Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 144 | 145 | (Page 146) | 147 | 148 | .... | 3278 | newer

  0 0


  0 0

   Baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari za jijini Dar es Salaam, waliohudhuria kongamano la elimu kwa jamii ya kupambana na aina zote za unyanyasaji na udhalilishaji lililoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Shikamana, ambapo hutoa mafunzo mbalimbali kwa vijana wa shule za sekondari, Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii jijini.
   Juu na chini anaonekana Mwanaharakati wa mambo ya maendeleo ya jamii Joyce Kiria akitoa ushuhuda wa maisha yake  kwa wanafunzi wa shule za sekondari mbalimbali za jijini Dar es Salaam, waliofika katika  kongamano la elimu kwa jamii ya kupambana na aina zote za unyanyasaji na udhalilishaji lililoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Shikamana, ambapo hutoa mafunzo mbalimbali kwa vijana wa shule za sekondari, Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii jijini.


  0 0

  Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Isere Sports, Abbas Ally Isere (kulia) akimkabidhi jezi seti moja Dige Shaaban Nkusa kwa ajili ya timu ya vijana wa kijiji cha Mwembeni wilayani Kondoa ili kuimarisha michezo vijijini.

   KAMPUNI ya Isere Sports imetoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. mil. 1.7 kwa ajili ya kuendeleza vijana katika wilaya ya Kondoa.

  Akikabidhi vifaa hivyo jana, Mkurugenzi wa Masoko wa Isere Sports, Abbas Isere alisema ametoa vifaa hivyo ili kuwasaidia vijana kupenda michezo ili kujenga afya na kujikinga na vitendo vya uhalifu. 

  Abbas alisema vifaa alivyotoa ni kwa ajili ya vijiji vya Changaa kwa Mafunchi ambako wamepewa jezi, mipira na soksi, katika kijiji cha Mwembeni kata ya Hondomairo wilayani Kondoa wamekabidhiwa vifaa kama hivyo.

  Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya vijana wa Changaa, Issa Lubuva alisema umefika wakati kwa wananchi waishio mijini kuwakumbuka vijana waliobaki nyumbani kwa kuwapatia vifaa vya michezo.

  Naye Dige Shaaban aliyepokea vifaa kwa niaba ya kijiji cha Mwembeni alisema wachezaji wengi wapo vijijini lakini hawajapata fursa ya kuonesha vipaji vyao hivyo vifaa hivyo vitasaidia kutoa wachezaji kutoka wilaya ya Kondoa.


  0 0

  MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida atakuwa mgeni rasmi katika tamasha la Mastaa chipukizi zaidi ya 320 litafanyika Jumapili 26, 2013 katika ukumbi wa Starlight Hotel kuanzia saa 4 asubuhi.

  Mwenyekiti wa Shiwata, Caasim Taalib alisema Madabida ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) atapata nafasi ya kuona vikundi mbalimbali vya sanaa kikiwepo kikundi cha Kaole, Splendid, Super Shine Taarab pamoja na wasanii mbalimbali wa Bongo Flava, Maigizo,Ngoma, Dansi na Sarakasi nao wamethibitisha kushiriki.

  Taalib alisema wasanii wakongwe wa bongo flava walioalikwa ni Stara Thomas, Safi Theatre Group, Ommy G na waigizaji wakongwe wa Kaole na Splendid wataonesha umahiri wao katika fani ya sanaa Kauli Mbiu ikiwa ni Kilio cha Msanii .

  Vikundi vingine vitakavyonesha vipaji vyao ni Kepteni Shaibu, Tanzania Disabled, Uyoga Boga Village, Ndafu Arts Group, CGC, Magengistar Crew, Dodo Arts Group, Culture Arts Group, Wachapa Kazi Academy, Soweto Picture, Shiwata Commedy, Mwavionelachi, Manuari Arts Group, Tandale Morden Taarab na Begeja Wushu, Taalib alisema tamasha hilo ambalo limepata kibali cha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pia wamealikwa Shirikisho la Sanaa za Maonesho Tanzania,Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Shirikisho la Muziki Tanzania na Shirikisho la Sanaa za maonesho Tanzania.

