Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1470 | 1471 | (Page 1472) | 1473 | 1474 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Na Ally Daud.

  WIZARA ya Afya ,Maendeleo  ya Jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto kupitia kitengo cha Magonjwa yasioambukiza (NCD) chini ya Kurugenzi ya Tiba inaendesha mafunzo ya kupambana na magonjwa yasioambukiza kwa watoa huduma ngazi za mikoa na wilaya.

  Akifungua mafunzo hayo leo jijini Morogoro Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dkt. Margaret Mhando amesema kuwa wameamua kuanzisha mpango huo ili kuwapa nguvu na uwezo watoa huduma kwa ajili ya kupambana na magonjwa hayo.

  “Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yamekuwa yakiongezeka kwa kasi sana duniani na haswa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania hivyo hatuna budi kuongeza juhudi za kupambana nayo” alisema Dkt. Mhando

  Aidha Dkt. Mhando amesema kuwa pamoja na juhudi zinazofanywa na Wizara katika kupambana na magonjwa hayo kila mkoa na wilaya lazima ziangalie uwezekano wa kuifanya NCD kuwa kipaumbele katika mipango yao ya  maendeleo.

  Kwa mujibu wa Dkt. Mhando amesema kuwa viashiria vya magonjwa yasiyo ya kuambukiza imeonyesha kuongezeka kwa hali ya juu ambapo  idadi ya watu wanaovuta sigara ni asilimia 15.9 wanaokunywa pombe ni asilimia 29.3, wenye uzito uliopita kiasi 34.7, shinikizo la damu ni asilimia 25.9 na wagonjwa wa kisukari ni asilimia 9.1.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasioambukiza Dkt. Sarah Maongezi amesema kuwa wanatakiwa kupunguza moja ya tatu ya vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa kukinga, kutibu na kuzingatia afya ya akili Kufikia mwaka 2030.

  Aidha Dkt. Maongezi amesema kuwa  wanatarajia waganga wa ngazi za mikoa na wilaya kufanya kazi kwa nguvu na kwa ukaribu zaidi na kitengo cha magonjwa yasiyo ya kuambukiza cha Wizara ili huduma hizi ziwafikie watu wote hadi ngazi ya jamii.  Mafunzo hayo ya siku tatu yanayofanyika jijini Morogoro yanalenga kuwafundisha madaktari na watoa huduma kuhusu kupambana na ya magonjwa yasioambukiza ikiwemo kisukari, magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, kansa, ajali za barabarani  na uzito kupita kiasi.
   Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dkt. Margaret Mhando akipitia baadhi ya nyaraka za kufundishia kabla ya kufungua mafunzo ya kupambana na magonjwa yasioambukiza kwa watoa huduma ngazi za mikoa na wilaya yaliyofanyika Mkoani Morogoro.
   Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasioambukiza Dkt. Sarah Maongezi akiongea na madaktari na watoa huduma hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kupambana na magonjwa yasioambukiza kwa watoa huduma ngazi za mikoa na wilaya yaliyofanyika Mkoani Morogoro.
   Mratibu wa Magonjwa yasioambukiza Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Digna Riwa akitoa mafunzo kwa waganga na watoa huduma hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kupambana na magonjwa yasioambukiza kwa watoa huduma ngazi za mikoa na wilaya yaliyofanyika Mkoani Morogoro.
   Baadhi ya madaktari kutoka mikoa tofauti nchini wakifuatilia kwa makini mafunzo kutoka kwa mkufunzi hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kupambana na magonjwa yasioambukiza kwa watoa huduma ngazi za mikoa na wilaya yaliyofanyika Mkoani Morogoro.

  Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dkt. Margaret Mhando katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya madaktari kutoka mikoa tofauti nchini wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kupambana na magonjwa yasioambukiza kwa watoa huduma ngazi za mikoa na wilaya yaliyofanyika Mkoani Morogoro.

  0 0

  Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa ufafanuzi wa uamuzi wake wa kuzuia biashara ya usafirishaji wa wanyamahai nje ya nchi kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo na kusema kuwa uamuzi huo ulitolewa kwa lengo la kupanga vizuri biashara hiyo kwa faida ya serikali na wafanyabiashara wenyewe.

  Ufafanuzi huo umetolewa jana na Waziri wa Wizara hiyo, Prof. Jumanne Maghembe katika kikao alichokiitisha wizarani hapo na wafanyabiashara wa wanyamahai wa makundi ya wadudu, vyura, mijusi, ndege, nyani na tumbili ambao walitaka kupata ufafanuzi wa hatima ya biashara yao kutoka serikalini.

