Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1471 | 1472 | (Page 1473) | 1474 | 1475 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Kivuko kilichopo katika Bandari ya Kilwa Masoko ambacho hakitumiki mara kwa mara ambapo wanachi hutumia boti zinazotoza nauli ya shilingi 1,000.

  Na Adili Mhina, Kilwa.
  Mamlaka ya Bandari imeshauriwa kuiangalia bandari ndogo ya Kilwa Masoko katika kuboresha miundombinu na vitendea kazi ili kuongeza ufanisi wa shughuli bandari hapo ikiwa ni njia mojawapo ya kuweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara nchini. 

  Ushauri huo umetolewa hivi karibuni na Kaimu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri alipoiongoza timu ya wataalamu wa ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango kukagua shughuli za maendeleo katika bandari hiyo.

  Katika ziara hiyo, Mwanri alionesha kutoridhishwa na utendaji kazi wa bandari hiyo baada ya kubaini kuwa hakuna tishari wala  vifaa vinavyoweza kutumika katika kupakia na kupakua mizigo huku akielezwa kuwa mfanyabiashara anapoleta meli banadarini hapo analazimika kutafuta vifaa vya kupakulia mizigo yake mwenyewe. 
  Mhandisi Omari Athuman (mwenye shati ya Mikono mirefu) akimuonesha jambo Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Florence Mwanri juu ya Bandari ndogo ya Kilwa Masoko.

  “Bandari hii ni fursa kubwa kiuchumi haipaswi kuwa katika hii wakati Serikali ya sasa inajitahidi kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara. Hivyo, ni muhimu kwa Mamlaka ya Bandari kupitia bajeti yao kuangalia  uwezekano wa kupata vifaa hivyo ili kuondoa usumbufu na gharama kwa wafanyabiashara wanaotumia bandari hii,” alisema.

  Alieleza kuwa kwa sasa bandari hiyo inaweza kufanya vizuri na kuwa na uwezo wa kujiendesha yenyewe kama mazingira yake yataboreshwa kwa kuwa shughuli za usafirishaji zinaweza kuchangamka baada ya kiwanda cha saruji kujengwa eneo hilo huku kiwanda cha mbolea na kiwanda cha kuchakata  mihogo vikitarajiwa kujengwa Kilwa. 

  Alieleza kuwa uwekezaji katika eneo hilo ni muhimu kwani bandari hiyo pia inatumika kusafirisha watalii kutoka ndani na nje ya nchi  kutokana na kuwepo vivutio mbalimbali vya utalii katika Wilaya ya Kilwa.
  Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akiulizia juu ya utendaji kazi wa kivuko (hakipo pichani) wakati wa ziara ya Tume ya Mipango katika Bandari ndogo ya ya Kilwa masoko.

  Hata hivyo, Mwanri alisisitiza kuwa kabla ya kufanya uwekezaji mkubwa bandarini hapo ni lazima ufanyike upembuzi yakinifu ili kuwa na taarifa za kisayansi juu ya aina ya uwekezaji unaohitajika. Utafiti wa soko pia unahitajika kuweza kubaini fursa za kibiashara zinazoweza kupatikana ikiwa uwekezaji mkubwa utafanyika. 


  0 0

    Na Amina Kibwana-Globu ya Jamii.
  Kampuni ya Multichoice Tanzania imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vevye thamani ya shilingi milioni 5 kwenye kituo cha watoto yatima cha Al Madina kilichopo Tandale kwa tumbo, kwa ajili ya mahitaji ya sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya.

  Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Maharage Chande amesema kuwa wanaushirikiano wa muda mrefu na kituo hicho, ndio maana wameamua kuja kuleta zawadi mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia katika sikukuu pamoja na kuwalipia kodi ya nyumba wanayoishi.

  “Leo tunatoa vyombo vipya vya kulia chakula,nguo, vyakula pamoja na sare za wanafunzi 50 kwa ajili ya watoto ambao ni wanafunzi”

  Kwa upande wake mlezi wa watoto katika kituo hicho Kurutumu Yusuph ameeleza baadhi ya changamoto zinazowakabili katika kituo hicho ni pamoja ulipaji kodi ya nyumba, sare za shule pamoja na ada.

  Hata hivyo Kurutumu alitoa shukrani zake kwa Multichoice Tanzania kwa kushirikiana nao kwa kipondi kirefu na kuwapatia msaada pale wanapohitaji ili kukidhi changamoto zinazowakabili..

