Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110133 articles
Browse latest View live

Magese aipongeza Serikali kwa kumpa ushirikiano, mrembo wake apata nafasi ya tano

$
0
0
MKURUGENZI wa Kampuni ya Millen Magese Group (MMG), Millen Magese  ameishukuru Serikali kupitia kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye, huku akifurahishwa na uwakilishi mzuri wa Miss Tanzania Julitha Kabete (19), aliyeingia kwenye tano bora katika mashindano ya Afrika.

Kabete  alipeperusha vema Bendera ya Tanzania kwa kuingia hatua ya tano bora ya mashindano yaliyofanyika Jumamosi nchini Nigeria na  kuitoa Tanzania kimasomaso.

Akizungumza na waandishi wa habari, Millen alisema ni faraja kubwa kwake na nchi yake kwa  Julitha kuingia hatua ya tano bora, lakini sababu kubwa ikiwa ni ushirikiano iliyoupata.

"Napenda kuchukua fursa hii kwa heshima nyingi na taadhima kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa ushirikiano wa hali ya juu, kupitia Waziri Nape Nnauye kwa ushirikiano na mwongozo wa kipekee, wazazi na familia nzima ya Julitha kwa malezi yenu kwa binti , Kamati nzima ya Miss Tanzania chini ya Mkurugenzi Hashim Lundenga (Tunashukuru sana), kwenu wanahabari hatuna maneno sahihi ya shukrani, asanteni sana," alisema Magese.

Naye mshindi huyo wa tano wa Miss Afrika, Julitha Kabete, alisema anashukuru kwa ushirikiano aliupata, lakini pia nchi yake kupata thamani ya kipekee katika shindano hilo kupata nafasi tano za juu.

Kabete alisema kuwa licha kutopata nafasi ya kwanza, lakini ameweza kuiwakilisha vema nchi katika shindano hilo, kwa sababu ushindani ulikuwa mkali sana.

"Kwangu ni faraja kubwa kwa kuwa balozi mzuri wa Tanzania na kuweza kuwashinda wenzangu wengi ikiwemo na mwenyeji wetu ambaye hakuingia katika hatua ya tano kama ambayo mimi nimeipata nina furaha kubwa sana,"alisema Kabete.


Alisema kuna mkataba mpya ambao utaingiwa kati ya Tanzania na waandaaji wa shindano hilo la Miss Africa katika kutoa ushirikiano wa ushiriki wa shindano hilo.

Katika shindano hilo lililofanyika Novemba 26, mwaka huu nchini Nigeria, taji la shindano hilo lilienda kwa mnyange Neurite Mendes (23) wa Angola, aliyenyakua kitita cha dola za Marekani 25,000 sawa na sh.milioni 52 ya Kitanzania na  gari jipya (brand new 2016 Ford Escape), safari maalum ya mafunzo nchini Uingereza na Ubalozi wa Mazingira– Afrika.

Mshindi wa pili katika shindano hilo ni Refilwe Mthimunye wa Afrika Kusini alipata dola za Kimarekani 15, 000 ni sawa na zaidi ya sh. milioni 32, na Jencey Anwifoje kutoka nchini Cameroon, akiibuka wa tatu na kupata dola za kimarekani 10,000 sawa na zaidi ya  sh.milioni 20.

Shindano la Miss Afrika 2016 lilichagizwa kwa heshima ya mji wa Calabar na jimbo la Cross River, chini ya Gavana wa Cross River Profesa Ben Ayade.

Kampuni tanzu ya Millen Magese (MMG) imeanzishwa kwalengo la kuibua, kuinua, kutambua na kukuza vipaji katika Bara la Afrika na ngazi ya Kimataifa.

MMG imeweza kufika nchi mbalimbali barani Afrika na mwaka 2012 iliweza kuendesha shindano la kwanza ya aina yake ambapo wanamitindo wawili kutoka Tanzania walipata nafasi ya kupata mikataba nchini Afrika Kusini.

Wanamitindo kutoka mashindano hayo wameweza kuendelea kufanya vizuri maonesho mbalimbali ya kitaifa na kimataifa. Mwaka huo huo wa 2012 MMG kupitia mradi wa TIFEX iliwezesha wabunifu kutoka nchini kupata uzoefu na uelewa wa wiki za mitindo duniani.

MAABARA YA KISASA YA KOMPYUTA YA SHULE YA SEKONDARI MIKOCHENI YAZINDULIWA

$
0
0
Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda ameitaka jamii kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli za kuboresha Sekta ya elimu kwa kuchangia maendeleo ya elimu ili kuleta mabadiliko ya elimu nchini.