  Katika risala iliyosomwa na kiongozi wa wafanyabiashara hao, Adam Rashid Warioba kwa Waziri Maghembe, aliiomba Serikali kutoa ufafanuzi wa hatma ya biashara yao iliyofungiwa ambayo imekuwa tegemeo pekee katika kuendesha maisha yao huku wakitaka kujua hatma ya wanyamahai waliohifadhiwa na gharama zao walizolipia Serikalini.

  Akitoa ufafanuzi wa uamuzi wa Serikali kufungia biashara hiyo kwa wafanyabiashara hao, Prof. Maghembe amesema wanyamahai wengi kutoka nchini Tanzania wamekuwa wakisafirishwa nje ya nchi bila ya kufuata utaratibu maalum ikiwemo vibali vya kukamata na kuwasafirisha wanyama hao jambo ambalo limekuwa likiikosesha serikali mapato mengi.

  “Wapo kati yenu ambao walikuwa wanasafirisha wanyamahai kinyume cha sheria, bila vibali vyovyote, na wanyama wa Tanzania walikuwa wakimatwa kwenye bandari na viwanja vya ndege, ambao wanasafirishwa kinyume cha sheria, wengi tu, na ndio maana Serikali ikasema hii biashara tusimamae kwanza tuwekwe utaratibu ambao kila mtu ataufuata, na ambao hautaweza kututia aibu huko nje” alisema.

  Alisema sababu nyingine iliyopelekea serikali kufunga biashara hiyo kwa muda ni bei ndogo inayouzwa wanyama hao nje ya nchi ambayo haiwanufaishi wafanyabiashara na Serikali ukilinganisha na thamani yake kwa kile wanachoenda kufanyiwa, alitolea mfano tumbili ambao hufanyiwa utafiti wa madawa mbali mbali na baadae kuuzwa mabilioni ya fedha huku tumbili huyo akiuzwa kwa dola 25 tu.

  “Nimefurahi yule bwana aliyesema tumbili mmoja ni dola 25, lakini akasema hao ndio wanafanyamedical research (utafiti wa madawa) yote duniani, sasa sisi tunapata dola 25 na wenzetu wanafanya research (utafiti) wanatuuzia madawa yote billions of dollars (mabilioni ya dola za kimarekani), tuweke utaratibu na ninyi mtakapokuwa mnafanya hii biashara mpate sio lazima serikali ndio lazma ipate, mpate kilicho sawa na thamani ya wanyama mnaowauza”, alisema Prof. Maghembe.


  0 0

  Shukran

  0 0

  Mbunge waArusha mjini Godbless Lema na mkewe Neema Lema


  Na,Vero Ignatus.Arusha.

  Kesi iliyokuwa isikilizwe leo 22 disemba 2016 inayomkabili mbunge wa Arusha mjini Godbless Leman na mkewe Neema Lema ya kumtukana mkuu wa mkoa Mrisho Gambo imeahirishwa kutokana na hali ya lema kuwa mbaya gerezani.

  Taarifa za Lema kushindwa kufika mahakamani zimetolewa na wakili wa serikali Elizabeth Swai leo asubuhi kwa hakimu mfawidhi katika mahakama ya hakimu mkazi Augustino Rwezile ,alisema alipata taarifa kutoka kwa Afisa Magereza mshatakiwa kwanza anumwa hivyo siku ya leo alipewa mapumziko pamoja na hayo taarifa hizo hazijaeleza kwa undani ni tatizo gani linamsumbua mbunge huyo.

  Pia alisema alipewa cheti cha mgonjwa cha zahanati ambacho kilionyesha mahudhurio ya mgonjwa kwenye zahanati hiyo kutokana na kuwepo na taarifa za kuumwa za mbunge huyo na kushindwa kufika mahakamani,aliiomba mahakama ipange tarehe nyingine .  Leo ilikuwa ni siku ya kusomewa hoja za awali kwa mbunge huyo na mkewe Neema Lema , ambapo pia shahidi wa kwanza kutoka jamhuri alikuwa Georgr Katabazi alikuwa anatoa ushahidi.

  Hata hivyo hakimu mfawidhi Augustino Rwezile amesema kuwa kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 18 Januari 2017


  Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema na mkewe Neema Lema wanakabiliwa na kesi ya mkumtukana mkuu wa mkoa Mrisho Gambo.

