Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1432 | 1433 | (Page 1434) | 1435 | 1436 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Na Bashir Nkoromo

  Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, imeainisha maeneo ya magulio kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo ndogo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuzitaka mamlaka zinazohusika kutenga maeneo ya wafanyabiashara hao kabla ya kuwatimua katika maeneo yasiyoruhisiwa.Akizungumza na waandishi wa habari leo Ofisini kwake, Mkuu wa Wilaya hiyo, Salum Hapi, ameyataja maeneo hayo kuwa yapo katika kata za Kinondoni, Bunju, Msasani, Mabwepande, Kunduchi na Kata ya Wazo.

  Hapi amesema, vitu vitakavyoruhiswa kuuzwa kwenye magulio hayo ni bihaa za sokoni, vyombo vya nyumbani, nguo mpya na mitumba, viatu, urembo, na kwamba kwa ujumla ni bidhaa ambazo hutumiwa na watu katika maisha ya kila siku. Ametaja mpangilo unaotakiwa kwenye magulio hayo kuwa ni, kupangwa eneo moja bidha zinazofanana, viwepo vyoo vya muda, na usafi wa eneo la gulio ambao utasimamiwa na Mtendaji Mwenyewe wa eneo husika.

  MPANGILIO NA RATIBA KAMILI YA MAGULIO HAYO


  0 0


  0 0


  0 0


  SIMU.TV: Tanzania imeungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya watoto njiti ikilenga kupunguza idadi vifo vya watoto wanaozaliwa njiti. https://youtu.be/6mnF6FeuygU

  SIMU.TV: Baraza la usimamizi na uthibiti wa mazingira NEMC limekamata magari yaliyokuwa yakijihusisha na uchimbaji holela wa mchanga kwenye daraja la Magole wilayani Kilosa. https://youtu.be/xYvGdX0L7dw

  SIMU.TV: Zaidi ya ngombe 2500 wamekutwa wakiharibu vyanzo vya maji vya mto Katuma uliopo wilayani Mpanda katika mkoa wa Katavi. https://youtu.be/7jyNk7Iy-1Q

  SIMU.TV: Wakazi wa Mji Mwema katika wilaya ya Kigamboni wanaojihusisha na uchumbaji wa kokoto wamelalamikia agizo la mkuu wa wilaya hiyo la kuwataka waondoke maeneo hayo ya uchimbaji. https://youtu.be/XW5BIR888ys

  SIMU.TV: Serikali imetoa muda wa mwezi mmoja na nusu kwa mikoa yote nchini ambayo haijamaliza tatizo la madawati kuhakikisha inamalizia changamoto hiyo. https://youtu.be/2HHeK1Vrw1Y

  SIMU.TV: Benki ya Amana tawi la Mbagala jijini Dar es Salaam imezindua huduma mpya ya mikopo kwa wajasiriamali wadogo ili kukuza mitaji yao. https://youtu.be/bSHKFXPqrcI

  SIMU.TV: Halmashauri nchini zimeshauriwa kutumia vifaa nyenye ubora katika ujenzi wa barabara na usafi wa mazingira ili kuepuka gharama za marekebisho ya mara kwa mara kwa vitendea kazi. https://youtu.be/PnpmiKY2VQw

  SIMU.TV: Ongezeko la wawekezaji katika sekta ya mawasilino nchini imewezesha serikali kufanikisha lengo la kuwarahisishia wananchi huduma za mawasiliano. https://youtu.be/z5in97ceLPk

  SIMU.TV: Ligi ya vijana wenye umri wa chini ya miaka ishirini imeendelea leo wakati timu ya Azam imekubali kutoshana nguvu na timu ya Mbao Fc kwa mabao mawili kwa mawili. https://youtu.be/To_ALIGmt9E