  "Ni kweli dstv wanatusaidia kwa mambo mengi hivyo tunawashukuru sana na tunamuomba M/mungu awape moyo wa kuendelea kutusaidia" amesema kuruthumu.

  Kituo cha watoto yatima cha Al Madina kina jumla ya watoto 61, wasichana 25 na wavulana 36 kimeanza kupata msaada kutoka katika Kampuni ya Multichoice Tanzania tangu mwaka 2009 hadi sasa ambapo mnamo mwezi wa sita mwaka huu kituo kilipelekewa cherehani 5 kwa ajili ya kujipatia kipato.


  Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (kushoto), akimkabidhi sare za shule mama mlezi wa kituo hicho, Kuluthum Yusuf.
  Bwana Chande akimkabidhi mlezi wa kituo hicho mafuta ya kula. Wengine ni wafanyakazi wa Multichoice Tanzania na watatu kushoto ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Alpha Joseph.

  Mlezi wa kituo hicho, Kuluthum Yusuf (kushoto), akimuonesha nguo zinazotengenezwa na kituo hicho kupitia mradi wao wa ushonaji ambao kwa kiasi kikubwa umetokana na msaada kutoka katika kampuni hiyo ya Multichoice Tanzania.Picha na Dotto Mwaibale.  Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (kulia), akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo. Kushoto ni mama mlezi wa kituo hicho, Kuluthum Yusuf.


  0 0

   Wakazi wa kijiji cha Kibamba kilichopo Kata ya Mipeko wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega Kwa kushiriki katika ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho ikiwa ni sehemu ya ahadi Yake.

  Pia amesema mapema mwezi uliopita Mbunge huyo alitembelea kijiji chao nakukuta changamoto kubwa ya huduma ya Afya hivyo alitoa ahadi Kwao kwamba atahakikisha Zahanati inajengwa kijijini hapo.

  Akizungumza kijijini hapo jana kwa niaba ya wananchi wezake mkazi Sharrifa Mkumbo alisema kuwa Ulega anaonesha kwamba yeye ni Kiongozi wa watu kwani anastahili kupongezwa.

  "Tunashukuru sana kwakweli Baba huyu Mungu aendelee kumlinda kwani tunaamini siku chache zijazo tunakwenda kupata suluhisho la Afya katika kijiji chetu."alisema Sharrifa.

  Naye Mwenyekiti wa Kijiji hicho Salum Mlango aliwaeleza wananchi kuwa Mbunge wanayo na zaidi ni kuendelea kutoa ushirikiano kwake nakudai kuwa alihaidi kushiriki msingi wa ujenzi wa Zahanati hiyo na leo ametimiza.

  "Ndugu waandishi kama mnavyoona wenyewe wananchi wamehamasika na leo Mbunge amekuja mwenyewe kushiriki nasi."alisema .
   
   Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kibamba katika Ujenzi wa Zahanati katika Kijiji hicho Wilayani Mkuranga
   Mbunge wa Mkuranga Bw Abdallah Hamisi Ulega Akishiriki katika Ujenzi huo wa Zahanati katika Kijiji cha Kibamba Wilayani Mkuranga.
   Akiongea na Mmoja Wa Wanakijiji cha Kibamba kuhusiana na Ujenz huo wa Zahanati kijijini hapo
    Mbunge wa Mkuranga Bw Abdallah Hamisi Ulega Akishiriki kubeba matofali kwa ajili ya Ujenzi huo wa Zahanati katika Kijiji cha Kibamba Wilayani Mkuranga.
   Akiongea na Mmoja Wa Wanakijiji cha Kibamba kuhusiana na Ujenz huo wa Zahanati kijijini hapo  0 0

   Mkurugenzi wa Manispaa Magharibi A Said Juma Ahmada akikusanya mchanga Barabara ijulikanayo kama Mkapa Rood kuashiria uzinduzi wa usafi wa Barabara za Manispaa hiyo.
    Wanakikundi wa Kikundi cha Mwera Hawai (TUSIJITENGE) wakifanya usafi wa Barabara ya Mkapa katika siku ya uzinduzi wa usafishaji Barabara za Manispaa ya Magharibi A.
    Mkurugenzi wa Manispaa Magharibi A Said Juma Ahmada na wanakikundi cha “Tusijitenge”wakizoa mchanga na kupakia katika Gari la kuzolea taka.
   Wanakikundi cha Usafishaji cha Kijichi wakifanya usafi Barabara ya Kibweni Manispaa ya Magharibi A katika zoezi la kuzifanyia usafi barabara za Manispaa ya Magharibi A.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  TANROADS Mkoa wa Kagera inasimamiwa na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kagera Eng. Andrew. L. Kasamwa. Mkoa wa Kagera una barabara zenye urefu wa km 1917.59 kati ya km 7505.42 zilizo mkoa wa Kagera. Kati ya hizo km 862.88 ni Barabara Kuu na km 1052.71 ni Barabara za mkoa.