  0 0

  Anna Sangai (mbele) programu programu kutoka TGNP Mtandao akiwasilisha mada katika mkutano na wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayo. Anna Sangai (mbele) programu programu kutoka TGNP Mtandao akiwasilisha mada katika mkutano na wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayoAnna Sangai (kulia) programu programu kutoka TGNP Mtandao akiwasilisha mada katika mkutano na wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayo. Anna Sangai (kulia) programu programu kutoka TGNP Mtandao akiwasilisha mada katika mkutano na wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayoAnna Sangai (kulia) programu programu kutoka TGNP Mtandao akiwasilisha mada katika mkutano na wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayo. Anna Sangai (kulia) programu programu kutoka TGNP Mtandao akiwasilisha mada katika mkutano na wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayo.Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kipunguni, Hija Mzome (mbele-kulia) akiwasisitisha washiriki wa mkutano huo kukubali kubadilika na kuachana na vitendo vya kikatili vilivyopitwa na wakati hasa ukeketaji. Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kipunguni, Hija Mzome (mbele-kulia) akiwasisitisha washiriki wa mkutano huo kukubali kubadilika na kuachana na vitendo vya kikatili vilivyopitwa na wakati hasa ukeketaji.


  0 0

  Na Zainab Nyamka, 
  Globu ya Jamii.
  Serikali imevipiga marufuku Klabu za ligi kuu Tanzania hususani Simba, Yanga na Azam kuwatumia wachezaji wa kigeni mpaka watakapokamilisha taratibu zao za uhamiaji.
  Uamuzi huo umekuja siku chache baada ya klabu ya Ndanda FC kutuma malalamiko TFF kwamba Simba iliwatumia wachezaji wake wawili wa kigeni Daniel Agyei na James Kotei kwa madai kwamba hawana vibali vya kufanya kazi nchini.
  Klabu hizo zimepewa maagizo kwamba wachezaji na makocha wote wa kigeni ambao hawajakamilisha taratibu za uhamiaji hawatoruhusiwa kuzihudumia klabu zao hadi hapo watakapokamilisha taratibu hizo.
  Idara ya uhamiaji kupitia kwa afisa uhamiaji John Msumule leo alitoa tamko kwa klabu zote za Ligi Kuu Tanzania bara kutoendelea kuwatumia wachezaji wake wa kigeni hadi watakapotimiza masharti ya uwepo wao nchini kisheria na uhamiaji wamezitaka klabu za Simba, Yanga na Azam FC kuhakikisha wachezaji wake na makocha wao wa kigeni wanapata vibali vya kufanyia kazi nchini pamoja na kuishi. 
  Hata hivyo kwa upande wa Yanga wao wachezaji wao wana vibali vya kazi na vya kuishi nchini isipokuwa makocha wao ndio wana vibali vya kazi pekee.
  Kwa upande wa watani zao wa jadi Simba wao hawajatimiza vigezo hivyo kwa wachezaji wao wa kigeni na makocha wao, hivyo hawaruhusiwi kuendelea kuwatumia wachezaji wao ambao hawana vibali mpaka watakapo vipata vibali ingawa uomgozi wa klabu ya Siumba ulisema kuwa wachezaji hao wamekamilika kila kitu.

  0 0
  DROO ya kupanga ratiba ya michuano ya kimataifa ya Shirikisho la Afrika (CAF) imefanyika leo mchana kwa timu za Tanzania Yanga na Azam kupamgiwa timu zao.

  Klabu ya Yanga imepangiwa kuanza na Ngaye De Mbe ya Nchini Comoro huku Azam akisubiri mshindi katika ya Mbabane Swallons na Opara United. 

  Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Februari 11, 12 na 13 na Yanga wataanzia  ugenini kwenye mechi ya kwanza kama  watafanikiwa kushinda dhidi ya Ngaya De Mbe watakutana na mshindi kati ya Zanaco (Zambia)vs APR (Rwanda) na baada ya hapo wataingia hatua ya makundi Total caf club championship 2017.

  0 0

  HAKUNA Ubishi kwamba Tanzania ni nchi inayohitaji teknolojia nyingi mpya ili iweze kukua haraka kiuchumi kwa kuendana na kauli ya Serikali inayotaka kuona Tanzania inakuwa nchi ya viwanda.

