Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1429 | 1430 | (Page 1431) | 1432 | 1433 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Serikali imesema kuwa Tanzania ina fursa nzuri katika uwekezaji wa huduma za kifedha na kuwavutia wawekezaji wa mataifa tofauti na malalamiko ambayo yamekuwa yakienezwa na baadhi ya taasisi hizo hapa nchini.

  Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijazi wakati wa ufunguzi wa tawi la jipya la Kariakoo la benki ya United Bank Limited (UBL) Tanzana Limited.

  Hivi kaibuni kulikuwa na malalamiko mbalimbali kutoka kwa baadhi ya taasisi za kifedha na kutoa viashiria vya kufirisika, jambo ambali alisema, uzinduzi wa tawi la Kariakoo la benki ya UBL ni ishara tosha kuwa sekta ya uwekezaji wahuduma za kifedha hipo imara na kuendelea kuwavutia wawekezaji.

  Waziri Kijazi alisema kuwa uchumi wa Tanzania kwa sasa unakuwa na bodi ya wakurugenzi wa benki ya UBL imevutiwa nayo na kuamua kuwekeza nchini. Alisema kuwa benki hiyo kwa sasa imetumia jumla ya dola za Kimarekani milioni 32 (Sh 67.2 bilioni) kutoa mikopo kwa wateja wake na huduma nyingine

  “Benki ya UBL Tanzania ilianza rasmi Mwezi Septemba mwaka 2013 na kufanikiwa kupata faida iliyopelekea kuzindua tawi lingine huku ikiwa na mipango ya kufungua matawi kadhaa katika mikoa ya Dodoma, Mwanza na Arusha, hii ni ishara tosha kuwa sekta ya huduma ya kifedha Tanzania inakuwa na kupata maendeleo makubwa,” alisema Dk Kijazi.

  Kwa upande wake, Rais na Mtendaji Mkuu wa UBL Bw. Wajahat Husain alisema kuwa wamefuraishwa na hali ya uwekezaji hapa nchini na kuamua kuwekeza, ikiwa ni tawi la kwanza la benki hiyo kwa bara la Afrika.

  Husain alisema kuwa wameichagua Tanzania kutokana kukuwa kwa uchumi, hali bora ya kisiasa, maliasili na huduma za bandari ya Dar es Salaam ambayo ni kiungo cha wafanyabiashara, si kwa Tanzania tu, bali hata kwa nchi sita jirani. Alisema kuwa kupanuka kwa mtandao wa benki hiyo kwa Dar es Salaam kutaifanya benki hiyo kuwa kiungo muhimu cha masuala ya kiuchumi.

  “Tumefurahi kuwekeza hapa nchini, benki yetu ni miongoni mwa beki kubwa sana nchini Pakistani, tukiwa na matawi zaidi ya 1,300 na kutoa huduma wengi, tumevutiwa na hali ya uwekezaji hapa nchini na muda mfupi tuliowekeza, tumeona matunda yake na kuamua kupanua wigo,” alisema Husain ambaye pia ni Mwenyekiti wa Benki hiyo nchini.

  Alisema kuwa wapo tayari kwa soko la ushindani la hapa nchini na nyenzo yao kubwa ni kutoa huduma za kisasa zenye ufanisi mkubwa.


  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji akikata utepe kuzindua  tawi jipya la Benki ya UBL Kariakoo katika hafla fupi iliyofanyika jana. Kulia ni Rais, Afisa Mtenadaji Mkuu wa United Bank Limited (UBL) Pakistan ambaye pia ni Mwenyekiti wa UBL Tanzania, Bw. Wajahat Husain na kushoto ni Afisa Mtenadaji Mkuu wa UBL Tanzania, Faisal Jamall. 
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji wa pili kutoka kulia akikata keki maalum katika hafla ya uzindua tawi jipya la Benki ya UBL Kariakoo katika hafla fupi iliyofanyika jana. Kulia kwake ni Rais, Afisa Mtenadaji Mkuu wa United Bank Limited (UBL) Pakistan ambaye pia ni Mwenyekiti wa UBL Tanzania, Bw. Wajahat Husain na kushoto ni Afisa Mtenadaji Mkuu wa UBL Tanzania, Faisal Jamall
  Rais, Afisa Mtenadaji Mkuu wa United Bank Limited (UBL) Pakistan ambaye pia ni Mwenyekiti wa UBL Tanzania, Bw. Wajahat Husain(kulia) akimkabidhi tuzo maalum Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji katika hafla ya uzindua tawi jipya la Benki ya UBL Kariakoo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye tawi hilo jana.
  Wageni mbalimbali na wafanyakazi wa benji ya UBL wakifuatilia uzinduzi wa tawi la benki hiyo jana.

  0 0
  0 0

  Serikali ya Tanzania imeshukuru msaada mkubwa unaotolewa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na mfumo imara wa utoaji haki kwa kuzingatia demokrasia na uwajibikaji.

  Serikali imesema kumekuwepo na mabadiliko makubwa katika mfumo ya utoaji haki nchini kutokana na misaada iliyotolewa na nchi hizo kupitia Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambao unasaidia mpango huo wa UNDAP.