  Mwenyekiti aliwaomba viongozi wengine wa bendi za muziki, taarab, vikundi vya sanaa,mapromota,maprodusa na wadau wote kushiriki katika tamasha hilo ili kujenga ushirikiano wa pamoja.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akimkabidhi Mkuu wa Mabalozi na Balozi wa DRC hapa nchini, Mhe. Juma Khalfan Mpango Mwenge wa Umoja wa Afrika (OAU/AU) kuashiria kuanza kwa maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja huo yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam
  "Brass Band" ikiongoza maandamano kutokea Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuelekea Viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 OAU/AU.


  Mhe. Membe, Mabalozi, wananchi na wageni waalikwa wakiwa katika maandamano hayo kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0
 • 05/25/13--20:00: NGOMA AZIPENDAZO ANKAL
 • Mbeya all stars wanatisha na ngoma yao ya 'Mbeya Home'

  0 0
 • 05/25/13--20:00: Ngoma azipendazo ankal
 • Sam wa Ukweli alitetemesha na ngoma yake ya 'Sina Raha'

  0 0
 • 05/25/13--21:00: Mkataa kwao mtumwa
 • Mambo ya 'Kioda' toka Songea hayo...

  0 0


  0 0

  Injinia Mbogo Futakamba, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Usalama wa Chakula na UShirika akizungumza wakati wa Kikao cha Tatu cha Kazi kilichokuwa kikijadili kuhusu maeneo mapya takayoweza kuingizwa katika Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu ( SDGs). Naibu Katibu Mkuu aliongoza ujumbe wa Tanzania katika Kikao hicho kilichomalizika mwishoni mwa wiki hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York.Tanzania ni kati ya Nchi 30 zilizochaguliwa kushiriki majadiliano hayo. Maeneo ambayo yalijadiliwa katika Kikao hicho ni ; upatikanaji wa chakula na lishe bora, kilimo endelevu, mmomonyoko wa udongo, ukame na kuongezeka kwa jangwa, upatikanaji wa maji na ushughulikiaji wa maji taka.


  0 0

  Jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.
  Mkuu wa Wilaya ya Kilwa,Mh. Abdalah Ulega akizungumza na wadau waliokutana leo kwa ajili ya kujadili Amani na Maendeleo ya Wilaya hiyo kufuatia machafuko yanayoendelea hivi sasa mikoa ya Kusini kutokana na Kutokuwepo Ushirikishwaji baina ya watendaji wa Serikali na Jamii hali inayochangia jamii nyingi Nchini Kukosa Imani na Serikali yao.
  Baadhi ya Wadau waliohudhulia mkutano huo.


  Na Abdulaziz video-kilwa

  Serikali wilayani Kilwa imetakiwa kuwa na uwazi katika fursa mbalimbali za maendeleo kwa kushirikisha jamii ili kufanikisha wilaya hiyo kuinuka kiuchumi kupitia Raslimali zilizopo Wilayani humo.

  Hayo yameelezwa na baadhi ya wadau waliokutana leo kwa ajili ya kujadili Amani na Maendeleo ya Wilaya hiyo kufuatia machafuko yanayoendelea hivi sasa mikoa ya Kusini kutokana na Kutokuwepo Ushirikishwaji baina ya watendaji wa Serikali na Jamii hali inayochangia jamii nyingi Nchini Kukosa Imani na Serikali yao.

  Wakichangia katika kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa PEC wilayani humo na kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, siasa ,asasi za jamii na watendaji wa serikali waliokutana katika kikao kilichoitishwa na Mkuu wa wilaya hiyo,Abdalah Ulega kimelenga kuzungumzia hali ya amani ,usalama na maendeleo ya kilwa ambapo alitoa fursa kwa wananchi hao kujadili kwa undani na kuweka mikakati ya kuhakikisha Amani Inadumishwa ndani ya wilaya hiyo na Mkoa.

  Awali akitoa taarifa ya Mapato ya mrahaba wa Gesi asilia ya Songo Songo kwa Wilaya,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Addoh Mapunda alibainisha kuwa licha ya wananchi wanaoishi eneo la Songosongo kunufaika na gesi inayopatikana kwenye kijiji cha Songosongo alieleza Kuwa Madiwani wa Halmashauri hiyo wamepitisha 35% ya malipo ya mrahaba huo wa gesi utumike katika kuboresha elimu Nae Mkuu wa Wilaya Hiyo,Abdallah Ulega aliwasihi wananchi wa Wilaya hiyo kujipanga na Kushirikiana na Serikali yao kudumisha Amani ikiwa pamoja na kufungua fursa kwa Wananchi kueleza changamoto na kero mbalimbali walizonazo kabla hawaichukia Serikali kutokana na Ushawishi wa Dini na Siasa ikiwemo na Mataifa mbalimbali.

