Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1477 | 1478 | (Page 1479) | 1480 | 1481 | .... | 3283 | newer

  0 0

  *GARI LAKO HAITAIBIWA TENA!!!*  
  *Hakuna malipo ya mwaka*. 
  Sasa unaweza kufunga Car Track kwenye gari yako na uweze kutrack kujua iko wapi, Unaweza funga eneo ambalo hutaki gari/bajaj/pikipiki  yako itoke, Unaweza kujua kama Gari yako ime Over Speed, Unaweza pia kuzima Gari yako popote na muda wowote upendao, Kukupa mahali sahihi Gari yako ilipo kupitia Ramani ya Google Map.                       

   Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi Trace It Africa Ltd 0752666614 / 0713 666616
   *Sole Distributor Mac Auto Accessories - Sinza Mori*call us 0715000890 or 0752 300300

  0 0


   Zawadi za Noeli kwa watoto wa Kituo cha Watoto cha Mama wa Rehema - Madale jijini Dar es salaam zikushushwa katika gari kabla ya kukabidhiwa
  John Bernard, kulia, akikabidhi zawadi za watoto wa Kituo cha Mama wa Rehema kwa walezi, masista wanaosimamia kituo.

   Sehemu ya watoto wanaotunzwa katika  Kituo cha Mama wa Rehema Madale
   Kina mama waliotembelea watoto wa Kituo cha Mama wa Rehema-Madale wakiwa wamewabeba baadhi ya watoto wakati wa sikuku ya Noeli.

   mmoja wa walezi wa watoto Sista Ishengoma akishukuru na kutoa neno mara baada ya kupokea zawadi ya Noeli kwa niaba ya watoto.

  0 0

   Meneja mradi wa ujenzi wa kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Mhandisi Mwanaidi Mkwizu (aliyevaa suti) akitoa melezo kwa Timu ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango.
   Timu ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeo ikiendelea na ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo ndani ya jengo la abiria.
   Mwonekano wa sehemu ya mbele wa Jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal III).
   Eneo watakapopita abiria kutoka ndani ya jengo la abiria wakielekea kupanda ndege. Habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0
 • 12/26/16--23:00: Msaada tutani: Kadudu's fund

 • Our friend Abdul-Said Yahya aka "Kadudu" is being detained by Immigration - ICE. 
  We are kindly asking for your help and your assistance in raising the funds necessary to cover his legal fees.
  We appreciate and thank you in advance for your help and support.
  Please help us spread the Word!

  0 0

  Na John Gagarini

  TAASISI ya Misaada ya Bo’s Love Childrens Home Foundation kutoka nchi ya China imetoa msaada wa kiasi cha shilingi milioni 25.2 na vyakula kwenye kituo cha kulea watoto cha Msimbazi kilichopo Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Christmass na kuukaribisha mwaka mpya wa 2017.

  Akizungumza na waandishi baada ya kukabidhi fedha na vyakula hivyo kwenye kituo hicho ikiwa ni sherehe ya uzinduzi wa taasisi hiyo mwenyekiti wa shirika hilo Bo Sun alisema kuwa wameamua kutoa msaada huo kwa ajili ya kuwafariji watoto wasiokuwa na wazazi wanaoishi kwenye kituo hicho.
  Sun alisema kuwa walitembelea na kuona jinsi gani watoto hao wanavyolelewa kwenye kituo hicho na kuona kuwa kituo hicho kinahitaji misaada ya hali na mali kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao.

  “Tumekuwa tukisaidia vituo mbalimbali vya kulea watoto na yatima na watu wanaotusaidia wamekuwa wakichanga fedha kwa ajili ya kuwasaidia ili nao wapate faraja,” alisema Sun.Aidha alisema kuwa fedha zilizotolewa ni michango ya wafanyabiashara mbalimbali wa China ambao wako hapa nchini na wameguswa na jambo hilo na kuamua kusaidia kituo hicho.

  “Kuna wawakilishi watendelea kukisaidia kituo hichi na hata maeneo mengine kwa watoto wenye mahitaji tunaomba na watu wengine wajitokeze kusaidia watoto kama hawa kwani wanahitaji upendo,” alisema Sun.

