Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1435 | 1436 | (Page 1437) | 1438 | 1439 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameanza ziara yake ya siku 10 ndani ya jiji la Dar es salaam kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzitafutia ufumbuzi.
  Ziara hiyo imeanzia katika wilaya ya Kigamboni ambapo kabla ya kwenda kusikiliza kero za wananchi mtaani, Mkuu huyo alizungumza na viongozi wa wilaya hiyo pamoja na kuzindua mpango mkakati wa mkuu wa wilaya ya Kigamboni
  Akiongea na viongozi hao wa wilaya ya Kigamboni, Makonda amesema anafanya ziara hiyo ili kugundua kero za wananachi pamoja kuwahamasisha wafanyakazi wa serikali kuwajibika."Nataka wafanyakazi wafanyekazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya Rais wetu, nimegundua asilimia 80 ya wafanyakazi wa serikali hawafanyi kazi, asilimia 80 ya watumishi umma hawafanyi kazi, ni wapiga majungu, wasoma magazeti, niwambea. Kilichobaki ni kusubiri mwisho wa mwezi kwa ajili ya mshahara," alisema Mkonda.
  Pia Makonda alisema hataki kuona wananchi wanakimbilia kwa mkuu wa mkoa kuomba msaada wa utatuzi wa changamoto zao wakati serikali inawafanya kazi kuanzia ngazi ya vitongoji.Aidha mkuu huyo alitembelea pia mtaa wa Maweni, Mjimwema ambapo alishuhuda uharibifu mkubwa wa mazingira na kumtaka mkuu wa wilaya hiyo pamoja na vyombo vya ulinzi kuwashghulikia wote watakaoendelea kuchimba kokoto eneo hilo.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizindua mpango kazi wa manispaa ya Kigamboni leo jijini Dar es Salaam.   Katika ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Hashim Mgandilwa na kulia ni Mkurungenzi wa manispaa ya Kigamboni,Stepheni Katembe.
   Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa  akizungumza machache katika   uzindunzi wa mpango kazi wa manispaa ya Kigamboni leo jijini Dar es Salaam.
  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda na Kamisha wa Polisi Simon Sirro, wakimuangalia mmoja wa vijana wa kituo cha kuwasaidia vijana waliothirika na dawa za kulevya cha PEDEREF Sober,Kigamboni  ambaye alikuwa akitia ushahidi wa jinsi alivyoathiriwa na dawa hizo kwa kubeba dawa tumboni, wakati wa ziara ya mkuu huyo wa mkoa, wilayani humo,leo.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akikagua uharibifu wa mazingira machimbo ya kokoto Mjimwema jijini Dar  es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Hashim Mgandilwa.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akikagua machimbo ya kokoto yalipo Mjimwema jijini Dar  es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza na vijana wa Sober House  iliyopo  Vijibweni leo jijini Dar es Salaam.
   amanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro  akiwa katika picha ya pamoja na vijana kutoka asasi mbalimbali zisizo za kiserikali zinazo jitolea  kusikiliza  changamoto na kero za wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam.


  0 0  0 0
 • 11/19/16--13:29: BAMIZA CHARTS THIS WEEK


 • 0 0

   Mdau wa Globu ya Jamii Dkt. Ramadhani Marijani akipongezwa na mama yake mzazi baada ya kudaka nondozzz  ya  uzamivu ya utawala wa umma  (PhD in Public Admnistration) Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Wikiendi hii. 
   Mdau wa Globu ya Jamii Dkt. Ramadhani Marijani akivishwa shada la maua kwa kudaka nondozzz
  Mdau wa Globu ya Jamii Dkt. Ramadhani Marijani akipozi na familia yake baada ya kudaka nondozzzz UDSM

  0 0
  0 0


  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amewataka wananchi waliowekewa alama za kubomoa nyumba zao zilizopo pembezoni mwa barabara ya Njombe-Makete hadi Mbeya KM 205 waanze kuhama kwenye nyumba hizo ili kupisha zoezi la ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.

  Akizungumza mara baada ya kukagua barabara hiyo Eng. Ngonyani amesema awamu ya kwanza ya ujenzi wake itaanza wakati wowote kuanzia sasa mara baada ya kupatikana mkandarasi na mkandarasi mshauri ambayo itahusisha sehemu ya Njombe hadi Makete KM 109.4.

  “Kuweni waadilifu waliowekewa alama za kijani kwenye nyumba zao watalipwa fidia lakini wenye alama nyekundu hawatalipwa hivyo ni vizuri wote kutafuta maeneo mengine ya makazi ili kuepuka usumbufu mara zoezi la ujenzi litakapoanza”. Amesema Eng. Ngonyani.

