Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1462 | 1463 | (Page 1464) | 1465 | 1466 | .... | 3283 | newer

  0 0


  0 0


  0 0


  Na Zainab Nyamka, Glob
  u ya Jamii.
  MSANII wa muziki wa kizazi Kipya 'Bongo Fleva' Abbas Bakari  'Abby skills' amewashukuru mashabiki wake kwa kuupokea wimbo wake wa Averina na kusema kuwa wakae tena kwa mkao wa kula kwani kuna nyimbo saba zipo tayari.

  Abbyskills ameachia wimbo wa Averina mwanzoni mwa  Novemba na umeweza kumpatia show kadhaa na tayari ameanza kupata mafanikio kwa kupitia wimbo huo aliowashirikisha wasanii Ali Saleh Kiba 'Ali kiba' na 'Mr Blu'.
  Amesema kuwa, menejiment yake ambayo kwa sasa yupo chini ya lebo ya KING STUDIO amejipanga kuhakikisha anazidi kuwapa burudani mashabiki wake na zaidi nyimbo zipo tayari zinasubiri kupakuliwa tu.
  Abbyskills ameendelea na kusema kuwa , ujio wa wimbo wa Averina umekuwa na manufaa makubwa sana kwake kwani ndani ya mwezi mmoja na nusu ameweza kupata show ikiwemo FIESTA ya mwaka huu iliyofanyika Novemba 05.
  Kwa sasa Abby Skills anajiandaa kuachia nyimbo mpya inayotarajiwa kutoka Februari 2017 na amewaambia mashabiki wake wakae mkao wa kula kwani atakuja na kikubwa zaidi ya Averina.

  0 0

  Na Lydia Churi-Mahakama .

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman amewataka Mawakili nchini kuzingatia Maadili na kufuata misingi ya haki katika kutekeleza majukumu yao ili kesi ziendeshwe kwa haki, haraka na kwa wakati ili kuongeza imani ya wananchi kwa Mahakama.

  Akizungumza wakati wa sherehe za kuwapokea na kuwaapisha Mawakili leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, Jaji Mkuu amesema endapo Mawakili watatekeleza wajibu wao kwa kutenda haki watasaidia kupunguza mlundikano wa kesi zilizopo kwenye Mahakama mbalimbali nchini kuanzisha zile za Wilaya mpaka mahakama ya Rufani.

  Aidha, Jaji Mkuu amewataka Mawakili kushirikiana Mahakama pamoja na wadau wengine katika kuutekeleza Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania ambao pamoja na mambo mengine pia unalenga kupunguza mlundikano wa kesi kwenye mahakama mbalimbali nchini.

  Mhe. Othman pia amewashauri Mawakili walioapishwa leo kujiendeleza kielimu ili waweze kuongeza ujuzi utakaowasaidia kupambana na changamoto mbalimbali za kitaaluma na kwenda na wakati.
  Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Chande akiongea mbele ya mawakili 258 hawapo pichani wakati wa sherehe ya 55 ya uhapisho huo iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
  Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Chande katikati akiongoza Majaji wengine kupokea salamu ya utiifu kutoka kwa mawakili 258 waliopishwa hawapo pichani wakati wa sherehe ya 55 ya uhapisho huo iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya Mawakili wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Chande hayupo pichani baada ya kuapishwa wakati wa sherehe ya 55 ya uhapisho huo iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya Mawakili wakiwa wamesimama kusubiri kula kiapo kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Chande wakati wa sherehe ya 55 ya uhapisho huo iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
  Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Chande katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Mawakili waliopishwa wakati wa sherehe ya 55 ya uhapisho huo iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.  0 0

  Na Woinde Shizza,Arusha

  Mahakama ya hakimu mkazi mkoani Arusha imefuta kesi iliyokuwa ikimkabili aliyewahi kuwa mwenyekiti wa UVCCM mkoani hapa, Lengai Ole Sabaya baada ya upande wa Jamhuri kusema kuwa haitaki kuendelea na kesi hiyo

  Akitoa maelezo ya kesi hiyo Hakimu wa Mahakama ya Hakimu mkazi ya mkoa wa Arusha, Gwantwa Mwangoka amesema kuwa shauri hilo lililetwa na serikali mahakamani hapo, hivyo mahakama imeona haja ya kuendelea na shauri hilo.

