Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1431 | 1432 | (Page 1433) | 1434 | 1435 | .... | 3284 | newer

  0 0
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Bibi. Maria  Sasabo( wa pili kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa watendaji wa kampuni ya Startimes Tanzania jinsi ya televisheni za kidijitali zinavyofanya kazi wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni hizo uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.

    Mkurugenzi Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. Leo Liao (kulia) akimueleza jambo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Bibi. Maria  Sasabo(kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni za kidigitali kutoka kampuni ya StarTimes Tanzania uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Bibi. Maria Sasabo akizungumza na wadau sekta ya Habari na Mawasiliano wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni ya kidigitali kutoka kampuni ya Startimes Tanzania uliofanyika Novemba 16, 2016 Jijini Dar es Salaam.
   Meneja Masoko na Mahusiano wa StarTimes Tanzania Bw. Juma Sharobaro akizungumza wakati wa kuchezesha bahati nasibu ya kumpata mshindi wa moja ya televisheni za kidigitali katika hafla ya uzinduzi wa televisheni hizo uliofanyika Novemba 16, 2016 Jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. Leo Liao(kushoto) akikabidhi zawadi ya moja ya televisheni za kidigitali yenye upana wa inchi 40 kwa mshindi wa televisheni hiyo Bw.John Paul  wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni hizo uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.


  0 0
  0 0
  0 0

  Tiba hii inaitwa JIKO. Kila mwanaume anae itumia, INAMPONYESHA KABISA tatizo la UKOSEFU na UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME. Imethibitishwa na MKEMIA MKUU WA SERIKALI YA TANZANIA

  Kufahamu jinsi tiba hii inavyo fanya kazi, bofya link hii hapa chini :


  Kwa mahitaji yako ya tiba hii, wasiliana na duka la NEEMA HERBALIST & NUTRITIONAL FOODS CLINIC kwa simu namba 0766 53 83 84.

  Tunapatikana UBUNGO jijini DAR ES SALAAM, jirani na SHULE YA MSINGI UBUNGO NATIONAL HOUSING nyuma ya jengo la UBUNGO PLAZA. · Kwa wateja waliopo DAR ES SALAAM, wasio na nafasi ya kufika ofisini kwetu, watapelekewa dawa mahali walipo ( HOME & OFFICE DELIVERY ).

  · Kwa wateja waliopo mikoani, watatumiwa dawa kwa njia ya mabasi mbalimbali.

  · Kwa wateja waliopo Zanzibar, watatumiwa dawa kwa njia ya usafiri wa boti.

  · Kwa wateja wa Mombasa, watatumiwa dawa kwa basi la TAHMEED COACH.

  · Kwa wateja wa NAIROBI watatumiwa dawa kwa basi la DAR EXPRESS.

  · Na kwa wateja wa UGHAIBUNI ( DIASPORA), watatumiwa dawa kwa njia ya POSTA au DHL.

  · Kwa taarifa zaidi kuhusu huduma zetu, tembelea kila siku website yetu www.neemaherbalist.com


  0 0

  *Ni matokeo ya kikao kati ya balozi Mgaza na Mkurugenzi Mkuu Saudi Arabian Airline
  *Vivutio vingi vya utalii nchini Tanzania vyatajwa kwenye kikao hicho cha aina yake

  Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Balozi Hemedi Mgaza kulia, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines, Mh Saleh Bin Nasser Al Jasser, katika kikao chao maalum cha kujadili namna ya ndege za shirika hilo kuanza safari za kutoka Saudi Arabia hadi nchini Tanzania. Picha zote kwa Hisani ya Ofisi ya Balozi wa Tanzania Saudi Arabia.

  Na Mwandishi Wetu, Saudi Arabia

  WATALII, wafanyabiashara, mahujaji wa Watanzania pamoja na watu kutoka nchi za Kiarabu hususan Saudi Arabia, huenda wakapata fursa ya kuwasili Tanzania kwa urahisi endapo mchakato Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines wa kutoa ndege za kutoka Saudi Arabia hadi nchini Tanzania utakapofanikiwa kama ulivyoanza kushughulikiwa.
  Mapema wiki hii Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Balozi Hemedi Mgaza alifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines, Mhe.  Saleh Bin Nasser Al Jasser, ambapo shughuli mbalimbali za utalii na vivutio vya Tanzania vilijadiliwa, kama njia ya kuangalia namna bora ya ndege hizo kufanya safari zake vizuri kwa kuzingatia mkataba wa ushirikiano wa mambo ya anga baina ya Tanzania na Saudi Arabia Bilateral Air Service Agreement (BASA).

  Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Balozi Hemedi Mgaza kulia akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines, Mh Saleh Bin Nasser Al Jasser kushoto.
  Kikao kinaendelea kati ya balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Balozi Hemedi Mgaza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines, Mh Saleh Bin Nasser Al Jasser kushoto.
  Akizungumza katika kikao hicho, Balozi Mgaza alisema kuwa Tanzania ni nchi yenye vivutio vingi vya Utalii kama mbuga nzuri za wanyama pamoja na Mlima wa Kilimanjaro ambao ni alama bora za utalii nchini humo inayochochea wageni wengi kuingia na kutoka katika nchi hiyo yenye amani na upendo.

  Alisema endapo kutakuwa na ndege za moja kwa moja kutoka Saudi Arabia hadi nchini Tanzania, Shirika linaweza kutoa huduma bora bora kwa kupitia sekta ya utalii pamoja na ile ya mahujaji.
  “Unapozungumzia sekta ya utalii, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuna vivutio vingi vinavyosisimua, hivyo naamini kuna kila sababu ya Shirika hili la Ndege kuangalia jinsi ya kuanzisha safari za moja kwa moja.
  “Nchi yetu imepiga hatua katika sekta mbalimbali na viwanja bora vya ndege vipo katika hali nzuri, huku tukiamini kuwa endapo wazo hili litafanikiwa nchi yetu Tanzania itapiga hatua kubwa kwa sababu watu wengi watahamasika kufika kutalii bila kusahau watakaotaka kuwekeza kwenye mbio za serikali za kuifanya nchi yetu kuwa nchi ya viwanda,” Alisema Balozi Mgaza.
  Kwa sasa mashirika makubwa yanafanya safari zake kama vile Emirates, Oman Air, Etihad Airways, Fly Dubai, Qatar Airways, Egypt Air na Turkish Airlines jambo linalochochea kiu kubwa kwa abiria wa Saudi Arabia na Tanzania wanaopenda kuingia na kutoka kwenye nchi hizi mbili.


  0 0

  Maafisa wa idara ya wanyapori wakiangalia mmoja wa mizoga iliyokufa kutokana na ugonjwa wa Kimeta katika Shoroba ya Selela wilayani Monduli mkoa wa Arusha.

  Daktari wa Mifugo wa halmashauri ya wilaya ya Monduli,Yandu Marmo akimkagua mnyama aliyekufa kwa ugonjwa wa Kimeta.  Ndege wakiwa wamejikusanya kula mizoga iliyokufa kwa ugonjwa wa Kimeta.


  Maafisa wa Shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa) na Idara ya Wanyamapori wakiwa kwenye Shoroba ya Selela kudhibiti ugonjwa wa Kimeta,katikati ni Meneja Uhusiano wa Tanapa,Pascal Shelutete na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara,Noelia Myonga kulia kwake wajidaliana jambo.

  Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara,Noelia Myonga(kushoto) akizungumza wakati wa kupanga mikakati ya kudhibiti ugonjwa wa Kimeta ambao unahusisha watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Idara ya wanyamapori.

  0 0

  WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa, amezindua kituo cha udhibiti na usimamizi wa mifumo ya usambazaji umeme katika jiji la Dar  es salaam kilichoko Mikocheni jijini Dar es Salaam, leo Novemba 16, 2016.
  Kituo hicho kipya na cha kisasa, kimejengwa kwa ufadhili wa serikali ya Norway na Tanzania, chini ya mpango wa Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Umeme jijini.
  “Serikali ya awamu ya Tano, iliwaahidi Watanzania, wakati tukiomba kura, ya kwamba, tutaboresha huduma ya umeme kote nchini, na leo hii ni ushahidi tosha tunatekeleza kwa vitendo ahadi zetu.” Alisema Waziri Mkuu ambaye alimwakilisha Rais wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli.
  Akimkaribisha waziri Mkuu, Waziri wa Nishati na Madini, Mh. Profesa Sospeter Muhongo amesema, watanzania wanahitaji umeme tena ulio bora, na sasa kituo hicho ni jawabu la kuwapatia umeme ulio bora.

