Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1472 | 1473 | (Page 1474) | 1475 | 1476 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amemuapisha Mhe. Kisare Matiku Makori kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Magufuli  hivi karibuni.

  Akimuapisha Mkuu huyo wa Wilaya RC Makonda ameeleza kuwa wananchi wa Ubungo wanamatumaini na uteuzi wake na lengo kuu la kuanzisha wilaya ya Ubungo ni kusogeza huduma za wananchi karibu hivyo inabidi ahakikishe anatatua changamoto zao kwa kuwafuata huko waliko na asiridhike na ripoti anazoletewa ofisini kwani kumekuwepo na changamoto kubwa ya uwajibikaji hivyo inabidi hajiridhishe kwanza.

  Katika hatua nyingine RC Makonda amewaagiza wakuu wa wilaya wote kutoruhusu wananchi kubomolewa nyumba zao mpaka kuwepo hukumu halali ya mahakama kwani wananchi wamekuwa wanaonewa na kudhulumiwa haki zao, hivyo wakuu wa wilaya kwa kushirikiana na jeshi la polisi wahakikishe haki inatendeka kwa kufuatilia ukweli na kujiridhisha kwa kuzikagua nyaraka husika.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya huyo Makori ameomba ushirikiano kwa viongozi wenzake ili aweze kutimiza majukumu yake kikamilifu na kuahidi kuwa atafanya siasa za kuleta maendeleo ili kila mwananchi anufaike na rasilimali zilizopo.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimwapicha Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Matiku Makori kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Magufuli kwa Wakuu wa Wilaya hivi karibuni. Leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
   Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Matiku Makori akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda  kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Magufuli kwa Wakuu wa Wilaya hivi karibuni. Leo jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimkabidhi katiba na ilani ya chama cha mapinguzi (CCM) Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Matiku Makori mara baada ya kumwapisha leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya wa mkoa wa Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Ubungo.

  0 0


  0 0


   
  Katibu Mkuu kiongozi Balozi John Kijazi akitangaza uteuzi wa viongozi ya Tume ya Uchaguzi, Tume ya Maadili na Majaji wa Mahakama ya Rufaa Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 22, 2016.PICHA NA IKULU  0 0

  Na Humphrey Shao,
  Globu ya Jamii.
  Kiungo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania na Simba Sports Club iliyokuwa ikiitwa Sunderland Arthur Mwambeta amewaomba wadau mbalimbali wa mchezo wa soka nchini na Chama cha Mapinduzi (CCM) kumsaidia kupata chombo cha usafiri kitakachomtoa sehemu moja mpaka nyingine baada ya kukatwa miguu yote miwili kutokana na maradhi yanayomkabili.
  Mwambeta amesema hayo  jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum na Globu ya Jamii katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam, ambako amelazwa katika jengo la Kibasila ward namba 11 baada ya kukatwa mguu Ijumaa iliyopita.

  "Nimeugua maradhi haya pindi tu nilipoacha kucheza mpira hali iliyopelekea kukatwa mguu wangu wa kwanza mwaka 2015 na mwaka huu ijumaa iliyopita ndipo nilipokatwa mguu wangu wa pili na kubaki kama hivi mnavyoniona. Siwezi tena kusogea kutoka sehemu moja kwenda nyingine kama ilivyokuwa awali...Hivyo mtu yoyote anayeweza kunisadia naomba ajitokeze " amesema Mambeta.

  Amewaomba wadau kumchangia kupitia nambari hii 0714435312 ili aweze kujikwamua katika changamoto mbalimbali za kimaisha.

  Pia alitoa wito kwa wapenzi na wanachama wa CCM kujitokeza kumsadia kwani wao ni moja ya watu waliokuwa wahamasishaji wakubwa kupitia TANU mpaka ilipozaliwa CCM wakitumia mpira kama sehemu ya hamasa.
   Wachezaji wa zamani wakiongozwa na Kitwana Manara wamekuwa wakimjulia hali Arthur Mwambeta ambaye amekatwa miguu yote miwili
  0 0
 • 12/23/16--03:27: Article 24
 •  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan (kushoto) akimkaribisha Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kulia) kwenye Ofisi za Tume zilizoko Posta jijini Dar es salaam. Mhe. Jaji Semistocles Kaijage ameapishwa leo Ikulu jijini  Dar es salaam kuiongoza Tume hiyo kwa kipindi cha miaka 5.

