Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

JARIDA LA WIZARA YA NISHATI NA MADINI TOLEO NA 146


PRIDE Tanzania Yatoa Misaada kwa Wateja Wake Walioathirika na Tetemeko la Ardhi Bukoba

$
0
0
PRIDE (Promotion of Rural Initiative and Development Enterprise)ni shirika lisilo la kiserikali (NGO) linalotoa huduma za kifedha kwa masharti nafuu kwa wafanyabiashara ndogondogo na wa kati. Huduma hizo zina lengo la kuchangia pato la taifa na kuondoa umasikini nchini. 

PRIDE ilisajiliwa mnamo Mei 1993 chini ya wadhamini wasio na hisa (Company Limited by guarantee, not Having Share Capital) kulingana na Sheria ya Makampuni Cap, 212 ya mwaka 2012.na kuanza rasmi shughuli zake mwaka 1994 mjini Arusha.Kwa sasa Shirika lina matawi 85 yalioenea nchi nzima.

Tangu kuanzishwa, PRIDE imeweza kukopesha wajasiliamali mbalimbali nchini wapatao 1,700,000 nakutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni miatisa (bil. 900.0).

Katika kuungana naWatanzania, PRIDE Tanzania walitoa misaada mbalimbali moja kwa moja kwa wateja wao wa tawi la Bukoba ambao waliathirika na tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.Msaada huu ulilenga kuwawezesha wateja wa PRIDE kukarabati makazi yao. 

Vilevile PRIDE ilichangia katika mfuko wa maafa wa serikali kwa kutoa mifuko ya saruji na mabati.
pr2
Mteja wa PRIDE Tanzania, tawi la Bukoba, Bw. Revocatus Siliden akionyesha madhara aliyoyapata kwenye nyumba yake baada ya kutokea tetemeko la ardhi huko Mkoani Kagera.
pr3
Afisa wa PRIDE Tanzania, Ndugu Samson Tenga akimkabidhi Mteja wa PRIDE Tanzania, Tawi la Bukoba mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba yake ambayo ilibomoka kutokana na janga la tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
pr4
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Mstaafu Salum Kijuu akifurahia jambo na mmoja wa wawakilishi wa wateja wa PRIDE Tanzania, tawi la BukobaBi. Mariam Seleman ambae pia ni muathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
pr5
Diwani wa Kata ya Miembeni, Manispaa ya Bukoba, Mkoa wa Kagera (Shati la Kijani) Bw. Richard Gaspar pamoja na maafisa wa PRIDE Tanzania wakimkabidhi mifuko ya saruji mteja wa PRIDE, ambaye nyumba yake iliathirika na tetemeko la ardhi lililotokea Bukoba.
pr6
Meneja wa Kanda ya Ziwa, Bi. Hilda Nsombo akikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Mstaafu SalumKijuu msaada wa mabati na mifuko ya saruji kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.

WAZIRI SIMBACHAWENE AFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI NA MAADILI YA VIJANA WAZALENDO 47 KIVUKONI JIJINI DAR ES ESALAAM

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene amesema ili kusimamia mabadiliko na maendeleo ya nchi na maadili inatakiwa kuwa na kiongozi mbabe na mtemi.

Simbachawene aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya uongozi na maadili kwa wahitimu 47 wazalendo waliyoyapata Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere Kivukoni Kigamboni jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza kazi ya ujenzi ya kujitolea ya mwezi mmoja wilayani Mkuranga mkoani Pwani.

Alisema ili kusimamia mabadiliko na maendeleo nchi inatakiwa kuwa na mtu mbabe na mtemi na si kutegemea kundi fulani la watu kwani kwa kufanya hivyo kila kundi litahitaji kupendelewa baada ya kujiona bora kuliko jingine.

Alisema bila kuwa na viongozi wenye maadili nchi haiwezi kusonga mbele kwani tangu kuachwa kwa vijana kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambako kulikuwa kukitolewa mafunzo ya maadili athari zake zilijitokeza na ndipo kwa kipindi cha miaka 20 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilijikuta kikivamiwa na matajiri wakitaka nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi za ubunge, urais na kuingia katika ujumbe wa mkutano mkuu wa chama kwa njia ya fedha.

“Napenda kusema kuwa tunahitaji mabadiliko makubwa ya kukifumua chama chetu hasa katika mfumo mzima wa kupata viongozi kwani uliopo umetufanya tupoteze baadhi ya nafasi katika majimbo na hata katika uchaguzi ndogo kutokana na mfumo mbaya tulishindwa vibaya baada ya wanachama wetu kumpigia kura mtu mwingine kwa hasira huko vikao vyote vikiendeshwa kwa misingi ya fedha” alisema Simbachawene.
Muhitimu, Ebeneza Emmanuel akipokea cheti kutoka kwa 
mgeni rasmi.
Petro Magoti akikabidhiwa cheti.
Mhitimu Happiness Agathon akipokea cheti.
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.

