Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1461 | 1462 | (Page 1463) | 1464 | 1465 | .... | 3272 | newer

  0 0
  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Wenyeviti na Makatibu wa CCM wa mikoa, alipokutana nao katika kikao maalum kilichofanyika jana, katika ukumbi wa Sekretarieti kwenye Ofisi Ndogo  Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Zakia Meghji, na kulia ni Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo na Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi.
  Watendaji wakiwa ukumbiniKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Wenyeviti na Makatibu wa CCM wa mikoa, alipokutana nao katika kikao maalum kilichofanyika jana, katika ukumbi wa Sekretarieti kwenye Ofisi Ndogo a Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Wengine walioko meza kuu, kutoka kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Mohamed Seif Khatibu, Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo na Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi.

  0 0

  Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa inayoadhimishwa kila mwaka kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 10 kuelimisha jamii kuzuia ukatili wa kijinsia. WiLDAF inashirikiana na mtandao wa mashirika yanayopinga ukatili wa kijinsia (MKUKI), wadau wa maendeleo na mashirika mengine kuadhimisha kampeni hizi kitaifa. 

  Yafuatayo ni matukio mbalimbali ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili kama yalivyofanyika sehemu mbalimbali nchini Tanzania chini ya kauli mbiu: Funguka! Pinga ukatili wa kijinsia. Elimu salama kwa wote. 

  Maandamano ya amani kupinga ukatili wa kijinsia Uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa jiji la Dar es salaam ulianza kwa maandamano ya amani ambapo maelfu walishiriki maandamano hayo kutoka Biafra hadi Millenium towers jijini Dar es salaam. Maandamano hayo yalifanyika tarehe 25 Novemba 2016.
  Waziri Ummy Mwalimu mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alikua mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho hayo yaliyofanyika tarehe 25 Novemba 2016, jijini Dar es salaam. 

  Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Ummy alisema serikali ya awamu ya tano imefanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kwamba watoto wanapata elimu salama bila aina yoyote ya ukatili wa kijinsia ikiwemo kutoa elimu bora bila malipo. "Lengo kuu la elimu bila malipo ni kuhakikisha kuwa watoto wetu hususan wa kike wanapata fursa ya kwenda shule kusoma na kufikia ndoto zao katika maisha." 

  Aidha alitoa wito kwa wadau na serikali kwa ujumla kutumia nafasi zao kupinga vitendo vyote vya udhalilishaji na ukiukwaji wa haki za binadamu vilevile kwa jamii kuwa na malezi bora na kuzingatia maadili kwa watoto na vijana wetu. 

  Mama Anne Makinda mgeni rasmi katika kongamano la kitaifa la Haki za Wanawake. Aliyekuwa spika wa Bunge la Tanzania mama Anne Makinda alikuwa mgeni rasmi katika kongamano la kwanza la kitaifa la Haki za wanawake lililofanyika ukumbi wa Millenium Towers jijini Dar es salaam tarehe 28 Novemba 2016. 

  Kongamano hilo lililoratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la LSF lilikuwa na lengo la kujadili namna mbalimbali za kuwawezesha wanawake kisheria na kiuchumi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. 

  Jamii imeaswa kuhusika kikamilifu katika mapambano ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kuhakikisha watoto wanapata elimu bora na salama. Kongamano hilo lilipambwa na kauli mbiu isemayo; Jitambue! Jiamini, Simamia Haki yako. Wageni mbalimbali wanaharakati wa Haki za binadamu walihudhuria kongamano hilo la aina yake wakiwemo Dr. Helen Kijo Bisimba, Mary Rusimbi, Edda Sanga na Dr. Judith Odunga. 


