Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1473 | 1474 | (Page 1475) | 1476 | 1477 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Na Felix Mwagara (MOHA)

  NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amewataka vijana nchi kuwa makini na baadhi ya Mashirika yasiyokuwa ya Serikali ambayo yanajishughulisha na uhamasishaji wa mapenzi ya jinsia moja (ushoga).

  Mhandisi Masauni alisema, Mashirika hayo hayapaswi kuwepo nchini kwani yanafanya kazi kinyume na mila na desturi ya nchi yetu na yanapaswa kufutwa haraka iwezekanavyo endapo yatagundulika.

  Akizungumza katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni,  jijini Dar es Salaam, Mhandisi Masauni aliongeza kuwa, vijana wanapaswa wawe makini katika maisha yao, kamwe wasikubali kupotoshwa pamoja na kuendeshwa na kundi lolote ambalo linafanya kazi kinyume na taratibu za nchi.

  “Kuna baadhi ya mashirika ambayo yanajihusisha kwa kutoa elimu na kuhamasisha ndoa za jinsia moja, mashirika hayo yanafanya kazi kinyume na sheria ya nchi, hivyo tunayachunguza na tukiyagundua hakuna cha Mswalie Mtume, tutayafuta haraka iwezekanavyo,” alisema Masauni.

  Pia aliwataka Watanzania kutoa taarifa ya uwepo ya taasisi hizo binafsi zinazofanya shughuli hizo nchini muda wowote wakizigundua ili zifuatiliwe kwa umakini na hatimaye zifutwe haraka iwezekanavyo kwa kuwa zinaharibu jina zuri la Tanzania.

  Masauni ambaye alikuwa na Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Hamid Masoud Jongo katika sherehe hiyo, licha ya kuwashukuru waandaaji wa tukio hilo kwa kumualika, pia aliwahasa Waislam nchini wawe na umoja, wapendane na waache kulalamika kwa kuwa mafundisho ya dini hiyo yanaelekeza mambo mema ambayo kila Muislam anatakiwa kuyafuata.

   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa koti) akiwasili katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni,  jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake Masauni aliwataka vijana kuwa makini na mashirika ambayo yanahamasisha ushoga nchini, na pia alitangaza kuyafuta mashirika hayo endapo yakigundulika. Kushoto ni Shekhe wa Wilaya ya Kigamboni, Abdalla Idd na Shekhe Mohammed Mussa (aliyevaa miwani).
   
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni,  jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake Masauni aliwataka vijana kuwa makini na mashirika ambayo yanahamasisha ushoga nchini, na pia alitangaza kuyafuta mashirika hayo endapo yakigundulika. Kulia kwake ni Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Hamid Masoud Jongo.
   
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia aliyekaa) akimsikiliza Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Hamid Masoud Jongo alipokuwa akizungumza na Waislam katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni, jijini Dar es Salaam leo. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo, Mhandisi Masauni, katika hotuba yake aliwataka vijana kuwa makini na mashirika ambayo yanahamasisha ushoga nchini, na pia alitangaza kuyafuta mashirika hayo endapo yakigundulika
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia aliyekaa) na  Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Hamid Masoud Jongo (wapili kulia waliokaa) wakimsikiliza Shekhe wa Wilaya ya Kigamboni, Abdalla Idd alipokuwa akizungumza na Waislam katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni, jijini Dar es Salaam leo. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo, Mhandisi Masauni, katika hotuba yake aliwataka vijana kuwa makini na mashirika ambayo yanahamasisha ushoga nchini, na pia alitangaza kuyafuta mashirika hayo endapo yakigundulika. 
  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  0 0


  0 0

   Mpiga picha maarufu Mpoki Bukuku amefariki dunia leo katika Taasisi ya Mifupa (MOI), alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali akiwa akitokea kazini jana usiku maeneo ya Mwenge jijini Dar es salaam.

  Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kwa Umma (MOI) Almas Jumaa.

  "Ni kweli Mpoki amefariki dunia mchana huu, alipokelewa jana usiku baada ya kupata ajali ya gari maeneo ya Mwenge  ITV, taarifa zaidi tutazitoa baadaye," alisema Almas.