NEC YAZIONYA ASASI ZINAZOTAKA KUTOA ELIMU YA MPIGA KURA

$
0
0

Hussein Makame, NEC

TUME ya Taifa ya Uchaguzi imesema haitasita kuifutia kibali cha kutoa Elimu ya Mpiga Kura Asasi yoyote itakayotoa maneno ya kuleta uchochezi au kupigia debe sera za chama fulani cha siasa kwani kufanya hivyo kukiuka matakwa ya Kisheria.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe wakati akijibu swali la mmoja wa wajumbe wa mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma leo.

Mjumbe huyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stela Manyanya alitaka kufahamu Tume ina utaratibu gani kuhakikisha baadhi ya Asasi zinazofadhiliwa kutoa elimu ya mpiga kura kutumia nafasi hiyo kuhasisha sera za chama fulani.

Bw. Kawishe alisema Kifungu cha 4 (C) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kimeipa mamlaka Tume kuzipa kibali Asasi na kuzisimamia na kuratibu Elimu ya Mpiga Kura na haitasita kufuta kibali hicho iwapo masharti yatakiukwa. 
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji Mstaafu Mary Longway (wa pili kushoto) wakati kabla ya kutoa elimu ya mpiga kura kwenye mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.Wa pili kulia ni Katibu Tawala wa mkoa huo Bw. Hassan Bendeyeko na kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe. 
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji Mstaafu Mary Longway (kulia) akieleza jambo wakati akitoa elimu ya mpiga kura kwenye mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge na katikati ni Katibu Tawala wa mkoa huo Bw. Hassan Bendeyeko. 
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe, akitoa elimu ya mpiga kura kwenye mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. 
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji Mstaafu Mary Longway (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge vitabu vya Taarifa ya Tathmini Baada ya Uchgauzi wa Rais,Wabunge na Madiwani baada ya kutoa elimu ya mpiga kura kwenye mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. 
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma  uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wakifuatilia elimu ya mpiga kura. 

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOV 19

KAMILISHENI UJENZI WA MAGOMENI KOTA KWA WAKATI - WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

NAIBU WAZIRI MPINA ALITOZA FAINI YA SHILINGI MILIONI THELATHINI GEREZA LA KEKO NA MILIONI ISHIRINI, KIWADA CHA MADAWA CHA KEKO, KWA KOSA LA UCHAFUZI WA MAZINGIRA

$
0
0
 Kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Naibu Waziri Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina (Mb.) Amelitoza faini ya shilingi milioni thelathini  Gereza la keko kwa kosa la kutiririsha maji taka yanayozalishwa gerezani hapo  hivyo kuhatarisha maisha ya Binadamu na viumbe hai wengine.

Akiwa katika ziara nyingine ya ukaguzi wa mazingira jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri Mpina Alilitaka Baraza hilo kutoa agizo kwa mkuu wa gereza hilo litakalokuwa na maelekezo ya  kujenga miundombinu ya majitaka ambayo ni rafiki kwa mazingira sambamba na kulipa faini hiyo kwa muda uliyotajwa.



“Taasisi za Serikali zinapaswa kuwa mfano kwa kutii sheria za nchi hususani sheria ya mazingira nimeshasema mara nyingi na ninarudia hapa tena taasisi za serikali haziruhusiwi kuchafua mazingira kwa namna yoyote ile kwa mujibu wa sheria. “ alisisitiza Mpina.



Aidha Mpina ameitaka Manispaa ya Temeke kusimamia kuwa makini na zoezi la usafi wa mazingira katika maeneo ya Keko na kuwachukulia hatua wananchi wote wanaotiririsha maji taka katika mifereji ya maji ya mvua.



Akitoa ufafanuzi wa adhabu hiyo mwanasheria wa Baraza la mazingira, Suguta  Heche, amesema kuwa Tasisi za serikali na mashirika ya umma yana wajibu wa kufuata sheria za nchi hususani sheria za mazingira na ukiukwaji wa sheria hizo utaambatana na adhabu kama zinatolewa kwa mashirika na makampuni binafsi.



Awali Naibu Waziri Mpina alitembelea kiwanda cha kutengeneza dawa cha Keko Pharmaceutical limited na kutoridhishwa na uharibifu wa mazingira unaofanywa na kiwanda hicho wa kutiririsha maji taka katika makazi bila kutibiwa, na kutokuwa na kibali cha utiririshaji kutoka kwa bonde na kuwatoza faini ya shilingi milioni ishirini inayopaswa kulipwa ndani ya wiki mbili, na kuelekeza usafi wa mazingira kufanyika katika mifereji ya maji ya mvua na kuwaasa wakazi wa maeneo jirani kutokutupa takataka katika maeneo hayo.



