Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110031 articles
Browse latest View live

TAARIFA YA KUPOTEA KWA MTOTO DAMIAN JAMES WA KATORO MKOANI GEITA


DKT. SHEIN AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CUBA NCHINI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na mgeni wake Balozi wa Cuba katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Jorge Luis Lopez alipofika Ikulu Mjini Unguja leo kumuaga Rais kwa kumaliza muda wake wa kazi hapa Nchini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na mgeni wake Balozi wa Cuba katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Jorge Luis Lopez alipofika Ikulu Mjini Unguja leo kumuaga Rais kwa kumaliza muda wake wa kazi hapa Nchini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana na mgeni wake Balozi wa Cuba katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Jorge Luis Lopez baada ya mazungumzo yao leo alipofika Ikulu Mjini Unguja kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wake wa kazi. Picha na Ikulu.

WAZIRI MKUU AHOJI KUCHELEWESHWA KULIPWA KWA WAKULIMA WA KOROSHO

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atamuita Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho, Bw. Hassan Jarufo ili aje amueleze ni kwa nini wakulima wa zao hilo wanacheleweshewa malipo yao kinyume na maagizo ya Serikali.

Ametoa kauli hiyo leo mchana wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa mkoa wa Lndi mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo kwenye Ikulu ndogo wilayani Nachingwea. Waziri Mkuu amewasili wilayani Nachingwea akiwa njiani kuelekea Ruangwa kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.

“Niliagiza wanunuzi waje na bond (dhamana ya mauzo), waziweke benki ndipo waingizwe kwenye mnada. Kwa maana hiyo mnada ukimalizika, benki inakata fedha husika na kuingiza kwenye chama cha wakulima.”

“Hapa tatizo ni kwamba hatukusimamia vizuri zuala hili. Tulipaswa tujiridhishishe kwanza kama mnunuzi amelipa fedha benki. Tatizo la biashara hii watu wengi ni madalali, wanaangalia hali ikoje na wakibaini kuna cha juu, ndiyo anaagiza na kuamua kuja kulipa. Kama angekuwa amelipa benki, ile hela ya awali ingekatwa katika fedha ya dhamana aliyokwishaitoa,” amesisitiza.

Oktoba 16, 2016 wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja cha Sokoine wilayani Nachingwea, mkoani Lindi, Waziri Mkuu alisema alishatoa maelekezo tangu Aprili, mwaka huu kwamba wanunuzi wa korosho ni lazima watoe asilimia 25 ya malipo wanayotaka ili kuepuka tatizo la madalali kuingilia kati biashara hiyo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi na Wakuu wote wa wilaya za mkoa huo wawahimize wakulima wapande miche mipya ya korosho kwa sababu mikorosho iliyopo imezeeka na haitoi mazao ya kutosha.

“Mnatakiwa muwahimize wananchi wapande miche mipya mara tu mvua zitakapoanza ili ianze kukua wakati wakusubiria kung’oa ile ya zamani. Nimeambiwa korosho bora hazipaswi kuzidi punje 190 ili zijae kwenye kilo  moja. Ubora wa miti ya korosho ukishuka na idadi ya punje pia inapungua,” amesema.

Amesema kigezo kikuu cha ununuzi wa korosho hivi sasa ni idadi ya punje na kwa Ruangwa na Nachingwea, idadi inakuwa kubwa kwa sababu punje zake ni ndogo. “Wenzetu wa Tandahimba walipanda miche mipya tangu miaka minne iliyopita kwa hiyo sasa hivi wanavuna korosho zenye ubora,” ameongeza.

Amempongeza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba kwa uamuzi wake wa kuvunja mfuko wa wakfu wa korosho (CIDTF) na akamtaka afute mifuko kama hiyo kwenye mazao mengine kama katani, chai na kahawa kwani inafanya kazi ambazo zinaweza kufanywa na bodi za mazao hayo.

“Waziri Tizeba alishaanza na zao la pamba, sasa aende kwenye mazao mengine ili fedha ambazo watu wa mfuko huu walikuwa wakizitumia kulipana posho tu, sasa ziende kwenye bodi kuhamasisha wakulima walime zaidi na ikibidi wapewe hata mashine za kupulizia dawa,” ameongeza.

