na mwakilishi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Kitropiki  Tanzania (TPRI) mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa mkakati wa mwaka kati yaTaasisi za Serikali na Serikali kupitia msajili wa hazina.
  Mhadhiriwa Chuo Kikuu cha Dar essaalaam Prof. Paramagamba Kabudi akitia saini mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa mkakati wa mwaka kati yaTaasisi za Serikali na Serikali kupitia msajili wa hazina leo Jijini Dar esSalaam.Kushoto kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar esSalaam Profesa Rwekaza Mukandara


  PichanaDaudiManongi-MAELEZO.

  0 0


  Tunatarajia kufanya mazishi ya ndugu yetu, marehemu Ubwa Jaha, siku ya Jumamosi:Desemba 31, 2016, baada ya sala ya adhuhuri 12:30pm. Maiti itasaliwa msikiti wa Bellevue, Washington.

  Kwa taarifa hii tunaomba mchango wa haraka wa  fedha kwa ajili kufanikisha mazishi hayo.
  Gharama inayotukabili ni dola elfu nne  ($4,000).
  Hivi sasa maiti imehifadhiwa funeral home, Kent. Kadiri tutakavyochelewa, gharama zinapanda zaidi.
  Tafadhali pitisha mchango wako:
  Bank of America.
  Ahmed Kayanda.
  Acct. 68316520

  Au wasiliana na mimi (425) 890-7428.

  Tafadhalini sana tushirikiane katika hili.


  Ahsante.
  Ahmed

  0 0


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Ruangwa wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo kuhutubia mkutano wa hadhara Desemba 30, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya ya Ruangwa Desemba 30, 2016.
  Baadhi ya wananchi wa mji wa Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo mjini Ruangwa Desemba 30, 2016.
  Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa wakigalagala kuonyesha furaha katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya ya Ruangwa, Desemba 30, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea zawadi ya mkeka kutoka kwa wananwake wa Ruangwa katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya ya Ruangwa Desemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Kikosi cha Yanga leo hii kimefanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa Uhuru tayari kwa safari hapo kesho kuelekea Visiwani Zanzibar kwenye Michuano ya kombe  la Mapinduzi.

  Kikosi cha Yanga kitaondoka kesho na boti ya saa tisa alasiri kuelekea visiwani huko wakiwa na msafara wa wachezaji 26 pamoja na benchi la ufundi  huku mechi ya kwanza Yanga SC itachezwa saa 2.30 usiku dhidi ya Jang'ombe Amani Stadium.

  Yanga SC inamkosa Vicente Bossou aliyekwenda nchini Senegal kujiunga na timu yake ya taifa ( Togo ) kwa ajili ya michuano ya AFCON inayoanza January 14, 2017. 

   Mechi ya kwanza Yanga SC watacheza saa 2.30 usiku dhidi ya Jang'ombe Amani Stadium.

  Orodha ya wachezaji wanaokwenda Zanzibar katika mashindano hayo;
  Makipa 
  1. Deogratius Munishi
  2. Beno Kakolanya
  3. Ali Mustafa

  Walinzi
  4. Nadir Haroub
  5. Pato Ngonyani
  6. Vicent Andrew 
  7. Hamisi Hassani
  8. Mwinyi Haji
  9. Kelvin Yondani
  10. Juma Abdul 
  11. Oscar Joshua

  Viungo
  12. Haruna Niyonzima
  13. Justin Zullu
  14. Saimoni Msuva
  15. Juma Mahadhi
  16. Geofrey Mwashuiya
  17. Deusi Kaseke
  18. Saidi Juma
  19. Thabani Kamusoko
  20. Yusuph Mhilu

  Washambuliaji
  21. Donald Ngoma
  22. Amisi Tambwe
  23. Emanuel Martin
  24. Obrey Chirwa
  25. Mateo Anthony 
  26. Malimi Busungu

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku kulia akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kikundi cha Golani Shutashuta,Saidi Bakari  wakati alipokwenda akikagua mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji eneo la Golani Shutashuta Kata ya Pande Jijini Tanga jana wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea kuona namna wanavyotekeleza majukumu yao na changamoto ambazo zinawakabili
  Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akikangalia naamna mradi huo unavyopandwa.
  Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akikagua hoho wakati alipokuwa akitembelea mradi huo wa kilimo cha Umwagiliaji wa Kikundi cha Golani Shutashuta eneo la Kata ya Pande Jijini Tanga.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0

  Timu zitakazoshiriki kombe la Mapinduzi msimu huu zinatarajiwa kupata asilimia kumi ya mapato ya uwanjani baada ya kulipiwa gharama zote za siku ya mchezo.

