Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

UJENZI WA GATI LA NYAMISATI KUANZA MWAKANI

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amewahakikishia wananchi wa Wilaya za Kibiti, Rufiji na Mafia kuwa ujenzi wa gati la kisasa katika eneo la Nyamisati utaanza wakati wowote baadaye mwakani na kukamilika ifikapo Machi 2018.

Akizungumza mara baada ya kukagua eneo litakapojengwa gati hilo katika pwani ya Nyamisati wilayani Kibiti Eng.Ngonyani amewataka viongozi na wananchi wa wilaya hizo kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki ambacho Serikali inatafuta ufumbuzi wa kudumu.

“Endeleeni kutunza mazingira ya eneo hili na kutunza mazingira ya bahari ili kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi katika eneo lenu, Serikali imejipanga kukabiliana na changamoto inayowakabili sasa hivyo toeni ushirikiano unaohitajika ili kuiwezesha Mamlaka ya Bandari nchini(TPA) kutekeleza ujenzi wa gati hili”. Amesisitiza Eng. Ngonyani.

Naye Mbunge wa Mafia Mhe. Mbaraka Dau amemhakikishia Naibu Waziri Ngonyani kuwa kukamilika kwa gati la kisasa katika pwani ya Nyamisati kutahuisha shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa Mafia na Mkoa wa pwani kwa ujumla.

“Kukamilika kwa gati hili kutavutia wasafirishaji wengine kuleta vyombo vya usafiri na hivyo kushusha gharama za usafiri kati ya Kibiti na Mafia ambapo sasa ni zaidi ya shilingi elfu kumi na tatu kwa safari”. Amesema Mhe. Dau.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ngonyani amekagua barabara ya Ikwiriri-Lindi, Nanyumbu –Masugulu-Mtambaswala na Mangaka -Tunduru na kumtaka Meneja wa Wakala wa barabara Mkoa wa Mtwara Eng.Dotto Chacha kuhakikisha barabara inakuwa salama wakati wote kwa kudhibiti madereva wanaoegesha magari barabarani isivyostahili.

Naibu Waziri Ngonyani yupo katika ziara ya kukagua Miundombinu ya barabara, Bandari na Mawasiliano katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng.Edwin Ngonyani (wa kwanza kushoto) akitoa maelekezo kwa kaimu Meneja wa Wakala wa barabara (TANROADS) Mkoa wa Mtwara Eng. Dotto Chacha alipokagua barabara ya Mangaka-Mtambaswala na Mangaka –Tunduru.
Kaimu Meneja wa Wakala wa barabara (TANROADS) Mkoa wa Mtwara Eng. Dotto Chacha akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng.Edwin Ngonyani (katikati) eneo la mzunguko wa Mangaka linalohitaji marekebisho katika barabara ya Mangaka –Mtambaswala na Mangaka –Tunduru ambao ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika.
Muonekano wa barabara ya Mangaka-Mtambaswala inayounganisha Tanzania na Msumbiji ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika barabara hii inatarajiwa kuchochea uchumi wa mkoa wa Mtwara.

WAJUMBE BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR WATEMBELEA BANDARI YA TANGA

$
0
0
Tanga, WAJUMBE 14 wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi Baraza la Uwakilishi la Zanzibar wamesema ujio wa Mradi wa Bomba la Mafuta Tanga litaongeza ajira kwa vijana wakiwemo Wanzanzibar waishio Tanga.


Wajumbe hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hamza Hassan Juma walitembelea bandari ya Tanga eneo la upakuzi wa shehena ya mizigo na eneo itakapojengwa bandari mpya ya Mwambani.

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, Hassan alisema Serikali ya Zanzibar imejipanga kuimarisha bandari zake ikiwemo ya Wete na Mkoani Kisiwani Pemba ikiwa ni maandalizi ya ujio wa Bomba la Mafuta.

Akizungumzia kilio cha wafanyabiashara na wasafiri wa Pemba na Tanga kwa kutumia usafiri wa baharini, Hassan alisema kero hiyo Serikali inaitambua na jitihada za kuwa na meli ya uhakika inafanywa.

Alisema kuna baadhi ya wafanyabiashara wa Pemba ambao walikuwa wakichukua bidhaa Tanga wamekatisha na baadhi yao mitaji kufa kutokana na kutokuwepo kwa usafiri wa uhakika wa baharini.