Meya huyo Mstaafu ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Maabara ya kisasa ya kompyuta ya Shule ya Sekondari Mikocheni, Dar es Salaam kwa udhamini wa kampuni ya intaneti ya Raha Broadband kwa kushirikiana na yeye mwenyewe hivi karibuni.
Hiyo inakuwa ni miongoni mwa Maabara chache bora za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini kwa shule za Umma.
Mwenda aliutaka uongozi wa shule hiyo kuitunza maabara hiyo na kuitumia vizuri ili faida yake ionekane kwenye matokeo ya mitihani ya shule hiyo.
"Tukubaliane kuwa mtaitunza maabara hii vizuri ili umuhimu wake uonekane katika matokeo ya mitihani ya wanafunzi". Alisema Mwenda.
Aidha aliishukuru kampuni ya Raha Broadband kwa kuchangia kompyuta na vifaa pamoja na huduma ya intaneti kwa kila mwezi vyenye thamani ya shilingi milioni 18 na kuwataka viongozi wa Manispaa hiyo kuwashawishi wananchi nao kuchangia maendeleo ya elimu kwa shule za Manispaa hiyo.
Kwa upande wake Meya huyo Mstaafu alichangia shilingi milioni 3.9 ikiwa ni ukarabati wa Chumba cha maabara, madirisha, milango pamoja na meza za kompyuta.
Naye Meya mpya wa Manispaa hiyo, Benjamin Sitta alimshukuru Meya huyo Mstaafu pamoja na kampuni ya Raha kwa mchango wao na kuomba waendelee kumsaidia kwa shule nyingine za Manispaa hiyo.
Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kushoto), Meya mpya wa Manispaa hiyo, Benjamin Sitta (wa pili kulia), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Raha Broadband, Aashiq Shariff (wa pili kushoto) na Diwani wa Kata ya Mikocheni, Bethel Kimei (Mama Langa).

 Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta na Meya Mstaafu wa Manispaa hiyo, Yusuf Mwenda (kushoto) wakimtazama mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mikocheni, Jamila Msami akitumia kompyuta baada ya ufunguzi rasmi wa Maabara ya kisasa ya kompyuta ya shule hiyo kwa ufadhili wa Kampuni ya intaneti ya Raha Broadband, Dar es Salaam juzi.

 Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maabara ya kisasa ya kompyuta ya Shule ya Sekondari Mikocheni, Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya intaneti ya Raha Broadband, Aashiq Shariff na Meya mpya wa Manispaa hiyo, Benjamin Sitta.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

ULEGA AWASHUKURU WANACC MKURANGA KWA KUMCHAGUA

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akizungumza na Makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Lukanga Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani, wakati wa katika Kikao cha Halmashauri kuu ya Kata hiyo, kufuatia ziara yake ya kuwashukuru wanaCCM wa Jimbo hilo kumchagua, iliyofanyika leo.
Diwani kata ya Mkamba, Hassan Dunda akizungumza na Makada wa CCM Kata ya Lukanga Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
Katibu wa Tawi Kijiji cha Mkola, Shamte Ngelemange akichangia mada katika mkutano wa Makada wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Lukanga.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Lukanga Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI ARUSHA

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MHE. Kassim Majaliwa  anatarajiwa kutembelea Jiji la Arusha kuanzia kesho tarehe 01 hadi 03/12/2016 na kukagua miradi ya maendeleo, kuongea na watumishi wa Jiji, kukutana na wafanyabiashara pamoja na kuzungumza na wananchi. 

Kwa mujibu wa Afisa habari wa Jiji la Arusha Nteghenjwa Hosseah, kesho tarehe 01/12/2016 Waziri mkuu MHE. KASSIMU MAJALIWA atatembelea National Milling Company (NMC) na pia atakagua ujenzi wa barabara ya Friends Corner - Muriet yenye urefu wa Km 7 inayojengwa kwa kiwango cha Lami kupitia mradi wa Mpango Mji Mkakati (TSCP) na kusimamiwa na Ofisi ya Rais Tamisemi. 

Hosseah amesema siku ya tarehe 02/12/2016 Waziri Mkuu atakutana na kuzungumza na watumishi pamoja walimu katika Ukumbi wa AICC Arusha na baadae atakutana na wafanyabiashara katika Ukumbi huo.

"Katika nsiku ya tatu ya ziara yake Mhe Majaliwa  atatembelea na kukagua viwanda vya Lodhia pamoja na Hans Paul vilivyoko mtaa wa Viwanda – Njiro na baadae atakutana na wanachi wote kwenye Mkutano wa hadahara utakaofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuanzia saa nane mchana.