  Akishukuru kupatiwa misaada hiyo ya chakula na fedha taslimu mkuu wa kituo hicho cha kulea watoto Anna Francis alisema kuwa kituo chake kinashukuru kwa msaada huo na kuwataka watu zaidi wajitokeze kusaidia.
  Francis alisema kuwa changamoto kubwa waliyonayo ni fedha kwa ajaili ya kuwalipa mishahara watumishi 24 ambao wanawahudumia watoto waliopo kwenye kituo chake.

  “Tuna watoto 52 na tunawashukuru watu kama hawa wanaokuja kutusaidia lakini mbali ya changamoto ya fedha pia magonjwa nayo ni changamoto kubwa sana ambapo watoto wamekuwa wakiugua mara kwa mara,” alisema Francis.
   Mkuu wa kituo cha kulea watoto cha Msimbazi Sista Anna Francis akiwa amebeba mtoto akiwa na wageni waliotembelea kituo hicho na kutoa misaada ya vyakula na fedha.
   Mwenyekiti wa Taasisi ya Bo’s Bo Sun aliyemshika  mtoto wa kituo cha kulea watoto cha Msimbazi akiwa na baadhi ya wageni waliojitolea michango kwa ajili ya kukisaidia kituo hicho wakiwa katika picha ya pamoja
   Bo Sun mwenyekiti wa taasisi ya Bo’s katikati ba Sara Hong wakikabidhi fedha kwa mkuu wa kituo cha kulea watoto cha Msimbazi Anna Francis walipotembelea kituo hicho kutoa misaada ikiwemo ya chakula na fedha.
  Baadhi ya watoto wakiwa na walezi wao kwenye kituo hicho cha kulea watoto cha Msimbazi.   

  0 0

  Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wamempongeza Mbunge wao na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo ndani ya mwaka mmoja.

  Pongezi hizo zimetolewa na wananchi wa jimbo hilo wakati wa mkutano wa Tathmini ya Maendeleo na Uchumi ya jimbo uliofanyika hivi karibuni katika Kijiji cha Murangi, Musoma Vijijini na kushirikisha wananchi wa jimboni humo, madiwani, wadau wa maendeleo na watendaji wa Halmashauri husika.

  Awali akifungua mkutano huo mzee wa Kijiji cha Murangi, Musoma Vijijini, Clifford Biseko alisema wanamusoma vijini wanajivunia maendeleo yanayodhihirika kila kukicha kutokana na mchango wa mbunge huyo. Aliongeza kwamba Profesa Muhongo ni mtu sahihi kwa nafasi hiyo na kuwa hawajuti kumchagua na wanamwombea afya njema ili azidi kushirikiana nao katika kusukuma gurudumu la maendeleo jimboni humo.

  Alisema katika kipindi kifupi cha uongozi wake, wameshuhudia masuala makubwa ya maendeleo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, kilimo, sanaa na michezo. Akizungumzia suala la afya, Biseko alisema, Musoma Vijijini haikuwahi kuwa na gari hata moja la wagonjwa lakini tangu Profesa Muhongo awe Mbunge tayari jimbo hilo linayo magari manne.

  Mzee wa Kijiji cha Murangi- Musoma Vijijini, Clifford Biseko (kulia) akifungua rasmi mkutano wa kujadili uchumi na maendeleo ya Jimbo la Musoma Vijijini. Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo hilo, Profesa Sospeter Muhongo. 
  Madiwani wa Musoma Vijijini wakijitambulisha wakati wa mkutano wa Tathmini ya Maendeleo na Uchumi ya Jimbo la Musoma Vijijini. Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo hilo na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. 
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Musoma, Flora Yongolo akitambulisha watendaji mbalimbali kutoka kwenye halmashauri hiyo.


  Baadhi ya wananchi wa Musoma Vijijini waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza Mbunge wao, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).


