Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 143 | 144 | (Page 145) | 146 | 147 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Bi Mboni Mgaza akiwasalimia wakazi wa Kata ya Kwale, Wilayani Mkinga ambapo zaidi ya Wananchi Mia Tano (500) wamejiunga na NSSF kama wanachama wa hiari.
  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF Bw. Crescentius Magori akisoma hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Bi Mboni Mgaza na Meneja Wa NSSF mkoa wa Tanga Bw. Frank Maduga. Kulia kwake Ni Bi Eunice Chiume, Meneja Kiongozi wa Uhusiano na Uhuduma kwa Wateja.
  Mwenyekiti wa Kijiji cha Kichalikani akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Bi Mboni Mgaza hotuba ya wakazi wa Kata ya Kwale.
  Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Bi Mboni Mgaza akiwakabidhi wanachama wapya wa hiari wa NSSF katika Kata ya Kwale.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0
 • 05/24/13--14:17: adha ya foleni jijini dar

 • 0 0

  Chama cha Wabunge wanawake katika Bunge la Tanzania (TWGP) leo wamefanya semina ya siku moja kwa wabunge wote wanawake kwa lengo la kuongeza uelewa mpana katika namna bora ya uwasilishaji Miswada au hoja binafsi Bungeni.

  Akifungua semina hiyo, Mwenyekiti wa chama hicho cha Wabunge wanawake Bungeni. Mhe. Anna Abdallah amewataka wabunge wanawake wote bila kujali vyama vyao kuhakikisha wanaitumia vizuri Ofisi ya mshauri mkuu wa mambo ya sheria wa Bunge katika kuwasilisha Miswada au hoja Binafisi.

  Amesema wabunge wanawake wanawajibu wa kutatua matatizo yanayowakabili wananchi hususani wanawake nchini ikiwa ni pamoja na kuleta hoja au miswada Bungeni yenye kulenga kuifanya serikali iweze kutatua kero zinazowakabili wananchi wake.

  “Waheshimiwa wabunge, pamoja na kwamba mimi nikipindi changu cha nane hivi sasa bado kuna mwamko mdogo kwa waheshimiwa wabunge wanawake kuleta miswada au hoja binafsi bungeni. Naamini tukiitumia vizuri Ofisi hii pale tutakapokuwa tuna mawazo yetu, watatusaidia sana kutuandalia hoja binafisi au miswada kulingana na matakwa yaliyopo ya kikanuni”alisema Mhe. Anna Abdallah

  wakichangia mada zilizowasilishwa hapo, wabunge wengi wanawake wameomba kuwe na utaratibu mzuri wa kuhakikisha kuwa kila mara elimu hii inatolewa kwa lengo la kujikumbusha baadhi ya taratibu za kikanuni na hata kisheria katika uwasilishaji wa hoja binafsi na miswada binafsi Bungeni.

  “Kuna haja ya kuwa na semina katika maswala haya angalau mara moja kila wakati wa vikao vya Bunge ili kujikumbusha mambo kadhaa yanayotawala katika uwasilishwaji wa miswada binafsi au hoja Binafsi mwenyekiti kwa kuwa tuna mambo mengi tungependa kuyaleta Bungeni kupata baraka zake. Kwa kujikumbusha na mambo haya tutaiva kwelikweli katika kuwawakilisha wananchi wetu mwenyekiti”. Alichangia Mhe. Anne Kilango Malecela.

  Jumla ya mada tatu ziliwasilishwa katika Semina hiyo iliyoandaliwa na chama hicho cha wabunge wanawake Bungeni (TWGP) kwa kushirikiana na Ofisi ya msahuri wa maswala ya sheria wa Bunge ambazo zote zililenga kuwapa uelewa wabunge kuhusu namna bora na mambo ya kuzingatia wakati wa kuwasilisha miswada binafsi na hoja binafsi Bungeni kwa wabunge wanawake.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wanawake Bungeni (TWGP) . Mhe. Anna Abdallah (Mb) akifungua rasmi semina hiyo siku moja kuhusu namna bora ya uwasilishaji wa Miswada binafsi na hoja Binafisi Bungeni kwa wabunge wanawake. Kushoto ni katibu wa chama hicho Mhe. Angela kairuki na aliyekulia ni Makamu Mwenyekiti Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa.


  0 0


  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete ni miongomi mwa marais wa bara la Afrika watakaohudhuria Sherehe za kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Umoja  wa  nchi za Afrika (AU) zinazo fanyika rasmi leo Jumamosi Mei 25, 2013 katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia. 

