Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1469 | 1470 | (Page 1471) | 1472 | 1473 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,wakiwa wanaelekea katika kituo cha wazee na wasiojiweza  cha Sarame Magugu, Wilayani Babati Mkoani Manyara, kutoa msaada wa shuka na vyandarua na  vyakula mbalimbali , dawa na mahitaji mengine yenye thamani ya zaidi ya sh10 milioni yaliyotolewa msaada na Vodacom Tanzania Foundation.
  Meneja ruzuku na mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald, akimkabidhi, mmoja kati ya wazee wa kituo cha wazee na wasiojiweza Sarame Magugu, Wilayani Babati Mkoani Manyara, Aaron Owiso, ambapo waliwakabidhi wazee hao mashuka, vyandarua, vyakula, dawa na mahitaji mengine yenye thamani ya zaidi ya sh10 milioni.
  Mzee Maalim Masaja (kushoto)anayelelewa katika kituo chawazee wasiojiweza cha Sarame Magugu, Wilayani Babati Mkoani Manyara, akipokea mfuko wenye mchele kwa niaba ya wenzake toka kwa Meneja ruzuku na mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald, ambapo msaada huo ulitolewa na Vodacom Tanzania Foundation kwa wazeeikiwa ni pamoja na mashuka, vyandarua, vyakula, dawa na mahitaji mengine yenye thamani ya zaidi ya sh10 milioni.

  0 0  Kumekuwa na taarifa inasambazwa katika mitandao ya kijamii, makundi ya ‘WhatsApp’, ‘Facebook’ na majukwaa mbalimbali ikieleza kuwa Serikali imepiga marufuku watumishi wa umma kukopa Benki,SACCOS,VICOBA na Taasisi mbalimbali za kifedha.

  Taarifa iliyotolewa leo tarehe 20 Desemba 2016 na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeeleza kuwa taarifa inayosambazwa, ambayo imetafsiri mawasiliano ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni ya kupotosha, hivyo watumishi wote wa umma wanaombwa kuipuuza.

  Vilevile watumishi wa umma wametakiwa kuzingatia kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali HAINA mamlaka ya kuzuia wala kuruhusu mtumishi yeyote wa Serikali kukopa au kutokopa katika Taasisi yoyote ya Fedha nchini.

  Watumishi wa umma pia wamekumbushwa kuwa mikopo yote ya watumishi wa umma katika Taasisi za Fedha hutolewa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu zilizopo ili mradi mtumishi awe ametimiza vigezo.

  Aidha, watumishi wa umma wameaswa kuacha tabia ya kusambaza taarifa zisizo za kweli na ambazo zina mamlaka husika ya kuzitoa ikiwa ni pamoja na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.


  0 0

  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

  Shirikisho la soka nchini TFF limesema kuwa ligi kuu ya Vodacom haitasimama kwa ajili ya kupisha kombe la mapindzu bali vyote vitakwenda sambamba.

  Hayo yamesemwa na afisa mtendaji mkuu wa bodi ya ligi nchini, Boniface Wambura alipokuwa akizungumza na kituo kimoja cha televisheni juu ya muingilio wa ligi hiyo na ligi kuu ya Vodacom.

  “lazima watu watambue kuwa TFF katika hili tumejipanga kwa kushirikiana na wenzetu shirikisho la soko visiwani Zanzibar(ZFA) kwa kutengeneza ratiba ambayo aiwezi kuathiri wala kupelekea kusimamishwa kwa ligi kuu bara ambayo inaendelea hivi sasa”amesema Wambura.

  Amesema kuwa katika kuzingatia hilo timu zinazoshiriki ligi ya mapinduzi kutoka bara ni tatu hivyo zote zimeweza kutengewa muda wa kucheza mapinduzi kisha kurejea kucheza michezo ya ligi kama ratiba inavyo hitaji .

  Ameweka wazi kutokana na ratiba ya mapinduzi timu zote zinazoshiriki ligi kuu bara ni lazima zitafuata makubaliano ya kucheza michezo mingine visiwani kisha kurejea kucheza michezo ya ligi kama ilivyopangwa.

  Wambura aliwatoa hofu wapenzi wa ligi kuu ya Vodacom kuwa na amani kwa ligi itaendelea kama ilivyopangwa nchi nzima.

  0 0

  Mradi huo ulifadhiriwa na Pink Ribbon Red Ribbon pamoja na washirika wengine kama wanavyoonekana katika picha. Mitandao ya simu ilisaidia kutoa nambari za bure ambazo ni 117 kwa ajili ya wananchi kupiga ili kuelimishwa kuhusu Saratani.