    Baadhi ya Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakimpokea Mwenyekiti mpya wa Tume hiyo mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Posta, jijini Dar es salaam.

    Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kulia) akiwa Ofisini kwake kwa mara ya kwanza mara baada ya kuapishwa leo. Mhe. Jaji Semistocles Kaijage ameteuliwa kuongoza Tume hiyo kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia tarehe 20 Desemba, 2016.
  Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ofisini kwake leo.


  0 0


  MBUNGE  wa   jimbo la  Chalinze Ridhiwani  Kikwete  amepongeza  jitihada   kubwa  zinazofanywa na  wataaluma  wa Halmashauri ya  Chalinze  katika  kuboresha  mradi  wa maji wa Wami  kwa ajili ya  wananchi  wa Chalinze .

  Akizungumza  baada ya  kutembelea  mradi  huo jana mbunge  Kikwete  alisema  kuwa  mradi  huo ambao  ulianzishwa na aliyekuwa  mbunge  wa jimbo   hilo  Dkt  Jakaya  Kikwete  ambae  ni rais mstaafu  wa awamu ya  nne ni  mmoja kati ya  miradi bora  iliyoleta  ukombozi mkubwa wa  upatikanaji  wa  maji safi na  salama kwa wananchi wa  mji  wa Chalinze .

  Hivyo  alisema  kusudi la  kufanya  ziara  katika eneo la mradi huo mto  Wami  ni  kuona  shughuli mbali mbali  zinazofanywa na wataalam kwa  ajili ya  kuendelea  kuboresha  mradi huo ili kuwawezesha  wananchi  wake  kupata  huduma ya  uhakika ya maji  safi  na  salama wakati  wote .

  " Mradi   huu  uliletwa na aliyekuwa  mbunge wa  jimbo la Chalinze mh Dkt  Jakaya  kikwete ni mradi ambao ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa  jimbo la Chalinze  na niwapongeze   sana wataalam  wa Halmaszhauri kwa  kazi  nzuri  wanayoifanya  ya  uboreshaji wa maradi huu" alisema  mbunge Kikwete 

  Alisema  kuwa  amefurahishwa na  jitihada  zinazoendelea  kufanywa na  wataalam  wa  Halmashauri hiyo  kuhakikisha  wananchi  wanapata  maji na  kazi kubwa yake mbunge  akiwa ni mwakilishi  wa  wananchi ni  kuendelea  kuisimamia  serikali  kwa  kuwawakilisha wananchi  wake  vema bungeni.

    Huku  akiwataka  wananchi  kuendelea  kutunza  miundo mbinu ya maji  ili  kuwezesha mradi  huo  kuendelea kuwa  msaada  kwao .

  0 0
  Na Amina Kibwana, 
  Globu ya Jamii
  Kituo cha radio cha Efm kwa kushirikiana na kampuni ya multichoice Tanzania kimekabidhi makapu yaliyosheheni bidhaa za vyakula sambamba na ving'amuzi na vifurushi vya mwezi mmoja kwa washindi 24 wa shindano la kapu la sikukuu kwa kusherehekea sikukuu ya krismas na mwaka mpya.
  Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya ilala Sophia Mjema ametoa shukrani zake kwa uongozi wa efm na Dstv pamoja na kuwaasa washindi wote waendelee kuangalia Dstv na kusikiliza efm ili waendelee kufaidika kwani kusikiliza redio kutawasaidia kujua mambo mbalimbali ya kijamii.
  "Nashukuru uongozi wa Efm na Multichoice Tanzania kwa kuonyesha kuwajali wateja wao kwani jambo kama hili ni nadra sana kutokea."

  Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya Multichoice Alfa Mria amesmea kuwa kampuni imeamua kuwatunuku washindi washindi hao ving'amuzi na vifurushi vya mwezi mzima vya Dstv ili kuwafanya wao na familia zao kusherehekea sikukuu ya krismas na mwaka mpya kwa furaha huku wakitazama Dstv.
  " Hatujawatunuku washindi wa kapu la sikukuu tu bali tumewatunukia Watanzania kwani hivi karibuni tumeshusha bei za ving'amuzi vyetu kwa silimia 16 wakati king'amuzi cha Dstv Bomba chenye chanell zaidi ya 70 kikiwa kimepunguzwa bei hivyo hii ni zawadi kwa watanzania wote."

