Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1460 | 1461 | (Page 1462) | 1463 | 1464 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Ofisa habari  wa Shirikisho la Mpira wa Miguu TanzaniaTFF Alfred Lucas 

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeanza mazungumzo na Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyoko Muhimbili, Dar es Salaam ili kwa pamoja waanze  kushiriana kutoa mafunzo kwa madaktari na wahudumu wa afya kwa wanamichezo wa soka katika kushughulikia matatizo ya moyo.
  Akizungumza leo Jijini Dar es salaam, Ofisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema kuwa mafunzo haya yataboresha uwezo wa madaktari wa mpira wa miguu sambamba na kusambazwa kwa vifaa maalumu vya tiba ya moyo kwenye klabu za soka nchini.
  Lucas amesema hii ni hatua thabiti inayochukuliwa na uongozi wa TFF baada ya kutokea vifo vinavyosababishwa na mshtuko wa moyo kwa wachezaji ukiwamo ugonjwa wa ‘cardiac arrest’ ambao kwa taarifa za awali zimeonyesha ndio chanzo cha  kifo cha Mchezaji wa Mbao FC U20, Ismail Mrisho Khalfan.
  Marehemu Ismail Mrisho Khalfan alifariki dunia baada ya kuanguka uwanjani Desemba 4, 2016 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera wakati timu yake ya Mbao ikicheza na Mwadui katika mechi ya ligi ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20.
   Kifo hicho kimegusa hisa za wanafamilia wengi wa mpira wa miguu akiwamo Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu Ulimwenguni (FIFA), Bw. Gianni Infantino ambaye juzi alituma salamu za rambirambi kwa Rais Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Jamal Emil Malinzi kutokana na kifo cha ghafla cha Mchezaji.
  Rais Infantino, ametuma salamu za rambirambi ambazo zinakwenda sambamba na za Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania, Ndugu Nape Nnauye na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Issa Hayatou.
  Ismail aliyeanguka uwanjani dakika ya 74, alipata huduma ya kwanza uwanjani hapo kwa madaktari waliokuwa uwanjani, lakini baadaye taarifa za kitabibu zilionyesha amefariki dunia.

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akibovya Komputa kuashiria katika uzinduzi Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na Watoto 2017 - 2022, leo jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

  SERIKALI imesema haitavumilia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vikiendelea kufanyika, hali ambayo inasababisha baadhi ya wanawake na watoto kukosa haki zao.

  Hayo yamesemma na Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu wakati akizindua Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na Watoto 2017 -2022, amesema tatizo la ukatili dhidi wanawake na watoto ni kubwa nchini na limeathiri maendeleo yao na ya taifa kiujumla.
  Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria katika uzinduzi Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na Watoto 2017 - 2022, leo jijini Dar es Salaam.

  Ummy  amesema kwa mujibu wa takwimu za jeshi la polisi vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vilivyoripotiwa 2015 vilifikia 22,876 kati ya hivyo vitendo vya ubakaji vilikuwa 3,444 , shambulio , kujeruhi na matusi vilikuwa 14, 561.

  Amesema  ukatili dhidi ya watoto unafanywa majumbani na shule hivyo kila shule ya msingi na sekondari kutaundwa timu za ulinzi pamoja na kila kata kuwa na timu ya ulinzi.

  Naye Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango ameagiza Wilaya, Mikoa na Miji midogo  kutenga bajeti ya mpango huo ili uweze kutekelezeka wenye thamani ya zaidi ya sh. Bilioni Tano.
  Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu pamoja na Mawaziri Mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na Watoto 2017 - 2022, leo jijini Dar es Salaam.

  Katika uzinduzi huo mawaziri nane wametoa msimamo wao katika utekelezaji wa mpango kazi huo.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0


  0 0

  Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na waandishi wa waandishi leo wa habari ofisi kwake makao makuu Kanda maalum ya Dar es Salaam.

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
  Jeshi la Polisi mkoa wa Dar es Salaam limekamata watuhumiwa 22 hatari wa makosa ya wizi kwenye taa za Chang’ombe na kungwineko jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa kikosi maalum cha kupambana na wizi wa kutumia silaha na wizi wa nguvu cha Polisi Kanda maalum DSM kimefanikiwa kuwakamata watuhumiwa hatari 22.

