Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1482 | 1483 | (Page 1484) | 1485 | 1486 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Mkurugenzi wa shuke ya sekondari Lord Baden  Powell Kanali (kst) Iddy Kipingu (katikati) akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam. Kulia niu Meneja Masoko New Habari Michael Budigile pamoja na mratibu wa mchakato wa uteuzi wa watoto wenye vipaji  Michael Mauris.

  Na Anthony John, 
  Globu ya Jamii.
    IKIWA tunaelekea kwenye  uenyeji wa michuano ga soka la vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 mwaka 2019, Kanali Idd  kipingu kupitia shule yake ya Lord Barden Powell ameandaa muchuano ga kupata vijana 20 watakaosoma na kucheza  mpira katika shule hiyo.

   Akizungumza leo hii jijini hapa Dar es salaam wa Mratibu wa mradi huo Michael Maurus, amesema jumla ya vijana 150 wamejitokeza katika mchuano huo na unaotarajiwa kuanza januari1 hadi tareh 3 katika viwanja vya shule hiyo.
   "Mbali na maandalizi ya michuano hiyo lakini mradi huo ni mahususi kwa ajili ya kuendeleaza vipaji vya vijana wanaomaliza darasa la saba kujiunga na shule na shule hiyo"amesema.
    Kanali mstaafu kipingu amesema  kuwa vijana wanaotakiwa katika shule hiyo ni wale wenye umri wa miaka 13 na 14 ambao mpaka michuano hiyo ya vijana ikifika watakuwa wameshakomaa.
   " Tunataka vijana wenye vipaji kwani  ni jambo la aibu kuona Tanzania tunakuwa wenyeji wa michuano ya vijana, alafu tunashudia kombe likiondoka machoni kwetu, hii sasa basi tunaanza maandalizi mapema" amesema kipingo.

  0 0

  Basi dogo ya abiria aina ya Toyota Coaster inayofanya safari zake kati ya Mbagala Rangi tatu kuelekea Kimanzichana Mkoani Pwani, limeingia kwenye mtaro usiku huu uliopo usoni kabisa mwa kiota maarufu cha DarLive, Mbagala jijini Dar es salaam, baada ya dereva wake kushindwa kulimudu  kutokana na mwendo kasi aliokuwa nao. hakuna majeruhi wana mtu kupoteza maisha kwenye tukio la ajali hiyo.
  Watu wa BeakDown wakifanya maarifa ya kulichomoa Basi hilo kutoka mtaroni baada ya ajali hiyo.


  0 0

   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati) akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wilayani Ngorongoro mkoani Arusha jana katika ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu. Kulia ni Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Freddy Manongi na Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha (kushoto). 
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wilayani Ngorongoro mkoani Arusha jana katika ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu,  ametoa wiki mbili kwa watumishi wenye mifugo na majengo ndani ya eneo la mamlaka ya hifadhi hiyo kujiandikisha kwa uongozi wa mamlaka hiyo ikiwa ni mkakati wa utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu. 

  Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha akichangia katika mkutano huo. Alieleza kuwa salama ya Hifadhi ya Ngorongoro itategemea uwekaji wa mizania sawa baina ya uhifadhi na maendeleo ya wananchi wa eneo hilo.

   Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Freddy Manongi (katikati) akizungmza katika mkutano huo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof. Alexandre Songorwa (kulia).

  BOFYA HAPA KUSOMA HABARI KAMILI

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akipokea zawadi za pampers ambazo zitatumika kwa watoto waliolazwa kutoka kwa Mary Mabano ambaye mwaka 2008 alifanyiwa upasuaji na madaktari wa Taasisi hiyo na kuwekewa Valve moja ambayo inamsaidia kupitisha damu vizuri baada ya upasuaji huo amepona na amejaliwa kupata mtoto mmoja. Siku ya jana tarehe 28/12/2016 Mary alikuwa anatimiza umri wa miaka 23 na aliamua kusherehekea siku hiyo na wagonjwa wa moyo.
  Mary Mabano akimlisha keki mgonjwa wa Moyo Nasra Hamis ambaye amefanyiwa upasuaji na kuwekewa Valve ambayo inamsaidia kupitisha damu vizuri katika moyo wake.
  Madaktari Bingwa wa Moyo, Wauguzi , wagonjwa wa Moyo, ndugu, jamaa na marafiki wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa sherehe ya kuzaliwa kwa Mary Mabano ambaye aliyesherehea siku hiyo na wagonjwa wa Moyo waliolazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). Wa tano kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi.