Awali akizungumza na wajumbe hao wa Baraza la Wawakilishi, Kaimu Meneja wa Badari Tanga, Henry Arika, alisema mchakato wa mradi wa bomba la mafuta unaenda kwa kasi na kuwataka wawekezaji kutoka Zanzibar kuja kuwekeza.

Alisema Tanga ziko fursa nyingi za uwekezaji na yako maeneo mengi hivyo kupitia ujio wa mradi wa Bomba la mafuta amewataka wawekezaji wa ndani kuchangamkia.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Henry Arika (katikati) akitoa maelezo kwa wajumbe 14 wa Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar walipotembelea bandari ya Tanga kujifunza
Afisa Mtekelezaji Mkuu Bandari ya Tanga, Donald Kaire, akitoa maelezo kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar walipofanya ziara bandari hiyo juzi. Katikati ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Henry Arika.

JUNDOKAN SO HONBU TANZANIA YAZIDI KUIMARIKA CHINI YA SENSEI RUMADHA FUNDI

$
0
0
Mtindo wa Karate wa Okinawa Goju Ryu shina la Jundokan So Honbu Tanzania linalo ongozwa na mkufunzi wake mwakilishi sensei Rumadha Fundi, kwa ushirikiano na uongozi wa dojo zote mbili, yaani Jamhuri na Zanaki  linazidi kuwa imara chini ya uongozi wa wakilishi wa matawi makuu mawili ya mtindo huo wa Goju Ryu.

Ingawa ni dojo au shule mbili, lakini zote zina lengo moja tu kulitumikia jamii ya wana Goju Ryu Karate. Sensei Rumadha, alipata fursa yakuwa na mazoezi na shule hizi mbili na pia kuafikiana na wanafunzi waandamizi wa shule hizo na kuleta mabadiliko katika mbinu za ufundishaji, ikiwa pamoja na kushirikiana kwa mazoezi ya pamoja mara kwa mara kati ya dojo hizo.
Jundokan Zanaki Dojo.

Mtindo huu wa Okinawa Giju Ryu, uliletwa hapa nchini na mwasisi wa mtindo huu, Sensei Nantambu Camara Bomani mwaka 1973, na  unaendelea kufundisha maadili, nidhamu  na mbinu  za kujilinda kama jinsi inavyo fundishwa kiasilia hivi sasa huko  Okinawa, Japan.

Sensei Rumadha pia, ameleza kujitolea kutoa mchango wake katika shule hizo, ikiwa na kuzitembelea mara moja kila mwaka na kuwa na semina ikiwemo kufanya majaribio au “Mitihani” ya mikanda ya ngazi za juu na vilevile mafunzo ya utafiti utumiaji kata au “Bunkai” kwa wanafunzi wa ngazi ya kati na  ya juu.

Sensei Rumadha alikaririwa akisema,  alipokelewa kwa ukarimu na unyenyekevu katika dojo zote mbili na wanafunzi waandamizi  na walimu pia. Senpai Yusuf Kimvuli, Senpai Abdul Waheed, Senpai Bilal, Senpai  Mwinyimvua, Sensei Maulid Pambwe, Sensei Mwagala chini ya Jamhuri dojo, pia kwa upande wa Zanaki Sensei Melkia, Sensei Rashid Almas, Senpai Seif, na uongozi wote wa Zanaki dojo akiwemo Mohammed Murudker.
Jundokan Jamhuri Dojo

Mipango ipo njiani kujadili na kupendekeza wanafunzi watakao fanya mitihani ya mikanda mieusi mwakani baada ya idhini ya Kancho Yoshihiro Miyazato toka makao makuu ya mtindo huo huko Naha, Okinawa.

Mara tu baada ya mkufunzi mkuu wa Jundokan Tanzania, Sensei Rumadha Fundi atakapo hudhuria Kongamano”Jundokan European Gasshuku 2017 ”  la kila mwaka mtindo wa Goju Ryu Jundokan So Honbu, utakao fanyika mjini Warsaw, Poland  mwezi July na kupata ushauri toka kwa viongozi watakao kuja toka Okinawa, Japan akiwemo mwenye kiti wa chama hicho  Kancho Yoshihiro Miyazato na washauri wake wakuu wa mbinu za juu wa Jundokan, Sensei  Tetsu Gima na Sensei Tsuneo Kinjo.