PROF. MBARAWA AKUMBUSHA KAMPUNI ZA MAWASILIANO KUJISAJILI SOKO LA HISA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amezitaka Kampuni za Mawasiliano kukamilisha taratibu za usajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam kwa kuuza asilimia 25 ya hisa zote kadri ya Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana inavyoelekeza mwishoni mwa mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Prof. Mbarawa ametaja kampuni hizo kuwa ni zile zenye leseni za mawasiliano zilizotolewa kabla ya tarehe 1 Julai 2016 kwa ajili ya Miundombinu ya Mawasiliano, Huduma za Mawasiliano, na Huduma za Matumizi.



“Watoa huduma wote wa Mawasiliano wajisajili na kuuza hisa zao kwa wananchi ndani ya mwezi wa Disemba”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Ameongeza kuwa kwa Kampuni zilizopata leseni baada ya tarehe mosi Julai, 2016 watatakiwa kutimiza sharti hilo la kisheria kwa kipindi kisichozidi miaka miwili tangu kusajiliwa.



Waziri Prof. Mbarawa amesisitiza kuwa Kampuni zitakazokiuka Sheria hiyo zitachukuliwa hatua za kisheria kupitia kifungu cha 21 (C) cha EPOCA, 2010.

Aidha, amewataka wananchi kutumia fursa hiyo kununua hisa hizo na kuwa sehemu ya wamiliki wa makampuni ya Mawasiliano ili kuongeza kipato na kushiriki katika maamuzi ya kampuni hizo.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu utekelezaji wa sheria ya EPOCA kulingana na mabadiliko yaliyofanywa katika Sheria ya Fedha No. 2 ya mwaka 2016, jijni Dar es Salaam.

Zantel watembelea wateja wao mjini Unguja

$
0
0
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania, Benoit Janin (katikati), akizungumza na  baadhi ya wateja na mawakala wa kampuni hiyo mjini Zanzibar nje ya Soko la Malindi jana, ili kupata mawazo yao juu ya ubora wa huduma na bidhaa za Zantel wazipatazo na jinsi ya kuzoboresha.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania, Benoit Janin (katikati), pamoja na baadhi ya maofisa wa kampuni hiyo wakimsikiliza mmoja wa mawakala wao, Juma Abdallah Safi (kulia), nje ya Soko la Malindi, Zanzibar  jana, walipokwenda kuwatembvelea mawakala na wateja wa kampuni hiyo ili kupata mawazo yao juu ya ubora wa huduma na bidhaa za Zantel wazipatazo na jinsi ya kuzoboresha.     
  Mkuu wa Zantel, Mohamed Khamis Baucha (kulia), akizungumza na baadhi ya wateja wao nje ya soko la Malindi, Zanzibar jana  walipokwenda kuwatembvelea mawakala na wateja wa kampuni hiyo ili kupata mawazo yao juu ya ubora wa huduma na bidhaa za Zantel wazipatazo na jinsi ya kuzoboresha.     
 Meneja Biashara Wateja wa Makampuni wa Zantel Kassongo Faraji (kulia), Ofisa Mauzo na Usambazaji, Mabuga Abdallah (wa pili kulia), wakimsikiliza mmoja wa mawakala wa Zantel mjini Zanzibar jana walipokwenda kuwatembvelea mawakala na wateja wa kampuni hiyo ili kupata mawazo yao juu ya ubora wa huduma na bidhaa za Zantel wazipatazo na jinsi ya kuzoboresha. 

SAFARI YA FARID MUSSA NCHINI HISPANIA YAIVA, KUONDOKA KESHO NCHINI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


Mshambuliaji kinda wa Azam, Farid Mussa anatarajiwa kuondoka kesho kwenda nchini Hispania kujiunga na timu yake ya Club Deportivo Tenerife baada ya safari yake kusuasua kwa muda mrefu huku ikisemekana klabu yake hiyo ikimbania kwenda kukipiga huko huku klabu yake mpya inayoshiriki ligi daraja la kwanza "segunda division" ikituma tiketi ya ndege.

