Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1449 | 1450 | (Page 1451) | 1452 | 1453 | .... | 3270 | newer

  0 0
  0 0

   Mlimbwende anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma 2016/17), Anna Nitwa (wa pili kulia) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (wa pili kushoto) pamoja na madaktari wakati wakielekea kwenye Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Desemba 1, 2016.

  Mrembo huyo ambaye aliguswa na hali aliyoikuta hapo awali wakati alipotembelea Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti) hasa pale alipoona mazingira ya choo cha kina Mama hao kuwa si ya kuridhisha kwa afya ya mama na Mtoto na ikizingatiwa kuwa watoto hao wanahitaji uangalizi wa hali ya juu, alijitolea kukikarabati Choo hicho na Desemba 1, 2016 alikikabidhi kwa uongozi wa Hospitali hiyo ya Mkoa wa Dodoma.

  Akizungumza mbele ya wanahabari pamoja na uongozi wa Hospitali hiyo, Mrembo Anna Nitwa alisema "Siku ya Novemba 4, 2016 nilitembelea Wodi ya Watoto Njiti wakati wa kujiandaa na siku ya maadhimisho ya watoto wazaliwao kabla ya wakati ambayo ilikua Novemba 17, Niliona mazingira ya choo kilichokua kinatumiwa na Wazazi wa Watoto Njiti pamoja na wauguzi wao, hakikua katika hali nzuri. Hivyo niliahidi kushirikiana na washikadau mbalimbali ili kuweza kukarabati.

  Aliendelea kusema kuwa "Wazazi wangu pamoja na watu wachache walioguswa waliweza kushirikiana nami kuchangia fedha za kukarabati choo hicho, na kazi ya ukarabati imekamilika na sasa nimekikabidhi.

  Kwa Upande wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde aliyeambatana na Mrembo huyo Hospitalini hapo, alimpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya na kumuahidi kuijenga korido ambayo itaunganisha Wodi hiyo na choo ili kuwasaidia wakina mama hao kuwa katika mazingira ya ulinzi hasa nyakati za usiku, kwani kwasasa choo hicho kipo kwa nje ya wodi hiyo, hivyo korido ikijengwa itawasaidia sana. 

  Kwa upange wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Dodoma,Dkt. James Charles alitoa shukrani kwa Mrombo huyo kwa jitihada zake za kufanikisha ukarabati huo, na hasa kwa moyo wake wa kujitolea, na kuwaomba Watanzania wengine kujitolea kufanikisha mahitaji mengine Hospitalini hapo.
  Mlimbwende anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma 2016/17), Anna Nitwa (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (katikati) wakiwa katika Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Desemba 1, 2016.
  Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde akiangalia namna Choo hicho kilivyokarabatiwa kwa jitihada za Miss Dodoma 2016/17, Anna Nitwa.
  Mlimbwende anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma 2016/17), Anna Nitwa akiwa amewabeba watoto Mapacha, wakati alipotembelea Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Desemba 1, 2016.

  0 0

  Mwendesha bodaboda akiiangalia Gari ndogo aina ya Toyota Raum yenye namba za usajili T 690 CMS iliyopata ajali usiku wa kuamkia leo katika eneo la Kiguza, Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio la ajali hiyo, wanaeleza kuwa Gari hiyo iliyokuwa ikitokea upande wa Hoyoyo kuelekea Mkuranga, iliacha njia na kwenda kugonga mti uliokuwepo kando ya barabara hiyo, kwa madai ya dereva wake kushindwa kuona vizuri baada ya kumulikwa na taa kali (full light) ya gari iliyokuwa inakuja mbele yake. Hakuna aliyepoteza maisha kwenye ajali hii. 
  Inavyoonekana gari hiyo baada ya kupiga mzinga.
  Break Down au wazee wa kubeba visivyojiweza, wakiipiga cheni gari hiyo.
  Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, 
  Globu ya Jamii