Tanzania ni moja ya nchi pekee katika Afrika mashariki yenye wana Karate wa mtindo wa Goju Ryu wenye uzoefu wa mafunzo ya Karate kwa miaka mingi.
Sensei Rumadha na masenpai Waheed kushoto na senpai Yusuf Kimvuli .
Uongozi wa Jundokan Jamhuri Dojo na bendera yao toka Naha, Okinawa , Japan .

ATCL YATAKIWA KUBADILISHA MENEJIMENTI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa muda wa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kufanya mabadiliko katika menejimenti ya Shirika hilo ili kuongeza ufanisi na kuboresha utendaji kazi.

Ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza katika mkutano wa Menejimenti pamoja na wafanyakazi wa Shirika hilo na kuwataka kutoa huduma bora ili kulifanya Shirika hilo kuwa miongoni mwa mashirika bora ya ndege barani Afrika.

“Nataka ndani ya mwezi mmoja uwe umeshafanya mabadiliko katika menejimenti, mabadiliko lazima yaanzie juu kwanza kwa watoa maamuzi na ishuke hadi kwa wafanyakazi wazembe na wasio waadilifu”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Menejimenti na Wafanyakazi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Waziri Mbarawa amepinga nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi wa Shirika hilo hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali ipo katika juhudi za kulifufua na kuliimarisha Shirika hilo.

Aidha Waziri Mbarawa ameitaka Idara ya Masoko ya shirika hilo kuzunguka katika taasisi zote zilizo chini ya Wizara yake na kuzishawishi kuweza kutumia huduma za usafiri wa anga wa ATCL.

“Serikali imekamilisha upande wake wa ununuzi wa ndege, sasa kazi inabaki kwenu, sitaki watu wa masoko kukaa ofisini”, amesema Prof. Mbarawa.

Ameongeza kuwa wafanyakazi wa ATC wanatakiwa kujipanga kutoa huduma iliyotukuka kwa wateja wake ili kuweza kuhimili ushindani uliopo katika mashirika ya ndege nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Eng. Ladislaus Matindi akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani), wakati Waziri huyo alipokutana na menejimenti ya shirika hilo pamoja na wafanyakazi wake jijini Dar es Salaam.

“Inabidi tofauti kubwa ionekane kati yenu na mashirika mengine, yeyote ambaye anaona hawezi kutoa huduma bora kwa mteja atafute sehemu nyingine kwani hapa hatufai ”, amesisitiza Waziri Mbarawa.

Profesa Mbarawa amelitaka shirika hilo kutumia mfumo wa kisasa wa kukata tiketi kwa njia ya simu na kompyuta ili kuwarahishia watumiaji wa shirika hilo kuweza kupata tiketi kwa haraka na urahisi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Eng. Ladislaus Matindi amemhakikishia Waziri Mbarawa kufanyia kazi maagizo aliyotoa na kuahidi kuboresha utendaji kazi wa shirika hilo kwa lengo la kuteka soko la ushindani wa usafiri wa anga nchini.

“Kwa sasa tumeanza vizuri na naamini uwezo wa kuzalisha faida zaidi tunao, tunaahidi kuboresha utendaji kazi ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya Serikali ya Awamu ya Tano”, amesema Eng. Matindi.
Wafanyakazi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani), alipozungumza na uongozi wa Shirika hilo na Wafanyakazi jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akimpongeza mmoja wa watoa huduma wa ndege za ATCL kwa utoaji wa huduma bora kwa wateja katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Waziri Mahiga akutana na Waziri wa Biashara za Kimataifa na Maendeleo wa Finland

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Waziri wa Biashara za Kimataifa na Maendeleo wa Finland, Mhe. Kai Mykkanen alipomtembelea kwa mazungumzo Wizarani Jijini Dar es Salaam. Wawili hao wamezungumzia masuala mbalimbali kuhusu masuala ya biashara, uwekezaji na maendeleo ya huduma za kijamii nchini. Mhe. Kai katika mazungumzo hayo ameahidi kupitia Wizara yake ataendelea kushirikiana na Tanzania katika kuongeza kasi ya ukuaji wa shughuli za maendeleo sambamba na kuendelea kushawishi sekta binafsi za Finland kuja kuwekeza nchini. 
Mhe. Waziri, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Waziri wa Biashara za Kimataifa na Maendeleo wa Finland Mhe. Kai Mykkanen 
Mazungumzo yakiendelea 
Mhe. Waziri, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimsikiliza Waziri wa Biashara za Kimataifa na Maendeleo wa Finland Mhe. Kai Mykkanen walipokutana kwa mazungumzo Wizarani Jijini Dar es Salaam 

Article 11

JIKO: TIBA YENYE NGUVU ZA AJABU!

