Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

THE FUTURE FOR STUDENTS CAREER DEVELOPMENT TRAINING

$
0
0
This training is aimed for all  First Year and 
a bit to Second Year  college students -  and NOT for Finalists...
 SPEAKERS....
 Dr. Blandina Kilama
Ms. Emelda Mwamanga Mtunga - CEO Bang! magazine, 
Founding manager - Dare to Dream foundation.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU NOVEMBA 14, 2016

NSSF YASHIRIKI MAONYESHO YA FINANCIAL SERVICES EXPO JIJINI DAR

$
0
0
 Mwanachama mpya akikamilisha taratibu za kujiunga na NSSF, wakati wa maonyesho ya Financial Services Expo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanachama aliyejiunga na NSSF akikamilisha taratibu za kujiunga na NSSF kwa kuweka alama ya dole gumba katika fomu yake.
Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abas Cothema (kushoto), akitoa elimu kwa mwanachama wa NSSF wakati  wa maonyesho ya Financial Services Expo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa wadau aliyetembelea maonyesho hayo akipitia taarfa za NSSF.

PRESIDENT OF ZANZIBAR OPENS A NORWEGIAN-FUNDED PEDIATRIC WARD AT MNAZI MMOJA HOSPITAL

$
0
0
President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council, Dr. Ali Mohammed Shein greets a representative from the Norwegian Embassy, Victor Mlunde as he arrives at the National Mnazi Mmoja Hospital for inauguration of the Norwegian-funded pediatric ward.
President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council, Dr Ali Mohammed Shein greets Ms Theresia Mcha, a representative of the Royal Netherlands Embassy as he arrives at the Mnazi mmoja hospital to officially open Norwegian and Dutch funded children's wards.
President of Zanzibar, Dr Ali Mohammed Shein delivers his keynote speech to mark the official opening of Children's ward at Zanzibar Mnazi Mmoja Hospital.
Zanzibar Ministry of Health's Principal Secretary, Dr Juma Malik Akil briefing the Chief Guest and audience on the Norwegian-funded Children's ward.

CLICK HERE FOR MORE PHOTOS

EAC-USAID HOLD TECHNICAL BILATERAL MEETING

$
0
0
A Technical working-level bilateral meeting was held today between the officials of East African Community and United States Agency for International Development (USAID), on the sidelines of the ongoing 22nd Session of the Conference of Parties (COP22) to the United Nations Framework Convention on Climate Change (UNFCCC) and the 12th Meeting of Parties to Kyoto Protocol (CMP12) taking place in Bab Ighli in Marrakech, Morocco.

Leading the USAID Team was Mr. John Furlow, the Senior Climate Change Specialist based in Washington, DC, while the EAC Team was led by Mr. Jean Baptiste Havugimana, the Director of Productive Sectors and accompanied by Mr. Ladislaus Kyaruzi, the Principal Environment and Natural Resources Officer who heads the EAC Climate Change Coordination Unit, and other Senior officials.
Mr. Jean Baptiste Havigumana, the Director of Productive Sectors (with mic),​ briefs the USAID officials on the progress of the EAC-USAID partnership.

The EAC and USAID officials discussed the ongoing projects supported by USAID and noted tremendous milestones being recorded for example in the Planning for Resilience in East Africa through Policy, Adaptation, Research, and Economic Development (PREPARED) project, which has effectively taken root in the region.

Other projects include the Aflatoxin Control Programme and the Sanitary and Phytosanitary Programmes meant to ensure high quality agricultural, livestock and fishery products for intra Community trade, regional trade and external trade especially with USA under the AGOA trade facility.
Leading the USAID Team is Mr. John Furlow, the Senior Climate Change Specialist (3rd left, black suit) based in Washington, DC ​

The EAC Director of Productive Sectors, Mr. Jean Baptiste Havugimana, noted that the establishment of both the Project Implementation Committee (PIC) and the Project Coordination Committee (PCC) at the EAC Secretariat had greatly enhanced coordination of the various projects being supported by various partners and also improved on accountability, efficiency and value for money.

The EAC Director highlighted the 5 key priority areas for the next one year as follows; continued implementation of the Regional Climate Change Policy, which was adopted by the EAC Policy Organ in 2011; implementation of the tools developed by PREPARED on climate change vulnerability impact and strengthening data availability in the Partner States; implementation of the Anti-poaching and fight against illegal trafficking of wildlife and wildlife products strategy; sustainability of the Climate Change Coordination Unit at the EAC Secretariat; and lastly; implementation of the EAC Roadmap for implementation of the Paris Agreement on Climate Change.