  Eng. Ngonyani amesema kwa kuwa kazi ya ujenzi na ulipaji fidia zinagharamiwa na Serikali ni vema zoezi la ujenzi wa barabara likaanza wakati Serikali ikitafuta fedha kwa ajili ya fidia.“Ili tuweze kufanikiwa katika mambo yote tumeona tuanze na zoezi lenye gharama kubwa ambalo ni ujenzi wa barabara kisha zoezi la fidia litaendelea wakati ujenzi wa barabara unaendelea”. amesisitiza Eng. Ngonyani.

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi ameishukuru Serikali kwa jitihada za ujenzi wa daraja la Ruhuhu linalounganisha Mkoa wa Njombe na Ruvuma na ameiomba Serikali kuangalia namna ya kuweka lami barabara inayokwenda kwenye hospitali ya Mkoa wa Njombe na ile inayoenda hospitali ya misheni ya Ikonda wilayani Makete ili kuwezesha barabara hizo kupitika kwa urahisi wakati wote wa mwaka.

  Katika hatua nyingine Mbunge wa Makete Profesa, Norman Sigara amemuomba Naibu Waziri Eng. Ngonyani kuhakikisha Mkandarasi anayejenga barabara ya Njombe –Makete na Makete –Mbeya kupitia Kitulo anaanza kazi iyo kwa wakati ili kuongeza kasi ya wananchi kubomoa nyumba zao katika maeneo ya hifadhi ya barabara na hivyo kuunganisha kirahisi mkoa wa Njombe na Mbeya kwa barabara ya lami.

  Naibu Waziri Ngonyani yupo katika ziara ya kukagua Miundombinu ya Barabara, Bandari na Mawasiliano katika mikoa ya Nyanda za juu Kusini ambapo tayari amekamilisha ziara yake katika Mikoa ya Pwani, Lindi na Ruvuma.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akifafanua jambo kwa wananchi wa kijiji cha Mang’oto Wilayani Makete ambapo aliwataka walioko kwenye hifadhi ya barabara wabomoe nyumba zao na kutafuta nyumba mbadala ili kuwezesha zoezi la ujenzi wa barabara kuanza na zoezi la fidia lifuate baadaye.
  Mbunge wa Makete Profesa, Norman Sigala akifafanua jambo kwa wananchi wa Jimbo hilo kuhusu umuhimu wa kutafuta nyumba mbadala ili kupisha ujenzi wa barabara ya Njombe –Makete KM 109 utakaoanza hivi karibuni.
  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi (kulia), akimshukuru Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani kufuatia hatua ya ujenzi wa daraja la Ruhuhu linalounganisha mkoa wa Njombe na Ruvuma.
  Wanananchi wa kijiji cha Mang’oto Wilayani Makete wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Hayupo pichani).


  0 0

  Waziri wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith Kombo, akizungumza kwenye Uzinduzi wa Tamasha la Uoneshaji wa Filamu kwa njia ya Sinema mkoani Geita, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Nape Nhauye.

  Uzinduzi huo ulifanyika jana katika Ukumbi wa Desire Park Geita ambapo Taasisi ya Sanaa Na Mazingira ya Kijani Consult Tanzania imeanzisha kampeni ya kuonesha bure Filamu mbalimbali kwa ajili ya kufikisha elimu kwa umma ikiwemo elimu ya Utunzaji wa Mazingira (Mabadiliko ya Tabianchi), Ufugaji wa kuku wa kienyeji, Usalama barabarani, Madawa ya kulevya, Madhara ya ndoa za utotoni miongoni mwa mambo mengi ya kijamii. Mradi huo umefadhiriwa na ZIFF.

  Kutokana na Mwitikio wa wanatasnia ya Filamu mkoani Geita kuonesha shauku ya kuwa na Maonesho hayo ya Filamu, Mhe.Kombo alisema mwakani Tamasha la Kimataifa Zanzibar pia litafanyika mkoani Geita ikiwa ni sehemu ya ZIFF ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa ZIFF.
  Na BMG
  Mhe.Kombo alisema mwakani Tamasha la Kimataifa Zanzibar pia litafanyika mkoani Geita ikiwa ni sehemu ya ZIFF ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa ZIFF.
  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fessoo, akizungumza kwa niaba ya Serikali kwenye uzinduzi huo ambapo aliwahakikishia Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita na nchini kwa ujumla kwamba Serikali itahakikisha inaboresha zaidi sanaa ya filamu ikiwemo kuendelea kutoa mafunzo ya filamu kwa wanatasnia hiyo ili filamu zinazozalishwa ziwe na ubora.

  Aidha alidokeza kwamba Serikali inatoa baraka zote kuhusiana na Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar, pia kufanyika mkoani Geita hapo mwakani.
  Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga, akizungumza kwenye Uzinduzi wa Uoneshaji wa Filamu mkoani Geita, ambapo alisisitiza kwamba sanaa ni ajira hivyo wanatasnia hiyo watumie fursa mbalimbali ikiwemo mafunzo yanayotolewa na serikali ili kuboresha zaidi kazi zao.


