Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1433 | 1434 | (Page 1435) | 1436 | 1437 | .... | 3272 | newer

  0 0
  0 0  0 0  0 0

  NYOTA mpya wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Samuel Afful, ameweka wazi kuwa kikosi hicho kitakuwa moto kuelekea michuano mbalimbali itakayoshiriki kuanzia mwezi ujao kutokana na ujio wake na aina ya wachezaji aliowaona ndani ya timu hiyo.

  Mshambuliaji huyo kutoka Ghana amesaini mkataba wa miaka mitatu juzi akitokea timu ya Sekondi Hasaacas ya huko, anaungana na nyota wengine Waghana waliosajiliwa na Azam FC msimu huu, beki wa kati Daniel Amoah, winga Daniel Atta Agyei na mshambuliaji Yahaya Mohammed.

  Afful, 20, alifunga bonge la bao kwa shuti kali kwenye mechi yake ya mwisho ya majaribio dhidi ya Ruvu Shooting Jumatatu iliyopita katika ushindi wa 3-1 wa Azam FC.

  Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz Afful alisema kwa aina ya wachezaji ambao Azam FC imewasajili kutoka Ghana akiwemo yeye basi itarajia kuwa na safu tishio ya ushambuliaji kwenye mechi zinazokuja.  0 0


  KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, inatarajia kuendelea na mpango wake wa kitaifa wa kusaka wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 (U-17) Jumamosi Ijayo Novemba 19, mwaka huu (kesho) katika Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya kuanzia saa 1.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana.

  Azam FC wikiendi iliyopita iliendesha zoezi hilo Dar es Salaam lililohudhuriwa na vijana 433 na kuchaguliwa saba pekee, na hivyo kufanya idadi kamili ya waliochaguliwa kwenye mchujo wa kwanza kufikia 50 miongoni mwa vijana 2,593 walisailiwa mpaka sasa katika maeneo manne ambayo Azam FC imeendesha zoezi hilo (Dar es Salaam, Tanga, Morogoro & Dodoma na Visiwani Zanzibar).

  Mara baada ya zoezi hilo kukamilika kwenye maeneo yote, vijana wote watafanyiwa mchujo wa mwisho mwezi ujao katika Uwanja wa Azam Complex kabla ya timu hiyo kuundwa rasmi kwa vijana bora watakaofanya vizuri kuchukuliwa.

  Vijana wanaotakiwa kuhudhiriwa zoezi hilo na wale walizaliwa kuanzia mwaka 2000, 2001, 2002, 2003 au 2004, ambapo uhakiki wa vyeti utafanyika kwa wale watakaochaguliwa.

  Kwa majaribio mengine ya wazi katika maeneo mengine kuzunguka Tanzania yatatangazwa hivi karibuni.

  0 0

  Na Veronica Simba.  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Ujumbe kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA) na kufanya mazungumzo kuhusu maendeleo ya miradi mbalimbali ya sekta ya nishati nchini inayofadhiliwa na shirika hilo.  Kikao hicho kilifanyika Novemba 17 mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara na kuhudhuriwa na viongozi waandamizi kutoka sekta ya nishati ambao ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Sekta ya Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli - James Andilile, Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati Sehemu ya Petroli – Mwanamani Kidaya na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba.

  Ujumbe wa JICA uliongozwa na Mwakilishi wake Mkuu hapa nchini, Toshio Nagase.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akisisitiza jambo katika kikao baina yake na Ujumbe kutoka JICA. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Nishati - Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli - James Andilile, Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati Sehemu ya Petroli – Mwanamani Kidaya na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba. 
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kulia), akiwasikiliza baadhi ya Maofisa kutoka JICA, wakati wakisaini Kitabu cha Wageni ofisini kwake baada ya kikao baina yao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hivi karibuni.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka JICA, walipomtembelea ofisini kwake hivi karibuni na kufanya mazungumzo kuhusu maendeleo ya miradi mbalimbali ya Sekta ya Nishati inayofadhiliwa na Shirika hilo hapa nchini.
   Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Digital Grid kutoka Japan, inayojishughulisha na usambazaji wa vifaa vya umeme wa jua hapa nchini, Bwana Akita (kulia), akielezea kuhusu utendaji kazi wa kampuni yake kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, watendaji mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Wizara pamoja na Ujumbe kutoka JICA.
  Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, James Andilile (mwenye tai nyekundu-kulia), akifafanua jambo kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, wakati wa kikao baina ya Waziri na Ujumbe kutoka JICA. Kulia kwa Waziri ni Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Sekta ya Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo.

