Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

Wasanii wapewa warsha juu ya masuala ya Ukombozi wa Mwanamke

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi (kulia) akifungua Warsha ya Wasanii Juu ya Masuala ya Ukombozi wa Mwanamke Kimapinduzi hasa kwa kuangalia vipaumbele vya TGNP katika sekta ya Afya, Maji, Elimu, Kilimo na Viwanda. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliandaliwa na TGNP Mtandao. Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi (kulia) akifungua Warsha ya Wasanii Juu ya Masuala ya Ukombozi wa Mwanamke Kimapinduzi hasa kwa kuangalia vipaumbele vya TGNP katika sekta ya Afya, Maji, Elimu, Kilimo na Viwanda. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliandaliwa na TGNP MtandaoMajadiliano katika warsha hiyo yakiendelea. Majadiliano katika warsha hiyo yakiendelea.Baadhi ya maofisa wa TGNP Mtandao wakiwa katika warsha hiyo. Baadhi ya maofisa wa TGNP Mtandao wakiwa katika warsha hiyo.Baadhi ya washiriki wa washa ya Wasanii Juu ya Masuala ya Ukombozi wa Mwanamke Kimapinduzi hasa kwa kuangalia vipaumbele vya TGNP katika sekta ya Afya, Maji, Elimu, Kilimo na Viwanda. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliandaliwa na TGNP Mtandao. Baadhi ya washiriki wa washa ya Wasanii Juu ya Masuala ya Ukombozi wa Mwanamke Kimapinduzi hasa kwa kuangalia vipaumbele vya TGNP katika sekta ya Afya, Maji, Elimu, Kilimo na Viwanda. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliandaliwa na TGNP Mtandao.Baadhi ya washiriki wa washa ya Wasanii Juu ya Masuala ya Ukombozi wa Mwanamke Kimapinduzi hasa kwa kuangalia vipaumbele vya TGNP katika sekta ya Afya, Maji, Elimu, Kilimo na Viwanda. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliandaliwa na TGNP Mtandao. Baadhi ya washiriki wa washa ya Wasanii Juu ya Masuala ya Ukombozi wa Mwanamke Kimapinduzi hasa kwa kuangalia vipaumbele vya TGNP katika sekta ya Afya, Maji, Elimu, Kilimo na Viwanda. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliandaliwa na TGNP Mtandao

RC MAKONDA AANZA UJENZI WA MAHAKAMA 20

$
0
0
Na  Anthony Johny Globu Jamii.

 MKUU wa Mkoa Wa Dar es salaam Paul Makonda ameahidi kuanza Ujenzi wa Mahakama 20 za Mwanzo katika Mkoa wa Dar es salaam ili kupunguza msongamano wa mahabusu katika vituo vya polisi na Magereza.

Hayo ameyasema leo Makonda wakati alipotembelewa na Waziri wa Katiba na Sheria, Harrison Mwakyembe,  ofisini kwake, amesema ujenzi huo wa Mahakama utapunguza mzigo kwa Serikali na itasaidia wakazi  walio nje kidogo jiji la Dar es salaam kuweza kupata haki kwa wakati.

Makonda alitoa wito kwa badhi ya Wadau mbalimbali kujitokeza ili kusaidia ujenzi wa Mahakama hizo, Amesema mtu yeyote atakaye kwenda kinyume na sheria hatakama alisaidia kujenga Mahakama,  sheria itafata mkondo wake.

Nae Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe amempongeza Makonda kwa  kutafuta vijana wanasheria na kuwapeleka katika kila Wilaya katika  jiji la Dar es salaam ilikuweza kuwaidia  wananchi  kuwanyonge kupata haki katika masuala ya kisheria.

" Sisi kama Wizara tunampongeza Mkuu wa Mkoa  kwa kuwatafuta vijana mbambali wanasheria na kuwapeleka katika kila Wilaya ilikuweza kuwasaidia wananchi hawa kupata msaada wa kisheria ilikupunguza uonevu kwa baadhi ya watu".amesema Mwakyembe.