  SIMU.TV: Mbunge wa jimbo la Mikumi Joseph Haule amekabidhi vifaa vya michezo kwa timu 30 za kata za jimbo hilo kwa ajili ya mashindano ya kombe la Profesa jay cup. https://youtu.be/4HK5z2wZkOM

  SIMU.TV: Nahodha wa timu ya Uingereza Wayne Rooney amemuomba msamaha kocha wa timu ya taifa kufuatia picha zilizosambaa zikimuonesha akiwa amelewa. https://youtu.be/p7KgNimZ3QE

  SIMU.TV: Klabu ya Azamu Fc imekamilisha usaji wa wachezaji wawili kutoka nchini Ghana kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara. https://youtu.be/-fNF3S_ITKI

  SIMU.TV: Klabu ya Mbeya city imewataka mashabiki wake kuendelea kuwa wavumilivu wakati ikijiandaa kutoa taarifa rasmi ya usajili wa dirisha dogo la msimu huu. https://youtu.be/XSCt4XyucN4

  SIMU.TV: Timu ya soka ya wanawake ya mkoani Mtwara imepiga hodi kwa mkuu wa mkoa huo Halima Dendego kuomba msaada wa kuwawezesha kwenda mkoani Pwani kwa ajili ya michuano ya ligi ya wanawake. https://youtu.be/5JoLeZiZWpM

  0 0
 • 11/17/16--13:38: KUMBUKUMBU
 • Marehemu Mama  Lydia Mkufya Stephen

  Leo tarehe 18/11/2016 ni miaka minane tangu umetwaliwa.

  Tunakukumbuka sana na kuna wakati tunahisi kabisa hapa ungelikuwepo ungetupa ushauri na kadhalika.
  Tunakushukuru sana kwa malezi yako kwani yale uliyotuasa tunayafanya na kuona faida yake .

  Tunaamini uko na sisi kiroho na kuna siku moja tutaonana.

  Tunazidi kumwomba Mungu aendelee kututunza hasa baba yetu ili maisha ya sisi tuliobakia yaendelee.

  Unakumbukwa na mumeo, wanao, wakwe, wajukuu ,wadogo zako, marafiki na majirani wote.

  Bwana ametoa na Bwana ametwaa
  jina lake lihidimiwe
  Amina.  0 0


  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuwashukuru wakazi wa Dar es Salaam kwa  kushiriki katika zoezi la kuhakiki Namba ya Utambulisho Mlipakodi (TIN).
  Kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi kutaka kuhakiki taarifa zao, Mamlaka imeamua kuongeza muda wa uhakiki hadi tarehe 31 Januari, 2017. Pamoja na kuongeza muda wa uhakiki, Mamlaka pia imeongeza vituo vya kuhakiki.
  TRA pia inawakumbusha wananchi kuwa wale wenye TIN za biashara wanatakiwa kuhakiki katika ofisi za kodi Mkoa husika na wenye TIN zisizo za biashara (yaani TIN iliyotokana na maombi ya leseni ya udereva au ya kuingiza mzigo bandarini) wanaweza kuhakiki katika kituo chochote hapa Dar es Salaam.
  Vituo vya uhakiki vilivyopo ni kama  ifuatavyo:
  Pamoja na vituo hivyo, Mamlaka imeanzisha kituo kinachohama (Mobile Office) ambacho kinatoa huduma sehemu mbalimbali.  Ili kuongeza ufanisi, Mamlaka itaendelea kuboresha huduma zake kwa kuongeza vitendea kazi na vituo vingine vya kuhakiki.
  Mwisho, Mamlaka inawasihi  wananchi kuepuka kutumia  Matapeli (Vishoka) kwani zoezi hili linamtaka mlengwa kufika mwenyewe kwenye kituo husika.
  Kwa ufafanuzi zaidi tafadhali wasiliana na kituo cha huduma kwa walipakodi kwa kupiga simu za bure: 0800 780078 / 0800 750075 barua pepe: huduma@tra.go.tz

  Pamoja Tunajenga Taifa Letu
  Limetolewa na:
  Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
  TRA- Makao Makuu

  0 0

   Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameahidi kushirikiana na Taasisi zote zilizo chini ya Wizara yake kwa kuhakikisha zinajiendesha kwa faida ili Serikali ifaidike na mapato yatokanayo na biashara za Taasisi na Mashirika yote kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi pamoja na kupunguza umaskini.