  Kila klabu itapatiwa asilimia hizo 10 baada ya kulipiwa gharama zote ya siku ya mchezo na kinachobakia watapatiwa asilimia hizo.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa kamati inayosimamia kombe la Mapinduzi Sharifa Khamis amesema msimu huu wanatarajia kuwapatia kila timu asilimia 10 ya mapato ya uwanjani baada ya kulimia gharama zote za mchezo.

  “Vilabu vimelalamika hasa vya Zanzibar hali zao ni mbaya sana, kwaiyo kwa pamoja tumekubaliana kwa kila timu tutaipatia asilimia 10 ya mapato ya uwanjani baada ya kulimia gharama zote za mchezo.”

  Aidha kamati ya kombe la Mapinduzi msimu huu imepanga kila timu kuwapatia nafasi 35 kwa wachezaji pamoja na viongozi  kuingia bure uwanjani katika mashindano hayo.

  “Tumekubaliana na vilabu kila timu tutaipatia nafasi 35 za kuingia bure uwanjani kuangalia mashindano hayo.”

  Pazia la Mashindano ya Kombe la Mapinduzi linatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake Disemba 30, 2016 katika uwanja wa Amaan saa 2:15 Usiku ambapo kutakuwa na mchezo wa Derby ya Jangombe kati ya Taifa ya Jangombe na Jangombe boys ambapo mashindano ya msimu huu yameshirikisha vilabu 9, vitano vikitokea Zanzibar, vitatu Tanzania bara na kimoja kutaka Uganda ambao ndio mabingwa watetezi timu ya URA.

  KUNDI A: Simba, URA, KVZ, Taifa ya Jangombe na Jangombe Boys.

  KUNDI B: Yanga, Azam, Zimamoto na Jamhuri.

  RATIBA KAMILI YA MAPINDUZI CUP

  30/12/2016 Taifa ya jang’ombe vs Jang’ombe boys saa 2:30 usiku.

  1/1/2017 KVZ VS URA Saa 10:00 alasiri, Simba vs Taifa ya Jang’ombe saa 2:30 usiku.

  2/1/2017 Azam vs Zimamoto saa 10:00 alasiri, Yanga vs Jamhuri saa 2:30 usiku.

  3/1/2017 Jang’ombe boys vs URA saa 10:00 alasiri, KVZ vs Simba saa 2:30 usiku.

  4/1/2017 Zimamoto vs Yanga saa 10:00 alasiri, Jamhuri vs Azam saa 2:30 usiku.

  5/1/2017 KVZ vs Jang’ombe boys saa 10:00 alasiri, Simba vs URA saa 2:30 usiku.

  6/1/2017 Taifa ya jang’ombe vs KVZ saa 2:30 usiku.

  7/1/2017 Jamhuri vs Zimamoto saa 10:00 alasiri, Yanga vs Azam saa 2:30 usiku.

  8/1/2017 Simba vs Jang’ombe boys saa 10:00 alasiri ,Taifa ya jang’ombe vs URA 2:30 usiku.

  10/1/2017 Saa 10: 00 nusu fainal ya kwanza , Saa 2:30 nusu fainal ya pili.

  13/1/2017 FAINAL saa 2: 30 usiku.

  0 0


  Na Amina Kibwana,Globu ya jamii

  Halmashauri ya manispaa ya kinondoni imezindua utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa jiji la dar es salaam kwa kusaini mkataba wenye thamani ya bilioni 22 na mkandarasi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara.

  Akizungumza na waandishi wa habari maeneo ya makumbusho kata ya kijitonyama leo,Mstahiki meya wa Manispaa hiyo Benjamini Sitta amesema kuwa mpango wa mradi huu unalenga  kuboresha miundombinu ya barabara ambayo itasaidia kupunguza msongamano wa magari, kuondoa adha ya mafuriko na kuongeza thamani ya makazi ya watu pamoja na kupinguza umaskini.