$
0
0
Tiba hii inaitwa JIKO. Kila mwanaume anae itumia, INAMPONYESHA KABISA tatizo la UKOSEFU na UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME. Imethibitishwa na MKEMIA MKUU WA SERIKALI YA TANZANIA

Kufahamu jinsi tiba hii inavyo fanya kazi, bofya link hii hapa chini :


Kwa mahitaji yako ya tiba hii, wasiliana na duka la NEEMA HERBALIST & NUTRITIONAL FOODS CLINIC kwa simu namba 0766 53 83 84.

Tunapatikana UBUNGO jijini DAR ES SALAAM, jirani na SHULE YA MSINGI UBUNGO NATIONAL HOUSING nyuma ya jengo la UBUNGO PLAZA. · Kwa wateja waliopo DAR ES SALAAM, wasio na nafasi ya kufika ofisini kwetu, watapelekewa dawa mahali walipo ( HOME & OFFICE DELIVERY ).

· Kwa wateja waliopo mikoani, watatumiwa dawa kwa njia ya mabasi mbalimbali.

· Kwa wateja waliopo Zanzibar, watatumiwa dawa kwa njia ya usafiri wa boti.

· Kwa wateja wa Mombasa, watatumiwa dawa kwa basi la TAHMEED COACH.

· Kwa wateja wa NAIROBI watatumiwa dawa kwa basi la DAR EXPRESS.

· Na kwa wateja wa UGHAIBUNI ( DIASPORA), watatumiwa dawa kwa njia ya POSTA au DHL.

· Kwa taarifa zaidi kuhusu huduma zetu, tembelea kila siku website yetu www.neemaherbalist.com

Vyama vya Ushirika Vianzishe Viwanda Vidogovidogo

$
0
0
Vyama vya Ushirika vimetakiwa kushiriki katika kuanzisha viwanda vidogovidogo ambavyo vitawezesha uchakataji wa mazao ya wakulima, wavuvi na wafugaji, kuweka kwenye madaraja na kufungasha tayari kwa ajili ya mauzo.

Wito huo umetolewa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini Bw. Tito Haule katika Ufunguzi wa Kikao Kazi cha Warajis Wasaidizi Wa Vyama Vya Ushirika Wa Mikoa kilichofanyika leo mjini Dodoma Novemba 15, 2016.

“Sekta ya Ushirika ina mchango mkubwa katika kuwezesha kutimia kwa azma ya Serikali ya kukuza uchumi, hivyo kila mmoja wetu katika eneo lake tuweke msukumo katika vyama vya ushirika ili viweze kuwa sehemu ya utekelezaji wa azma hii ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuipeleka nchi yetu katika uchumi wa viwanda ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuongeza kasi ya kufikia lengo la Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025,” alisema Mrajis. 

Viwanda vinavyomaanishwa siyo lazima viwe viwanda vyenye kuhitaji mitambo mikubwa bali vinaweza kuanzishwa viwanda vidogovidogo ambavyo vitawezesha uchakataji wa mazao.

Bw. Haule akizungumzia kuhusu majukumu yatakayopewa kipaumbele na Tume ya Maendeleo ya Ushirika alisema ni kusimamia na kudhibiti badala ya kuwa wasuluhishi wa migogoro katika Vyama vya Ushirika.

“Sote tunafahamu kwamba kuna udhaifu mkubwa katika eneo la usimamizi na udhibiti wa vyama vya ushirika na hivyo kusababisha utii wa sheria kutozingatiwa katika uendeshaji wa shughuli za vyama vya ushirika. Hivyo, kipaumbele changu cha kwanza ni Usimamizi, cha pili ni Usimamizi na cha tatu ni Usimamizi”, alisema Bw. Haule.








HAPPY BDAY MH RC DR REHEMA NCHIMBI

$
0
0
  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh. Dr Rehema Nchimbi  akiwa kwenye chumba cha wazazi akiwapatia akina mama waliojifungua watoto zawadi mbali mbali.

Wanafamilia tunapenda kuungana na watanzania wote kumtakia heri ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa mama yetu mpendwa Dr Rehema Nchimbi, Mungu azidi kumlinda na kumtunza ili aendelee kutumika kwa faida ya Taifa letu.