TANZIA

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi anasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi wa Wizara Bwana Elvis Nyambita Magare, Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Ramani Idara ya Upimaji na Ramani kilichotokea tarehe 11/11/2016 Nyumbani kwake mtaa Mindu Upanga Jijini Dar es salaam. Ratiba ya kuaga Mwili wa Marehemu ni leo tarehe 14/11/2016 saa 4:00 Asubuhi hadi 7:00 Mchana na Kusafirishwa. Mazishi yatafanyika siku ya Jumatano tarehe 16/11/2016 Kijiji cha Shirati Wilaya ya Rorya Mkoani Mara.

WAZAZI WAMESHAURIWA KUWALEA WATOTO WAO KATIKA MAADILI MEMA ILI TAIFA LIONDOKANE NA MATENDO MAOVU

$
0
0
Na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

Wazazi wameshauriwa  kuwalea watoto wao katika maadili mema ili Taifa liondokane na matendo maovu. Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Naibu Mkuu wa Madrasatul Musbah iliyopo Mtaa wa Nzasa na Kigoma manispaa ya ilala, Sheikh Kassim Mzee.

Akizungumza katika Tamasha la wazi kati ya Madrasa na Wazazi iliyoandaliwa na Madrasa hiyo, Sheikh Mzee amesema ni vyema watoto wakaandaliwa katika maadili mema mapema kama ambavyo wao wanafanya katika madrasa yao kwa kuwafundisha mambo mbalimbali kwa lugha ya kiarabu kwa lengo la kumjua Mwenyezi Mungu kwakuzingatia yale aliyoamrisha na yale aliyoyakataza.
Tamasha hilo la siku ya wazi kati ya Madrasa na Wazazi, Sheikh Mzee amefafanua kuwa wameamua kufanya tamasha hilo kwa lengo la kuwaonesha wazazi jinsi wanavyotakiwa kuwafundisha watoto wao (wanafunzi), ambapo wanafunzi hao wanaonesha kwa vitendo yale waliyokuwa wanajifunza darasani, nakudai  kuwa huo ni mwanzo ila watajitahidi kufanya matamasha  kama hayo kila mwaka, ili kuleta chachu kwa wazazi wengine kuona umuhimu wa kuwapa elimu watoto wao na kuwa watoto wema katika jamii ili Taifa liondokane na matendo maovu .
Wanafunzi wa madrasatul Musbah wakionyesha kwa vitendo namna ya kumuandaa maiti kabla ya kwenda kuzika leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wazazi na wanafunzi wakiwa katika tamasha la wazi kati ya Wazazi na Madrasa leo jijini Dar es Salaam.

mambo ya Gado


WAZIRI NAPE AMKABIDHI BENDERA MREMBO JULIETH KABETE KUIWAKILISHA NCHI MISS AFRIKA

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

WAZIRI wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amekabidhi bendera ya Taifa kwa mlimbwende Julieth Kabete ambaye ameshiriki Shindano la Miss Tanzania na kufanikiwa  kushika namba nne Julietha ambapo anakwenda nchini  Nigeria kushiriki  shindano ya Afrika, litakalofanyika baadae mwezi huu. 

Shindano hilo linatarajiwa kufanyika  nchini humo katika jimbo la Cross River, mjini wa Calabar, kuanzia Novemba 14,  kilele itakuwa Novemba  26 ambapo kwa heshima iliyopewa mji na jimbo lake, Gavana wa Cross River Profesa Ben Ayade ameongeza zawadi ya gari jipya litakalosafirishwa mpaka nchi husika anayotoka mshindi mbali na zawadi ya dola 5000 atakazozipata.
Akizungumza jana, wakati wa shughuli hiyo, Waziri Nape alisema, wanaimani mrembo huyo aliyechaguliwa kwa kuzingatia vigezo vyote atafanya vizuri kwenye mashindano hayo na kuiwakilisha vema Tanzania.