  Mojawapo ya njia inayoweza kusaidia kukuza haraka teknolojia nchini ni kwa Watanzania kwenda nje ya nchi kusoma kisha kurudi na ujuzi kuliendeleza taifa. Hivi ndivyo ilivyofanya nchi nyingi Duniani, hatimaye leo nchi hizo zimevuka kwenye lindi la umaskini.

  Kwa wale ambao wanafuatilia historia ya Tanzania watakubaliana na ukweli kwamba nchi hii ilikotoka haikuwa na teknolojia nyingi muhimu, zikiwamo zile zilizosaidia kuharakisha maendeleo.

  Kwamba, mambo mengi nchini yamekuwa yakifanyika kwa staili za kijadi, kwa mfano hata kupata mchele, mtu alilazimika kutumia nguvu kubwa kutwanga mpunga au ilikuwa ni lazima kutumia kinu kutwanga mahindi ili kupata unga, lakini ni kupitia teknolojia mpya, leo kuna mashine nyingi za kufanya kazi hizo katika maeneo mbalimbali nchini.

  Kwa sasa kuna teknolojia nyingi nchini, nyingi zikitokea nje ya nchi. Nyingi za teknolojia hizi zililetwa na wafanyabiashara au wasomi wachache waliokwenda nje, kwani sio wengi ambao wamekuwa na ufahamu kuhusu vyuo vya nje.

  Ukilinganisha na mataifa mengine kama Kenya, Nigeria na mengineyo ya Afrika Mashariki, Tanzania imekuwa na idadi ndogo ya watu wanaokwenda kusoma nje, sababu kubwa pamoja na mambo mengine ni kutokuwa na ufahamu kuhusu vyuo vya nje.

  Aidha wapo wengine wana imani isiyo sahihi kwamba kusoma nje inamuhitaji mtu kuwa na fedha nyingi, imani ambayo sio kweli, kuna vyuo nchini ni gharama zaidi kuliko vya nje.

  Kwa mfano baadhi ya kozi nje unaweza kusoma Shahada kwa maana ya ada na gharama za malazi kwa mwaka ni kati ya dola 3100 hadi 5000, sawa na Shilingi milioni sita hadi kumi. Hapa nchini kuna shule hutoza ada ya dola 5000 (zaidi ya milioni kumi za Kitanzania) kwa mwaka kwa elimu ya msingi au sekondari.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Education Link akifafanua jambo kwenye  maonyesho ya vyuo vya nje yanayoendelea katika viwanja vya kumbukumbu  ya Azimio la Arusha, Jijini Arusha. 
  Meneja wa Global Education Link tawi la Arusha, Regina Lema (wa pili kutoka kushoto) akimsikiliza kwa umakini mmoja wa watu waliofika kwenye  maonyesho ya vyuo vya nje yanayoendelea katika viwanja vya kumbukumbu ya Azimio la Arusha, Jijini Arusha

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  JESHI la Polisi limesema linaendelea kufanya upelelezi kupotea kwa raia, Benard Focus 'Ben Saanane', (pichani) na kutaka wananchi kutoa taarifa zinazohusiana na huyo mtu kupotea.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishina wa Jeshi la Polisi, Robert Boaz, amesema jeshi la polisi lilipopata taarifa walianza kufanyia kazi kwa upelelezi kwa kupotea raia huyo.

  Amesema taarifa za kupotea zililipotiwa kituo cha polisi na mtu aliyejitambulishwa kuwa ni rafiki yake na baada ya kuokea taarifa hizo jalada la uchunguzi lilifunguliwa na taratibu zote za kiupelelezi zinazohuusu mtu aliyepotea zilifuatwa na bado upelelezi na suala hilo unaendelea.

  Boaz amesema wananchi wamekuwa pamoja wakitoa taarifa mbalimbali na kuahidi kwamba taarifa zote zitafanyiwa kazi na pindi wanavyopata wawasilishe katika vituo vya Polisi.

  Aidha amesema wakati upelelezi wa matukio hayo ukiendelea ,tunawaomba wananchi kuendelea kuwa watulivu , Jeshi la Polisi litaendelea kutoa taarifa kadri ya upelelezi utavyokuwa unaendelea.

  Wakati huo huo, Kamishina Boazi, amesema maiti saba iliyokutwa katika Mto Ruvu kati ya Desemba 9/12 miili sita ilizikwa kutokana na hali zake kuwa mbaya.