  Mpoki Bukuku amewahi kufanya kazi kama Mpiga Picha Mkuu katika gazeti la Mwananchi, linalochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti. Pia amewahi kufanya kazi magazeti kadhaa likiwemo Majira na Nipashe.

  MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU 
  MAHALI PEME PEPONI-AMIN

  Tumepoteza nguzo 
  katika tasnia ya habari

   Leo, kama ilivyo kwa wengine wengi, nimepokea kwa mshtuko mkubwa na kutoamini, kuhusiana na kifo cha ghafla cha mmoja wa wapigapicha waandamizi wa The Guardian Limited, Bw. Mpoki Bukuku (44), aliyefariki asubuhi kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.
  Kwa familia yake, wamempoteza baba, mume na zaidi ya yote rafiki wa kweli, lakini kwetu sisi The Guardian Limited, tumempoteza pia rafiki wa kweli na nguzo katika tasnia ya uandishi wa habari.


    Bukuku alikuwa ni mwanadamu tu kama ilivyo kwa yeyote kati yetu, lakini katika uandishi wa habari, alikuwa ni mtu aliyeipenda fani yake na hakuogopa kupambana alimradi apate habari nzuri. Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana kuna wakati kiu yake ya kupata habari nzuri kuliko wengine wote ilimuweka matatani.


  Wale wanaoelewa uandishi wa habari wa picha watabaini kwamba ujasiri na kuipenda kazi ni sifa kuu mbili za kila mpigapicha ili kupata habari nzuri na yenye nguvu. Bukuku alikuwa na sifa zote hizo mbili. Alikuwa shujaa na mwenye mapenzi na kazi yake hasa wakati akifuatilia habari kubwa kokote kule katika nchi hii.


   Alipigwa na hata kuteswa na maadui wa uhuru wa vyombo vya habari, lakini bado mahaba yake katika kufanikisha habari bora hayakuzimwa. Alikuwa ni mwandishi wa habari siyo kwa bahati mbaya, bali ni kwa kuchagua na ndiyo maana alikuwa na mapenzi wakati akitimiza wajibu wake wa kutekeleza kazi mbalimbali za kihabari alizopangiwa na wahariri wake.


  Bukuku amemaliza safari yake duniani, kimwili hayuko nasi lakini kiroho na kiuweledi, mara zote atakuwa nasi daima.


  Sisi katika Kampuni ya The Guardian Limited tunaungana na famila, ndugu na marafiki katika kippindi hiki kigumu, kuombeleza msiba wa mtu ambaye tumekuwa tukifanya naye kazi kwa miaka mingi. Kampuni itaiunga mkono kwa ukamilifu familia ya marehemu Bukuku.


  Kwa niaba ya wafanyakazi wote wa The Guardian Limited, kwa heshima kubwa natoa salamu zangu za rambirambi kwa mjane wa Bukuku, Lucy, watoto na wadau wote wa tasnia ya habari nchini Tanzania, kwa kifo cha ghafla na kushtua cha mmoja wetu.

  Richard Mgamba
  Mkurugenzi Mtendaji,
  The Guardian Limited
  Desemba 23, 2016.

  0 0


  0 0


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli wamemtembelea na kumpa pole Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kufuatia kifo cha Dada yake aitwaye Efrazia Pengo aliyefariki dunia jana tarehe 22 Desemba, 2016 katika Kijiji cha Mwazye, Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa akiwa na umri wa miaka 79. Mhe. Rais Magufuli na Mhe. Mama Janeth Magufuli wamemtembelea Kardinali Pengo katika makazi yake yaliyopo Kurasini Jijini Dar es Salaam.
   Rais Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli  wakilakiwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo walipomtembelea katika makazi yake yaliyopo Kurasini Jijini Dar es Salaam leo Desemba 23, 2016.