  Kufuatia uwepo wa Gesi asilia ya Songosongo wilaya ya Kilwa upata mrahaba wa Mil 100 kwa Mwezi ambapo asilimia 35 hutumika katika kuboresha Elimu,Asilimia 20 kijiji cha Songosongo huku 45% zikichangia katika shughuli za maendeleo wilayani humo.

  0 0

  The Countdown to the launch of Big Brother The Chase has begun! With just two days to go, many surprises await eagerly anticipating audiences across the continent, including the all important Big Brother house. A character in its own right, the house is always subject to interest and now AfricaMagic has unveiled a sneak peek in the Big Brother house.

  Modern, trendy and contemporary are just some of the words that define the imagery of the house. This year’s look is definitely distinctive, featuring a solid use of bright colour with a sophisticated polish. The décor is fresh and airy with a cosmopolitan and yet youthful demeanor, dominated by straight lines and square finishes.

  Audiences and housemates can also expect intriguing fixtures that will certainly create talkability. There are also unique accessories thoughout the house creating a cosy and homey ambiance. The house is also technically well equipped and Biggie can watch 24/7, thanks to 56 cameras and 137 microphones.

  More of the house will be revealed on Sunday May 26 at 20:00 when audiences from over 50 African countries are introduced to the 28 housemates for the first time. Tune into the Big Brother live launch show on AfricaMagic, AfricaMagic Entertainment and AfricaMagic World, as well as on DStv channel 197 and 198. The launch will also stream live on the Big Brother website.
  Big Brother The Chase is headline sponsored by Airtel and is produced by Endemol.

  The excitement is building and audiences can also join the conversation on Facebook and Twitter. Africa biggest reality series will be screened live 24/7 on DStv channels 197 and 198.

  0 0

  Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania, Phocus Lasway (kulia) akikabidhi vazi la suti mpya maalum kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) kwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah wakati wa hafla maalumu ya kuonesha vazi hilo la suti mbele ya wageni mbali mbali waliohudhulia hafla hiyo,iliyofanyika jana jioni kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar. Wa pili kulia Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe.
  Wachezaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) wakipita jukwaani huku wakiwa wamevalia suti hizo wakati wa hafla maalum ya kuonyesha mavazi yao hayo iliyofanyika jana jioni Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar.
  Wachezaji wa Taifa Stars, benchi la ufundi na maofisa wakuu wa TBL wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kuonesha suti mpya
  Wachezaji wa Taifa Stars na benchi la ufundi katika picha ya pamoja.
  Wadau wa soka nchini wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi suti mpya kwa Taifa Stars.

  0 0

  Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam Serikali imesema itaendelea kuhakikisha makandarasi wazalendo wanaendelea kupata msaada unaotakiwa ili kuendeleza sekta ya ujenzi hapa nchini.

  Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli alipokua akifunga mkutano mkuu wa mwaka wa majadiliano wa bodi ya makandarasi Tanzania uliomalizika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  “Serikali inathamini kazi yenu na itaendelea kuwaunga mkono kila inapowezekana,” alisema.

  Dkt. Magufuli alisema serikali imetenga kiasi cha Tshs 500.4 bilioni kwa ajili ya miradi mbalimbali ya mfuko wa barabara kwa mwaka huu na kuahidi kuwa miradi hiyo itafanywa na makandarasi wa ndani.

  Alisema kila serikali duniani inasaidia watu wake na serikali ya Tanzania itafanya kila juhudi kusaidia makandarasi wa ndani kama njia ya kusaidia wananchi wake.

  “Mkipewa kazi hakikisheni mnafanya vizuri na kwa kufuata maadili, kanuni na sheria,” alisema.

  Alisema haiwezekani asilimia 60 ya kazi katika sekta ya ujenzi kumilikiwa na makandarasi wa nje wakati wao ni asilimia 10 tu ya makandarasi hapa nchini. Kuna jumla ya makandarasi wazalendo 7,000 hadi sasa.