  Hayo yameelezwa wakati ujumbe mzito wa kutoka nchi za Nordic ulipotembelea Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria. Nchi hizo za Nordic pamoja kutoa mchango wake mkubwa katika bajeti za serikali ya Tanzania pia hutoa mchango mkubwa kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya shughuli zake nchini.

  Mataifa hayo ni ya Sweden, Norway, Denmark, Finland na Iceland ambayo kwa pamoja yanaitwa mataifa ya Nordic ni wadau muhimu wa Umoja wa Mataifa na pia kwa serikali ya Tanzania.

  Ujumbe kutoka nchi hizo upo nchini kwa ajili ya kuimarisha mahusiano kati yao na Mashrika ya Umoja wa Mataifa yanayofanyakazi kama taasisi moja na nchi hizo (Delivering as one) kwa lengo la kuimarisha na kusukuma mbele malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).Katika ziara hiyo iliyoanzia Novemba 14 wajumbe hao waliweza kuangalia utekelezaji mbalimbali wa miradi ya Umoja wa Mataifa na hasa hatua za mwanzo za miradi ya UNDAP ll.

  Ujumbe huo wenye watu 13 kutoka Wizara za Mambo ya Nje za mataifa hayo wanatarajia kuzuru pia Kigoma na Dodoma wakimaliza Dar es Salaam.

  Wakiwa Dar es Salaam, jana na leo watakutana na wawakilishi wa taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali na AZAKI na pia wanatarajia kutembelea ofisi za Bunge.Taarifa iliyotolewa katika mkutano huo imesema ingawa msaada wa Umoja wa Mataifa umekuwa siku zote ukililenga eneo maalumu linaloshughulikiwa na mashirika tofauti ya Umoja wa Mataifa, imekuwa nguvu kupima athari zake katika maeneo mbalimbali yaliyokusudiwa.
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Awa Dabo akielezea dhumuni la ziara ya ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana na wataalam kutoka Umoja wa Mataifa ulipotembelea wizara hiyo jana 14/11/2016 jijini Dar Es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akitoa neno la ukaribisho kwa ujumbe kutoka nchi za Nordic ulipotembelea wizara wake jana 14/11/2016 jijini Dar Es Salaam.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)Mkurugenzi Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Bw. Patience Ntwina (aliyesimama) akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kwa ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana na wataalam kutoka Umoja wa Mataifa ulipotembelea wizara hiyo jana 14/11/2016 jijini Dar Es Salaam.


  0 0

  Tiba hii inaitwa JIKO. Kila mwanaume anae itumia, INAMPONYESHA KABISA tatizo la UKOSEFU na UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME. Imethibitishwa na MKEMIA MKUU WA SERIKALI YA TANZANIA

  Kufahamu jinsi tiba hii inavyo fanya kazi, bofya link hii hapa chini :


  Kwa mahitaji yako ya tiba hii, wasiliana na duka la NEEMA HERBALIST & NUTRITIONAL FOODS CLINIC kwa simu namba 0766 53 83 84.

  Tunapatikana UBUNGO jijini DAR ES SALAAM, jirani na SHULE YA MSINGI UBUNGO NATIONAL HOUSING nyuma ya jengo la UBUNGO PLAZA. · Kwa wateja waliopo DAR ES SALAAM, wasio na nafasi ya kufika ofisini kwetu, watapelekewa dawa mahali walipo ( HOME & OFFICE DELIVERY ).

  · Kwa wateja waliopo mikoani, watatumiwa dawa kwa njia ya mabasi mbalimbali.

  · Kwa wateja waliopo Zanzibar, watatumiwa dawa kwa njia ya usafiri wa boti.

  · Kwa wateja wa Mombasa, watatumiwa dawa kwa basi la TAHMEED COACH.

  · Kwa wateja wa NAIROBI watatumiwa dawa kwa basi la DAR EXPRESS.

  · Na kwa wateja wa UGHAIBUNI ( DIASPORA), watatumiwa dawa kwa njia ya POSTA au DHL.

  · Kwa taarifa zaidi kuhusu huduma zetu, tembelea kila siku website yetu www.neemaherbalist.com


  0 0

  Na Dotto Mwaibale

  WASAIDIZI wa kisheria wanawake kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG), wamemuunga mkono Rais Dk. John Magufuli katika uhimizaji wa kufanya usafi Soko la Temeke Sterio jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza katika tukio hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki sokoni hapo Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa EFG, Shaban Rulimbiye alisema wameamua kufanya usafi wa mazingira katika masoko sita yaliyopo chini ya mradi wa kupinga ukatili wa kijinsia masoko unaoendeshwa na shirika hilo.

  "Tunamuunga mkono rais wetu kwa jitihada zake anazozifanya za kuhimiza usafi ndio maana wasaidizi wetu wa kisheria kutoka katika masoko hayo tupo nao hapa Temeke kufanya usafi na baada ya hapo watatoa elimu kwa wafanyabiashara ya kupinga ukatili huo " alisema Rulimbiye.

   Alisema ukatili wa kijinsia masokoni si kumshika maungoni mfanyabiasha na matusi hata pale wanawake wanapofanya biashara zao kwa kuziweka chini bila ya kuwa katika mazingira mazuri pia ni ukatili wa kijinsia.

  Alisema mpango huo wa kufanya usafi katika masoko hayo ni endelevu na kuwa kila Jumamosi watakuwa wakifanya hivyo kumuunga mkono rais.