    Rais Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli  wakiwa na  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo walipomtembelea katika makazi yake yaliyopo Kurasini Jijini Dar es Salaam leo Desemba 23, 2016.
   Rais Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli  wakimfariji Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo walipomtembelea katika makazi yake yaliyopo Kurasini Jijini Dar es Salaam leo Desemba 23, 2016. Picha na IKULU

  0 0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 23 Desemba, 2016 amewaapisha viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Majaji wa Mahakama ya Rufani aliowateua jana tarehe 22 Desemba, 2016.

  Hafla ya kuwaapisha viongozi hao imehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjellah Kairuki, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju na Viongozi wengine mbalimbali.

  Walioapishwa ni Mhe. Mhe. Jaji Semistocles Simon Kaijage aliyeapishwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mhe. Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid aliyeapishwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Harold Reginald Nsekela aliyeapishwa kuwa Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Viongozi hawa watashika nyadhifa hizo kwa kipindi cha miaka mitano.

  Kwa upande wa Majaji walioapishwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani ni Mhe. Jaji Rehema Kiwanga Mkuye, Mhe. Jaji Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi na Mhe. Jaji Dkt. Gerald Alex Mbonimpa Ndika, Mhe. Jaji Jackobs Casthom Mwatebela Mwambegele.

  Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uturuki hapa nchini Mhe. Yesamin Eralp ambapo viongozi hao wamezungumzia uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Uturuki hususani katika masuala ya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo.

  Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli wamemtembelea na kumpa pole Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kufuatia kifo cha Dada yake aitwaye Efrazia Pengo aliyefariki dunia jana tarehe 22 Desemba, 2016 katika Kijiji cha Mwazye, Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa akiwa na umri wa miaka 79.

  Mhe. Rais Magufuli na Mhe. Mama Janeth Magufuli wamemtembelea Kardinali Pengo katika makazi yake yaliyopo Kurasini Jijini Dar es Salaam.


  Gerson Msigwa

  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

  Dar es Salaam

  23 Desemba, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Semistocles Kaijage kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) anayechukua nafasi ya Mhe. Jaji Mstaafu Damian Lubuva aliyemaliza Muda wake, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
   Mhe. Jaji Semistocles Kaijage akisaini hati ya kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa kiapo cha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ikulu Jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Mstaafu Hamid Mohamed Hamid kuwa Makamu kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapishaJaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mhe. Jaji Harold Nsekela kuwa Kamishna wa Maadili katika Sekretariat ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Rehema Kiwanga Mkuye kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Sivangilwe Sikalaliwa Mwangesi kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Mhe. Jaji Dkt. Gerald Ndika kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Jackobs Mwambegele kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  0 0


  0 0  0 0


   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiwasili katika mgodi wa Jasi uliopo katika kijiji cha Makangaga wilayani Kilwa, mkoani Lindi. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Wachimbaji Mkoa wa Lindi, Peter Ludovick.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza jambo wakati wa ziara ya ukaguzi wa shughuli za uchimbaji madini ya Jasi Mkoani Lindi. Kulia kwake ni Kwanza Kilwa Mining Products, Mwalimu Zuberi akifuatiwa na Mwenyekiti wa Wachimbaji Mkoa wa Lindi, Peter Ludovick na Makamu Mwenyekiti wa Wachimbaji Lindi, Faridu Shaweji.

   Madini ya Jasi yakiwa yamerundikwa kandokando ya barabara kuu yakisubiri soko. Takribani tani 26,000 imerundikwa hapo kwa ajili ya kurahisisha usafirishaji pindi soko linapopatikana.
   Madini ya Jasi yakiwa yamelundikwa kandokando ya barabara kuu yakisubiri soko.
   Moja ya mgodi wa madini ya Jasi ambapo uchimbaji unaendelea kutegemea na soko. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA


  0 0

  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini linawakumbusha wamiliki na waendeshaji wa kumbi za burudani kufuata sheria, kanuni na taratibu walizopewa kwenye vibali vyao vya uendeshaji wa kumbi.