  0 0

  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akipokea Tuzo kutoka kwa Mjasiriamali na Mkurugenzi wa kampuni ya Malkia Investment ltd Bi. Jenifer Shigole aliyoshinda katika tuzo za za African entrepreneurship Awards zilizofanyika nchini Morocco na kuibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha masuala ya Elimu na Mazingira na kujishindia mtaji wa dola laki moja na nusu.Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana Bi.Venerose Mtenga na wa kwanza kushoto ni Meneja wa Programu wa kampuni ya Malkia Investment Bw.Juma Rajabu.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akizungumza na vyombo vya habari kuhusu Tuzo aliyoshinda Mjasiriamali na Mkurugenzi wa kampuni ya Malkia Investment ltd Bi. Jenifer Shigole katika tuzo za African entrepreneurship Awards zilizofanyika nchini Morocco na kuibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha masuala ya Elimu na Mazingira na kujishindia mtaji wa dola laki moja na nusu.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akipokea cheti alichoshinda Mjasiriamali na Mkurugenzi wa kampuni ya Malkia Investment ltd Bi. Jenifer Shigole katika tuzo za African entrepreneurship Awards zilizofanyika nchini Morocco na kuibuka mshindi wa kwanza na kujishindia mtaji wa dola laki moja na nusu.
  Mjasiriamali na Mkurugenzi wa kampuni ya Malkia Investment ltd Bi. Jenifer Shigole Bi. Jenifer Shigole akiwaonyesha waandishi wa habari(hawapo pichani) tuzo aliyoshinda nchini Morocco na kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika kipengele cha masuala ya Elimu na Mazingira na kujishindia mtaji wa dola moja na nusu. Kushoto ni Meneja wa Programu wa kampuni ya Malkia Investment Bw.Juma Rajabu.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akipokea Tuzo kutoka kwa Mjasiriamali na Mkurugenzi wa kampuni ya Malkia Investment ltd Bi. Jenifer Shigole aliyoshinda katika tuzo za African entrepreneurship Awards zilizofanyika nchini Morocco na kuibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha masuala ya Elimu na Mazingira na kujishindia mtaji wa dola laki moja na nusu.
  Picha na Daudi Manongi-MAELEZO.

  0 0

   The Management of the Centre for Foreign Relations (CFR) wishes to inform all graduands of Certificate, Ordinary Diploma and Postgraduate Diploma that the graduation ceremony will be held on Friday 13th January, 2017. The Ceremony will start from 2.00 p.m. at the Centre’s Campus, along Kilwa Road, Kurasini, opposite Jitegemee Secondary School.

  This is an important event, thus, you are advised to attend and witness the climax of your academic pursuit at the Centre for Foreign Relations. 
  ·              Graduands intending to participate in the ceremony should confirm their participation by paying Tshs. 60,000/= only. The money should be deposited in the NMB Bank Account No. 2011100061 not later than 6th January, 2017 and a payment receipt submitted to the Centre’s accounts office for registration. The collection of gowns should be done on 11th January, 2017. 
  ·              Graduands should report at the Centre’s Campus for Rehearsalson 12th January, 2016from 10.00 a.m. Only the names of the candidates who will be on the list will be read during the ceremony. 
  ·              All participants are expected to bear their own transport, food and accommodation costs. 
  You are all invited to attend. 
  Director

  Centre for Foreign Relations

  P.O. Box 2824

  DAR ES SALAAM

  Tel: 022 2851007  14th December, 2016


  0 0


  0 0


  Balozi wa India Sandeep Arya akiongea na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa maonesho ya bidhaa za vyakula kutoka India uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, Dar Es Salaam.

  Wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini mkutano huo wa uzinduzi wa maonesho hayo.

  Balozi wa India Sandeep Arya akipata maelezo toka kwa mmoja wa wafanyabiashara wa bidhaa za vyakula toka india mara baada ya  hafla ya uzinduzi wa maonesho ya bidhaa vya vyakula kutoka India uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, Dar Es Salaam.