  Afisa Habari wa TANROADS Bi. Aisha Malima amemtembelea Meneja wa TANROADS Kagera leo tarehe 22. 12. 2016 kuangalia utekelezaji wa ujenzi wa barabara za TANROADS mkoani Kagera. Moja ya mradi waliotembelea ni Kyaka – Bugene – Kasulo Lot1: sehemu ya Kyaka – Bugene yenye km 59.1 inayojengwa kwa kiwango cha lami. 

   Aidha barabara hii itakuwa na daraja moja, box makalavati 11 na makalavati ya pipe 132 na inafadhiliwa kwa asilimia mia moja na Serikali ya Tanzania. Mhandisi Mshauri akiwa TECU na kazi ya ukandarasi utekelezwa na Kampuni ya CHICO.

  Katika taarifa fupi ya Meneja wa TANROADS Kagera amesema “Hadi sasa barabara hii imekamilika kwa asilimia 97.2 ambayo ni km 57 na sasa bado kama km 2 tu ili mradi ukamilike na tunatarajia kukamilika Februari 2017”.

  Aidha meneja aliongeza kwa kusema “Hali ya barabara ziliyo chini ya TANROADS mkoa wa Kagera zipo katika hali nzuri na wastani na barabara moja tu ya Rusumo – Lusahunga ambayo imeisha muda wake wa matumizi ndiyo iko katika hali mbaya. Hata hivyo katika mwaka huu wa fedha 2016/17 tumetengewa fedha kiasi cha shilling billion 5 ili kuifanyia matengenezo kwa sehemu zilizo katika hali mbaya zaidi ili iendelee kupitika kwa usalaama huku tukisubiri ukarabati mkubwa”.

  Katika ziara hii Bi. Aisha Malima aliomba wananchi wa mkoa wa Kagera wakiwemo madereva walinde miundombinu ya barabara na samani za barabarani kwani zinajengwa kwa fedha nyingi za kodi zetu. Aliongeza kwa kusema “Kumekuwa na uharibifu wa barabara ambapo madereva kumwaga mafuta barabarani, kupiga jeki katika barabara za lami, kugonga nguzo za madaraja , kuiba alama za barabarani na makalavati ya chuma n.k.”
  Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kagera Eng. Andrew Kasamwa (katikati) akipewa taarifa mradi wa Kyaka – Bugene (km 59.1) kutoka kwa Kaimu Mhandisi Mshauri – Eng. Hatibu Kapombe (TECU). Pamoja katika mkutano ni Bi. Aisha Malima – Afisa Habari TANROADS na Wakandarasi CHICO.
  Bi. Aisha Malima Afisa Habari wa TANROADS akisalimiana na Mhandisi Mshauri wa Mradi wa Kyaka – Bugene (km 59.10) Eng. Hatibu Kapombe.
  Kazi ya ujenzi wa barabara zikiendelea katika mradi wa Kyaka – Bugene eneo la Kishoju escarpment.
  Meneja wa TANROADS Kagera Eng. Andrew Kasamwa (kushoto) akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kyaka – Bugene eneo la Kishoju Escarpment.
  Daraja la Mwisa lililokamilika katika barabara ya Kyaka – Bugene.  0 0


  VIUNGA vya ukumbi wa Aroma mjini Moshi vimesheheni akinamama wengi katika siku hii ya Jumamosi, kama ilivyo kawaida kwa siku kama hiyo, ambapo wote wanaonekana kuwa na nyuso za furaha kutokana na mijadala inayoendelea. 

  Lakini tofauti na Jumamosi nyingine ambapo akinamama wa kikundi cha Wamama wa Kahawa ambao ni wanachama wa Tanzania Women Coffee Association - TAWOCA mjini humo kujadili masuala mbalimbali ya ujasiriamali, siku hii inaonekana kuwa ya tofauti kwa sababu licha ya idadi ya akinamama kuongezeka, lakini kuna tukio kubwa na muhimu ambalo limewakutanisha. 