  MAHAFALI ya 10 Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) yafana kwa wahitimu 944 kutunukiwa shahada mbalimbali za masomo ya Afya huku Mkuu wa Chuo Rais Mstaafu, Alhaji D Ali Hassan Mwinyi akiwatunukiwa wanafunzi saba shahadan ya uzamivu.
  Mahafali hayo yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam, Makamu Mkuu wa Chuo MUHAS, Ephata Kaaya amesema kuwa azma ya Chuo chao ni kuwa na wanafunzi wa kike na wakiume kwa idadi sawa kwani katika mwaka huu wa mahafali wanafunzi 372 sawa na aslimia 39.4 ni wanawake kwa hiyo bado wanaendela na mpango wa kuwawezesha wanafunzi wa kike kujikunga na programu mbalimbali zinazotolewa hapa chuoni.
  Kaaya amesema kuwa , katika kuendeleza kutoa nafasi kwa wanafunzi MUHAS wamefanikiwa kupata imefanikiwa kukamilisha ukarabati wa kliniki mpya ya wagonjwa wa afya ya kinywa na meno watakaokuwa wanajilipia wenyewe na vifaa tiba vimeshapayikana kutoka shirika lisilo la kiserikali la The Miracle Corners Of the World (MCW)la Nchini Marekani na vinategemewa kuwaili nchini na kufungwa kwenye kliniki hiyo mwezi Januari.
  Katika ,mahafali hayo, wahitimu saba waliweza kutunukiwa shahada za uzamivu kwa kufanya tafiti mbalimbali za magonjwa na dawa ambao ni Siana Nkya,Ramadhan Nondo, Dickson Mkoka, Gladys Mahiti, Grace Shayo, Coline Mahende na Richard Mwaiselo.
  Mkuu wa Chuo pia aliweza kuwatunukiwa wahitimu wawili wa shahada ya uzamili wa Sayansi Maalumu ambao ni Mohamed Mnacho na John Ngendahayo huku wahitimu nane wakipatiwa shahada ya juu katika masuala mbalimbali pia 183 shahada ya uzamili na wahitimu 376 walitunukiwa stashahada,

  Makamu Mkuu wa Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Profesa Ephata Kaaya akitoa hotuba kwa wahitimu wa Chuo hicho katika mahafali ya 10 yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam, Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho cha MUHAS, Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi na Mwenyekiti wa MUHAS  Mariam Joy Mwafisi.


   Mkuu wa Chuo 
   Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (
  MUHAS), Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi  akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Chuo cha Afya na Syansi Shirikishi kwenye mahafali ya 10 yaliyofanyika chuoni hapo leo Jijini Dar es salaam.


   Mkuu wa Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi akimtunuku Shahada ya uzamivu (PhD) Grace Shayo katika mahafali  ya 10 yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam.


  Wahitimu saba wa shahada ya Uzamivu (PhD) wa Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili wakiwa wametulia baada ya kula nondozzzz.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
   


  0 0  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Temeke  Mhe. Felix J. Lyaniva ametoa wito kwa Watanzania kujivunia bidhaa za Tanzania kupitia viwanda vyetu nchini, akisistiza kuwa Tanzania ina viwanda vinavyoweza kuzalisha bidhaa za kwetu na wananchi wajifunze kujivunia na kutumia bidhaa zetu wenyewe  ili kukuza uchumi wa viwanda.