  Amesema mwili mmoja waliuchukua na kupeleka katika hospitali ya Bagamoyo kwa ajili ya utambuzi lakini haukuweza kutambuliwa na kuamua kuzika na upelelezi unaendelea.

  0 0

  Na Ripota wa globu ya Jamii Ileje.

  Upepo na mvua kubwa vimesababisha uharibifu wa mali na miundo mbinu katika kata ya Mbebe Wilayani Ileje mkoani Songwe na kusababisha majeruhi wengi na kifo cha mtu mmoja katika kata hiyo.

  kwa mujibu wa ripota wa globu ya jamii aliyepo wilayani humo amesema kuwa mvua za mwaka hu katika Wilaya hiyo ni chache lakini ni hatari sana kwani tukio hilo la na Mvua za upepo mkali ni lapili hali inayotishia usalama wa wakazi wa eneo hilo.

  kwa upande wake mkuu wa Wilaya hiyo Joseph Mkude amesema kuwa ameshafika katika eneo la tukio lilitokea janga hilo la upepo na kuzungumza na wananchi namna ya kuchukua tahadhari.

  "Nimewaambia wananchi wawe waungwana kwa kusaidia siku ya leo, kwani kuanzia kesho halmashauri itatoa utaratibu hata hivyo katika ajali hiyo ni mtu mmoja tu ambaye amefariki huku wengine wakiwa wamekimbizwa katika hospitali ya Itumba kwa ajili ya matibabu zaidi"amesema Dc Mkude
   Baadhi ya nyumba zilizoharibiwa na Mvua kubwa ilionyesha wilayani humo
   Mkuu Wa Wilaya ya Ileje Joseph Mkude akikagua barabara
   Mkuu Wa Wilaya ya Ileje Joseph Mkude akiongea na Wananchi

  0 0

  Pichani kulia ni mrembo wa Taifa Miss Tanzania 2016 Diana Edward akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kuwasili  leo (21 Desemba 2016) akitokea Washington DC Marekani, ambapo alikwenda kushindana katika mashindano ya urembo ya Dunia. Miss World Beauty Contest 2016.
  Miss Tanzania 2016 Diana Edward aliwasili nchini muda wa saa 10 alasiri na Shirika la ndege la Emirates, na kulakiwa na Waandishi wa Habari, Wazazi wake, baba na mama mzazi, wadau, pamoja na wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania.

  Uongozi wa Kampuni ya Lino International Agency Limited utatoa ratiba ya shughuli zake za kijamii hapo baadae, baada ya mapumziko ya mwisho wa mwaka.

  Tunawatakia Heri na Baraka za Sikukuu ya X Mass pamoja na Mwaka mpya wa 2017.
  Mrembo wa Taifa Miss Tanzania 2016 Diana Edward akilakiwa na wazazi wake mara baada ya kuwasili  leo (21 Desemba 2016) akitokea Washington DC Marekani, ambapo alikwenda kushindana katika mashindano ya urembo ya Dunia. Miss World Beauty Contest 2016.

  0 0

  Na Antony John wa Globu ya jamii.
  Shuleya  Ibun Jazary Acdemic primary shool imefanya maafali ya 5 leo hii kitika ukumbi wa karimjee Hall jijini Dar es salaam ilikuwapongeza vijana wao walio hitimu Darasa la Saba na kufanaya vizuri katika maatoke yao.
  Akizungmza katika mahafali hayo Mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Bakwata Sheikh Hamis Mataka  kwaniaba ya Mufti kuu wa Tanzania amesema  tunawapongeza wanafunzi hawa kwa matokeo mazuri waliyo yapata na wajibuchangamoto kwa kuigawa elimu ya elimu ya dunia na elimu ya dini.
  ‘’Watoto wengi huwa wanaosoma shule hizi za dini wanakuwa wanazingatia elimu ya dini lakini watoto hawa wamejibu changamoto kwa kufanya vizuri katika vyote yani katika elimu ya dini na elimu ya dunia hivyo nawapongea sana", amesema Mataka.
  Hivyo hivyo mkuu wa shule hiyo Othuman Kaporo amewapongeza waanafunzi hayo kwa kumaliza darasa la saba na kuongeza kuwa wanafunzi wote wanaomaliza katika shule yake ni desturi yao kufanya vizuri kiwilaya,kimkoa na kitaifa katika mitihani yao.
   Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata,Sheikh Khamis Mataka akizungmza katika mahafali ya Shuleya Ibun Jazary Acdemic primar shool katika kitika ukumbi wa karimjee Hall jijini Dar es salaam.
   Mkurugenzi wa Tasisi za Mkuu wa shule hiyo Ibun Jazary Othman Kaporo akizungmza katika mahafali ya Shuleya Ibun Jazary Acdemic primar shool katika ukumbi wa karimjee Hall jijini Dar es salaam.
   Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata,Sheikh Khamis Mataka akimkabidhi tuzo mwanafundi aliyefanya vizuri kwenye masomo, Ghukba Kassim Rashid leo  katika ukumbi wa karimjee Hall jijini Dar es salaam.
   Wageni mbalimbali pamoja na wazazi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata,Sheikh Khamis Mataka
  Wageni mbalimbali pamoja na wazazi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata,Sheikh Khamis Mataka.