  "Leo tunazindua rasmi jiko la umeme-jua, yaani parabolic solar cooker, ambalo kupitia udhamini wa mradi wa akinamama wa Green Voices, hatimaye limeweza kupatikana baada ya jithada za miezi kadhaa," ndivyo anavyoanza kuelezea Farida Makame, mshiriki kiongozi wa mradi wa Green Voices wa kikundi hicho, huku akionyesha kifaa kinachofanana na dish kama la satellite ambacho katikati yake kumewekwa sufuria inayong’aa kama taa kubwa ya umeme. 

  Anasema kwamba, jiko hilo linaweza kupika kila aina ya chakula kwa kutumia mionzi ya jua ya moja kwa moja bila kuathiri mazingira. "Kwa kutumia jiko hili maana yake huhitaji kutafuta mkaa wala kuni, hivyo kuokoa misitu ambayo inateketea kila siku kutokana na ukataji wa miti kwa ajili ya kutafuta nishati ya kupikia," anaongeza. 

  Mgeni rasmi katika uzinduzi wa jiko la umeme-jua, Robert George, ambaye ni Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Moshi, akisikiliza maelezo ya namna jiko hilo linavyofanya kazi kutoka kwa Mkurugenzi wa Uhawilishaji Teknolojia wa Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini – CAMARTEC, Mhandisi Noela Byabachwezi. Kushoto kwa Noela ni mshiriki kiongozi wa mradi wa Green Voices Moshi, Farida Makame. Wengine pichani ni washiriki wa kikundi hicho. Uzinduzi wa jiko hilo lililotengenezwa na CAMARTEC kwa ufadhili wa Green Voices ulifanyika hivi karibuni mjini Moshi. 
  Jiko la umeme-jua ambalo limetengenezwa na CAMARTEC kwa ufadhili wa mradi wa Green Voices Tanzania kwa ajili ya kikundi cha akinamama wa TAWOCA Moshi. Jiko hilo linafaa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na uharibifu wa mazingira. 
  Wanakikundi wa TAWOCA Green Voices Moshi wakihakikisha jinsi joto la jua linavyosaidia kupika kwa kutumia jiko la umeme-jua. Kushoto ni mgeni rasmi katika uzinduzi wa jiko hilo, Robert George, ambaye ni Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Moshi. 
  Mgeni rasmi katika uzinduzi wa jiko la umeme-jua, Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Moshi, Robert George, pamoja na akinamama wakisikiliza maelezo ya namna jiko hilo linavyofanya kazi kutoka kwa Mkurugenzi wa Uhawilishaji Teknolojia wa Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini – CAMARTEC, Mhandisi Noela Byabachwezi. 


  0 0  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

  Hali ya usafiri imeendelea kuwa tete katika kituo kikuu cha mabasi  Ubungo kutokana kuwepo kwa uhaba wa usafiri kwa wasafiri wanaokwenda mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania na Nyanda za juu kusini.

  Globu ya jamii ilifika katika kituo hicho cha mabasi na kujionea ni jinsi gani wasafiri wakipata taabu ya kupata mabasi,licha ya mammlaka ya usafirishaji majini na nchi kavu (SUMATRA) kuomba wenye magari yenye vigezo kufika katika kituo hicho kwa ajili ya kupewa kibali cha kusafirisha abiria mikoani.

  Akizungumza na globu ya Jamii,Mwananchi mmoja wa wasafiri anayekwenda Rombo mkoani Moshi, Elikunda Towo, amesema kuwa walikuwa wakihitaji usafiri tangu jana lakini wamekosa .

  "Magari yaliyopo hapa yanagoma kupakia abiria yakisema kuwa ni mabovu na hawana uhakika wa safari ,hivyo hawawezi kupakia lakini ghafla unaona basi limejaa na linaondoka, sasa tunajiuliza hizo basi abiria wanapakilia kwa staili ipi,huku Sumatra wakiwa wamejazana hapa katika kituo cha mabasi" anasema huku akihoji abiria huyo .

  Ameongeza kuwa ni vyema serikali ikandeleza umakini katika kusimamia magari hayo,ili abiria waweze kusafiri kwa uhakika kuliko ilivyo hivi sasa.ambapo  kundi kubwa la abiria likiwa linakaa hapo Kituoni Ubungo bila mafanikio yoyote ya kupata usafiri.

  Abiria mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Jamila Mwampulule amesema  kuwa walifanikiwa kukata tiketi katika basi la Rungwe, lakini ilivyofika asubuhi wakajikuta wanarudishiwa nauli kwa kuambiwa basi loa ni bovu huku kukiwa hakuna usafiri mwingine mbadala wa kwenda Mbeya.
    
  Mmoja wa abiraia aliyekosa usafiri katika kituo cha mabasi Ubungo akiwa amekaa chini na mtoto wak mara baada ya kuchoka na kadhia ya kukosa usafiri.