  “ufuatiliaji ulifanyika ka kuwakamata watuhumiwa hao kwa nyakati tofauti kama ifuatavyo mnamo tarehe 11.12.2016 huko Temeke maeneo ya Keko Magurumbasi na mataa ya VETA Chang’ombe askari walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa 10 kwa makosa ya wizi kutoka maungoni na wizi kutoka kwenye magari” amesema Kamanda Sirro.

  Amesema kuwa wakati huohuo jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam kupitia kikosi chake cha kupambana na wizi wa magari kimefanikiwa kukamata magari matatu katika mikoa mbalimbali kama ifuatavyo

  1.gari Toyota T386 CGY aina ya Verosa rangi nyeusi mali ya Abraham Robert wa jijini Dar es Salaam ambapo gari hili lilikamatwa Mbeya likiwa limetelekezwa.

  2.Gari Toyota T946DGH aina ya IST rangi ya fedha ikiwa imeendeshwa na mtuhumiwa aitwaye Hamad Said ,miaka 27 mkazi wa Kimara Dar es Salaam ambapo gari hiyo ilikamatwa mkoani Morogoro,gari hiyo iliibiwa maeneo ya Kawe beach .

  0 0

  Aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mbarak Abdulwakil (kushoto) akimtambulisha Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora mbele ya menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais. Utambulisho huo umefanyika leo Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya Menejimenti wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora mara baada ya kutambulishwa.

  0 0

  A Seminar themed Implementing the African Union (AU) Declaration on Land: The Role of Regional Economic Communities, organized by the EAC Secretariat in collaboration with the United Nations Economic Commission for Africa (UNECA) was held on 7th December 2016 at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania.

  The seminar was held back to back to Sessions of the Ordinary Meeting of the African Union (AU)/UNECA Land Policy Initiative (LPI) Steering Committee that met on 6th December 2016. Prior to the LPI Steering Committee meeting, an experts planning and review meeting was held in the same venue from 4th - 5th December 2016. 

  All the meetings were hosted by the EAC and marked the first meetings of LPI Implementing Partners and Steering Committee in the EAC as a Regional Economic Community (REC).
  Group photo opportunity of the participants of the EAC-UNECA Seminar themed Implementing the African Union (AU) Declaration on Land: The Role of Regional Economic Communities held at the EAC Headquarters, Arusha, Tanzania.

  The seminar, which was attended by officials from the United Nations Economic Commission for Africa, African Union Commission, Land Policy Initiative Secretariat, and the EAC Secretariat, aimed at raising awareness on the AU agenda on land and the mandate of the RECs/EAC in this regard; and draw lessons from existing LPI/REC partnerships for possible consideration to enhance technical and financial support to implement AU Declaration on Land, by the Community.

  READ MORE HERE

  0 0


  0 0  0 0

  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC kabla ya kufungua rasmi Kikao hicho leo jijini Dar es Salaam.

   Katibu Mkuu  wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza machache kabla ya kumkaribisha  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli,katika kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC kabla ya kufunguliwa rasmi  leo jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na  Katibu Mkuu  wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC kabla ya kufunguliwa rasmi  leo jijini Dar es Salaam.
  Pichani kulia ni  Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Philip Mangula pamoja na Makamu Mwenyekiti wa (CCM Zanzibar) Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, kabla ya kuanza kikao hicho jijini Dar es Salaam. 
   Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akiwahutubia kabla ya kufungua rasmi Kikao hicho leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Wajumbe waliohudhuria kikao hicho cha NEC wakifatilia kwa makini Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC wakimkaribisha Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kufungua rasmi Kikao hicho leo jijini Dar es Salaam.PICHA NA MICHUZI JR.


  0 0

  Tanzania yetu maliasili zetu Hakuna jambo zuri kama kusherekea Sikukuu ukiwa kwenye mandhari  tulivu ambayo itakufanya ussosike na chakula kizuri  huku ukifanya vitu vipya au kuona vitu tofauti ambavyo huvioni mara kwa mara katika mzunguko wako wa maisha.