Amesema katika ujenzi huo wa Mahakama za mwanzo kutawasaidia wakazi mbalimbali wa jiji la  Dar es salaam kuwa na uhakika wa kupata haki kwa wakati mwafaka na kupunguza baadhi ya migogoro katika jamii na serikali..
 Waziri wa  Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari juu ya amempongeza Makonda kwa  kutafuta vijana wanasheria na kuwapeleka katika kila Wilaya ya Dar es salaam ilikuweza kuwaidia  wananchi wanyonge katika masuala ya kisheria, leo jijini  Dar es Salaam. Kukia ni Mkuu wa Mkoa Wa Dar es salaam Paul Makonda. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
 Mkuu wa Mkoa Wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujenzi  wa Mahakama utapunguza mzigo mkubwa kwa Serikali na itasaidi wakazi Nje ya Dar es salaam na Ndani katika  kupata Haki Zao za kisheria kwa haraka leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa  Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe
 Waziri wa  Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe akisanikitambu cha wageni katika ofisi ya mkuu wa mkoa leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Katibu Mkuu wa Sheria na Katiba,  Profesa Sifuni Mchome,  Naibu Katibu Mkuu wa Sheria na Katika, Amon Mpanju

PROF. MBARAWA: ATOA TAHADHARI UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewatahadharisha watanzania kuepuka vitendo vya uharibifu wa miundombinu ya barabara husasan katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

Ameyasema hayo wakati akikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Dodoma-Babati yenye urefu wa KM 188.1, sehemu ya Mela-bonga ambapo imeripotiwa kuwepo vitendo vya uharibifu wa miundombinu kwa muda mrefu.



'Napenda kutoa wito kwa watanzania kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka kwa kuacha vitendo vya kuchoma matairi barabarani, kwani hali hii hupelekea kuharibu barabara kwa kiasi kikubwa ambazo Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuzijenga", amesema Prof.Mbarawa.



Aidha, amekemea vitendo vya baadhi ya madereva kumwaga mafuta barabarani na baadhi ya wananchi kupitisha mifugo kwenye barabara ambapo vyote kwa pamoja vinaharibu miundombinu ya barabara.

Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Serikali ikiwemo kuwaripoti wale wote wanaohujumu miundombinu ya barabara nchini.



Sambamba na hilo, amewaasa madereva wa vyombo vya moto kuwa makini barabarani kwa kuzingatia sheria za alama za barabara ikiwemo kuendesha vyombo hivyo kwa mwendo unaotakiwa ili kudhibiti ajali za barabarani zinazoweza kuepukika.



Kuhusu mradi wa ujenzi wa barabara ya Dodoma- Babati yenye urefu wa KM 188.1, Waziri Prof. Mbarawa amesema kuwa barabara hiyo inatarajiwa kukamilika mwakani kwani kwa sasa ipo katika hatua za mwisho za ujenzi wake.



"Kazi inaenda kwa kasi kubwa, matumaini yangu ni kwamba ifikapo mwishoni mwa mwaka 2017, barabara hii itakamilika kwa viwango bora tulivyokubaliana kwenye mkataba", amesisitiza Profesa Mbarawa.

Amefafanua kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutapunguza umbali wa masaa kwa abiria wanaosafiri kupitia njia ya Singida wanaotoka Dodoma na mikoa ya jirani kuelekea Manyara, Moshi na Arusha.



Ameongeza kuwa barabara hiyo itasaidia kuiunganisha Tanzania na Nchi za kutoka Kusini na Kaskazini mwa bara la Afrika, hivyo kufungua fursa za kibiashara kwa wananchi na kuongeza pato la Taifa kupitia sekta ya utalii.

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mkoa wa Dodoma, Eng. Leonard Chimagu, amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kusimamia ujenzi wa barabara hiyo kwa viwago vinavyostahili na kuahidi kukamilika kwa wakati.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.


 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya H.P Gauff, Eng. Kini C. Kuyonza (wa tatu kulia), inayosimamia mradi wa ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga yenye urefu wa KM 88.8. wakati alipokagua barabara hiyo, wilayani Babati.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiongea na mmoja wa madereva wa Basi linalofanya safari zake katika mikoa ya Dodoma-Babati, wakati alipokagua ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga yenye urefu wa KM 88.8.
 Ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga yenye urefu wa KM 88.8 inayojengwa kwa kiwango cha lami ukiendelea. Mradi huo unajengwa na Mkandarasi wa Kampuni ya M/s China Railway Seventh Group na unatajiwa kukamilika mwezi Agosti mwakani.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akishindilia nondo kwenye moja ya ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga yenye urefu wa KM 88.8, inayojengwa kwa kiwango cha lami, alipokuwa akikagua mradi huo.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

NAIBU KATIBU MKUI MPYA WA CCM AKABIDHI MADAWATI 200 YALIYOCHANGWA NA CCM MOROGORO

$
0
0


Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akikabidhiwa madawati 200 na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro, Karogeris. Madawati hayo yametolewa na CCM mkoa huo kwa ajili ya kuiunga mkono serikali katika suala la upatikanaji madawati
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akimpongeza Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk. Steven Kebwe wakiwa wamekalia madawati hayo bada ya makabidhiano.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi kwa jumla nye ya Ofisi ya CCM mkoa wa Morogoro leo


Karogeris akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara kufungua semina hiyo.