DK.SHEIN AKUTANA NA BALOZI WA KENYA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Balozi wa Kenya katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Chirau Ali M​w​akwere alipofika Ikulu Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Balozi wa Kenya katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Chirau Ali M​w​akwere alipofika Ikulu Mjini Unguja leo. Picha na Ikulu, Zanzibar.

Wakazi wa Tabata, Arusha walamba Milioni 46/- za m-Bet

$
0
0
Emmanuel Cornel Matema mwenye umri wa miaka 38 wa Tabata, jijini Dar es Salaam na Mkazi wa Tabora, Ramon Hamisi Mane (22) wamefanikiwa kujishindia kila mmoja kiasi cha Sh milioni 23 baada ya kubashiri vyema matokeo ya mechi mbalimbali za ligi za Ulaya kupitia Kampuni ya m-Bet.
Washindi wote hao, wamekabidhiwa vitita vyao katika hafla fupi iliyofanyika ofisi za m-Bet, jijini Dar es Salaam leo Jumatano Novemba 30, 2016 chini ya usimamizi wa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abbas Tarimba. 
Akizungumza katika hafla hiyo, Tarimba aliwapongeza washindi hao na kuwataka kuhakikisha wanazitumia vema fedha hizo ili ziweze kusawasaidia katika kuboresha maisha yao. 
“Nichukue fursa hii kuwapongeza m-Bet kwa kuendesha bahati nasibu hii ambayo imeonekana kuwanufaisha Watanzania wengi waliojishindia mamilioni ya shilingi hadi sasa. Lakini pia nitoe rai kwa washindi kuhakikisha wanazitumia ipasavypo fedha wanazoshinda ili ziweze kuboresha maisha yao na si vinginevyo, ukizingatia kwa sasa maisha ni magumu sana,” alisema Tarimba.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa m-Bet, Dhiresh Kabba, alisema kuwa wawili hao walifanikiwa kuzoa kitita hicho baada ya kufanikiwa kutabiri matokeo ya mechi 15 za ligi za Ulaya.
“Tunafarijika kuwakabidhi Matema na Mane kitita chao kiasi cha Sh milioni 23 ambapo watagawana sawa sawa,” alisema Kabba.
Aliwataka watanzania kuchangamkia kutumia mtandao wa intaneti kuonyesha ushabiki halisi wa soka akisema kuwa Perfect 12 ni mchezo wa ziada unaoruhusu kutabiri mechi 12 kwa Tsh 1,000 tu ambapo ukipatia zote  unaondoka na kitita chako mchana kweupe. 
Akielezea furaha yake kwa kushinda fedha hizo, Matema ambaye ni mjasiriamjali, alisema: “Nawashukuru sana m-Bet kwa kuniwezesha kushinda fedha hizi ambazo nitazitumia kuongeza mtaji wa biashara zangu na mahitaji binafsi.” 
Naye Mane ambaye ni mwanafunzi na mjasiriamali, alisema: “Fedha hizi zitanisaidia sana katika biashara zangu, lakini zaidi ikiwa ni masomo kwani nimekuwa katika wakati mgumu linapokuja suala la ada na mahitaji mengineyo ya shule. Ahsante sana m-Bet.” 
Kuhusu m-Bet, ni Kampuni iliyosajiliwa chini ya Sheria za Tanzania na kupewa leseni na Bodi ya Michezo ya kubahatisha tanzania kwa lengo la kufanya upatikanaji rahisi na mwingiliano wa huduma ya mchezo wa kubahatisha (Sim Betting) nchi nzima.
“Kushiriki, ingia www.m-bet.co.tz, chagua kucheza kawaida au Perfect 12 ambapo kwa Shilingi 1000, unachagua matokeo 12. Ukipata yote sawa, unanyakua kikapu cha m-Bet,” alisema Kaba
 Washindi wa M-bet,Emmanuel  Katema (kushoto) na Ramon  Mane wakifurahia zawadi yao  wakati walipokabikdhiwa hundi ya mfano ya Sh.Milioni Arobaini na sita (46,000,000) baada ya kuibuka washindi wa Perfect 12. Makabidhiano hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam leo Novemba 30, 2016

 Kaimu Mkurugenzi wa  Uendedshaji na Sheria wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, James Mbalwe akiwakabidhi hundi ya mfano wa Sh. Milioni Arobani na sita (46,000,000/=) , wa washindi  wa M-bet, Ramon  Mane (kulia) na  Emmanuel  Katema (wa pili kulia), ambao waliibuka  washindi  wa Perfect 12. Makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam leo Novemba 30 yalihudhuriwa na Mkurugenzi wa M-bet, Dhiresh Kaba ( wa pili kushoto).