  0 0

  Hapa ni katika ukumbi wa mikutano hotel ya Empire mjini Shinyanga ambapo leo Jumatano Desemba 21,2016 waandishi wa habari mkoani Shinyanga wamepewa mafunzo kuhusu masuala ya watu wenye ualbino.
  Mafunzo hayo yameandaliwa na Chama cha watu wenye Ualbino nchini (TAS) kupitia programu ya Elimu kwa Jamii kuhusu mambo ya Ualbino 'Community Awareness Raising Program' inayofadhiliwa na shirika la Open Society Foundations.
  Mgeni rasmi Mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga George Mdoe aliyemwakilisha kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga akifungua semina hiyo ambapo a
  lisema hivi sasa serikali inahitaji watu wenye ualbino wajumuike katika jamii ndiyo maana baadhi yao wameondolewa katika kambi zao mfano Buhangija katika manispaa ya Shinyanga na kurudishwa katika jamii yao ili kuondoa tofauti yao na watu wengine katika jamii.
   Mwezeshaji katika semina hiyo Kadama Malunde akiwasilisha mada kuhusu mchango wa vyombo wa habari katika vita dhidi ya mauaji ya watu wenye ualbino nchini Tanzania. Malunde alisema vyombo vya habari vimekuwa na mchango mkubwa sana katika kuongeza ufahamu wa jamii juu ya masuala ya watu wenye ualbino kitaifa na kimataifa,kupunguza matukio ya ukataji viungo vya watu wenye ualbino na mauaji, kuelezea juhudi mbalimbali za TAS kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
  Afisa Mahusiano na Habari Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania Josephat Torner akisikiliza hoja kutoka kwa mwandishi wa habari gazeti la Jamboleo Stephen Kidoyayi.  0 0


  Na Benny Mwaipaja, 
  WFM, Dar es salaam.
  Serikali ya Kuwait imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa dola za Kimarekani Milioni 34 kwa ajili ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa Kilometa 85 kwa kiwango cha lami kutoka eneo la Chaya hadi Nyahua mkoani Tabora.
  Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na mwakilishi wa Balozi wa Kuwait hapa nchini, Bw. Mohammad Rashid Alamiri, aliyeongoza ujumbe kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait, ulipomtembelea na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na Kuwait.
  Dkt. Mpango ameushukuru Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (Kuwait Fund) kwa kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu utakaochochea maendeleo kwa Watanzania hususani wanaoishi maeneo hayo kutokana na umuhimu wa barabara katika kukuza uchumi wa Taifa.
  Amesema kuwa kipande hicho cha barabara kutoka Chaya hadi Nyahua, ambacho kiko Barabara Kuu itokayo Dar es salaam kwenda katika mikoa ya Tabora na Kigoma, licha ya umuhimu wake katika kukuza biashara na usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo ikiwemo inayokwenda nchi jirani, ilikuwa haijapata fedha kwa ajili ya ujenzi wake.
  “Riba waliyoiweka mezani kwa mazungumzo ni asilimia 2 lakini nimewaomba waangalie uwezekano wa kuiteremsha walau ifikie asilimia 1.5 na wamependekeza kipindi cha kuanza kulipa mkopo kiwe miaka ishirini ijayo lakini nimewaomba wasogeze hadi kufikia miaka 25 kama ilivyo kwa mradi wa Hospitali ya Mnazimmoja” aliongeza Dkt. Mpango