Kwa upande wake Bwana Selemani Ndugwana, Meneja uthibiti na Ubora wa kiwanda hicho cha dawa alipokea adhabu hiyo, na kusema kwamba ni kubwa sana wanaomba serikali iwapunguzie adhabu hiyo, kwa kuwa ni kosa la mara ya kwanza. Akiwakilisha wakazi wa eneo la keko mtendaji wa kata hiyo Bwana Samweli Magali alisema kero ya uchafuzi wa mazingira unaotoka kwenye kiwanda hicho cha madawa ni kubwa na ni hatarishi kwa afya za wakazi wa eneo hilo.


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina akifanya akipita pembezoni mwa mfereji wa maji taka, ambapo uko karibu na makazi ya watu
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina akikakagua uchafuzi wa mazingira unaofanywa na gereza la keko lililopo temeke jijini Dar es salaam.        

 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina akizungumza na waandishi wa habari mapema hii jana mara baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa mazingira jijini Dar es salaam.     

WAZIRI MWIJAGE AZINDUA RASMI KAMATI YA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NCHINI

$
0
0
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Mh Charles Mwijage amezindua rasmi Kamati ya Kuboresha Mazingira ya Biashara Tanzania,Kamati yenye lengo la kufanya uchambuzi wa kina wa  kufanya biashara nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kamati hiyo jijini Dar es Salaam,Waziri Mwijage amesema utashi wa Serikali ya Awamu ya Tano ni kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi  unaoongozwa na viwanda kama inavyoelekezwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.

Amesema kuwa “Uwekezaji wa mazingira bora ni zoezi endelevu hivyo kazi yetu Sekta ya Umma na Sekta binafsi ni kujipima katika maboresho”.

Katibu Mkuu-Sera,Ofisi ya Waziri Mkuu(PMO),Dkt.Hamisi Mwinyimvua amezungumzia Jitihada za Serikali kuhusu Maboresho ya Mazingira ya Biashara zilizokwisha fanyika na kuahidi kuendelea kufanyika.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mh. Charles Mwijage akizungumza na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Biashara wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Kuboresha Mazingira ya Biashara jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu-Sera,Ofisi ya Waziri Mkuu(PMO), Dkt.Hamisi Mwinyimvua akizungumzia Jitihada za Serikali kuhusu Maboresho ya Mazingira ya Biashara zilizokwisha fanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mh. Charles Mwijage akiwa katika picha ya pamoja na ziongozi mbalimbali jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.



TAASISI YA DORIS MOLLEL YA YATOA MSAADAWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Katika kuadhimisha Siku ya Watoto Njiti duniani,Taasisi ya Doris Mollel inayojihusisha na maswala ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati wameamua kuadhimisha siku hii kwa kumpelekea wheel chair, vyakula pamoja na box la sabuni kwa mama aliyejulikana kwa jina la Zainab Rashidi ambae ni mlemavu,mwenye watoto wawili waliozaliwa kabla ya wakati.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam,Msaidizi wa Kitengo cha Elimu-Taasisi ya Doris Mollel Rahma Amood amesema “Tumeamua kufanya hivi kwa lengo la kuhamasisha Taasisi nyingne na watu wengne waweze kuwakumbuka watoto hawa na kuweza kuwasaidia”. 

Doris Mollel Foundation kesho itaadhimisha siku hii kwa kutembea kilometa 3 visiwani Zanzibar kwa matembezi yatakayolenga kupunguza Watoto Njiti wanaozaliwa kote nchini. 

Kwa upande wake Mama huyo mwenye Watoto wawili waliozaliwa kabla ya wakati,Bi.Zainabu Rashid ameishukuru Taasisi hiyo kwa kumpa msaada huo kwa kumkumbuka.
Msaidizi wa Kitengo cha Elimu-Taasisi ya Doris Mollel, Rahma Amood akikabidhi msaawa wa wheel chair, vyakula pamoja na box la sabuni kwa mama aliyejulikana kwa jina la Zainab Rashidi leo jijini Dar es Salaam.
Msaidizi wa Kitengo cha Elimu-Taasisi ya Doris Mollel, Rahma Amood akimwelekeza, Zainab Rashidi njisi ya kutumia wheel chair leo jijini Dar es Salaam.
Msaidizi wa Kitengo cha Elimu-Taasisi ya Doris Mollel, Rahma Amood akiwa katika picha ya pamoja na Zainab Rashidi.
Msaidizi wa Kitengo cha Elimu-Taasisi ya Doris Mollel, Rahma Amood akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Zainab Rashidi.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

WAZIRI MKUU ATOA SIKU 18 UMEME UKAMILIKE MLANDIZI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku 18 kwa Mkandarasi wa umeme kwenye kiwanda cha Kiluwa Steel Group awe amemaliza kazi ya kuweka ume mkubwa ili kiwanda hicho kianze kazi.

Ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Novemba 19, 2016) wakati akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali wa Serikali na wa Mkoa wa Pwani waliofika kiwandani hapo eneo la Mlandizi wakati akikagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Julai 12, mwaka huu alipozuru kiwanda kwa mara ya kwanza.