Mkurugenzi wa M-bet, Dhiresh Kaba (katikati) akiungana na washikndi wa M-bet, Emmanuel  Katema (kushoto) na Ramon  Mane, kushangilia mara baada ya makabidhiano ya mfano wa hundi wa Sh. Milioni Arobaini na Sita kwa wahindi hao walioibuka kidedea wa  Perfect 12.

MADIWANI HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA WAINGIA MTAANI KUKUSANYA MAPATO

$
0
0
Meya wa jiji la Mbeya David Mwasilindi


 Na Jamii Moja blog,Mbeya
Halmashauri ya jiji la Mbeya imebuni njia mpya ya ukusanyaji wa mapato  ili kufikia malengo yake ya ukusanyaji wa kiasi cha shilingi bilioni  11 katika  mwaka wa fedha wa  2016/17 .


Katika kufanikisha mpango huo halmashauri imewashirikisha madiwani na wataalmu wake katika kufanya kazi ya ukusanyaji wa mapato kupitia vyanzo vyake vya ndani .


Moja ya njia hiyo halmshauri imeanza kuwatumia Madiwani pamoja na wenyeviti wa mitaa katika ukusanyaji wa fedha kupitia vyanzo vyake vya ndani vya mapato .


Akielezea mkakati huo  Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Ndugu David Mwashilindi amesema katika kuhakikisha halmshauri inafikia lengo lake la ukusanyaji wa mapato imeamua kuongeza nguvu kazi kwa kuwaingiza madiwani na wenyeviti ambao wapo karibu na wananchi.


Kazi kubwa  wanayo ifanya madiwani na wenyeviti kwa kushirikiana na wataalam ni kuhakikisha wanavitambua vyanzo vyote vya mapato vinavyostahili kuingia katika mapato ya halmashauri  ikiwa na kubaini mianya iliyokuwa ikitumiwa na wahusika kukwepa kulipa kodi,”amesema Mwasilindi.


Amesema kuziendesha halimamshauri hizi inategemea sana mapato ya ndani hivyo lazima kuweka jitahada za makusudi katika kufikia malengo husika .


Amesema katika kipindi cha nyuma halmasahuri hiyo hali ilikuwa katika hali mbaya kwani kwa mwezi walikuwa wanakusanya kiasi cha shilingi milioni 120 hadi 200 lakini mara baada ya kuanza kwa jitihada hizo imesaidia kupandisha mapato ambapo kwa sasa imefikia kiasi cha shilingi milioni 700 kwa mwezi.


Amesema zoezi hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa ambapo sanjali na kukusanya mapato pia kuna sauala la utoaji wa elimu kwa wananchi ili kuelewa namna ya kulipa  tozo zilizo wekwa kisheria.


Amesema zoezi hilo litadumu kwa muda wa siku tano na mara baada ya hapo kutafanyika kwa tahimini ya pamoja ili kubaini changamoto zilizopo katika zoezi.

INTRODUCING


TPDC YAKANUSHA TAARIFA ZINAZOENEZWA KWENYE MITANDAO NA VYOMBO VYA HABARI KUWA IMESHINDWA KUKIUZIA KIWANDA CHA DANGOTE GESI ASILIA KWA BEI NAFUU

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini(TPDC) Mhandisi Kapulya Musomba akizungumza na waandishi wa habari kukanushaTaarifa zinazoenezwa na kampuni ya Dangote pamoja na washirika wake kupitia mitandao ya Kijamii na vyombo vya Habari kuhusu kushindwa kukiuzia gesi asilia kwa bei rahisi kiwanda hicho.Kulia kwake ni Kaimu Kamishana wa Madini Mhandisi John Shija,Kaimu Meneja manunuzi TPDC Bw.Donal Aponde na Meneja Mawasiliano wa TPDC Bi.Maria Msellemu.

NHC YAKUSANYA ZAIDI YA BILIONI 5 KWA WADAIWA WAKE

$
0
0
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mikoa na Utawala Bw. Raymond Mndolwa akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC Upanga wakati alipoelezea madeni yaliyolipwa na wadaiwa sugu na ambayo yanaendelea kulipwa , Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawaliano NHC Bi Susan Omari.
.......................................................................................