  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuwalinda watoto wa kike na ndiyo maana inasisitiza waachwe wasome hadi wamalize kidato cha sita.

  Alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi wa vijiji mbalimbali vya wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi ambako anapita kuwasalimia wananchi wa jimbo lake na kuhimiza kazi za maendeleo. Waziri Mkuu yuko Ruangwa kwa siku nne kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.

  “Tumesema mtoto wa kike aachwe asome hadi kidato cha sita, akifika chuo kikuu atakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi yake lakini kwa sasa waacheni watoto wa kike wasome. Ninyi vijana, mkibainika mmewapa mimba mabinti wanaosoma, adhabu yake ni miaka 30 jela,” alisema.

  Alisema nia ya Serikali ni kupata watumishi ambao ni wataalamu wa kada tofauti kama madaktari, wanasheria, mafundi, walimu na hata Wakuu wa Wilaya ambao ni wanawake.

  Aliwaonya wazazi ambao huwa wanakubali kuongea pembeni (kupewa fedha) na wanaume waliowapa mimba mabinti zao na kuwaeleza kuwa, kwa mujibu wa sheria ilivyo, nao pia wanastahili kupewa adhabu ya kifungo jela.

  “Mzazi ukigundua binti yako ana ujauzito toa taarifa haraka ili mhusika akamatwe mara moja. Usikubali kuongelea jambo hili pembeni, nawe pia utawekwa ndani pamoja na huyo mhusika ambaye tayari ni mhalifu,” alisema na kuongeza:

  “Mwanao akisema anataka kuoa, mzazi inabidi upeleleze kwanza anataka kumuoa nani. Asije kuwa anamuona binti ambaye bado anasoma. Akisema anaoa na wewe ukamkubalia tu, ikija kubainika kuwa ni mwanafunzi, wewe na mkeo mnakwenda jela miaka mitano mara sita,” alisema huku akionyesha ishara ya kukunja ngumi.

  Akiwa kwenye baadhi ya vijiji, Waziri Mkuu alielezwa kwamba kuna shule ambazo zina walimu wa kiume watupu na akamtaka Afisa elimu asimamie suala hilo kwa kuwahamisha baadhi ya walimu kutoka Ruangwa mjini na kuwapeleka shuke za vijijini.

  “Kuna shule pale Ruangwa mjini zina walimu wamerundika lakini hapa naambiwa hakuna Mwalimu wa kike hata mmoja. Hili tatizo kwa wanafunzi wa kike. Wana masuala ambayo hawawezi kuongea na walimu wa kiume, ni lazime awepo Mwalimu wa kike wa kusikiliza shida zao,” alisema na kumsisitiza afisa elimu afuatilie tatizo hilo kwenye shule zote.

  Mapema, akitoa taarifa ya mkoa mbele ya Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi alisema mkoa huo unakabiliwa na tatizo la utoro mashuleni kwani wanaoandikishwa darasa la kwanza si wote wanaomaliza darasa la saba na vivyo kwa wanaoanza kidato cha kwanza na kumaliza kidato cha nne.

  “Takwimu zinaonesha mkoa wa Lindi unalo tatizo kubwa sana na ambalo tunaendelea kulipa uzito wa pekee la kudhibiti wanafunzi wanaoandikishwa kuanza shule lakini wanashindwa kukamilisha kipindi chao cha miaka saba shuleni. Idadi kubwa ya wanafunzi ni watoro,” alisema.