BINTI WA KITANZANIA ANYAKUA TUZO YA MJASIRIAMALI BORA AFRIKA

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 19.12.2016

MRADI MKUBWA WA UMEME WA BACKBONE UMEKAMILIKA, KUZINDUALIWA JANUARI

$
0
0
NA K-VIS BLOG, Iringa

MRADI wa umeme wa Backbone wa ujenzi wa njia kuu ya umeme ya msongo wa Kilovolti 400 ya urefu wa Kilomita 670 kutoka Iringa hadi Shinyanga kupitia mikoa ya Dodoma na Singida, umekamilika kwa asilimia 100, Meneja wa Mradi huo, Mhandisi  Khalid Reuben James amewaambia wahariri wa vyombo vya habari mjini Iringa leo Desemba 19, 2016.

Pia  mradi huo unaohusisha kukamilika kwa upanuzi wa vituo vine vya kupoza na kusambaza umeme kwenye mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga utawezesha kuvipatia umeme vijiji takriban 121, vinavyopitiwa na mradi huo, alisema Mhandisi James.

“Mradi huu ni wa muhimu sana kwenye gridi ya taifa kwa sababu utaongeza uwezo wa kusafirisha umeme kutoka kanda ya Kusini Magharibi, ambako kuna vyanzo vingi vya umeme na kupeleka Kanda ya Kaskazini Magharibi ambako kuna shughuli nyingi za kiuchumi ikiwemo migodi ya madini.” Alifafanua Mhandisi James.

Kwa mujibu wa Mhandisi huyo, mradi huo ulianza mwaka 2013, na ulikadiriwa kugharimu kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 470, ambazo zimetolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na wafadhili wakiwemo, Benki ya Dunia, dola za Kimarekani, milioni 150, Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB),  na Shirika la Maendeleo la Kijapani, (JICA), Dola za Kimarekani milioni 129.7, Benki ya Uwekezaji ya nchi za Jumuiya ya Ulaya, (EIB), Dola za Kimarekani milioni, 134.5, Shirika la Kiuchumi la Maendeleo ya Korea ya Kusini, (EDCF), Dola za Kimarekani milioni 36.416, na Serikali ya Norway, Sweden na Tanzania, kupitia kwa wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dola za Kimarekani milioni 33.4.

“ Ndugu zangu, mradi huu unatoa hakikisho kwa serikali kuwa mipango yake ya kujenga uchumi wa viwanda unawekana pasina shaka, kwani mradi huo mkubwa, utawezesha sasa, kuwapatia wateja umeme ulio bora na wa uhakika,” alsiema.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, wako kwenye ziara ya kutembelea mradi huo ambao unatarajiwa kuzinduliwa rasmi mapema mwezi Januari, 2017.



 Meneja wa mradi mkubwa wa umeme wa Backbone, Mhandisi Khalid Reuben James, akitoa maelezo kwa wahariri (jawapo pichani), walipotebelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Tagamenda kilichoko nje kidogo ya mji wa Iringa, wakati wa ziara ya wahariri kukagua ujenzi wa mradi wa Backbone unaotoka mkoani Iringa hadi Shinyanga kupitia mikoa ya Dodoma na Singida, Desemba 19, 2016
 Wahariri wakitembelea mitambo ya umeme kituo cha Tagamenda
 Mhandisi huyu wa Tanesco, akitumia ramani ya mradi huo kuwaelimisha wahariri ukubwa wa mradi huo
 Wahariri wakiangalia nguzo zinazobeba nyaya (conductors), za mradi wa Backbone, kwenye kituo cha Tagamenda.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA WAWILI NA WAKURUGENZI WATATU WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi akizungumza na vyombo vya habari wakati wa kutangaza uteuzi wa Wakuu wa Wilaya wawili na Wakurugenzi watatu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, uliofanywa na Rais Dkt. Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 19 Desemba, 2016 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya wawili na Wakurugenzi watatu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Kisare M. Makori kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Bw. Kisare M. Makori anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Humphrey Polepole ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Itikadi na Uenezi.

Halikadhalika, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Avod Mmanda Herman kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara iliyopo katika Mkoa wa Mtwara.
Bw. Avod Mmanda Herman anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Khatib M. Kazungu ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Ramadhan Geodrey Mwangulumbi kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga iliyopo Mkoani Shinyanga.

Bw. Ramadhan Geodrey Mwangulumbi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Lewis Kalinjuna ambaye anastaafu kwa mujibu wa Sheria.
Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw Rojas John Romuli kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda iliyopo katika Mkoa wa Katavi.
Bw. Rojas John Romuli anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ngalinda Hawamu Ahmada aliyefariki dunia hivi karibuni.

Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Rashid K. Gembe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga iliyopo katika Mkoa wa Tanga.

Bw. Rashid K. Gembe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Mkumbo Emmanuel Barnabas ambaye uteuzi wake ulitenguliwa hivi karibuni.
Uteuzi wa huu unaanza mara moja na wateule wote wanatakiwa kuripoti Makao Makuu ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mara wapatapo taarifa hii.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
19 Desemba, 2016 

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA WATENDAJI WAKUU WA MAKAMPUNI YA CHINA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini China kuja kuwekeza nchini katika maeneo mbalimbali ikiwemo uvuvi katika bahari,madini, utalii, ujenzi wa viwanda na miundombinu.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Watendaji Wakuu wa makampuni makubwa kutoka nchini China ambao walikuja hapa nchini kutafuta fursa za uwekezaji.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wawekezaji hao kuwa Tanzania ni nchi salama kwa ajili ya kuwekeza kutokana na amani iliyopo na kwa sasa Serikali inaendelea na mkakati kuondoa vikwanzo vinavyokwamisha uwekezaji ikiwemo ukiritimba na rushwa nchini.

Amesema Tanzania na China zinamahusiano mazuri na ya muda mrefu hivyo ni muhimu mahusiano hayo yakaendelea kuimarishwa zaidi kama hatua ya kukuza biashara kati ya nchi hizo mbili kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa Tanzania na China.
Amesisitiza muhimu wa kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya Chama cha Wafanya Biashara wenye Viwanda na Wakulima nchini (TCCIA) na Chama cha Wafanya biashara kutoka China kama hatua ya kuimarisha kwa angalia fursa bora za uwekezaji kati ya China na Tanzania.

Makamu wa Rais pia ameishukuru nchi ya China kwa kuichangua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi Nne za bara la Afrika kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda.

Kwa upande wao, Watendaji hao wa makampuni makubwa kutoka nchini China wamesema kwa sasa wapo mbioni kujenga kiwanda kikubwa cha kutengeneza vifaa tiba katika eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam na wameshapewa ekari 160 kwa ajili ya kujenga kiwanda hicho.

Watendaji hao wameiomba serikali ya Tanzania isaidie kuhakikisha pindi mradi huo utakapoanza kujengwa huduma za msingi ikiwemo umeme na maji zinapatikana kwa urahisi kwenye eneo hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Chama Cha Wafanyabiashara wa China nchini Tanzania ambao walimtembelea ofisini kwake leo.

BAADA YA UZINDUZI, SASA NI SHOO KATIKA KUMBI MBALIMBALI- FELLA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

UONGOZI wa bendi ya mpya ya muziki wa taarab nchini 'Yah TMK Modern Taarab', umewataka wapenzi wa muziki huo, kuipokea bendi yao ambayo inaanza rasmi maonyesho yake ya katika kumbi mbalimbali hapa nchini. 

Mkurugenzi wa bendi hiyo Said Fella,alisema kuwa mara baada ya kufanya utambulisho wa bendi yao uliyofanyika Jumamosi kwenye Ukumbi wa Dar Live, Yah TMK inaanza rasmi maonyesho yake katika kumbi mbalimbali za burudani hapa nchini. 

Fella alisema bendi hiyo itaanza onesho lake la kwanza Desemba 23 mwaka huu kwenye ukumbi wa CCM Kigamboni wakati mkesho wa Christmas watakuwa kwenye Ukumbi wa Mpo Africa uliopo Tandika. 

Alisema Desemba 25 bendi hiyo itakuwa ndani ya ukumbi wa Lekem uliopo Buguruni na siku ya Desemba 26 itakuwa na Lanch Time Mazense. Fella alisema kuwa bendi yao imejipanga kutoa buriuudani ya aina yake kama wapenzi waliyokuja kwenye utambulisho walivyojionea. 

"Lengo ni kutoa burudani nasi tumejipanga kutoa burudani ya aina yake, wanamuziki wapo vizuri na kila mtu anajisikia kufanya kazi yake kivizuri kabisa"alisema Fella. 

Bendi hiyo yenye wanamuziki mbalimbali nguli, akiwepo Mwanahawa Ali, Fatma Mcharuko, Aisha Vuvuzela, Omar Tego, Mauwa Tego na wapiga vyombo Mohamed Mauji, Mussa Mipango, Chid Boy (kinanda) na Babu Ally Kichupa. 
Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Taarab, Mwanahawa Ally akitumbuiza kwenye usiku wa uzinduzi wa bendi ya Yah TMK Taarab.
Mwanamuziki wa Taarabu, Omar Tego akitumbuiza kwenye usiku wa uzinduzi wa bendi ya Yah TMK Taarab. 
wanamuzi wa bendi ya Yah TMK Taarab wakitoa burudani.