  Maonesho ya bidhaa za vyakula yakiendelea.
  Habari kamili BOFYA HAPA

  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Mstaafu Damiani Lubuva akiongoza kikao cha Wajumbe wa Tume na Sekretarieti kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani mjini Zanzibar leo Desemba 14, 2016 . Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan.
  Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe.Jaji Mstaafu Mary Longway akizungumza jambo wakati wa kikao cha Wajumbe na Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo Desemba 14, 2016 mjini Zanzibar.
  Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Hamid M. Hamid (kushoto) akizungumza jambo wakati wa kikao cha Wajumbe na Sekretarieti ya Tume mjini Zanzibar leo. Katikati ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu Damian Lubuva na Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan (kulia).
  Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Prof. Amon Chaliga akieleza jambo wakati wa kikao cha Wajumbe na Sekretarieti ya Tume kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani, Zanzibar. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu Damian Lubuva na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Hamid M. Hamid (katikati).
  Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe akizungumza na Wajumbe na Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi mjini Zanzibar kwenye kikao cha maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani Zanzibar leo Desemba 14, 2016.
  Wajumbe na Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakiwa kwenye picha ya pamoja wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu Damiani Lubuva mjini Zanzibar leo Desemba 14, 2017. Picha/Aron Msigwa – NEC, Zanzibar.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda (kulia) akipokea moja ya madawati 50 yaliyotolewa na Dr.Amon Mkoga Foundation na kukabidhiwa kwake na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Ndugu. Amon Mkoga, wanaoshuhudia (kushoto alievaa kaunda suti ni Katibu Tawala Wilaya ya Kisarawe, Mtela Mwambapa, katika Afisa Mauzo kutoka Kampuni ya Noble Motors, Josephu Simon ambao ndio wadhamini wa mradi huo.
  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda (kulia) akitoa shukrani mara baada ya kupokea madawati.
  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda (katikati), Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Ndugu. Amon Mkoga, kushoto Afisa Mauzo kutoka Kampuni ya Noble Motors, Joseph Simon ambao ndio wadhamini wa mradi huo wakiwa katika picha ya pamoja.


  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo amepokea magari hamsini ya kubebea wagonjwa pamoja na magari 8 ya kuratibu shughuli za huduma za afya ya mama na mtoto yenye thamani ya shilingi bilioni 5.9 ambayo yamekabidhiwa kwa Wabunge wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Kagera, Mwanza, Mara, Simiyu, Geita na Kigoma

  Waziri Ummy amelishukuru Shirika la Afya Duniani (WHO) na UNFPA kwa kuendelea kushirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili watanzania, ikiwemo vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga. 

  Alizitaja changamoto zilizoonekana katika mikoa hiyo ni huduma hafifu ya rufaa kwa wanawake wajawazito kwa kukosa magari ya kubebea wagonjwa, ukosefu wa damu salama, ushiriki mdogo wa jamii katika mambo yanayohusu afya ya mama ikiwemo kutotambua dalili hatari za wakati wa ujauzito pamoja na baadhi ya watumishi wasiokuwa na stadi za kuokoa maisha ambayo yanachangia wingi wa vifo vitokanavyo na uzazi

  Tafiti zilizofanyika mwaka 2010 na tathmini iliyofanyika mwaka 2015 wakati wa kuandaa mpango kazi wa matokeo makubwa sasa, Mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Kigoma ilionekana kuwa na viashiria hafifu vya afya ya mama na mtoto kwa mfano; utumiaji mdogo wa uzazi wa mpango, wanawake wachache wanaojifungulia katika vituo vya kutolea huduma ya afya pamoja na vifo vingi vitokanavyo na uzazi.

  Wizara ya Afya imekua ikifanya jitihada mbalimbali katika kukabiliana na tatizo hilo ambapo kwa awamu hii ya tano tumetengeneza mpango mmoja utakaohusika na masuala ya uzazi wa afya ya mama na watoto na vijana ambapo ndani ya miaka minne hadi kufikia mwaka 2020 tuwe tumepunguza vifo vya akina mama wajawazito kutoka 432 hadi 292 kutoka kila kizazi hai laki moja na kwa upande wa watoto chini ya miaka mitano Tanzania imefanikiwa kufikia lengo namba nne la malengo ya maendeleo ya milenia kwa kupunguza vifo kutoka 50 hadi 40 katika vizazi hai 1,000.