  Hayo ameyasema akiwa mgeni rasmi kwenye makabidhiano ya nyenzo za ushonaji kwa wasiiona wanaoendelea na mafunzo maalum ya ushonaji yanayoratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).
  Mhe Lyaniva aliongeza kwa kusema tarehe 7 hadi 11 Desemba katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere kutakuwa na Maonesho ya Viwanda vya Tanzania, na katoa wito kwa wananchi waje waone viwanda vya Tanzania na bidhaa zinazolishwa Tanzania wakiwemo wasioona wanaopata mafunzo maalum ili watambue uwezo wao wa ukuzaji wa uchumi wa viwanda.
  Bw Shadrack Nkelebe, Meneja wa kiwanda cha nguo cha Urafiki amesema wamedhimiria kufanya kazi kwa karibu na Bw Abdallah Nyangalio anapoendelea kutoa mafunzo. Amesema  kwa nafasi yao ya uzalishaji wanavyo vitenge na khanga za kutosha  hivyo wanatoa ili kusaidia mafunzo maalumu ya ushonaji kwa wasioona maana kazi wanayofanya ni nzuri na yenye manufaa kwa taifa maana yanaleta maendeleo.
  "Wakati wa maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) tulivutiwa sana na utendaji kazi wake lakini ni fundisho kwetu kwamba haya yanawezekana", alisema.
  Nae Bw Abdallah Nyangalio mkufunzi na mlemavu wa macho wakati akipokea nyenzo hizo ameshukuru kupatiwa vifaa hivyo ambavyo vitamwezesha katika mafunzo yao na ana imani watafika mbali na kwamba tangu waanze mafunzo hayo tarehe 19 mwezi Oktoba, 2016 wanafunzi wamepiga hatua kubwa
  Kaimu Mkurgenzi wa TanTrade Bw Edwin Rutageruka,  amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Temeke na Meneja Mkuu wa Kiwanda cha URAFIKI kwa msaada  wa nyenzo (Cherehani kutoka kwa Mkuu wa Wilaya na Majora kutoka Urafiki ) ambazo zitawasaidia katika mafunzo maalum ya ushonaji kwa wasiiona.
  "Lengo la Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ni kuhakikisha baada ya mafunzo hayo walemavu hawa wasioona watafutiwe na kupata masoko ya ndani na je ya nchi", alisema na kutoa wito kwa wananchi waje kuona kiwanda cha mlemavu asiyeona katika  kipindi hicho cha maonesho ya viwanda vya Tanzania maana atashiriki.  
   Mkuu wa Wilaya ya Temeke  Mhe. Felix J. Lyaniva akikakata utepe kama ishara ya kukabidhi msaada wa  cherehani kwa Bw.  Abdallah Nayngalio ambaye ni mkufunzi asiyeoona anayetoa  mafunzo maalum kwa ya ushonaji kwa wasioona yanayoratibiwa na Mamlaka ya  Maendelo ya  Biashara Tanzania (TanTrade). Kulia ni Bw Edwin Rutageruka, Kaimu Mkurgenzi wa TanTrade akifuatiwa na  Meneja Mkuu wa kiwanda cha URAFIKI  Bw Shadrack Nkelebe.
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke  Mhe. Felix J. Lyaniva akishuhudia Meneja Mkuu wa kiwanda cha nguo cha URAFIKI Bw Shadrack Nkelebe akimkabidhi majola ya vitenge kwa Bw Abdallah  Nyangalio ambaye ni mkufunzi asiyeoona anayetoa mafunzo  maalum ya ushonaji kwa wasioona yanayoratibwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade). Kulia ni Bw Edwin Rutageruka, Kaimu Mkurgenzi wa TanTrade. Habari na picha na Theresa Chilambo wa TanTrade.


  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba kufanya uchunguzi kwa nini mbolea ya minjingu inayozalishwa nchini haitumiki na badala yake inaagizwa mbolea kutoka nje ya nchi.

  Ametoa agizo hilo jana (Jumamosi, Desemba 3, 2016) wakati alipotembelea kiwanda cha Fibre Board 2000 Limited ambacho kinatengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo mbolea ya Minjingu, wakati akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani Arusha.Alisema mbolea hiyo licha ya kuwa na viwango vya ubora vinavyohitajika, haitumiki nchini kwa sababu ya kuingiliwa na masuala ya kisiasa dhidi ya matumizi yake.

  “Nchi jirani ya Kenya inaiona mbolea hii bora kuliko sisi wa ndani? Mheshimiwa Waziri wa Kilimo are we serious? Tunazalisha mbolea hapa tunasema haina kiwango lakini Kenya wanaitaka na wameagiza tani 300,000,” alisema.

  Waziri Mkuu aliongeza kuwa “Jambo hili lazima liangaliwe ndani ya Wizara kwa nini mnaagiza mbolea kutoka nje wakati ndani tunazalisha hii ni mianya ya rushwa, rushwa ulaji ulaji tu. Waziri lichukulie maanani jambo hili hatutaki siasa katika sekta ya kilimo,”.Alisema kumekuwa na mijadala mingi kuhusu mbolea ya minjingu kumbe baadhi ya watendaji wanatengeneza mianya ya kwenda kununua mbolea nje ambako hutumia fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika katika miradi mingine ya maendeleo.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa kiwanda cha Fibre Board 2000 Limited, Tosk Hansi  amesema kampuni hiyo inayozalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo mbolea ya minjingu, imetoa ajira kwa watu zaidi ya 1,800 wengi wao wakiwa ni vijana ila inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya urasimu wakati wanapoomba vibali vya uvunaji mazao ya misitu.
  Awali, kampuni hiyo ya Fibre Board 2000 limited imemkabidhi Waziri Mkuu mchango wa madawati 1,000 kwa ajili ya shule mbalimbali za mkoani Arusha ili kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU

  JUMAPILI, DESEMBA 4, 2016.