  0 0


  Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Mikumi.

  HIFADHI ya Taifa ya Mikumi imeelezea hofu yake ya kutoweka kwa baadhi ya wanyama adimu katika hifadhi hiyo kutokana na kasi ya kuuwawa kwa kugongwa na magari ya abiria, binafsi, mizigo yanayopita bara bara ya kutoka dar es salaam na kwenda nyanda za juu kusini iliyopo ndani ya hifadhi hiyo.

  Uwepo wa barabara ya lami inayopita katikati hifadhi hiyo na kuongeza kasi ya kugongwa wanyama kila mwaka huku na kutia hofu ya kutoweka kwa baadhi ya wanyama adimu iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa.

  Hofu hiyo inatokana na takwimu zinazoonyesha kuwa wastani wa mnyama mmoja anagongwa kila siku huku pia zikionyesha kuwa kwa kipindi cha miaka 25 iliyopita hadi kufikia mwaka 2015 wanyama wa aina mbalimbali zaidi ya 3,435 walikufa kwa kugongwa na magari.

  Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya mikumi , Donat Mnyagatwa wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari wanawake waliotembelea hifadhi hiyo kwa lengo la kuitangaza zaidi ikiwa ni sehemu ya ziara ya siku kumi katika hifadhi za taifa za Saadan, Mikumi, Udzungwa na Ruaha mkoani Iringa.

  Alisema kuwa kwa mujibu wa takwimu zilizopo wanyama waliogongwa kuazia mwaka 1992 walikuwa 72 idadi ambayo imekuwa ikingezeka kwa kasi kila mwaka ambapo kwa kipindi cha mwaka jana 2015 wanyama wa aina mbalimbali waliogongwa na kufa ni 237.

  Hata hivyo Mnyagatwa alitaja takwimu za miaka tisa iliyopita ikianzia na mwaka 2007 waliokufa kwa kugongwa ni wanyama 43, 2008 wanyama 82, 2009 wanyama 45, 2010 wanyama 19, 2011 wanyama 125, 2012 wanyama 111, 2013 132 na mwaka 2014 wanyama 351.

  “Hifadhi hii ina ukubwa wa Kilomita za mraba 3230 lakini barabara imepita Km 50 ndani ya hifadhi inaweza kukadiriwa ama kuonekana ni jambo dogo lakini lina athari kubwa mno kwani tunaweza kupoteza baadhi ya aina ya wanyama kutokana na ongezeko la kasi la kufa kwao kutolingana na kasi ya kuzaliana”alisema.

  Aidha mhifadhi Mnyagatwa alitaja changamoto nyingine za uwepo barabara hiyo kuwa ni pamoja na hifadhi hiyo kupoteza mamilioni ya fedha kwa kufa wanyama, uchafuzi wa mazingira pamoja na kufanyika utalii wa bure ambao unapoteza mapato mengi ya serikali .

  "Ndugu zangu waandishi wa habari tunaomba sana mtusaidie hili suala la changamoto ya barabara hili ni tatizo kubwa hivyo tunaamini kuwa mtasaidia katika hili "alisema Mhifadhi Mkuu huyo.

  Alitaja chanagamoto nyingine ni pamoja na ujangili, kuzuka kwa moto, kubadili tabia za wanyama kwani baadhi ya watu wamekuwa wakiwarushia wanyama matunda na vyakula vya binadamu na kuota kwa mazao ya biashara yanayosafirishwa kupitia barabara hiyo yanapomwagika ndani ya hifadhi hiyo.

  Alisema kuwa baadhi ya madereva nyakati za usiku wamekuwa wakigiiza kuharibika kwa magari katikati ya hifadhi ili waweze kufanya ujangili .

  Akizungumzia kuhusu kutoweka kwa wanyama kipindi cha masika Mhifadhi utalii wa hifadhi ya Mikumi ,Abdalah choma alisema kuwa kipindi kizuri cha kutembelea hifadhi hiyo ni kipindi cha masika ambacho wanyama wengi hujikusanya sehemu moja katika hifadhi hiyo hivyo kutoa fursa kwa watalii kuona wanyama wengi hasa nyakati za asubuhi na jioni.
   Waandishi wa habari  wanawake kutoka Mikoa mbalimbali wakimsikiliza Ofisa wa Tanapa Abdallah Choma akiwapa maelezo juu ya hifadhi ya Mikumi
   Mkuu wa hifadhi ya Mikumi Donat Mnyagatwa akiongea na waandishi wa habari wanawake waliofanya ziara katika hifadhi ya mikumi
  Baadhi ya vivutio vilivyopo katika hifadhi ya Mikumi


  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Waislamu nchini waendelee kushirikiana na Serikali kulinda na kudumisha amani na utulivu uliopo nchini.Aidha, amewasihi waislam kuimarisha umoja ,upendo ,mshimano miongoni mwao kwa kushirikiana na jamii zinazowazunguka bila kujali tofauti zao za kiimani.