  "Katika uboreshaji wa miundombinu barabara zitajengwa kwa lami nzito na huduma nyingine za watumiaji wa barabara kama maeneo ya waendao kwa miguu,taa za barabarani,mitaro ya majia pamoja na alama za vivuko ambavyo vitambadilisha sura ya manispaa ya Kinondoni na jiji la Dar es Salaam kwa ujumla."

  Aidha meya ametaja  barabara ambazo Zitahusika katika mpango huu ni pamoja na soko la makumbusho km1.45,MMK km 0.9,Nzasa km 1.25, Viwandani km 1.68 na Tanesko soko la samaki ambazo zitajengwa ndani ya mwaka mmoja na kwa kiwango  cha juu.

  Kwa upande wake mkandarasi kutoka Estim Construction Jagdish Bhudia amesema kuwa watajenga barabara kwa kiwango kinachotakiwa kama kwa kutumia lami nzito ili ziweze kudumu kwa muda mrefu bila kuharibika.

  Hata hivyo mstahiki meya wa manispaa ya kinondoni ameongeza kwa kuwataka wanachi wote wa manispaa hiyo kutoa ushirikiano wa kutosha katika mradi huu ambao unalenga kuboresha miundombinu  na kuimarisha huduma za kiuchumi, kibiashara na kijamii.
   Mstahiki Meya wa Manispaa ya kinondoni Benjamini Sitta akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kusaini mkataba huo jijini dar es salaam,kushoto ni mhandisi wa manispaa hiyo Abdul  Digaga

  Baadhi ya Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mapema Leo Jijini Dar es salaam.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amelazimika kuendesha harambee ya papo kwa papo ma kuchangisha sh.milioni 138.26 ili kufanikisha ujenzi wa shule mpya ya sekondari wilayani Ruangwa.


  Hatua hiyo hiyo inafuatia wingi wa wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza lakini hawakufanikiwa kupata nafasi katika mkupuo wa kwanza.

  “Katika kikao cha Halmashauri ya Wilaya cha hivi karibuni ilionekana kuna haja ya kujenga shule mpya ya sekondari ili kukabiliana na wingi wa watoto waliofaulu mtihani wa darasa la saba na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza. Tunawashukuru sana wenzetu ambao wametoa maeneo yao bure ili shule ijengwe haraka,” amesema.

  Katika harambee iliyofanyika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Ruangwa leo mchana (Ijumaa, Desemba 30, 2016), Waziri Mkuu amefanikisha kupatikana kwa fedha kiasi cha sh. milioni 120.65 na mifuko 550 ya saruji  na mabati 360 (vyenye thamani ya sh. milioni 17.61) ambavyo vitatumika kujenga madarasa manne ya kidato cha kwanza yanayotakiwa kuwa yamekamilika ifikapo Januari 15, 2017.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Bw. Andrea Chezue, jumla ya watoto 319 walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza lakini walikosa nafasi sababu ya ukosefu wa madarasa na walitakiwa kusubiri hadi chaguo la pili ambalo kwa kawaida hufanyika Februari, kila mwaka.

  “Wanafunzi waliofaulu na kukosa nafasi jumla yao ni 319 lakini kwa hapa Ruangwa mjini ni 179 na waliobakia 140 wanatoka kwenye kata za jirani za Nachingwea na Mandarawe. Shule hii ya sekondari itahudumia kata tatu. Kwa hiyo Halmashauri imepanga kujenga madarasa manne hapa mjini ili watoto wote waweze kuanza mara moja,” amesema.

  Mkurugenzi huyo amesema ili kupunguza tatizo hilo mwakani, wataendeleza ujenzi wa madarasa manne manne waweze kuwa na mikondo minne kwa kila kidato. “Halmashauri ya Ruangwa imetenga sh. milioni 75, wananchi wa Kata ya Ruangwa wametoa sh. milioni 1.2 na wananchi wa kata ya Nachingwea wametoa sh. milioni 2.25,” amesema.

  Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo hilo, amechangia sh. milioni 33 kutoka kwenye mfuko wa jimbo ili kuharakisha ujenzi wa madarasa mawili ya kuanzia. Wengine waliochangia harambee hiyo ni kampuni ya Paco Gems Ltd, (sh. milioni 6), Baraka Solar (sh. milioni moja), Ofisi ya Mkuu wa Mkoa (sh. milioni 1), Kampuni ya Asamalema (sh. milioni 1) na mfanyabiashara wa Ruangwa, Bw. Abdallah Namkudai (sh. 200,000).

  Wengine ni kampuni ya wanyumbani construction mifuko 100 ya saruji, kampuni ya Lindi Jumbo (mabati 100 na mifuko 100 ya saruji), kampuni ya madini ya Nazareth (mifuko 150 ya saruji), kampuni ya URANEX inayochimba madini ya Graphite (mabati 260), mgodi wa dhahabu wa Namungo (mifuko 100 ya saruji) na Kampuni ya ujenzi ya Nahungo Construction Ltd. (mifuko 100 ya saruji).

  Waziri Mkuu amewashukuru wote waliojitolea kuchangia ujenzi wa shule hiyo. Amerejea jijini Dar es Salaam jioni hii.

  IMETOLEWA NA
  OFISI YA WAZIRI MKUU

  IJUMAA, DESEMBA 30, 2016.

  0 0

  Na Amina Kibwana, Globu ya Jamii.

  Takwimu za ukuaji wa uchumi nchini unaonyesha unaendelea kukua kwa kiasi kubwa zaidi kulinganisha na mataifa mengine na kuwa  miongoni mwa Nchi  za bara la Afrika , Kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo uchumi wake unakuwa ikifuatiwa na Congo DRC na Rwanda,Kenya, Uganda, Burundi, Afrika ya Kusini, Zambia na Malawi.

  Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa fedha na Mipango Dkt Phillip Mpango amesema kuwa kukua kwa uchumi kunapimwa kwa kuangalia  shughuli mbalimbali za kiuchumi zikiwemo ni pamoja na uzalishaji wa chakula na mazao mbalimbali ya kilimo, mifugo na uvuvi, uzalishaji wa bidhaa za viwandani na migodini, ujenzi wa miundombinu na utoaji wa huduma mbalimbali za kwa jamii ikiwemo  afya, elimu na maji.

  "Kasi ya kuongezeka au kupungua kwa uzalishaji wa bidhaa na huduma katika nchi ni mojawapo ya vitu vinavyotazamwa katika kutathmini afya ya uchumi wa Taifa kwa ujumla ambapo kiashiria kimojawapo kinachotumika kupima ukuaji wa uchumi ni ukuaji wa pato la Taifa."

  Aidha Dkt Mpango ameongeza kuwa kiashiria kingine ni mfumuko wa bei bao unapima mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya ambapo ulipungua kutoka asilimia 6.5 januari 2016 hadi asilimia5.5 juni  na kupungua zaidi hadi kufikia asilimia 4.5 na kupanda hadi asilimia 4.8 mwezi novemba 2016.

  Amesema katika mwezi huo wa Novemba takribani nchi zote zilikuwa na ongezeko la mfumuko wa bei kutokana na kuyumba kwa ugavi wa chakula katika nchi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na kupanda kwa bei kwa bei za mafuta katika soko la Dunia.

  Dkt Mpango amesema  kwa tathimi ya upande wa mabenki unaonyesha kuwa benki yanaendelea kuimarika huku yakiwa na mitaji na ukwasi wa kutosha kwa kuangalia uwiano kati ya mali inayoweza kubadilishwa kuwa fedha taslimu na amana zinazoweza kuhitajika katika muda mfupi ambao ulikuwa kwa asilimia 37.46 ukilinganishwa na uwiano wa chini unaohitajika kisheria wa asilimia 20.

  " amana za wateja katika benki zilipungua kidogo kutoka Trilioni 20.73 mwezi Desemba 2015 kufikia shilingi Triliani 20.57 mwezi septemba kutokana na uamuzi wa Serikali kuhamisha sehemu ya fedha za taasisi na mashirika ya Umma kutoka benki ya biashara kwenda benki kuu ya Tanzania."