“Nilipokuwa hapa mara ya kwanza niliagiza itengenezwe njia ya reli kutoka njia panda ya reli ya kati, lakini pia niliagiwa uwekwe umeme wa msongo mkubwa ili kiwanda kiweze kuanza uzalishaji mapema mwakani. Nimefarijika kukuta maagizo haya yametekelezwa kwa kiasi kikubwa isipokuwa hili la umeme,” amesema.

“Mkandarasi ameomba siku 14, nimempa hadi tarehe 7 Desemba ahakikishe umeme unafanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa. Sasa hivi wameanza test lakini muda ili transforma iweze kuhimili mzigo mkubwa… hili ni suala la kitaalamu kwa hiyo tuwape muda.”

Waziri Mkuu pia amesema amefarijika kusikia kwa orodha ya watu wanaodai fidia sababu ya kuoisha njia ya reli ijengwe, imeshawasilishwa kwa Mkuu wa Mkoa na mwenye kiwanda yuko tayari kuwalipa maa taratibu zitakapokamilika.

Mapema, akiwasilisha taarifa fupi, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Eng. Evarist Ndikilo alisema haelewi ni kwa nini mkandarasi huyo anazidi kuomba siku 14 ili kukamilisha wakati aliahidi kuwa 14 za awali zingetosha kukamilisha kazi hiyo.

Kuhusu fidia kwa wananchi na Halmashauri ya Wilaya hiyo, Mkuu huyo wa Mkoa alisema wananchi waliopisha njia wanadai fidia ya sh. milioni 95.76 na Halmashauri inadai sh. milioni 307.26 na kwamba jumla yote inafikia sh. milioni 403.

MCHEZAJI LANGA LESSE BERCY WA JAMHURI YA CONGO

$
0
0
Kama ilivyoripotiwa hapo awali, Shiikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya kutoridhika na kujiridhisha kuwa mmoja wa wachezaji wa Jamhuri ya Congo-Brazzaville, alikiuka kanuni za mashindano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, mwaka huu  lilimkatia rufaa mchezaji Langa-Lesse Bercy katika Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).
Kutokana na rufaa hiyo dhidi ya mchezaji huyo wa Congo, Langa Lesse Bercy, CAF liliagiza apelekwe Makao Makuu ya Shirikisho hilo, lililoko Cairo, Misri  kwa ajili ya kurudia na kuthibitisha umri wake kwa kipimo cha MRI (Magnetic Imaging Resonance).
TFF iliagizwa na CAF igharimie zoezi zima ikiwa ni pamoja na kulipia gharama za usafiri wa mchezaji husika na daktari wake  pamoja na kulipia gharama za vipimo. TFF ilikubaliana na matakwa hayo ya CAF na kulipia.
Kipimo ilikuwa kifanyike leo Novemba 19, 2016 saa 5.00 asubuhi mjini Cairo, Misri. Ujumbe wa TFF wa watu wanne ukiambatana na madaktari wawili uliwasili mjini Cairo tangu Novemba 17, 2016 ili  kuwa shuhuda wa zoezi la kipimo hicho.
Jana usiku saa 5.00 TFF ilipokea ujumbe kutoka CAF kuwa mchezaji Langa Bercy ameshindwa kusafiri kwenda Cairo kwa kuwa yuko katika eneo lililoko "vitani",eneo hilo halikutajwa.
TFF inaendelea kufuatia kwa karibu jambo hili ili kuhakikisha haki inatendeka .
Kadhalika Aidha TFF inaomba wadau wa mpira wa miguu wawe na subira katika kipindi hiki.

TaWaSaNet yawakutanisha wadau mbalimbali wa mazingira nchini

$
0
0
Mtandao wa asasi za kiraia unaojihusisha na masuala ya Maji na mazingira Nchini (TaWaSaNet) umeandaa mkutano  uliowakutanisha wadau Mbalimbali wa Mazingira Nchini, ili kuadhimisha  wiki ya usafi wa Mazingira inayoenda sambamba na siku ya choo na kunawa mikono Duniani inayo adhimishwa novemba 19 ya kila mwaka.

Akizungumza katika mkutano huo mgeni rasmi Naibu waziri wa Afya Jinsia wazee na Watoto Dkt Khamisi Kigwangala amesema, wizara yake imejipanga kusimamia kwa ukaribu  utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya  kitaifa na kimataifa inayolenga upatikanaji wa vyoo bora mashuleni na kwenye vituo vya Afya.

Dkt Kigwangala ameipongeza Taasisi ya TaWaSaNet kwa kufanikisha na kuandaa mkutano huo kwa kuwa wadau wazuri wa mazingira na kuzitaka asasi nyingine za kiraia kuunga mkono jitihada za serikali ya Awamu ya Tano katika kuendeleza kampeni mbalimbali za usafi  hapa Nchini.