  0 0


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema amekabidhi pikipiki 200 zenye thamani yash. milioni 400 kwa vijana 200 wa Jiji la Arusha, ili kuweza kuwakwamua kiuchumi

  vijana hao ambao walikuwa wakiendesha pikipiki za watu ambazo hazina tija. 
  Pikipiki hizo zimechangwa na wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani Arusha baadaya Mkuu wa Mkoa huo Bw. Mrisho Gambo kubuni mpango huo ambao umewawezesha

  vijana kupata pikipiki bila riba wala dhamana. 
  Waziri Mkuu alikabidhi pikipiki hizo jana jioni (Jumamosi, Desemba 3, 2016) marabaada ya kumaliza kuhutubia maelfu ya wananchi waliohudhutia katika mkutano wa hadhara kwenye uwanja cha Sheikh Amri Abeid. 
  Baada ya kukabidhi pikipiki hizo, Waziri Mkuu aliwataka vijana kuhakikisha wanakuwawaaminifu kwa kufanya kazi kwa bidii ili pikipiki ziweze kuwasaidia kuwainua kipato.

  Katika hatua nyingine
   Waziri Mkuu alisema  mwananchi yeyote hata kama si mtumishi wa umma anawajibu wa kuiheshimu Serikali na kuitumikia. Hivyo aliwataka vijana hao kuwa waadilifu.
   
  “Serikali ya awamu ya tano imeanza kazi na moja kati ya majukumu yetu ni kuboresha nidhamu ndani na nje ya Serikali hivyo ni lazima ipate heshima yake,” 
  “Tumeamua kuwatumikia. Tumeamua kuwahudumia watanzania wote bila ya kujali itikadi zao za kisiasa na kidini na Mheshimiwa Rais anataka kuona wananchi wake akifurahia Serikali yao,” alisema. 
  Kwa upande wake Bw, Gambo alisema pikipiki hizo zilizokabidhiwa kwa vijana hao zimetolewa sanjari na bima kubwa (Comprehensive Insurance) kwa vijana 200 ambapo kila Kata ilitoa vijana wanane

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alisema zaidi ya sh. bilioni 800 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Arusha. Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi alisema kati ya fedha hizo sh. bilioni 476 zitatumika katika ujenzi wa miradi wa maji ili kumaliza kero hiyo. 
  “Mkoa wa Arusha unakabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji safi na salama, hivyo fedha hizo zinalenga kumaliza tatizo hilo ambalo limechangiwa na uharibifu wa mazingira,” alisema. 
  Alisema kiasi kingine cha sh. bilioni 264 kilitolewa ili kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika mkoa huo. “Umeme Arusha hautakiwi kukatikakatika huu ni mji wa utalii. Tanesco imarisheni mtandao wa usambazaji,”.

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipoingia kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha kuhutubia mkutano wa hadhara Jumamosi.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua kiwanja chenye mgogoro karibuna  na soko la Kilombero Arusha ambacho alitangaza katika mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuwa serikali imekichukuwa na kuliagiza jiji la Arusha liweke mazingira kuwawezesha  wafanyabiashara wadogowadogo kuendesha shughuli zao hapo. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kofia gumu  Roman Mollel ikiwa ni ishara ya kumkabidhi pikipiki katika tukio la kukabidhi pikipiki 200  kwa vijana wa bodboda wa Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abed jijini Arusha , Desemba 4, 2016
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Pikipiki Bw. Dennis Shangari katika tukio la kukabidhi pikipiki 200 kwa vijana  wa bodaboda kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