   Shamrashamra zimetawala kila pembe ya jiji la Addis, wakati viongozi wa nchi za Afrika wakiwasili mmoja baada ya mwingine katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole. 

   Muungano wa Afrika wakati huo ukijulikana kama OAU, ulizaliwa Mnamo Mei 25, 1963 jijini Addis Ababa, ukianza na nchi za 32 na baadaye nchi 21 zikajiunga miaka ilivyozidi kwenda, huku Afrika ya kusini ikijiunga kuwa mwanachama wa 53 mwaka 1994. 

  Mwaka 2001 OAU iligeuzwa kuwa AU katika mkutano uliofanyika Lusaka, Zambia. Jumamosi hii kutakuwa na sherehe za kilele kuadhimisha miaka hiyo 50 ya AU na kuhudhuriwa na marais karibia wote wa Afrika. 

   Kauli mbiu ya sherehe za hapo kesho ni mjadala mkuu kuhusu ushirikiano wa nchi za Afrika na kuimarishwa kwa muungano huo. Mwenyekiti wa tume ya muungano huo, Dr Nkosazana Dlamini Zuma, anaseme kuwa hii itakuwa fursa kwa AU kujadili kuhusu uwezo wa bara hili na ambacho kinaweza kufikiwa katika miaka 50 ijayo
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa alipowasili Ijumaa usiku  tayari kujiunga na viongozi wenzie wa nchi za Afrika katika sherehe za miaka 50  tangu kuanzishwa kwa Umoja  wa  nchi za Afrika (AU) zinazofanyika leo katika makao makuu ya umoja huo
  Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete wakiwasili Addis Ababa
  Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipata maelezo ya maandalizi ya sherehe hizo toka kwa balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Profesa Joram Biswaro mara baada ya kuwasili Addis Ababa

  0 0
 • 05/24/13--20:00: NGOMA AZIPENDAZO ANKAL
 • Said Karoli hatosahaulika kwa ngoma yake ya 'Maria Salome'

  0 0
 • 05/24/13--21:00: Mkataa kwao mtumwa
 • Wssukuma na Nyoka wao...Mambo ya Bujora haya

  0 0


  0 0

  Warembo wa Miss Kigamboni 2013 wakipewa somo na Miss Tanzania mwaka 1999,Hoyce Temu wakati alipowatembelea kwenye kambi yao kwa lengo la kuwafunda warembo hao,Hoyce aliwaaambia warembo hao mambo mbali mbali kuhusiana na masuala ya urembo likiwemo suala la nidhamu na kujitambua katika jamiii. Shindano la miss kigamboni litafnyika juni 7 mwaka huu,huko Kigamboni jijini Dar.
  Miss Tanzania mwaka 1999,Hoyce Temu (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Warembo wa Miss Kigamboni 2013.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na Makamu Wakuu wa Vyuo Vikuu vya Jamhuri ya Watu wa China baada ya kuzungumza nao, Ofisini kwake jijini Dar es salaam May 25, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0
 • 05/25/13--03:52: taarifa ya msiba
 • Habari ndugu zangu, naomba kuwajulisha kuwa mwandishi mwenzetu wa zamani wa habari za michezo Shishee Belela amefariki dunia na anatarajiwa kuzikwa leo Jumamosi Mei 25, 2013 saa kumi alasiri Manzese, Dar es Salaam.

  Shishee alifariki dunia jana asubuhi, naamini sote tunamkumbuka hasa kwa wale ambao wana zaidi ya angalau miaka saba katika fani watakuwa wamewahi kufanya naye kazi kwa namna mbalimbali. Mara ya mwisho alikuwa akifanya kazi Uhuru na Mzalendo. 

  Kwa niaba ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini  (TASWA) naomba tuungane katika msiba huo na tumuombee Mwenyezei Mungu amuweke mahali pema peponi. Amin.

  Nawasilisha.


  Katibu TASWA

  0 0
 • 05/25/13--03:53: Article 14
 • SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD
  WAZEE WA KAZI

  GOOD NEWS FOR TANZANIA
  HUDUMA MPYA YA KIFURUSHI 
  NEW DOOR TO DOOR SERVICE
  TUNACHUKUA MZIGO MLANGONI KWAKO UK NA TUTAUFIKISHA MLANGONI KWAKO DAR
  UKILIPA HAPA UK HAULIPI TENA DAR, SISI TUTAKULETEA MZIGO NYUMBANI KWAKO!
  Baada ya kushughilikia kwa kina mapungufu yaliyojitokeza mwanzo, 
  sasa tumerudi na huduma ya kifurushi tena ikiwa imeboreshwa zaidi.
  BEI ZETU KAMA KAWAIDA HAZINA KIGUGUMIZI NA SI ZA KUUMIZA

  AIR CARGO TO DAR NOW £3.50 INCLUSIVE CLEARANCE!
  AIR CARGO TO ZANZIBAR NOW £3.00 INCLUSIVE CLEARANCE!
  AIR CARGO TO NAIROBI/MOMBASA NOW £2.80 INCLUSIVE CLEARANCE!
  KIFURUSHI KWA KONTENA DAR/ZANZIBAR NOW £2.20 INCLUSIVE CLEARANCE!