Nnauye amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha washiriki wa shindano la Miss Tanzania wanapata fursa nyingine na sio kama mshindi akishapatikana wengine wanaachwa, na tukishaongea na waandaji wa shindano hilo na walituhakikishia kuwa watafanya vizuri kuweza kuhakikisha wanaangalia fursa zingine kwa warembo walioshiriki na  hivyo tunaamini mrembo huyo anavigezo vyote na atakwenda kufanya vizuri.

Mratibu wa Millen Magese Group (MMG), Matukio Chuma, amesema kuwa, wanamitindo kutoka kwenye shindano hilo wameweza kuendelea kufanya vizuri kupitia Swahili Fashion Week na anaamini kuwa Julieth ataiwakilisha nchi yetu vyema.

Taasisi hiyo imekuwa ikifanya shughuli zake ndani na nje ya bara la Afrika, ikiwemo nchini Marekani, Millen Magese amekuwa Kinara, Balozi wa kuheshimika na aliye mfano ndani na nje ya Bara la Afrika.

Shindano hilo la Miss Afrika 2016 ambalo limebeba kauli
mbiu ya Kutunza, Kujali na Kuthamini Uchumi wenye kutoa kipaumbele kwa Mazingira kama nyenzo kwa ajili ya Maendeleo endelevu litashirikisha warembo mbalimbali kutoka nchi za Afrika na Julieth amechaguliwa katika shindano lililoendeshwa na kampuni ya Millen Magese (MMG), inayoshughulika na kusaka vipaji vya warembo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amekabidhi bendera ya Taifa kwa mlimbwende Julieth Kabete ambaye ameshiriki Shindano la Miss Tanzania na kufanikiwa  kushika namba nne Julietha ambapo anakwenda nchini  Nigeria kushiriki  shindano ya Afrika, litakalofanyika baadae mwezi huu. Katika picha akiwa pamoja na baadhi ya waandani wa Miss Tanzania Hashim Lundenga na mwakilishi wa Milen Magese Matukio Chuma na mama mzazi wa Julieth.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kabla ya makabidhiano ya bendera kwa mrembo Julieth Kabete (kushoto) anayekwenda nchini nigeria kushiriki shindano la Miss Afrika mapema mapema mwezi huu.
 Mwakilishi wa Millen Magese Group (MMG) Matukio Chuma (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kabla ya makabidhiano ya bendera kwa mrembo Julieth Kabete (kushoto) anayekwenda nchini nigeria kushiriki shindano la Miss Afrika mapema mapema mwezi huu. 

Picha na Zainab Nyamka.

Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya Steps Entertainment yatembelea Bodi ya Filamu Tanzania

$
0
0
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa  Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya Steps Entertainment Bw. Dilesh Solank alipomtembelea Ofisi za Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
 
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akizungumza na wawakilishi kutoka Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya Steps Entertainment walipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
 
 Baadhi ya watendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania na wawakilishi kutoka Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya Steps Entertainment wakimskiliza Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo Bibi. Joyce Fissoo (hayupo pichani) alipotembelewa na wawakilishi hao kutoka Setps leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya Steps Entertainment Bw. Dilesh Solank akisaini kitabu cha wageni alipotembelea ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto aliyekaa ni Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo Bibi. Joyce Fissoo na wanaoshuhudia ni Mwanasheria wa Steps Entertainment Cloud Ngalaba na Mkuu wa Uzalishaji Bw. Carlos John.

TEASER JOTO LA ASUBUHI JUMANNE NOVEMBER 15, 2016

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu yatoa notisi ya siku 30 kwa wadaiwa sugu

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul Razaq Badru akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wadaiwa sugu katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari, MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaadizi wa Mawasiliano wa Bodi hiyo Bw. Cosmas Mwaisobwa.

Na: Frank Shija, MAELEZO

Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kupewa notisi ya siku thelethini (30) wawe wameanza kulipa madeni yao kabala hatua zaidi hazijachukuliwa dhidi yao.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul – Razaq Badru alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO kuhusiana na wadai sugu leo Jijini Dar es Salaam.

Badru amesema kuwa notisi hiyo inawalenga wanufaika wa waliokopeshwa na muda wa mataraji ukapita bila wao kuwasilisha taarifa zao na kulipia madaeni ya mikopo ya eleimu ya juu waliyokopeshwa tangu mwaka wa masomo 1994/95.

Alisema kuwa jumla ya wanufaika 93,500 walinbainika na kupelekewa Ankara ya madeni yao ili waweze kulipa hata hivyo kati yao ni wadaiwa 81,055 ndiyo wanaendelea kulipa madeni yao.