  Dkt. Mpango amesema Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wake huo wa Maendeleo wameonesha nia ya kutoa mkopo wenye masharti nafuu kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Hospitali ya Mnazi Mmoja iliyoko Visiwani Zanzibar.
  “Nawahakikishia kuwa baada ya muda si mrefu wananchi wa mikoa ya Tabora na Kigoma watarajie kuona mkandarasi akiingia kazini ili kujenga barabara hii muhimu sana kwao na kwa uchumi wa Taifa kwa ujumla” Alisisitiza Dkt. Mpango.
  Ameeleza kuwa ujenzi wa kipande cha barabara hiyo kutoka Chaya hadi Nyahua unatarajia kugharimu shilingi Bilioni 61 lakini Kuwait haitatoa fedha zote hivyo ameuomba Mfuko huo uangalie uwezekano wa kutoa kiasi hicho chote cha fedha ili uweze kukamilika mapema.
    Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akizungumza na ujumbe kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait, kuhusu miradi ya miundombinu itakayofadhiliwa na Mfuko huo, ukiwemo mradi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Chaya kwenda Nyahua mkoani Tabora. Kulia ni mwakilishi wa Balozi wa Kuwait hapa nchini Bw. Mohammad Rashid Alamiri, Makao Makuu ya Wizara, Jijini Dar es salaam.
  Maafisa waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakimsikiliza Mwakilishi wa Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Bw. Mohammad Rashid Alamiri (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza katika Kikao kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), katika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
  Wataalamu toka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (kushoto) na wataalamu kutoka Tanzania (kulia) wakijadili kuhusu mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Kuwait, utakao saidia kujenga barabara Mkoani Tabora, Mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo, Jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akipeana mkono na Mwakilishi wa Balozi wa Kuwait Bw. Mohammad Rashid Alamiri huku wakifurahia jambo baada ya kumalizika kwa mkunano kati yao uliojikita katika mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo barabara na sekta ya afya, Mkutano huo umefanyikaatika Makao makuu ya Wizara, Jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia), akisalimiana na Mshauri wa masuala ya ufundi kutoka Kuwait Bw. Mohammad Alhadidi, baada ya kumalizika kwa kikao kati ya Waziri huyo na Wajumbe kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait, katika ukumbi wa Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe toka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (Kuwait Fund) baada ya kumalizika kwa kikao kati yake na wajumbe hao ambapo mbali na kutoa mkopo wa ujenzi wa barabara kutoka Chaya kwenda Nyahua mkoani Tabora, walionesha nia ya kutoa mikopo mingine yenye masharti nafuu katika miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania. Kikao hicho kimefanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo, Jijini Dar es salaam. (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

  0 0  0 0


  0 0  Na Antony John 
  wa Globu Ya Jamii
  Wafanya biashara mbalimbali katika soko la Karikoo wamesema hali ya kibiashara bado imekuwa ngumu katika kipindi hiki cha kuelekea katika sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya.
  Wakizungumza na Globu ya Jamii wafanya biashara hao wamesema hali ya kibiashara imekuwa ngumu kwa kuwa watu wengi hawaendi kununua bidhaa sokoni hapo kwa sababu wanaogopa ukubwa wa bei katika kipindi hiki cha kuelekea katika msimu huu wa sikukuu.
  Wafanya biashara hao wamewataka wateja kutokuwa na wasiwasi wa kwenda kununua bidhaa sokoni hapo kwa kuwa bei bado ipo vile vile hazijaongezeka  katika kipindi hiki.
  Aidha wafanya biashara hao waliwaomba wateja watakao kwenda kununua bidhaa Sokoni hapo wasiishie nje ya Soko na badala yake kwenda kununua bidhaa ndani ya Soko hilo kwa kuwa bei za Ndani ya Soko ni rahisi kuliko za nje.
   Mfanya biashara wa Soko la Kariakoo Alhaji Kabula akizungumza na Globu ya Jamii kuhusiana na bei ya Mchele Leo hii katika Soko hilo la Kariakoo.
   Mfanyabiashara wa nyama Zacharia Zacharia katika Soko la Karikaoo akizungumza na Michuzi Tv juu ya hali ya bei ilivyokuwa kwa kipindi hiki cha kuelekea katika sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya.


  0 0

  codes

  DAC has handed-over 10 refurbished children's bicycles to PASADA which formed part of the assistance the club provided the organisation from the proceeds of the World Aids Day 2016 Charity Ride that was held on Saturday, 3rd December 2016. 
  In addition to the bike donation, DAC paid for the repair and maintenance of 15 of the centre's old bikes and has committed to provide maintenance of the bicycles for the next 3 months. 
  PASADA is a social service agency striving to provide holistic care and support to those living with HIV. To find out more about the centre and it's activities, please go to www.pasada.or.tz. 
  We thank each and everyone who joined us on the fundraising drive.