  Aidha Waziri Ummy amewataka Wabunge, Wakurugenzi na Waganga Wakuu wa Wilaya kuyatumia magari hayo ipasavyo yaani, kwa shughuli iliyokusudiwa, vilevile kuyakatia bima ya ajali pamoja na kuiomba jamii, Taasisi zisizo za kiserikali kuunganisha nguvu kwani vifo vitokananyo na uzazi vinazuilika. 

  IMETOLEWA NA


  Nsachris Mwamwaja

  MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-AFYA

  14/12/2016  0 0


  Na Bashir Nkoromo.

  Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, amesema, anazitambua changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa Chama Cha Mapinduzi na kuahidi kushirikiana na wafanyakazi hao kuzipatia ufumbuzi.


  Mpogolo amekutana na wafanyakazi hao ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo, katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, kilichofanyika jana, Ikulu jijini Dar es Salaam.  "Mimi nimekuwa katika chama hiki mda mrefu sana, kwa hiyo sehemu kubwa ya changamoto zinazowakabili wafanyakazi nazijua hivyo nitatumia juhudi zangu na maarifa kuhakikisha changamoto hizo zinapungua au kuisha kabisa".  "Lakini kubwa zaidi ni mimi na ninyi wafanyakazi kushirikiana kwa pamoja katika kupambana na changamoto hizi na hatimaye tukifikishe chama kunakotarajiwa, na bila shaka mnajua lengo kuu la Chama chochote ni kuwa na nguvu na inayokipa uwezo wa kuongoza kwa kushika dola", alisema Mpogolo.  Alisema, pamoja na kuwa katika Chama kwa mda wa kutosha kujifunza ana kuelewa mengi, lakini bado atahitaji ushauri kwa baadhi ya wafanyakazi wazoevu, hivyo wafanyakazi wasisite kumpa ushauri wao pale watakapokuwa wanaona kwamba ushauri wao utasaidia kusonga mbele.  Mpogolo aliwataka wafanyakazi kuongeza bidii ya kazi kila mmoja katika nafasi yake, akisema ni lazima watambue kuwa kila mfanyakazi wa Chama katika eneo aliloko mchango wake unahitajika sana, na aelewe kuwa isingekuwepo haya ya chama kumwajiri kama hakitarajii tija kutoka kwake.  Mapema, Mpogolo aliwasili ukumbini akifuatana na Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Rajab Luhwavi ambaye ameteuliwa hivi karibuni kuwa Balozi.  Luhwavi aliwaomba wafanyakazi kumpa ushirikiano Naibu Katibu Mkuu huyo mpya akimwelezea kuwa ni Kada wa Chama ambaye amefanya kazi katika idara nyingi na nyeti hivyo anayo hazina ya mambo mengi anayofahamu katika chama.

  Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akizungumza na wafanyakazi wa Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi na kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utawala na Uendeshaji, Salum Khatib Reja. PICHA BASHIR NKOROMO
   Wafanyakazi wakiwa tayari kumsikiliza Mpogolo

   Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM, Rodrick Mpogolo akiingia ukumbini kuzungumza na wafanyakazi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo. Kulia ni Mkuu wa Utawala bakari Hamad na wapili ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utawala na Uendeshaji, Salum Khatib Reja.


  0 0


  Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam.