MWIGULU NCHEMBA AINGILIA KATI SAKATA LA MAUAJI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI MKOANI PWANI

$
0
0

NA VICTOR MASANGU, PWANI

KUTOKANA na kuwepo kwa ongezeko la wimbi la migogoro ya ardhi kila kukicha katika baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Pwani kati ya jamii ya wakulima na wafugaji na kupelekea wakati mwingine kuibuka kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ambayo yanasababisha hali ya uvunjifu wa amani na baadhi ya viongozi na wananchi wengine kupoteza maisha kikatili kimeundwa kikosi kazi maalumu kwa ajili ya kuweza kukomesha kabisa vitendo hivyo.

Matukio ya namna hiyo katika Mkoa wa Pwani yanaonekana kumsikitisha na kumlazimu Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba kuingilia kati sakata hilo kwa kutangaza rasmi kupambana vilivyo na watu wote ambao watabainika wanajihusisha na vitendo hivyo vya mauaji ili waweze kukamatwa haraka na kuweza kufikishwa katika vyombo vya dola ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

Waziri nchemba ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kuwatembelea askari polisi, magereza, uhamiaji pamoja zimamoto wa Mkoani Pwani kwa ajili ya kuweza kukagua shuguli mbali mbali za utekelezaji ya majukumu yao ya kila siku ikiwemo na kuweza kubaini changamoto zinazowakabili pamoja na kuweka mikakati kwa ajili ya kuweza kuzitafutia ufumbuzi.

“Kumekuwepo katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani kuna baadhi ya viongozi wa vijiji pamoja na wakulima na wafugaji kupoteza maisha, kwa hili sisi kama Wizara hatuwezi kulivumilia hata kidogo kwani kwa sasa tumejipanga ii kuweza kuwabaini watu ambao wanahusika katika vitendo hivyo,”alisema Waziri.

Alisema kuwa anasikitishwa kuona mauaji yanafanyika kitu ambacho ni kinyume kabisa na sheria na taratibu za nchi, kwa mwananchi yoyote kuamua kujichukulia sheria mikononi kwa kufanya vitendo vya mauaji hivyo ameahidi kulivalia njuga suala hilo na wale wote watakaobainika wataweza kuchukuiwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
 Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba kushoto akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka wakizungumza jambo baada ya kulikagua gari ambalo lilikamatwa likiwa na wahamiaji haramu 150  Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani ambao ni raia wa Ethiopia.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba wa kulia na kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha  mjini Silvestry Koka  wakiangalia gari ambayo ilikamatwa Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani ikiwa na wahamiaji haramu wapatao  150 ambao ni  raia  kutoka nchini Ethiopia ambao walikamatwa wakati wakiwa  wapo safari kuelekea miko ya kusini. (PICHA NA VICTOR MASANGU).


Zantel yafungua duka na kituo cha huduma kwa wateja jengo la China Plaza, Kariakoo, Dar es Salaam leo

$
0
0

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania, Benoit Janin (kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka na kituo cha huduma kwa wateja cha kampuni hiyo katika jengo la China Plaza, Kariakoo, Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni wakala wa huduma kwa wateja, Asengo Adam na Meneja wa duka hilo, Yasmeen Ismail.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania, Benoit Janin (katikati), akiangalia wakati wakala wa huduma kwa wateja katika duka la kampuni lililopo katika jengo la China Plaza, Magdalena Mbayuwayu (kulia), akihudumia wateja wakati wa uzinduzi rasmi wa duka na kituo hicho, Kariakoo, Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Meneja wa duka hilo, Yasmeen Ismail.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Zantel Tanzania, Gabriel Magambo (katikati), akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa duka na kituo cha huduma kwa wateja cha kampuni hiyo katika jengo la China Plaza Kariakoo, Dar es Salaam leo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania, Benoit Janin (katikati), akimsikiliza meneja wa duka na kituo cha huduma kwa wateja cha kampuni hiyo katika jengo la China Plaza, Yasmeen Ismail wakati mhudumu katika duka hilo Magdalena Mbayuwayu (kulia), akihudumia wateja mara baada ya hafla ya uzinduzi rasmi wa duka na kituo hicho, Kariakoo, Dar es Salaam leo.

UNICEF NA EQUIP WASISITIZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA MASHULENI.