  Hata hivyo Mpango amesema kwa kuzingatia mwenendo wa ukuaji wa uchumi kwa kipindi cha Januari hadi septemba 2016 matarajio ni kwamba kasi ya ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2016 na 2017 unatarajiwa kufikia hadi asilimia 7.2 kama ilivyokaririwa awali.
  Waziri wa fedha na Mipango Dkt Phillip Mpango akizungumza na waandishi wa habari juu ya ukuaji wa uchumi wa nchi kutokana kuongezeak kwa uzalishaji wa chakula na mazao mbalimbaliu ya kilimo, biashara, viwanda na migodi.
  Waandishi na watumishi mbalimbali wa sekta ya fedha nchini wakimsikiliza
  Waziri wa fedha na Mipango Dkt Phillip Mpango hahyupo pichani.
  Picha na Chalila Kibuda-Globu ya Jamii. 

  0 0


    Naibu Kamishna wa Magereza, Edith Mallya akimkaribisha Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(katikati aliyeketi) kabla ya kuongea na Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam katika Baraza Maalum la kufunga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka mpya 2017(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa D ar es Salaam, SACP. Augustine Mboje. Baraza hilo limefanyika Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salaam Desemba 30, 2016.
   Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akijibu kero mbalimbali zilizoulizwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam(hawapo pichani) katika Baraza Maalum la kufunga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka mpya 2017
   Askari wa Jeshi la Magereza kutoka vituo mbalimbali vya Magereza ya Mkoa wa Dar es Salaam wakisikiliza hotuba ya Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(hayupo pichani) katika Baraza Maalum la kufunga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka mpya 2017.
   Afisa Utumishi wa Jeshi la Magereza, Mrakibu wa Magereza Elmas Mgimwa akitolea ufafanuzi kuhusiana na masuala ya kiutumishi yaliyoulizwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam(hawapo pichani) katika Baraza hilo.
  Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa umakini mkubwa hotuba ya Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa kwenye Baraza hilo (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0


   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuashiria ufunguzi  wa Msikiti   Masjid Muhammad (S.A.W) uliojengwa na Kampuni ya Al-Buwardy huko Fujoni Mzambarauni Wilaya ya Kaskazini B" Mkoa wa kaskazini Unguja leo (kushoto) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar pia Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Mhe,Balozi Seif Ali Iddi
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akikata Utepe fkama ni ishara ya  ufunguzi  wa Msikiti   Masjid Muhammad (S.A.W) uliojengwa na Kampuni ya Al-Buwardy huko Fujoni Mzambarauni Wilaya ya Kaskazini B" Mkoa wa Kaskazini Unguja leo chini ya usimamizi wa Bw,Yakoub Othman (hayupo pichani) pia wakiwepo (kulia} Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe,Vuai Mwinyi Mohamed na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman (kushoto)
   Sheikh Othman Maalim alipokuwa akitoa mawaidha baada ya ufunguzi wa  Msikiti   Masjid Muhammad (S.A.W) uliojengwa na Kampuni ya Al-Buwardy huko Fujoni Mzambarauni Wilaya ya Kaskazini B" Mkoa wa Kaskazini Unguja leo,ambapo umefunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati waliokaa)
   Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Kijiji cha Fujoni Mzambarauni na Vijiji jirani wakiwa ndani ya Msikiti   Masjid Muhammad (S.A.W) uliofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) ambao umejengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Al-Buwardy,chini ya Usimamizi wa Bw,Yakoub Othman mwakilishi wa kampuni hiyo

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akitoa nasaha zake kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu baada ya swala ya Ijumaa leo alipoufungua Msikiti   Masjid Muhammad (S.A.W) uliojengwa na Kampuni ya Al-Buwardy huko Fujoni Mzambarauni Wilaya ya Kaskazini B" Mkoa wa kaskazini Unguja,uliojengwa chini ya usimamizi wa Bw,Yakoub Othman (hayupo pichani) kwa ufadhili Kampuni ya Al-Buwardy.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0
  0 0


  0 0
  0 0

  Na: Frank Shija – MAELEZO

  WADAU waombwa kujitokeza na kuongeza kasi ya udhamini wa miradi inayotekelezwa kwa malengo ya kukwamua jamii kuondokana na changamoto mbalimbali wanazo kabiliana nazo.

  Hayo yamebainishwa jana Jijini Dar es Salaam na Katibu wa Mradi wa Binti Jitambue Bi. Lilian Boniface wakati wa mkutano wao na wahandishi wa habari kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mradi huo kwa kipindi cha miezi 11.