  Kampuni moja ya Ujerumani ya Ferrostaal, inatarajia kujenga kiwanda kikubwa cha mbolea katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, kitakacho gharimu zaidi ya Euro Bilioni 1 nukta 2 (1.2bln) ambacho kinatajwa kuwa kitakuwa moja ya viwanda vikubwa vya mbolea Barani Afrika.
  Hayo yamesemwa na Balozi wa Ujerumani hapa nchini, EGON KOCHANKE, wakati alipomtembelea na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Jijini Dar es salaam, ambapo wawili hao wamezungumzia masuala kadha wa kadha yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Ujerumani uliodumu kwa muda mrefu.
  Balozi Kochanke amesema kuwa kiwanda hicho kitakachojengwa kwa ubia kati ya kampuni hiyo ya Ujerumani na wawekezaji wazawa na wengine kutoka Bara la Asia, inatokana na  hamasa kubwa ya serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli katika kuhamasisha ujenzi wa viwanda.
  “Kiwanda hiki kitakuwa kikubwa zaidi ya mara mbili ya kiwanda cha saruji cha Dangote kilichoko Mtwara na kitagharimu Euro Bilioni 1.2, kitasisimua uchumi wa nchi pamoja na kukuza ajira” alisema balozi huyo aliyeambatana na naibu Balozi wa Ujerumani hapa nchini, John Reyels na Mkurugenzi wa Ushirikiano wa nchi hiyo Julia Hannig.
  “Mbali ya Kampuni hiyo ya Ferrostaal, wawekezaji wengine ni kampuni ya Mbolea ya Minjingu, na kampuni nyingine kutoka Pakistan ambayo kwa pamoja wameingia ubia wa kujenga kiwanda hicho cha mbolea kitakachokuwa uwekezaji mkubwa” Aliongeza Balozi Egon Kochanke.
   Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw. Egon Kochanke (katikati) pamoja na ujumbe wake wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani),  Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.  
   Ujumbe wa Ujerumani ukiongozwa na Balozi wan chi hiyo nchini Tanzania, Egon Kochanke (katikati) ukiwa katika mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Kulia) wakati wa mazungumzo kuhusu uhusiano uliopo kati ya nchi hizo mbili, Jijini Dar es salaam. Kulia kwa Balozi  ni Mkurugenzi wa Ushirikiano Bi. Julia Hannig na na kushoto kwake ameketi Naibu Balozi wa Ujerumani hapa nchini Bw. John Reyels.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) akiangalia nyaraka alizokabidhiwa na  Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw. Egon Kochankewakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.  Kulia kwa Waziri ni Mchumi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Melckzedek Mbise na anayefuata ni katibu wa Waziri Bw. Makamba.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii .


  MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekabidhi vifaa mbalimbali kwa wakazi wa Dar es Salaam vyenye thamani ya 164,272,000/= ikiwa ni sehemu ya ahadi zake katika ziara ya Dar mpya.

  Makonda amesema kuwa anatimiza ahadi zake kwa wahusika kama ifuatavyo Sober house kigamboni kwa kuwapa jiko la gesi, mitungi 2,king’amuzi televisheni moja ya nchi 49 na magodoro 50 pia ameweza kutoa zawadii ya pikipiki kwa watendaji wa ofsi yake kwa kuwapa morarli ya kazi pamoja na mwenyekiti wa serikali ya mtaa Mivinjeni kata ya buguruni.

  Aidha mkuu wa mkoa ametoa zawadi kwa watumishi wane ambao ni Dr.Grace Magembe,mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Mruto kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke,Edward Otieno katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji na Aron Joseph Mkkurugenzi uendeshaji wa DAWASCO.

  Pia ametoa mitaji ya biashara kwa wajasiliamali wawili kwa kwa kukabidhi kiasi cha fedha cha shilingi miioni moja kwa kijana mmoja na shilingi laki mbili kwa mwanamke mjasiliamali kwa ajjili ya kuimarrisha biashara yake.

  Msaada mwingne alitoa mkuu huyo wa mkoa ni pamoja na mabati 2000 kwa ajili ya sekondari ya Jeshi ya jitegemee na shule ya msingi Annex Mbagala mabati 1000 na shule ya msingi ya katoliki kupewasaruji mifuko 1000 .