  0 0  0 0

   Wananchi wa kijiji cha Nyatanga kilichopo Kata ya Panzuo Tarafa ya Mkamba mkoani Pwani wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega alipokuwa akizungumza nao na kupanga nao mikakati ya kujikwamua na umaskini kwa namna moja ama nyingine.
   Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega akikagua jengo la Zahanati ya Nyatanga iliyojengwa kwa fedha za wananchi wa kijiji cha Nyatanga kilichopo Kata ya Panzuo Tarafa ya Mkamba mkoani Pwani. 
   Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa wa kijiji cha Nyatanga kilichopo Kata ya Panzuo ,Tarafa ya Mkamba ambapo yupo katika ziara za kikazi katika  jimbo lake hilo la Mkuranga mkoani Pwani.Mh.Ulege ameendelea na ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wake,ikiwemo pia na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo
   Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya  Mkuranga mkoani Pwani,Mhandisi Mshamu Munde akifafanua jambo katika mkutano uliofanyika kwenye  kijiji cha Nyatanga kilichopo Kata ya Panzuo ,Tarafa ya Mkamba mkoani Pwani.Picha Emmanuel Massaka Globu ya Jamii.


  0 0

   Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi (hawapo pichani) wakati alipowasili wilayani humo kufuatilia utendaji kazi na utoaji huduma wa sekta ya ardhi kwa wananchi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Bw. Said Mtanda.
   Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Bw. Said Mtanda akitoa ufanunuzi kwa wananchi mbele ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula kuhusu masuala mbalimbali ya ardhi  yanayotakiwa kufuatwa na wananchi pindi wanapofuatilia huduma za ardhi.  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kanondo kilichopo wilayani Nkasi mkoani Rukwa  mara baada ya kuwasikiliza kuhusu matatizo wanayokutana nayo katika sekta ya ardhi.

  0 0
  0 0

  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles  Mwijage (pichani) amesema kuwa wawekezaji na wamiliki wa viwanda wasiwe na wasiwasi kwa kuwa Tanzania ina mazingira mazuri ya uwekeza tofauti na inavyotafsiriwa na baadhi ya watu ambao wa nia ya kuwahujumu wawekezaji.
  Akizungumza katika kipindi cha Mizani ya Wiki cha Azam TV, Mhe.   Mwijage amefafanua kuwa serikali haina nia yoyote ya kukihujumu kiwanda cha Dangote kwa kuwa lengo la serikali ya awamu ya Tano ni kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Kwa kupata zaidi Usikose kuangali kipindi cha Mizani ya Wiki ifikapo saa mbili na nusu Azam Two.

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Hamad Massaun amewahimiza viajana nchini kushiriki michezo ili kuinua vipaji vitakavyowezesha Tanzania kupata wachezaji wazuri watakaoliwakilisha vyema taifa katika michezo ya kimataifa.

  Massaun alitoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa mgeni rasmi katika kilele cha michezo ya hisani iliyoandaliwa na klabu ya Gymkhana ya jijini Dar Es Salaam kwa lengo la kusaidia kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park  ambacho kinahudumia vijana katika michezo mbalimbali.

  Massaun alisema ikiwa wazazi watawasimamia vyema watoto wao katika michezo tangu wakiwa wadogo basi hapo baadaye nchi yetu itakuwa na wachezaji wengi ambao wataiwakilisha vyema nchi katika masdhindano mbalimbali.

  “Katika nchi nyingine wachezaji wakubwa hawakuibukia ukubwani, walianza kujiimarisha tangu udogo wao na ndio maana wanafanya vizuri hivyo na sisi tujielekeze huko ili tuwe  na wachezaji bora kama wao na serikali itaendelea kutoa msaada wa kila aina unaohitajika ili kufanisha azma hiyo ” Alisema Massaun.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ufundi wa Kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park Bw. Ray Power alisema misaada itakayopatikana kutokana na michezo hiyo ya hisani itatumika kuwaendeleza vijana wadogo waliopo katika kituo hicho ambacho kimejumuisha michezo mbalimbali.