  Dkt. Mpango aliyasema hayo katika uzinduzi wa Bodi ya Wajumbe wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), uliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.

  Katika uzinduzi huo Waziri Mpango ameishauri NIC kutoa elimu ya kutosha kwa Wananchi walioko vijijini na mijini ili watambue umuhimu wa Bima mbalimbali zinazotolewa na Shirika hilo.

  Aliongeza kuwa Shirika hilo linatakiwa kubuni mikakati mizuri ya kuongeza huduma za bima nchini hasa katika Sekta ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi kwa kuwa sekta hizo zimeajiri idadi kubwa ya wananchi ililiweze kupata faida na kutoa gawiwo kwa serikali.

  “Naishauri Bodi iwe bunifu na kuhakikisha kuwa huduma za bima zinaelekezwa kwa wananchi waliowengi vijijini ambao wanakosa huduma hizo kwa kipindi kirefu ili waweze kunufaika na huduma hizo badala ya kung’ang’ania mijini kama zinavyofanya Benki” alisisitiza Dkt. Mpango

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Sam Kamanga, amesema kuwa Menejimenti itashirikiana bega kwa bega na Bodi iliyozinduliwa  ili kurudisha hadhi ya Shirika hilo, lakini pia itafanya kazi kwa uaminifu na umakini mkubwa ili kuongeza idadi ya wateja ambao watachangia mapato ya Serikali.

  Amesema kuwa Shirika hilo limejiekeza kupanua wigo wa utoaji wa huduma zake kwa kuanzisha Bima kwaajili ya wakulima, wafugaji na wavuvi kwa kuwa eneo hilo halijaweza kufikiwa na huduma hizo.

  Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Bw. Laston Msongole, amesema kuwa Bodi hiyo itahakikisha kuwa shirika hilo linakuwa la kisasa na lenye tija kwa taifa.

  Amesema katika kipindi kifupi cha kulifufua shirika hilo limeweza kupata faida ya zaidi ya shilingi Bilioni 6.8 hatua iliyoliwezesha kuwalipa wateja wao madai yao ya bima.

  “Katika Kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya Tano, NIC imewalipa wateja wake madai yao yanayofikia kiasi cha shilingi Bilioni 1.26 sawa na asilimia 9.8 ya makusanyo yote ya biashara ya Bima katika kipindi cha Oktoba 2015/2016.

  Ameiomba serikali iridhie maombi ya Shirika hilo ya kuiruhusdu iuze baadhi ya rasilimali zake yakiwemo majengo na viwanja ili lipate mtaji wa kutosha na kuliwezesha kulipa madai ya wateja wao ambao wameanza kulitumia tena shirika hilo kwa kasi baada ya kuboreshwa.

  Shirika la Bima la Taifa (NIC) linashughulika na biashara ya Bima za Maisha na zisizo za maisha, ikiwemo kuuza bima za mali na ajali ambazo ni Bima za moto, magari, meli, ndege, wizi na ujenzi hali kadhalika kushughulikia biashara ya soko la pamoja la mashariki na kusini mwa Afrika (COMESA) na taasisi nyingine za kikanda.