  Takwimu za kidato cha nne zinaonyesha kuwa idadi ya watahiniwa wa shule walikuwa 4,764 (wavulana 2411 na wasichana 2,353) na watahiniwa wa kujitegemea walisajiliwa 335 na kati yao watahiniwa 290 (asilimia 86.6) walifanya mtihani na watahiniwa 45 ambao ni sawa na asilimia 13.4 hawakufanya mtihani.

  Kwa upande wa masomo ya sayansi, shule zilizofanya mitihani ya sayansi ya vitendo (actual practical) zilikuwa ni 78 (Kilwa 19, Liwale 11, Lindi Manispaa 9, Ruangwa 4, Lindi vijijini 14 na Nachingwea 21) watahiniwa ambao hawakufanya mtihani baada ya kusajiliwa ni 100 (wavulana 50 wasichana 50).

  0 0

  Watu watano wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa baada ya kudondokewa na mwamba wa mawe katika shimo la mgodi wa zamani wa Resolute, uliopo Nzega mkoani Tabora.

  Akizungumzia swala hilo, Mkuu wa wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupulla alisema tukio hilo limetokea jana saa 7:00 baada ya kundi la wachimbaji wadogo wa mgodi wa Umoja kuvamia eneo hilo ambalo limepigwa marufuku na Serikali.


  Alisema eneo hilo limezuiwa kuchimbwa kutokana na hatari iliyopo lakini baadhi ya wachimbaji wamekuwa wakiingia kwa kificho kuchimba.


  Aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni Joseph Mpenda, mkazi wa shinyanga, Mohamed Mohamed mkazi wa Singida , Manona Nyombi mkazi wa Bariadi na Modesta Leonard mkazi wa Nzega.


  Waliojeruhiwa ni Kangwa Mayenga mkazi wa Bariadi, Agness Antony mkazi wa Chato, Deus Alphonce mkazi wa Igunga na aliyefahamika kwa jina moja la Mapunda mkazi wa Chato. Chanzo - Mwananchi.

  0 0


  Toa maoni kama unathamini nchi yako. Hizi ni rangi za Tanzania 
  sio Simba au Yanga ni rangi za nchi yetu - Alex Kajumulo.

  0 0
  0 0

  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii.

  Bondia wa ngumi za kulipwa nchini mwenye makazi yake Mkoani Morogoro ameondoka mjini humo kwenda Dar es Salaam kuitikia wito wa Polisi.

  Cheka ambaye alijisalimisha katika kituo cha Polisi Morogoro baada ya kupokea wito wa kufika kituoni kufuatia kupata barua ya wito huo.
  "Nimefika kituoni na kuelezwa kuwa nimefunguliwa mashtaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa Promota Siraju Kaike  hivyo nimefika hapo na kujidhamini na kuamua kwenda kituo cha Polisi Osterbay kwa ajili ya kutoa maelezo" amesema Cheka.

  Amesema kuwa mashabiki wake wawe na imani nae kwani huo sio utapeli kama unavyozungumzwa bali ni mapromota uchwara wanataka kula migongoni mwa mabondia.

  "Lazima nikwambie ndugu mwandishi Mimi nishakuwa mkubwa sasa na hizi ngumi zinauma hivyo Biashara ya pesa baadae ilishapitwa na wakati" alisema Chema.

  Hivyo tuombe mungu mambo yote yatajulikana mahakamani.

  0 0

  Dereva boda boda Kasian Haule ambaye alimpakia Denis Komba na nyoka wake.
  ...................................

  Tukio lililo zua taharuki kwa wakazi wa songea mkoani Ruvuma na kupewa nafasi kubwa katika vyombo vya habari vya Tanzania na nje ya Tanzania pamoja na mitandao ya kijamii, huku likiacha gumzo midomoni mwa watu, kuhusiana na kifo cha DENIS KOMBA kufariki dunia baada ya nyoka wake aliyekuwa anasadikiwa kummiliki, kuuawa na wananchi DESEMBA 26 MWAKA HUU, majira ya saa 4 na nusu usiku , katika maeneo ya hospital ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma. Ruvuma TV imezungumza na KASIANI HAULE, ambaye ndiye dereva boda boda aliyekuwa kakodiwa na marehe DENISI KOMBA Bonyeza hiyo Video upate ukweli wa tukio.