  Wanaelekezwa kuhakikisha wanakuwa na vibali halali vya uendeshaji wa kumbi zao, kuzingatia muda wa matumizi wa ukumbi, kuepuka kelele zinazosumbua kwenye maeneo maalum hasa makazi ya watu na kuhakikisha ulinzi na usalama wa maisha ya watu na mali zao.  Aidha, BASATA linawakumbusha wamiliki wote wa kumbi za sherehe na burudani kwamba ni marufuku kukusanya watoto katika kumbi zao kupitia kile kinachoitwa ‘Disko Toto’ katika msimu huu wa Sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya ili kuepuka maafa yanayoweza kujitokeza.  Uzoefu unaonesha kwamba, nyakati za sikukuu kama hizi wamiliki wa kumbi wamekuwa wakijisahau na kuandaa madisko ya watoto hali mbayo imekuwa ikisababisha maafa ambayo yangeepukika kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu.  Aidha, baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa kumbi wamekuwa wakijisahau na kuendekeza faida pasi na kujali maelekezo ya vibali vyao, wamekuwa wakijaza watu kupita viwango vya madaraja waliyopangiwa na BASATA.  BASATA mamlaka inayotoa vibali vya kumbi za sherehe na burudani linasisistiza kwamba halitafumbia macho ukumbi wowote utakaokiuka maelekezo haya sambamba na kuruhusu maonesho machafu yenye kudhalilisha utu wa binadamu hasa yale yanayoonesha maungo ya ndani. Hatua kali na za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka maagizo haya.  BASATA linawatakia wasanii na wadau wote wa 
  Sanaa Heri ya Christmas na Mwaka Mpya.


  SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI

  Godfrey L. Mngereza


  KATIBU MTENDAJI, BASATA


  0 0

  Participants from EAC Partner States display their certificates after successful completion of training of trainers together with EAC DSG(in black suit and red neck tie) as well as  Mr. Fabio Gigantino, who represented the Italian Ambassador. For full report CLICK HERE

  0 0

  SIMU TV: Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro amesema watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi wakati wa msako wa waharifu; https://youtu.be/9j9MxtuOOqE

  TBC: Jeshi la polisi limekamata zaidi ya magunia miambili ya mkaa yaliyokuwa yakisafirishwa kwenda Mwanza kinyemela; https://youtu.be/EkwsUh1w_Ak

  SIMU TV: Mkuu wa wilaya ya Hai amewakamata na kuwaweka ndani maafisa wawili wa ushirika kwa kushindwa kutekeleza agazo alilowapa; https://youtu.be/8saJQ2iRZZA

  SIMU TV: Waziri wa ardhi William Lukuvi aziagiza halmashauri kanda ya kaskazini kusimamia na kulinda maeneo wanayoishi kabila la Wahadzabe; https://youtu.be/DxpnU1NPYkQ

  TBC: Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu awataka wananchi Zanzibar kuzitumia Madrasa katika malengo yaliyokusudiwa; https://youtu.be/kkvHFB4ayhA

  SIMU TV: Watu wawili wafariki dunia na wengine kulazwa kutokana na kulipuka kwa ugonjwa wa Kipindupindu mkoani Dodoma; https://youtu.be/4rmhl8dZgfg

  SIMU TV: Mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji EWURA yawasilisha mapendekezo ya bei elekezi ya gesi asilia; https://youtu.be/tTL_eC2J50c

  SIMU TV: Mjasirimali Rukia mkazi wa Kijitonyama Dar es Salaam awataka wajasiriamali kuwa wabunifu katika biashara zao; https://youtu.be/i3wKwCf5ar8

  SIMU TV: Timu ya Yanga yabanwa mbavu kwa kutoa sare ya goli moja kwa moja na timu ya African Lyon katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara; https://youtu.be/7XJGrUvzuuM

  SIMU TV: Timu ya Simba kesho itashuka katika dimba la Uhuru kukipiga na timu ya JKT Ruvu katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara; https://youtu.be/hsvr8C1aKeY

  SIMU TV: Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema awataka wananchi kupenda kushiriki katika michezo ya bahati nasibu; https://youtu.be/yrcGZ83FjUU

  SIMU TV: Msaani wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz anatarajia kutumbuiza mkoani Iringa Disemba 25 mwaka huu; https://youtu.be/3uwpCwMRK94