  Hata hivyo aliihimiza bodi ya makandarasi kuendelea kufuta usajili wa kampuni za makandarasi ambazo zinakiuka maadili ya kazi ili kulinda uchumi wa nchi na kulinda usalama wa wananchi na mali zao.

  “Endeleeni na kufuta usajili wa wale wanaokiuka maadili...nawapongeza kwa hili,” alisema.

  Alizitaka benki hapa nchini kuonyesha uzalendo kwa kubuni njia za kuwasaidia makandarasi na pia kulegeza masharti ya mikopo kwao. Kwa upande wake, Msajili wa CRB, Injinia Boniface Muhegi alisema ni vyema makandarasi waheshimu ushauri wa kitaalamu wanaopewa ili kuweza kutekeleza kazi zao kwa ufanisi.

  Alisema kuanzia sasa bodi yake itakaza uzi kwenye usajili wa makandarasi na kuwafanyia tathmini kila baada ya miaka mitatu. Pia alisema kuanzia sasa bodi kwa kushirikiana na mamlaka nyingine husika zitahakikisha kuwa hakuna mkandarasi mmoja atakaerundikiwa kazi nyingi wakati wengine hawana na kusema kuwa rushwa itapigwa marufuku kwa nguvu zote.

  Awali, Mwenyekiti wa bodi ya CRB, Eng. Consolata Ngimbwa alissitiza makandarasi nchini kuungana ili kuwa na nguvu na pia kuweza kushindana na wale wa nje ambao wengi wao wana nguvu za mitaji, na utaalamu.

  “Tuungane ili na sisi tuweze kupata sifa za kupata miradi mikubwa,” alisema.

  Akifafanua zaidi alisema kuwa makandarasi wa madaraja ya juu washirikishe wale wa madaraja ya chini ili waweze kufanya kazi pamoja kwa faida yao wote na kwa faida ya taifa kwa ujumla.

  “Makandarasi wa madaraja ya juu waruhusu ushirika na wale wa madaraja ya chini ili kuleta mafanikio zaidi,” alisema. Mkutano huo wa siku mbili ulilenga kuangalia changamoto na mafanikio katika sekta ya ujenzi Tanzania ndani ya miaka kumi na tano iliyopita.

  Mapendekezo ya mkutano huo yatapelekwa kwa wadau husika na baadae kufuatilia utekelezaji wake. Takwimu zinaonyesha kwamba sekta ya ujenzi inachangia asilimia saba ya pato la taifa huku ukuaji wake kwa mwaka ikikadiliwa kuwa ni asilimia kumi na moja ikiwa ni sekta ya pili kwa kasi ya ukuaji huku sekta ya madini ikiongoza. Asilimia sitini ya bajeti ya maendeleo nchini inakwenda kwenye sekta ya ujenzi huku asilimia themanini ya fedha hizo zikienda kwa wanachama wa bodi ya usajili wa mandarasi wa ujenzi.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizingumza na Marais Wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Mzee Benjamin Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Afrika Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim kuhusiana na sherehe za miaka 50 ya AU alipokutana nao jijini Addis Ababa, Ethiopia, leo Mei 26, 2013. Viongozi hao wastaafu ni miongoni mwa wageni mashuhuri walioaliokwa kwenye sherehe hizo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika Mkutano wa Kanda wa Usimamizi wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika DRC na nchi za Maziwa Makuu katika makao makuu ya Umoja wa Afrika leo Mei 26, 2016.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na wanahabari baada ya kuhudhuria Mkutano wa Kanda wa Usimamizi wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika DRC na nchi za Maziwa Makuu katika makao makuu ya Umoja wa Afrika leo Mei 26, 2016.PICHA NA IKULU.