  “Kati ya vitu ambavyo sitarajii kuvisikia ni mgao wa umeme, lakini pia bei ya umeme, kuusu bei tutakaa, pembeni na watu wa TANESCO kulizungumzia hili. “ Alitoa hakikisho Waziri Muhongo.Kwa upande wake, Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Mh. Kai Mykkanen, alisema, teknolojia iliyotumika kwenye mitambo ya kituo hicho ni ya kisasa ijulikanayo kama Distribution SCADA System, na inauwezo wa kutambua hitilafu ya umeme kwa haraka na hivyo kurahisisha kurekebisha hitilafu hiyo kwa wakati.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, (katikati) na viongozi wengine kutoka kushoto, Mwenyekiti wa bodi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Palangyo,Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, (Waziri Mkuu), Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba, wakishangilia baada ya kukata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa kituo cha cha udhibiti na usimamizi wa mifumo ya usambazaji umeme katika jiji la Dar  es salaam kilichoko Mikocheni jijini Dar es Salaam, leo Novemba 16, 2016

   Waziri Mkuu na wageni wengine wakitembelea chumba cha mitambo yaudhibiti nausimamizi wa mifumo ya usambazaji umeme Distribution SCADA System
   Waziri Mkuu akitembeela moja ya mitambo inayopatikana kwenye kituo chicho (Server)
   Mtaalam wa mitambo, wa shirika la Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), Bi, Mwajua Turkey, kushoto, akimpatia maelezo waziri mkuu wakati akitembelea kituo hicho muda mfupi kabla ya kukizindua rasmi


  0 0

  Na Genofeva Matemu – WHUSM

  Wazalishaji wa kazi za filamu nchini wametakiwa kuzalisha kazi zenye ubora na viwango vinavyotakiwa ili Tanzania iweze kupambana na mataifa mengine katika sekta ya filamu.

  Rai hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo wakati wa ziara iliyofanywa na Bodi ya Filamu pamoja na makampuni mbalimbali ya watayarishaji Jana Jijini Dar es Salaam katika Studio ya Wanene Entertainment.

  “Ili kuleta maendeleo chana ndani ya Sekta ya Filamu hatuna budi kuwa mabalozi wa tasnia hii kwa kuboresha ubora wa filamu zetu na kuweza kuliteka soko la ndani na nje ya nchi” alisema Bibi. Fissoo.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Wanene Entartainment Bw. Darsh Pandit amesema kuwa kampuni ya Wanene imekubali kushirikiana na watayarishaji wa filamu za ndani ili kutoa filamu zenye ubora ambazo zitaleta mapinduzi kwenye tasnia ya filamu nchini.

  Kwa upande wao watayarishaji wa ndani wa kazi za filamu wameliomba Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kuanzisha kitengo maalum cha kutafsiri filamu za kitanzania ili ziwe na tafsiri inayoendana na kazi husika.

  Wazalishaji wa filamu kutoka makampuni mbalimbali hapa nchini wametembelea studio hiyo ili kuweza kuangalia uwezekano wa kushirikiana katika kuzalisha filamu zenye ubora kupanua wigo wa tasnia ya filamu hapa nchini.

  Baadhi ya Watayarishaji waliofanya ziara hiyo katika Studio za Wanene Entertainment ni pamoja na kampuni za Inspiration Image, Cut2cut Entertainment, 5 Effects, Steps na UWAFIMU.
  Watayarishaji wa filamu kutoka makampuni mbalimbali wakiangalia moja ya kifaa kinachotumika kuandaa filamu katika Studio za Wanene Entertainment walipotembelea studio hizo katika kuboresha ubora wa filamu nchini Jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto waliokaa ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo akijaribu kupiga ngoma zinazotumika kuandaa kazi za muziki na filamu katika Studio ya Wanene Entertainment wakati wa ziara iliyofanywa na watayarishaji wa kazi za filamu kuboresha ubora wa filamu nchini Jana Jijini Dar es Salaam.
  Watayarishaji wa filamu kutoka makampuni mbalimbali wakiangalia moja ya chumba kinachotumika kuandaa filamu katika Studio za Wanene Entertainment walipotembelea studio hizo katika kuboresha ubora wa filamu nchini Jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
  Watayarishaji wa filamu kutoka makampuni mbalimbali, watendaji kutoka Bodi ya Filamu pamoja na watayarishaji kutoka Studio ya Wanene Entertainment katika picha ya pamoja wakati wa ziara iliyofanywa na watayarishaji hao katika Studio za Wanene Entertainment kuboresha ubora wa filamu nchini Jana Jijini Dar es Salaam.