  NDEGE ZINAONDOKA KILA WIKI MARA MBILI
  MZIGO WOWOTE LETE TU
  MINIMUM WEIGHT IS 40KILOS
  KAMA UNATAKA KUAGIZA KITU AU KUFANYA BOOKINGS TUWASILIANE KWA NAMBA HAPA CHINI

  0 0

  Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia katika ufunguzi wa kongamano la pili la Maridhiano lilolofanyika hoteli ya Bwawani.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Mzee Hassan Nassor Moyo akizungumza katika kongamano la pili la Maridhiano lilolofanyika hoteli ya Bwawani.
  Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano Ismail Jussa Ladhu, akizungumza katika kongamano la pili la Maridhiano lilolofanyika hoteli ya Bwawani.
  Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Hassan Nassor Moyo (kushoto) na Mjumbe wa kamati hiyo Ismail Jussa Ladhu, wakibadilishana mawazo kabla ya ufunguzi wa kongamano la maridhiano lililofanyika hoteli ya bwawani.
  Baadhi ya washiriki wa kongamano la pili la maridhiano Zanzibar lililofanyika hoteli ya Bwawani, wakisikiliza hotuba ya Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, katika ufunguzi wa kongamano hilo. (Picha, Salmin Said, OMKR).

  0 0
 • 05/25/13--04:07: YALE YALEEEE.......
 • Lori aina ya Fuso lenye nambari za usajili T 669 CEK likiwa limeigonga pikipiki iliyokuwa inakatiza kwenye taa nyekundu mapema leo katika eneo la Majumba sita njia panda ya Segerea.Waendesha pikipiki wengi wamekuwa wakiuendeleza uzembe huu ambao umekuwa ukifumbiwa macho sana na Watu wa Usalama Barabarani.
  Huyu ndie dereva wa pikipiki hiyo akiugulia maumivu kabla ya kupatiwa msaada wa kukimbizwa hospitali.Picha na Adam Mzee.

  0 0

  Kaimu Mwenyekti vyuo vikuu, wilaya ya Dar es salaam, Assenga Abubakar (Kushoto),Katibu Msaidizi Mkoa wa vyuo vikuu,anayeshughulikia na mikoa ya Dar es salaam na Zanzibar na Kepteni mstaafu,Alhaji Mohamed Ligola wakiwa kwenye mkutano na viongozi wa matawi ya vyuo ya CCM Dar es Salaam.
  Baadhi ya viongozi wa matawi ya CCM ya vyuo vikuu mkoa wa Dar es salaam wakiwa kwenye mkutano wao ambao pamoja na kujadili masuala mbali mbali ya kisiasa na masaula ya gesi Mtwara pia walipata wasaa wa kupata Darasa la Itikadi.

  0 0
 • 05/25/13--04:14: dogo katika biashara
 • Anton Nyoni (15) akiwa amebeba vibao vya kutundikia nguo majumbani ambavyo alikuwa akiuza kati ya tsh 2000 hadi 1500 kutoka na ukumbwa kama alivyokutwa katika kituo cha mabasi cha Ikweta kandokando ya barabara ya sokoine manispaa ya Songea jana.

  0 0

  H.E. President Jakaya Mrisho Kikwete (right), President of the United Republic of Tanzania Thursday (May 23, 2013) met with Hon. Dr. Alexander Stubb, Minister for European Affairs and Foreign Trade at the State House in Dar es Salaam.  

  President Kikwete (center) in a group photo with Hon. Dr. Alexander Stubb (left) and Hon. Heidi Hautala (right), Minister for International Development, prior to the beginning of their discussion that highlighted the current mobile connection industry that has become a big demand for farmers in the country, including the alternative ways of using land such as forestry farming. 

  H.E. President Kikwete in discussion with Hon. Dr. Alexander Stubb (2nd right), Minister for European Affairs and Foreign Trade, Hon. Heidi Hautala (2nd left), Minister for International Development and H.E. Sinikka Antilla (left), Ambassador of Finland in the United Republic of Tanzania.  Minister Stubb is in the country with a business delegation from Finland to discuss and explore areas of partnership in development such as higher education, innovative agricultural programs and infrastructure building.  