  0 0

  Uingereza imesema itasaidia kufadhili matumizi ya ndege zisizokuwa na rubani kusafirisha damu na vifaa vingine vya hospitali kwenye vituo vya afya nchini Tanzania. 

  Lengo ni kupunguza kwa kiasi kikubwa muda unaotumiwa kutuma akiba ya damu kwenye kliniki za afya katika mataifa ya Afrika kwa njia ya barabara na njia nyinginezo.

  Mfumo utakaotumiwa utahusisha matumizi ya kamba ama uzio kuunganisha sehemu moja hadi nyingine, na mabonde hadi mabonde yenye makazi ya watu , mfumo huo sawa na ule umbao ulianza tayari kutumiwa nchini Rwanda mwezi Oktoba 2016.

  Wataalam wamepongeza mpango huo, lakini wanahoji kuwa ”ndege hizo za mizigo zisizokuwa na rubani (drones)” kwa kutoweza kutumiwa na binadamu.

  Shirirka la Uingereza la maendeleo ya kimataifa (Dfid) halijasema ni kiwango gani cha pesa litawekeza katika mradi huo nchini Tanzania na ni kwa muda gani .

  Mfumo wa kamba wa ndege zisizokuwa na rubani (drones) – unaoitwa Zips – husafirisha ndege hizo kwa kuziweka kwenye mbawa ndogo za ndege zinazofyatuliwa kutoka kwenye kifaa maalum na kwa kufuata mfumo ulioandaliwa awali kwa kutumia data za eneo.
  Faida ya mfumo huo ni kwamba ndege inaweza kukabiliana na hali ya hewa ya upepo mkali kwa muda .

  Kwa nadharia, ndege hizo zinaweza kupaa kwa takriban maili 180 ama kilomita 290 kabla ya kuishiwa nguvu za nishati. Ndege hiyo husafiri chini ya futi 500 kutoka ardhini ama mita 152 kuepuka anga ya juu inayotumiwa na ndege za abiria.

  Tanzania, Rwanda na Malawi – ambazo zinatumia aina tofauti za ndege hizi zisizokuwa na rubani kwa usambazaji wa huduma za matibabu – zote zina sheria tofauti kuhusu utumiaji wa ndege zisizokuwa na rubani , suala ambalo lilizifanya kuwa mahala pema kwa majaribio ya aina hii.

  Mapema mwaka huu, Tanzania pia iliidhinisha kisheria matumizi ya ndege zisizokuwa na rubani katika Mbuga ya wanyama ya Tarangire kama sehemu ya juhudi za kuzuwia uwindaji haramu wa wanyamapori.

  Dfid linakadiria kuwa usafirishaji damu na usambazaji wa huduma nyingine za afya kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani kutoka nje ya mji mkuu wa Tanzania , Dodoma, kunaweza kuokoa $58,000 kwa mwaka ikilinganishwa na matumizi ya gari ama pikipiki kusambaza huduma hizo .

  Lakini msemaji wa Dfid amesema kwamba kuokoa muda wa shughuli ya usambazaji wa huduma hizo ndio la muhimu zaidi.

  “Safari za ndege hizo zinatarajiwa kuanza mapema mwaka 2017, na watakapofanya hivyo inakadiriwa kuwa mpango huo utasaidia katika uzazi salama wa watoto zaidi ya 50,000, ikiwa ni pamoja na kupunguza muda wa wanawake na watoto wachanga wanaosubiri kupata matibabu ya kunusuru maisha yao wa dakika 19 – utakaopungua kutoka dakika 110 ambao ndio unaotumiwa katika usafiri wa kawaida ” alibainisha.

  Taasisi ya afya ya Ifakara -iliyobobea katika tiba za malaria, HIV, na kifua kikuu na matatizo ya afya ya akili- itakuwa ndio mshirika wa Dfid katika mpango huu .