  Uelewa kuhusu dalili za awali za maambukizi ya Saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake mkoani Mwanza, umeongezeka na hivyo kufanya idadi ya wanawake wanaojitokeza kupima maambukizi hayo kufikia wanawake 60 kwa mwezi.
  Hatua hiyo imefikiwa kutokana na juhudi zinazofanywa na serikali kupitia wizara ya afya kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali ikiwemo TAYOA katika kuhakikisha akina mama nchini wanafahamu umuhimu wa kufanya uchunguzi wa awali kuhusu maambukizi ya saratani kwa ujumla.

  Hayo yamebainishwa Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Shirika la TAYOA, Elizaberth Ndakidemi, kwenye mkutano wa kushirikishana uzoefu, changamoto pamoja na mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa Saratani ya shingo ya kizazi mkoani Mwanza, unaotekelezwa na shirika hilo.

  Katika mradi huo ulioanza kutekelezwa mwezi April mwaka 2014, zaidi ya akina mama elfu 20 mkoani Mwanza wamefikiwa na kupewa elimu kuhusiana na saratani ya shingo ya kizazi, kuwaongezea ujuzi watoa huduma za afya wapatao 70 katika ngazi za jamii pamoja na kusaidia upatikanaji wa vifaa vya uchunguzi wa dalili za awali za saratani hiyo katika vituo vya afya mkoani Mwanza ambapo tamati ya mradi huo ni Disemba 31 mwaka huu.

  Aidha mradi huo umesaidia kuwasafirisha akinamama 392 mkoani Mwanza, kwenda katika hospitali za rufaa ikiwemo Bugando kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa Saratani ya shingo ya kizazi ambapo miongoni mwao zaidi ya akina mama 70 wamepatiwa matibabu.
  Awali Mratibu Miradi wa Shirika la TAYOA, Isaack Ghalib, amebainisha kwamba wakati mradi huo unaanza kulikuwa na dhana potofu kuhusiana na ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi ambayo wanawake wengi walikuwa wakiamini wamerogwa na hivyo kuchelewa kufika hospitalini huku baadhi yao wakikimbiwa na waume zao.
  Akizungumza kwa niaba ya Mratibu wa afya ya uzazi mkoani Mwanza, Mratibu wa Afya ya Uzazi ngazi ya jamii, Esperance Makuza, amewahimiza watoa huduma wa afya walionufaika na mafunzo yaliyotolewa katika mradi huo, kuyatumia mafunzo hayo kutoa huduma zinayostahili ili kuwanusuru akina mama na madhara yatokanayo na saratani hiyo.

  Inaelezwa kwamba zaidi ya asilimia 80 ya akina mama wanaougua saratani ya shingo ya kizazi nchini hupoteza maisha kutokana na kuchelewa kufanya uchunguzi na kupatiwa tiba mapema, ikizingatiwa kwamba saratani hiyo hutibiwa ikiwa mgonjwa atawahi matibabu.

  Aidha akina mama wanakumbushwa kuzingatia kanuni bora za kiafya ikiwemo kufanya mazoezi, kujiepusha na uvutaji wa sigara, ulevi pamoja na wapenzi wengi ili kuondokana na maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na masuala ya afya pamoja na ukatili wa kijinsia kwa vijana na wanawake nchini la Tanzania Youth Alliance (TAYOA), Elizaberth Ndakidemi, akizungumza hii leo wakati wa mkutano wa kushirikishana uzoefu, changamoto pamoja na mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa Saratani ya shingo ya kizazi mkoani Mwanza, unaotekelezwa na shirika hilo.#BMGHabari
  Wadau wa afya mkoani Mwanza, wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la TAYOA, Elizaberth Ndakidemi, wakati akizungumza kwenye mkutano wa kushirikishana uzoefu, changamoto pamoja na mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa Saratani ya shingo ya kizazi mkoani Mwanza.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la TAYOA, Elizaberth Ndakidemi, akizungumza hii leo wakati wa mkutano wa kushirikishana uzoefu, changamoto pamoja na mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa Saratani ya shingo ya kizazi mkoani Mwanza, unaotekelezwa na shirika hilo.

  0 0

   Mkaguzi Mkuu wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Mwadini Ahmada Mwadini (kushoto) akifanya ukaguzi katika moja ya Duka la dawa kuangalia usalama wa dawa zinazouzwa na duka hilo lililopo mtaa wa kilimani.
   Mkaguzi Mkuu wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Mwadini Ahmada Mwadini (kushoto) akifanya ukaguzi katika moja ya Duka la dawa kuangalia usalama wa dawa zinazouzwa na duka hilo lililopo mtaa wa kilimani.
  Maafisa ukaguzi kutoka Bodi ya Chakula, Dawa na vipodozi wakiangalia dawa zinazoendelea kuuzwa na duka la Fahud liliopo Mkunazini Mjini Zanzibar.