Akitolea ufafanuzi suala hilo, Ofisa habari wa Azam, Jafari Iddy amesema kuwa safari ya Farid imeshakamilika na tayari vibali vyake vya kwenda kufanyia kazi vimeshapatikana na jana timu ya Tenerife imetuma tiketi ya ndege.

Iddy amesema kuwa, vibali vya kufanyia kazi nchini Hispania vilikuwa havijapatikana na ndiyo sababu iliyomfanya Farid achelewe kuondoka ila baada ya kupatikana tena kwa msaada mkubwa wa kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba.

"Tunaishukuru sana serikali kwa msaada mkubwa waliotusaidia wa kufanikisha kupatikana kwa vibali vya Farid hususani Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ambaye mara nyingi alikuwa anatuulizia tumefikia wapi pamoja na ubalozi wa Hispania nchini na kwa sasa safari imekamilika kesho saa tano usiku ataondoka kuelekea nchini Hispania kwa ajili ya kuanza kazi rasmi kwenye timu yake mpya,"amesema Iddy.

Ameweka wazi kuwa Farid anakwenda nchini Hispania kwenye timu ya Tenerife kwa mkopo baada ya fedha walizotaka kuzitoa timu hiyo kuwa ni ndogo na Azam hawakuridhika nayo kwahiyo kwakuwa bado alikuwa na nia ya kucheza soka la kulipwa hawakuwa na budi ya kumuachia aende.
Ofisa habari wa klabu ya Azam Jafari Iddy  akionesha tiketi ya ndege iliyotumwa na timu ya Tenerife kwa ajili ya safari ya kwenda nchini Hispania.
 Mshambuliaji Farid Mussa akiwa anapambana na wachezaji wa timu ya Tenerife wakati alipokwenda kwa majaribio kwenye timu hiyo.

Dk.Shein akutana na Balozi Mdogo wa Oman

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Balozi Mdogo wa Oman katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayefanyia kazi zake Zanzibar Mhe,Ahmed Bin Humoud Al Habsi, alipofika Ikulu Mjini Unguja leo kujitambulisha.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akibadilishana mawazo na Balozi Mdogo wa Oman katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayefanyia kazi zake Zanzibar Mhe,Ahmed Bin Humoud Al Habsi, baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Unguja leo kujitambulisha.Picha na Ikulu, Zanzibar.

YANGA KIBARUANI KESHO,NGOMA AREJEA MAZOEZINI

$
0
0
Kikosi cha Yanga

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Ligi kuu ya Vodacom kuendelea tena kesho katika viwanja viwili kwa kwuakutanisha Mabingwa watetezi Yanga wakikutana na Ndanda kwenye uwanja wa Taifa huku Mtibwa wakiwakaribisha Majimaji uwanja wa Manungu mjini Morogoro.

Yanga wanashuka dimbani wakikumbuka sare 1-1 dhid ya African Lyon waliyoipata mwishoni mwa wiki huku Mtibwa akiondoka na ushindi wa goli 2-0 waliopata kwa Ndanda na Majimaji wakiambulia sare na Azam.

Kocha mkuu wa Yanga, George Lwamdamina ameendelea na mazoezi na kikosi chake huku Donald Ngoma akijumuika na wenzake baada ya kuukosa mchezo uliopita akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Katika mazoezi hayo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, wachezaji wa Yanga wameonekana kujinoa vilivyo kwani wanataka ushindi kwa hali yoyote na kuweza kuwafunga Ndanda ambapo kwenye mechi ya awali walitoka sare Mkoani Mtwara.

Ila leo kikosi cha Yanga kikiwa katikati ya mazoezi, timu ya Ndanda walifika na wao kutaka kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru na kupelekea Lwandamina kusitisha mazoezi hayo na kuwaruhusu wachezaji kwenda kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao wa kesho.

Mtibwa nao wamejizatiti kushinda mchezo baada ya kutoka na ushindi ugenini dhidi ya Ndanda na wamesema kuwa raundi hii ya pili itakuwa ni ya ushindi tu kwao hawatakubali kupoteza hata mchezo mmoja.