  Rulimbiye aliyataja masoko ambayo yapo chini ya mradi huo ambayo yatanufaika na usafi huo wa mazingira kuwa ni Temeke Stereo, Mchikichini, Kisutu, Feri, Gezaulole na Tabata Muslim.

  Makamu Mwenyekiti wa soko la Temeke Sterio, Issa Ndilima alilishukuru shirika hilo kwa mpango huo wa usafi kwani umeleta hamasa kwa wafanyabiashara wa soko hasa katika mafunzo wanayopata kupitia wasaidizi wa kisheria kupinga ukati wa kijinsia masokoni.
  Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Shaban Rulimbiye (kushoto), akiwaongoza kufanya usafi Soko la Temeke Sterio Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Dk.John Magufuli katika suala zima la usafi wa mazingira.
  Mifagio ikipigishwa kwata ya usafi.
  Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Shaban Rulimbiye (kushoto) na Charles Beatus wakifanya usafi.
  Usafi ukiendelea.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)  Bw. Joel Laurent(kulia) akimkabidhi Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda moja ya projecta zitakazotumika katika kufundishia chuoni hapo, Misaada mingine ni Ubao maalum za kufundishia (Smart Board) 4 na Komputa 22.
   Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)  Bw. Joel Laurent (mweyesuti) alipotembelea chuo hicho kuangalia misaada ya vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano walivyovitoa chuoni hapo ikiwemo Ubao maalum za kufundishia (Smart Board) 4,Projecta 4 na Komputa 22, wa mwisho kulia ni Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Sylvia Lupembe.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw. Joel Laurent akiongea na Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda(mwenye shati jeupe) ambapo alishauri kusimamia matumizi sahihi ya vifaa hivyo vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano vinatumika kwa manufaa ili kuleta matokeo yenye tija, mbele mwenye suti ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Dkt. Tumaini Katunzi na Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Sylvia Lupembe.
   Makamu Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Dkt. Tumaini Katunzi na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw. Joel Laurent wakifuatilia maelekezo ya namna ubao maalum wa smart board unavyofanya kazi wakati wa kufundishia ikiwa ni moja ya msaada uliotolewa na mamlaka ya elimu.
   Sehemu ya Komputa 22 zilizotolewa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwenye chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC).

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunngano wa Tanzania Bi Samia Suluhu amewasihi viongozi wa serikali na wananchi kutumia ndege za Shirika la Ndege Tanzania(ATC) ili kudumisha uzalendo na kuchangia pato la shirika hilo kwa lengo la kuhimili ushindani na kukuza uchumi wa nchi.

  Ametoa rai hiyo jijini Dar es salaam alipopewa hati ya kusafiria kupitia ndege za shirika hilo wakati akisafiri na ujumbe wake kuelekea mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi.“Napenda kutoa wito kwa viongozi wa Serikali na wananchi kwa ujumla kutumia ndege zetu ili shirika letu lifanye kazi vizuri zaidi, kufanya hivi kutaongeza pato na kukuza uchumi wa nchi ”, amesema Makamu wa Rais.

  Ametanabaisha kuwa kwa kutumia ndege za Shirika la ATC kwa safari za ndani Serikali itaokoa fedha nyingi zinazotumika kwa kukodi ndege za mashirika binafsi.“Mimi na ujumbe tumeamua kusafiri na ndege za shirika la ndege Tanzania kutokana na kubana matumizi, gharama tuliyotumia kwa safari hii ni shilingi Milioni saba na laki sita ambapo tungekodi ndege binafsi tungetumia milioni arobaini”, amefafanua Makamu wa Rais.

  Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amempongeza Makamu huyo kwa kitendo cha uzalendo alichokionyesha na kutaka viongozi wengine wa Serikali na wananchi kwa ujumla kuiga mfano huo ili kuliinua shirika hilo na kuongeza uchumi.

  “Nampongeza Makamu wa Rais kwa kuamua kutumia ndege za Shirika hili kwa safari za ndani, kitendo hiki kimeonesha nia ya dhati ya serikali ya kulifufua shirika hili, naomba wananchi nao waendelee kutumia ndege za shirika hili katika safari zao za ndani kama alivyofanya Makamu wa Rais”, amesema Waziri Mbarawa.

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akionyesha mfano wa hati ya safari ya kuelekea Mwanza kupitia Shirika la ndege la Tanzania (ATCL), kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa.

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiongea na waandishi wa habari kabla ya kufanya ziara ya kikazimkoani Mwanza kupitia Shirika la ndege la Tanzania (ATCL), leo jijini Dar es salaam.

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipokea maoni kutoka kwa wasafiri wanaotumia usafiri wa anga katika uwanja wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA) wakati alipokagua utoaji wa huduma uwanjani hapo.

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipokea maoni kutoka kwa wasafiri wanaotumia usafiri waa anga katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere wakati alipotembelea kukagua huduma zitolewazo uwanjani hapo.