   Msaidizi Mfamasia Kombo Masoud Khatib akitoa maelezo kwa mkaguzi wa Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi  Amne Nassor Issa wakati maafisa hao walipofanya ukaguzi wa kushtukiza katika maduka ya dawa ya Mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga.

  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kumalizika kwa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume  ni mwanzo wa safari ndefu ya mafanikio  kwa Zanzibar katika azma yake ya kuitumia Sekta ya Utalii kuwa muhimili wa Uchumi Mkuu wa Visiwa vya Zanzibar.
  Alisema azma hiyo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imelenga kutafuta njia nyengine mbadala za kukuza uchumi wake na mapato ya Taifa ambayo kwa sasa yanaendelea kutegemea zao moja tu la karafuu.
  Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Uongozi wa juu wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi { BCEG } ambayo ndio inayojenga  eneo la maegesho ya Ndege kwenye Uwanja wa ndege wa Zanzibar kwenye Makao Makuu yake Jengo la Jian Geing laza Mjini Beijing Nchini China.
  Akimalizia ziara yake ya siku Tano Nchini Jamuhuri ya Watu wa China akiuongoza Ujumbe wa Viongozi Wanne wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif  alisema ongezeko la idadi ya Watalii wanaoingia Zanzibar kwa sasa ni vyema ikaenda sambamba na uimarishwaji wa sekta hiyo muhimu kwa wakati huu.
  Balozi Seif aliueleza Uongozi huo wa juu wa BCEG ukiongozwa na Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Bwana  Fan Jun kwamba Kampuni na Taasisi za ujenzi za China kutokana na umakini wake katika kazi zitaendelea kushirikishwa na Serikali katika uimarishaji wa miundombinu tofauti ya Maendeleo.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza  watendaji na Uongozi mzima wa Kampuni ya Ujenzi ya BCEG kwa kazi kubwa wanayotekeleza katika ujenzi wa miradi  mikubwa ya mawasiliano akiitolea mfano ile ya Bandari na Viwanja vya Ndege.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kushoto akizungumza na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya BCEG Mhandisi Fan Jun  Kushoto kwenye Makao Makuu ya Kampuni hiyo Jengo la Jian Going laza Mjini Beijing Nchini China.
   Meneja Mkuu wa Shirika la Bima la China (SINO SURE) Bwana Wu Han Kulia akibadilishana mawazo na Balozi Seif mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao Mjini Beijing.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wa Pili kutoka Kushoto akiwa na Ujumbe wake akizungumza na Uongozi wa Shirika la Bima la China (SINO SURE) Mjini Beijing akimalizia ziara ya siku Tano Nchini China.
    Balozi Seif Kati kati walioko mbele akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Juu wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya BCEG mara baada ya kumaliza mazungumzo yao ya ushirikiano. Kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Meneja wa Kampuni ya BCEG Bwana Yongchun Chang, Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar DSr.id Salum Mohamed, Katibu Mkuu wake Nd. Khamis Mussa, wakati upande wa kulia ya Balozi Seif ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya BCEG Mhandisi Fan Jun na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mh. Mohamed Ahmed Salum na Msaidizi Meneja wa BCEG wa masuala ya Kimataifa Bwana Shulong Ma. Picha na –OMPR – ZNZ.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  0 0
 • 12/20/16--11:19: Article 6


 • 0 0

  Msemaji wa Polisi, Advera  Bulimba – ACP
  Na Dotto Mwaibale
  JESHI la Polisi nchini limefanikiwa  kumkamata mtuhumiwa wa utapeli anayejulikana kwa jina la  Wilfred Massawe (36) , Kabila mchaga na  mkazi wa  Buza, Temeke jijini Dar es Salaam.

  Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari Dar es Salaam leo, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidi wa Polisi (ACP), Advera  Bulimba amesema  mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia mbinu mbalimbali kutapeli zikiwemo kujitambulisha kama kiongozi wa serikali kwa kutumia mtandao wa Whatsapp,  huku akieleza kuwa yupo nje ya nchi na kuna tatizo la msiba ambao umetokea nchini na unamuhusu na hivyo alikua akitoa maelekezo kwa watendaji wa serikali waweze kusaidia gharama za matibabu hospitalini, gharama za kusafirisha mwili wa marehemu na gharama za mazishi.

  Alisema pia alikuwa akitumia mbinu ya kujifanya kiongozi mkubwa wa dini ya kikristo (Askofu) na kuwaambia waumini na viongozi mbalimbali kuhusu maandalizi ya makongamano ya kidini kwa lengo la kuwaomba michango kuweza kufanikisha makongamano hayo.