  Ametoa wito huo leo mchana (Ijumaa, Novemba 18, 2016) wakati akishiriki sala ya Ijumaa katika msikiti wa Kichangani, Magomeni jijini Dar es Salaam. Amesema uwepo wa dini umewezesha nchi kuendelea kuwa na amani na utulivu hivyo kila mmoja ahakikishe suala hilo linaendelezwa.

  Pia amewashauri waumini na viongozi wa dini kuzingatia maadili ya dini ili kuepusha migongano isiyo ya lazima hasa taasisi zinapokuwa na miradi.Waziri Mkuu alitolea mfano msikiti huo wa Kichangani chini ya Sheikh Walid umeweza kusuluhisha hitilafu wenyewe bila kukimbilia Serikalini au mahakamani kusuluhishwa.Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema Waislamu wana jukumu la kuwafunza elimu ya dini watoto wao na kuhakikisha wanakua kwenye imani na kujengeka katika maadili mema.

  Amesema dini inajenga maadili mema kwa mtoto na kumwezesha kukua katika misingi ya uvumilivu na inamuwezesha kumtambua Mwenyezi Mungu.“Nimefarijika kuona vijana wengi wameshiriki katika sala hii ya Ijumaa. Nawaomba wazazi waendelee kuelimisha watoto umuhimu wa kufanya ibada,” amesema.

  “Tuendelee kuwafundisha vijana wetu umuhimu wa kushiriki kikamilifu kwenye masuala ya kidini ili wakikua waweze kuiendeleza kwa vizazi vijavyo,” amesema.Waziri Mkuu amewaomba waumini hao waendelee kuwaombea viongozi wa kitaifa ili waweze kutekeleza vizuri majukumu yao na kufikia malengo yanayotarajiwa na wananchi.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S. L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM.
  IJUMAA, NOVEMBA 18, 2016.

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mshauri wa Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Edwin Nnuduma  kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam wakati alipotembelea mradi huo Novemba 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mshauri wa Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Edwin Nnuduma  kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam wakati alipotembelea mradi huo Novemba 18, 2016. Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally  Happy.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokagua Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam Novemba 18, 2016.  Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Happy. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).  0 0

  YAHYA HAMAD KAIMU MWENYEKITI KAMATI YA SAA 72 YA TFF 

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kunashukuru wanafamilia wa soka kwa salamu mbalimbali za rambirambi kutokana na msiba wa Mwenyekiti wa Azam FC na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu, Sheikh Said Muhammad aliyefariki dunia Novemba 7, 2016 katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam.

  Hayati Sheikh Said Muhammad kualikuwa hazina katika mpira wa miguu nchini kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutoa mchango ya mawazo na miongozo katika Kamati ya Utendaji ya TFF. 

  Itakumbukwa kwamba Sheikh Muhammad aliongoza Klabu ya Azam kwa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) kwa mara ya kwanza tangu klabu hiyo ianzishwe.

  Kutokana na kufariki kwa Sheikh Muhammed, Rais wa TFF, Jamal Malinzi amempendekeza Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Bwana Yahya Hamad - kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uendeshaji Ligi (Kamati ya Saa 72) ili kushughulia masuala yote ya mechi zilizochezwa tangu mwanzo wa Novemba, 2016 baada ya kifo cha Sheikh Muhammad.

  Tunachukua nafasi hii kutoa wito kwa klabu kumpa ushirikiano Bwana Hamad katika majukumu yake mapya akiongoza kamati hiyo yenye wajumbe ambao ni Baruan Muhuza (Azam Tv), Boniface Wambura (Mtendaji Mkuu Bodi ya Ligi), Jonas Kiwia (Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano TFF), Philemon Ntahilaja (Mdau wa Mpira wa Miguu), Charles Ndagala (Katibu Kamati ya Waamuzi ya TFF), Kanali Mstaafu wa JWTZ, Isaron Chacha na Steven Mnguto ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya ligi. 