  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Bima la Taifa (NIC) pamoja na waandishi wa Habari (hawapo pichani), kabla ya uzinduzi rasmi wa Bodi ya NIC Jijini Dr es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Sam Kamanga, akielezea mikakati mipya ya Shirika hilo katika kuboresha utoaji wa huduma za Bima za aina mbalimbali kwa wateja wao, wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Shirika hilo, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango  (kulia), akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw. Laston Msongole (Kushoto), vitendea kazi ikiwemo sheria za masuala ya Bima na miongozo mingine ya sekta hiyo ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa Bodi ya Shirika hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Bima la Taifa (NIC) pamoja na viongozi wengine wa Serikali na Maafisa wa Shirika hilo baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Bodi ya Shirika hilo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Sam Kamanga na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw. Laston Msongole. (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Fedha na Mipango)


  0 0

  Asasi Ya Vijana, Tanzania Youth Vision Association kwa Kushirikiana Na International Republican Institute zimetoa mafunzo ya kuboresha Uwezo wa Vijana kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba nchini katika Mikoa mitatu ilijumuisha Wilaya Nne, ikiwemo Kinondoni, Dodoma Mjini, Chamwino Na Tanga Mjini.

  Mafunzo hayo yameweza kufikia vijana 500 kwa njia ya Warsha na Vijana aa wananchi zaidi ya 100,000 kupitia mitandao ya kijamii.

  Lengo kuu la Mafunzo hayo ni kuongeza uelewa na ushiriki wa Vijana katika mchakato wa Mabadiliko ya Katiba. Katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Katibu Mtendaji wa TYVA ndugu Saddam Khalfan alisema, TYVA inaamini Katiba ni Sheria mama na mwongozo ambao una uhusiano wa moja kwa moja na maisha yetu ya kila siku.

  Alibainisha watu wengi wamekua wakisoma au kuisikia Katiba, na wengine wakidhani Katiba ni maalumu kwa ajili ya wanasheria au wasomi tu. Kuna uhusiano mkubwa kati ya Katiba bora ya Nchi, Demokrasia na Maendeleo ya Jamii.

  Mwanaharakati Na Mtetezi wa HAKI za Binadamu ndugu Deus Kibamba alipata kuwaelezea washiriki wa mafunzo hayo historia ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba, Ushiriki wa wananchi katika mchakato wa Katiba, hatua muhimu katika Mchakato wa utengenezaji Katiba, Mambo ya Msingi yaliyomo katika Katiba inayopendekezwa na Mambo muhimu kuelekea kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa.
  Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba akitoa elimu kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba pamoja na historia ya mchakato huo kwa vijana wa wilaya ya Chamwino mkoani  Dodoma.
  Afisa wa IRI, Tony Alfred akizungumza jambo wakakati wa mafunzo ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba kwa vijana wa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
  Makamu mwenyekiti wa TYVA, Kamala Dickson akizungumza jambo kwenye mkutano huo.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza na Mameneja wa Shirika ambao wapo katika mafuzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi ya NHC yanayotarajiwa kuchukua miaka mitatu yenye lengo la kuboresha utendaji na utekelezaji wa malengo ya Shirika kwa ufanisi unaopaswa.
  Mshauri Mwelekezi wa Mafunzo ya Rasilimaliwatu, Zuhura Sinare Muro akizungumza na Mameneja wa Shirika ambao wapo katika mafuzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi ya NHC yanayotarajiwa kuchukua miaka mitatu yenye lengo la kuboresha utendaji na utekelezaji wa malengo ya Shirika kwa ufanisi unaopaswa.

  Baadhi ya Mameneja wa Shirika la Nyumba la Taifa ambao wapo katika mafuzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi ya NHC yanayotarajiwa kuchukua miaka mitatu yenye lengo la kuboresha utendaji na utekelezaji wa malengo ya Shirika kwa ufanisi unaopaswa.
  Picha ya pamoja ya Mameneja wa Shirika ambao wapo katika mafuzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi ya NHC yanayotarajiwa kuchukua miaka mitatu yenye lengo la kuboresha utendaji na utekelezaji wa malengo ya Shirika kwa ufanisi unaopaswa.