  Katika kilele hicho Naibu Waziri Massaun alitoa zawadi mbalimbali kwa washindi katika michezo tofauti iliyoshirikishwa ikiwemo mpira wa miguu, tenesi, magongo na gofu. 
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Hamad Massauni akisalimiana na wachezaji wa timu ya watoto kutoka shule ya IST ya jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi katika michezo ya hisani iliyoandaliwa na klabu ya Gymkhana jana ikiwa na lengo la kusaidia kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park cha jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Hamad Massauni (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya watoto kutoka shule ya IST (wenye jezi za blue) na timu ya watoto wa kituo cha Dar es Salaam Academy (wenye jezi nyeusi) kabla ya mchezo wao wakati alipokuwa mgeni rasmi katika michezo ya hisani iliyoandaliwa na klabu ya Gymkhana jana ikiwa na lengo la kusaidia kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park cha jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Hamad Massauni akimkabidhi kombe la ushindi nahodha wa timu ya watoto wa kituo cha Dar es Salaam Academy baada ya kuibuka mabigwa katika michezo ya hisani iliyoandaliwa na klabu ya Gymkhana jana ikiwa na lengo la kusaidia kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park cha jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Amali, Maalim Abdalla Mzee wakati alipotembelea Ujenzi wa Skuli mpya ya Sekondari katika Kijiji cha Mkonjoni Wilaya ya Kaskazini B Unguja kuangalia ujenzi wa Skuli ya hiyo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe,Vuai Mwinyi Mohamed wakiangalia kisima kiliopo katika kijiji cha Mkonjoni Wilaya ya Kaskazini B Unguja ambacho Wananchi wakijiji hicho hujipatia huduma ya maji kwa matatizo makubwa na usumbufu.


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwafariji wanawake waliolazwa kwenye wodi ya wazazi katika hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru wakati alipotembelea wodi hiyo na kukuta wakiwa wamelala watatu kwenye kitanda kimoja Desemba 4, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akielekea kwenye wodi ya wazazi katika hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru wakati a;lipoitembelea Desemba 4, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Monduli baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo kuanza ziara ya siku moja ya kazi wilayani humo Desemba 4, 2016. 


  0 0

  Mkurugenzi wa MM Connects Ltd, Emmanuel Makaki( kushoto) akifurahia tuzo yake ya ubora katika Mauzo ya Rejareja iliyotolewa na Vodacom Tanzania, mara baada ya kukabidhiwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshangilia ni timu ya wafanyakazi wa kampuni hiyo kitengo cha Mauzo ya Rejareja ambao walitembeklea duka hilo lililopo Kariakoo jijini.
  Wateja wa Vodacom Tanzania, wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa kitengo cha Mauzo ya Rejareja wa Vodacom Tanzania, Brigita Stephen (wa pili kushoto) wakati yeye na timu ya wafanyakazi wenzake wa kitengo hicho walipotemvbelea duka la Vodacom Samora Avenue jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi wa Deltaafrica, Mohamme Araz (kulia) na wafanyakazi wenzake wakifurahia tuzo yao ya ubora katika Mauzo ya Rejareja iliyotolewa na Vodacom Tanzania, wakati wafanyakazi wa kitengo cha Mauzo ya Rejareja walipotemblea duka lake la Vodacom Samora Avenue jijini Dar esSalaam leo.


  0 0

  Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' (TBN) kilichosajiliwa rasmi na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani, mwezi Aprili, 2015 na kupewa namba ya usajili, S. A 20008.  Kinapenda kuwataarifu kuwa kinatarajia kuanza mkutano wake mkuu na mafunzo kwa Bloggers kesho Jumatatu tarehe 5 -6 mwezi wa 12/2016.

  Mkutano huo na mafunzo kwa wanachama utafunguliwa rasmi na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk. Hassan Abbas katika Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Golden Jubilee Tower jijini Dar es Salaam. Mkutano huo uliodhaminiwa na Benki ya NMB na wadhamini wengine unatarajia kuanza majira ya saa mbili na nusu asubuhi na kufanyika kwa siku mbili mfululizo.

  Katika mkutano huu wanatasnia watapewa semina juu ya uendeshaji mitandao ya jamii kwa manufaa, upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuziangatia maadili na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji (kujipatia kipato) hasa ukizingatia kuwa wapo baadhi yetu tunaifanya kazi hii kama ajira nyingine.

  Aidha katika mkusanyiko huu mbali na washiriki kupata mafunzo pia watapata muda wa kujadili masuala mbalimbali ya umoja wao na kutoka na mkakati wa kuijenga zaidi TBN kwa mafanikio ya wana Blogu.
  Mkutano huu ni matokeo mazuri ya ushirikiano kati ya TBN na wataalam wa masuala ya habari na mitandao ya kijamii, ambao kwa pamoja tumeandaa semina hii kwa wanahabari wa mitandao ya kijamii hasa 'Bloggers' kwa lengo la kujifunza zaidi na kujadili masuala mbalimbali ya chama na tasnia nzima.