  0 0

  Mtanzania Fredy Uisso (kushoto) aliyekwenda Alabama nchini Marekani kushiriki mashindano ya upishi, akikabidhiwa tuzo na Mkurugenzi Mtendaji wa World Food Championships, Mike Mc Cloud mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nne wa mashindano hayo usiku wa kuamkia leo. Uisso anaandika historia ya kuwa Mwafrika wa kwanza kuchaguliwa kushiriki fainali za mashindano hayo na kuibuka mshindi nafasi hiyo huku akiwabwaga wapishi 21 kutoka hoteli kubwa na maarufu duniani walioshiriki fainali hizo zilizoanza Novemba 8 mwaka huu.


  0 0


  Na Raymond Mushumbusi WHUSM

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amesema serikali haijamtelekeza mshindi wa shindano la Urembo la Tanzania kwa mwaka 2016 bali wanaendelea kumpa msaada wa hali na mali ili kufanikisha ushiriki wake katika mashindano ya urembo ya dunia.

  Mhe. Nape ameyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam alipokuwa akikabidhi Bendera ya Taifa kwa mshiriki kutoka Tanzania anayekwenda kushiriki mashindano ya Miss Afrika 2016 yatakayofanyika Novemba 28 mwaka huu.

  “Haiwezekani Serikali ikabariki mchakato mzima wa Miss Tanzania mshindi akapatikana alafu akatelekezwa na  tukakaa kimya sio kweli” Alisistiza Mhe. Nnauye.

  Mhe. Nnauye ameongeza kuwa watanzania wawe na desturi ya kutangaza mambo mema yanayotokana na shindano hilo la urembo badala ya kutafuta mapungufu na kuyakuza na yakaonekana kuwa ni tatizo kubwa katika machakato huo.

  Aidha amewahakikishia watanzania kuwa Miss Tanzania yuko salama na atashiriki vizuri katika mashindano ya Miss World kwa mwaka 2016 watanzania wazidi kumwombea na ikiwezekana kwa mwaka huu mrembo wa Dunia atokee Tanzania.

  Katika mashindano ya urembo kwa mwaka 2016 mrembo yaliyofanyika Jijini Mwanza na Bi Diana Edward Luqumay alishinda taji hilo na anatarajia kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Urembo ya Dunia 2016 yatakayofanyika mwishoni mwa mwaka huu Washington Dc nchini marekani na yatashirikisha nchi 119.


  0 0


  Na: Debora Charles

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Ally Hapi leo jumatatu tarehe 14/11/2015 amefungua rasmi mafunzo ya ujasiliamali kwa awamu ya kwanza.

  Katika Uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya amewata Vijana kuondokana na mawazo ya kuajiriwa pindi wanapohitimu vyuo vya Elimu ya juu na hata wale wasio na elimu hiyo, bali wajikite kutumia fursa zilizopo kujiajiri jambo ambalo litawasaidia kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira na kujenga uchumi wao na wa taifa.

  Hayo yamebainishwa leo na mkuu wa wilaya ya kinondoni, Ally Hapi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya ujasiliamali wilaya ya Kinondoni kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kubuni, kuanzisha na kusimamia biashara na miradi mbalimbali.

  Hapi amesema kuwa hakuna serikali duniani yenye uwezo wa kuajiri watu wake wote wenye uwezo wa kufanya kazi kutokana na ufinyu wa nafasi za ajira kulinganisha na mahitaji halisi. Bali wanaweza kujenga maisha yao kwa kubadilisha fikra na kuamua kujiajiri katika vikundi.Amesema, kuwa jukumu la serikali ni kuwawekea sera, mikakati na mazingira mazuri kwa vijana ili waweze kujiari katika shughuli za ujasiriamali.

  "Kazi tunayoifanya hapa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, ambayo inaeleza wazi jukumu la serikali ya awamu ya Tano katika kuwasaidia vijana wa elimu tofauti kujiajiri na kufanya shughuli za ujasiriamali katika vikundi. Tumeanza na awamu hii ya kwanza itakayonufaisha vijana elfu moja, na tutaendelea na awamu nyingine hadi tumalize vijana wote elfu kumi waliojiandikisha." 
  Alisema Hapi.

  Hata hivyo, DC Hapi amesema ameanzisha mafunzo hayo kwa nia ya kuwaondoa uwoga vijana na kuwajengea ujasiri na uthubutu katika kuamua kujiajiri kwani amebaini vijana wengi na hasa wanaohitimu vyuoni ni wazito na waoga kujiajiri, jambo ambalo ameeleza kuwa linatokana na mfumo wa elimu kujikita katika nadharia zaidi kuliko kuwaandaa vijana kifikra na kivitendo kuanzisha shughuli zao binafsi za kiuchumi.

  "Rais wetu Dr. John Magufuli ameahidi kupitia Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kuwa mikopo itatolewa katika ngazi ya mitaa na vijijini ili kuwawezesha vijana kujiajiri katika vikundi. Sisi kama Kinondoni tumeamua kujiandaa kwanza kwa kutoa mafunzo kwa watu wetu. Ili wajue nidhamu ya kukopa, kulipa deni, kubuni wazo la biashara, kuanzisha na kusimamia biashara na kutumia fursa zilizopo kujenga uchumi wao.