 Pichani ndie mama mzazi wa mh  Dr Rehema Rehema Nchimbi Bibi Mwl Selina Daudi. Pongezi kwake kwa kutuletea kiongozi wa wote.

Mama DR Rehema Nchimbi akifurahia jambo na watoto wake.



Onyesho La sanaa za Ufundi lafana Sweden

$
0
0
Ni onyesho la sanaa za ufundi nchini Sweden lililoandaliwa na msanii kutoka Tanzania Kennedy Mmbando. Lengo la onyesho hilo ni kutangaza uzuri wa mazingira aa Tanzania pamoja na umuhimu wa kumlinda myama Tembo. Onyesho linaendelea mpaka December 14

Waziri Mahiga azungumza na Wadau wa Maendeleo kutoka nchi za Nordic na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Tanzania.

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akifafanua jambo kwenye Mkutano na Wadau wa Maendeleo kutoka nchi za Nordic uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Nchi za Nordic zinatoa mchango mkubwa katika shughuli mbalimbali za maendeleo nchini ikiwemo kilimo na miradi ya maji. Nordic inaundwa na Nchi tano ambazo ni Norway, Finland, Iceland,Sweden na Denmark. 
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Bw.Alvaro Rodrigues akizungumza wakati wa mkutano 
Mkutano ukiendelea 

Dkt Kalemani azindua mradi wa Umeme (kW 430) mkoani Njombe.

$
0
0
Na Teresia Mhagama.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amezindua mradi wa umeme wa Kilowati 430 unaotokana na maporomoko ya maji katika Kata ya Ikondo mkoani Njombe ambapo mpaka sasa zaidi ya wateja 1140 wameunganishiwa umeme huku zoezi hilo likiwa ni endelevu.


Uzinduzi huo uliofanyika katika Kata  hiyo ulihudhuriwa na Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU), Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa wilaya ya Njombe, wananchi wa Kata ya Ikondo, Shirika lililotekeleza mradi huo la CEFA, watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO).



Dkt. Kalemani alisema kuwa mradi huo umetekelezwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya CEFA  kutoka Italia     na kugharamiwa kwa pamoja kati ya Jumuiya ya Ulaya na Serikali ya Tanzania kwa jumla ya Dola za Marekani 110,209.



Aliongeza kuwa mradi huo wa umeme utasambazwa katika vijiji vilivyoko kata za Ikondo, Matembwe na Lupembe na ziada itakayobaki inaingizwa kwenye gridi ya Taifa.



" Habari njema ni kuwa tayari vijiji Saba vimeunganishiwa umeme kupitia mradi huu, hii inatimiza moja ya malengo ya Serikali ya kuhamasisha na kuwezesha upatikanaji wa nishati bora katika maeneo ya vijijini kupitia asasi za kiraia," alisema Dkt. Kalemani.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa Mradi wa Umeme wa Maji wa Kilowati 430 katika Kata ya Ikondo mkoani Njombe.  Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Rehema Nchimbi (wa kwanza kushoto), Mbunge wa Lupembe,  Joram Hongoli (wa pili kushoto),  Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU), Jane Nunes (wa Tatu kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt Gideon Kaunda (wa pili kulia) na Balozi wa Italia nchini, Roberto Mengoni (wa Nne kulia).
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kutoka kulia) akipiga makofi mara baada ya uzinduzi rasmi wa Mradi wa Umeme wa Maji wa Kilowati 430 katika Kata ya Ikondo mkoani Njombe.  Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Rehema Nchimbi (wa kwanza kushoto), Mbunge wa Lupembe,  Joram Hongoli (wa Tatu kushoto),  Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU), Jane Nunes (wa Nne kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt Gideon Kaunda (wa pili kushoto). 

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kushoto) akiangalia moja ya mitambo ya kuzalisha umeme  Umeme wa Maji wa Kilowati 430 katika Kata ya Ikondo mkoani Njombe.  Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Rehema na wa kwanza kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga.

MHE. GAMBO AWATAKA WAFADHILI KUTOA CHAKULA MASHULENI

$
0
0
Na Nteghenjwa Hosseah - Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amewataka wafadhili na wadau wa watoto kubuni miradi inayoendana na kusaidia  Mpango wa Serikali wa Elimu bure kwa shule za Msingi na Sekondari  ili kupunguza changamoto zinazojitokeza kwa sasa na kuuwezesha mpango huu kutekelezwa  kwa mafanikio makubwa.