  SIMU TV: Rais Dkt John Magufuli amemuapisha Jaji Semistocles Kaijage kuwa mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC ; https://youtu.be/6WuBDqTy_AI

  SIMU TV:  Rais Dkt John Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wamemtembelea na kumjulia hali Kadinali Pengo ambae amefiwa na dada yake; https://youtu.be/GE7OFyeM74c

  SIMU TV:  Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage amesema chaguzi zote ndogo zitafanyika January 22. 2017 ; https://youtu.be/TKRA9mlTqbU

  SIMU TV:  Kukithiri kwa uharibifu wa mazao unaofanywa na wanyama pamoja na ukame wa kudumu vimetajwa kuwa ni sababu za kuzuka kwa njaa Mara; https://youtu.be/soYW6Eer35Q

  SIMU TV:  Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake vimezidi kuathiri maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wilayani Karatu; https://youtu.be/iRXrwGqr6Tc

  SIMU TV:  Chama cha watu wenye Ualbino leo kimeikumbusha serikali kuwaharakishia upatikanaji wa Bima kwa ajili ya kutunza afya zao; https://youtu.be/GsV7gnV9sIQ

  SIMU TV:  Serikali imeombwa kupunguza baadhi ya kodi kwa bidhaa zinazozalishwa ndani ili ziweze kushindana na zile zinazoingizwa kutoka nje; https://youtu.be/O29kWYfqkDI

  SIMU TV:  Mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji EWURA imekutana na wadau wa nishati ya gesi nchini ili kujadili bei ya elekezi ya gesi; https://youtu.be/a4hPPCksCCE


  SIMU TV:  Klabu ya soka ya Stand United imesema licha ya kupoteza mchezo wao wa kwanza bado akili zao wamezielekeza kwa Kagera Sugar; https://youtu.be/fn7-RxrPNwI

  SIMU TV:  Kocha mkuu wa klabu ya Azam amesema timu yake itafanikiwa kutinga katika hatua ya makundi baada ya kufanya mazoezi ya nguvu; https://youtu.be/1Oaiq0Xbyaw

  SIMU TV:  Timu ya taifa ya Senegal imefanikiwa kuwa kinara katika viwango vya soka duniani baada ya kushika nafasi ya 33 kidunia na namba moja Afrika; https://youtu.be/Klk9gU3CSRs

  0 0

  Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amewapatia hati miliki za Ardhi kwa jamii ya wa Hadzabe wanaoishi wilayani Karatu Mkoani Arusha.

  Waziri Lukuvi amefika katika maeneo yao na kuwapa hati miliki za kimila kwa vijiji na wanayoishi jamii ya wa Hadzabe na jamii nyingine za kifugaji ili kulinda maeneo yao ya malisho na maeneo wanayotumia kuwinda wanyama.

  Jamii ya wa Hadzabe ni watu ambao huishi kwa mfumo wa maisha ya kuwinda, kufuga wanyama pori na kula mimea na matunda ya miti inayowazunguka. Jamii hii kwa miaka mingi imekuwa ikiishi bila kufuata mipaka ya maeneo yao na hivyo kusababisha migogoro ya ardhi kwa jamii nyingine zinazoishi karibu na maeneo yao.
  Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwapatia hati miliki za Ardhi kwa jamii ya wa Hadzabe wanaoishi wilayani Karatu Mkoani Arusha.

  Pamoja na ziara hiyo Mhe. William Lukuvi amtatua migogoro ya Ardhi ya wananchi wa wilayani Karatu Mkoani Arusha na wananchi walio na kero za migogoro ya ardhi na kuzipatia ufumbuzi pamoja na kupokea vielelezo vya kero za wananchi walizoziwasilisha kwa Waziri ili azitolee maamuzi.

  Wananchi wa vijiji vya Mang’ola juu na Midabini wilayani Karatu Mkoani Arusha walisimamisha msafara wa Mhe. Lukuvi ili awasikilize kero zao za ardhi, ambapo Waziri Lukuvi alisimama na kuzitatua pamoja na kumuagiza Mkuu wa wilaya ya karatu Bibi Therezia Mahongo kutafutia ufumbuzi baadhi ya migogoro hiyo.