WALIOFAULU NI LAZIMA WAENDE SEKONDARI – MAJALIWA

$
0
0
*Asema atafuatilia ajue kwa nini kuna tozo kwenye maghala ya Serikali

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitavumilia kuona mamia ya vijana waliofaulu mitihani ya darasa la saba na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza wanabaki nyumbani eti kwa kuwa hakuna madarasa ya kutosha.

“Serikali haitaridhika kuona vijana waliofaulu vizuri wanashindwa kwenda kidato cha kwanza. Halmashauri zilijua tangu mapema ni wanafunzi wanaenda shule za msingi kwa hiyo inataka kuona wote waliofaulu wanakwenda sekondari kwa asilimia 100,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo mchana wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa mkoa wa Lndi mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo kwenye Ikulu ndogo wilayani Nachingwea. Waziri Mkuu amewasili wilayani Nachingwea akiwa njiani kuelekea Ruangwa kwa mapunziko ya mwisho wa mwaka.

Amesema Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kutoa elimu ya bure kwa kila mtoto sasa iweje watoto wengine wanafaulu na wanashindwa kujiunga na elimu ya sekondari. “Tumesema elimu ni bure hakuna sababu ya kufanya wengine wasiende shule wakati azma ya Serikali ni kutoa elimu ya bure. Hakikisheni wote wanaingia katika chaguo la kwanza,” amesema.

Amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri ambazo zimefaulisha wanafunzi lakini hazina madarasa na madawati ya kutosha warudi mezani na kujipanga upya ili kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanapangwa na kuanza na wenzao katika chaguo la kwanza kwani wakisubiri chaguo la pili wanakuwa wamechelewa.

“Kama tumepokea vijana wengi kwenye udahili wa kidato cha kwanza, ni dhahiri kuwa ,tutapata Vijana wengi watakaomaliza kidato cha nne. Sote tunajua kuna agizo la kila tarafa kuwa na sekondari moja ya kidato cha tano na sita, nataka utekelezaji wa agizo hili usimamiwe kuanzia sasa.”

“Tafuteni moja kati ya shule kwenye tarafa zenu na ipandishwe hadhi kwa kuwekewa miundombinu inayotakiwa ya bwalo, jiko, mabweni, mifumo ya maji, madarasa na vyoo vya kutosha,” amesema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema atafuatilia ili abaini ni kwa nini taasisi ya maghala ya Serikali inadai tozo kwa wakulima wanaohifadhi mazao kwenye maghala hayo.

Waziri Mkuu amesema atapitia sheria ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ili kuona kama inaruhusu tozo hizo na kuangalia sheria gani inawaruhusu kutoza kodi. Alihoji inakuwaje taasisi ya Serikali inatoza tozo kwenye maghala ambayo yamejengwa na wananchi.

Akitoa mfano kuhusu ghala la Liwale, Waziri Mkuu amesema: “Kuna viagency vimeanzishwa kazi yao ni kutoza mapato tu. Inakuwaje kunakuwa na taasisi imekaa tu na kuanza kutoza tozo kwa wananchi wanaotumia facility za Serikali. Sheria ya kutoza tozo imetokana na nini na hizo zinakwenda kwa nani, je srikali imeanza kufanya biashara?,” alihoji.

“Nimepata taarifa kuwa walikuja kuzuia mazao yasitoke hadi wao walipwe, hapana huu siyo utaratibu. Ni kwa nini tuwanyang’anye fedha wale waliojenga ghala? Wao walijenga ghala kutokana na ubunifu halafu unasema unawapa sh. 7/- kwa kilo wakati wewe umetoza sh.25/- kwa kilo moja. Hapana hilo halikubaliki,” amesisitiza.

Waziri Mkuu amesema kama Serikali inaruhusu kuwepo kwa tozo hizo kwa jambo ambalo wananchi wamelibuni wenyewe, basi ilipaswa kudai kodi na hiyo kodi ilitakiwa kukusanywa na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) na siyo vinginevyo.

Waziri Mkuu amesema atafuatilia wakala mbalimbali walioanzishwa kwenye wizara kwani kuna nyingine zinafanya kazi ambazo zilistathili kufanywa na idara kwenye wizara mama.
     