  Msimu wa Sikukuu ndiyo huu!!! Fanya sikukuu yako kuwa ya kipekee kwa kutembelea HIFADHI ZA TAIFA. Tuendelee kusapoti Utalii wa Ndani kwa kutembelea #HifadhiZetu. More info piga 0784133217| 0765908073. 

  HapaKaziTU


  0 0

  Meneja wa mabondia nyota nchini, Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile amesema amejifunza na anaendelea kujifunza masuala mbalimbali ya kuendeleza mchezo wa ngumi za kulipwa duniani kupitia kwa mapromota wakubwa kama Don King.

  Ndambile kwa sasa yopo nchini Marekani akihudhuria mkutano wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) ulioanza jana kwenye ukumbi maalrufu wa Hollywood. Akiwa Mtanzania pekee katika mkutano huo, Ndambile alisema kuwa ameweza kujiunganusha na mapromota nyota duniani ili kuleta maendeleo katika mchezo huo hapa nchini.

  Alisema kuwa ameweza kujadiliana na mapromota kadhaa ambao wanajua umuhimu wa mchezo wa ngumi za kulipwa na kupitia kampuni yake ya Advanced Security Limited ataweza kuandaa mapambano ya ngumi ya Kimataifa, yenye ubora wa hali ya juu.

  “Ubora huo utatokana na mbinu za kutafuta masoko ya ‘kuuza’ pambano au mapambano ya ngumi, mchezo wa ngumi unapendwa sana, hivyo nikiwa Mtanzania pekee niliyepata fursa hiyo, nitaitumia ipasavyo ili kufikia malengo niliyojiwekea na kwa faida ya Tanzania,” alisema Ndambile kwa njia ya simu.

  Alisema kuwa ameweza kupata ‘contact’ za mabondia makubwa, lengo kuu ni kuongeza wigo wa kazi zake na kufikia hatua ya juu kabisa katika ngumi za kulipwa.“Kinchotakiwa hapa ni kuwa makini na ‘serious’ katika kazi, ukichukulia mchezo wa ngumi kimchez mchezo, hautafikia mbali, lakini ukiuchukulia kama kazi na lengo ni kuendeleza vipaji na kujiongezea kipato, utafaidika wewe na mabondia wao,” alisema.

  Promota na meneja wa bondia Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na bondia nyota na tajiri duniani, Floyd Mayweather Jr wakati wa mkutano mkuu wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) unaoendelea kwenye ukumbi wa Hollywood Marekani.
  Promota na meneja wa bondia Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na promota nyota dunaini, Don King wakati wa mkutano mkuu wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) unaoendelea kwenye ukumbi wa Hollywood Marekani.
  Promota na meneja wa bondia Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na bondia nyota Wladimir Klitschko wakati wa mkutano mkuu wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) unaoendelea kwenye ukumbi wa Hollywood Marekani.
  Promota na meneja wa bondia Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa mkuu wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) unaoendelea kwenye ukumbi wa Hollywood Marekani.


  0 0


  0 0

  Na Mdau Kutoka Tanzania-Diaspora,  
  Hivi karibuni , Mh. Lukuvi alitangaza kiama na wamiliki wa ardhi ambao sio raia. Uamuzi huo wa kufanya hilo zoezi umetutisha sana Diaspora na mtazamo wa Serikali ya 5 kwa Diaspora.

  Naelewa sisi Diaspora tuliochukua uraia wa nje tumeukana uraia kisheria. Hilo jambo ni wazi na tunakubali.

  But the facts are;
   Diaspora tunafikia na kupita Millioni 3 ulimwengu mzima.
   Wengi tunahangaika tunasaidia nyumbani, tumetoka familia maskini. Tunasomesha ndugu zetu. Mtu anabeba maboxi masaa 18 kwa siku ili mwisho wa mwezi atume pesa nyumbani kwa ndugu zake.

  Wengi tunawekeza Tanzania, cha kwanza ni kununua ardhi, ili tujenge nyumba yakufikia tukirudi. Baadhi yetu tumezika ndugu zetu kwenye hizo ardhi, tumerithi hizo ardhi. Na ndio kitu chetu cha kujivunia. 
  "Mimi natoka Tanzania na nyumbani nina hii ardhi, na nina mpango wa kuwekeza nifanye maendeleo".
  Tunajaribu kuanzisha biashara, na kufanya chochote kuinua familia zetu. Tunahofu kubwa hatuna mtetezi Tanzania, na ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Chama ambacho wengi wetu tunakisapoti sana kwa sababu kimejitoa kutufanyia mengi. Na tulikipigania vibaya mno kwenye Uchaguzi 2015 na kubadilisha upepo wa uchaguzi nchini.