Katika mkutano huo Kigwangala ametoa Tuzo kwa wanahabari mahiri kwenye uandishi wa makala usafi na mazingira ambapo  Bw.Gervas Hubile amepata tuzo ya makala bora ya usafi wa mazingira kwa upande wa radio na Bi Salome Gregory ametwaa tuzo ya Makala bora ya usafi wa mazingira kwa upande wa magazeti.

 Naibu waziri wa Afya Jinsia wazee na Watoto Dkt Khamisi Kigwangala akizungumza na wadau mbalimbali wa mazingira juu ya kutoa tuzo kwa wanahabari mahiri kwenye uandishi wa makala usafi na mazingira leo jijini Dar es Salaam.  
 .Afisa Sera wa Taasisi ya Tanzania Water and Sanitation Network (TAWASANET), Darius Mhawi wa (kwanza kushoto) akizungumza machache  kwenye utoaji wa tuzo kwa wanahabari mahiri kwenye uandishi wa makala usafi na mazingira leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu waziri wa Afya Jinsia wazee na Watoto Dkt Khamisi Kigwangala akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali  leo jijini Dar es Salaam.picha na Yasir Adam wa Globu ya jamii.

KLABU YA ROTARY YA OYSTER BAY YASHIRIKIANA NA WADAU KUTOA UFADHILI WA ELIMU KWA WANAFUNZI WA VYUO

$
0
0


Wanafunzi 20 kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini wamepata ufadhili wa elimu unaofikia jumla ya Tshs Milioni 70 kutoka Klabu ya Rotary ya Oyster Bay, fedha zilizokusanywa kutokana na michango ya makampuni na watu binafsi.

Lengo la mradi huu ni kutoa msaada wa kifedha kwa wanafunzi wa Kitanzania wenye alama za juu kimasomo na waliopata nafasi za kujiunga na vyuo lakini wakakosa fedha za kulipia masomo.

Wanafunzi hao walikabidhiwa hundi za malipo katika tafrija fupi iliyofanyika tarehe 18 November katika mgahawa wa Waterfront uliopo Slipway jijini Dar es Salaam. Tafrija hiyo iliandaliwa kwa lengo la kuadhimisha miaka 100 ya mfuko wa Rotary ambapo fedha zilizochangishwa katika hafla hiyo zitawekwa kwenye mfuko huo wa Rotary ujulikanao kama Rotary Foundation.

Rotary Foundation iliyoanzishwa miaka 100 iliyopita ina lengo la kuwawezesha wanachama wa Rotary duniani kote kukuza amani kwa kuboresha afya, kusaidia elimu na kutokomeza umasikini. Mradi wa Klabu ya Rotary Oyster Bay wa ufadhili wa masomo unaenda sambamba na juhudi za Rotary International za kusaidia elimu.

Mradi wa ufadhili wa masomo katika Klaby ya Rotary ya Oyster Bay ulianza mwaka 2010 na wanafunzi wawili kwa msaada wa mfadhili mmoja. Katika kipindi cha miaka mitano, mradi huu umefanikiwa kuwa mradi mkubwa zaidi ukilinganisha na miradi mingine inayofanywa na klabu hiyo. Mwaka huu, klabu ya Rotary ya Oyster Bay imetoa ufadhili kwa wanafunzi 20 kwenye aina mbalimbali za masomo ikiwemo uhasibu, uhandisi, udaktari na sheria na inajivunia kuanza kuona matunda yake ambapo mmoja wa wanafunzi hao amehitimu na kuanza kazi ya udaktari.

Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali nchini Tanzania hutuma maombi ya ufadhili na mchakato wa kina hufanyika ili kuchagua wanafunzi wanaokidhi vigezo. Maendeleo ya wanafunzi wanaochaguliwa kupata ufadhili huangalia kwa ukaribi ili kubaini kama wanastahili kuendelea kupata ufadhili wa masomo katika mwaka unaofuata.

Mradi huu wa ufadhili Kwa wanafunzi unawezeshwa na michango kutoka kwa makampuni na watu binafsi ambapo mwaka huu michango imetoka Karimjee Scholarships, Karimjee Jivanjee Scholarships, D.B Shapriya Scholarships, R Sheth Scholarships, K Shah Scholarships, Nasim Manji, JDC Scholarships, Eleanor and Paul Best, Diamond Trust Bank, S Rhemtullah, pamoja na Gajjar Autoworks and Premium Finishes Limited.

C-Park Sound yatikisa Dar

$
0
0

 Bendi ya muziki wa dansi ya C-Park Sound ya Kinondoni, Dar es Salaam imeendelea kutawala anga la muziki huo vitongoji vyote vya jiji ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita ilidhihirisha kuwa ni moto wa kuotea mbali.