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, DESEMBA 27, 2016.

MTINDO WA KPLANLONGO 'AZONTO' UNAVYOTAMBULIWA NCHINI GHANA

$
0
0

Ripota wa Globu ya Jamii.
Asili ya neno Azonto ni kutoka katika ardhi ya nchi ya Ghana ambapo ngoma ya kplanlongo ilikua ndiyo aina au stepu zake za kiuchezaji, achilia mbali Accra lakini ngoma ya kplanlongo pia huchezwa maeneo ya Tema, Nagua na  Tesha ikiwa ni maeneo ya Pwani ya nchi ya Ghana na hadi kufikia aina ya uchezaji wa kplanlongo uitwe  Azonto kwani ni neno lenye maana ya  msichana wa mtaani ambaye maisha yake sio mazuri kwa hapa kwetu Tanzania unaweza kufananisha na kitorondo na lilianza kutumika miaka ya 1900 kwa kukosoa watu waliokuwa wakipinga kuongezwa kwa shule za wasichana na kuwapeleka wasichana kwenda kusoma hivyo mtindo huo ukatumika katika kampeni za kuhamasisha ujenzi wa shule za wasichana na kuwahimiza umuhimu wa kusoma.

Utamaduni wa mwafrika kupitia makabila ya kibantu ni wa kufanana toka kaskazini hadi kusini na ziko fikra za waafrika wengine zinazo amini kuwa utamaduni wa muziki ni asili ya Afrika na kwamba mzungu aliona zeze akaenda ulaya akaboresha na kuwa gitaa, akaona malimba akaenda akaboresha ikawa kinanda achilia hilo baragumu la pembe akaenda akatengeneza saksafoni .

Afrika ilikua na muziki ila uduni wa vyombo ndiyo ukaweka sura ya kuitwa ngoma za asili,  nchini Ghana kuna makabila mengi kama ilivyokuwa hapa kwetu Tanzania na yanashiriki katika mambo mbalimbali ya kitamaduni kupitia ngoma zao na  miongoni mwa makabila hayo ni kama vile Ashanti, Fante, Akyeni, Kwahu, Ga Ewe, Mamprusi na Dangomba.

Ngoma maarufu za kiasili ni Bamaya Kplanlongo, Klama na Adowa. Sasa Mimi nataka niende na wewe katika kuifahamu hii ngoma ya Kplanlongo ambayo ndo ngoma ya vijana kama ilivyokuw huku kwetu singeli au kiduku maana ilianza kuchezwa pwani kwenye viunga vya jiji la Accra,  Kplanlongo ndiyo yenye mtindo wa kucheza wa Azonto,pia huchezwa katika matukio kama matamasha au mikutano ya kisiasa . 
Uchezaji wake unaegemea katika kuonyesha ishara  za shughuli za kila Siku za mtu kama vile kufua nguo, kupiga pasi nguo,kujiweka sawia  mfano kwa kuchana nywele, kuvaa nguo, kusali, kuendesha  shuguli mbalimbli za michezo kama kuogelea na mengineyo . Baada ya staili hiyo kuibuliwa na kupendwa nchini Ghana  na duniani kote nchi hiyo imeunda  chombo kinachoitwa Azonto Ghana Commission ambacho kazi yake ni kuwatambua wasanii  maarufu wanaotumia staili ya azonto pia kutumika kama idara ya kuinua vikundi vya asili na mtu yoyote mwenye uwezo wa wa kucheza miondoko hiyo na ndicho kinachopewa mamlaka ya kusimamia mkakati mzima wa kutumia staili ya azonto.

Pia idara hiyo inawajibu wa kuitangaza azonto kuwa asili yake ni  Ghana na wachezajj wengi hasa wa Afrika Magjaribi wanapenda kuicheza staili hiyo pale washangiliapo magoli au ushindi wa timu mfano Asamoah Gyan, Emmanuel Adebayor, Mbaraka Wakasso, Emmanuel Ayimang-badu ni kati ya wachezaji wazuri wa wa azonto. Moja kati ya vitu wanavyovipenda waghana ni pale inapotokea mchezo wa soka baina ya Ghana na Togo  bila kujali nani kapoteza kifuatacho ni ushindani wa kucheza azonto baina yao.