  Awali wakili upande wa Jamhuri, Grace Makidenya aliwasilisha ombi mahakamani hapo la kuiomba mahakama kuiondoa kesi hiyo
   
  aliyewai kuwa Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya (katikati) akiwa anatoka mahakamani (picha na maktaba).
   
  Kwa upande wake wakili anayemtetea Sabaya amesema kuwa ipo mamlaka anayokuwa nayo DPP kuondoa shauri mahakamani hivyo kesi iliyokuwa inamkabili imefutwa hivyo hakuna kesi inayomkabili tena.

  Wakati huohuo
  mtuhumiwa huyo alikamatwa kwa mujibu wa sheria namba 255 ya  mwenendo wa makosa ya jinai nchini. 

  Mara baada ya kufutiwa kesi na mahakama hiyo, Lengai Ole Sabaya alikamatwa tena na polisi ,mwandishi wa habari hizi alifanya jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi mkoani hapa Charles Mkumbo  ili aweze kuzungumzia sakata la kukamatwa kwa Sabaya, Kamanda amesema kuwa hiyo ni teknikali ya kisheria bali kesi ni hiyohiyo na jeshi la polisi linafanya taratibu zao na zikikamilika watamrudisha tena mahakamani.

  Miezi kadhaa iliyopita aliyekuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi ‘UVCCM’ Arusha, Lengai Ole Sabaya alishtakiwa kwa kosa la kujifanya ofisa usalama wa Taifa na kughushi kitambulisho cha usalama wa taifa. 

  Kesi hiyo imetolewa maaamuzi na mahakama ya hakimu mkazi Arusha leo December 14 2016 ambapo imemuachia huru Lengai Ole Sabaya baada ya upande wa Jamhuri kusema hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema atabadilisha uongozi wa menejimenti ya kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL), kwa kushindwa kutekeleza uendeshaji na usimamizi wa kampuni hiyo.

  Akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo na kuonesha kutoridhishwa na huduma zinazotolewa na MSCL, Prof. Mbarawa amesema kutokana na kampuni kushindwa kujiendesha kibiashara na kulipa mishahara kwa wafanyakazi wake amelazimika kuchukua maamuzi hayo ili kuinusuru kampuni hiyo.  “Sijaridhishwa na taarifa za mahesabu yenu katika uendeshaji wa huduma za meli katika ukanda wa Ziwa Viktoria, Hamuwezi kusafirisha mizigo milioni 3.6 na nyie mkapata faida ya laki 2.. hamuomyeshi umakini kwenye utendaji”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.  Aidha, katika kuhakikisha huduma za Kampuni hiyo zinaimarika Serikali kupitia Waziri huyo imeahidi  kutoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya ukabarati wa meli nne zilizokuwa zimekufa katika ukanda huo ili kuboresha huduma za usafiri wa Ziwa.  Prof. Mbarawa amezitaja meli zitakazokarabatiwa ni Mv. Clarious, Mv Serengeti, Mv Sangara na Mv. Ukerewe ambazo zinahitaji ukarabati wa injini, mifumo ya umeme na ufundi na gia boksi.


   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL), wakati alipotembelea ofisi hizo mkoani Mwanza.
   Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL), Bw. Erick Hamis akitoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu hali ya utendaji wa kampuni hiyo katika ukanda wa Ziwa Viktoria, mkoani Mwanza.
   Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  John Mongella, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na menejimenti na wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL), wakati wa ziara ya Waziri huyo katika ofisi hizo mkoani Mwanza.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  John Mongella, wakati alipotembelea ofisi za Kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL), mkoani Mwanza.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
  KAMATI ya waamuzi Nchini imewashusha waamuzi Rajab Mrope na Ahmada Seif kutoka ligi kuu mpaka ligi daraja la kwanza.