  0 0

  *Ni matokeo ya kikao kati ya balozi Mgaza na Mkurugenzi Mkuu Saudi Arabian Airline
  *Vivutio vingi vya utalii nchini Tanzania vyatajwa kwenye kikao hicho cha aina yake

  Akizungumza katika kikao hicho, Balozi Mgaza alisema kuwa Tanzania ni nchi yenye vivutio vingi vya Utalii kama mbuga nzuri za wanyama pamoja na Mlima wa Kilimanjaro ambao ni alama bora za utalii nchini humo inayochochea wageni wengi kuingia na kutoka katika nchi hiyo yenye amani na upendo.

  Alisema endapo kutakuwa na ndege za moja kwa moja kutoka Saudi Arabia hadi nchini Tanzania, Shirika linaweza kutoa huduma bora bora kwa kupitia sekta ya utalii pamoja na ile ya mahujaji.


  “Unapozungumzia sekta ya utalii, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuna vivutio vingi vinavyosisimua, hivyo naamini kuna kila sababu ya Shirika hili la Ndege kuangalia jinsi ya kuanzisha safari za moja kwa moja.


  “Nchi yetu imepiga hatua katika sekta mbalimbali na viwanja bora vya ndege vipo katika hali nzuri, huku tukiamini kuwa endapo wazo hili litafanikiwa nchi yetu Tanzania itapiga hatua kubwa kwa sababu watu wengi watahamasika kufika kutalii bila kusahau watakaotaka kuwekeza kwenye mbio za serikali za kuifanya nchi yetu kuwa nchi ya viwanda,” Alisema Balozi Mgaza.


  Kwa sasa mashirika makubwa yanafanya safari zake kama vile Emirates, Oman Air, Etihad Airways, Fly Dubai, Qatar Airways, Egypt Air na Turkish Airlines jambo linalochochea kiu kubwa kwa abiria wa Saudi Arabia na Tanzania wanaopenda kuingia na kutoka kwenye nchi hizi mbili.

  Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Balozi Hemedi Mgaza kulia, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines, Mh Saleh Bin Nasser Al Jasser, katika kikao chao maalum cha kujadili namna ya ndege za shirika hilo kuanza safari za kutoka Saudi Arabia hadi nchini Tanzania. Picha zote kwa Hisani ya Ofisi ya Balozi wa Tanzania Saudi Arabia.

  Na Mwandishi Wetu, Saudi Arabia.


  WATALII, wafanyabiashara, mahujaji wa Watanzania pamoja na watu kutoka nchi za Kiarabu hususan Saudi Arabia, huenda wakapata fursa ya kuwasili Tanzania kwa urahisi endapo mchakato Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines wa kutoa ndege za kutoka Saudi Arabia hadi nchini Tanzania utakapofanikiwa kama ulivyoanza kushughulikiwa.


  Mapema wiki hii Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Balozi Hemedi Mgaza alifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines, Mh Saleh Bin Nasser Al Jasser, ambapo shughuli mbalimbali za utalii na vivutio vya Tanzania vilijadiliwa, kama njia ya kuangalia namna bora ya ndege hizo kufanya safari zake vizuri kwa kuzingatia mkataba wa ushirikiano wa mambo ya anga baina ya Tanzania na Saudi Arabia Bilateral Air Service Agreement (BASA).

  Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Balozi Hemedi Mgaza kulia akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines, Mh Saleh Bin Nasser Al Jasser kushoto.
  Kikao kinaendelea kati ya balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Balozi Hemedi Mgaza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines, Mh Saleh Bin Nasser Al Jasser kushoto.