  Pia ameimarisha kikosi cha jeshi la wananchi wa Tanzania kwa kutoa Zawadi ya Tumba kwa ajili ya bendi ya jeshi na kutoa zawadi ya gari kwa ajilli ya kuimarisha huduma katika Zahanati ya kikosi cha kikosi cha kutuliza ghasia kanda maalum ya Dar es Salaam Ukonga.
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali kwa wakazi wa Dar es Salaam vyenye thamani ya 164,272,000/=leo jijini Dar es Salaam.picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
    Kamanda wa kikosi cha kutuliza ghasia kanda maalum ya Dar es Salaam, Acp.Stanley Kulyamo akipokea gari la wagonjwa kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda leo Jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda , akikabidhi  shilingi laki mbili kwa mjasiliamali ,Zuhura Waziri mkazi wa Mwembe Yanga kwa ajili ya kuongeza mtaji wake wa Supu.
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikabidhi hundi  kwa mchungaji Epafra  Zabron Shinji wa kanisa la AIC Tanzania.
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akikabidhi mifuko ya Saruji kwa Mkuu wa shule ya St Joseph Goba , Sister Caroline Kokutekana, kama sehemu ya kutimiza ahadi yake wakat wa mahafali ya shule hiyo.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Serikali imeanza ujenzi na upanuzi wa viwanja 11 ikiwa ni hatua ya kuendelea kuboresha na kukuza usafiri wa anga hapa nchini.  Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la abiria katika kiwanja cha ndege cha Mwanza, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 150 zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya upanuzi wa viwanja hivyo.Ameongezeza kuwa miradi itakayotekelezwa katika viwanja hivyo ni pamoja na ujenzi wa majengo ya abiria na upanuzi wa barabara za kuruka na kutua ndege.

  "Maboresho ya miundombinu ya viwanja vya ndege yatachochea ongezeko la pato la Taifa, hivyo basi Serikali imeonesha nia ya dhati katika kuhakikisha usafiri huu utakuwa ni wa uhakika na nafuu kwa wananchi”, amesema Profesa Mbarawa.  Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amevitaja baadhi ya viwanja hivyo kuwa ni kiwanja cha ndege cha Shinyanga, Tabora, Sumbawanga, Kigoma, Mtwara, Songea na Iringa.  Kuhusu ujenzi wa Jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha  Mwanza, Profesa Mbarawa amesema kuwa Serikali imeshatoa kiasi cha shilingi bilioni 7.6 kwa ajili ya kumlipa mkandarasi na msimamiz wa mradi huo ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti mwakani.  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Salum Msangi amesema Mamlaka itaendelea na uboreshaji wa miundombinu ya viwanja vya ndege lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa watanzania wanapata huduma zilizo bora na kukuza pato la Taifa.  Ameahidi kuendelea kutatua changamoto ya ndege hai wanaohatarisha uharibufu wa miundombinu za injini za ndege katika uwanja huo ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha usalama wa anga na watumiaji wake.  Naye, Mkandarasi wa Kampuni ya Japan Engineering Construction Group (JECP), anayejenga jengo hilo, Yuzhang Xiong, amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kukamilisha ujenzi huo kwa wakati kwani kwa sasa jengo limefika  katika hatua nzuri.


   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG), anayejenga jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Mwanza, Yuzhang Xiong, wakati alipokagua maendeleo ya mradi wa ujenzi huo.
   Meneja Mipago, Ubunifu na Tathimini wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Eng. Mbila Mdemu akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, kuhusu mradi wa jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Mwanza.
   Muonekano wa jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Mwanza kinachojengwa na Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG), ambapo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti mwakani.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wakazi wa Pasiansi wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa Daraja la Furahisha na upanuzi wa Barabara ya Makongoro-Uwanja wa Ndege, mkoani Mwanza.
  Muonekano wa Daraja la Furahisha mkoani Mwanza, ambalo linatarajiwa kukamilika mwazoni mwa mwezi Januari mwakani. Ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 80.  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

  Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bw. Onorius Njole akitoa mada ya masuala ya baadhi ya Miongozo iliyotolewa na Mamlaka ili kuboresha utendaji katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa Mameneja na Maafisa wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Mkoani Morogoro hivi karibuni.
  Mkurugenzi wa Tafiti, Tathmini na Sera, Bw. Ansgar Mushi akifafanua jambo la kitaalamu katika Semina iliyotolewa na SSRA kwa Mameneja na Maafisa wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, mkoani Morogoro hivi karibuni.
  Mameneja na Maafisa wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wakisikiliza kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa na watoa mada toka SSRA katika Semina ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii.