  Alitaja baadhi ya matukio aliyofanikiwa kutapeli ni pamoja na kuwatapeli viongozi wa serikali, wafanyabiashara, mameneja na wakurugenzi wa taasisi za umma, wanasiasa pamoja na waumini wa madhehebu ya dini.

  Aidha, matukio yote hayo alikuwa akiyafanya peke yake na alikua akiyaendesha kwa mawasiliano ya njia ya ujumbe mfupi (SMS) bila kuzungumza kwa simu.

  Bulimba alisema Jeshi la Polisi linakamilisha taratibu za kisheria ili mtuhumiwa huyo afikishwe mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

  Jeshi la Polisi nchini linaendelea kutoa tahadhari kwa wananchi wote kuwa makini na mtandao wa matapeli hao na yeyote mwenye  taarifa za matapeli anaombwa kuzifikisha haraka katika kituo chochote  cha Polisi kilicho karibu ili waweze kushugulikiwa haraka.

  0 0


  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina, kulia akiwa katika ziara ya ukaguzi wa Mazingira Keko magulumbasi katika mfereji wa maji taka mseleleko Jijini Dar es salaam mara baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi wanaoishi maeneo hayo. 
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina akimsikiliza Mtaalamu wa Mazingira kutoka NEMC, Jaffar Chimgege katika ziara hiyo ya ukaguzi wa mazingira jijini Dar es salaam. 

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina, akiwa ameongozana na wananchi wanaoishi maeneo ya Keko Magulumbasi katika ziara ya ukaguzi wa Mazingira. 

  0 0

  Akizungumza katika makabidhiano hayo, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kwamba wamejisikia furaha kufikisha vitendea kazi hivyo kwa serikali ya mkoa wa Morogoro.

  Alisema taasisi yao inafanya kazi ya utoaji wa mikopo ya fedha taslimu kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi zilizoidhinishwa pamoja na ile mikopo ya viwanja kwa Watanzania wote, wakiwamo wajasiriamali.“Bayport tumejipanga kuhakikisha kwamba tunaboresha utendaji kazi wa watumishi wetu wa umma kwenye ofisi za mikoa na wilaya, hivyo zoezi la kutoa kompyuta litakuwa endelevu kadri tulivyoelekezwa na serikali baada ya kuwapelekea wazo letu la kununua na kusambaza msaada huu kwao.
  “Pamoja na kutoa misaada mbalimbali ya kijamii, tunaahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ya kutoa huduma bora ya mikopo kwa watumishi wa umma, ambapo kusudio letu ni kuona wateja wetu wanajikwamua zaidi kwa kuanzisha au kuendeleza biashara zao ili waongeze vyanzo vya kipato na kuacha kutegemea mishahara,” alisema Cheyo.Naye Mkuu wa Mkoa Morogoro, Dkt Kebwe, aliwashukuru Bayport kwa kujitolea kwenye jamii na kuwakabidhi kompyuta sita ili ziwasaidie mkoani kwao, akiamini kuwa zitachangia utendaji uliotukuka kwa watumishi wa umma.

  “Tunawashukuru Bayport kwa kuona tunastahili msaada huu mkubwa kwetu, tukiamini kuwa watumishi wetu watafanya kazi kwa moyo ili kuhakikisha kuwa kila mtu anatimiza wajibu wake ipasavyo kama wote tunavyokusudia,” alisema Dkt Kebwe na kuwasihi Bayport waendelee kujitoa kusaidia matatizo yanayoikabili jamii ya Morogoro na Tanzania kwa ujumla.

  Kwa mujibu wa Kebwe, Mkoa wao upo kwenye mchakato mkubwa wa kupambana na changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuupatia maendeleo Mkoa wao wa Morogoro.Mikoa na wilaya mbalimbali za Tanzania Bara zinatarajiwa kunufaika na misaada ya kompyuta kwa ofisi za umma kama dira na dhamira ya taasisi ya Bayport kurahisisha utendaji kazi utakaochangia kuleta maendeleo hapa nchini.


  Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, kushoto, akimkabidhi moja ya kompyuta sita zilizotolewa na Taasisi yao kwa ajili ya kuusaidia Mkoa wa Morogoro katika vifaa vya ofisini ili kurahisisha utendaji kazi. Anayepokea ni Mkuu wa Mkoa Morogoro, Mheshimiwa Dkt Stephen Kebwe, leo mkoani Morogoro. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.

  TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo imekabidhi kompyuta sita kwa uongozi wa Mkoa wa Morogoro, kwa kupitia Mkuu wake wa Mkoa, Mheshimiwa Dkt Stephen Kebwe, ili zisaidie utendaji kazi wa watumishi wa umma katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya Mvomero, Manispaa ya Morogoro Mjini pamoja na Morogoro Vijijini.