  0 0


  Ni miaka minne toka tumpoteze baba yetu mpendwa Mhe. Jackson Mvangilwa Makwetta, Leo tunakukumbuka ukiwa Baba kwa kutufundisha mengi yaliyo Mema Duniani.
  Pia ulikuwa ni kiongozi wa muda mrefu katika nchi yetu na ulie
  pendwa na wengi kutokana na Uwazi, Ukweli,Uwajibikaji, hekima juhudi katika kazi ukiwa katika wizara tofauti ulizohudumu ikiwamo Elimu, kilimo,Nishati na Madini,Mawasiliano,Ulinzi na Utumishi.
  Watoto wako na watanzania bado tunadhamini mchango wako na tutakukumbuka daima.
  Upumzike kwa Amani

  0 0

  Unapo wadia mwisho wa mwaka wizi kupitia mtandao umekua ukishika kasi zaidi – Mataifa mengi duniani yamekua yakikumbwa na wimbi kubwa la uhalifu mtandao unao ambatana na upoteaji wa pesa. Itakumbukwa mwaka jana kuelekea mwisho wa mwaka ndio kirusi kipya aina ya ModPOS kilionekana kwa mara ya kwanza na kilifanikiwa kudhuru maeneo mengi na kusababisha kiasi kikubwa cha fedha kupotelea mikononi mwa wahalifu.

  Mwezi huu wa kuminamoja pekee tayari kumekua na matukio mengi yenye mlengo wa kuwapatia pesa wahalifu mtandao. Kwa sasa Uhalifu mtandao kpitia kirusi cha RANSOMWARE kinachoendelea kushikakasi wamefanikiwa kupata mamilioni ya fedha. Kirusi hiki kinapelekea mhalifu mtandao kumfungia uwezo mmiliki halali kutumia kifaa chake akimtaka alipe kiasi cha pesa ili kurudishiwa huduma. Uhalifu huu umepiga hodi Barani Afrika na hadi sasa wengi wameendelea kua waathirika.

  Mifumo ya hospitali, mashule na watu binafsi ni miongoni mwa waathirika wa kubwa wa uhalifu huu ambapo kila mfumo ulio fungiwa na kirusi cha Ransomware ili kufunguliwa kiasi cha dola Miatatu (300) na zaidi kimekua kiki hitajika. Kupitia matukio yaliyo ripotiwa duniani kote, takwimu halisi ya pesa zilizo ingia mikononi mwa wahalifu mtandao kwa mwezi huu wa kuminamoja pekee kutokana na Ransomware bado haija patikana ingawa ina kadiriwa kuzidi dola milioni 829.

  Aidha, Mabenki nayo hayako salama – Idadi ya Mabenki yaliyo vamiwa kimtandao imeendelea kukua zaidi kuanzia mapema mwezi huu huku hali hii ikitegemewa kuendelea zaidi maeneo mengi. Tukio kubwa zaidi kwa sasa ni kutokea uingereza ambapo hadi sasa benki ya Tesco baada ya kushambuliwa kimtandao zaidi ya Paundi milioni mbili zimeweza kupotelea mikononi mwa wahalifu mtandao na benki hiyo imelazimika kuwalipa wateja wake.


  0 0

  Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) akimkabidhi zawadi mwanafunzi bora wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (Duce), Haji Mohamed wakati wa Mahafali ya Tisa ya chuo hicho, jijini Dar es salaam. Jumla ya wanafunzi 1,179 walihitimu na kulamba nondozz zao za awali. 

  Nondozz (Digrii) walizolamba ni  Elimu ya Jamii na Ualimu (B.A.Ed.) wanafunzi 864, Elimu katika Elimu ya Jamii (B.E.D. Arts) wanafunzi 52, Elimu katika Sayansi (B.Ed. Science) wahitimu 73, Sayansi ya Ualimu (B.Sc.Ed.) wahitimu 190.(PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG). 
  Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete (hayupo pichani) akiwatunuku Nondozz (digrii) ya awali ya elimu ya jamii na ualimu wakati wa Mahafali ya Tisa ya chuo hicho jana jioni. Jumla ya wanafunzi 1,179 walihitimu na kulamba nondozz zao za awali.  

  Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandara akifurahi wakati wimbo wa kabila la wahaya wa Akanana Kalile Kona ukipigwa wakati wa mahafali hayo 
  Ni muziki kwa kwenda mbele.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI 

  0 0

  Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw. Joel Laurent (mweyesuti) alipotembelea chuo hicho kuangalia misaada ya vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano walivyovitoa chuoni hapo ikiwemo Ubao maalum za kufundishia (Smart Board) 4,Projecta 4 na Komputa 22, wa mwisho kulia ni Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Sylvia Lupembe.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw. Joel Laurent mwenye suti akiongea na Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda(mwenye shati jeupe) ambapo alishauri kusimamia matumizi sahihi ya vifaa hivyo vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano vinatumika kwa manufaa ili kuleta matokeo yenye tija, Makamu Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Dkt. Tumaini Katunzi na Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Sylvia Lupembe.
  Makamu Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Dkt. Tumaini Katunzi na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw. Joel Laurent wakifuatilia maelekezo ya namna ubao maalum wa smart board unavyofanya kazi wakati wa kufundishia ikiwa ni moja ya msaada uliotolewa na mamlaka ya elimu.


  0 0

  Wasanii wa kikundi cha sanaa cha Bagamoyo African Culture wakionyesha uhamiri wao wakati wa sherehe ya Kendwa Rocks Full Moon iliyofanyika mjini Zanzibar hivi karibunii. Full Moon Party hudhaminiwa na Zantel na hujumuisha watanzania na watalii kutoka nchi mbali mbali duniani.
  Wasanii wa kikundi cha sanaa cha Bagamoyo African Culture wakitumbuiza wakati wa sherehe ya Kendwa Rocks Full Moon iliyofanyika mjini Zanzibar hivi karibunii. Full Moon Party hudhaminiwa na Zantel na hujumuisha watanzania na watalii kutoka nchi mbali mbali duniani.
  Wasanii wa Karafuu Band wakitoa burudani wakati wa sherehe ya Kendwa Rocks Full Moon iliyofanyika mjini Zanzibar hivi karibunii. Full Moon Party hudhaminiwa na Zantel na hujumuisha watanzania na watalii kutoka nchi mbali mbali duniani. 
  Maofisa mauzo wa Zantel Tanzania wakijiandaa kutoa huduma katika sherehe ya Kendwa Rocks Full Moon inayofanyika kila mwezi wakati wa mbalamwezi kamili mjini Zanzibar. 

  0 0

  Na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

  Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji, Charle’s Mwijage  amefanya ziara kutembelea viwanda vilivyopo Mkoa wa Pwani na kuangalia maendeleo ya mkoa huo katika sekta ya viwanda.Katika ziara hiyo Waziri Mwijage alipotembelea kiwanda cha Viuadudu cha kibaha, Sayona Fruits, Global Packaging kiwanda cha kuunganisha matrekta pamoja na kiwanda cha Eveline.

  Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara hiyo, Mwijage  amesema ujenzi wa viwanda katika mkoa wa Pwani unakua kwa kasi na kuonngeza ajira kwa watanzania.

  Amesema kitendo cha mmiliki  wa kiwanda cha Sayona kuwapa  wanakikjiji  fursa ya kupata elimu mpaka ngazi ya chuo kikuu na kisha kuajiliwa katika kiwanda hicho ni uungwana ambao watafanya kazi ya kufundisha wafanyakazi wenzao.

  “Wafanyakazi wa Sayona kupatiwa fursa ya kwenda chuo kikuu kujifunza ili kuja kuwafundisha wenzao, kasi hiyo imenifurahisha sana” amesema Waziri Mwijage.
   Waziri  wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo mara baada ya kuwasili mkoani pwani kwaajili ya ziara ya siku moja.
   .Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s akizungumza na meneimenti ya kiwanda cha viua vidudu kilichopo kibaha, mkoani Pwani Kulia ni Kaimu Meneja Mkuu wa Kiwada hicho,Samwel Mziray mkoani Pwani. 

   Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akipata maelezo kwa Kaimu Meneja Mkuu wa Kiwanda Viua Vidudu hicho,Samwel Mziray katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama. 
   Waziri  wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha viua vidudu, Kibaha.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Walter Mguluchuma wa Katavi yetu Blog

  Hifadhi ya Taifa ya Katavi inapatikana kusini Magharibi mwa Tanzania karibu na Ziwa Tanganyika katika Wilaya za Mpanda ,Tanganyika na Mlele Mkoa wa Katavi inapatikana katika latitude 6.63.7.34 kusini na na longitude 3.74.31.84 Mashariki.