  Abiria waliokosa usafiri wakiwa kando ya kituo cha Polisi. Usalama barabarani wakisubiri kupewa huduma
  Sehemu ya kituo cha mabasi Ubungo ikionekana kwa juu majira ya saa mbili asubuhi huku abiria wakiwa wengi kuliko magari
  Abiria wakiingia katika daladala,inayofanya safari zake Gongolamboto na Simu 2000 likiwa katika kituo kikuu cha mabasi ubungo likipakianabria wa kwenda mkoa wa Kilimanjaro.


  0 0


  0 0

    Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa  akiwa ambebebelea zawadi waliyoipata ya sekta ya benki ndogo na kati kwa ubora wa uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2015, pamoja na viongozi wengine wa benki hiyo.

  Na Zainab Nyamka, 
  Globu ya Jamii
  BENKI ya DCB yaibuka kidedea kwa kupata zawadi ya kwanza kwa sekta ya benki ndogo na kati kwa ubora wa uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2015.
  Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa amesema kuwa hii ni tuzo inayoandaliwa kila mwaka na bvodi ya uhasibu Tanzania (NBAA) ambapo yalianza toka mwaka 2011.

   Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa akizungumza na waandishi wa habari juu ya zawadi waliyoipata kwenye sekta ya benki ndogo na kati kwa ubora wa uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2015.

  Mkwawa amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne benki ya DCB imeweza kufanya vizuri kwa kushika nafasi tatu za juu na kuwa moja ya miongoni mwa benki zinazofanya vizuri na  katika uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za hesabu na kwa mwaka 2015 imeweza kushika namba moja.

  Amesema kuwa benki yao inafuata miongozo ya utawala bora na kuwataka wawekezaji kuwa na imani juu ya usalama wa fedha zao walizoziwekeza na kuahidi kuendeleza mafanikio hayo kiujumla.

     Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa akionyesha kifaa kitakachokuwa kinatumiwa na mawakala wa benki hiyo katika mfumo utakaoenda wa DCB PESA unaotarajiwa kuanza Januari 2017.

  Mkwawa ameweka wazi mafanikio ya benki hiyoikiwemo ni kutimiza miaka 14 ya utoaji huduma bora za kibenki kwa wajasiliamali, kuongezeka kwa matawi kutoka mawili mwaka 2005 hadi matawi tisa 2016 na mwakani 2017 wanatarajia kufungua tawi la 10 mkoani Dodoma.

  Mafanikio hayo ni pamoja na kuwa na mtaji imara wa bilioni 32 na upanuaji na uboreshaji wa huduma za kisasa kwa wateja wetu kupitia mawakal ambapo watawezesha wateja kupata huduma mbalimbali za kibenki kupitia mawakala walioidhinishwa na DCB katika vitongoji kwa kupitia DCB PESA inayotarajiwa kuanza Januri 2017.
  Mawakala wa DCB wakiwa makini kusikiliza.

  0 0

   LIGI kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea tena kesho  Ijumaa kwa mchezo  Na. 129 utakaozikutanisha timu za African Lyon na Young Africans kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam  utakaochezeshwa na Mwamuzi, Ludovic Charles kutoka mkoani Tabora akisaidiwa na John Kanyenye wa Mbeya (Mshika Kibendera Na. 1) na Alnord Bugado wa Singida (Mshika Kibendera Na. 2), Mwamuzi wa Akiba – Mezani anatarajiwa kuwa Israel Nkongo kutoka Dar es Salaam.

  Jumamosi Desemba 24, 2016 kutakuwa na mechi sita ya Mbeya City na Toto African kwenye Uwanja wa Sokoine jijiji Mbeya katika mchezo Na. 130 utakaosimamiwa na Kamishna George Komba wa Dodoma wakati Mwamzi wa kati atakuwa Shakaile ole Shangalai wa Pwani huku wasaidizi wake wakiwa ni Khalfan Sika pia wa Pwani na Vecent Milabu wa Morogoro. Mwamuzi wa akiba atakuwa Cherles Mwamlima.

  Mchezo Na. 131 utazikutanisha timu za Kagera Sugar na Stand United katika Uwanja wa Kaitaba, uliko Kagera ambako utasimamiwa na Kamishna Nassoroi Hamduni wa Kigoma huku Mwamuzi akiwa ni Jacob Adongo wa Mara akisaidiwa na Joseph Masija na Robert Luhemeja kutoka Mwanza na Mezani atakuwa Jonesia Rukyaa wa Kagera.