  Hon. Bernard K. Membe (MP) (left), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation and Ambassador Dora Msechu, Director of the Department of Europe and Americas listening to President Kikwete discussion with delegation from Finland. 

  Finland delegation that consisted of top businessmen in talks with President Kikwete (not in the photo) at the State House in Dar es Salaam.  The businessmen discussed with President Kikwete the need to mobilize farmers through KILIMO KWANZA program by facilitating them with communication technological devices that are affordable and useful in transmitting useful agricultural information among them.  The businessmen had recently signed a joint-venture deal with Vodacom aim at providing affordable mobile phones as a way of enhancing communication among farmers in rural areas.

  Hon. Bernard K. Membe (MP) (left), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation and Ambassador Dora Msechu (2nd left), Director of the Department of Europe and Americas in the Ministry, listening to President Kikwete discussion with his guests at the State House.  President Kikwete further discussed telecommunication sector and the need to have more investors that can help build more infrastructures in rural areas to help economy grow in the country.   Others in the photo are Mr. Lumbila Fyataga (3rd left), Deputy Private Secretary to the President, Ms. Upendo Mwasha (right - back roll), Foreign Service Officer in the Ministry and Mr. Thobias Makoba, Assistant Private Secretary to Minister Membe.  
  H.E. President Kikwete (2nd left - front roll), in a group photo with Hon. Dr. Alexander Stubb (left - front roll), Minister for European Affairs and Foreign Trade, Hon. Heidi Hautala (2nd right - front roll), Minister for International Development and other top businessmen from Finland.

  All photos by Tagie Daisy Mwakawago of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu katikati akiwa na wajumbe wa kamati ya maadili ya Mahakama ya Mkoa huo mara baada ya uzinduzi wa kamati hiyo jana mjini Songea,wa tatu kushoto ni wakili mfawdhi wa Serikali kanda ya Songea Andikalo Msabila na wa pili kulia katibu tawala wa mkoa wa Ruvuma Hassan Bendeyeko na wengie pichani ni wajumbe wa kamati hiyo. PICHA NA MUHIDIN AMRI

  0 0

  Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twiga Stars), Rogasian Kaijage amewaita kambini wachezaji 30 ikiwa ni mwendelezo wa kuijenga na kuiimarisha timu hiyo.

  Twiga Stars itakuwa na kambi ya siku kumi kuanzia Jumapili (Mei 26 mwaka huu) ambapo baadaye inatarajia kucheza mechi moja ya kirafiki kabla ya wachezaji kurudi kwenye klabu zao.

  Kambi hiyo ni mwendelezo wa programu iliyopendekezwa na kocha kuijenga na kuiimarisha timu hiyo kwa vile haina mashindano mwaka huu, na itakuwa kambi ya pili baada ya ile iliyofanyika Machi mwaka huu.

  Wachezaji walioitwa na klabu zao kwenye mabano ni Asha Rashid (Mburahati Queens), Aziza Mwadini (Zanzibar), Belina Julius (Lord Barden), Ester Chabruma (Sayari), Ester Mayala (TSC Academy), Eto Mlenzi (JKT), Evelyn Sekikubo (Mburahati Queens) na Fatuma Bushiri (Mburahati Queens).

  Fatuma Hassan (Mburahati Queens), Fatuma Omari (Sayari), Flora Kayanda (Tanzanite), Hamisa Athuman (Marsh Academy), Hellen Peter (JKT), Maimuna Said (JKT), Mwajuma Abdallah (Tanzanite), Mwanahamisi Omari (Mburahati Queens), Mwanaidi Tamba (Mburahati Queens) na Mwapewa Mtumwa (Sayari).

  Nabila Ahmed (Marsh Academy), Pulkeria Charaji (Sayari), Rehema Abdul (Lord Barden), Rukia Khamis (Uzuri Queens), Semeni Abeid (Tanzanite), Sharida Boniface (Makongo Sekondari), Sophia Mwasikili (Sayari), Therese Yona (TSC Academy), Vumilia Maarifa (Evergreen) na Zena Khamis (Mburahati Queens).

  0 0

  Muono wa jicho la samaki katika Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa leo Mei 25, 2013.
  Viongoi mbali mbali wa nchi za Umoja wa Afrika (AU) wakiwakumbuka waliotangulia mbele ya haki.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa leo Mei 25, 2013. 
  Marais Wastaafu wakiwa katika Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya AU katika makao makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa leo Mei 25, 2013.PICHA NA IKULU.

older | 1 | .... | 143 | 144 | (Page 145) | 146 | 147 | .... | 3285 | newer