  0 0

  Baadhi ya wananchi wa kata ya MWENGEMSHINDO Manispaa ya SONGEA mkoani RUVUMA ambao maeneo yao yamechukuliwa na MAMLAKA ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA) kwa kipindi cha miaka tisa iliyopita bila kuwalipa fidia yoyote, wamemuomba rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania DOKTA JOHN POMBE MAGUFULI kuingilia kati suala hilo ili waweze kupata haki yao.story kamili bonyeza hiyo video. 

  0 0

   
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba (Kulia) akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 22 wa Dunia wa Mabadiliko ya Tabianchi, huko Maracckech - Morocco. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mbarak Abdulwakil.  0 0


  Wakili Nyinula Watson Mwakyusa kushoto toka TAWLA na Msajili wa NGOs kutoka Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiendesha kikao cha ushirikiano baina ya NGOs na Wizara hiyo.
  Wadau mbalimbali kutoka Mashirika yasiyo ya Kiserikali wakipitia nyaraka  mbalimbali wakati wa Mkutano wa Ushirikiano baina ya Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika yasiyo ya kiserikali leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Washiriki kutoka moja ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali wakifuatilia jambo kwa makini wakati wa Mkutano wa Ushirikiano baina ya Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika yasiyo ya kiserikali leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imebuni na kuanza kutekeleza mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa bure kwa watoto wenye umri chini ya Miaka mitano.

  Akizungumza na wanahabari Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu RITA Emmy Hudson amesema kuwa mpango huo umebuniwa ili kuleta suluhisho la changamoto iliyokuwa ikisababisha watoto kushindwa kusajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa kwa wakati.

  Aidha amesema kuwa mpango huo ambao ulianza katika Mikoa ya Mwanza, Mbeya na Songwe hivi karibuni ulizinduliwa katika mikoa ya Iringa na Njombe hivyo basi ni mpango endelevu na wa kudumu.
  Emmy ameongeza kuwa utekelezaji huo umefanikiwa kwa mikoa hiyo ambapo Njombe imepanda kutoka 8.5% ya watoto walisajiliwa hadi kufikia 98%.
   Kaimu Afisa Mtendaji  Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Emmy Hudson akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa bure kwa watoto wenye umri chini ya Miaka mitano leo jijini Dar es Salaam.kuliani Meneja Usajili (RITA) Angela Anatory na kushoto ni Mkurugenzi wa Tehama(RITA) Cuthbert Simalenga
   Meneja Usajili (RITA) Angela Anatory akifafanua jambo katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam lishoto ni Kaimu Afisa Mtendaji  Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Emmy Hudson
  Sehemu ya waandi wa habari wakimsikiliza Kaimu Afisa Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Emmy Hudson.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya  jamii

  0 0
 • 11/18/16--06:43: Article 18

 • 0 0

                                                                      NA RABI HUME.

  KAMPUNI ya Paraa Mwanga ambayo inajihusisha na uuzaji wa sola imefanya uzinduzi wa kampeni ambayo imepewa jina la Tunaangaza Afrika ambayo itawawezesha watanzania kushiriki na kushinda kwa kutumia 500 tu.

  Akizungumza kuhusu kampeni hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Paara Mwanga, Neela Krishnamurthy alisema malengo ya kampuni yao ni kusaidia maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma ya umeme na hivyo kupitia kampeni hiyo wananchi watakuwa wakishiriki na kushinda zawadi ya sola za kampuni hiyo ambazo zitawasaidia kupata mwanga katika nyumba zao.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Paara Mwanga, Neela Krishnamurthy akielezea kampeni ambayo wameanzisha itakayowawezesha watanzania kushinda vifaa vya umeme wa jua (sola) vinavyouzwa na kampuni hiyo.

  “Kutakuwa na droo na itafanyika kila wiki na kutakuwa na mshindi, atakuwa akipatiwa tv na tutakuwa tunampatia sola, kila wiki atakuwa anatangazwa mshindi mmoja hadi shindano limalizike,” alisema Krishnamurthy.

  Nae Meneja wa Kampuni ya Paraa Mwanga, Michael Mbughi amezungumza kuhusu kampuni hiyo na kusema kuwa ni kampuni mpya Afrika ambayo kwa kuanza imeanzia Tanzania ili kuwezesha jamii ya watanzania na zaidi maeneo ya vijijini kupata vifaa vya umeme ambavyo vinauzwa na kampuni hiyo.
  Meneja wa Kampuni ya Paraa Mwanga, Michael Mbughi akizungumza kuhusu kampuni hiyo na bidhaa inazoziuza katika maeneo ambayo wanafanya kazi.