  Ugawaji wa kompyuta hizo ni mwendelezo wa taasisi hiyo kugawa vitendea kazi hivyo baada ya kumkabidhi kompyuta 125 kati ya 205 kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Angellah Kairuki, huku kompyuta zote zikiwa na thamani ya Sh Milioni 500.
  Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo mwenye miwani akifurahia jambo na Mkuu wa Mkoa Morogoro, Mheshimiwa Dkt Stephen Kebwe mwenye suti nyeusi. Kulia kwa Cheyo ni Afisa Tawala wa Mkoa Morogoro, Victor Ndiva na nyuma ni Mercy Mgongolwa, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services.
  Hapa ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo mwenye miwani akipiga picha ya furaha na Mkuu wa Mkoa Morogoro, Mheshimiwa Dkt Stephen Kebwe mwenye suti nyeusi. huku akiwa ameshikana mkono na Afisa Tawala wa Mkoa Morogoro, Victor Ndiva. Nyuma kwa Cheyo ni Mercy Mgongolwa, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services.

  0 0

  Mkuu wa Chuo cha Ualimu cha Al Haramain, Mwaalim Suleiman Urassa, akizungumza wakati wa mahafali hayo, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
  Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Mwalimu Nuhu Jabir, akitoa taarifa ya shule hiyo, wakati wa mahafali hayo.
  Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Imam Mkuu wa Msikiti wa Al Maamur na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa, Sheikh Issa Othman, akitoa hotuba yake, wakati wa mahafali hayo hivi karibuni.
  Mhitimu Zuhura Abdallah wa Ngazi ya Cheti wa Elimu ya Awali, akipokea cheti chake kutoka kwa mgeni rasmi, Sheikh Issa Othman.
  Wahitimu wa Ualimu na wa Kidato cha Nne wakiingia kwenye viwanja vya mahafali hayo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA  0 0


  Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mteule Mhe. Kisare Makori akishuhudiwa na viongozi wapya wa CCM aliowateua hivi karibuni. Kutoka kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole, Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Ngemela Eslom Lubinga na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg. Rodrick Mpogolo walipoenda kujitambulisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2016.
  Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mteule Mhe. Kisare Makori (kushoto) pamoja na viongozi wapya wa CCM aliowateua hivi karibuni. Kutoka kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole, Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Ngemela Eslom Lubinga na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg. Rodrick Mpogolo walipoenda kujitambulisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2016.
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mteule Mhe. Kisare Makori (wa pili kushoto) akibadilishana mawasiliano na na viongozi wapya wa CCM walioteuliwa hivi karibuni. Kutoka kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg. Rodrick Mpogolo na kushoto ni Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Ngemela Eslom Lubinga walipoenda kujitambulisha kwa Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2016. PICHA NA IKULU

  0 0
 • 12/20/16--12:36: Esther Katinde' Burial Fund
 • Esther Katinde' Burial Fund

  On Saturday morning (12/17/16) Esther Katinde entered into surgery at the Orlando Regional Medical Center for complications due to a condition called Scleroderma. Esther passed away during the procedure. She suffered tremendously with physical pain along with the many hardships related to getting and receiving medical care. 

  We are asking you to assist with the final arrangements. She was a wonderful wife, mother, friend, and Christian woman. She will be dearly missed by many. We hope to bury Esther in her native home as she requested. Please pray with and for us. We are grateful for your kindness and generous support.
  Help spread the word!


  for any condolence greetings you can reach out with this information.
  Jina: Joel Katinde
  Address: 1722 Montview Street, Orlando Fl, 32805
  Phone: 407-496-3772
  WhatsApp: 407-496-3772
  Facebook: Joel Katinde

  www.gofundme.com/Esther-Katinde-burial-fund

  0 0

  Na Stella Kalinga .

  Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation imekabidhi Serikali jumla ya Nyumba 28 kati ya 48 zinazotarajiwa kujengwa kwa ajili ya watumishi wa Idara ya Afya na Majengo Mawili ya Upasuaji kwa ajili ya huduma za akina mama wajawazito Mkoani Simiyu.

  Akipokea na kufungua Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya cha Ngulyati Wilayani Bariadi na Nyumba za Watumishi katika Hospitali ya Mkula wilayani Busega, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto , Mhe.Ummy Mwalimu ameishukuru Taasisi hiyo kwa kuuunga mkono Serikali katika uboreshaji wa huduma za Afya, hasa katika ujenzi wa miundombinu ya Afya.