  Chanzo: bbcswahili

  0 0

  Rais wa Marekani, Barack Obama ameamuru kutimuliwa kwa wanadiplomaisa thelathini na tano (35) wa Urusi kufuatia tuhuma za Urusi kutaka kuingilia kati uchaguzi wa Marekani kupitia njia ya mtandao.

  Makazi ya wanadiplomasia wawili wa Urusi yamefungwa na baadae kuwekewa vikwazo.
  Rais Obama amesema Urusi imekuwa ikiwadhalilisha maafisa wa Marekani na ametahadharisha hatua zaidi kuchukuliwa.

  Obama ameendelea kusema wamarekani wote sharti washtushwe na vitendo vya Urusi, hii ikionekana kama njia ya kumjibu mrithi wake Donald Trump ambae amesema kila mtu aishi maisha yake.

  Kwa upande wake, Rais mteule mara kwa mara amekuwa akizipuuzia taarifa hizo za udukuzi, lakini hivi amesema atakutana na wakuu wa mashushu wa Marekani ili kulijadili hilo.

  Urusi nayo imekana tuhuma za kufanya udukuzi mfumo wa mtandao wa chama cha Democratic.
  Msemaji wa serikali ya Urusi amesema Urusi nayo italipiza kwa kiwango hicho hicho.CHANZO: BBCSwahili


  0 0
 • 12/29/16--23:45: BEI YA MADAFU LEO


 • 0 0

  Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini (TPBC) imetangaza kumfungia kwa miaka miwili Bondia wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka kufuatia kitendo chake cha kugoma kupanda ulingoni kuzichapa na Bondia Abdallah Pazi "Dullah Mbabe" pambano lililokuwa lifanyika Desemba 25 mwaka huu, katika Ukumbi wa PTA Saba saba jijini Dar es salaam, lililoandaliwa na Promota Siraju Kaike kupitia kampuni yake ya Kaike Promosion.
  Rais wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini (TPBC) Chaurembo Palasa akitoa ufafanuzi zaidi kwa Waandishi wa Habari mapema leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar kuhusiana na sakata la Bondia Francis Cheka,kulia kwake ni Katibu Msaidizi wa 

  Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini (TPBC), Chatta Michael 

  Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Katibu Msaidizi wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini (TPBC), Chatta Michael amesema kuwa Kamisheni yake ilitoa kibali cha kufanyika kwa mpambano huo baada ya kujiridhisha kuwa taratibu zote zimefuatwa na mabondia wameridhia na kukubaliana na muandaaji, Ila wameshangwaza na Bondia Francis Cheka kugoma kupanda ulingoni kwa madai ya malipo wakati alishasaini mkataba na muandaaji ulioonyesha kuwa ameshachukua kiasi cha shilingi milioni tatu (3,000,000) na baada ya mpambano alitakiwa kupewa kitita chake cha milioni sita.

  Amesema kitendo kilichofanywa na Cheka kinaweza kupoteza uaminifu baina ya mabondia na waandaaji wa mapambano, kujiondoa kwa waandaaji katika mchezo huo kwa kuona hakuna uaminifu na pia kinaweza sababisha uvunjifu wa amani kwa watazamaji, iwapo wataendelea kudanganywa uwepo wa mapambano hewa. 

  Hivyo Kamati ya utendaji ya Kamisheni hiyo iliyokaa Desemba 27, na kupitia kanuni za mchezo huo, imemkuta Bondia Francis Cheka na makosa ya kimakubaliano na kutangaza kumfungia kujihusisha kwa namna yeyote na mchezo huo na kutakiwa kupipa faini ya shilingi laki tano (500,000).

  0 0

  Kutokana na kuendelea kushamiri kwa migogoro ya wakulima na wafugaji hapa nchini ,mbunge wa chalinze Mh Ridhiwani Kikwete ameiomba serikali kuchukua hatua stahiki ili kulinda raia wake dhidi ya migogoro hiyo...

  Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kitonga kata ya Vigwaza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, Ridhiwani amesema katika kijiji hicho kuna wafugaji ambao wameingiza mifugo kwenye ranchi pamoja na kijijini pasipo kufata taratibu za kisheria,jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwa wakulima wa kitonga,hivyo ni vema serikali ikachukua hatua stahiki juu ya jambo hilo..

  kama ilivyoandikwa kwenye vitabu vya dini kuwa ombeni nanyi mtapewa,kilio cha mbunge ridhiwani kikapokewa vyema na mkuu wa mkoa Mhandisi Ndikilo kwa kutoa siku 30 ,kwa wafugaji waliovamia maeneo ya wakulima kuondoa mifugo yao haraka iwezakanavyo,"Mlipokuja hamkugonga hodi hvyo na mnapoondoka msituulize mtaenda wapi,haiwezekani ufugaji wako mtu mmoja uwe kero kwa jamii inayokuzunguka hii si sawa"...alisema Ndikilo

  RC Ndikilo katika hatua nyingine ameagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wafugaji wote waliongiza mifugo hiyo kuondoka haraka iwezekanavyo, licha ya wafugaji katika kijiji cha kitonga kudai kuwa wana ngombe wapatao laki 5,lakini ukweli unaonesha kuwa kuna zaidi ya kiasi hicho,huku akimtaka mmoja wafugaji anayeonekana kuwa mbabe kijiji hapo aliyefahamika kwa jina moja la leki kuhakikisha anatii agizo la kuondoka ndani ya mwezi mmoja haraka iwezekanavyo..

  akionekana kuchukizwa zaidi na vitendo vya wafugaji kuwanyanyasa wakulima ndikilo amesema ni vyema wafugaji wakaelewa kuwa kila mmoja ana wajibu wa kutii sheria ili watu waishi kwa amani na upendo..

  kwaupande wake mbunge wa chalinze mara baada ya kauli ya mkuu wa mkoa akawataka wananchi wa chalinze kutoa ushirikiano kwa serikali ili kurahisisha zoezi la kuondolewa kwa mifugo iliyoiungia kinyemela..

  Wafugaji wa kwanza kuingia mkoa wa pwani waliiongia mwaka 1940 ambao walikuwa wamasai na tangu hapo ukawa mwanzo wa pwani kuwa na mifugo...
  wanakijiji cha Kitoga wakisikiliza katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akizungumza katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza 


  0 0


  0 0

  Daraja la mto wa MUHUWESI ambalo wachimbaji wadogowadogo wanafanya kazi hiyo ya kuchimba madini hali ambayo itapelekea kubomoka kwa daraja hilo

  Sehemu ambayo wachimbaji hawa wanachimba

  Baadhi ya wachimbaji(Habari na Ruvuma Tv)


  0 0

  Na Rhoda Ezekiel- Kigoma,

  KAMATI ya usalama na maadili na kamati ya siasa ya Wilaya ya Kasulu imetoa adhabu kwa Mbunge wa Viti maalumu wa Mkoa wa kigoma,Josephin Ngezabuke na madiwani sita wa Halmashauri ya mji wa Kasulu kwa tuhuma za kuchochea mgogoro wa madiwani kumpinga Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu kwamba aondolewe hafai.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari jana katibu muenezi wa Wilaya ya Kasulu Masoud Kitowe alisema kumekuwa na mgogoro Mkubwa uliodumu kwa miezi mitano wa Baadhi ya madiwani wa Act na CCM waliomuandikia barua Mkurugenzi ya kudai Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Kasulu aondolewe hafai na Chama Cha mapinduzi hakikupatiwa barua hiyo ambayo ingeweza kuwasaidia kujua chanzo cha tatizo nini.

  Alisema katika mgogoro huo madiwani wa CCm walio shiriki ni watano na kati ya hao mmoja ambaye ni Seleman diwani wa kata ya Kumnyika amepewa adhabu ya kalipio ambayo ataitumikia kwa miezi 18 kwa kosa na kushiriki kuandika barua ya kumkataa mwenyekiti wa Halmashauri hiyo wakati jambo hilo bado halijajadiliwa katika Kikao cha Chama kwamujibu sisi kama chama tulipo pata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi tuliwaita madiwani walio husika na kupewa onyo.