Jumamosi iliyopita, katika baa maarufu ya C-Park (zamani Matema) gazeti hili, lilishuhudia mamia ya mashabiki wakiburudika na muziki wa bendi hiyo huku wakisifu na kupiga makofi mara kwa mara kutokana na kuguswa mitima yao.


“Bendi hii kiboko, yaani siamini watu wote hawa wanaifuata bendi hii tu, au kuna promosheni hapa? Sio rahisi baa kujaza watu hivi wakati leo kumbi maarufu za Kinondoni nyingi ziko tupu. Kwa kweli nimewavulia kofia hawa vijana wa C-Park Sound,” akasema mpenzi mmoja anayejiita Lukaku.


Kiongozi wa bendi hiyo, Magazine, ameliambia gazeti hili kuwa, kujaza watu, kushangiliwa sana na kutuzwa pesa na zawadi nyingine ni kitu cha kawaida kabisa kwa bendi yake kwa hiyo hashangazwi na matukio ya aina hiyo.


“Tunajua nini tunafanya. Kila wiki tuko hapa baa ya C-Park, Kinondoni B, tunapiga muziki aina zote, tena kwa ubora wa asilimia mia moja. Hatubahatishi, kila anayekuja hapa huja tena na tena,” akajinasibu Magazine. 

DC WA HANDENI,MH GONDWE AFANYA ZIARA YA KUSULUHISHA MGOGORO WA WAFUGAJI NA WAKULIMA MSITU WA HIFADHI YA LUGALA KIJIJI CHA KITUMBI WILAYANI HANDENI

$
0
0

Pichani wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni,Bw. William Makufwe akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya walipokuwa wakisikiliza kero za wanakijiji cha Kitumbi
Mkuu wa Wialaya ya Handeni,Mh Godwin Gondwe akizungumza na wanakijiji wa kijiji cha Kitumbi .

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Bw. William Makufweakizungumza na wanakijiji wa kijiji cha kitumbi.
Afisa ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. Sixtus Akiwaelewesha wanakijiji wa kijiji cha kitumbi kuhusu ardhi.
Baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha kitumbi wakitoa kero zao kwa Viongozi


WANATASNIA WA FILAMU MKOANI GEITA WAPEWA MTIHANI WA KUANDAA TAMASHA LA FILAMU.

$
0
0
Na George Binagi-GB Pazzo.

Wanatasinia ya Filamu mkoani Geita wamepewa mtihami ambao hata hivyo ni mwepesi ikiwa watakuwa na dhamira ya dhati ya kuikuza tasnia hiyo. 

Mtihani huo umetolewa hii leo na Waziri wa Afya Zanziar, Mahmood Kombo, aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kwenye kikao baina ya wasanii wa filamu mkoani Geita na Bodi ya Filamu nchini.

Mtihani wenyewe ni wanatasnia hao kwa kushirikiana na chama cha Waigizaji mkoa wa Geita, kuandaa Tamasha la Filamu mkoani Geita ambalo litasaidia kuinua tasnia hiyo mkoani humo, Kanda ya Ziwa na hata nchini kwa ujumla."Mkitayarisha Tamasha lenu, mimi mwakani nitakuja pamoja na familia yangu". Amesisitiza Waziri Kombo akitolea mfano Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar namna linavyofana na kuwatangaza wasanii pamoja na kuwaongezea kipato.

Hata hivyo wanatasnia ya filamu mkoani Geita kwenye risala yao wamesema wanahitaji kupewa mafunzo zaidi juu ya namna ya kuboresha filamu zao pamoja na upatikanaji wa stemp/stika kwa ajili ya ulinzi wa kazi hizo hivyo bodi ya filamu nchini iwasaidie katika hilo ambapo Katibu Mtendaji wa bodi hiyo, Joyce Fesso, amekubalina na maombi yao na kuahidi kufikisha mafunzo ya filamu mkoani Geita kama ilivyokuwa hivi karibuni mkoani Mwanza.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fesso (kushoto), akizungumza kwenye kikao cha Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita hii leo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Geita.

Mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye, aliyewakilishwa na Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Mahmood Thabith Kombo (wa piAli kushoto).

Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti Chama cha Waigizaji mkoani Geita, Rosemary Michael na anayefuata ni Herman Matemu ambaye ni Kaimu Afisa Tawala mkoa wa Geita.
Na BMG
Baadhi ya wanatasnia ya Filamu mkoani Geita waliohudhuria kikao baina yao na Bodi ya Filamu mkoani humo, wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fesso, ambapo amewasisitiza kuungana pamoja na kutengeneza filamu moja iliyo bora kwa ajili ya kuwatambulisha kwenye soko la filamu na pia kuutambulisha mkoa wa Geita badala ya kuwa na filamu nyingi zisizo na ubora.
Kutoka kulia ni mgeni rasmi, Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Mahmood Thabith Kombo ambaye amemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye.Wanaofuata ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fessoo, Mwakilishi wa balozi wa Tanzania nchini Denmark, Dotto Kahindi pamoja na Mratibu wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (Zanzibar International Film Festival), Robert Manondolo.
Mgeni rasmi kwenye kikao baina ya Bodi ya Filamu nchini na Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita, Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Mahmood Thabith Kombo (katikati) ambaye amemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye, akisisitiza wasanii mkoani Geita kushikamana na kushirikiana na viongozi wao pamoja na Serikali na kuandaa Tamasha la Filamu kwa kuwa fursa hiyo wanayo.