  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Afisa Mradi, Kitengo cha Kujenga Uwezo kutoka shirika lisilo la Kiserikali la  ‘The Foundation For Civil Society’ Nasim Losai, akitoa mada wakati wa ufungaji wa Tamasha la Tano la Watu wenye Ulemavu lililoanza jana Nov 16, 2016 kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo limefungwa hii leo hayo. 
   Mkufunzi Mwelekezi, Salma Maoulid, akisimamia zoezi la maswali na majibu wakati wa kufunga Tamasha la Tano la Watu wenye Ulemavu lililoanza jana kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
   Afisa Uchumi Mwandamizi, Mchambuzi na Mipango, Andrea Aloyce, akitoa mada kwa washiriki wakati wa kufunga Tamasha la Tano la Watu wenye Ulemabu lililoanza jana Nov 16, 2016 kwenye Hoteli ya Blue Pearl – Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Governance & Economic Policy Centre, Moses Kulaba, akitoa mada kwa washiriki wakati wa kufunga Tamasha la Tano la Watu wenye Ulemabu lililoanza jana Nov 16, 2016 kwenye Hoteli ya Blue Pearl – Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. 
   Mkarimani akiwatafsiria walemavu Viziwi kila kilichokuwa kikizungumzwa ukumbini hapo.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Sisi tunaamini kabisa kwamba:
  TANZANIA IS MORE THAN A WILDLIFE SAFARI COUNTRY. 
  Sisi tunataka Dar es salaam isiwe tu Transit ama njia panda ya kuelekea maeneo mengine. Tunataka watalii wabaki hapa DAR watudondoshee vidola vyao na sisi tuvipate hapa. Visiishie  kwenye mbugani  tu. Hivyo basi tumeanzisha libeneke linalojulikana kama katika jiji la Dar  au kwa Kimombo  "IN DAR ES SALAAM". Mambo yote tisa, kumi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) kupitia chapa yake ya ‘Valeur Superior Brandy’, kwa kushirikiana na kampuni ya Vuvuzela Company Ltd, wanatangaza rasmi fainali ya shindano la “Valeur Comedy Nights” msimu wa pili, ambalo ni shindano la kusaka vipaji vya sanaa ya uchekeshaji.

  Fainali hiyo inatarajiwa kufanyika Jumamosi tarehe 19 Novemba 2016, Katika ukumbi wa 40/40 Baa, Tabata ambapo kutakuwa na washiriki 18 waliopatikana kutoka katika fainali za wilaya za mkoa wa Dar es Salaam. Mashindano haya ni kusaka mshindi wa mkoa wa Dar es Salaam.

  Akizungumuza na waandishi wa Habari, Meneja wa Kanda wa Mauzo na Usambazaji wa Kampuni hiyo, Mwesige Mchuruza alisema, “Msimu wa pili wa “Valeur Comedy Nights” umeendelea kupokelewa vizuri na wateja wetu. Kutokana na kwamba huu ni msimu wa pili, wateja wanalifahamu vizuri shindano hili na tumeona wacheheshaji wengi wakijitokeza kushindana. Washirika wetu kutoka Kampuni ta Vuvuzela Company Ltd kwa mara nyingine tena wametoa msaada mkubwa kwani wamewapa washiriki mafunzo na kuwatayarisha kwa fainali hizi”.

  Mashindano hayo yalianza Septemba 6, 2016 yakijumuisha zoezi la kusajili watu kushiriki katika mashindano hayo.