  Katika ratiba ya ligi kuu iliyotoka waamuzi hao hayakuwepo majina yao, na rasmi sasa yameonekana kwenye ratiba ya ligi daraja la kwanza.

  Maamuzi hayo yamekuja baada ya Kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi (kamati ya masaa 72) kuwaondoa kwenye ratiba ya ligi kuu na shauri lao kulirudisha kwenye kamati ya waamuzi.

  Mrope aliondolewa kwenye ratiba hiyo baada ya kuonyesha udhaifu kwenye mechi ya Mbeya City dhidi ya Yanga kwa kutokuwa na maamuzi sahihi kwa kulikubali goli, kuliktaa na mwisho kulikubali tena mechi iliyomalizika kwa Mbeya City kushinda 2-1.

  Ahmada Seif aliondolewa kwa kosa la kutokuhimili mchezo wa African Lyon dhidi ya Mbao Fc kwa kutoa penati iliyozua utata kwenye mechi hiyo iliyomalizika kwa Lyon kushinda 3-1.

  Kamati ya waamuzi bado haijatoa maamuzi ya Mwamuzi Martin Saanya na Samuel Mpenzu ambao nao pia waliondolwa kwenye ratiba ya ligi kuu Vodacom..  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akimfafanulia jambo Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) nchini, Dr Qasim Sufi alimpomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Mazungumzo yao yalijadili masuala mbalimbali ya Wahamiaji pamoja na uimarishaji wa ushirikiano kati ya Wizara na shirika hilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) nchini, Dr Qasim Sufi alimpomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Mazungumzo yao yalijadili masuala mbalimbali ya Wahamiaji pamoja na uimarishaji wa ushirikiano kati ya Wizara na shirika hilo. 

  KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

  0 0

  Kamati ya kuwezesha na kuboresha usafiri wa anga ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imekutana kwa siku tatu mjini Zanzibar  ikiwa ni sehemu ya mikakati ya nchi wanachama kuboresha sekta hii ya uchukuzi katika nchi wanachama.

  Mkutano huo wa 41 umefunguliwa  rasmi na Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Ali Abeid Amani Karume, ambaye amesema  miundombinu katika viwanja vingi vya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki vinahitaji kuboreshwa ili kumudu ushindani wa kibiashara katika sekta hii. 

  Aidha, amezungumzia umuhimu wa nchi wanachama kupunguza tozo kwa kampuni zinazotoa huduma za usafiri wa anga ili kuvutia uwekezaji zaidi katika sekta.  Waziri huyo  amesisitiza umuhimu wa   watalaam wa usafiri wa anga katika nchi za Afrika Mashariki kupatiwa mafunzo ya kutosha  kuimarisha ujuzi  na uwezo wa utendaji kumudu majukumu yao.


  Awali wajumbe zaidi ya 70 wa kamati ya Kuwezesha Usafiri wa Anga katika nchi za Afrika Mashariki walitembelea kiwanja cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume (AAKIA) ili kujionea  miundombinu na huduma zinazotolewa katika kiwanja hicho cha ndege.  Wajumbe hao wa kamati ya Afrika Mashariki kutoka nchi za Burundi, Rwanda, Kenya,  Uganda na Mwenyeji Tanzania hukutana mara mbili kwa mwaka kwa lengo la kujadili  ubora wa utoaji huduma za usafiri  anga kwa abiria na mizigo .

  Kamati hiyo hujadili changamoto na kupendekeza suluhu za kuboresha sekta hiyo kwa lengo la kuwezesha sekta hii kutoa mchango katika kukuza uchumi wa nchi wanachama.


   Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza S. Johari akizungumza katika  mkutano wa kamati ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki Unaofanyika  Zanzibar.
   Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , Balozi Amani Karume, akifungua  rasmi mkutano wa Kamati ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki uliofanyika Zanzibar leo.
  Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , Balozi Amani Karume, akiwapongeza Wajumbe waliostaafu wa Kamati ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki kwa mchango  wao katika Kamati.
   Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki walipotembelea Kikosi cha Zimamoto katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume(AAKIA) 
   Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Amani  Karume,(Kulia) akishiriki Mkutano wa 41 wa Kamati ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki unaofanyika Zanzibar, Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari


  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania (CMSP) mara baada ya kukutana na viongozi hao kwa lengo la kujadili masuala ya kiutendaji ofisini kwake leo.