$
0
0
Na Ripota wa Globu ya Jamii, Morogoro.

Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulika na watoto UNICEF pamoja Taasisi iliyo chini ya shirika la World Vision yaani Education Quality Improvement Program ( Equip) kwa pamoja wameweza kuendesha semina elekezi kwa wadau wa mazingira mahala pa kazi wakiwemo maafisa maendeleo ya jamii,maafisa ustawi wa jamii, walimu , mabwana afya, pamoja na watendaji kutoka wilaya ya morogoro katika uboreshaji wa mazingira ya kufanyia kazi pamoja na mazingira ya wananchi kwa ujumla. 

Semina hiyo ni pamoja na kutambua umuhimu wa mazingira ktk maisha ya binadamu ambapo Mkurugenzi wa UNICEF Salvatory Mwakibibi na Mjumbe toka Equip, Erasto Henjewele kwa nyakati tofauti wameweza kutoa semina hiyo elekezi ambayo imewataka wajumbe wa semina kuwajibika kikamilifu katika uboreshaji wa mazingira na utunzaji wa mazingira kwa kushiriki upandaji wa miti kipindi hiki cha mvua ktk maeneo yao ya kazi yaliyopendependekezwa kwaajili ya shughuli hiyo . 

Pia suala la utunzaji wa vyanzo vya maji kwa kuelimisha wananchi kutofanya shughuli zozote za kibinadamu ambavyo huharibu mazingira na kusababisha ukame. 

Semina hiyo imekuja baada ya kuonekana mkoa wa morogoro umekumbwa na ongezeko la watumiaji wakubwa wa mkaa na kuni hivyo Taasisi mbalimbali zimefikia hatua ya kuamua kuendesha mafunzo na kushiriki kwenye upandaji wa miti mahala pa kazi ili kupunguza jangwa ambalo linawezakujitokeza siku za mbele. 

Mafunzo hayo yanaambatana pamoja na uteuzi wa mwakilishi kuteuliwa kutoka kila kata ambaye ataenda kupata mafunzo zaidi ya uhifadhi misitu kutoka kwa wataalamu wa maliasili wa Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma,hifadhi inayopakana na ziwa Tanganyika na kwa kipindi chote cha semina wajumbe wameombwa kuwa makini kushiriki zoezi hadi mwisho ili kwenda kuleta ufanisi wa kiutendaji watakaopoenda kusimamia zoezi la upandaji wa miti mahala pa kazi na maeneo maalumu yaliyotengwa kwaajili upandaji huo. 

Ifahamike Equip wamekua wakitoa mafunzo zaidi katika masuala ya kielimu lakini kwa sasa wamefika mbali zaidi hadi kushirikiana na UNICEF kwa kutambua umuhimu wa uboreshaji wa mazingira ya kujifunzia hivyo mwanafunzi au mtoto anayepata elimu kuanzia shuleni hadi maisha ya nyumbani ana uwezo mkubwa wa kuondoka tatizo la uharibifu wa mazingira.
Mwakilishi wa UNICEF Dkt Jamal Gulaid (kushoto) akimkabidhi majarida ya mazingira Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Stephen Bushiri wakati wa semina elekzi kuhusiana na utunzaji wa mazingira kwenye mkoa wake. 
Miongoni mwa wajumbe wa semina . 
Uongozi wa Taasisi ya Equip katika picha pamoja na wajumbe wa UNICEF wa pili kutoka kulia ni mwakilishi Dkt Jamal Gulaid akifuatiwa na katibu Tawala Mkoa wa Morogoro moro,Stephen Bushiri.

SERIKALI YAWASHUKURU WATAALAM WA KUJITOLEA WALIOMALIZA MUDA WAO WA KUTOA HUDUMA NCHINI

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akizungumza na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi leo.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akiwa katika mazungumzo na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi leo.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akimkabidhi zawadi Mtaalam wa kujitolea kutoka Japani aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini, Bw. Hiroshi Mikuni, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi leo.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akiwa katika picha ya pamoja na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini, baada ya hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi leo.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akiagana na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini, mara baada ya hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi leo.