  Ndanda itaendelea kubaki nyumbani kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara na baada ya kucheza na Simba juma lililopita na kupoteza mchezo huo, safari hii inaikaribisha Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo Na. 132 utakaosimamiwa na Kamishna Jimmy Lengwe wa Morogoro wakati Mwamuzi atakuwa Andrew Shamba wa Pwani akisaidiwa na Haji Mwalukuta wa Tanga na Jeremiah Simon wa Dar es Salaam. Mezani atakuwa Abubakar Mtulo.

   Mchezo Na. 133 utafanyika Uwanja wa Uhuru, kati ya
   Simba na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam 
  utasimamiwa na Tito Haule wa Morogoro na kuchezeshwa na Mwamuzi Hans Mabena wa Tanga akisaidiwa na Omari Kambangwa wa Dar es Salaam na Khalfan Sika wa Pwani wakati Mbaraka Rashid wa Dar es Salaam atakuwa Mwamuzi wa Akiba – mezani.


  0 0


  Na Zainab Nyamka, 
  Globu ya Jamii.

  MSANII wa kizazi kipya Baraka Da Prince kwa pamoja na Mwigizaji maarufu wa Bongo Movie, Rose Ndauka wamesema kuwa wamejiandaa vema kumsindikiza Mchekeshaji maarufu nchini , Emanuel 

  Matebe a.k.a Mc Pilipili katika Tamasha la Chrismass la kids Festival litakalofanyika mkoani Dodoma katika viwanja vya Nyerere Square Desemba 25 na 26 mwaka huu. Wasanii hao pia Desemba 26 mwaka huu watatoa burudani nyingine kama hiyo katika ukumbi wa royal village na kuwapa fursa watu wa Dodoma kupiga picha na Tuzo aliyoipata Mc.Pilipili ya Mshereheshaji bora wa mwaka 2016. 

  Akizungumza hivi karibuni na Ripota wa Globu hii,Muigizaji nguli Rose Ndauka alisema kuwa tamasha hilo litakuwa la kipekee katika mkoa wa Dodoma ambapo ataweza kupanda jukwaani pamoja na Mchekeshaji huyo na kutoa burudani ya aina yake. 

  Alisema pia ataamua kuongea ukweli juu ya uhusiano wake na Mc Pilipili katika tamasha hilo kwani  watu wengi wamekuwa wakiandika katika mitandao mbalimbali ya kijamii juu ya ukaribu waliokuwa   nao. "Nataka kuwaambia watu wangu wa Dodoma kule kwa kina Mc.Pilipili mkae tayari kwa ujio wangu kwani siku hiyo ndio itakuwa siku yangu maalum ya kupanda jukwaani na Mc.Pilipili katika  kuhakikisha nina wavunja mbavu mashabiki zangu pia naombeni mjitokeze kwa wingi kuitikisa siku hiyo kwenye mji Dodoma na viunga vyake,"alisema 

  Kwa Upande wake Emanuel Matebe a.k.a Mc Pilipili alisema tamasha hilo litakuwa ni tamasha la aina yake kwani litawakutanisha wasanii mbalimbali nchini wa muziki wa kizazi kipya pamoja na waigizaji wakiwemo Baraka da Price,Rose Ndauka ,Katarina Karatu pamoja na Casto . 

  Alisema katika tamasha hilo Decemba 25 mwaka huu watoto wataweza kuingia kwa kiingilio cha shilingi 2000 huku wakubwa sh.5000 huku katika tamasha la Desemba 26,kutakuwa na kiingilio cha VIP ikiwa 30000 na kawaida 10000. 

  "Nawakaribisha ndugu zangu wa Dodoma katika matukio haya mawili siku hiyo itakuwa siku ya pekee kwangu kuonyesha kipaji changu nyumbani hivyo nitahakikisha nawatendea haki ipasavyo  huku nikirudisha tuzo ya Mshereheshaji bora nyumbani niliyopewa katika tuzo za Insta Award  ambayo mashabiki zangu watapata fursa ya kupiga nayo picha,"alisema


  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea fedha taslimu sh. milioni 10 kutoka Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) zikiwa ni msaada kwa ajili ya watu waliopatwa na maafa kutokana na tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

  Makabidhiano ya mchango huo yamefanyika leo mchana (Alhamisi, Oktoba 22, 2016) kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

  Akikabidhi mchango huo, Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT, Dk. Brown Mwakipesile amesema kanisa hilo limeona lina wajibu wa kuisadia Serikali kuwapunguzia machungu watu waliopatwa na maafa kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 17.