  TBN inaendelea kuishukuru Serikali kupitia taasisi zake ikiwemo Mamlaka ya Udhibiti Mawasiliano nchini (TCRA) kwa kutoa ushirikiano mkubwa hadi kuwezesha chama hiki cha wamiliki/waendeshaji mitandao ya jamii kukamilisha mchakato wa usajili wake.

  Lakini kwa namna ya pekee nayapongeza pia makampuni mengine yakiwemo PSPF, NHIF, SBL, na Coca Cola kwa kuungana nasi katika kufanikisha tukio hili la kuwaleta pamoja bloggers kwa lengo la kuwanoa zaidi juu ya shughuli wanazozifanya.

  Kimsingi lazima tukubali kuwa mitandao hii imekuwa tegemeo kubwa la vyanzo vya habari na kusambaza taarifa mbalimbali tena kwa muda mfupi, hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kuwanoa wanaoiendesha ili kupunguza matumizi mabaya ya mitandao hii.

  TBN inaamini njia pekee ya kupambana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ni kuendelea kutoa elimu kwa waendeshaji na watumiaji ili mwisho wa siku wasikubali kutumika vibaya au kuitumia vibaya mitandao hii katika kutoa taarifa. Kwa dunia ya sasa hakuna atakayepinga kuwa mitandao hii imekuwa ikielimisha umma, ikikosoa jamii na kiburudisha juu ya masuala anuai ya kijamii.


  Imetolewa na; Mwenyekiti wa Muda wa TBN
  Joachim E. Mushi

  0756469470

  0 0

   Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba, Fidel Castro, nyumbani kwa Balozi wa Chuba hapa nchini, Jorge Luis Lopez Tormo (aliyesimama), Mtaa wa Alli Bin Said, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
    Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula akimpa pole  Balozi wa Chuba hapa nchini, Jorge Luis Lopez Tormo baada ya kusaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba, Fidel Castro, nyumbani kwa balozi huyo,, Mtaa wa Alli Bin Said, Oysterbay jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa zamani Adamu Malima ambaye naye alifika kusaini kitabu hicho
    Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula akimpa pole  Balozi wa Chuba hapa nchini, Jorge Luis Lopez Tormo baada ya kusaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba, Fidel Castro, nyumbani kwa balozi huyo,, Mtaa wa Alli Bin Said, Oysterbay jijini Dar es Salaam. 
   Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula akizungumza na Balozi wa Chuba hapa nchini, Jorge Luis Lopez Tormo baada ya kusaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba, Fidel Castro, nyumbani kwa balozi huyo,, Mtaa wa Alli Bin Said, Oysterbay jijini Dar es Salaam. 

  0 0

  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za Mahfali ya Skuli ya Feza Zanzibar (Private) kwa wanafunzi wa Kidato cha 4,6 na 7 mwaka 2016,iliyofanyika juzi Skulini hapo Chukwani Wilaya ya Magharibi.
  Baadhi ya waalimu waliopewa zawadi katika sherehe za Mahfali ya Skuli ya Feza Zanzibar (Private) kwa wanafunzi wa Kidato cha 4,6 na 7 mwaka 2016,iliyofanyika juzi Skulini hapo Chukwani Wilaya ya Magharibi,ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma.
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma (wa pili kulia)  akimkabidhi cheti mmoja wa wanafunzi wa Darasa la saba katika sherehe za Mahfali ya Skuli ya Feza Zanzibar (Private) kwa wanafunzi wa Kidato cha 4,6 na 7 mwaka 2016,iliyofanyika juzi Skulini hapo Chukwani Wilaya ya Magharibi,(kulia) Mwalimu Mkuu Ally Yussuf Nungu.
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma (kushoto) akimkabidhi cheti mmoja wa wanafunzi wa Kidato cha Nne katika sherehe za  Mahfali ya Skuli ya Feza Zanzibar (Private) kwa wanafunzi wa Kidato cha  4,6 na 7 mwaka 2016,iliyofanyika juzi Skulini hapo Chukwani Wilaya ya Magharibi,(katikati) Mwalimu Mkuu Ally Yussuf Nungu.


older | 1 | .... | 1449 | 1450 | (Page 1451) | 1452 | 1453 | .... | 3270 | newer