  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation,Sandra Oswald akimkabidhi moja ya msaada Godfery Mkukuta ambaye ni mlemavu anayelelewa katika kituo cha kulelea watoto walemavu cha Siuyu Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.Msaada huo wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 15/- Msaada huo umetolewa na Vodacom Tanzania Foundation,kulia ni msimamizi wa kituo hicho Padri Tom Ray Sac.
   Meneja ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation,Sandra Oswald(kulia)akimsukuma Said Ally kwenye baiskeli yake ambaye ni mlemavu anayelelewa katika kituo cha kulelea watoto walemavu cha Siuyu Wilaya ya Ikungi mkoani Singida,alipofika kituoni hapo kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 15/- kwa niaba ya Vodacom Tanzania Foundation.
  Said Ally ambaye ni mlemavu anayelelewa katika kituo cha kulelea watoto walemavu cha Siuyu Wilaya ya Ikungi mkoani Singida(kushoto)akipokea blanketi kwa niaba ya watoto wenzake wa kituo hicho toka kwa Meneja ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation,Sandra Oswald,alipofika kituoni hapo kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali wenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 15/-kwa niaba ya Vodacom Tanzania Foundation.

  0 0


  Bwawa la kuogelea lililopo katika Hoteli ya Itungi Lodge kata ya Vingunguti jijini Dar es salaam
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala ,Omary Kumbilamoto kabla ya kuzindua bwawa la kuogelea na hoteli hiyo ya Itungi Lodge katika kata ya Vingunguti jijini Dar es salaam. 
  Naibu Meya wa Manispa ya ilala akiwa ameongozana na wajumbe wanzake kukagua sehemu ya bwawa la kuogelea lililopo katika Hoteli ya Itungi kata ya Vingunguti 
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala akikata utepe kuashiria uzinduzi wa bwawa la kuogelea na hoteli ya kitalii ya kwanza kujengwa Vingunguti 
  Mkurugenzi wa Hoteli ya Itungi Lodg,Nicholas Andrew Mwituka akizungumza katika hafla hiyo.  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe Omary Kumbilamoto amezindua hoteli mpya ya kitalii na bwawa la kwanza la kuogelea katika kata ya Vingunguti jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.

  Akizungumza na wakazi wa Vingunguti wakati wa uzinduzi wa Hoteli hiyo ya Itungi Lodge, Kumbilamoto amesema kuwa bwawa hilo ni moja ya vivutio vipya vya Vingunguti kwani ndio la kwanza tangu kuanza kuundwa kwa mji huo ambao ni maarufu kwa machinjio ya Nyama.

  “Mtu unaweza kuona kama ni kitu cha kawaida lakini ni jambo kubwa sana kwani kuanzia Kariakoo mpaka unafika Gongolamboto bwawa la kuogelea ni moja tu kwa sasa ambalo linapatikana hapa Vingunguti hivyo tunapaswa kujivuna na kumsifu muwekezaji huyu” amesema Mhe. Kumbilamoto. 

  Kwa upande wake Mkurugenzi na mmiliki wa hoteli hiyo Bw. Nicholas Andrew Mwituka amewaomba wakazi wa Vingunguti kutumia uwepo wa hoteli hiyo kama fursa ya kujiongezea kipato na ajira mpya kwa vijana wanaozunguka eneo hilo.

  Amesema kuwa wageni wote kutoka nje ya nchi ambao watakuja kununua nyumba hapo Vingunguti hawatakuwa na sababu ya kwenda kulala mbali hivyo pesa zote na huduma za kisasa watazipata hapo hapo Vingunguti.

  0 0
 • 12/27/16--00:08: KUMBUKUMBU
 •  MAREHEMU DEUSDEDITI M. GOGADI.

  Ni siku, miezi hatimaye mwaka mmoja sasa tangu ulipotangulia mbele za haki mpendwa baba yetu DEUSDEDITI M. GOGADI.
  Hatutasahau upendo, ucheshi na busara zako daima pengo lako halitazibika kamwe. Unakumbukwa  sana na mke wako Tecla Gogadi, watoto wako Jacqueline, Neema na Monica Gogadi, mkwe wako, mashemeji zako, ndugu, jamaa na marafiki.
  Mkesha wa kumuombea baba yetu utafanyika Nyumbani Kijitonyama tarehe 30/12/2016 kuanzia saa mbili na asubuhi tarehe 31/12/2016 saa 12.30 asubui tutajumuika katika ibada Takatifu  Kanisa Katoliki la Mwenge Maximilian Kolbe jijini Dar es salaam. 

  RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA NA NURU YA DAIMA IMWANGAZIE APUMZIKE KWA AMANI. AMEEN.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Wakazi zaidi ya 200 wa kata ya buguruni waridhia kumpisha muwekezaji kujenga Kiwanda kikubwa  ili kutekeleza sera ya Viwanda nchini.

  Akizungumza na Globu ya Jamii, Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto amesema kuwa wakazi hao ambao mara ya kwanza waligoma kwa hofu ya fidia wameamua kuridhia mradi huo baada ya kikao cha mkuu wa mkoa na Muwekazaji huyo.

  “Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alikaa na muwekezaji na kukubali kulipa fedha ambayo wananchi hawa wataridhika nayo hivyo ameniagiza mimi nije niunde kamati ya watu tisa ambao watawakilisha wengine katika kikao kimoja kitakacho kutanisha mkuu wa mkoa na muwekzaji huyo”amesema Kumbilamoto.

  Ameongeza kuwa katika kundi hilo la watu tisa kutakuwa mwenyekiti, katibu ,katibu msaidizi na wajumbe wengine kutoka kundi hilo la watu hao.

  Ametaja kuwa katika kutekeleza sera ya Rais John Pombe magufuli kwenda katika Tanzania ya Viwanda ni vyema kukawa na maridhiano mazuri baina ya muwekezaji na wananchi ili kupunguza migogoro isiyokuwa ya lazima.

  Ametaja kuwa pindi zoezi hilo la ulipaji wa fidia litakapo kamilika eneo hilo litaweza kujengwa kiwanda kikubwa kitakachoweza kuajiri watu zaidi ya 1000.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala akizungumza na wakazi wa Kata ya vingunguti katika kikao cha maridhiano juu ya muwekezaji kununu nyumba zao.
  Wakazi wa Vingunguti wakimsikiliza kwa Makini Naibu Meya Omary Kumbilamoto juu ya mpango wa muwekezaji huyo na maagizo kutioka kwa mkuu wa mkoa.
  Naibu meya Omary Kumbilamoto akiteta jambo na baadhi ya wakazi wa eneo hilo katika eneo ambalo nyumba zinahitaji kununuliwa.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  MCHEKESHAJI maarufu na muigizaji katika tasnia ya filamu nchini, Steven Mengele maarufu kama Steve Nyerere amewataka wasanii wa filamu nchini kuacha kujitenga na waandishi wa habari kwani wao ni watoto wa baba mmoja.

  Steve amesema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na mwandishi wa globu ya jamii juu nini kinachotakiwa kufanywa ili tasnia ya filamu iendelee.

  “kuna mahali wasanii tunachemka hasa hili lakutokuwa na mahusiano mazuri na wanahabari huku tukitambua kuwa ili kazi yako ifike haraka kwa jamii ni lazima ushirikiane na vyombo vya habari lakini hapa kwetu kuna baadhi ya wasanii wamekuwa wakiwakwepa waandishi wa habari hata katika mambo ya kawaida katika jamii” amesema Steve.

  Amesema kuwa katika ulimwengu wa leo hakuna sababu ya msanii kumkwepa mwandishi wa habari kwani wote ni watoto wa baba mmoja tatizo vyumba tofauti.

  Steve ametumia muda huo kwa kuwapongeza wanahabari licha ya kupitia mambo magumu lakini wamekuwa karibu na kila msaniii katika nchi pindi majanga yanapotokea au furaha.

  Amesema waandishi ni watu wa ajabu sana kwakuwa wao awajui kuchukia kwani hata ukimtukana yeye yupo tu na wewe atakuandika kwa mazuri au mabaya ili mradi tu jamii ijue unachokifanya.
  Amesisitiza kuwa msanii yeyote atakayejitenga na waandishi wa habari umaarufu kwake itabaki kuwa hadithi katika maisha yake ya sanaa.