  0 0

  The Board of Directors of the African Development Fund (ADF) has approved a loan of UA 67.27 million (USD 93.51 million) to the United Republic of Tanzania for on-lending to the Tanzania Agricultural Development Bank (TADB). The funding will contribute to supporting Tanzania’s agriculture sector and achieving the country’s development goals.
  The TADB is a national development finance institution, the mission of which is to develop the agriculture sector in Tanzania. The sector provides employment for about 67% of the population and has a very big potential for expansion given the abundance of arable land and the availability of inland water resources. However, the sector needs to be developed if Tanzania is to achieve sustainable economic development and poverty reduction. 
  Specifically, in order for the country to achieve the Sustainable Development Goals and its Tanzania Development Vision 2025, the agriculture sector must sustainably grow at over 10% per annum. Unfortunately, over the past ten years, the sector has grown at an average of 4.4% per annum and contributed an average of 29.3% of Gross Domestic Product (GDP). These rates have recently declined to 3.2% per annum and 26% of GDP (Q2 2016), respectively.
  A major problem facing the country’s agriculture sector is the unavailability of medium to long-term finance to support, among other things, agricultural production, processing and marketing. The TADB is designed to address this through the provision of much-needed funding to a sector that is key to the country’s development.
  Concluding his remarks following the Board discussions, the AfDB President Akinwumi Adesina underscored that: “The TADB is expected to play a key role in facilitating attainment of sustainable food self-sufficiency and food security in Tanzania and in promoting and supporting the transformation of agriculture from subsistence to commercial farming in order to effectively and sustainably contribute to inclusive economic growth and poverty reduction.”

  0 0

  Idadi ya Watu wazima wanaotumia huduma za kifedha kupitia simu za mkononi imeongezeka kutoka asilimia 61 ya mwaka 2014 hadi kufikia asilimia 80 ya mwaka 2016. Akiongea wakati akiwasilisha matokeo ya tafiti ya matumizi ya huduma rasmi za kifedha nchini Meneja Mradi wa Sauti za Wananchi kutoka asasi ya TWAWEZA Nellie Njovu alisema kuwa ongezeko hilo limevuka lengo la serikali waliojiwekea kufikisha huduma za kifedha kwa asilimia 50 ya watanzania ifikapo 2016. 

  Aidha Bi. Nellie alisema kuwa asilimia 80 ya watumiaji wa huduma za kifedha kupitia mitandao ya simu wamesema wanaridhishwa na huduma zinazotolewa na ni mtumiaji mmoja kati ya kumi anayesema haridhishwi na huduma hizo. Matokeo haya yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutpka kwa wahojiwa 1800 kutoka maeneo mbalimbali Nchini kati ya terehe 14 hadi 26 septemba 2016.

  0 0

  NA EVELYN MKOKOI  - DSM .

  Tawi la baraza la wafanyakazi katika Ofisi ya makamu wa Rais limetakiwa kuwa ndo sehemu sahihi ya kujadili na kutatua migogoro ya wafanyaki na siyo majukwaa ya siasa.

  Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Nchi anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe January Mkamba, Lipokuwa akizungumza na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli jijini dar es Salaam.

  Mhe.Makamba alisema kuwa vikao vya baraza la wafanyakazi vimekuwepo kisheria na ni muhimu wajumbe kukaa pamoja kujadili masuala ya msingi yanyowahusu watumishi kwani wao ndo waliowachangua hivyo, majadiliano yanayokuwepo katika vikao hivyo ni nyenzo muhimu ya kuondoa migogoro na migomo mahala pa kazi.

  “Nyie ni miongoni mwa watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais ambao kwa namna moja au nyingine mmeaminiwa na kukabidhiwa dhamana ya kuwawakilisha wenzenu katika chombo hiki muhimu, katika kuamua na kushauri Baraza juu ya masuala mbalimbali yanayolenga kuleta ufanisi na utulivu ndani ya Ofisi yetu.alisisita Makamba”.