Mhe. Gambo ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa kushirikishana tuliojifunza wakati wa utekelezaji wa mpango wa pamoja tuwalee uliotekelezwa kwa miaka sita kwenye Kanda ya Kaskazini  na ambao kwa sasa umemaliza muda wake ulifanyika kwenye Hotel ya Mt Meru Jijini hapa.


Akizungumza katika Mkutano huo Mkuu wa Mkoa amesema kazi kubwa imefanyika wakati utekelezaji wote wa mradi  na mafanikio yake tumeonekana kwani watoto wamefikiwa na kusaidiwa kutoka katika mazingira hatarishi yaliyokuwa yanawakabili na wengine kupatiwa kadi za msamaha wa matibabu na zaidi mradi huu umekabidhiwa kwa Halmashauri husika ambazo  zitaendelea kusimamia na kutekeleza  mipango iliyowekwa chini ya mradi wa Pamoja Tuwalee.


Aliendelea kusema kuwa kukamilika kwa mradi huu katika awamu ya kwanza ni wazi kabisa kwamba ni maandalizi ya mradi mwingine ambao utakua na malengo yanayoshabihiana na programu ya awali hivyo ni vyema kwa kuwa walengwa bado ni watoto niwatake wadau kubuni miradi utakaolenga kusaidia Elimu bure na kwa kuwa watoto wote wanapata Elimu bure kupitia mpango huu basi ni vyema mkaelekeza nguvu kwenye utoaji wa Chakula kwa wananfunzi suala ambalo tumeona ni changamoto kwa watoto wetu.
   Mkuu wa Mkoa wa Arusha akizungumza na wadau wa Mkutano 

    Mkurugenzi wa WEI-TANZANIA Bi. Lilian Badi (aliyesimama) akielezea mafanikio ya Mradi wakati wa Mkutano wa kuhitimisha mradi wa Pamoja Tuwalee.
  Mkurugenzi Mkuu wa World Education Inc Bi.Gill Garb akitoa taaria ya utekelezaji wa mradi wa Pamoja Tuwalee kupitia WEI-Bantwana.
 Mwakilishi wa US-AID Tanzania Bi. Maria Busquets akielezea namna ambavyo Shirika lake limefanikisha utekelezaji wa mradi wa Pamoja Tuwalee.
 Mkurugenzi wa Kituo cha Maendeleo ya Wanawake, watoto na vijana (CWCD) Bi. Hindu Ally Mbwego akielezea mafanikio ya mradi kupitia Kituo chake ambao ndio watekelezaji katika Halmashauri za Jiji la Arusha, Karatu na Moshi.
Picha ya pamoja ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha (katikati mbele), Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi waliotekeleza mradi huu, viongozi wa WEI, US AID, CWCD pamoja na  Wadau  wa watoto walioshirki katika Mkutano wa kuhitimisha mradi wa Pamoja Tuwalee.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SAIDA KAROLI: MENEJA WANGU AMEMTAPELI DIAMOND MAMILIONI, MIMI NILIMPA WIMBO BURE

JUMIA YAZINDUA KAMPENI YA 'BLACK FRIDAY'


SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) LANG'ARA MAONYESHO YA WADAU WA BIMA DAR

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa maonyesho ya wadau wa bima yaliyoandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania (IIT) yanayofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam, wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bima ya Mgen Charles Sumbwe , Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya G A Tanzania, Amit Srivastavr na Mkurugenzi Mtendaji wa kamapuni ya Bima ya Maxinsure, Bhaskar Nair. 
Mmoja wa wananchi aliyefika kwenye manesho ya wadau wa bima Gudumo Gaironga(kushoto) akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga (kulia) alipokuwa akimfafanulia jambo wakati wa maonyesho ya wadau wa bima yaliyoandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania (IIT) yanayofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 
Kamishina wa wa Bima Tanzania Ezraell Kamuzora (kulia) akiwapongeza wafanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wao Sam Kamanga (kushoto) wakati alipotembelea banda lao lililopo kwenye maonyesho ya wadau wa bima yaliyoandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania (IIT) yanayofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga akimpongeza mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) anayesoma kozi ya maswala ya bima Baraka Dinis kwa kujitolea kutoa damu kwa ajili ya kuchangaia Mpango wa Taifa wa Damu salama kwenye maonyesho ya wadau wa bima yaliyoandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania (IIT) yanayofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Elisante Maleko.