Hii ndo ngoma ya Kplanlongo na mtindo wake wa azonto.

ITC YA MCHEZAJI ZAHORO PAZI YAWASILI NCHINI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Sakata la mchezaji Zahoro Pazi aliyesajiliwa na timu ya Mbeya City limefikia tamati leo baada ya FC Lupopo ya Jamhuri  ya Kidemokrasia ya Kongo kutuma hati yake ya uhamisho  wa kimataifa (ITC) kwenda katika shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF).

Mbeya City walishindwa kumtumia mchezaji huyo ingawa ni mtanzania kwa kuwa hakuwa na hati ya uhamisho kutoka katika timu yake ya awali kuchelewesha kumtumia kwa mchezaji huyo.

Zahoro aliyesajiliwa katika dirisha dogo la usajili kwa sasa anaweza kuitumikia klabu yake hiyo mpya ya Jijini Mbeya baada ya ITC yake kuwasili TFF


MWENYEKITI MPYA WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI ALIPOZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI NA WATENDAJI WA TUME

Tanzania Kufungua Ofisi za Ubalozi Nchini Jamhuri ya Korea

$
0
0
Na Frank Shija – MAELEZO.

Tanzania yadhamiria kuimarisha uhusiano baina yake na Jamhuri ya Korea kwa kufungua Ofisi zake za Ubalozi Mjini Seoul, nchini Korea.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga leo jijini Dar es Salaam wakati akipokea msaada wa Dola za Kimarekani 50,000 kwa ajili ya kusaidia urejeshaji wa miundombinu iliyoharibika kutokana na Tetemeko la Ardhi lilitokea Mkoani Kagera mnamo tarehe 9 Septemba 2016.

Balozi Mahiga amesema kuwa nchi ya Jamhuri ya Korea imekuwa na uhusiano mzuri na wa muda mrefu na Tanzania ambapo kupitia uhusiano huo imekuwa ikisaidia katika mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya afya akitolea mfano Hospitali za Mloganzila na Chanika ambazo zote zimejengwa kwa ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Mahusiano la Korea (KOICA).

“Korea imekuwa na Ofisi za Ubalozi hapa nchini kwa zaidi ya miaka 25 hivyo wameona ni wakati sasa kwa Tanzania kuwa na Ofisi yake Ubalozi nchini nnchini Korea,” Alisema Balozi Mahiga.

Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Bw. Song, Geum – Young amesema kuwa msaada huo unatokana na namna ambavyo waliguswa na janga la Tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu na makazi ya wananchi.

Ameongeza kuwa msaada huo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi aliyoitoa kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu na kumpa Pole mnamo tarehe 22 Septemba mwaka huu.
Balozi Song Geum-Young pia amemhakikishia Waziri Mahiga kuwa Korea itaendeleza na kuimarisha uhusiano wake na Tanzania na kwamba itatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa hapa nchini ikiwemo ujenzi wa Daraja la Salender, Meli, Hospitali ya Mloganzila, Chanika na mingineyo.


NDUGU YETU MPOKI BUKUKU AMEPUMZISHWA KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE LEO HUKO MKOANI DODOMA

$
0
0
 Familia ya Marehemu Mpoki Bukuku, ikiwa imelizunguka Jeneza lenye mwili wake wakati wa ibada maalum ya Mazishi yake iliyofanyika mchana wa leo katika eneo la Makaburi ya familia yao, Msalato Mkoani Dodoma.
 Jeneza lenye Mwili ya Marehemu Mpoki Bukuku likishushwa kaburini wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika mchana wa leo  katika eneo la Makaburi ya familia yao, Msalato Mkoani Dodoma.
 Mjane wa Marehemu akiweka shada la maua kwenye kaburi la Mumewe.
 Mama Mzazi wa Marehemu akiweka shada la Maua
Watoto wa Marehemu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