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kushoto) akipongezana na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Namibia, Kamishna Jenerali Evaristus Shikongo baada ya kusaini makubaliano ya kutoa mafunzo kwa maafisa wa Jeshi la Magereza wa nchini Namibia. Tukio hilo lilishuhudiwa na maafisa mbalimbali wa majeshi hayo. Makubaliano hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Namibia, Kamishna Jenerali Evaristus Shikongo akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Namibia, Kamishna Jenerali Evaristus Shikongo akiijaribu moja ya silaha inayotumika kwa ajili ya kutuliza ghasia wakati wowote inapotokea ndani na nje ya gereza. Shikongo alionyweshwa silaha mbalimbali ambazo zinatumika kwa ulinzi na kutuliza ghasia Magerezani katika maonyesho yaliyoandaliwa kwa ajili yake na Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia cha Jeshi la Magereza, Ukonga Dar es Salaam.
  Askari wa Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani, wakimuonesha mbinu za kupambana na adui pasipo kutumia silaha Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Namibia, Kamishna Jenerali Evaristus Shikongo (hayupo pichani) pamoja na makamishna wengine wa jeshi hilo ambao walitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ya Jeshi hilo, Ukonga jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, ACP Mbaraka Semwanza akitoa taarifa fupi ya chuo hicho kwa Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Namibia, Kamishna Jenerali Evaristus Shikongo (katikati). Kushoto aliyekaa ni Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk Juma Malewa, kulia ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga, anayefuata ni Kamishna wa Rasilimali Watu, Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza nchini Namibia, Clementine Feris. Picha na Felix Mwagara.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Ilala ambaye pia ni Naibu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mushi (kulia) akipokea Tuzo za Bia Bora Afrika ambazo Bia ya Safari Lager inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ilishinda katika Mashindano ya Bia Afrika yaliyofanyika nchini Ghana. Tuzo hizo zitatembezwa katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kwa siku mbili. Anaemkabidhi tuzo hiyo ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
  Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Ilala ambaye pia ni Naibu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mushi wakinyanyua Tuzo za Bia ya Safari Lager ilizoshinda katika mashindano ya Bia Afrika yaliyofanyika nchini Ghana. Tukio hilo lilifanyika jana katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam wakati wa ziara maalum ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kuonesha Tuzo ilizoshinda Bia yake ya Safari Lager ambapo zitatembezwa katika mitaa mbalimbali ya jiji hilo kwa siku mbili.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala ambaye pia ni Naibu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Raymond Mushi akizungumza na wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye eneo la wazi la Ilala Mchikichini kushuhudia Kombe la Ushindi wa Bia Bora Barani Afrika ulioupata Bia ya Safari Lager.
  Wakazi wa jiji la Dar wakiwa wamefurika kwa wingi kushuhudia Kombe hilo la Ushindi wa Bia Bora Barani Afrika Ulioupata Bia ya Safari Lager.

  0 0

  Meneja wa Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto) akimkabidhi ufunguo wa gari mshindi wa The Vodacom Mic King 2013, Martin Fundi. Katikati ni Meneja Matukio wa Dar Live, Abdallah Mrisho. Martin Fundi akifungia mlango wa gari lake.
  ...Akiingia.
  ...Akiliwasha gari lake.
  Mashabiki wakiwa wamelizunguka gari la Martin Fundi.

  Martin Fundi kutoka Kimara usiku wa kuamkia leo ameibuka kidedea katika shindano la The Vodacom Mic King 2013 na kujinyakulia gari jipya aina ya Toyota Funcargo (new model). Shindano hilo lililokuwa likidhaminiwa na Kampuni ya simu ya Vodacom lilidumu kwa takribani miezi sita na usiku wa kuamkia leo ndiyo limefika tamati.
  (PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL)

  0 0
 • 05/26/13--03:27: TNBC yaipa changamoto TCCIA
 • Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Bw. Raymond Mbilinyi akizungumza na wafanyabiashara wa Mkoa wa Dar ES Salaam wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha wenye Viwanda Biashara na Kilimo Mkoa wa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki(Kulia) ni Makamu wa Rais wa TCCIA Taifa, Bw. John Mayanja, katikati ni Rais wa Chama hicho Mhandisi Aloyce Mwamanga na mwisho Kulia ni Katibu Mkuu Bw. Isaac Dalushi.
  Rais wa Chama cha wenye viwanda Biashara na Kilimo nchini (TCCIA), Mhandisi Aloyce Mwamanga(Kulia) akimkaribisha Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC ), Bw. Raymond Mbilinyi aweze kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha wenye viwanda Biashara na Kilimo Mkoa Dar es Salaam, mkutano huo uliofanyika mwishoni.

older | 1 | .... | 144 | 145 | (Page 146) | 147 | 148 | .... | 3278 | newer