Shirika la Nyumba la Taifa lilitoa taarifa ya madeni ya idara na taasisi mbalimbali za serikali pamoja na watu binafsi mwezi Septemba 2016. Deni lililokuwa linadaiwa ni kama ifuatavyo: 
Serikali Shs 9, 346, 682, 763.63  Watu binafsi Shs 2,569,446,334.64 na dola za kimarekani 380, 933.62 

Baada ya agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Shirika lilitoa notisi kwa taasisi zote za serikali na watu binafsi kulipa malimbikizo yao ndani ya siku saba (7) ambazo Mhe. Rais aliagiza.

Jumla ya shilingi 5,981,320,179.15 zimelipwa na taasisi mbalimbali za serikali zilizokuwa zinadaiwa na deni lililobaki la shilingi 3,365,362,584.48 limeendelea kufuatiliwa na tu tunaamini idara na taasisi husika zitamaliza deni lake ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba 2016. Ni vizuri pia ikaeleweka kuwa ni sehemu kidogo ya idara na taasisi za serikali ambazo zimepanga katika majengo yetu.

Tunatoa shukrani za dhati kwa Mhe. Rais kwani kwa mara ya kwanza serikali na taasisi zake zilizokuwa zinadaiwa ziliweza kutekeleza agizo hilo kwa kiwango kikubwa sana. Tunampongeza sana Mhe. Rais kwa msukumo wa kuliunga mkono Shirika la Nyumba la Taifa katika jitihada zake za kuboresha makazi ya Watanzania.

Ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais za kuhamishia ya nchi mkoani Dodoma, Shirika limeelekeza fedha zote zilizokusanywa kwenye madeni kuanza ujenzi wa nyumba 300 za makazi kwenye eneo la Iyumbu pembeni mwa Jengo la Utawala la Chuo Kikuu cha Dodoma na ujenzi huo umekwishaanza.

Pamoja na watu binafsi kulipa, wapo ambao wameendelea kulimbikiza madeni. Tunawataarifu wapangaji binafsi wa makazi na biashara kwamba zoezi kabambe la kuwaondoa wote wanaodaiwa limekwishaanza na yoyote mwenye deni yafuatayo yatatekelezwa: 
Kuwaondoa kwenye majengo ya Shirika na kuuza samani zao kufidia deni linalodaiwa; 
Kuwatoa kwenye vyombo vya habari ikiwemo magazeti; na 
Kuwapeleka mahakamani ili ikibidi njia nyingine za kisheria zitumike kilipa deni la Shirika. 

Tunapende kuwahimiza wapangaji wetu watimize wajibu wao ili kuepuka usumbufu hasa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MWASILIANO NA HUDUMA KWA JAMII

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA

BALOZI WA KUWAIT NCHINI MHE. JASEM AL NAJEM ATEMBELEA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE

$
0
0

Na Anna Nkinda - JKCI

Serikali ya Kuwait imeahidi kuisaidia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) vifaa vitakavyotumika katika utunzaji na utoaji wa damu , mashine  na vifaa vya upasuaji ambavyo vitatumika katika chumba cha upasuaji.

Ahadi hiyo imetolewa leo na  Balozi wa nchi hiyo Mhe. Jasem Al Najem alipotembelea  Taasisi hiyo kwa ajili ya kuangalia ni  jinsi gani nchi yake inaweza kuisaidia katika upatikanaji wa vifaa  tiba.

Mhe. Balozi Al Najem alisema vifaa vitakavyotumika katika utunzaji na utoaji wa damu vitapatikana kabla ya kumalizika  kwa mwaka huu ambapo vifaa  pamoja na mashine za upasuaji vitapatikana mwanzoni mwa mwaka ujao wa 2017.

“Serikali ya nchi yangu inaangalia namna ya kushirikiana zaidi na Taasisi hii pamoja na Taasisi zingine zilizopo Dar es Salaam, Zanzibar na maeneo mengine hapa nchini ili watanzania waweze kupata huduma bora”, alisema Mhe. Balozi Al Najem.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi  alishukuru Serikali ya Kuwait kwa kuahidi kuwapatia vifaa pamoja na mashine  zitakazotumika katika matibabu ya wagonjwa wa moyo.

“Tuna vyumba vitatu vya upasuaji, vinavyotumika ni viwili kwani kimoja hakina vifaa, kupatikana kwa vifaa pamoja na mashine kutoka nchini Kuwait kutatufanya tuwe na vyumba vya upasuaji vitatu ambavyo vitasaidia  kutoa huduma ya upasuaji kwa wagonjwa .