  0 0

  Safari ya kuekea kilele cha Uhuru inaanza majira ya saa 5:00 usiku kwa kuianza safari kutoka Kibo Hut.
  Jua likachomoka wakati safari ikiendelea.
  Matumaini yakaanza kuonekana baada ya alama ya Gilmans Point kuanza kuonekana. Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii anaonekana mbele kushoto.
  Gilmans Point hatimaye washiriki wakafika lakini hii ni hatua ya kwanza bado hatua mbili ili kufika Uhuru Peak.
  Hatimaye safari ya siku sita ya Wanahabari na askari wa jeshi la Ulinzi ya kupanda Mlim Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika ikafika tamati. Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Na.Vero Ignatus, Arusha.

  Mwanafunzi wa kidato cha pili wa shule ya sekondari Mringa, Vanessa Josephat [16] mkazi wa Sakina jijini hapa amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi kichwani na walinzi wa kampuni ya ulinzi ya kifaru waliokuwa wakiwatoa kwa nguvu kwenye nyumba yao yenye mgogoro . 

  Tukio hilo limethibitishwa na kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha Charles Mkumbo ambaye alisema kuwa polisi inamshikilia Fabian Charles mlinzi wa kampuni ya kifaru pamoja na silaha aina ya shoot gun iliyo tumika katika tukio hilo huku majeruhi amelazwa katika hospitali ya KCMC kutokana na hali yake kuwa mbaya . 

  Kamanda mkumbo alisema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa tatu asubuhi katika eneo la sakina jijini hapa, ambapo alisema walinzi watatu wa kampuni hiyo waliokuwa wakilinda nyumba hiyo inayomilikiwa na Josephat Nehemia walitumia silaha hiyo kuwafyatulia familia inayoishi hapo ili waondoke na ndipo silaha hiyo ilipomjeruhi mwanafunzi huyo . 

  Taarifa zinaeleza kuwa December 21 mwaka huu kampuni ya udalali ya Marc Recorders Limited wakiwa na mabaunsa na watu wengine walivamia nyumba hiyo na kuwatoa nje wamiliki wa nyumba hiyo na kuondoka na vyombo vyao vya ndani wakidai nyumba hiyo imeshauzwa kwa , Thobias Ludovick Senya baada ya mmiliki kushindwa kulipa deni la shilingi million 3.7 alilokuwa akidaiwa na taasiai ya fedha Heritage. 

  Baada ya tukio hilo familia hiyo yenye watu wapatao kumi wakiwemo watoto na kichanga walianza kulala nje kando ya geti la nyumba hiyo wakipigwa na baridi kali pasipo kuwa na msaada wowote 

  Mmiliki wa nyumba hiyo Josephat Nehemia Ogaga alisema baada ya familia yake kutolewa nje wakati yeye akiwa safarini walikuja walinzi hao wa kampuni ya kifaru na kuanza kulinda na baada ya yeye kurejea alifanikiwa kuwaondoa walinzi hao na kuirejesha ndani familia yake akidai taratibu za kuuza nyumba yake hazikufuatwa ila kilichofanyika ni uhuni . 

  “Nikweli nilikuwa nadaiwa na Heritage financial shilingi milioni 3 .7 na nililipa deni na kubaki shilingi million 1.8 hivyo hatua ya kuja kuuza nyumba yangu yenye thamani shilingi million 200 kwa deni hilo ni uhuni mtupu umefanyika” alisema Nehemia 

  Hata hivyo siku moja baadae walinzi hao walirejea tena wakiwa na silaha za moto na kuanza kufyatua risasi ovyo ndani ya nyumba hiyo kwa lengo la kuwatisha familia hiyo ili waondoke ndani ya nyumba hiyo ambapo moja ya risasi ilimjeruhi mwanafunzi huyo kichwani ambaye amelazwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya matibabu 

  Kamanda Mkumbo amezitaka kampuni za ulinzi kutoingilia migogoro bila kufuata utaratibu kwani vyombo vyenye mamlaka ya kushughulikia migogoro kama hiyo vipo na hivyo amezitaka kampuni za ulinzi kufuata taratibu zao za utendaji wa kazi na kuacha kukimbilia maslahi yao ya kupata fedha haraka,

  Mkumbo alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.