  Hatutaki vijana wetu wakope fedha hizo wakiwa hawajapata elimu ya kutosha kuwawezesha kufanya ujasiriamali wa kisasa. Matokeo yake fedha zitatolewa na zitashindwa kuleta matunda yaliyokusudiwa."
  Alisema Mh. Hapi
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi akizungumza na vijana wajasiriamali wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wajasiriamali vijana wa Manispaa ya Kinondoni jana Jijini Dar es Salaam.
  Mkufunzi wa Ujasiriamali Bi. Debora Charles akitoa mada wakati wa mafunzo ya wajasiriamali vijana kutoka Manispaa ya Kinondoni jana Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya ujasiriamali kutoka Manispaa ya Kinondoni wakifuatilia mafunzo ya ujasiriamali wakati wa mafunzo hayo jana Jijini Dar es Salaam.


  0 0


  0 0

  Umoja wa Mataifa umeingia ushirikiano na FURSA ili kuongeza uelewa wa malengo ya maendeleo endelevu kwa vijana zaidi ya 10,000 katika mikoa mitatu ya Dodoma, Dar es Salaam pamoja na Kigoma. 

  Fursa, ambayo imekuwa ikifanyika kwa miaka mitatu iliyopita, imejikita katika kuwajengea uwezo vijana wa kuzitambua fursa katika maeneo yao wanayoishi lakini pia namna ya kutengeneza miradi na biashara kupitia fursa hizo. 

  Ushirikiano wa Fursa na Umoja wa Mataifa utalenga kuwafikia vijana wanaohudhuria semina za Fursa kuelewa namna Malengo ya Dunia yanavyohusiana na maisha yao ya kila siku na wajibu wa kila kijana katika kushiriki kuyakamilisha. 

  Akizungumza wakati wa kuzindua semina za Fursa mkoani Dodoma, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez alisema semina za Fursa zimeweza kubadilisha maisha ya vijana wengi na hivyo ushirikiano wake na Umoja wa Mataifa katika kufikia vijana utatoa nafasi ya vijana kuyaelewa Malengo ya Dunia. 

  ‘Vijana wengi wana ari ya kushiriki katika kufanikisha Malengo ya Dunia, ndio maana Umoja wa Mataifa umeamua kushirikiana na Fursa ili kuhakikisha vijana wengi zaidi wanayafahamu malengo haya lakini pia wanashiriki katika kuyatekeleza’ alisema Alvaro. 

  Kwa upande wake, Mwanzilishi wa Fursa, Ruge Mutahaba amesema kwa zaidi ya miaka mitatu sasa Fursa imefanikiwa kuwafikia zaidi ya vijana milioni 5, na kuwapa mbinu na maarifa ya kuweza kutumia fursa katika maeneo yao. 


  ‘Tunaushukuru Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Fursa kuwafikia vijana katika mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam na Kigoma, ili sio tu wapate nafasi ya kupata mafunzo ya Fursa na biashara balipia mafunzo juu ya Malengo ya Dunia’ alisema Ruge.
   Timu ya wazungumzaji wa Fursa wakiwa katika picha ya pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi waShirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu.
   Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi waShirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumza na vijana waliohudhuria semina ya Fursa mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki hii.
   Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu akitoa mafunzo ya malengo ya maendeleo enedelevu kwa vijana wa Dodoma waliojitokeza wakati wa semina za Fursa zilizofanyika Dodoma mwishoni mwa wiki hii.
   Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi waShirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi mmoja wa vijana waliopata mafunzo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa mjini Dodoma. Anayetazama kushoto ni Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu.
  Baadhi ya vijana waliopata mafunzo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa mjini Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja na Mratibu      Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
  MASHINDANO ya kuchezea mpira  (Football Freestyle)  yaliyoandaliwa na chama cha mchezo huo Freestyle Football Tanzania (FFT) yanatarajiwa kuanza Novemba 19 kwa Wilaya tatu za Jiji la Dar es Salaam Temeke, Ilala na Kinondoni na  uzinduzi wa shindano hilo unatarajiwa kuanzia kwenye viwanja vya Mwembe Yanga.

  Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo unayodhaminiwa na kinywaji cha Red bull ikishirikiana na Clouds TV kupitia kipindi cha Sports Bar anatarajiwa kuwa Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea.

  Akizungumza na Mratibu wa shindano hilo Jacob Mbuya amesema kuwa washiriki  wa shindano hilo watajiandikisha bure  na washiriki wanatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 15 na kuendelea huku fomu za ushiriki zinapatikana Clouds TV na Ofisi za chama hicho zilizopo Kinondoni pamoja na mitandao ya kijamii kupitia kurasa zao.

  Mashindano yanatarajiwa kuanzia Wilaya ya Temeke Novemba 19 na kutapatikana washiriki watano na baadae kuhamia kwenue wilaya   ya Ilala ambayo pia itatoa washiriki watano  huku Kinondoni ikitoa sita ambao wataingia Fainali itakayochezwa Coco Beach, Disemba 11 na kwa upande wa  Wilaya ya Ilala shindano hilo litafanuyika kwenye viwanja vya Boma, Novemba 26 kabla ya kuelekea Kinondoni kwenye uwanja wa Tp Sweet Corner, Disemba 3. Rais wa Freestyle Football Tanzania (FFT)  Pascal Chang'a amesema kuwa wameamua kuanza kufanya mashindano haya na kupata vipaji ambao watawapa fursa ya kwenda kimataifa zaidi kwani huwezi kwenda kushiriki kama hujafanya nchi kwako na alitaja baadhi ya sheria za mchezo huo kuwa ni kila mshiriki atapewa sekunde 30 za kuchezea mpira, mchezaji atakuwa peke yake jukwaani na pia akidondosha mpira atakuwa amepoteza pointi.
  Naye Afisa Masoko wa Mahans Oysterbay Drinks, Hanson Heddy amesema kwua wameamua kushirikiana na FFT ili kuweza kuibua vipaji vya vijana katika mchezo huu na pia wao wamedhamini kwa kila kitakachokuwa kinahitajika.
  Katibu wa Freestyle Football Tanzania (FFT) Morisson Nossey akizungumza na waandishi wa habari wakati kuhusiana na mashndano ya kuchezea mpira yanayotarajiwa kuanza Novemba 19, kushoto ni Afisa Masoko wa Mahans Oysterbay Drinks, Hanson Heddy na kulia ni Mratibu wa Shindano hilo Jacob Mbuya.