Akiwa katika Taasisi hiyo Mhe. Balozi Al Najem alitembelea vyumba vya upasuaji wa moyo, chumba cha wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU) na kutoa  zawadi kwa watoto waliolazwa.
Daktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akimuelezea takwimu za upasuaji wa wagonjwa wa Moyo zinazofanywa na Taasisi hiyo Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem (kushoto). Wapili kulia ni Dkt. Barjces Almutairi kutoka Mfuko wa Kusaidia wagonjwa wa nchini Kuwait akifuatiwa na Daktari Bingwa wa Moyo Tulizo Shemu Sanga.
Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akimpa zawadi ya gari na ndege ya kuchezea Mtoto Jumanne Mndeme ambaye amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo huku Mama yake Jumanne akishuhudia.
Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akiongea jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati balozi huyo alipotembelea Taasisi hiyo na kuahidi kuisaidia vifaa vya kutunzia damu na kununua vifaa kwa ajili ya upasuaji wa moyo katika chumba cha upasuaji. Kulia ni Daktari Bingwa wa Moyo Peter Kisenge.

MALINZI AOMBOLEZA VIFO VYA WACHEZAJI CHAPECOENSE

$
0
0
 Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Shirikisho la Mpira Brazil (CBF), kutokana na vifo vya wachezaji wa timu ya soka Chapecoense Real ya Brazil.

Rais wa TFF Malinzi, katika salamu za rambirambi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Brazil (CBF), Lucca Victorelli  amesema ajali hiyo iliyoua watu wengi ni tukio la kusikitisha kwenye familia ya soka duniani na limetokea katika kipindi kigumu.

Rais Malinzi ambaye alituma salamu hizo pia kwa mashabiki wa Chapecoense na Jumuiya ya soka na wanafamilia wengine wa nchini Brazil, amesema: “Mawazo yetu yapo kwa wahanga wa ajali hiyo, familia na jamaa zao.”

Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri juzi Jumatatu kutoka Brazil kupitia Bolivia kwenda Colombia ilibeba abiria 81 wakiwamo wafanyakazi na wachezaji wa Chapecoense Real ya Brazil kabla ya kuanguka kwenye milima ya Colombia.
Wachezaji hao wa Chapecoense Real ya Brazil walikuwa wakisafiri kwenda kucheza mechi ya fainali ya michuano ya ubingwa wa Kombe la Amerika ya Kusini (Copa Sud Americana). Walikuwa ni miongoni mwa abiria 81.

Michuano hiyo ni ya pili kwa ukubwa katika Bara la Amerika ya Kusini, iliyotarajiwa kuchezwa leo Jumatano Novemba 30, 2016 ambako Chapecoense Real ingecheza dhidi ya Atletico Nacional ya Colombia.

Ndege hiyo ilikuwa imebeba wachezaji wa timu ya Chapecoense Real ya Brazil, awali ilitoa taarifa ya hali ya hatari iliyosababishwa na hitilafu kwenye mfumo wa umeme, na hatimaye kuanguka muda mfupi baadaye karibu na mji wa Medelin.

Taarifa za vifo hivyo, zimethibitishwa na Mkuu wa Mamlaka ya Anga ya Brazil, Alfredo Bocanegra aliyesema walionusurika ni Watu watano wakiwamo wachezaji watatu wa Chapecoense na wafanyakazi wawili wa ndege hiyo.

Wachezaji walionusurika wanatajwa kuwa ni Alan Ruschel, golikipa Danilo na Jackson Follmann na kwamba walipatiwa huduma ya kwanza katika hospitali iliyoko katika mji wa Le Ceja nchini Colombia.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA SINGIDA AFARIKI DUNIA, MWILI KUAGWA LEO SAA 11 JIONI MUHIMBILI

$
0
0
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) EX Peter Kakamba amefariki dunia alfajiri ya tarehe 30/11/2016 katika hospital ya taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kakamba alizaliwa mwaka 1963 katika kijiji cha Kawajense Wilayani Mpanda, mkoa wa Katavi. Alisoma shule ya msingi Shanwe Kawajense  mwaka 1973 hadi 1980, Kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya Sekondari Kantalamba mwaka 1981 hadi 1984 ambapo kidato cha tano na sita alisoma katika shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro mwaka 1985 hadi 1987. Mwaka 1992 hadi 1994 alisoma Astashahada ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Marehemu alijiunga na Jeshi la Polisi mwaka 1988 ambapo katika utumishi wake alipandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Konstable wa Polisi (1989), Sagenti wa Polisi (1991), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1997), Mkaguzi wa Polisi (2003), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (2006), Mrakibu wa Polisi (2008), Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (2011), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2015) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (2016).
Baadhi ya nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa  Mwendesha Mashtaka wa Polisi katika mkoa wa Iringa, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi, Afisa mnadhimu wa Polisi katika Mikoa ya Iringa na Geita, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa na mpaka anafariki alikuwa Kamanda wa Polisi katika mkoa wa Singida.
Kufuatia kifo hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu anatoa pole kwa Maofisa, Wakaguzi,Askari, ndugu, jamaa na marafiki kwa Msiba huo.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, 
Jina la Bwana lihimidiwe - Amen.