TAASISI YA DORIS MOLELL FOUNDATION YAANDAA MATEMBEZI KUKABILIANA NA VIFO VYA WATOTO NJITI

$
0
0
Na Bakari Madjeshi,Globu ya Jamii

Katika kuhakikisha kuwa vifo vya Watoto Njiti vinapungua hapa nchini,Taasisi ya Doris Mollel Foundation imeandaa Matembezi ya Hisani ili kukabiliana na vifo vya watoto hao kupungua.

Matembezi hayo yenye kauli mbiu ya "Okoa Maisha ya Mtoto Njiti" yatafanyika Visiwani Zanzibar kutokana na Wanawake wengi visiwani humo kukabiliwa kwa asilimia kubwa na suala hilo la Watoto kuzaliwa Njiti.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mwanzilishi wa Taasisi hiyo, Doris Mollel amesema kuwa Watoto wengi wanakufa kutokana na kushindwa kupumua wenyewe, hivyo wao kama Taasisi imewasukuma kusaidia suala hilo.

Dorice ametoa  shukrani kwa Wadhamini waliojitolea kuasaidia kukabiliana na suala hilo ikiwa ikiwa ni Vodacom Foundation Tanzania, GSM Foundation, Clouds Media Group na UTT AIMS, Michuzi Media Group na wengine wengi.

Pia ametoa shukrani kwa Viongozi wa Serikali kama Mhe. Angela Kairuki, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Wizara za Afya Tanzania Bara na Visiwani.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Vodacom Tanzania, kupitia kwa Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Mwasiliano, Jacquiline Materu amesema wameamua kudhamini Kampeni hiyo ikiwa ni fursa nzuri kuondoa vifo vya Mama na Mtoto.

Naye Afisa Mwandamizi Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS amesema wanashirikiana Doris Mollel Foundation toka mwaka Jana amesema watasaidia Kampeni hiyo ya Okoa Mtoto Njiti kuhakikisha wanapunguza vifo vya akina mama na Mtoto.
 Muanzilishi wa Taasisi ya Dorice Mollel, Dorice Mollel akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Novemba 16, 2016 juu ya matembezi ya hisani ya kuadhimisha Kilele cha Siku ya Mtoto Njiti Duniani, yanayotarajiwa kufanyika Novemba 19, 2016 Mjini Unguja Visiwani Zanzibar, ambapo Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mama Asha Balozi ndie anaetarajiwa kuyaongoza matezi hayo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu na kushoto ni Afisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano - UTT AMIS, Martha Mashiku.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Novemba 16, 2016, juu ya matembezi ya hiari yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya watoto njiti yanayotarajiwa kufanyika Mjini Unguja, Zanzibar mwishoni mwa wiki hii. Kulia ni Muanzilishi wa Taasisi ya Dorice Mollel, Dorice Mollel.
Afisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano - UTT AMIS, Martha Mashiku (kulia) akielezea namna walivyoshirikiana na Taasisi ya Dorice Mollel Foundation katika kufanikisha matembezi hayo.

ZAHANATI YA MCHOMORO KUKAMILIKA MWEZI MACHI

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo ambae pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amewahakikishia wananchi wa Kata ya Mchomoro Wilayani humo kuwa jengo la Zahanati ya kijiji hicho litakamilika na kuanza kutoa huduma mwezi Machi mwakani kama ilivyopangwa. 

Jengo hilo ambalo ujenzi wake unatokana na kuharibika kwa jengo la zamani kulikosababishwa na ujenzi wa barabara ya Songea- Tunduru linatarajiwa kuendelezwa ili kuwa kituo cha afya na hivyo kuhudumia idadi kubwa ya wananchi wa Kata hiyo. 

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo hilo Eng. Ngonyani amewakabidhi wasimamizi wa ujenzi huo fedha kwa ajili ya kukamilisha hatua upauaji wa jengo hilo na kusisitiza umuhimu wa matumizi sahihi ya fedha hizo ili ziwiane na ubora wa kazi. 