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi anaendelea na Ziara zake za utatuzi wa Migogoro ya Ardhi nchini, ambayo imejikita zaidi katika kutatua migogoro ya ardhi ya Mikoa ya kanda ya Magharibi, Kaskazini na ile ya Kanda ya Ziwa hapa nchini.

  Hadi sasa Mhe. Lukuvi ndani ya mwezi huu wa Desemba ameishatatua migogoro ya ardhi ya Mkoa wa Kigoma na wilaya zake za Kigoma mjini, Kasulu na Kibondo na katika Mkoa wa Shinyanga na wilaya zake za Kishapu na Shinyanga mjini na katika mkoa wa Geita amefanya ziara katika wilayani Chato.

  Pia Mhe. Lukuvi ametatua migogoro ya ardhi ya Mkoa wa Mara katika wilaya za Musoma na Bunda ambapo kwa Arusha ametatua migogoro ya wilaya ya Arumeru na Karatu.
  Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (wa nne kulia mbele) akiwasili wilayani Karatu kwa ajili ya kuwapatia hati miliki za Ardhi jamii ya wa Hadzabe.
  Wa Hadzabe wakimkaribisha Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kwa kumvusha taji.
  Wa Hadzabe wakifurahi na Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi baada ya kuwapa hati miliki za Ardhi.
  Wakazi wa kijiji cha Midabini wilayani Karatu Mkoani Arusha wakisimamisha msafara wa Mhe. Lukuvi ili awasikilize kero zao za ardhi, ambapo Waziri Lukuvi alisimama na kuzitatua.
  Wakazi wa kijiji cha Mang’ola juu wilayani Karatu Mkoani Arusha waliosimamisha msafara wa Mhe. Lukuvi wakimsikiliza wakati akitatua mgogoro wao wa Ardhi.

  0 0
  0 0
  0 0


  0 0

   Bw. Harusi Zubeir Imani akimfunua ushungi mkewe, Bi. Zawadi Mohamed baada ya kumeremeta, katika hafla iliyofanyika nymbani kwao, Mbagala Chamazi, jana Desemba 23, 2016.
   Maharusi wakikalibishwa nyumbani kwa shangwe na vigelegele.
   Bw. Harusi Zubeir Imani na mkewe, Bi. Zawadi Mohamed wakiwa na nyuso za furaha, baada ya kumeremeta.
   Bw. Harusi Zubeir Imani akishikana Mkono na Baba Mkwe wake wakati wa kufungishwa ndoa.
   Bw. Harusi Zubeir Imani akipongezwa na Baba yake, Mzee Imani Mpangule baada ya kumalizika ka ibada ya ndoa.
   Bw. Harusi akipongezwa na marafiki zake.
  Dufu zikipigwa kusherehesha shughuli hiyo.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua gwaride lililoandaliwa na Jeshi la Magereza wakati alipowasili kwenye gereza la Ukonga jijini Dar es salaam kukagua maadlizi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya Askari Magereza Desemba 24, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea heshima kutoka kwa gwaride lililoandaliwa na Jeshi la Magereza wakati alipowasili kwenye gereza la Ukonga jijini Dar es salaam kukagua maadlizi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya Askari Magereza Desemba 24, 2016.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokwenda kwenye Gereza la Ukonga kukagua maandalizi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya askari Magereza Desemba 24, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua maadalizi ya eneo la ujezi wa nyumba za askari magereza katika gereza la Ukonga jijini Dar es salaam Desemba 24, 2016. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni na kushoto kwake ni Kaimu Kamishina Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Ali Malewa.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Jeshi la Magereza baada ya kukagua maandalizi ya eneo zitakapojengwa nyumba za makazi za Askari magereza katika gereza la Ukonga jijini Dar es salaam Desemba 24, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

older | 1 | .... | 1473 | 1474 | (Page 1475) | 1476 | 1477 | .... | 3285 | newer