JESHI LA POLISI LAFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA WA UTAPELI


WAZIRI MKUU MAJALIWA AITEMBELEA FAMILIA YA MAREHEMU SITTA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mama Margart Sitta, mjane wa Spika mstaafu,  Sumuel Sitta wakati alipoitembelea familia ya marehemu jijini Dar es salaam Desemba 19, 2016. Kulia ni mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kushoto  kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na familia ya aliyekuwa Spika Mstaafu, Samuel Sitta wakati walipoitembelea familia hiyo, nyumbani kwa marehemu jijini Dar es salaam Desemba 19, 2016. Kulia kwake ni mjane wa marehemu, Margareth Sitta. Wengine pichani kutoka kushoto ni watoto wa marehemu, Benjamin Sitta, John Sitta na Sam Junior.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary wakisalimiana na mama Margaret Sitta, mjane wa alieyekuwa Spika mstaafu, Samuel Sitta wakati walipoitembelea familia ya Spika huyo jijini Dar es salaam Desemba 19, 2016. Wengine pichani ni watoto wa marehemu, kutoka kushoto ni  Benjamin Sitta, Sam Junior na John Sitta. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Azam FC yaanza kuiwinda Majimaji, kuifuata kesho

$
0
0
 Kikosi cha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, kilipoanza mazoezi leo asubuhi kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Majimaji utakaofanyika Uwanja wa Majimaji, mjini Songea, Jumamosi hii.
 Wachezaji wa Azam FC wakifanya mazoezi tofauti ya viungo
 Beki wa kati wa Azam FC, Aggrey Morris, akiruka juu kwenye mazoezi ya viungo ya kuruka koni.
 Beki wa kati wa Azam FC, Yakubu Mohammed, akimzuia winga Enock Atta Agyei
  Kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, akijaribu kumtoka winga Enock Atta Agyei
Kipa wa Azam FC, Mwadini Ally, akiruka juu wakati wa mazoezi ya magolipa chini ya Kocha wa Makipa, Jose Garcia.

WASANII KURASIMISHA KAZI ZAO KUONGEZA PATO LAO NA TAIFA

$
0
0

Na Beatrice Lyimo Na Georgina Missama- Maelezo-Dar Es Salaam.


Serikali imetoa wito kwa wasanii nchini kurasimisha kazi zao ili kuweza kutambulika, kupata haki zao na kuongezea pato lao na la taifa.

Wito umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura wakati wa Mkutano na waandishi wa habari ulikuwa unahusu ubunifu wa vipaji na jinsi ya kuviendeleza.

“Sanaa inaongeza uelewa, sanaa ni chanzo kikubwa cha ajira hasa kwa vijana inayopelekea kukua kwa pato la taifa ingawa kuna changamoto kwa wasanii kutojitokeza au kujisajili ili kuweza kutambulika katika jamii”, alifafanua Naibu Waziri Wambura.

Alisema kuwa ili kutekeleza agizo la Rais wakati wa hotuba ya uzinduzi wa Bunge kuhusu haki za wasanii nchini, Wambura aliwataka wadau mbalimbali wa sanaa na sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha maslahi ya wasanii yanaboreshwa na kupinga uharamia wa kazi za wasanii.
Aidha, Wambura aliwataka wasanii kufuata Sheria, Kanuni na taratibu kwa kushirikiana na taasisi zinazohusika na masuala ya sanaa ikiwemo Tasuba, Basata, Cosota, Bodi ya Filamu ili kuwawezesha kufanya kazi kwa unafuu.

“Kama tunataka maendeleo ya kweli ni lazima kuthubutu, unapokuwa huna lengo au ndoto ni mkasa mkubwa katika jamii hivyo tunapaswa kuwa na ndoto zinazopelekea maendeleo yetu” alifafanua Wambura.

Kwa upande wake Rais wa Taasisi ya TCDB Mwalimu Calorus Bujimu, alisema kuwa taasisi imeandaa programu ya kukuza kazi za wasanii nchini kwa lengo la kuibua vipaji vya wasanii na kuvikuza.
Alisema kuwa uanzishwaji wa programu hiyo ni matokeo ya utafiti yaliyobaini kuwa uwepo wa wasanii wengi wenye vipaji katika Nyanja mbalimbali za sanaa, lakini wanakabiliwa na changamoto za kiuchumi na kukosa ubunifu.

TGN YAANDAA WARSHA YA KUCHANGIA SERA MPYA YA ARDHI KWA KUWASHIRIKISHA WADAU MBALIMBALI

$
0
0
Na Amina Kibwana,Globu ya Jamii

Mtandao wa Jinsia (TGNP) imeandaa warsha ya kuchangia sera mpya ya ardhi kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali kupitia fursa yake iliyopata kutoka Wizara ya ardhi maendeleo na makazi ili kuweza kujua namna ambavyo jinsia imeibuka katika kuchangia sera hii.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini dar es Salaam, Meneja Idara ya Ujenzi wa nguvu za pamoja Grace Kisetu, amesema kuwa katika warsha hiyo wameweza kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoka katika Halmashauri wanazofanyia kazi zikiwemo Kishapu,Morogoro,Mbeya,Mara  na Shinyanga  pamoja na asasi zisizokuwa za kiserikali na wanajamii kutoka sehemu ambazo tunafanyia kazi na baadhi ya washiriki kutoka wizra ta ardhi.