“Hakikisheni mnazingatia makubaliano ili zoezi la kuezeka jengo hili la Zahanati likamilike kabla ya Januari na hivyo kuwezesha zahanati hii kuanza kazi mapema mwezi Machi”. Amesema Eng.Ngonyani. 
Muonekano wa jengo la zahanati ya Mchomoro wilayani Namtumbo ambayo ipo katika hatua za za mwisho za ujenzi wake, Zahanati hiyo inatarajiwa kuendelezwa ili kuwa kituo cha afya ya kata hiyo.
Mbunge wa Namtumbo Eng. Edwin Ngonyani akitoa maelekezo kwa mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa zahanati ya Mchomoro mara baada ya kukagua ujenzi wa zahanati hiyo
Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa zahanati ya Mchomoro wakijadiliana jambo mara baada ya kupokea fedha kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Eng. Edwin Ngonyani kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo.

PROF. MBARAWA AZINDUA BODI MPYA YA TRL

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti mpya wa bodi ya TRL, Profesa John Kondoro alipozindua bodi hiyo jijini Dar es Salaam jana mchana. 



Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Masanja Kadogosa akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na wafanyakazi wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akifafanua jambo kwa wafayakazi wa TRL alipoongea nao jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Masanja Kadogosa.Kulia ni Mwenyekiti ya Bodi ya TRL, Prof. John Kondoro.
Wafanyakazi wa kampuni ya Reli Tanzania (TRL), wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ( hayupo pichani), alipoongea nao jana  mchana jijiini Dar es Salaam. 

WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UPR AFRIKA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe amekutana na mwakilishi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Kupitia Hali ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika Bw, Gilbert Onyango na kuzungumza jinsi ya kusaidia utekelezaji wa mapendekezo 130 ambayo Serikali iliyakubali mbele ya Baraza la Haki za Binadamu wakati wa kupitia Ripoti ya Tathmini ya Hali ya Haki za Binadamu
.Mhe. Waziri Mwakyembe amesema Serikali kama ambavyo ilivyoridhia mapendekezo hayo itasimama imara kuhakikisha yanatekelezwa kikamilifu na hivyo kuimarisha hali ya haki za binadamu nchini.

Amesema nia ya Serikali ni kuona haki za bindamu nchini zinaheshimiwa bila ya kuingilia au kukiuka mila, tamaduni , desturi na imani za kidini ambazo Tanzania imekuwa ikizifuata au kuziamini tangu enzi.

Nae bw. Onyango alisema kwamba wao kama taasisi isiyo ya kiserikali wanafanya kazi na serikali mbalimbali duniani, taasisi zisizo za serikali na Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha haki za binadamu zinaimarishwa na kuthaminiwa na kuongeza kuwa lengo hasa la kukutana kwake ni kujitambulisha na kuomba kufanya kazi na serikali katika kuhakikisha mapendekezo yaliyokubaliwa yanatekelezwa kikamailifu.

Pia aliomba kupatiwa nafasi ya kutoa mafunzo jinsi ya utekelezaji huo kwa taasisi na watumishi wa umma wanaohusika na utekelezaji wa mapendekezo hayo ili kufanikisha mpango wa utekelezaji wa mapendekezo hayo.

Alisema kwamba lengo lao kuu ni kuunganisha mpango wa tathmini ya hali ya haki za binadamu nchini ili uendane na mpango wa malengo ya milenia ili kuweza kufikia maendeleo ya kweli huku haki za binadamu zikiimarishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Mwezi Septemba 2016, Serikali iliyakataa mapendekezo 94, kuyaangalia upya mapendekezo 25 na kukubali 130 kati ya 227 yaliyotolewa na mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa, likiwemo suala la hali ya kisiasa Zanzibar. Tamko hilo lilitolewa kwenye mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu wakati wa kupitisha Ripoti ya Tathmini ya Dunia (UPR) mbele ya Baraza la Haki za Binadamu wakati wa kupitia Ripoti ya Tathmini ya Hali ya Haki za Binadamu kwa nchi wanachama uliofanyika mjini Geneva nchini 

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe (katikati) akiongea na mwakilishi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Kupitia Hali ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika Bw, Gilbert Onyango (kulia) alipomtembelea leo (16/11/2016) ofisini kwake jijini Dar Es Salaam. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji haki Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Bw. Patience Ntwina (kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Katiba Bw. Stanley Kamana.

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe (kushoto) akiongea na mwakilishi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Kupitia Hali ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika Bw, Gilbert Onyango alipomtembelea leo (16/11/2016) ofisini kwake jijini Dar Es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe (kushoto) akiongea na mwakilishi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Kupitia Hali ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika Bw, Gilbert Onyango alipomtembelea leo (16/11/2016) ofisini kwake jijini Dar Es Salaam.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images