  Shindano hili la kapu la sikukuu liliwataka wasikilizaji wa Efm kusikiliza mlio wa jingle bells uliokuwa ukizunguka kwenye vipindi tofauti kisha kutambua muda ambao mlio huo umesikika.jina la kipindi na jina la mtangazaji wa kipindi husika kilichokuwa hewani muda huo pamoja na kuangalia king'amuzi cha Dstv na kujibu maswali kutoka Multichoice Tanzania.
    Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (katikati), akimkabidhi zawadi msanii Irene Paul.
   Maelekezo ya upokeaji wa zawadi hizo yakitolewa.
   DC Mjema akizungumza na wanahabari baada ya kukabidhi zawadi hizo.
   Washindi wa shindano hilo wakiwa katika picha ya pamoja.
  KWA MAPICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mfanyabiashara maarufu nchini, Jaffar Sabodo (73), amemshauri Rais John Magufuli abadilishe fedha ili kubana wafanyabiashara wakwepa kodi na kuficha fedha majumbani.

  Aidha, amesema kutokana na utendaji wa Rais, haoni sababu za vyama vya upinzani kuendelea kumpinga, na badala yake waache siasa na waungane naye kujenga Tanzania mpya.

  Kauli ya mfanyabiashara huyo iliungwa mkono na wachumi waliozungumza na gazeti hili kubainisha kuwa njia nzuri zaidi ni Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupunguza masharti kwa benki, hasa viwango vya riba, ili riba kwenye benki iwe kubwa jambo ambalo litafanya watu wakiweka fedha benki wapate faida.

  Sabodo alitoa ushauri huo jana alipozungumza na JAMBO LEO katika mahojiano maalumu nyumbani kwake Dar es Salaam, ambapo alisema licha ya hatua nzuri za Serikali ya Rais Magufuli kiuchumi na kwenye mapambano dhidi ya rushwa, ubadhirifu na ufisadi, wapo walioficha mabilioni ya fedha nyumbani badala ya benki ili kukwepa kodi.

  “Rais anafanya kazi nzuri, lakini ni wengi walioficha fedha nyumbani. Watanzania wanakufa njaa, wengine wameficha fedha. Hapo nashauri Rais abadilishe fedha hasa noti za Sh 5,000 na Sh 10,000. Hatua hiyo itasaidia kukabili ubadhirifu unaofanywa na watu wenye nia mbaya, lakini pia inaweza kuokoa uchumi na kufikia ndoto ya kuwa na Tanzania Mpya,” alisema Sabodo.
  Mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Jaffar Sabodo akizungumza jijini Dar es Salaam, kuhusu wafanyabiashara wanaoficha fedha majumbani na kumshauri Rais John Magufuli abadilishe fedha. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA)
  Sabodo akisisitiza jambo.  0 0

                               
                                     
                                          Na Mahmoud Ahmad Arusha.

  Suala la kuachiana viti vya kugombea udiwani,ubunge  kwa umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA)bado kizungumkuti katika Kata ya Mateves wilayani Arumeru  ambapo CUF na CHADEMA wasimamisha wagombea hali inayopelekea kugawa kura za wagombea hao wa Ukawa.

  Akizungumza na wanahabari Ofisini kwake Mkurugenzi wa Uchaguzi mkoa wa CUF Arusha Zuberi Mwinyi alisema kuwa wao wamesimamisha mgombea kwenye kata hiyo kutokana na mgombea wao kukubalika kwenye kata hiyo hivyo kuwataka wenzao kuwaachia kata hiyo kwani wanazo kata nyingi kwenye maeneo hayo.

  Mwinyi alisema kuwa Tulikuwa na makubaliano ya kuachiana kata na nafasi za Ubunge lakini wenzetu vyama wenza bado wamekuwa na Tamaa ya kusimamisha wagombea kila inapotokea nafasi wemekuwa mbele kusimamisha wagombea bila kujali makubaliano hali inayopelekea sisi kama chama kuamua kusimamisha mgombea wetu eneo hilo.