  Zoezi analofanya Mh. Lukuvi si sawa, ananyanga'nya ardhi za watu ambao wengine wamezika ndugu zao, wamerithi na wamehangakia kuzinunua. Hata kama sisi sio raia kwa kuchukua uraia wa nchi nyingine, mbele ya Mungu zoezi hilo sio la haki.

  Napenda kutoa ushauri;
   Kwa sasa Mh. Raisi aingilie kati hili zoezi afanye Executive Order;  

  1.) Kuwasamehe wazaliwa wa Tanzania tu, waliochukua urai mwingine.
  2.) Kuwaruhusu kumiliki ardhi ya Tanzania, wazaliwa wa Tanzania tu, waliochukua urai mwingine.

  Mpaka hapo sheria mpya itakapotungwa, ili tuweze kuwekeza nyumbani kwa raha na bila shaka.

  Tunaipenda sana nchi yetu Tanzania

  Na kila pumzi tunayovuta tunajivunia kuwa WaTanzania.  0 0  0 0

  Bw. Ngusa Dismas Samike ambaye 
  ameteuliwa kuwa Mnikulu Ofisi ya Rais, Ikulu.


  0 0

  Unakumbuka lile sakata la mmoja wa wagombea kiti cha Urais nchini Marekani kukumbwa na kashfa ya kutumia anwani ya barua pepe binafsi kufanya shughuli za Serikali? Au umeshawahi kuona barua pepe (Pengine unayo unaitumia) ikiwa na mchanganyiko wa herufi na namba, mfano, wateja wako watajali kweli ukiwa na barua pepe brian255@yahoo.co.tz au brian.mbunde@kampuniyako.co.tz? Sasa Extreme Web Technologies ni mshirika rasmi wa Microsoft kwa upande wa Tanzania na wanakufahamisha kwamba katika hii ulimwengu tunaoenda nao wa digitali unapokuwa na professional business email unajenga uaminifu katika biashara yako na unaonekana uko smart sana.

  Pengine bado unajiuliza “Professional Email” ni nini, ukiangalia mfano hapo juu wa barua pepe ya brian.mbunde@kampuniyako.co.tz inaonesha jina kamili la mhusika na kuna domain ya kampuni. Hii inamaanisha kwamba hauwafanyi watu waone jina lingine tofauti na jina lako halisi hivyo kuwapa mitazamo tofauti linapokuja suala la biashara (Uaminifu) na hapo ndipo Microsoft O365 inakuletea kile unachohitaji mahali unapokuwa. 
  Unapataje Barua pepe ya Biashara?

  Jinsi ya kupata ni rahisi sana, unachotakiwa kufanya ni kuwa tu na email na kisha kuwa na “domain” ambayo imehifadhiwa mahali (server). Baada ya hapo utapewa uhifadhi kumbukumbu unaofikia 1 TB, kuwekewa Microsoft Office kwenye kompyuta mpakato yako na kwenye simu yako pia. Huduma nyingine zinahusisha “HD Video Conferencing”. 

  0 0

  Na Humphrey Shao, 
  Globu ya Jamii 
  Mwanamuziki maarufu wa muziki wa taarabu hapa nchini Aisha Ramadhani a.k.a Isha Mashauzi (pichani)  anataraji kuachia kibao kipya cha kufunga na kufungua mwaka kitachokwenda kwa jina la "Kiss Me". 
  Akizungumza na Globu ya Jamii jijini Dar es salaam leo Isha Msahauzi amesema kuwa amekuwa kimya kwa kipindi kirefu hivyo kibao hicho kitaweza kuwarudisha mashabiki wake katika mstari. 
  “Hii ni zawadi ya kufunga na kufungua mwaka kwa mashabiki wangu. Hivyo mashabiki wangu wapendwa wajue kuwa nyimbo hiyo ambayo ipo katika viwango vya hali ya juu itakonga nyoyo zao",   amesema Isha Mashauzi, akiongezea kuwa imefanywa katika studio za Sophia Records  zilizopo kinondoni” 
  Ameongeza: "Waliniona  nimekuwa kimya katika taarabu sasa nimerudi tena na hiki kibao ambacho watafurahi wenyewe...."