  Mchuruza aliendelea kusema mshindi wa ‘Valeur Comedy Nights’ atapata pesa taslimu 2,000,000/= na mafunzo ya vitendo ya miezi 6 na Evans Bukuku katika kampuni yake ya Vuvuzela Company Ltd.
  Meneja Mauzo na Usambazaji Kinywaji cha Valeur kutoka Kampuni ya TDL, Mwesigwa Mchuruza akimkabidhi Hundi ya Shilingi Milioni Mbili Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vuvuzela, Evans Bukuku ikiwa zawadi ya mshindi wa kwanza kwa mshindi atakayepatikana katika fainali shindano la kuchekesha linayolotarajiwa kufanyika jumamosi Oktoba 19,2016 Katika Bar ya 40/40 iliyoko Tabata jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vuvuzela, Evans Bukuku(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa kutangaza zawadi za washindi katika fainali zinazotarajiwa kufanyika jumamosi Oktoba 19,2016 Katika Bar ya 40/40 iliyoko Tabata jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja Mauzo na Usambazaji Kinywaji cha Valeur kutoka Kampuni ya TDL, Mwesigwa Mchuruza.Kulia ni mshindi wa Mwaka jana, Hussein Athuman.

  0 0  0 0

   
   


  0 0


   Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  akimkabidhi zawadi mwanafunzi bora wa Chuo Kikuu Kishiriki cha  Elimu Dar es Salaam (Duce), Haji Mohamed wakati wa Mahafali ya Tisa ya chuo hicho leo. Jumla ya wanafunzi 1,179 walihitimu na kutunukiwa digrii za awali.
  Digrii walizotunukiwa ni Elimu ya Jamii na Ualimu (B.A.Ed.) wanafunzi 864, Elimu katika Elimu ya Jamii (B.E.D. Arts) wanafunzi 52, Elimu katika Sayansi (B.Ed. Science) wahitimu 73, Sayansi ya Ualimu (B.Sc.Ed.) wahitimu 190.

   Wahitimu wa digrii ya awali ya elimu ya jamii  na ualimu  wakati wa Mahafali ya Tisa ya chuo hicho jana  jioni. Jumla ya wanafunzi 864 walitunukiwa digrii hiyo.
   Mhitimu Bora wa Kike akipatiwa zawadi
   Warda Jumanne akipatiwa zawadi ya kuwa mmoja wa wanafunzi Bora wa Kike. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA  0 0

  Over the past two decades social media has become one of the most powerful sources of information. It facilitates free and seamless inter and cross-border communication and enables information to travel fast and wide. It also builds and destroys individuals and institutions, and promotes or demotes merchandise in a way never seen before.

  Facebook, Twitter, LinkedIn, Google and others are now the new media. While in the past people had to wait hours, sometimes days, to know what was happening around them, things have now dramatically changed. Citizen journalists, armed with no more than a smartphone, are able to break news to millions of people around the world in real time and keep stories alive with pictures and videos.This form of communication is a boon to users and consumers but is also a source of pain, anguish and disappointment for many.Fake news has permeated social media so much so that a new cliché has been born: ‘don’t believe anything you read on the internet’.
  Fiction disguised as news has saturated the social networks – distorting facts and spreading propaganda, innuendos and lies, sometimes with serious consequences in politics, government and business.

  Producers of fake news engage in mischief and spin information to please, hurt or damage reputations, or simply just to drive traffic. Fake newsmakers “sex” their stories to attract likes and spur social discourse, and photo-shop images to legitimize their stories.  For more CLICK HERE
  0 0

  Pilika pilika za Libeneke lako pendwa katika kuangazia maeneo mbalimbali ya mji mkuu Dodoma, ilifurahishwa na  uvaaji na uzingatiaji wa kofia ngumu yaani "Helmet" , ambapo madereva na abiria wengi wa vipando mbalimbali ikiwemo pikipiki na vyombo vinginevyo. Juu ni dereva sanjari na msaidizi wake wote wakiwa wamevaa kofia zao kujikinga kuepukana na kujipa tahadhari kabla ya Ajali
  Pichani ni Dereva wa  Bodaboda akiwa na abiria wake wakikatiza baadhi ya mitaa mjini Dodoma huku juu wakiwa wamevalia "Helmet" wote wawili kwenye kipando hicho.
  Bodaboda wa Dodoma safi sanaa kwa kuzingatia sheria ya uvaaji "Helment"
  Mambo safi Dodoma Mikoa mingine tuige hii kwa usalama wetu wenyewe.
  PICHA NA MR.PENGO  WA MMG