  0 0

    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Lindi Godfrey Zambi mara alipowasili katika uwanja wa ndege wa Nachingwea kwa ajili ya ziara ya kikazi katika wilaya ya Ruangwa Mkoani lindi kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi  Alli Mohamed Mtopa
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mkurugenzi wa Nachingwea (DED) Bakari Mohamedi Bakari katika kiwanja cha ndege cha Nachingwea wakati wa mapokezi ya waziri mkuu wilayani hapo waziri mkuu amefika kwa ziara ya kikazi katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi 
  Waziri mkuu Kassim Majaliwa na mkewe Mery Majaliwa wakifurahia ngoma ya kikosi cha JKT  843KJ kilichopo Nachingwea ambacho kilikuwepo katika mapokezi ya Waziri Mkuu katika uwanja wa ndege wa Nachingwea .Picha na Chris Mfinanga

  0 0

  Baadhi akina Mama,familia wakiwa wameketi kuzunguka Heneza na misa ikienaendelea.
   Maziko ya Mpigapicha Mpoki Bukuku yanatarajibkufanyika leo Kijijini kwao Msalato Dodoma yalipo makazi ya mamavyake nabyalipo makaburi ya Familia likiwepo la Baba yake na kaka yake. Tayari waombolezaji wameshaanza kuwasili na taratibu za mazishi zinaendelea.
  Wamama wa Kinyakyusa wakiimba kuzunguka Jeneza la Marehemu Mpoki Bukuku.

  0 0
 • 12/27/16--02:05: WANATOKA KUTEKA MAJI
 • Kamera ya Mtaa kwa Mtaa imeinasa taswira hii ya Watoto haya wakikivuka barabara wakati wakitoka kutema maji, eneo la Kigogo Jijini Dar es salaam.

  0 0


  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi, Dkt. Augustine Mahiga akihutubia katika hafla ya makabidhiano ya mchango uliotolewa na Ubalozi wa Korea kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Kagera mwezi Septemba, 2016 na kusababisha madhara makubwa, Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere.Kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Mhe.Song Geum Young 
  Waziri Mahiha akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Dola za Marekani elf 50 (shillingi millioni 108) kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Korea, Mhe. Song.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo y Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akiratibu hafla hiyo. 
  Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hafla ya makabidhiano, Kutoka kushoto ni Bw. Halmenshi Lunyumbu, Bw. Assah Mwambene, Bw. Ally Kondo na Bw. Freddy Maro. 
  Hafla ya makabidhiano ikiendelea. 
  Picha ya pamoja.


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Serikali ya Jamhuri ya Korea imetoa msaada wa Dola za Marekani elf 50,000 takribani milioni 108 kwa fedha za Tanzania kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea mkoani Kagera mwezi Septemba 2016.

  Msaada huo ulikabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa Korea nchini Tanzania, Mhe. Song Geum Young na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb) kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb).

  Baada ya kupokea msaada huo, Dkt. Mahiga aliishukuru Serikali ya Korea na kuahidi kuwa msaada huo ataukabidhi kwa Mhe. Waziri Mkuu ili uweze kutumika kama ulivyokusudiwa.

  Mhe. Mahiga alisema kuwa Korea imekuwa mbia mkubwa wa Tanzania tokea nchi hiyo ilipoanzisha mahusiano ya kidiplomasia na Tanznaia miaka 25 iliyopita. Alieleza kuwa katika kipindi hicho Tanzania imekuwa ikipokea misaada mbalimbali ya kiuchumi, kijamii na ya kibinadamu ukiwemo huu wa leo ulioelekezwa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi la mkoani Kagera. 