  Mratibu wa Shindano la kuchezea mpira Freestyle Football Jacob Mbuya akizungumza na waandishi wa habari na kutoa utaratibu wa ushiriki kwa vijana kuanzia miaka 15 na kuendelea kulia ni 

  Katibu wa  Freestyle Football Tanzania (FFT) Morisson Nossey kushoto ni Afisa Masoko wa Mahans Oysterbay Drinks, Hanson Heddy  na mwisho ni Rais wa Freestyle Football Tanzania (FFT)  Pascal Chang'a. Picha na Zainab Nyamka.


  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameziagiza Wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mawaziri, Watendaji Wakuu pamoja na Wataalamu wao kufanya uchambuzi wa kuorodhesha mambo ambayo yanaonekana kuleta changamoto kuhusu kero za Muungano.
  Alisema orodha ya uchambuzi huo katika kila Sekta baadaye unapaswa kuwasilishwa katika Kamati ya Sekriterieti ya Vikao hivyo iliyo chini ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
  Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akikiongoza Kikao cha Mawaziri, Manaibu Mawaziri pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara za SMZ kilichofanyika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar  kupokea mambo ambayo tayari yamekubalika kutekelezwa katika Vikao vya Kamati ya pamoja ya SMT na SMZ kuhusu kero za Muungano.
  Alisema kazi iliyopo hivi sasa kwa Watendaji wa Kamati hiyo ya pamoja kwa upande wa Zanzibar  ni kukumbushana kwa nia ya kutafuta mapungufu yaliyojitokeza ndani ya utekelezaji wa kero za Muungano hasa ikizingatiwa zaidi   mabadiliko ya Uongozi yaliyojitokeza ndani ya Wizara za Serikali.
  Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed alieleza kwamba suala lolote wanalolihisi Mawaziri hao linafaa kuwa agenda ni vyema likawasilishwa mapema kwenye Kamati ya Sekriterieti.
  Waziri Aboud alisema hatua hiyo itawapa fursa Watendaji wa Sekriteriet hiyo kuyapitia masuala hayo na kuyapa upendeleo wa kuingizwa katika agenda za Vikao vinavyotarajiwa kushirikisha Wajumbe wa Kamati ya Pamoja na pande hizo mbili.
  Mapema akitoa Taarifa ya Kikao hicho Katibu wa Kamati ya Sekriteriet ya Kero za Muungamo ambae pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Joseph Abdulla Meza alisema Kamati hiyo tayari imeshafanya tathmini ya vikao vilivyopita.
  Katibu Mkuu Meza alisema uchambuzi wa tathmini hiyo utaweza kuwasaidia Wajumbe wapya wa Kamati hiyo katika kujadili kwa kina masuala yanayohusu Changamoto za Muungano.
  Wakichangia agenda hizo baadhi ya Washiriki wa Kikao hicho walipendekeza kuwepo kwa uelewa wa pamoja wa Washiriki hao katika kujadili masuala ya changamoto za Muungano ambao ndio njia rahisi ya upatikanaji wa ufanisi wa haraka.
  Kikao cha Mwisho cha Kamati ya pamoja ya Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar cha kujadili Kero za Muungano chini ya Mwenyekiti wake Makamu wa Rais wa Muungano kilifanyika Mjini Dodoma Mnamo Tarehe 23 Juni mwaka 2013.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikiongoza Kikao cha Mawaziri, Manaibu Mawazini na Makatibu Wakuu wa SMZ  kupokea mambo na utekelezaji wake yaliyokubalika kutekelezwa katika Vikao vya Kamati ya pamoja ya SMT na SMZ kuhusu kero za Muungano.

   Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Joseph Abdulla Meza akiwasilisha Taarifa kwenye Kikao cha Mawaziri, Manaibu Mawazini na Makatibu Wakuu wa SMZ  kuhusu kero za Muungano.
  Baadhi ya Mawaziri, Manaibu Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Wizara za SMZ wakiwa katika Kikao cha kupokea mambo na utekelezaji wake yaliyokubalika kutekelezwa katika Vikao vya Kamati ya pamoja ya SMT na SMZ kuhusu kero za Muungano. Picha na  OMPR – ZNZ.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi kuwa serikali imeweka mipango na mikakati thabiti ya kukabiliana na idadi kubwa ya vifo vinasababishwa na saratani hasa saratani ya matiti na mlango wa kizazi kote nchini.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo katika viwanja vya furahisha jijini Mwanza wakati akizundua kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti na mabadiliko ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani humo.