  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akikata utepe kuashiria upokeaji wa  madawati ya msaada kutoka kwa Wakala wa  Huduma za Misitu nchini leo jijini Dar es Salaam. 
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi akizungumza mara baada ya kupokea madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni 5.6  kutoka kwa Wakala wa  Huduma za Misitu nchini leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
  Meneja wa Wakala wa Huduma za  Misitu Tanzania Wilaya ya Kinondoni, Alexander Mboya akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukabidhi madawati kwa mkuu wa Wilaya leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Alli Hapi.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Alli Hapi na Meneja wa Meneja wa wakala wa huduma za  Misitu Tanzania wilaya ya Kinondoni, Alexander Mboya wakiwa wamekaa kwenye madawati mara baada ya kukabidhi leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania (TCRA) , leo December 14 imefanya Ukaguzi wa mwisho, kujiridhisha na kuruhusu Kituo cha Utangazaji cha Radio5 Arusha kurudisha Matangazo yake hewani ifikapo December 16 mwaka huu 2016.
  Akiongea na Viongozi na baadhi ya Wafanyakazi wa Radio 5 baada ya kukamilisha ukaguzi wao, Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA Bw. Fredrick Ntobi amesema wao kama Mamlaka Waliamua kuja kufanya ukaguzi wao kwa ajili ya kujiridhisha kurudisha Matangazo ya Kituo hicho hewani December 16 ambapo ndiyo tarehe rasmi ya kuisha kwa adhabu waliyokuwa wametoa kwa  kituo hicho.
  Kituo cha Radio 5 kilisimamishwa na TCRA kurusha matangazo yaketoka  tarehe 16 September 2016 kwa kukiuka baadhi ya kanuni.
  Mamlaka hiyo ilifanya ukaguzi wa Studio ya Kurusha Matangazo (On air Studio), Studio ya kuzalisha Vipindi (Production Studio), Chumba cha Habari (News room), Control Room, ofisi zote za Kituo pamoja na Mnara wa Kurushia Matangazo ambapo kote wamekuta kila kitu kiko sawa kwa kazi kama Mamlaka inavyotaka.
  Hata hivyo Bw. Fredrick Ntobi akiwa ameongozana na Viongozi wa  TCRA kanda ya Kaskazini, amewakumbusha Watangazaji na Waandishi kufuata Maadili ya uandishi wa habari ili kulinda Vituo vyao na Kulinda taaluma zao kwa ajili ya kuendelea kuhabarisha na kuelimisha Jamii nzima ya Watanzania.
  “Mimi niwasisitize tu kuendelea kufuata maadili ya taaluma yenu ya uandishi wa habari, kufuata sheria na kanuni za uandishi wa habari ambao mmesomea, tumieni lugha Sanifu ambayo inakubalika kwa jamii na tasnia yenu na niwatakie maandalizi mema ya kurudi hewani pamoja na Sikukuu zinazokuja”. Alimaliza kwa Msisitizo Bw. Fredrick Ntobi.
  Hata hivyo kwa upande wa Mkurugenzi wa Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio5, Bw. Robert Francis, Amewataka Wasikilizaji wa Radio5 kukaa mkao wa Kuhabarika, Kupata Burudani na kuelimika zaidi kupitia Radio5 kwani Wamejipanga vyakutosha kurudi hewani kwa Kishindo.
  “Mimi niwaombe tu wasikilizaji wetu ambao najua wametumiss sana, wakae tayari Kuhabarika, kuelimika na kuburudika zaidi sababu mimi na Wafanyakazi wangu tumejipanga vya kutosha haswa ukizingatia kwamba mwaka mpya ndo huu unakuja. Kingine niwape pole tu wasikilizaji wetu wote kwa kutotusikia hewani kwa kipindi cha miezi mitatu, pamoja na Wadau ambao tumekuwa tukishirikiana kwa pamoja katika mambo mbali mbali niwaambie tu tunarudi rasmi Ijumaa ya tarehe 16 December 2016”. Alisema Mkurugenzi wa Radio5 Robert Francis.
  Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA Fredrick Ntobi wakizungumza jambo na Mkurugenzi wa Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio 5, Bw. Robert Francis,ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania TCRA, leo December 14 imefanya Ukaguzi wa mwisho, Kujiridhisha na Kuruhusu Kituo cha Utangazaji cha Radio5 Arusha kurudisha Matangazo yake hewani ifikapo December 16 mwaka huu 2016.  0 0


  Na Genofeva Matemu – WHUSM.