  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameteua wafuatao kujaza nafasi mbalimbali ndani ya sekretarieti ambazo zimekuwa wazi kutokana na waliokuwa wakizishikilia kupewa majukumu mengine ya kiserikali.

  #.Ndg. Rodrick Mpogolo anakuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndg. Rajabu Luhwavi ambaye ameteuliwa kuwa balozi.

  #. Col. Ngemela Eslom Lubinga- Kuwa Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dr. Asha-Rose Migiro aliyeteuliwa kuwa Balozi.

  #. Humphrey Polepole kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Ndg. Nape Nnauye aliyeteuliwa kuwa Waziri.
  #. Wajumbe wengine watabaki kama walivyo sasa.


  Aliyekuwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kuhusu mambo mbalimbali yaliyoamriwa na chama hicho kupitia vikao vyao vilivyofanyika hivi karibuni.Picha na Michuzi Jr.


  0 0

  Na Theresia Mwami TEMESA

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme - TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu leo amefungua mafunzo elekezi kwa watumishi wa karakana juu ya mfumo wa utozaji gharama za matengenezo ya magari katika karakana za TEMESA pamoja na mfumo wa utoaji taarifa za uzalishaji na matengenezo za kila mwezi.

  Dkt. Mgwatu amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuleta uwiano sawa katika gharama za matengenezo ya magari kwa karakana zote za TEMESA bila kujali mikoa zilipo karakana hizo.

  Aliongeza kuwa utaratibu utakaoelekezwa katika mafunzo hayo utasaidia kupunguza gharama za matengenezo ya magari ya serikali, suala linalolalamikiwa na wateja wa TEMESA kwa muda mrefu sasa.


  “Nataka sasa tuanze kutoza gharama za matengenezo ya magari kulingana na muda unaotumika kutengeneza gari husika (man hour), badala ya kutumia kigezo cha asilimia ya fedha iliyotumika kununulia vipuri kwa ajili ya matengenezo ya magari, kwani baadhi ya vipuri ni ghali sana lakini hutumia muda mchache sana kuvifunga,” alisema Dkt. Mgwatu.

  Dkt. Mgwatu alisema kuwa, kumekuwa na changamoto ya uwasilishaji wa taarifa za utendaji kutoka katika mikoa/vituo vya TEMESA, mara nyingi taarifa hizi hazifiki kwa wakati. Huku akisisitiza kuwa ni matumaini yake baada ya mafunzo hayo taarifa hizo zitakuwa zikifika kwa wakati tena zikiwa sahihi.

  Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji na Matengenezo, Mhandisi Sylivester Simfukwe alisema idara yake imejipanga kutoa huduma bora zinazokidhi viwango hasa katika matengenezo ya magari ya serikali, ili kuhakikisha kuwa uzalishaji unaongezeka na kero za wateja zinakwisha.

  Aliongeza kuwa mafunzo kama hayo yatatolewa kwa wawakilishi wa karakana zote za TEMESA nchi nzima.

  Mafunzo hayo elekezi juu ya Mfumo wa utozaji gharama katika karakana za TEMESA pamoja na mfumo wa utoaji taarifa za kila mwezi, yanafanyika kwa siku 5 katika ukumbi wa MT. Depot, Dar es salaam na yamehusisha watendaji wa TEMESA kutoka mikoa ya Tanga, Morogoro, Pwani, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara, pamoja na vituo vya MT. Depot na Kikosi cha Umeme.

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme - TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu akizungumza na watumishi wa karakana za TEMESA wakati akifungua mafunzo kwa watumishi hao Jijini Dar es Salaam.


  Baadhi ya watumishi wa karakana za TEMESA wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme - TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu(hayupo Pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa watumishi hao Jijini Dar es Salaam. 

older | 1 | .... | 1460 | 1461 | (Page 1462) | 1463 | 1464 | .... | 3285 | newer