  0 0

   Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja akiongoza Wachezaji wa timu ya Taifa ya mchezo wa kabadi walipowasili jijini Dar es salaam wakitokea nchini India kwenye mashindano ya mchezo huo uliofanyika hivi karibu nchini humo .
   Wachezaji wa timu ya Taifa ya mchezo wa kabadi wakiwasili jijini Dar es salaam wakitokea India kwenye mashindano ya mchezo huo uliofanyika hivi karibu nchini humo ambapo Tanzania imetolewa kwenye mashindano hayo .
  Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea nchini India kwenye mashindano ya mchezo wa kabadi uliofanyika hivi karibu nchini humo.
   

  0 0

  Walter Chilambo ni msanii maarufu nchini Tanzania, na alipata umaarufu baada ya kushinda mashindano ya Bongo Star search (BSS) wimbo huu ni wa kwanza wa gospel, na angependa support kutoka kwa Watanzania pamoja na Africa Mashariki.

  0 0

  Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara,kulia akibadilishana Matokeo na wachezaji wenzie,katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana (kushoto) na katibu mkuu wizara ya ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh Job Masima katikati katika mashindano ya Waitara Trophy Jumamosi Novemba 19 jijini Dar es salaam.
  Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara,kulia akibadilishana Mawazo na wachezaji mwenzi ambaye ni katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana (katikati) katika mashindano yaliyofanyika Jumamosi Novemba 19 jijini Dar es salaam kushoto ni katibu mkuu Wizara ya ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh Job Masima.
  Mshindi wa Jumla wa kombe la Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara, kutoka klabu ya Lugalo Juma likuli akiwa amenyenyua vikombe alivyokabidhiwa na Jaji Mkuu Mh Othman Chande aliyekuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo yaliyofanyika Jumamosi Novemba 19 jijini Dar es salaam.
  Mwenyekiti wa Klabu ya Lugalo brigedia Jenerali Michael Luwongo akiwa ameshika zawadi ya kikombe alichokabidhiwa na Chama cha Golf Tanzania TGU ikiwa ni ishara ya Kutambua Mchango wa Klabu hiyo katika kukuza mchezo wa Golf Nchini kulia ni mweka hazina wa TGU Akhil Yusuphali mara baada ya mashindano ya Waitara yaliyofanyika Jumamosi Novemba 19 jijini Dar es salaam.


  0 0

  Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa akizungumza na viongozi wa Kituo cha Maendelo Dakawa (hawapo pichani) wakati Waziri huyo na ujumbe wake walipotembelea kituo hicho na kujionea makaburi ya wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini kutoka Chama cha ANC.
  Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa(katikati) akiangalia makaburi ya wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini kutoka Chama cha ANC yaliyopo Dakawa wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
  Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa akiweka shada la maua katika eneo maalum katika makaburi ya wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini kutoka Chama cha ANC yaliyopo Dakawa wilayani Kilosa mkoani Morogoro.


  0 0

  Mashabiki wa muziki wa Singeli wakishuhudia Msaanii Mallo akifanya vitu vyake kwenye tamasha lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania la Mziki Mnene katika viwanja vya CCM Mwijuma Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo.

  Wasanii wa muziki wa Singeli wakionyesha vipaji vyao vya kusakata muziki huo kwenye tamasha lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania la Mziki Mnene katika viwanja vya CCM Mwijuma Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo.
  Beki wa timu ya soka ya veterani Mango Garden, Hamis Ramadhani (kulia )akimdhibiti Mshambuliaji, Nicolaus Benedict, kwenye pambano la kirafiki la Mziki mnene lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania kwenye viwanja vya Mango Garden, Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