  Aidha, Waziri Makamba alisema kwamba, Lengo la vikao vya Baraza ni kuleta ufanisi wa utendaji kazi mahala pa kazi kwa ajili ya manufaa ya Taifa kuelekezana, kushauriana na kukumbushana, kuhusu majukumu ya ofisi na ushiriki wa wafanyakazi katika kuyatekeleza na kuyasimamia, na aliongeza kwa kusema kuwa ni fursa ya kipekee ya kutafakari utendaji wa kazi na majukumu ya Ofisi kwa ujumla.

  Kikao hicho cha baraza la wafanyakazi cha Ofisi ya makamu wa Rais kimudhuriwa na wawakilishi kutoka TUGHE Taifa na Mkoa na Wawakilishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Zanzibar. 
  Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rias Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi la Ofisi ya Makamu wa Rais leo Jijini Dar es Salaam kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Professor Faustine Kamuzora na kulia ni Katibu wa Baraza hilo Bw. Isaya Kisiri.
  Katibu wa baraza la wafanyakazi Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Isaya Kisiri akifungua mkutano wa baraza hilo uliofanyika katika Ofisi ya Makamu wa wa Rais Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.  (kushoto) ni Katibu Mkuu mstaafu Bw. Mubarak Abdul Wakil.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Professor Faustin Kamuzora akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba aliyekaa katikati, katika Mkutano wa Baraza la wafanyakazi cha Ofisi Hiyo uliyofanyika Leo Jijini Dar es Salaam.
   Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Makamu wa Rais wakiimba kwa pamoja wimbo wa wafanyakazi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa wajumbe wa Baraza la wafanyakazi Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam leo.

  Katika Picha Sehemu ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mkutano wa baraza hilo jijini Dar Es Salaam leo. ( Picha na habari na Evelyn Mkokoi wa OMR)

  0 0

  Na. Ahmad Mmow, Nachingwea.

  Waendesha pikipiki za kusafirisha abiria (bodaboda) wilayani Nachingwea wameaswa wasikubali kutumiwa na wanasiasa nakufanywa ngazi ya kufikia malengo yao yakisiasa.

  Wito huo ulitolewa hivi karibuni na mkurugenzi mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya kupambana na umasikini na utunzaji mazingira (APEC), Respicius Timanywa.Wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya usalama barabarani iliyofanyika katika kijiji cha Chiola wilaya ya Nachingwea.

  Timanywa alisema madereva bodaboda ni kundi lenye nguvu katika jamii kutokana na kuundwa na vijana. Hivyo baadhi ya wanasiasa wamekuwa natabia ya kuwalaghai ili wawaunge mkono kwa kuwataka washiriki kutekeleza vitendo vya uvunjifu wa sheria. Ikiwamo kushiriki maandamano na mikutano isiyo halali.

  Mkurugenzi huyo ambae taasisi yake inashugulika pia na kupunguza maafa kwa waendesha pikipiki, alisema vijana hawana budi kukataa kutumika kufanya vitendo vitakavyo vuruga amani na utulivu uliopo nchini kwa maslahi ya wanasiasa.

  Badala yake wajiwekee malengo ya kufikia maendeleo kwakufanya kazi kwa juhudi na maarifa."Anzisheni vikundi vya ujasiriamali na fungueni akaunti ili muweze kuungwa mkono na serikali, muweze kukopeshwa kupitia fedha za mifuko ya vijana na wanawake," alisisitiza Timanywa.
  Waendesha Boda Boda wakisubir abiria


  0 0  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  WAFANYABIASHARA ndogo ndogo wa Kariakoo wametakiwa kuuza bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani ili kukuza uchumi wa viwanda. Hayo ameyasema leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipokutana na wafanyabiashara wandogo wandogo wa Kariakoo, amesema bidhaa zinazozalishwa katika viwanda vya ndani zikipata soko nchi itapata mapato pamoja na kukuza uchumi wa nchi yetu.