  Alisema kuwa sisi kama CUF tumewaachia wenzetu wa chadema kata zote za jiji la Arusha ambapo walishinda kata 24 na moja kuangukia mikononi mwa chama cha Mapinduzi (CCM), ili hali wao wameshindwa kutuachia kata hiyo moja kama wenza na kutusaidia kuweza kuwa na mwakilishi kwenye vikao vya kutnga sera je huku ni kujenga umoja au kubomoa.

  “Tulikuwa na makubaliano ya kuachiana kata na nafasi za ubunge jambo hili limeonekana kushindikana kwa wenzetu kuwa na tamaa huku tukiwadanganya wananchi kwa wimbo wa ukawa ukawa kumbe si hivyo wenzetu wapo kimaslahi zaidi na uroho wa madaraka”alisema Mwinyi.
  Mwenyekiti mwenza wa Ukawa James Mbatia akiwa na Viongozi wa CUF mkoa wa Arusha Mwenye shati la blue ni Katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF)mkoa wa Arusha Zuberi Mwinyi baada ya mazungumzo ya ushirikiano wa ukawa Hotel ya Safari jijini Arusha picha na Maktaba.

  KUSOMA ZAIDI  BOFYA HAPA

  0 0


  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

  Kamapuni ya Uhuru Music centre kwa kushirikiana na Dege Stationary imetoa msaada wa vifaa vya shuleni na chakula vyenye thamani ya  kiasi cha fedha shilingi milioni 3 kwa ajili ya kituo cha watoto yatima wa kituo cha Amani kilichopo Kigamboni.

  Akizungumza na globu ya jamii mkurugenzi wa Uhuru Music Centre, Maneno Sanga amesema kuwa wameamua kutumia sikukuu hii kutoa zawadi kwa watoto ambao ni yatima hili nao waweze kupata maisha sawa kama watoto wengine waliopo majumbani wakiwa na wazazi wao wakati huu wa msimu wa sikukuu.

  “katika zawadi hizi tumeweza kuleta vyakula ,vitabu pamoja na nguo za shule kwaajili ya watoto ambao wanataraji kujiunga na darasa la kwanza hapo mwakani hili mlezi wao asipate tabu ya kuingia gharama ya kuwanunulia vifaa” amesema Sanga.

  Amesema kuwa alipowaza kutoa zawadi kwa watoto yatima alimpigia simu rafiki yake wa karibu mbunge wa Kigamboni ,Dk Faustine Ndugulile ndipo alipoweza kumuunganisha na kituo hicho cha Amani.

  Kwa upande wake mbunge wa Kigamboni Dk.Faustine Ndugulile, amesema kuwa anamshukuru sana bwana Sanga kwa msaada wake kwa kushirikiana na rafiki zake kwa kuona kama Kigamboni ni sehemu muhimu ya kutoa msaada huo.

  Amesema kuwa vipo vituo vingi sana na Sanga ana marafiki lakini akaona Kigamboni ndio sehemu atayopeleka zawadi hiyo kwa watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu na kuchagua kituo cha Amani kama sehemu mojawapo.
   Mkurugenzi wa kituo cha Uhuru wa Music Centre, Maneno Sanga akiwa na mkurugenzi wa Dege Stationary wakikabidhi zawadi wa watoto wanaoishi katika Mazingira Magumu katika kituo cha Amani.
   Mtoto Melvin Ndugulile akikabidhi vitabu kwa watoto wenzie wa kituo cha Amani kilichopo kigamboni.
   Mbunge wa Kigamboni ,Dk Faustine Ndugulile akibeba mzigo ambao amepeleka katika kituo hicho cha Amani


  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

   Mbunge wa jimbo la Kigamboni Dk Faustine Ndugule amemuomba Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kuangalia upya tozo za daladala zinazo pita katika daraja la kigamboni ili kutoa unafuu kwa wananchi waishio Kigamboni kama ilivyokuwa madhumuni ya kujengwa kwa daraja hilo.

  Akizungmza na globu ya jamii Dk Ndugulile amesema kuwa wananchi wamekuwa watumwa kwa usafiri kwa miaka mingi huku wakitegemea daraja liwe mkombozi wao, lakini sasa imekuwa kinyume kutokana na gharama za kupita kwa daladala katika daraja hilo.