  Mhe.Waziri amesema Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuboresha huduma za Afya kwa kuongeza kiwango cha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, miundombinu ya Afya ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Hospitali, Vituo vya Afya, Zahanati na Majengo ya Upasuaji, hivyo upatikanaji wa majengo hayo utasaidia wananchi wa maeneo husika kupata huduma zinazotakiwa. 

  Mhe.Waziri ameongeza kuwa Serikali imeanza kwa kuboresha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa kuongeza bajeti, ambapo kwa Mwaka 2015 zilitengwa jumla ya shilingi bilioni 31 na mwaka 2016 zimetengwa shilingi bilioni 51.

  Amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine imejipanga kujenga kiwanda cha kutengeneza dawa Mkoani Simiyu, hivyo pindi kiwanda hicho kitakapokamilika dawa za Vituo Mbalimbali vya kutolea huduma za Afya zitanunuliwa Simiyu.

  Aidha, Mhe.Ummy Mwalimu ameutaka Uongozi wa Mkoa uhakikishe unasimamia ukusanyaji wa mapato katika Vituo vyote vya kutolea huduma za Afya, ili sehemu ya mapato hayo itumike kununulia dawa na vifaa tiba kwa lengo la kuwahakikishia wananchi upatikanaji wa huduma bora za afya.
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu(wa tatu kulia) akikata utepe katika ufunguzi wa Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya Ngulyati lililokabidhiwa kwa Serikali na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation.
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (kushoto) akisoma Jiwe la ufunguzi wa Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya Ngulyati lililokabidhiwa kwa Serikali na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation.
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu(wa pili kulia) akikagua baadhi ya vifaa tiba mara baada ufunguzi wa Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya Ngulyati lililokabidhiwa kwa Serikali na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Daudi Manongi-MAELEZO .

  Bodi ya Nishati Vijijini (REB) imemteua Mhandisi Boniface Gissima Nyamo-Hanga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala Dk.Lutengano Mwakahesya aliyestaafu mwezi Juni 2016.

  Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini Dk.Gideon Kaunda inaeleza kuwa uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria namba 8 ya mwaka 2005 ya Nishati Vijijini katika kikao kilichofanyika Tarehe 17 Desemba 2016.

  Aidha taarifa hiyo inaeleza kuwa kabla ya uteuzi huu Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

  Imeongeza kuwa Mhandisi Gissima ana uzoefu wa miaka 20 katika Sekta ya Nishati na pia ameshika nyadhifa mbalimbali tangu mwaka 2008 alipoajiriwa REA.

  Mbali na hayo Mhandisi huyu amehitimu Shahada ya Uhandisi katika fani ya Umeme, Shahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Uhandisi,Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara (MBA) zote kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Stashahada ya Juu ya Sheria na Upatanishi na Usuluhishi ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Dar es Salaam.

  Bodi ya Wakala wa Nishati ya Umeme Vijijini (REA) inaomba sekta mbalimbali kumpatia ushirikiano Mhandisi Boniface Gissima Nyamo-Hanga ili kumuwezesha  kutekeleza majukumu na malengo yake.

  Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Boniface Gissima Nyamo-Hanga


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Vijana wa kitanzania wahimizwa kutambua fursa za kiuchumi na kupambana na changamoto mbalimbali za kiuchumi zinazowazunguka na kujihusihsa katika shughuli  ili kuweza kujiletea maendeleo na kupunguza umaskini.

  Akizungumza wakati wa semina elekezi ya vijana iliyoendeshwa na Taasisi ya MIBOSCO wakati wa ufunguzi wa jukwaa la uchumi ka kuwawezesha vijana kiuchumi na kuwakutanisha takribani vijana 200, Afisa Vijana Mkoa wa Dar es salaam Nasalida Njashi amesema kuwa vijana wanatakiwa waache uoga wanatakiwa kujitokeza mbele ili kuweza kupambana na changamoto mbalimbalikwa ajili ya kuleta maendeleo.

  Njashi amesema hayo mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa MIBOSCO Moses Meena na kuwataka viongozi hao kutokaa nyuma na kusubiri misaada bali wanatakiwa waunde vikundi vya vijana wachache ili kuweza kupata mikopo ya riva nafuu kutoka kwenye mfuko wa serikali wa fungu la asilimia kumi kwa ajili ya vijana na wanawake ambapo itawasaidia kwenye kuanzisha miradi mbalimbali.

  Mkurugenzi Mkuu wa MIBOSCO Moses Meena amesema kuwa jukwaa lao limedhamiria kuleta mwamko na hamasa chanya kwa vijana na katika harakati za kujikomboa kiuchumi na mafunzo hayani mwendelezo wa shughuli zinazofanywa na Taasisi hiyo ikiwa ni harakati za kupambana na umaskini.