  Amesema serikali iko pamoja na wamachinga kuhakikisha wanafanya biashara kwa mujibu wa sheria kwa kuuza vitu vyenye ubora na wakibaini kuwepo kwa vitu ambavyo vinahatarisha maisha ya watanzania watachukuliwa hatua mara moja.

  Makonda amesema ni marufuku wageni kutoka nje ya nchi kufanyabiashara ya umachinga katika jiji la Dar es Salaam wao wanatakiwa kuleta utaalam tu. Aidha amewaasa wamachinga kuwafichua wale ambao wanaweka rebo katika bidhaa wakati hawazalishi wenyewe.Makonda amesema katika maeneo ambayo wanafanyia kazi wamachinga kufuata sheria na kanuni zilizowekwa bila kuharibu utaratibu.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza nawafanyabiashara ndogo ndogo marufu kama Machinga mtaa wa Kongo na kusikiliza kero zao leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza wafanyabiashara wa soko kuu la Kariakoo nakusikiliza kero zao leo jijiji Dar es Salaam.
  Ofisa Tawala wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akifafanua jambo katika mkutano wawafanyabiashara ndogo ndogo Machinga mtaa wa Kongo leo jijiji Dar es Salaam.
  Wafanyabiashara na wananchi wakimsikiliza mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda.Picha Emmanuel Massaka-Globu ya Jamii.

  0 0

  Kampuni ya Intaneti ya Yahoo inasema wavamizi wa mitandao waliiba data za zaidi ya ya watumiaji wake bilioni moja.

  Tukio hilo linaaminika kufanyika mnano mwaka 2013.
  Katika taarifa yake, Yahoo inasema uvamizi huo wa taarifa muhimu ni tofauti na ule ulioripotiwa mwezi Septemba mwaka huu, ambapo wavamizi hao waliiba taarifa kutoka kwenye akaunti mbalimbali za watumiaji zaidi ya milioni mia tano.

  Imeongeza kuwa data zilizoibiwa zinajumuisha majina, anuani, namba za simu,tarehe za kuzaliwa pamoja na nywila (namba za siri).
  Lakini kadi za malipo sambamba na akaunti za benki hazikuingiliwa.

  Tazama hii video hapa chini

  0 0  Jengo la kisasa la Kitegauchumi la Chama Cha Mapinduzi (CCM), lilipo Upanga jijini Dar es Salaam, lililozinduliwa leo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Abdulrahman Kinana.

  Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa Mali za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Anna Abdallah, ujenzi wa jengo umegharimu sh. Bilioni saba.Mama Anna Abdallah, amesema, jengo hilo limejengwa kwa hali ya juu na limewekwa kila kitu ikiwemo zamani.

  "Mpangaji anapotaka kuingia katika nyumba hii, yeye anachopaswa kufanya ni kuja na chakula na nguo tu, halazimiki kuingia na samani yoyote hata TV anaikuta ipo sebuleni", Alisema, Mama Anna. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua jengo la kisasa la Kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mama Zakia Megji na Mama Anna Abdallah. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikata utepe kuzindua rasmi jengo hilo. Kushoto kwake ni Mama Anna Abdallah na kulia kwake ni Mama Zakia Meghji.


  0 0


  0 0


  Katika mwendelezo wake wa kuwapatia wateja wake na watanzania wote kwa ujumla burudani za sikukuu, Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na wasanii wa WCB imeandaa matamasha mawili ya kukata na shoka ambayo yatafanyika katika msimu huu wa sikukuu.

  Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Nandi Mwiyomella, alisema matamasha hayo makubwa ya muziki wa kizazi kipya yatafanyika katika mikoa ya Dar e salaam na Iringa chini ya wasanii Diamond Platinumz, Rayvanny , Rich Mavoko, Harmonize na Queen Darleen.