  0 0  Na Fredy Mgunda,Mafinga

  MASHINDANO ya Mpira wa miguu yaliyodhaminiwa na Mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa yanayojulikana kama Mgimwa Cup yamefika tamati katika tarafa ya Sadan yenye kata tatu ambazo Ikwea,Sadan na Igombavanu na fainali zote zilifanyika katika kata husika ambapo kila mshindi wa kata alipata ng’ombe mmoja na mshindi wa pili alipata mbuzi moja,hivyo jumla ya ng’ombe tatu na mbuzi tatu zimetolewa katika tarafa ya Sada.

  Katika fainali ya kwanza ilichezwa katika viwanja vya kijiji cha Ugenza iliyopo katika kata ya Ikwea ilishuhudiwa timu ya Ugenza FC wakiibamiza timu ya Ikwea FC kwa goli 1-0 katika mchezo wa vuta nikuvute.

  Baada ya mchezo huo katibu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa Hassani Mtenga alikabidhi zawadi mbalimbali kwa washiriki wa michuano hiyo ambapo mshindi wa tatu ambaye ilikuwa timu ya Victoria FC alizawadiwa mipira miwili, mshindi wa pili Ikwea FC walipata mbuzi mmoja na mpira mmoja na mshindi wa kwanza ambaye ni Ugenza FC walipata Ng’ombe mkubwa na mpira mmoja.

  Mtenga aliwaasa wachezaji kuithamini michezo kwa kuwa sasa ni ajira hivyo wanajukumu la kujituma na kuipa kipaumbe michezo na kuacha tabia za kukaa kwenye vijiwe na vilabu ambako wanapoteza muda kwa kujadili mambo yasiyo ya msingi.Akifunga mashindano hayo mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa aliwaomba vijana hao wajiunge katika vikundi ili waweze kupata fedha kwa ajili ya kuanzisha miradi ya maendeleo ambapo itawasaidia kukuza uchumi wao na wa Taifa.

  Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamood Mgimwa na katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoani iringa Hassan Mtenga wakifuatila mchezo wa fainali katika kata ya Ikwea ambapo mshindi alipata ng'ombe mmoja na mshindi wa pili akipokea zawdi ya mbuzi mmoja ambapo zawadi zote hizo zimetolewa na mbunge huyo. 
  katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoani iringa Hassan Mtenga akikabidhi ng'ombe kwa mshindi wa kwanza katika kata ya Ikwea ambapo mshindi wa kwanza ilikuwa timu ya Ugenza FC walipata Ng’ombe mkubwa na mpira mmoja.

  Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamood Mgimwa na katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoani iringa Hassan Mtenga walipomkabidhi zawadi mshindi wa pili Ikwea FC mbuzi mmoja na mpira mmoja.


  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi wa Uholanzi nchini, Jaap Frederiks (katikati) wakati Balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uholanzi. Kulia ni Eugene Gies ambaye ni Katibu wa Uchumi na Sera za Biashara wa Ubalozi huo nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya alipokuwa anamfafanulia jambo Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Abdulla Ibrahim Alsuwaidi (kulia) alipomtembelea Waziri Mwigulu ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akimsikiliza Balozi wa Uholanzi nchini, Jaap Frederiks alipokuwa anamfafanulia jambo Waziri huyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, walipokuwa wanajadiliana masuala mbalimbali ua ushirikiano kati ya Tanzania na Uholanzi. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya. Kulia ni Katibu wa Uchumi na Sera za Biashara wa Ubalozi huo nchini, Eugene Gies.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

older | 1 | .... | 1432 | 1433 | (Page 1434) | 1435 | 1436 | .... | 3286 | newer