  “Tumeona ni vema kanisa la EAGT lishiriki kuisadia Serikali kuwafariji wananchi waliopata maafa kutokana na tetemeko hilo. Tumeona ni wajibu wetu kwa sababu waliopatwa na maafa ni watu wetu wote. Tunawaombea wote waliopatwa na shida waweze kupata nafuu mapema zaidi,” amesema.

  Askofu Mkuu Dk. Brown ametumia fursa hiyo kuipongeza Serikali kwa kusimamia vema suala hilo tangu lilipotokea hadi sasa na kuongeza kuwa wanamuomba Mwenyezi Mungu awape nguvu viongozi wa Serikali ya awamu ya tano ili waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo.

  “Ukiacha hili la tetemeko, tumeona jinsi Serikali ilivyosimamia vizuri suala la madawati hadi sasa kuna baadhi ya maeneo wamevuka hadi malengo. Tunamshukuru Mheshimiwa Rais Magufuli na Serikali nzima kwa kusimamia jambo hilo vizuri,” amesema.

  Amesema kanisa hilo linatoa shukrani nyingi kwa Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa jitihada zinazofanywa na Serikali yake kukabili mambo mbalimbali yanayowagusa wananchi walio wengi.

  Akitoa shukrani kwa Baba Askofu Mwakipesile na viongozi wa kanisa hilo aliombatana nao, Waziri Mkuu ameahidi kuwa Serikali itahakikisha michango hiyo inafikishwa Kagera kwa walengwa. “Nawashukuru sana kwa jinsi mlivyoguswa na kuamua kuwachangia wenzetu waliopatwa na maafa, tutahakikisha inawafikia walengwa,” amesema.

  Waziri Mkuu amesema anawashukuru sana viongozi wa dini zote kwa jinsi wanavyoisadia Serikali kuwahudumia wananchi kupitia sekta mbalimbali. “Tunatambua juhudi zinazofanywa na taasisi za dini zote kuunga mkono juhudi za Serikali, tunafarijika mno na tunawashukuru sana,” ameongeza.

  Amemuomba Askofu huyo pamoja na viongozi wengine wa dini wawaombee kwa Mungu viongozi waliopo madarakani ili awape hekima na busara na awawezeshe kuwaongoza vema Watanzania.

  Tetemeko hilo la ardhi liliharibu miundombinu ya barabara, shule, zahanati na kujeruhi watu 440. Pia lilisababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi na 9,471 zikipata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.
                              

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,

  S. L. P. 3021,
  11410 - DAR ES SALAAM
  ALHAMISI, DESEMBA 22, 2016.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea msaada wa shilingi milioni 10 kutoka   Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT,  Dkt. Brown  Mwakipesele  ukiwa ni mchango  wa kanisa hilo kwa  waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye makazi yake , Oysterbay jijini Dar es salaam Desemba 22, 2016. Katikati ni Mchungaji Pray God Mgonja wa kanisa hilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa kanisa la EAGT,  Dkt. Brown Mwakipesile kabla ya kupokea msada wa shilingi milioni 10 uliotolewa na kanisa hilo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika  kwenye makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 22, 2016. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT, Dkt.  Brown Mwakipesile kabla ya kupokea msaada wa Shilingi milioni 10 ukiwa ni mchango wa kanisa hilo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam, Desemba 22., 2016.

  0 0


  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  Jeshi la polisi limesema limeimarisha ulinzi kuelekea sikukuu za  Kristimasi na mwaka mpya hili kudhibiti vitendo vya uharifu .
  Akizungunza leo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba amesema jeshi la polisi katika kipindi cha sikukuu kuna watu wanajipanga kufanya uhalifu hivyo jeshi la polisi litafanya doria za kutosha.
  Amesema kumbi zote zinazofanya starehe za kupiga mziki ziingize watu kutokana na ukumbi na watakaozidisha watachukuliwa hatua.
  Afande Advera amesema wataondesha vyombo vya moto wataobainika  wametumia vilevi watachukuliwa kwani nia yao  nikutaka kusababisha ajali.
  Aidha amesema wazazi wanatakiwa kufanya ulinzi kwa watoto wao kutokana na watoto kupotea katika siku za sikuu na kusababisha vituo vya polisi kuwepo kwa watoto hao.
  Hata hivyo amesema  wananchi watoe ushirikiano kwa jeshi la polisi pale wanapohisi kuna watu wanaashiria kufanya uhalifu.
   Advera amesema kuwa wale ambao watatoa taarifa zikashindwa kutekelezeka wawasiliane na ngazi ya juu ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa watu waliofanya uzembe.
  Msemaji wa Jeshi la Polisi, 
  Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba


  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto (pichani) ameagiza kufungwa kwa ukumbi maarufu wa Starehe ujulikanao kwa jina la Kwetu Pazuri Tabata jijini Dar es salaam kwa kushindwa kukidhi vigezo.
  Akizungumza na Globu ya Jamii mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku mbili  Mhe. KumbilaMoto amesema kuwa wameamua kufunga ukumbi huo mara baada ya kufanya na ukaguzi na kujiridhisha kuwa haijakidhi vigezo.