  Katika jukwaa hilo kulikuwa na Afisa kutoka Baraza la Taifa la uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi George Maura na kuwataka vijana kuacha kusubiri kuanzishiwa miradi au masuala mbalimbali ya kiuchumi na kuwataka kuunda umoja wao kwa ajili ya kupata mikopo kutoka serikali, pamoja na kuwapatia sifa uongozi wa MIBOSCO kwa juhudi kubwa za kuwapatia ellimu ya ujasiriamali vijana wa Kunduchi Mtongani.

  Jukwa hilo lilihudhriwa pia na mtangazaji wa Clouds Maoud Kipanya, Wawakilishi kutoka NSSF na benki ya ACB kama wadau wa maendeleo.
  Afisa Vijana Mkoa wa Dar es salaam Nasalida Njashi akizungumza na vijana wakati wa jukwaa la uchumi la kuwawezesha vijana kiuchumi liloandaliwa na Taasisi ya MIBOSCO.

   Afisa Vijana Mkoa wa Dar es salaam Nasalida Njashi (katikati)akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa MIBOSCO Moses Meena (kushoto), Afisa wa Baraza la Taifa la uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi George Maura, Meneja wa NSSF Tawi la Mbezi Beach Stella Kabyemela na Mwakilishi kutoka benki ya ACB.

   Viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya vijana waliojitokeza kwenye Jukwaa la uchumi la kuwawezesha vijana kiuchumi.
  Afisa Vijana Mkoa wa Dar es salaam Nasalida Njashi akiangalia baadhi ya bidhaa zilizotengezenezwa na vijana wajasiriamali walio chini ya MIBOSCO.

  0 0

  Na Ramadhani Ali/Maelezo.

  Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) litapatiwa hati ya kuuza karafuu hai kwenye soko la Ulaya baada ya kutiliana saini na Kampuni ya Ganefryd ya Denmark makubaliano ya kuimarisha kilimo hai cha mazao tofauti (organic) kwa kuanzia na kilimo cha karafuu.

  Sherehe za kutiliana saini makubaliano hayo zilifanyika katika ofisi za eneo tengefu Saateni na ZSTC iliwakilishwa na Mkurugenzi Mwendeshaji Dkt. Said Seif na Kampuni ya Genefryd iliwakilishwa na Afisa wake Bw. Pale Christeusen.

  Akizungumza baada ya kutia saini makubaliano hayo, Dkt. Said amesema Zanzibar imekuwa ikifanya biashara ya karafuu kwa miaka mingi lakini hivi sasa itapanua wigo wa kuuza karafuu hai Ulaya na kupata faida kubwa.

  Alisema ili Zanzibar iweze kutoa karafuu hai tahadhari kubwa inapaswa kuchukuliwa wakati wa kuotesha miche, ukuaji wake na kufikia wakati wa kuzaa bila ya kuingizwa aina yoyote ya mbolea zenye kemikali. 

  Ameongeza kuwa uangalizi mkubwa pia unahitaji katika mchakato mzima wa kushughulika kilimo hicho kuanzia hatua ya kuchuma, kuanika, kuzihifadhi mpaka kuzisafirisha hivyo amewaomba wananchi kuunga mkono kuingia katika kilimo hai kwa vile karafuu ndio tegemeo lao na Taifa kwa jumla. 

  Amesema sambamba na kuanzisha kilimo hai cha zao la karafuu Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSTC amewataka wananchi kuendeleza zao hilo katika mfumo wa kawaida kwa kuongeza upandaji miche na kuacha tabia ya kukata mikarafuu kwa ajili ya kuni, kufanyia mkaa na kujengea.

  Afisa wa Kampuni ya Genefryd Bw. Pale Christeusen amesema hatua ya kutiliana saini makubaliano hayo ni kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili na kuongeza kipato cha mkulima wa karafuu na kuiongezea Serikali mapato.

  Bw. Christeusen amewashauri wakulima wa karafuu Zanzibar kuongeza kilimo hai cha karafuu kwa vile kinafaida kubwa katika soko la Ulaya.
   Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC) Dkt. Said Seif akitiliana saini na mwakilishi wa Kampuni  Denmark Bw. katika ofisi za Shirika hilo ziliopo Saateni Mjini Zanzibar.

   Wafanyakazi wa  ZSTC wakisafisha karafuu hai kabla ya kuhifadhiwa kwenye mifuko maalum kwa ajili ya kuuzwa kwa wateja. 
   Afisa Masoko wa ZSTC Nassor Salum Nassor akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kuhusu utaratibu unaotumika wa kupokea na kuzihifadhi karafuu hai kabla ya kuingizwa sokoni.
  Picha na Makame Mshenga. 