Aidha Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa wapo wadaiwa sugu takribani 142,470 wenye mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 239 hawajajitokeza wala kuanaza kulipa mikopo yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Dkt. Abdul Mussa amesema kuwa urejeshaji wa mikopo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi bilioni 25 zimerejeshwa hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu.

Hatua hii ya kutoa notisi ndani ya siku thelathini inafuatia kutokana na kuvunjwa kwa sheria namba ya 19A (1) cha sheria za Bodi ya Mikopo Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ambapo pamoja na hatua hiyo Bodi imeazimia kuchukua hatua nyingi za ziada.

Hatua hizo ni pamoja na kuyatangaza majina ya wadaiwa sugu hadharani ili waajiri, wadhamini wao na wadau wengine wenye taarifa za wasugu waziwasilishe,kuwasilisha majina ya wadaiwa kwenye taasisi zinazotunza taarifa za ukopaji na kukamilisha taratibu za kuwafikisha mahakamani kwa hatua za kisheria.

QATAR AIRWAYS YACHANGIA MADAWATI 100 SHULE YA MSINGI CHANZIGE B WILAYANI KISARAWE

$
0
0
Kampuni inayotoa huduma ya usafirishaji wa anga hapa nchini Qatar Airways kwa miongo kadhaa sasa, kupitia safari zake za Dar es Salaam, Kirimanjaro na Zanzibar imechangia madawai 100 katika shule ya msingi Chanzige B, iliyopo wilayani Kisarawe jijini Dar es Salaaam. Hiyo ikiwa ni sehemu ya mradi wa kusaidia juhudi za serikari kupitia mpango wa kuondoa uhaba wa madawati nchini kwa shule za Msingi pamoja na Sekondari, lakini pia wakiwa kama sehemu ya kurudisha shukrani kwa jamii.

Makabidhianao hayo yamefanyika katika viwanja vya shule ya Chanzibe B,ambayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali, akiwemo Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo, Meneja wa Qatar Airways Tanzania, Basel Haydar, pamoja na wafanyakazi wa Qatar Airways na wawakilishi kutoka ofisi ya Doha pamoja na Daktari Amon Mkoga, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Amon Mkoga Foundation, Bodi ya wakurugenzi na walimu wa shule ya msingi Chanzige B.
Wakati wakikabidhi mchango huo wa madawati, Meneja wa Qatar Airways Tanzania Basel Haydar, amemueleza Naibu Waziri kuwa Qatar Airways itaendelea na mpango wa kusaidia jamii kwa kushirikiana na Serikali katika kuinua na kuimarisha sekta ya elimu nchini.

Akiongea baada ya kupokea madawati hayo, Naibu Waziri Jafo ameipongeza kampuni ya Qatar Airways kwa msaada wanaouonyesha, “Nawapongeza Qatar Airways kwa msaada huu, hii inaonyesha wazi kuwa ni jinsi gani wanavyothamini elimu ya watoto wetu na mazingira kwa ujumla, ambayo yanajumuisha madawati haya waliyokabidhi.

Elimu nzuri ndiyo itakayopeleka kizazi chetu katika uzalishaji mkubwa na kukuza uchumi wa nchi yetu”

 Mwalimu Mkuu wa Chanzige B, Pius Karinga, ametoa shukurani kwa kusema kuwa “Tunaamini maboresho ya shule na mazingira ya kazi kwa Walimu nchini ni chachu ya kuongeza ufanisi wa kuimarika kwa Mwanafunzi ambaye atakuwa na uwezo imara na kuwa sehemu ya uzalishaji muhimu wa rasilimari watu nchini, hivyo basi tunatoa shukrani zetu zadhati kwa Qatar Airways kwa mpango wao wa kuboresha mazingira yetu”.

Qatar Airways ilichagua kushirikana na Daktari Amon Mkonga Foundation katika kusaidia sekta ya elimu nchini kwa kuwa wafanyakazi na sekta zingine mbalimbali wamepatikana kutokana na mazingira mazuri ya kujifunzia. Hivyo msaada uliotolewa leo ni sehemu ya kuisaidia na kuzalisha kiwango kikubwa cha rasilimali watu katika sekta mbalimbali hapo baadae.