  Mhe. Waziri alitaja misaada ambayo Korea imeipatia Tanzania ni pamoja na ujenzi wa daraja la Malagarasi mkoani Kigoma, ujenzi wa hospitali ya kisasa ya Mloganzila na ujenzi wa hospitali ya uchunguzi wa afya ya Mama iliyopo Chanika. Aidha, Korea hivi karibuni itaanza ujenzi wa daraja la Selander ambalo linatarajiwa kuanzia ufukwe wa Coco, Oysterbay hadi maeneo ya hospitali ya Aga Khan, Upanga jijini Dar es Salaam.

  Waziri Mahiga alibainisha pia kuwa Jamhuri ya Korea itatoa msaada mkubwa zaidi wa maendeleo kwa Tanzania kuliko nchi yeyote ya Afrika. Taarifa hiyo ilitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea, Mhe. Yun Byung-se alipofanya naye mazungumzo kando ya Mkutano wa nchi za Afrika na Korea uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia tarehe 06 na 07 Desemba 2016.

  Kwa upande wake, Balozi wa Korea nchini aliahidi kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania hususan kutoa atia misaada ya maendeleo ili iweze kutimiza azima ya Serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
  Dar es Salaam, 27 Desemba 2016.

  0 0

  Pichani ni baadhi ya Wanahabari na Wapiga picha nguli hapa nchini wakiwa katika picha ya pamoja na mchezaji bora wa soka Barani Afrika wakati huo, George Weah (wa tatu kulia) alipokuja Dar es salaam miaka hiyo. Je kuna yeyote unaweza kumtambua katika picha hii??.

  0 0

  Ujumbe wa Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete kufuatia tukio la kinyama lilimtokea Ndugu Augustino Mtitu mkulima wa kitongoji cha Upangwani, Kijiji cha Dodoma Isanga, Kata Ya Masanze Jimbo la Mikumi la kuchomwa mkuki mdomoni. ujumbe huo unaanzia hapa, Kwanza niruhusu nikupe Pole ndg yangu kwa lililokukuta. La msingi Serikali inatakiwa kujua, tunaposema na kutoa maoni yetu pale Bungeni tunamaanisha. yako mambo unaweza yafanyia utani lakini hapa tulipofika si kwa kuchukulia mzahamzaha.

  Waziri muhusika haya hauyaoni au niliposimulia juu ya Wananchi wa Jimbo la Chalinze kupigwa, kuvunjwa migongo na mwengine kupigwa mshale wa goti na kumpa Ulemavu wa Maisha mlizani natania. Sasa hili liwe fundisho. Serikali ni lazima ije na majibu sahihi juu ya kunusuru vita ya wenyewe kwa wenyewe .

  Jana mtu kavunjwa mgongo, mwengine mlemavu leo kapigwa mkuki wa mdomo umetokea shingoni. Lini tutasikia kilio hiki. Serikali sikieni kabla Damu ya Watanzania wanyonge wanaotegemea kilimo kama kiinua mgongo chao hawajapotea. Kuna sheria na mipango ya matumizi bora ya Ardhi. nini kinafichwa?

  Binafsi Nalaani Vitendo hivi na kuiasa Serikali yangu kujipanga vizuri kabla mambo hayajaharibika. yalianza Kilosa, Mvomelo, Chalinze, Handeni, Kiteto na sasa Mikumi (kutaja maeneo machache). Serikali jipangeni, kabla hapajachafuka.

  0 0

  Hatua ya Sada Almasi Shomary na mumewe Kazumari Malongo, harusi ilifanyika jijini Mwanza katika Msikiti Sheikh Amin Mtaa wa Rufiji na kufuatiwa na tafrija iliyofanyika katika Hoteli ya Gold Grest jijini Mwanza
  Bibi Harusi Sada Almasi Shomary akikata keki wakati wa mnuso uliofanyika katika Hoteli ya Gold Grest jijini Mwanza
  Bi Harusi akizungumza jambo ukumbini humo mbele ya wageni mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo
  Bwana Harsi Kazumari Malongo akimvalisha pete ya ndoa mkewe Bi' Sada Almasi Shomary na , katika tafrija iliyofanyika katika Hoteli ya Gold Grest jijini Mwanza

older | 1 | .... | 1477 | 1478 | (Page 1479) | 1480 | 1481 | .... | 3283 | newer