  Awali akifafanua changamoto walizokumbana nazo katika utekelezaji wa mradi huo Lilian amesema uhaba wa rasilimali fedha imekuwa kikwazo kikubwa kwao katika kutekeleza kwa ufasaha malengo ya mradi huo katika baadhi ya maeneo.

  “Nitumie fursa hii kutoa wito kwa Serikali na wadau wote wa maendeleo kutoa ufadhili kwa ajili kuimarisha utekelezaji wa mradi huu wa “Binti Jitambue” ili wasichana wengi zaidi waweze kunufaika na mradi huu muhimu kwao,” alisema Lilian.

  Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa Binti Jitambue, Sara Bedah Akwisombe amesema kuwa licha ya changamoto wanazokumbana nazo wamefanikiwa kuwafikia watoto wa kike wenye umri kati ya miaka 10 hadi 16 wapatao 4000 nakuwapatia elimu juu ya Afya ya uzazi,, makuzi na kujitambua.

  Aliongeza kuwa tathmini ya mradi huo imebaini kuwa takribani asilimia 80 ya wazazi hawapati muda wa kukaa na kuwaelimisha watoto wao juu ya masuala mbalimbali yanayohusu malezi na makuzi.

  Katika kutekeleza azma hiyo mwaka 2017 mradi huu pia utatekelezwa katika mkoa wa Tanga ikiwa ni muendelezo wa jitihada za kuwasaidia watoto wa kike kujitambua na kutambua thamani na fursa zao katika jamii.

  Binti Jitambue ni mradi ambao umeanzishwa tarehe 30 Januari, 2016, kwa lengo la kusaidia utipatikanaji wa elimu ya afya ya uzazi, malezi na makuzi, elimu ya kujitambua utu na thamani kwa watoto wa kike, ambapo awamu ya kwanza umetekeleza katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Kirimanjaro chini ya uratibu wa Taasisi ya Tanzania Youth Vision Association (TYVA) ya jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi ametoa wito kwa watumishi wa Umma Mkoani humo kuingia mwaka 2017 wakiwa na uelewa sahihi wa malengo ya serikali ya awamu ya Tano ya kuwatumikia wananchi kwa uweledi na kutatua matatizo yao kwa kasi ili kuinua maisha ya wananchi na Maendeleo ya Mkoa huo.

  Mwaka 2017,tunataka tupige hatua kubwa zaidi kupitia raslimali zetu ambazo zitawezesha maendeleo katika Mifugo, Ukulima Mazao ya Kisasa, Ufugaji Nyuki, Ufugaji Samaki, Uvunaji wa Maji ya Mvua, Utunzaji wa Mazingira na Usindikaji wa Mazao kwa malengo ya ujumla ya kumuendeleza mwananchi na kutosheleza mahitaji ya Wanasingida na Soko la Dodoma Makao Makuu ya Nchi. Tunafanikiwa iwapo wananchi wote, watendaji na Viongozi wote tutashirikiana na kuwajibika kwa uwaminifu, uwadilifu na uweledi. Aliongeza Dr Nchimbi

  Dkt Nchimbi amewataka wanchi wote wa Mkoani Singida washerekee Mwaka Mpya kwa amani bila kufanya mambo yeyote yatakayo ashiria uvunjifu wa amani ili kuufanya Mkoa huo kuwa ni kielelezo cha Utulivyo na amani na kuwafanya wageni wanaoingia Singida wasiwe na hufu na masha juu ya usalama wao.

  Nawashauri wananchi wa Mkoa wangu wa Singida kuukaribisha mwaka mpya kwa kwenda kwenye nyumba za ibada na kumshukuru Mungu kwa Uzima aliotupatia na pia kuombea Mkoa wetu wetu na Nchi kwa ujumla ili Mungu azidi kutukirimia neema zake, kwa wale watakao jaribu kuleta fujo napenda kuwaambia kuwa Jicho na Sikio la Serikali hapa Singida liko makini na watashughulikiwa kikamilifu. Alimalizia Mh Dr Nchimbi
  Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi.

older | 1 | .... | 1483 | 1484 | (Page 1485) | 1486 | 1487 | .... | 3285 | newer