  “gari moja yaani daladala linatakiwa kulipa shilingi 5000 kwa kila trip,jambo ambalo ni gharama kuliko biashara yenyewe ambayo ni huduma kwa wanachi hivyo kwa hesabu za haraka kama dereva atafanya trip 10 atatakiwa kulipa shilingi 50,000/- kitu hicho kinawawia vigumu kufanya kwa madereva wa daladala” amesema Dk Ndugulile.

  Amesema kuwa amefanya jitihada za kila namna kwa kuzungumza na mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF ambo wao ndio wanaendesha daraja hilo kwa kuwaandikia barua rasmi  hili waweze kupunguza tozo hizo kwa ajili ya daladala lakini bado aoni dalili.

  Ameongeza kuwa gharama za mkazi wa Kigamboni katika safari za mjini ni kubwa kuliko mtu yoyote licha ya kuwepo kwa miundombinu ya barabara na vivuko bado gharama za kifedha ni juu katika kutumia miundombinu hiyo.

  Mbunge wa jimbo la Kigamboni Dk Faustine Ndugule

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Sadiki Meck Sadiki akimsalimia na mwanafunzi Fadhili Mwidini wa shule ya Msingi Chemka iliyopo wilaya ya Hai. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe. Gelasius Byakanwa Mkuu wa mkoa alifika kukabidhi madawati pamoja na kuzindua vituo vya kunawa mikono vilivyofadhiliwa na Chuo cha Ufundi Arusha (ATC).picha zote na mahmoud ahmad wa globu ya jamii arusha
   Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) ,Dr.Richard Masika akitoa ufafanuzi juu ya vituo vya kunawa mikono vilivyofadhiliwa na chuo hicho katika shule ya Msingi Chemka iliyopo wilaya ya Hai. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Sadiki Meck Sadiki..
  Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) ,Dr.Richard Masika (wapili kutoka kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya vituo vya kunawa mikono vilivyofadhiliwa na chuo hicho katika shule ya Msingi Chemka iliyopo wilaya ya Hai,kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Sadiki Meck Sadiki. Kulia  ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe. Gelasius Byakanwa.
  Picha zote na Mahmoud Ahmad wa Globu ya Jamii  0 0

  Na Adili Mhina, Pwani.

  Tume ya Mipango imetembelea kiwanda cha vinywaji cha Azam kilichoko eneo la Mwandege Mkoani Pwani na kuonesha kuridhishwa na shughuli za uzalishaji za kiwanda hicho ikiwa ni moja ya mikakati ya kutekeleza malengo ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21) wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

  Timu ya wataalamu wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango ilifanya mazungumzo na Meneja anayesimamia ubora wa bidhaa kiwandani hapo, Bibi Lilian Mwashigadi na kuelezwa kuwa kiwanda hicho kipo katika hali nzuri na kinaendelea na shughuli za kuzalisha bidhaa zenye ubora unaotakiwa katika kukidhi mahitaji ya soko. 

  Bibi Mwashigadi alieleza kuwa kiwanda hicho ambacho kina jumla ya wafanyakazi 800 ambapo kati hao 500 ni ajira za moja kwa moja (direct labor) na 300 ni ajira zisizo za moja kwa moja (indirect labor) kina mikakati ya kuendelea kupanua soko la bidhaa zake kimataifa ambapo kwa sasa kinauza bidhaa katika nchi za Kenya na Rwanda. 

  Kuhusu upatikanaji wa matunda ya kutosheleza kiwanda hicho, Meneja huyo alieleza kuwa hakuna changamoto kwani hapa nchini kuna matunda yenye ubora unaokidhi mahitaji ya viwanda na kiwanda chake kinategemea malighafi hiyo kutoka kwa wakulima wadogo wadogo kutoka maeneo mbalimbali nchini.
   Wataalam kutoka Tume ya Mipango wakimsikiliza Meneja anayesimamia Ubora wa Bidhaa, Bibi Lilian Mwashigadi wakati wa ziara ya Tume ya Mipango katika kiwanda cha uzalishaji wa vinywaji kilichopo eneo la Mwandege Mkoani Pwani.
   Meneja anayesimamia Ubora wa Bidhaa, Lilian Mwashigadi (aliyevaa koti jeupe) akiwaonesha maofisa wa ukaguzi wa miradi kutoka Tume ya Mipango hatua za mwisho za uzalishaji wa juisi katika kiwanda cha uzalishaji wa vinywaji kilichopo eneo la Mwandege Mkoani Pwani.
   Meneja anayesimamia Ubora wa Bidhaa, Bibi Lilian Mwashigadi (mwenye koti jeupe) akionesha mtambo unaotumika katika uzalishaji katika kiwanda hicho.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack amefanya ziara katika Wilaya ya Kishapu na kukagua miradi ya maendeleo.Katika ziara hiyo Telack alikagua ujenzi wa mradi wa nyumba za walimu kata ya Kiloleli na vyoo kata za Mwamalasa, Masanga na Mwakipoya inayoendelea.