  Hifadhi hii ilitangazwa kuwa Hifadhi ya Taifa mwaka 1974 ikiwa na ukubwa wa kilometa za mraba 2253 iliongezwa ukubwa mwaka 1996 na kufikia ukubwa wa kilometa za mraba 4471 na kuifanya kuwa Hifadhi ya tatu kwa ukubwa Tanzania baada ya Ruaha na Serengeti .

  Ilipata jina lake kutokana na mzimu wa kabila la Wabende aliyejulikana kwa jina la Katabi ambapo mpaka leo watu mbalimbali wamekuwa wakifika ndani ya Hifadhi ya Katavi na kwenda kwenye mti ulioko kwenye Ziwa Katavi wakiamini kuwa mzimu Katabi alikuwa akiishi hapo zamani kabla ya kuwepo Hifadhi ya Taifa ya Katavi .

  Jina la Hifadhi hii lilijulikana kama Katabi kutokana na imani ya jamii hizo kwa mzimu Katabi inaaminika kwamba mzimu Katabi una uwezo wa kufanya miujiza ikiwemo kufanya mvua inyeshe , kuzuia magonjwa ya mlipuko kama vile ndui na kutatua shida za watu mbalimbali .
  Hawa ni Punda milia wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi
  Kama kibao kinavyo onekana hili ni Eneo la Tambiko ambapo watu huja kusali na kutoa sadaka mbalimbali 
  Simba akiwa na mzoga wa Kiboko 
  Twiga akiwa katika hifadhi ya Taifa ya Katavi.


  0 0


  Na Woinde Shizza,Arusha

  WANANCHI kutoka kata ya Engutoto jijini hapa,wanatarajiwa kutimiza ndoto zao za muda mrefu juu ya ukosefu wa viwanja baada ya mfadhili kujitokeza kuwajengea.

  Mfadhili huyo Hans Paul kupitia kampuni ya Dharam Singh Hanspaul & Son ltd alisema hayo mbele ya mkuu wa mkoa Arusha kuwa katika kutimiza adhma ya serikali kusaidia maendeleo ya michezo kwa vijana amejitolea kujenga viwanja viwili vya michezo.

  “Viwanja tutakavyojenga ni kwa mpira wa miguu na mpira wa Netiboli na vinatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 30 fedha za kitanzania na tunatarajia kuanza ujenzi huo ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2017,”Alisema Paul.

  Alisema kuwa lengo kuu la kujenga viwanja ni katika kuwawezesha vijana wapate muda wa kujihusiha na michezo ili kuepukana na tabia hatarishi ambazo zingeharibu ndoto za maisha yao.

  Baahi ya wakazi wa kata hiyo wakizungumzia neema watakayoipata kutoka kwa mfadhili huyo walisema “Ni jambo la kupongeza kwani vijana wengi wamekuwa hawana mahali pa kufanya mazoezi na kwa hali hii itasidia sasa kuanza kuona vipaji vya michezo katika kata hii.” Alisema mmoja wa wakazi hao.

  Kwa upande wake mkuu wa mkoa Arusha Mrisho Gambo alisema juhudi alizozifanya mfadhili huyo katika sekta ya michezo ni jambo la heri ambalo linatakiwa liwe mfano kwa wadau wengine katika kusaidia kuinua michezio katika jamii sambamba na kuwa michezo ni moja ya ajira kwa Vijana .

  Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(kwanza kulia) akizungumza na wadau wa maendeleo Bw. Hans Paul(pili kulia) ambaye amehaidi kujenga viwanja vya michezo ndani ya kata ya Engutoto na Bw. Jagjit Aggarwal 

  0 0

  Na Dotto Mwaibale

  WAZIRI wa Fedha Dk. Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yatakayofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)

  Maadhimisho hayo yatafanyika kesho kuanzia saa tatu asubuhi ambapo wadau mbalimbali wa masuala ya takwimu na wananchi watahudhuria.

  Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Meneja wa Idara ya Pato la Taifa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Daniel Masolwa alisema maadhimisho hayo ni muhimu sana na kuwa kauli mbiu yake ya mwaka huu ni " Kuimarisha Takwimu za Kiuchumi kwa Mtangamano wa Kikanda, Mabadiliko ya Miundo na Maendeleo Endelevu"

  Masolwa alisema lengo kuu la  kuadhimisha siku hiyo ni kuongeza uelewa mpana kwa watumiaji wote wa Takwimu Afrika kuhusu umuhimu wa takwimu katika kupanga mipango ya maendeleo katika sekta zote za kijamii na kiuchumi katika Bara la Afrika.

  Aidha alisema ni siku ambayo hutoa fursa kwa nchi kutathmini na kufuatilia malengo yaliyofikiwa katika Mipango ya Maendeleo ya ndani na nje ya Nchi.

  Alisema Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika huwa yanaandaliwa na kauli mbiu mbalimbali kila mwaka zinahusiana na umuhimu wa takwimu katika kupanga maendeleo na kutunga sera katika Bara la Afrika.

  Masolwa alisema umuhimu wa kuboresha na kuimarisha takwimu za kiuchumi na zenye ubora kwa utangamano wa kikanda barani Afrika utasaidia kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kufanikisha malengo endelevu, Agenda 2063 ya Afrika na mipango ya kitaifa ya kukuza uchumi.
   Meneja wa Idara ya Pato la Taifa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Daniel Masolwa (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yatakayofanyika kesho Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM). Kulia ni Ofisa Habari wa Idara Habari Maelezo, Beatrice Lyimo.
  Mkutano na wanahabari ukiendelea.

  0 0

  Tovuti ya wapenda soka ya KANDANDA imeandaa mchakato wa kuwapa nafasi mashabiki wa Kandanda (Mpira wa Miguu) nchini kutengeneza Kikosi bora chao cha wachezaji wa kandanda kwa mwaka 2016. Hivyo wasomaji wetu mnakaribishwa kupendekeza kikosi hicho kwa kubofya link hiyo hapo chini.


  0 0

  Picha na – OMPR – ZNZ.
                               
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliitahadharisha Jamii  kuelewa kwamba maendeleo kwa wana Taaluma wa Fani ya Sayansi iwe Maskulini au vyuoni  yataendelea kuwa ndoto iwapo  hakutakuwa na mipango imara ya  kuimarisha miundombinu kwenye Majengo ya Maabara katika maeneo husika.

  Alisema Wazazi kwa kushirikiana na Kamati za Maskuli na vyuo kupitia usimamizi wa Wizara inayosimamia masuala ya Elimu bado wana jukumu la kuhakikisha vilio vya Wanafunzi kutokana na kukabiliwa na ukosefu wa Maabara kwenye Taasisi zao vinamalizika.

  Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda alitoa tahadhari hiyo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi pamoja na kulizindua rasmi Jengo la Maabara ya Skuli ya Sekondari ya Kitope iliyomo ndani ya Wilaya ya Kaskazini “B”.

  Jengo hilo aliloligharamia yeye pamoja na kupata msaada wa nguvu za ufadhili wa baadhi ya vifaa kutoka Ubalozi wa Jamuhuri ya Watu wa China na Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Tigo limegharimu jumla ya shilingi za Kitanzania Milioni 38,780,000/-.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikata utepe kuashiria kuzindua pamoja na kukabidhi Jengo la Maabara la Skuli ya Sekondari ya Kitope aliloligharamia yeye pamoja na ufadhili wa Ubalozi China Nchini Tanzania na Kampuni ya simu za mkononi yaTigo.
  Mwalimu wa Masomo ya Sayansi wa skuli ya Sekondari Kitope Mwalimu Ali Mohamed aliyeshika kifaa cha Maabara akimuelezea Balozi Seif  urahisi wa kazi yao ya ufundishaji kwa sasa baada ya kupata  Maabara yenye kukidhi kiwango kinachokubalika kwa skuli za Sekondari.
  Mwalimu Ali Mohamed akiendelea kutoa maelezo kwa Balozi Seif  jinsi wanafunzi wa masomo ya sayansi katika skuli yao walivyofarajika kutokana na kujengewa maabara iliyokamilika kwa kazi zao za vitendo.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1431 | 1432 | (Page 1433) | 1434 | 1435 | .... | 3284 | newer