  Aidha kitowe alisema madiwani wanne waliojiorodhesha kwenye barua ya kushiriki kumpinga Mwenyekiti huyo kamati ya siasa pia imetoa adhabu ambayo kwa Mujibu wa Sheria za Chama cha mapinduzi hairuhusiwi kuitangaza hazarani nao watatumikia adhabu hiyo kwa miezi 12.

  Alisema Madiwani hao walipo hojiwa walikili mgogoro huo una chochewa na baadhi ya watu ambao ni Diwani wa Kata ya Murusi Steward Zinduse ambae alikuwa akigombea nafasi ya Mwenyekiyi wa halmashauri akashindwa pamoja na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Kigoma Josephini Ngezabuke nao pia wamepewa adhabu ambayo hairuhusiwi kitangazwa kwa mujibu wa sheria na barua walishapewa zinazo elezea adhabu zao.


  0 0
  MAMLAKA ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji, (EWURA), imetangaza ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia 8.5%.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlamgosi, (pichani), ongezeko hilo la bei ni kufuatia maombi ya Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), ambalo liliwasilisha maombi EWURA ya kutaka ongezeko la bei kwa asilimia 18.19, ifikapo Januari mwaka 2017.


  Akitangaza bei hizo mpya jijini Dar es Salaam, leo Mkurugenzi Mkuu huyo wa EWURA amesema, baada ya kufanya uchambuzi wa kina, Mamlaka yake imefikia uamuzi wa kuongeza asilimia 8.5 itakayoanza kutumika Januari Mosi, 2017 kutokana na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wake.


  Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) ambalo linanunua umeme wa jumla kupeleka Zanzibar limeongezewa kwa asilimia 5.7% ya bei ya umeme.

  Hata hivyo ongezeko hilo halitaathiri wateja wa majumbani ambao matumizi yao hayazidi uniti 75 kwa mwezi.


  Kundi la TIB linalohusisha viwanda vidogo, mabango na minara ya mawasiliano litakua na tozo ya mwezi ya shilingi 5,520.

  Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), linaendelea kufanya maboresho ya miundombinu ya umeme na kutekeleza miradi mipya ya kuunganisha wateja ili kuboresha huduma za umeme nchini.

  0 0


  Vero Ignatus,Arusha

  Sakata la viongozi wa Chadema na wananchi wa vijiji  vinne wilayani Karatu Mkoani Arusha wamekamatwa na polisi kwa kosa la kuchoma mashine ya kuvutia maji,kufuatia hatua za baadhi ya watu kukaidi amri ya Waziri Mkuu aliyetaka mashine hizo zote kuondolewa katika chanzo cha maji kilichokuwa na mgogoro wa muda mrefu.

  Waziri Mkuu,Kassimu Majaliwa Mnamo desemba 5 mwaka huu,alimwagiza Mkuu wa wilaya ya Karatu, Theresia Mahongo kuhakikisha kabla ya saa 12 jioni nay eye kumaliza kikao na wananchi awe ameziondoa mashine hizo zilizowekwa katika chanzo cha maji.

  Mbali ya hilo Waziri Mkuu aliagiza chanzo hicho cha maji kutunzwa na mashine zote ziwe umbali wa mita 500 na mto utunzwe kwa mita 60 tofauti na hapo hatua kali zichukuliwe.Kufuatia agizo hilo vifaa hivyo na vingine viliondolewa vyote kwa kusimamiwa na Mkuu wa wilaya Karatu mwenyewe na jeshi la polisi wilaya ya Karatu.

  Diwani wa viti maalumu Chadema kata ya Mang’ola ,Maria Patrice akizunzgumza na waandishi wa habari leo amesema kuwa baada ya agizo hilo kutekelezwa walirudi katika vikao vya jumuiya ya uongozi wa vijiji saba vya kata mbili za Mang’ola na Qaedenti kwa ajili ya kufanya maazimio ya agizo la Waziri Mkuu.