  Aliagiza miradi hiyo iwe imekamilika kabla ya Desemba 31 mwaka huu huku akionya tabia ya wakandarasi kuchelewesha miradi ya maendeleo wakati tayari wamekwisha lipwa fedha.“Nataka kuona miradi hii imekamilika na tunajua agizo hili lilishatolewa na Waziri wa TAMISEMI siku nyingi, wahandisi hamieni site kuhakikisha miradi inakamilika,” alisema Telack.

  Aidha, mkuu huyo wa mkoa katika ziara hiyo ya siku moja akiwa ameambatana na wataalamu kutoka halmashauri ya wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya aliwataka waendelee kusimamia miradi ya maendeleo.Kwa upande mwingine alikemea utoro mashuleni huku akiagiza wazazi wasiopeleka watoto shule ifikapao Januari wakamatwe na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

  Alisema kuwa kwa sasa Serikali inaendelea na utaratibu wa kutoa elimu bure hivyo ni lazima wazazi wapeleke watoto shule kupata elimu na baadaye kulisaidia taifa.“Nakuagiza mkuu wa shule hakikisha wanafunzi wote wanafika shule, hosteli ipo sasa kwanini wanafunzi hawafiki shule kwa hiyo nakupa kazi hiyo,” alisisitiza.

   Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto) akikagua mojawapo ya nyumba za walimu zinazojengwa katika Shule ya Sekondari Mwamashele wilayani humo.
   Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (mbele) akitembelea mifugo ya mmoja wa wafugaji wilayani humo wakati wa ziara yake.
   Mhandisi wa Ujenzi Wilaya ya Kishapu, Samson Pamphil (kushoto) akitoa maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa vyoo katika Kata ya Mwamamalasa kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack. Katikati ni Diwani wa kata hiyo, Justine Sheka.
   Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (katikati) akizungumza na watendaji alipofika Kata ya Mwamalasa wakati wa ziara yake. Wengine pichani wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya  Kishapu, Nyabaganga Taraba, Diwani wa kata hiyo, Justine Sheka na  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Joseph Swalala.


  0 0

  Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ofisini kwake jijini Dar es salaam  leo mara tu baada ya kuapishwa Ikulu.
  Na Antony John, Globu ya Jamii

   Chama cha Wananchi Cuf kimethibitisha kushiriki uchaguzi mdogo ujao wa jimbo la Dimani visiwani humo.

  Aizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage, amesema kuwa chama hicho kitawakilishwa na mgombea wake Abdulrazak Khatibu Ramadhani katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Dimani.

  “Wagombea wengine ni Hamadi Mussa, ACT Wazalendo, Abdala Kombo khamis, chauma.Abdulazak Khatibu cuf Peter A. Magwira DP, Ali khamis Abdalla NRA. Sau Amour haji ali,SAU. TLP Pandu Haji Punda, UMD,Abdullsamad Salum Ali, UPDP,Bakari Omar.

  Sambamba na hayo kaijage amesema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 31(1) b cha sheria ya Taifa ya uchaguzi sura ya 343 na kifungu cha 41( 1) vya sheria ya uchaguzi ya serikali yamitaa sura ya 292, tume imefanya uteuzi kwa wagombea wa ubunge na udiwani katika kata mbalimbali

  Aidha  ameongeza kuwa  jumla ya vyama vyenye wagombea kwa jimbo la dimani Zanzibar  ni 11 walioteuliwa kugombea ni 11 ambao wote ni wanaume kwa upande wa udiwani katika halmashauri 20 za Tanzania bara, vyama vyenye wagombea ni 13 jumla ya wagombea wa nafasi udiwani ni 72 kati ya wagombea hao wanawake ni 5 na wanaume ni67, hadi sasa pingamizi zilizokatwa ni sita ambapo tano ambapo tano zimekatwa  kwenye kata ya ihumwa manispaa ya Dodoma na moja katika kata ya isegehe halmashauri ya mjini wa klahama.