WATU 9 WAKAMATWA KWA UDUKUZI WA TOVUTI ZA SERIKALI THAILAND

$
0
0
Kijana aliye patikana na hatia ni Natdanai Khongdee (Umri, Miaka 19, pichani juu wa pili kulia) ambapo mkuu wa polisi wa Nchi hiyo Chakthip Chaijinda, (wa tatu kushoto) alimtangaza mbele ya vyombo vya habari vya Nchi hiyo.
-----------------------------------------------------------------------------
Na Yusuph Kileo
Mswada wa sheria mtandao nchini Thailand uliwekwa mezani kujadiliwa takriban wiki kadhaa zilizo pita. Muswada huo ambao ulikua ukingoja kupitishwa kuwa sheria umepelekea kelele nyingi nchini humo ambapo wananchi wake walitaka ufanyiwe marekebisho kabla ya kuwa sheria huku wengine wakiukataa kabisa. 
Wana usalama mtandao nchini humo walijaribu kutoa ufafanuzi ambao haukuzaa matunda na hatimaye kutaka msaada kutoka kwa wanausalama mtandao wa maeneo mengine. 
Wiki mbili zilizo pita wahalifu mtandao Nchini humo walitangaza kushambulia tovuti za serikali  ili kushinikiza mamlaka kufanyia kazi marekebisho ya sheria hizo za mtandao ambazo walidai hawakukubaliana nazo – Baadae walianza kushambulia tovuti mbali mbali na kusababisha mtafaruku mkubwa. 
Tovuti ya polisi ya nchini humo (Royal Thai Police Office) ni miongoni mwa tovuti zilizoshambuliwa kimtandao ambapo ilidukuliwa na baadae kuangushwa kabisa. Kitu ambacho kilipelekea hasira kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo.

Naibu waziri mkuu na waziri wa ulinzi Mh. Prawit Wongsuwon, alitangaza kukamata washukiwa tisa (9) wa uhalifu huo mtandao pamoja  na vifaa vyao huku akiongeza  kuwa serikali ya nchi hiyo haitalinyamazia tukio hilo na kusema watachukua hatua stahiki kwa kila atakaethibitika na uhalifu huo. 
Tayari kati ya tisa (9) waliokamatwa , Kijana mdogo mmoja amepatikana na hatia huku wengine nane (8) bado wanaendelea kufanyiwa uchunguzi. 



State University of Zanzibar (SUZA) Inaugurates Its CDL and TV

MAGAZETI YA LEO JUMATANO DESEMBA 28, 2016

Mradi wa Umeme Vijijini (REA III) kufika Vijiji vyote nchini

$
0
0
Serikali imesema vijiji vyote ambavyo havikufikishiwa huduma ya nishati ya umeme vitapata huduma hiyo kupitia Mradi mkubwa wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III). 

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo katika ziara yake katika kijiji cha Kwikuba, Mkoani Mara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili (REA II) ambao unamalizika.

Katika maeneo mbalimbali aliyotembelea Waziri Muhongo alielezwa kuwa vijiji vya ndani havina umeme kwani umeme umeishia kwenye vijiji vilivyopo katika barabara kubwa na kwenye senta za biashara.

Waziri Muhongo alisema Serikali inatambua vijiji ambavyo havikufikishiwa huduma husika na hivyo aliwaasa wananchi katika vijiji hivyo kuwa na subira kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha ndani ya miaka 10 vijiji vyote nchini view vimefikiwa na umeme.

Alisema Mradi huo wa REA III umetengewa zaidi ya trilioni moja ambayo ni mara tatu zaidi ya iliyotengwa kwa Mradi wa REA II ambao unamalizika kwa kuunganisha baadhi ya vijiji.

Aliongeza kuwa sasa hivi Serikali ipo katika utaratibu wa kuwapata Wakandarasi mahiri ambao watakabidhiwa jukumu la kutekeleza mradi huo ambao alisema ni mkubwa na wa kihistoria nchini.

Aidha akizungumzia mradi huo wa REA III, Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Amos Maganga alisema mbali na kuunganisha vijiji vyote, lakini pia mradi huo umelenga kuhakikisha unamaliza mapungufu yaliyojitokeza katika REA II.

Alisema katika utekelezaji wa mradi wa REA II kuna mapungufu yaliyojitokeza kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutokuwa na wigo mpana na hivyo kusababisha baadhi ya vijiji kurukwa na vingine kutofikiwa kabisa na vilevile uhaba wa baadhi ya vifaa katika maeneo mbalimbali.