  “Tuna mradi ulio na lengo la kuiangaza Afrika na hasa maeneo ya vijijini ambapo umeme haujafika, tumeona tuanzie Tanzania na baadae tutaenda katika nchi nyingine, na katika hilo tayari tumeenda Mbagala na kugawa bure sola katika kaya 10,

  “Tutatuma watu wetu na baadae tutakuwa na mawakala katika mikoa ambayo tutakuwa tunafanya kazi, bidhaa hizi zipo za aina tofautitofauti na kwa kuanza tutakuwa katika mikoa na Kagera, Katavi, Sumbawanga na Rukwa,” alisema Mbughi.  Mmoja wa wafaidika wa msaada wa sola kutoka kampuni ya Paraa Mwanga, Said Athman akiwasha taa baada ya kuunganishiwa umeme huo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa muda wa mwezi Mwezi Moja kuanzia leo tarehe 18-Nov-2016 kwa watendaji na viongozi waandamizi wa wilaya ya Ilemela wahamie kwenye wilaya hiyo haraka iwezekanavyo na waache tabia ya kukaa kwenye wilaya nyingine kwa kisingizio cha kukosa nyumba za serikali.

  Makamu wa Rais ametoa agizo hilo katika hotuba yake kwa wananachi na watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi jengo la utawala la Manispaa hiyo na kukabidhi madawati 1,074 yaliyotolewa na ofisi ya Bunge.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha kukerwa na tabia hiyo na amewataka viongozi hao wahamie karibu na maeneo yao ya kazi kabla ya muda aliotoa kwisha ili waweze kuwa karibu na wananchi katika kuwasaidia kutatua kero na matatizo yanayowakabili kwa haraka.
  2

  Akiwa katika wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wakati anaweka jiwe la msingi katika mradi wa ukarabati wa mchinjio ya Nyakato jijini Mwanza, Makamu wa Rais ameuagiza uongozi jiji la Mwanza kusimamia kikamilifu mradi wa ukarabati wa machinjio ya Nyakato na watendaji watakaobainika kuhujumu mradi ambao utagharimu zaidi ya shilingi bilioni Tatu wachukuliwe hatua kali za kisheria.

  Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo katika hotuba yake kwa wananchi na watendaji wa jiji la Mwanza waliohudhuria hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa ukarabati wa machinjio ya Nyakato unaohusisha uboreshaji wa jengo la machinjio,tanki la kuhifadhi maji,ujenzi wa vyumba vya baridi vya kuhifadhi nyama na ujenzi wa mtambo wa kutibu majitaka yanayotoka kwenye machinjio hiyo.

  Makamu wa Rais katika hotuba yake, amesema hategemei hata kidogo ukarabati wa machinjio hiyo ufanyike chini ya kiwango kwa sababu ni mradi wa kibiashara ambao ukikamilika na kuanza kufanya kazi utasaidia jiji la Mwanza kupata mapato yatakayosaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi.

  Makamu wa Rais pia amemwagiza Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ahakikishe anasimamia uundaji wa menejimenti ya machinjio hiyo ambayo itafanya kazi vizuri na sio kuingiza watu ambao hawana uwezo ambao watakwamisha utendaji kazi wa machinjio hiyo.

  Kuhusu ukusanyaji wa kodi, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahimiza watendaji wa Halmashauri zote za mkoa wa Mwanza waongeze kasi ya ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa njia ya kielekroniki kutoka kwenye vyanzo mbalimbali fedha ambazo zitasaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi mkoani humo.

  Makamu wa Rais pia ametoa wito maalum kwa wananchi nchini wahakikishe wanadai risiti wanaponunua bidhaa mbalimbali kwani kufanya hiyo watasaidia kuongeza mapato yake ambao yataelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia wananchi wa Nyamagana kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa machinjio ya Nyakato. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akipata maelezo ya ujenzi wa machinjio ya Nyamagana kutoka kwa Mhandisi wa jiji la Mwanza Ndugu Ezekiel Kunyalanyala (kushoto) kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa machinjio ya Nyakato.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa Jengo la Utawala Manispaa ya  Ilemela . 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akikikabidhi madawati kwa Mbunge wa Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula ambayo yalitolewa na Ofisi ya Bunge ambapo zaidi ya madawati 1074 yalikabidhiwa kwa wilaya ya Nyamagana na Ilemela. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipanda mti wa kumbukumbu mara baada ya kufungua jengo la Manispaa ya Ilemela. 


  0 0


  0 0
  0 0


  0 0

older | 1 | .... | 1433 | 1434 | (Page 1435) | 1436 | 1437 | .... | 3272 | newer