   Mshindi wa Jumla wa kombe la Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara, kutoka klabu ya Lugalo Juma likuli akiwa amenyenyua vikombe alivyokabidhiwa na Jaji Mkuu  Mh Othman Chande aliyekuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo yaliyofanyika Jumamosi Novemba 19  jijini Dar es salaam.(
   Mshindi wa Kundi la Wanawake wa kombe la Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara, kutoka klabu ya Lugalo  Sophia Mathias  akipokea zawadi ya Meza  aliyekabidhiwa na Mke wa Jenerali Mstaafu Waitara katika mashindano hayo yaliyofanyika Jumamosi Novemba 19  jijini Dar es salaam.(
   Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara,kulia akibadilishana Mawazo na wachezaji mwenzi ambaye ni katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana (katikati) katika mashindano yaliyofanyika Jumamosi Novemba 19  jijini Dar es salaam kushoto ni katibu mkuu Wizara ya ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh Job Masima.(
   Mwenyekiti wa  Klabu ya Lugalo brigedia Jenerali Michael Luwongo akiwa ameshika zawadi ya kikombe alichokabidhiwa  na Chama cha Golf Tanzania TGU ikiwa ni ishara ya Kutambua Mchango wa Klabu hiyo katika kukuza mchezo wa Golf Nchini kulia ni mweka hazina wa TGU Akhil Yusuphali mara baada ya mashindano ya Waitara yaliyofanyika Jumamosi Novemba 19  jijini Dar es salaam
  Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara,kulia akibadilishana Matokeo na wachezaji wenzie,katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana (kushoto)  na katibu mkuu wizara ya ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh Job Masima katikati katika mashindano ya Waitara Trophy  Jumamosi Novemba 19 jijini  Dar es salaam.(Picha zote na Luteni Selemani Semunyu).

  0 0

   Kaimu Mkurugenzi kituo cha Maendeleo Dakawa Bw. Elasto Nywage(kulia) akitoa maelezo ya kituo hicho kwa Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa wakati Waziri huyo na ujumbe wako walipotembelea kituo hicho na kujionea makaburi ya wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini kutoka Chama cha ANC. 
   Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa(katikati) akiangalia makaburi ya wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini kutoka Chama cha ANC yaliyopo Dakawa wilayani Kilosa mkoani Morogoro. 
   Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa akisoma jina  katika moja ya  makaburi ya wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini kutoka Chama cha ANC yaliyopo Dakawa wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
   Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa akiweka shada la maua katika eneo maalum katika makaburi ya wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini kutoka Chama cha ANC yaliyopo Dakawa wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
   Eneo la makaburi ya wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini kutoka Chama cha ANC yaliyopo Dakawa wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
   Kaimu Mkurugenzi kituo cha Maendeleo Dakawa Bw. Elasto Nywage(kulia) akimuonesha Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa(katikati) bango linaloelezea kuwa eneo hilo ndipo yalipo makaburi ya wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini kutoka Chama cha ANC katika wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
  Bango linaloelezea kuwa eneo hilo ndipo yalipo makaburi ya wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini kutoka Chama cha ANC wilayani Kilosa mkoani Morogoro. Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM.

  0 0  0 0  0 0
 • 11/20/16--12:30: Article 0


 • 0 0

   Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kiwanda cha kuunganisha magari ya zimamoto na matrekta cha Equator SUMMA kilichopo Mlandizi mkoani Pwani 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini TRL, Masanja Kadogosa (kulia) kuhusu ujenzi  wa reli  inayounganisha  reli ya kati na  kiwanda cha Kiluwa Still Group cha Mlandizi Pwani Novemba 19, 2016  . Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini TRL, Masanja Kadogosa (kulia) kuhusu ujenzi  wa reli  inayounganisha  reli ya kati na  kiwanda cha Kiluwa Still Group cha Mlandizi Pwani.Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Asumpter Mshama na kulia ni Mbunge wa Kibaha Mhe. Abuu Juma
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mitambo ya kiwanda cha chuma cha Kiluwa Still Group kilichopo Mlandizi Pwani


  0 0

  It is one thing to have the food you love delivered to you at your convenience but it is another thing to have the same food delivered to you with an awesome deal. Once again Jumia food Tanzania is bringing to you a Black Friday sale.

  To your surprise, this sale will delight you for six whole days! From the 21st November to the 27th November 2016, Jumia Food will be delivering their customers the best deals from a variety of spectacular restaurants in Dar es Salaam. 

  Mamboz SizGrill, Spur, Rhapsody, Skyz Pizza, Fishmonger, Boulevard Inn and Sala Thai are just some of the great restaurants offering buy on get one free or massive percentages off all your favourite items! Whether you love your meat, fancy some sophisticated seafood or pasta, or simply want the comfort of pizza, we have something for you!  

  At Jumia Food, we work hand in hand with restaurants to ensure customer satisfaction. We make ordering food convenient by connecting our customers with a variety of restaurants and cuisines from Swahili,Indian,Thai ,Barbeque, Mexican and Japanese, the list goes on.  

  “We strive to delight all of our foodie customers, so we love hosting these online food festivals to let our restaurant partners showcase their amazing food and give our customers the best value for money. Now the Christmas shopping season is upon us, we are here to help you refuel for less!” said Nina Holmes, Managing Director of Jumia Food. 

  We are excited for this Black Friday deals because we know they are jaw dropping! Visit our website at http://www.food.jumia.co.tz/ or download the free app!

  0 0


                 Kupata magazeti mengine BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1435 | 1436 | (Page 1437) | 1438 | 1439 | .... | 3272 | newer