Imetolewa na:
Advera John Bulimba - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.         

UPDATES: Mnajulishwa kuwa mwili wa Marehemu Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) EX Peter Kakamba, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, aliyefariki dunia Alfajiri ya Tarehe 30/11/2016 utaagwa leo tarehe 30/11/2016 Saa 11: 00 (Kumi na moja kamili Jioni) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam na baadaye utasafirishwa kwenda Mpanda  Mkoani Katavi kwa ajili ya Mazishi.


Benki ya CRDB kufungua matawi mapya 11 hadi kufikia mwisho wa mwaka huu wa 2016

$
0
0
Benki ya CRDB imesema imeshangazwa na habari zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa iko mbioni kufunga baadhi ya matawi yake kutokana na ukata. 
Akizungumza na waandishi habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Dkt.  Charles Kimei alisema kuwa hakuna ukweli wowote kwenye taarifa hizo, kwani hivi sasa Benki ya CRDB ipo kwenye hatua za mwisho za  kufungua matawi mapya 11. Hii ikiwa ni muendelezo wa sera yake ya kuhakikisha kuwa inafikisha huduma karibu zaidi na wateja.
“Nimeshangazwa  sana habari hizi za upotoshaji, ukweli ni kuwa mwaka jana (2015) tulifungua matawi 76 na kuajiri wafanyakazi 450. Mwaka huu (2016) tumeshafungua matawi 51 na tupo katika hatua za mwisho za kukamilisha matawi mengine 11.  Hii itafikisha jumla ya matawi mapya 62 na jumla ya  ajira mpya 600 kwa mwaka huu tu. Takwimu hizi zinaonyosha kuwa Benki ya CRDB inaendelea kuimarika na kuwa Benki kubwa zaidi nchini na katika ukanda huu wa Afrika Mashariki”.
Dkt. Kimei aliyataja matawi hayo mapya kuwa ni Muheza na Handeni (Tanga), LAPF (Dodoma), Ruangwa (Lindi), Soko la Mwanjelwa (Mbeya), Chato (Geita), Tarakea (Kilimanjaro), Mkwawa (Iringa), Mikumi (Morogoro), Wete (Pemba) na Kigamboni-Dar es Salaam.

“Naomba kuwatoa hofu wateja wetu juu ya taarifa zozote zenye lengo la kutuchafua kwani Benki  ya CRDB iko vizuri na inategemea matokeo makubwa ya kifedha ifikapo mwishoni mwa mwaka 2016” alisema Dokta Kimei.

KAMISHNA WA TRA AHITIMISHA MAFUNZO YA ‘SCANNER’ MPYA BANDARINI

$
0
0

Kamishna wa Mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya usimamizi na uendeshaji wa mashine za ukaguzi wa mizigo ‘scanner’ kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na TRA. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA, Bw. Abdulrahman Mbamba pamoja na Wakufunzi kutoka Kampuni iliyofunga mashine hizo.


Kamishna wa Mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya akikabidhi vyeti kwa wahitimu mbalimbali kutoka TPA na TRA.



Kamishna wa Mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu na Wakufunzi.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Waziri Mahiga asaini kitabu cha maombolezo ya Rais Mstaafu wa Cuba Fidel Castro

$
0
0
Mhe. Waziri Balozi Dkt. Augustine Mahiga akitoa heshima mbele ya picha ya Rais wa zamani wa Cuba hayati Fidel Castro alipoenda kusaini kitabu cha maombolezo 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisaini kitabu cha maombolezo .
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi wa Cuba nchini Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo alipowasili nyumbani kwa Balozi huyo mapema leo kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais Msataafu wa Cuba Fidel Castrol, Jijini Dar es Salaam 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimfariji Balozi wa Cuba nchini Mhe. Jorge Luis Lopez nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam kabla ya kusaini kitabu cha maombolezo 