  Amesema vijiji vyote viliafiki agizo hilo na kuahidi kutunza chanzo hicho cha maji umbali wa wa mita 500 kutoka katika chanzo hicho na mita 60 kutoka kwenye mto.Patrice ameendelea kueleza kuwa maazimio hayo yalikubaliwa na viongozi na wananchi wa vijiji vyote kwani kiliagizwa na Waziri Mkuu ni msisitizo kwani katika vikao vya nyuma vya vijiji hivyo hayo yote yalikubaliwa katika vikao.

  Alisema cha kushangaza baadhi ya viongozi na madiwani kukamatwa kwani ndio waliokuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wanatii amri ya Waziri Mkuu.Diwani huyo alisema kuwa aliambiwa kuwa baadhi ya wananchi wamerudisha mashine na vifaa vingine katika chanzo hicho cha maji na kufikia hatua ya wananchi wengine kukasirishwa na kitendio hicho cha kudharau mamlaka za juu zilizoagiza.

  ‘’Baadhi ya watu waliokamatwa hawahusiki kabisa na uchomwaji wa mashine hizo kwani polisi imeamua kukamata hovyo hovyo ila mie ninachojuwa desemba 26 na 27 mwaka huu baadhi ya wananchi walialikwa kufanya usafi katika chanzo hicho na kwa kuw amaji yalikuwa yakipungua siku hadi siku’’alisema diwani huyo

  Mkazi mwingine wa Kata ya Mang’ola aliyeomba kutotajwa jina lake alisema kuwa mgogoro huo ni wa muda mrefu sana kutoka mwaka 2007 na kijiji cha Qaedenti ndio chanzo mgogoro huo kwani wamekuwa waghumu kutii maagizo ya viongozi wa juu wa serikali pindi wanapotakiwa kukaa umbali wa mita 500 kutoka katika chanzo hicho cha maji.

  ‘’wamekuwa wakileta vurugu kila mara kwa sababu ya madai kuwa chanzo hicho ni chao lakini sio kweli kwani chanzo hicho hutoa huduma ya maji kwa vijiji saba bila ya kuwa na ubaguzi wowote’’alisema mwananchi huyo

  Alisema kuchomwa kwa mashine ni kutokana na wananchi kupatwa na hasira na jazba za baadhi ya wananchi kurudisha mashine na vifaa vingine katika chanzo hicho cha maji na kudharau agizo la Waziri Mkuu.

  Wakati huo huo Mbunge wa Jimbo la Karatu ,Willy Qambalo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu ,Jubillet Manyenyo wameachiwa kwa dhamana na wametakiwa kuripoti kituo kikuu cha polisi Arusha januari 4 mwakani.Wengine waliokamatwa na bado wanahojiwa na polisi Arusha ni pamoja na diwani wa kata ya Baray ,Thomas Darabe na diwani wa kata ya Mang’ola Lazaro Emmanuel .

  Kamata kamata hiyo imewakumba wananchi wengine ambao ni pamoja na Godwin Mussa,Safari Awak,George Pius,Baridi John,Bartazar Lohay,Jafari Thiophil,Vicent Airo ,sebastian Mosses na Daniel Ninida.Wengine waliokamatwa na polisi ambao ni ndugu ni pamoja na ndugu wawili ambao ni pamoja na Charles Lameck na Chrisopher Lameck .

  Habari kutoka ndani ya jeshi la polisi zinasema kuwa baada ya kuchukuliwa maelezo kwa watuhumiwa hao 15 majalada yanapelekwa katika ofisi ya Mwansheria wa serikali kwa ajili ya kufungua kesi.  Diwani wa viti maalumu Chadema kata ya Mang’ola ,Maria Patrice aliyevaa kitenge akiwa na baadhi ya wananchi wa wilaya ya karatu leo katika kituo cha polisi mjini kati Jijini Arusha.Picha na Vero Ignatus blog.
  Baadhi ya wananchi kutoka wilaya ya karatu wakiwa nje ya kituo cha polisi mjini kati leo.Picha na Vero Ignatus Blog.

older | 1 | .... | 1482 | 1483 | (Page 1484) | 1485 | 1486 | .... | 3270 | newer