  Wanatasnia wa filamu nchini wametakiwa kutumia fursa zilizopo kikamilifu ili kuifanya sekta ya filamu kuwa chachu ya maendeleo ya nchi na kuleta ushindani wa kazi za filamu zinazozingatia  ubobezi na hatimaye kuingia katika soko la ushindani.   Rai hiyo imetolewa na Naibu katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya filamu na michezo ya kuigiza leo Mkoani Mara.  “Nimatumaini yangu kuwa mafunzo mnayoyapata hapa yakijumuishwa na fursa mlizonazo za mandhari mahususi ya upigaji picha katika Mkoa wetu wa Mara, maeneo mazuri na asilia ya kitalii, utamaduni wetu, maliasili, lugha ya kiswahili na mambo mengine mengi mkiyazingatia katika uandaaji wa filamu zenu hakika ushindani wa filamu zetu utakuwa mkubwa sana” amesema Bibi. Millao.  Kwa upande wake Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa Lengo la warsha hiyo ni kuhakikisha kuwa wadau wanazalisha kazi bora na hatimaye wanapata mrejesho stahiki kutokana na kazi zao hivyo wadau walioshiriki warsha watumie fursa waliyoipata kwani warsha imezingatia ushirikishwaji wa hali ya juu kwa kuwapa wadau fursa ya kuchagia na kujadiliana.


    Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao (kulia) akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya filamu na michezo ya kuigiza leo Mkoani Mara. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
   Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (katikati) akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya filamu na michezo ya kuigiza leo Mkoani Mara. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao na kushoto ni Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba.
   Katibu wa chama cha waigizaji Mkoa wa Mara Bw. Jonson Bambai (aliyesimama) akichangia mada wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya filamu na michezo ya kuigiza leo Mkoani Mara.

  Baadhi ya wadau wa sekta ya filamu na michezo ya kuigiza kutoa mkoa wa Mara wakifuatilia kwa makini mada zilizokua zikiendelea wakati wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya filamu na michezo ya kuigiza leo Mkoani Mara.Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM, Mara

  0 0


  Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaniva akifungua semina kuhusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995 kwa waheshimiwa madiwani wa wilaya za Temeke na Kigamboni . Kulia kwake ni Kaimu Kamishna wa Maadili Bwana Waziri Yahaya Kipacha na kushoto kwake ni Mstahiki Meya wa Temeke Mhe. Abdallah Jafari Chaurembo. Semina hiyo imefanyika leo (14/12/2016) katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Katibu mkuu wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji, anayeshughulikia Biashara na uwekezaji mhe. Prof. Adolf Mkenda (kushoto) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendegu alipomtembelea leo ofisini kwake kabla ya kuanza ziara yake mkoani humo.
  Katibu mkuu wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji, anayeshughulikia Biashara na uwekezaji mhe. Prof. Adolf Mkenda (kushoto) akutana na kaimu mkurugenzi wa bodi ya korosho Tanzania Bw. Hassan M. Jarufu. Katibu mkuu yuko katika  ziara ya kusikiliza changamoto za korosho, maghala, vipimo na masoko mkoani mtwara.
   Katibu mkuu wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji, anayeshughulikia Biashara na uwekezaji Mhe. Prof. Adolf Mkenda akikagua karakana ya ukaguzi wa mizani katika ofisi ya Wakala wa Vipimo Mkoani Mtwara.
  Katibu mkuu wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji, anayeshughulikia Biashara na uwekezaji mhe. Prof. Adolf Mkenda akikagua ghala la kuhifadhia korosho za wakulima lililopo mkoani mtwara.

older | 1 | .... | 1461 | 1462 | (Page 1463) | 1464 | 1465 | .... | 3272 | newer