JAJI MKUSA AAPISHWA LEO

$
0
0
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akimuapisha Mhe,Jaji Mkusa Issac Sepetu kuwa kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akimkabidhi hati ya kiapo Mhe,Jaji Mkusa Issac Sepetu baada ya kumuapisha kuwa kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja.
ais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akipena mikono na Mhe, Jaji Mkusa Issac Sepetu baada ya kumkabidhi hati ya kiapo  alipomuapisha kuwa kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja.
 Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,Balozi Seif Ali Iddi (kulia) akimpongeza Mhe, Jaji Mkusa Issac Sepetu kwa kuteuliwa kwake kuwa kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar katika hafla ya kiapo iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali. 
 Viongozi waliohudhuria  katika hafla ya kuapishwa Mhe,Jaji Mkusa Issac Sepetu kuwa kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar (kutoka kushoto) Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe,Haroun Ali Suleiman na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja. (Picha na Ikulu)

VODACOM TANZANIA YAKABIDHI SIMU FEKI ZAIDI YA 500 ZILIZOKUSANYWA KUTOKA KWA WATEJA WAKE KWA AJILI YA KUTEKETEZWA

$
0
0
  Mkuu wa Bidhaa wa Vodacom Tanzania, Samson Mwongela (kushoto) akisaidiwa na Meneja Uhusiano kampuni hiyo, Matina Nkurlu (katikati), kuonyesha simu feki zilizokusanywa kutoka kwa wateja wao kwa ajili ya kuteketeza kama ilivyoagizwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), wakati  wa mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Gideon Chilambo ambaye ni  Mkurugenzi wa  kampuni ya Chilambo General Trade Company inayoteketeza bidhaa feki.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (katikati) akionyesha simu halisi aina ya Smart Prime 7 yenye ubora na kiwango inayouzwa kwa Tsh 250,000/-, wakati akizungumza  na  waandishi wa habari juu ya simu feki zilizokusanywa na kampuni yake kutoka kwa wateja kwa ajili ya kuteketezwa kama ilivyoagizwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Bidhaa wa kampuni hiyo, Samson Mwongela na kulia ni Gideon Chilambo ambaye ni  Mkurugenzi wa  kampuni ya Chilambo General Trade Company inayoteketeza bidhaa feki.

TBL yazindua muonekano mpya wa Chibuku Super

$
0
0
Mwanza Desemba 1,2016:Kampuni ya TBL Group, leo imezindua Chibuku Super kwenye chupa ya bia ya ml 500, huku ikitoa wito kwa watanzania kutumia vinywaji vinavyozalishwa hapa nchini ili kujenga uchumi wa taifa kwa ujumla.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa kiwanda kilichopo eneo la Pasiansi Mwanza , Meneja Masoko wa TBL Group, Bw. Oscar Shelukindo alisema uzinduzi wa bia hiyo ya Chibuku Super” kwenye chupa ya glasi inayorudishwa (Returnable) unatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika soko la Bia hapa nchini.

“Leo ni siku ya furaha kubwa sana kwetu TBL na kwa watumiaji wote wa Bia yetu hi ya asili , kwani tumeweza kuzindua Bia hii imetengenezwa kwa utaalamu wa hali ya juu na kwa kutumia mitambo ya kisasa kabisa, hivyo kuwahakikishia wanywaji Ubora wa hali ya juu, ina ujazo wa nusu lita na itauzwa kwa bei ya shilingi 700/- tu, kwa chupa na 14,000 kwa kreti,’’ alisema.

Akiizungumzia bia hiyo Shelukindo alisema inatengenezwa kwa kutumia malighafi za hapa nyumbani, ikiwemo nafaka ya mahindi na mtama bora toka kwenye ardhi ya Tanzania na hivyo kutoa kila sababu kwa watanzania kujivunia kinywaji chenye asili ya taifa lao.

“Chibuku Super ina kilevi cha asilimia 4, kinachomfanya mtumiaji aweze kuitumia kwa muda mrefu akiwa na marafiki, lakini pia inampa lishe nzuri kutokana na virutubisho vinavyopatikana katika nafaka zinazotumika kutengeneza bia hii,’’ aliongeza

 Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya TBL wakionyesha kwa waandishi wa habari chupa mpya ya Chibuku Super ya Ml 500 wakati wa hfla fupi ya uzinduzi  iliyofanyika jijini Mwanza leo.
 Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya TBL wakionja Chibuku super ya Ml 500 wakati wa hfla fupi ya uzinduzi  iliyofanyika jijini Mwanza leo.
Meneja Masoko wa TBL Group Oscar Shelukindo,akizungumza na waandisi wa kuhusiana na  muonekano mpya wa chupa ya Chibuku Super ya Ml 500 wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Mwanza leo. kulia ni Meneja Kiwanda  cha Chibuku Super Mwanza Herbert Ilembo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA 

AZAM FC KUSAKA VIJANA U-17 KIGOMA J’MOSI HII

Viewing all 110133 articles
Browse latest View live




Latest Images