TAASISI YA DORIS MOLLEL YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI KWA MATEMBEZI, VISIWANI ZANZIBAR

$
0
0
Washiriki wa Matembezi ya hisani ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani yaliyotaribiwa na Taasisi ya Doris Mollel wakiwa na bango lenye ujumbe wa kuadhimisha siku hiyo, iliyoadhimishwa kitaifa Mjini Unguja, Zanzibar Novemba 19, 2016. Matembezi hayo yalianzia katika Uwanja wa Amani kupitia Uwanja wa Tumbaku na kuishia Viwanja vya Maisara.
 Baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakijumuika pamoja Wadhamini na Waratibu wa Matembezi ya hisani ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani, wakishiriki Matembezi hayo, yalianzia katika Uwanja wa Amani kupitia Uwanja wa Tumbaku na kuishia Viwanja vya Maisara, Mjini Unguja, Zanzibar.
Brass Band ya Chuo cha Mafunzo, Zanzibar ikiongoza Matembezi ya hisani ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Dunian,  iliyoadhimishwa kitaifa Mjini Unguja, Zanzibar Novemba 19, 2016. Matembezi hayo yalianzia katika Uwanja wa Amani kupitia Uwanja wa Tumbaku na kuishia Viwanja vya Maisara.
Mkuu wa Kitengo ya Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu akiwa pamoja na Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel pamoja na washiriki wengine katika Matembezi ya hisani ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani, yaliyoadhimishwa kitaifa Mjini Unguja, Zanzibar Novemba 19, 2016.
Mgeni Rasmi katika hafla ya Matembezi ya hisani ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani, Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Harusi Said Suleiman  aliemuwakilisha Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mama Asha Balozi, akitoa hotuba yake, katika hafla ya Kilele cha siku ya Mtoto Njiti Duniani, iliyoadhimishwa kitaifa Mjini Unguja, Zanzibar Novemba 19, 2016. Vodacom ndio Wadhamini wakuu walioeza kufanyikisha shughuli hiyo. Kulia ni Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Mratibu wa Matembezi hayo, Doris Mollel na kushoto ni Mkuu wa Kitengo ya Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu. 

Jumla ya Miradi 59 Kutoka Mikoa, Wilaya na Taasisi za Umma Zanzibar kuingizwa katika maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Mapinduzi

$
0
0
Jumla ya Miradi 59 Kutoka Mikoa, Wilaya na Taasisi za Umma Unguja na Pemba imependekezwa kuingizwa katika maadhimisho ya Sherehe za kutimia Miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 zinazotarajiwa kuanza mapema mwezi Januari mwaka ujao wa 2017.

Miradi hiyo imeanza kujadiliwa katika Kikao cha kwanza cha Halmashauri ya Kitaifa ya Sherehe na Mapambo Zanzibar kilichokutana kupanga muelekeo wa sherehe hizo kilichofanyika katika ukumbi mdogo ya Jumba la Kasri ya Kifalme liliopo Forodhani Mjini Zanzibar.

Mwenyekiti wa Kikao hicho cha Halmashauri  ya Kitaifa ya sherehe na Mapambo ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema sherehe za Mapinduzi  kwa Mwaka ujao hazitakuwa na tofauti na zile zilizopita za mwaka huu. 

Balozi Seif waliwaagiza Wakuu wa Taasisi za Umma pamoja na Wakuu wa Mikoa yote kufanya uhakiki wa ziara katika kuangalia miradi inayoweza kuingizwa katika ratiba ya sherehe hizo kwa ajili ya uwekwaji wa mawe ya msingi au kuzinduliwa rasmi.

Wakichangia mada hizo baadhi ya wajumbe wa Kikao hicho walieleza ni vyema masuala ya Bajeti yakaendelea kujadiliwa na Uongozi wa Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Kamati ya Sekriterieti ili kupata nguvu zitakazowezesha kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya Kila Kamati.

Wakigusia suala la Gwaride la Maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar Wajumbe hao walieleza kwamba Vikosi vya ulinzi vinawajibika kukamilisha utaratibu mzima wa Gwaride Kuu kulingana na uzito wa Sherehe husika.