  Katika hotuba yake kwa mamia ya wananchi wa mkoa wa Mwanza waliojitokeza katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ikiwa ni nchi mojawapo Kusini mwa Jangwa la Sahara ina kiwango cha juu cha vifo vya saratani ya matiti na mlango wa kizazi ambapo asilimia 60 ya vifo vyote vinavyotokea Kusini mwa jangwa la Sahara vinasababishwa na saratani hiyo.

  Makamu wa Rais amesema kuwa vifo vingi vinatokana na uelewa mdogo, imani potofu,gharama kubwa za matibabu,unyanyapaa na kuwepo kwa vituo vichache wa kufanyia uchunguzi hapa nchini ambapo kwa sasa tiba ya mionzi inapatikana katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Roas, Dar es Salaam.

  Katika kukabiliana na tatizo hilo, Makamu wa Rais amesema kuwa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imepokea kiasi cha shilingi bilioni Tano kutoka Benki ya Dunia fedha ambazo zitawezesha vituo Vitatu kwa kila Halmashauri ambavyo vitasaidia kuboresha huduma za uchunguzi na matibabu ya mapema ili wanawake kote nchini hasa wale wale wa vijijini waweze kupata huduma hizo kwa urahisi na kwa ukaribu kwenye maeneo wanayoishi.


  “Wote ni mashuhuda kwa namna saratani ya mlango wa kizazi inavyosababisha vifo vingi hali ambayo hutokana na magonjwa wanaogundulika na ugonjwa kuwa tayari wamefikia hatua isiyotibika na kwa pamoja saratani hizi mbili husababisha zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote vya akinamama”

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa kizazi kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim (katikati) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania Dk. Serafina Mkuwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa kizazi kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akimsikiliza Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim kwenye moja ya mabanda yaliokuwa yanatoa huduma wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa kizazi kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiwapungia mkono wananchi waliojitokeza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa uzazi kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza. 
  Sehemu ya Wanawake waliojitokeza kwennye uzinduzi huo.


  0 0

  Na Dk. Juma Mohammed, 
  MAELEZO Zanzibar

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein amesaini Mswada wa sheria ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia na kusisitiza kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haikuvunjwa.
  Akizungumza Ikulu Mjini Zanzibar jana wakati akitia saini Mswada wa sheria ya utafutaji, uchimbaji wa mafuta na gesi asilia wa mwaka 2016, Rais Dk. Shein alisema kwamba taratibu zote zimefuatwa wakati wa mchakato wa kutunga kwa sheria hiyo na kuwaomba wananchi kuwapuuza wanaoeneza uzushi.
  Rais Dk. Shein alisema haja ya kuwepo kwa sheria hiyo inatokana na masharti ya kifungu cha nne Sheria ya Mafuta na Gesi Asilia 2015 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inataja kwamba shughuli za uendeshaji wa Mafuta na Gesi Asilia utafanywa Zanzibar kwa kusimamia na kuendeshwa na taasisi kwa mujibu wa Sheria za Zanzibar.
  “Kumekuwa na maneno mengi kwamba nisisaini sheria hii, Hakuna katiba wala sheria iliyovunjwa na tunawaomba wananchi kuendelea kuwa watulivu, kuheshimu sheria na kudumisha amani na mshikamano” Alisisitiza Rais Dk. Shein.
  Rais Dk. Shein amewataka wananchi wasikubali kuyumbishwa na wala wasibabaishwe na watu wasioitakia mema Zanzibar. Alisema kwamba sheria hiyo sasa itafungua milango kwa Makampuni mbalimbali kujitokeza kuanza kazi ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asili Visiwani Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitia saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016, katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambapo Viongozi mbali mbali wa Serikali na vyama vya Siasa walihudhuria hafkla hiyo,[Picha na Ikulu.] 15/11/2016.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akionesha hati muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,baada ya kusaini hati hiyo katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambapo Viongozi mbali mbali wa Serikali na vyama vya Siasa walihudhuria hafkla hiyo,[Picha na Ikulu.] 15/11/2016.
  Viongozi Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakiwa katika hafla ya utiaji saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
  Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi na Viongozi mbali mbali wakiwa katika hafla ya utiaji saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo
  Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe,Zubeir Ali Maulid (kulia) na Waziri wa Nishati na Madini Mhe,Profesa Sospiter Muhongo,wakiwa katika hafla ya Utiaji wa saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.


  0 0
  0 0

   http://3.bp.blogspot.com/-Ja9gYTH8Zw8/UoetfpR-U-I/AAAAAAACWMk/zcdGDbWBI9k/s1600/IMG_4156.jpg
  WAKULIMA wa korosho Wilaya ya Tunduru, wameondokana na umasikini kutokana na kupata soko la uhakika baada ya Kampuni ya Namela General Trade kushinda zabuni ya kununua zao hilo wakulima kwa bei ya Sh 3,757 kwa kilo, ikizishinda kampuni nyingine saba.

  Hadi kufikia Novemba 14, kulikuwa na zaidi ya tani 541 zilizoingizwa katika ghala la Chama Kikuu cha Ushirika Wilaya ya Tunduru (Tancu) ambako kampuni hiyo ilipewa kununua korosho tani 400 huku Kampuni ya Machinga iliyoshinda nafasi ya pili katika mnada huo, ikipata kibali cha kununua tani 141 kwa bei ya Sh 3,750.