  Aliongeza kuwa kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi, kampeni zinaanza tarehe 23/12/2016  hadi 21/1/2016 ambapo  kamati za maadili zitaundwa katika ngazi mbali mbali na zitakuwa na jukumu la kusimamia utekelezaji wa maadili katika kipindi chote cha kampeni.

  0 0

  Waziri wa Habari Utalii, Utamaduni na Michezo Mhe. Rashid Ali Juma amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) 
  Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Wizara hiyo Bw. Ameir Abdallah Ameir imesema walioteuliwa ni pamoja na Hassan Ali Hassan na Kombo Shaame Kai. 
  Wengine ni Aziza Saleh Mohammed, Ramadhan Omar Mohamed na Nassor Rajab Dachi. Taarifa hiyo imefahamisha kuwa uteuzi wa Wajumbe hao umeanza Disemba 23, 2016.

  0 0


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Yassemin Eralp  walipokutana kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 23, 20176
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika picha ya kumbukumbu na  Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Yasemin  Eralp walipokutana kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 23, 20176.Wengine kutoka kushoto ni Balozi zuhura Bundala, Balozi Joseph Sokoine na Bw. Hassan Mwamweta wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa.PICHA NA IKULU

  0 0


  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wazazi na walezi wa Tanzania Zanzibar waache tabia ya kuwaoza wasichana wa kike wakiwa na umri mdogo bali wawasomeshe kwa ajili ya manufaa yao ya jamii kwa ujumla.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati akizindua madrasa ya kisasa iliyojengwa kwenye eneo la Kilimani na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na ujenzi wa msikiti mkubwa kuliko yote nchini Tanzania unaojengwa katika eneo la Jitimai kidoti katika Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa michango ya wananchi katika siku yake ya kwanza ya ziara ya Kikazi Kisiwani Unguja.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kama wazazi na walezi watasomesha watoto wa kike elimu watakayopata itasaidia kwa kiasi kikubwa wasichana hao kufanya maamuzi sahihi na yenye tija katika jamii.

  Amesisitiza kuwa pamoja na elimu kuwa ni haki ya msingi kwa mtoto wa kike hivyo ni muhimu kwa jamii nzima ya Zanzibar ihakikishe watoto wa kike wote wanapata elimu kwani watakuwa na uwezo wa kuchagua na kuandaa mustakbali wa maisha yao ya baadaye ikilinganishwa na hali ilivyo sasa kwenye baadhi ya maeneo.

  Kuhusu elimu ya dini, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahimiza wazazi na walezi kuwalea watoto katika maadili mema kwa kuzingatia maandiko matakatifu ya Mtume Mohammad (S.A.W).

  Amesema vijana wengi wanaolelewa kwa kufuata misingi ya bora ya dini ni vigumu kurubuniwa na kujiingiza katika matendo yasiyofaa katika jamii.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiweka jiwe la msingi katika ufunguzi wa Madrasa ya Al-Madrasatul Munawwaratul Islamiyyah ya KilimaninTazari Zanzibar ikiwa sehemu ya ziara yake ya mkoa wa Kaskazini Unguja. 


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia wakazi wa Sheihiya ya Kilimani waliojitokeza kwa wingi kwenye ufunguzi wa Madrasa ya Al-Madrasatul Munawwaratul Islamiyyah ya KilimaninTazari Zanzibar ikiwa sehemu ya ziara yake ya mkoa wa Kaskazini Unguja. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akishiriki dua maalum mara baada ya zoezi la ufunguzi wa Madrasa ya Al-Madrasatul Munawwaratul Islamiyyah ya KilimaninTazari Zanzibar kukamilika ikiwa sehemu ya ziara yake ya mkoa wa Kaskazini Unguja.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ramani ya msikiti mkubwa unaojengwa kwa nguvu za wananchi alipotembelea Uwanja wa Jitimai uliopo Kidoti mkoa wa Kaskazini Unguja.  


  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

older | 1 | .... | 1472 | 1473 | (Page 1474) | 1475 | 1476 | .... | 3278 | newer