  "Tumefanya ukaguzi na kumchukua Meneja wa Bar hiyo na kumfikisha kituo cha Polisi Ukonga Stakishari kwa ajili ya kufunguliwa mashataka na baadae kufikishwa mahakamani"amesema Kumbilamoto.

  Amesema kuwa mara baada ya kutoka katika kituo hicho ,alifikishwa kituo cha Polisi kati na kukubali kulipa faini ya Milioni mbili na kukukiri makosa ya kufanya kazi ya Night Club bila kuwa na leseni huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
  Aidha tumewaonya juu ya tabia yao ya kupanga viti karibu na barabara jambo ambalo ni kinyume cha sheria za Tanroads, " hivyo  tumeamua tuifunge mpaka hapo watakapo jipanga upya",Kumbi la Moto amesema na kuongeza kuwa kwa muda mrefu watu walikuwa wakilalamika juu ya sehemu hiyo lakini hatua zilikuwa zinachelewa kuchukuliwa, hivyo nimefika katika eneo la tukio na kujionea hali halisi na kuamua kuifunga Bar hiyo.

  Aidha katika ziara hiyo pia amekagua ujenzi wa maabara ya Zahanati ya kata ya vingunguti ambayo inatarajia kukamilika hivi karibuni.

  0 0


  0 0

   Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania Standard Newspapers (TSN) wachapaji wa magazeti ya Daily News, Sunday News, Habarileo, Habarileo Jumapili na Spotileo imeadhimisha miaka 10 tangu kuanza kwa gazeti la Habarileo mnamo Desemba 21, 2006 kwa kukata keki huku Uongozi wa Kampuni hiyo ukitangaza shamra shamra za mwezi mmoja wa kusherehekea kuzaliwa kwa gazeti hilo.
  Aidha ili kushirikiana na wadau wengine, Kampuni imetangaza punguzo la asilimia 30 kwa mteja atakeatangaza tangazo lake ndani ya siku 30 za shamrashamra katika gazeti la Habarileo.
   Miongoni mwa wageni maalum waliohudhuria sherehe hizo ni Mhariri Mtendaji wa zamani wa Tanzania Standard Newspapers (TSN), Isack Mruma (wapili kulia) ambaye kwa sasa ni Ofisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambaye alishiriki kukata keki pamoja na Mhariri Mtendaji wa sasa Dk Jim Yonaz (wapili kushoto) na Naibu Mharidi Mtendaji, Tuma Abdallah. Kushoto akishuhudia ni Meneja Mauzo na Masoko, Januarius Maganga. 
   Isack Mruma akizungumza katika shamra shamra hizo na kuelezea changamoto mbalimbali alizokumbana nazo tangu kuanza kwa gazeti hilo.
   Wafanyakazi wa TSN wakifuatailia


  0 0  0 0


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Mstaafu,Salum Kijuu (katikati) akiwa katika picha ya pampja na Uongozi wa PRIDE Tanzania, ulioongozwa na Meneja wake wa Kanda ya Ziwa, Bi. Hilda Nsombo (wa tatu kulia) baada ya zoezi la upokeaji wa misaada mbalimbali kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera hivi katibuni. Wengine ni Meneja wa PRIDE tawi la Bukoba, Afisa wa PRIDE tawi la Bukoba pamoja na viongozi wa wateja wa PRIDE tawi la Bukoba.
  Meneja wa Pride Kanda ya Ziwa, Bi. Hilda Nsombo akikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Mstaafu, msaada wa mabati na mifuko ya saruji kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
  Afisa wa PRIDE Tanzania, Ndugu Samson Tenga akifanya tathmini kabla ya kumkabidhi Mteja wa PRIDE Tanzania, Tawi la Bukoba mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba yake ambayo ilibomoka kutokana na janga la tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera hivi karibuni.


older | 1 | .... | 1471 | 1472 | (Page 1473) | 1474 | 1475 | .... | 3272 | newer