  0 0

  TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeshukuru Umoja wa Mataifa kwa msaada wake mkubwa inaotoa kwa taasisi zisizo za kiserikali za kujengea uwezo wa kuweza kutetea haki za binadamu nchini Tanzania.

  Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa THBUB, Mary Massay wakati wajumbe wa nchi za Nordic ambao ni wafadhili wakubwa wa programu za Umoja wa Mataifa zinazotekelezwa nchini Tanzania walipozuru katika ofisi hizo kwa mazungumzo.

  “Kuna ongezeko kubwa la ufahamu kuhusu haki za binadamu, upatikanaji wa haki kwa makundi maalumu, uandishi wa habari kuhusu haki za binadamu na kuboreshwa kwa huduma za kisheria na ukaribu wa serikali wa kufanyakazi na wadau wa haki za binadamu,” alisema Massay akifafanua zaidi kuhusu manufaa ya ufadhili wa Umoja wa Mataifa katika kuboresha haki za binadamu nchini.

  Katika mazungumzo yao na ujumbe wa nchi za Nordic ambazo ni Sweden, Denmark, Norway Finland na Iceland kulikuwepo pia asasi mbalimbali zisizo za kiserikali kama Women’s Legal Aid Center, Tanzania Women Lawyers Association, Tanzania Women Judges Association, Legal Aid and Human Rights Center, Human Rights Defenders Coalition, na Tanganyika Law Society.

  Katika mazungumzo hayo asasi hizo zilielezea ufanyaji kazi wao mafanikio na changamoto wanazokumbana nazo na umuhimu wa ufadhili wa mashirika ya Umoja wa Mataifa.

  Akizungumzia changamoto zinazokabili Umoja wa Mataifa, serikali na asasi Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez alisema ipo haja ya kuwa na muono wa muda mrefu wa kuratibu shughuli zinazohusiana na maendeleo endelevu.  Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom Nyanduga (wa pili kushoto) akitoa neno la ukaribisho kwa wajumbe kutoka nchi za Nordic walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa (hawapo pichani) ulipotembelea tume hiyo jijini Dar es Salaam.

   Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto), Katibu Mtendaji wa THBUB, Mary Massay (wa pili kulia), Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Awa Dabo (kulia).(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
  Katibu Mtendaji wa THBUB, Mary Massay akizungumzia shughuli mbalimbali zinazofanywa na tume hiyo kwa ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa (hawapo pichani) ulipotembelea tume hiyo.  Kiongozi wa ushirikiano wa kimataifa wa Shirika la Misaada la Sweden (SIDA), Anders Rönquist (kulia) akizungumza kwa niaba ya wajumbe kutoka nchi hizo za Nordic ulipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) jijini Dar es Salaam.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya awamu ya Tano itaendelea kujenga na kuimarisha ushirikiano na taasisi za kidini nchini ili kuhakikisha miradi ya kijamii inayotekelezwa na taasisi hizo inaleta manufaa makubwa kwa wananchi wa Tanzania.


  Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo wakati akihutubia mamia ya wananchi  wa wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza kabla  ufunguzi wa mabweni ya wanafunzi wa Chuo cha Maafisa Tabibu yaliyojengwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Geita kwa gharama ya shilingi milioni 659.


  Makamu wa Rais amesisitiza kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa  unaotolewa na taasisi za kidini nchini unaolenga kuimarisha utoaji wa huduma bora za kijamii na hivyo Serikali inaendelea kudumisha mahusiano mema yaliyopo kati ya Serikali na taasisi hizo za kidini nchini.


  Makamu wa Rais pia amehimiza taasisi za kidini nchini kutumia vizuri misamaha ya kodi wanayopewa na Serikali ili kuhakikisha misamaha hiyo inakuwa na manufaa mazuri kwa jamii na sio vinginevyo.Kuhusu uhifadhi wa chakula, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameonya  vikali tabia ya baadhi ya wananchi kuuza mazao waliyovuna na baadaye kukabiliwa na uhaba wa chakula na kusema tabia hiyo sio nzuri na lazima ikomeshwe haraka iwezekanavyo.

  Makamu wa Rais amewaagiza viongozi wa wilaya kote nchini kupambana ipasavyo na wimbi la uuzaji kiholela nafaka hasa nje ya nchini ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa chakula kwa wananchi.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa mabweni ya wanachuo cha maafisa Tabibu Sengerema mkoani Mwanza.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi ya pongeza mara baada ya zoezi la ufunguzi wa mabweni ya wanachuo cha maafisa Tabibu Sengerema mkoani Mwanza kukamilika katikati ni Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Geita Mhashamu Flavian Kassala ,Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi pamoja na viongozi mbali mbali mara baada ya kukamilika kwa zoezi la ufunguzi wa mabweni ya wanachuo cha maafisa Tabibu Sengerema mkoani Mwanza.
              
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wanafunzi na wazazi waliojitokeza wakati wa ufunguzi wa mabweni ya wanachuo cha maafisa Tabibu Sengerema mkoani Mwanza.

older | 1 | .... | 1429 | 1430 | (Page 1431) | 1432 | 1433 | .... | 3282 | newer