“Tumeamua kuwashirikisha wadau hao ili waweze kutusikiliza na kujua chambuzi ambazo tumeweza kuzifanya ili waweze kujua ni lipi tunaloliona kwamba kwenye rasimu walioitoa pengine linahitaji kuboreshwa zaidi hususani tukiangalia je jinsia ni ninsi gani imechukuliwa na kuweza kujitokeza kwenye hiyo sera ya ardhi ya mwaka 2016”

Kwa upande wake Muwezeshaji wa warsha hiyo Magdalena Luwevangila ameongeza kuwa katika Warsha hii tunaangalia jinsi gani sera inaweza ikakidhi mahitaji ya watu wote hususan katika masuala ya kijinsia,wanawake watoto,wanaume na watu waliopo pembezoni ili iweze kufanya kazi na kumaliza migogoro ya ardhi mara tu inapojitokeza.

” migogoro ya ardhi inayojitokeza hasa kwa upande wa rushwa ambapo serikali za vijiji zimeshindwa kusimamia tatizo hili na badala yake ubadhilifu umekuwa mwingi, hivyo sera hii ijikite katika kutatua na kuondoa migogoro hiyo”.

Nae mmoja wa wadau ambaye ni Mkulima  kutoka Mkoa wa Mara Kata ya Nyakonga, Nyangi Marwa ameiomba serikali kuwaangali wanawake na wajane  waliopo pembezoni kwani wengi wao hawajui haki zao juu ya umiliki wa ardhi ili kuepuka kunyanyasaji hasa katika kipindi cha mirasi.


TGNP ni shirika ambalo lipo mstari wa mbele katika masuala ya kijinsia na imepata nafasi ya kuweza kuchangia katika suala zima la sera mpya ya ardhi , ambapo kutokana na warsha hiyo TGNP inatarajia kutengeneza kikosi kazi cha Taifa Kitakachoundwa na wadau mbalimbali ambacho kitaongeza nguvu na ufuatiliaji wa utekelezaji wa sera hizi  ili kuongeza nguvu kwenye ushawishi na utetezi wa usawa wa kijinsia hususan utekelezaji wa sera zetu .

MAHAKAMA YAWAPA SIKU KUMI MAWAKILI WA LEMA

$
0
0

Na.Vero Ignatus,Arusha

Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Dkt.Modesta Opiyo amewapa siku kumi(10)mawakili wa mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema wawe wamewasilisha notisi ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya mahakama ya chini iliyomnyima dhamana Lema .

Agizo hilo limekuja kutokana na Mahaka kutoridhishwa na hoja za maombi ya mapingamizi mawili yaliyowekwa na mawakili wa serikali dhidi ya taarifa ya dharura ya kusudio la kukataa rufaa ya mawakili wa Mbunge huyo. 

Jaji Dkt.Modesta Opiyo wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha alisema katika maamuzi yake kuwa pingamizi zilizowekwa hazina msingi kwani waleta maombi walifuata taratibu zote za katika kiapo na hati ya dharua ya kuitwa mahakamani,ambapo amesema mahakama haijaona ucheleweshwaji wa lazima.

Baada ya uamuzi huo Jaji Opiyo aliwataka mawakili wa Lema ,Shekh Mfinanga na Faraji Mangula kuwasilisha notisi ndani ya siku kumi kuanzia leo,hadi hapo tar 30dec2016 shauri hilo litakaposikilizwa tena.

****TUJIKUMBUSHE****

Mbunge Godbless Lema anakabiliwa na kesi hiyo ya uchochezi aliyosomewa katika mahakama ya wilaya ya Arusha mbele ya hakimu mkazi Deusdedit Kamugisha Novemba 8 mwaka huu na aliwekewa pingamizi na mawakili wa serikali ya kutopata dhamana baada ya hakimu kusema kuwa dhamana iko wazi.

Mbunge huyo wa Arusha Mjini alikamatwa Novemba 2 mwaka huu Mkoani Dodoama kwa kosa hilo baada ya kuhutubia katika mikutano ya hadhara katika kata mbalimbali za Jiji la Arusha kuwa ameoteshwa kuwa Rais Magufuli atakufa kabla ya mwaka 2020 hali inayodaiwa kuleta uchochezi kwa wananchi waliomchagua kuwa Rais wa nchi.
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akiteta jambo na mkewe Neema baada ya mahakama kumalizika leo.Picha na Vero Ignatus Blog.


Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images