  “Kama mnavyoelewa msimu huu huwa umeambatana na shamrashamra mbalimbali za sikukuu na mitoko ukiwa na familia yako, Desemba 24 kutashushwa shoo ya Nguvu katika fukwe za Jangwani Sea Breeze Hotel ambapo kutakua na tamasha la kihistoria la “Vodacom Wasafi Beach Party” na Iringa tamasha litafanyika siku ya Krismasi katika uwanja wa Samora na Matamasha yote yataanza saa nane mchana”.Alisema.

  Mwiyombella alisema burudani hii ya muziki inakwenda sambamba na promosheni ya Nogesha Upendo ya Vodacom inayolenga kuwapatia wateja wote wa mtandao wa Vodacom zawadi za sikukuu ikiwa ni shukrani kwa wateja ambapo pia wateja wanayo fursa ya kujishindia tiketi za bure za kushiriki katika matamasha haya makubwa katika msimu huu wa sikukuu.

  “Ili kujishindia tiketi ya bure anachotakiwa kufanya mteja wa Vodacom ni kupiga*149*01# kisha nunua kifurushi chochote cha Vodacom na moja kwa moja utakua umeingia katika droo ya kuweza kujishindia tiketi yako. Zawadi nyingine kem kem kupitia promosheni ya Nogesha Upendo ni fedha taslimu , muda wa maongezi, Vifurushi vya intaneti (Mb)”.Alisema.

  Naye Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayetamba katika anga za kimataifa,Diamond Platinumz akiongea kwa niaba ya wasanii wa WCB alitoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam na Iringa kujitokeza kwa wingi siku ya shoo hizo kwani zitakuwa ni shoo za kihistoria katika mikoa hii miwili kufanywa na Vodacom kwa kushirikiana na WCB,Napenda kuwahakikishia mashabiki wetu kwamba tutakamua vilivyo tukiwa na wasanii wenzangu wote wa WBC kwa “Kunogesha Upendo” Alisisitiza Diamond.
  Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Nandi Mwiyomella(kushoto)akimsikiliza Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa bongo fleva,Diamond Platinumz(kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa hafla fupi ya kutanga tamasha la”Nogesha Upendo”yatakayofanyika Disemba 24 katika fukwe za Jangwani Sea Breeze jijini Dar es Salaam na Disemba 25 Iringa katika uwanja wa Samora chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania.
  Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa bongo fleva,Diamond Platinumz(katikati)akipiga selfie na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania mara baada ya mkutano na waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na tamasha la”Nogesha Upendo”litakalofanyika Disemba 24 katika fukwe za Jangwani Sea Breeze jijini Dar es Salaam na Disemba 25 Iringa katika uwanja wa Samora chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania.

  Baadhi ya wasanii wa nembo ya WCB wakiongozwa na Diamond Platinumz wakiwasili katika makao makuu ya Vodacom Tanzania,yaliyopo Mlimani city jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha la”Nogesha Upendo”litakalofanyikaDisemba 24 katika fukwe za Jangwani Sea Breeze jijini Dar es Salaam na Disemba 25 Iringa katika uwanja wa Samora chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania.

  0 0

    Katibu mkuu wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji, anayeshughulikia Biashara na uwekezaji mhe. Prof. Adolf Mkenda (katikati) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendegu alipomtembelea leo ofisini kwake na kuanza ziara yake mkoani humo.
   Katibu mkuu wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji, anayeshughulikia Biashara na uwekezaji Mhe. Prof. Adolf Mkenda (kushoto) akizungumza jambo na kaimu mkurugenzi wa bodi ya Korosho Tanzania, Hassan M. Jarufu. Katibu mkuu yuko katika ziara ya kusikiliza changamoto za korosho, maghala, vipimo na masoko mkoani Mtwara.
    Katibu mkuu wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji, anayeshughulikia Biashara na uwekezaji Mhe. Prof. Adolf Mkenda akikagua karakana ya ukaguzi wa mizani katika ofisi ya Wakala wa Vipimo Mkoani Mtwara.
  Katibu mkuu wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji, anayeshughulikia Biashara na uwekezaji mhe. Prof. Adolf Mkenda

older | 1 | .... | 1462 | 1463 | (Page 1464) | 1465 | 1466 | .... | 3283 | newer