  0 0

  Office space for rent in a  modern executive new building with high grade quality finishes throughout along Bagamoyo road at the TANZANITE PARK building,  Victoria area in Dar es salam. 
  The spaces are suitable for banking halls, offices, executive board/meeting rooms, hotel and restaurant premises at the roof top complete with  gym and swimming pool areas with panoramic views of the Indian Ocean.

  For Viewing please contact:   Issa on 0767252641 or 0766930001 or alternatively  alternatively contact Sombyo.

    
  0 0


  Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya mikopo ya Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa (kushoto), akimkabidhi Ofisa Utumishi wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Emelda Kisosi, kompyuta kwa ajili ya kusaidia ufanisi wa kazi ofisi zao kama sehemu ya kujitolea kwa jamii. Kulia ni Ofisa TEHAMA wa Halmashauri ya Wilaya Arumeru, Edna Mwaipiana.


  Na Mwandishi Wetu, Arusha

  HALMASHAURI ya Wilaya Arumeru, mkoani Arusha, jana imepokea kompyuta mbili zilizotolewa msaada na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, kama sehemu ya ushirikiano na kusaidia na kukuza ufanisi wa kikazi kwa watumishi wa umma wilayani humo.

  Kompyuta hizo zinatoka ikiwa ni siku chache baada ya Mkoa wa Morogoro nao kupokea msaada kama huo kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa umma.

  Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Mercy Mgongolwa katikati akizungumza jambo katika makabidhiano hayo yaliyofanyika leo jijini Arusha. Kulia ni Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya Arumeru, Emelda Kisosi.

  Akizungumza katika makabidhiano hayo leo jijini Arusha, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, alisema wamefikisha kompyuta mbili katika wilaya hiyo kama orodha ya mahitaji waliyopokea kutoka Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Alisema anaamini kwa kufikisha kompyuta hizo, kutachangia ufanisi wa kikazi kwa kutumia vyema teknolojia ya kompyuta iliyokuja kupanua wigo wa utendaji bora wa kazi kwa Tanzania nzima kwa hali ya kupanga, kutatibu na kuhifadhi kumbukumbu muhimu za kiutendaji wakati wote.

  Picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya kompyuta hizo.
  Mercy Mgongolwa akikabidhi nyaraka za kompyuta hizo.

  “Huu ni mwendelezo mzuri wa ugawaji wa kompyuta 205 tulizonunua zenye thamani ya Sh Milioni 500, ambapo tayari kompyuta 125 zimefikishwa Makao Makuu ya Utumishi na wao kutuelekeza eneo na idadi ya ugawaji kwenye halmashauri za nchi yetu,” alisema.

  Naye Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya Arumeru, Imelda Kisosi, aliwashukuru Bayport kwa kujitolea vifaa hivyo muhimu vitakavyowapatia urahisi watendaji hao kuchapa kazi kwa nguvu zote ili wilaya yao isonge mbele.

  “Msaada huu ni mkubwa mno kwetu hivyo tunawashukuru na kuwaahidi ushirikiano wa hali ya juu sanjari na kuwataka Bayport waendelee kuwa karibu na jamii yetu kama njia ya kuwapatia maendeleo Watanzania wote, hususan wa wilayani kwao Arumeru, mkoani Arusha,” alisema Kisosi.

  Bayport Financial Services ni taasisi ya mikopo inayojitolea kwa hali na mali ambapo mbali na kununua kompyuta hizo 205, pia imekuwa ikishiriki kujenga madarasa katika shule mbalimbali, hali inayochangia kwa kiasi kikubwa kupanua kiwango cha elimu nchini.

  Huduma znazotolewa na Bayport ni pamoja na mikopo ya fedha taslimu kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi, mikopo ya viwanja, mikopo ya fedha kwa njia ya simu za mikononi maarufu kama ‘Nipe Boost’, Bima ya Elimu kwa Uwapendao na nyinginezo zinazopatikana katika ofisi zao za matawi 82 katika mikoa na wilaya mbalimbali za Tanzania Bara.

older | 1 | .... | 1470 | 1471 | (Page 1472) | 1473 | 1474 | .... | 3286 | newer