  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Serikali imesimamisha shughuli za Mfuko wa Wakfu wa Kuendeleza Zao la Korosho ili kupisha uchunguzi wa matumizi ya fedha za mfuko huo.

  Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Mfuko huo kushindwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu pamoja na kuwepo kwa malalamiko ya muda mrefu kuhusu utendaji wa mfuko huo.

  Uamuzi huo umechukuliwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafanikio na changamoto ya zao hilo.

  Dkt. Tizeba alisema kuwa lengo la uanzishwaji wa mfuko huo lililoafikiwa na Serikali pamoja na wadau wa korosho limekuwa halifanani na utekelezaji wake kwani maendeleo yote yanayoonekana kwenye zao hilo hayatokani na uwepo wa mfuko bali yanatokana na nguvu ya Serikali.

  “Baada ya kutafakari utendaji wa mfuko huo tumegundua kuwa mfuko umeshindwa kutimiza malengo yaliyodhamiriwa, umeshindwa kusimamia na kutekeleza maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Bodi ya Korosho hivyo tumeamua kusitisha shughuli za mfuko huo na kuanzia leo shughuli hizo zitatekelezwa na Bodi ya Korosho mpaka hapo tutakapotoa maelekezo mengine.”alisema Waziri huyo.

  Waziri aliongeza sababu nyingine za kusitishwa kwa Mfuko huo ni kujihusisha na vitendo vinavyohujumu wakulima wa zao hilo hasa wakati wa ununuzi wa pembejeo pamoja na kununua viuatilifu vilivyo chini ya kiwango kwa bei kubwa, matumizi mabaya ya fedha kinyume cha Sheria na Kanuni za mfuko pamoja na kushindwa kutekeleza agizo la Serikali kwa kuweka fedha kwenye amana za muda maalumu katika Benki mbalimbali badala ya kupeleka Benki Kuu.

  Aidha, Dkt. Tizeba alimtaka Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania anapowasilisha fedha zilizokusanywa na watu wanaosafirisha korosho nje ya nchi kuwasiliana kwanza na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho ili kufahamu usimamizi na utaratibu wa fedha hizo.

  Kwa upande mwingine, Dkt. Tizeba ameizuia Menejimenti ya mfuko huo kufanya muamala wowote wa fedha za mfuko mpaka hapo maelekezo ya hatima yao yatakapotolewa na badala yake miamala yote itafanyika kwa utaratibu utakaopangwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.

  Ameiagiza Bodi ya Korosho kusimamia kwa haraka jukumu la upatikanaji wa pembejeo na viuatilifu kwa sababu msimu wa zao hilo umekaribia.

  0 0

  ZAIDI ya wandesha bodaboda 500 wameweza kusajiliwa na mfuko wa Jamii wa GEPF katika fao la ‘Jikwamue Scheme’ ambapo huko wanapata huduma mbalimbali ikiwemo mkopo na siku za karibuni wataweza kufaidika na huduma za afya.

  Hayo yalisemwa Jijini Dar es Salaam na Ofisa Masoko, Elivine Faini, wakati wa kufunga mafunzo ya waendesha boda Jijini Dar es Salaam yaliyokuwa yakifanyika katika maeneo mbalimbali Jijini humo, ambapo GEPF walikuwa mmoja wa watoa mada.

  Faini alisema wameamua kujikita kwa kundi hilo kutokana na ukweli kwamba hakuna mfuko ambao mpaka sasa umewafikia na kuongeza kwamba nao wana mahitaji kama ilivyo kwa watu wa sekta nyingine katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

  Alisema ili kuweza kufaidika na fao hilo, mwendesha boda anatakiwa anatakiwa achangie sio chini ya miezi sita, ambapo ataweza kupata mkopo wa boda na kuondokana na adha ya kuajiriwa kwa kumiliki boda yake mwenyewe au kufungua biashara nyingine nje ya bodaboda na hivyo kujiongezea kipato.
  Mkuu wa Wilaya Temeke,Felix Lyaniva akimkabidhi cheti Mwakilishi wa Darasa la Kibaha,Akas Kiruwa katika hafla ya kuwatunuku vyeti madelewa wa pikipiki leo jijini Dar es Salaam.
  Viongozi wa Madara ya Mbalilmbli wa madereva wa pikipiki wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla ya kuwatunuku vyeti madelewa wa pikipiki leo jijini Dar es Salaam.
  Madereva wa pikipiki wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Temeke,Felix Lyaniva katika hafla ya kuwatunuku vyeti madelewa wa pikipiki leo jijini Dar es Salaam.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1469 | 1470 | (Page 1471) | 1472 | 1473 | .... | 3285 | newer