Wajumbe wa Kikao hicho cha Halmashauri ya Kitaifa ya Sherehe na Mapambo Zanzibar wanatarajiwa kukutana tena Tarehe 5 Disemba 2016  kupokea mapendekezo ya Wizara ya Fedha itakayojadiliaja na Kamati ya Sekriterieti ya Halmashauri hiyo sambamba na kupokea Miradi mengine mipya itakayowasilishwa na wajumbe wa Sekta husika.
Wajumbe wa Halmashauri ya Kitaifa ya Sherehe na Mapambo Zanzibar wakijadili muelekeo wa sherehe za Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kilichofanyika katika ukumbi mdogo ya Jumba la Kasri ya Kifalme liliopo Forodhani Mjini Zanzibar. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Kikao cha Halmashauri hiyo ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Balozi Seif kushoto akikiongoza Kikao cha Halmashauri ya Kitaifa ya Sherehe na Mapambo Zanzibar kujadili muelekeo wa sherehe za Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Wajumbe wa Halmashauri ya Kitaifa ya Sherehe na Mapambo Zanzibar wakiendelea kujadili mada mbali mbali juu ya muelekeo wa sherehe za Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Picha na – OMPR – ZNZ.

DKT. SHEIN ALIFUNGUA RASMI KONGAMANO LA KIBIASHARA BAINA YA TANZANIA NA COMORO, ZANZIBAR LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro Mhe,Mohamed Bacar Dossar (katikati) wakisimama pamoja na Viongozi wengine wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania na Comoro ukipigwa wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Biashara baina ya Comoro na Tanzania katika ukumbi wa Sea Cliff Mangapwani Wilaya ya Magharibi "A" Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe,Amina Salum Ali alipowasili kufungua Kongamano la Biashara baina ya Comoro na Tanzania katika ukumbi wa Sea Cliff Mangapwani Wilaya ya Magharibi "A" Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahamoud pamoja na Viongozi mbali mbali alipowasili kufungua Kongamano la Biashara baina ya Comoro na Tanzania katika ukumbi wa Sea Cliff Mangapwani Wilaya ya Magharibi "A" Unguja leo.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA CHUMA NA KIWANDA CHA KUUNGANISHA MAGARI NA TREKTA MKOANI PWANI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameliegiza Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha lifanye maamuzi ya kupima ardhi haraka na kutenga maeneo kwa ajili makazi na viwanda ili kujiandaa na uwekezaji mkubwa.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumamosi, Novemba 19, 2016) wakati akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali wa Serikali na wa Mkoa wa Pwani mara baada ya kukagua kiwanda cha kutengeneza magari ya zimamoto na matrekta cha Equator SUMA JKT Limited kilichopo Ruvu JKT, wilayani Kibaha mkoani Pwani.  

“Jiji la Dar es Salaam limejaa, na Kibaha mjini pia hawana ardhi ya kutosha kwa kimbilio pekee hivi sasa ni Kibaha Vijijini. Baraza la Madiwani fanyeni maamuzi, pimeni ardhi na mtenge maeneo ya makazi, viwanda na taasisi za elimu ili mkipata wawekezaji iwe rahisi kuwapa maeneo,” amesema.

Waziri Mkuu amesema ujenzi wa kiwanda hicho utakuwa mkombozi kwa taasisi nyingi na halmashauri nyingi nchini kwani zilikuwa zinashindwa kumudu bei ya kununua magari ya zimamoto. “Baadhi ya Halmashauri nyingi zilikuwa zinanunua gari moja kwa sh. milioni 500 na hiki ni kiasi kikubwa mno kwa hiyo kiwanda hiki kitakuwa mkombozi kwa taasisi nyingi na halmashauri zetu,” amesema.

Amesema maeneo mengi nchini yanahitaji magari ya zimamoto lakini yalikuwa yanashndwa kumudu bei za magari hayo. Aliyataja maeneo hayo kuwa ni viwanja vya ndege, bandari, taasisi zilizo chini ya TAMISEMI kama vile shule za sekondari za bweni, Majiji, miji mikuu, Manispaa na Halmashauri za Wilaya.

Amesema ameguswa kukuta kiwanda hicho pia kina uwezo wa kutengeneza matreka na zana za kilimo (farm implements) kwani asilimia kubwa ya Watanzania ni wakulima na wanategemea jembe la mkono. “Kupitia kiwanda hiki, matrekta mengi yataunganishwa na nina imani bei itakuwa ya chini ili wananchi waweze kumudu.”
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini TRL, Masanja Kadogosa (kulia) kuhusu ujenzi  wa reli  inayounganisha  reli ya kati na  kiwanda cha Kiluwa Still Group cha Mlandizi Pwani Novemba 19, 2016  . Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mitambo ya kiwanda cha chuma cha Kiluwa Still Group kilichopo Mlandizi Pwani Novemba 19,2016 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akizungumza baada ya kukagua  maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha Kiluwa Still Group cha Mlandizi mkoani Pwani  Novemba 19, 2016.  Kushoto ni  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa 
 Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kianda cha kuunganisha magari ya zimamoto na matrekta cha Equator SUMMA kilichopo Mlandizi mkoani Pwani Novemba 19,2016(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images