Aliwaasa wananchi ambao vijiji vyao havijafikishiwa huduma ya nishati ya umeme kuwa na subira kwani mradi mkubwa wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) hautaacha kijiji.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kwikuba kuhusiana na Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA

Baadhi ya wananchi wakiagana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) mara baada ya kumaliza kuzungumza nao
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akipokelewa na Mwenyekiti wa kijiji cha Kwikuba, Kamunyiro Kwibega.

DC HOMERA AKAGUA MICHE YA KOROSHO KWA AJILI YA MSIMU UJAO 2016/17

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mhe. Juma Zuberi Homera, jana desemba  27,2016 alikwenda CDC kujiridhisha na uandaaji wa miche za mikorosho kwa msimu mpya wa Kilimo 2016/2017 na hatimaye kuridhishwa na maandalizi ya miche ya mikorosho iko ya kutosha na itaanza kusambazwa Kwa mujibu wa utaratibu wa uendelezaji wa zao hilo.

Lakini pia ametoa maelekezo kwa maafisa elimu. alisema, "maafisa elimu wanapaswa kuhakikisha wana kwenda sambamba katika uzalishaji wa zao hili la biashara wilayani Tunduru kwa upande wa shule za msingi na sekondari kwa kuandaa hekari 5 za mikorosho kila shule maafisa kilimo, watendaji wa Kata na vijiji wanapaswa kusimamia zoezi hili na mbegu hizo watagawiwa bure kama mradi wa EK na kuhusu uzalishaji wa mbegu mwaka huu ni mzuri zaidi ukilinganisha na mwaka jana. 
Mfano, kitalu cha CDC kina miche zaidi ya 79,000, kangomba zaidi ya miche 49,000, Mbesa zaidi ya miche 25,000, Nalasi zaidi ya miche 20,000, Namasakata zaidi ya miche 20,000, Misechela zaid ya miche 25,000, Muhuwesi 15000, Majimaji zaidi ya miche 10,000, Namiungo zaidi ya miche 15,000, Nandembo zaidi ya miche 15000, na kitanda zaidi ya miche15000 kazi kwetu wanatunduru mbegu hizi za kisasa zinazaa baada ya miaka 3".

Alisisitiza, "lakini pia ni mbegu bora kuhusu minada mpaka sasa wanunuzi mnada wa 4,5,6, wameshalipa bado kuwafikishia vyama vya msingi baada ya kufanya ukokotozi "TWENDE NA MKOROSHO WANGU UCHUMI WANGU" tusisahau kupanda mazao ya Chakula kama mahindi, mpunga, mihogo nk. Tumuunge mkono Rais wetu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika kuinua kilimo nchini na chenye tija kwa wananchi wanyonge na wa hali ya chini. HAPA KAZI TU mungu ni Mwema".
 Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mhe. Juma Zuberi Homera,akiwa na baadhi ya wakulima wa Korosho 
 Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mhe. Juma Zuberi Homera,akishiriki kumwagilia miche ya zao la Korosho kwenye vitalu

Harambee ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi wilayani Bariadi

$
0
0
  Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA), Ndg.Mark Malekana akizungumza na  wananchi wa Gambosi(hawapo pichani)  wakati wa  Harambee ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi iliyofanyika jana katika kijiji cha Gambosi wilayani Bariadi.
 Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wa Gambosi (hawapo pichani) wakati wa  Harambee ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi iliyofanyika jana katika kijiji cha Gambosi wilayani Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kulia) akizungumza na wananchi wa Gambosi (hawapo pichani) wakati wa  Harambee ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi iliyofanyika jana katika kijiji cha Gambosi wilayani Bariadi.
 Kutoka kulia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) wakiwa na viongozi wengine wakati walipotembelea eneo la ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi kabla ya kufanya harambee ya ujenzi wa shule hiyo kijijini Gambosi (Bariadi).
 Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Gambosi wakienda kuchangia wakati wa Harambee ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi iliyofanyika jana katika kijijini hapo. Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

Viewing all 110031 articles
Browse latest View live




Latest Images