MAKAMU WA RAIS MH. SAMIA SULUHU HASSAN ASAFIRI NA NDEGE YA AIR TANZANIA KUELEKEA JIJINI MWANZA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa tiketi ya kusafiria ya Shirika la Ndege la Air Tanzania, kutoka kwa Waziri wa ujenzi uchukuzi na Mawasiliano Professa Makame Mbarawa, kabla ya kusafiri na Ndege hiyo kuelekea Jijini Mwanza kwa ziara ya kikazi, leo Novemba 14, 2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na marubani na wahudumu wa ndege mpya aina ya Bombardeir Q 400 baada ya kukabidhiwa ticket ya kusafiria na Waziri wa ujenzi uchukuzi na Mawasiliano Professa Makame Mbarawa kulia leo Novemba 14, 2016 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ambapo Makamu wa Rais alisafiri na ndege hiyo kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku nne.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na vyombo vya habari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, Jijini Dar es salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipungia wakati akiindia ndani ya Ndege ya Air Tanzania aina ya Bombardeir Q 400.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia baadhi ya Abiria waliokuwemo ndani ya Ndege hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na wasaidizi wake wakati wa safari hiyo.

TIC YAONYA MATUMIZI YA MAJINA YA TAASISI NA VIONGOZI BILA RIDHAA KWENYE MAKONGAMANO


MTAA KWA MTAA YA MICHUZI TV NA MAMBO MBALIMBALI YA MJI WA IRINGA

NEWS ALERT: DPP amwondolea mashtaka mbunge wa sumve Mhe Richard ndassa

$
0
0
Na Mwene Said, 
Globu ya Jamii, Dar es Salaam.

Hatimaye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imemwachia huru Mbunge wa Sumve (CCM),  Richard Ndassa (56) baada ya upande wa Jamhuri kuomba kumuondolea kesi  kushawishi na kuomba  rushwa ya Sh.milioni 30.
Ndassa alikuwa anakabiliwa na shtaka la kushawishi na kuomba rushwa kutoka  kwa Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Felichesmi Mramba.
Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dennis Lekayo leo aliwasilisha maombi ya kumwondolea Ndassa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa.

Lekayo alidai kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), ameona hana nia ya kuendelea na mashtaka yaliyopo mahakamani dhidi ya mshtakiwa chini ya kifungu cha 98 (a) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).
Aidha kwa mujibu wa kifungu hicho kinampa mamlaka DPP ya kumwondolea mashtaka mtuhumiwa kabla ya kusikiliza ushahidi lakini anaweza kukamatwa na kushtakiwa upya.
Hakimu Nongwa alisema kwa kuwa upande wa Jamhuri umeomba kumwondolea mshtakiwa mashtaka na kwamba hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo, mahakama yake imekubali ombi hilo.
"Mahakama hii inamwachia mshtakiwa chini ya kifungu cha 98 (a) kama upande wa Jamhuri ulivyowasilisha maombi yao dhidi ya mshtakiwa" alisema Hakimu Nongwa.
Mapema mwaka huu,  Mbunge huyo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji  ya Umma, alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa shtaka la kushawishi na kuomba rushwa ya Sh. milioni 30.
Katika kesi ya msingi, Lekayo alidai kuwa Machi 13, mwaka huu, jijini Dar es Salaam,  Ndassa aliomba rushwa Sh.milioni 30 kutoka kwa Mramba.
Ilidaiwa kuwa aliomba rushwa ili awashawishi wajumbe wenzake wa kamati hiyo  watowe mapendekezo mazuri  katika mahesabu ya fedha ya Tanesco kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
Katika shitaka la pili, mwakilishi huyo wa wananchi siku ya tukio la kwanza pia aliomba rushwa ya huduma ya umeme kwa kumshawishi Mramba atowe huduma hiyo kwa ndugu wa mbunge huyo Matanga Mbushi,Richard Ndassa na rafiki wa ndugu yake Lameck Mahewa.
Mbunge huyo alikana mashitaka yake na alikuwa nje kwa dhamana.

Muhimbili Yawapima Kisukari Wafanyakazi Wake LEO

$
0
0
Siku ya Kisukari Duniani- Muhimbili Yawapima Kisukari Wafanyakazi Wake LEO Na Neema Mwangomo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Leo imeadhimisha siku ya kisukari duniani kwa kuwapima kisukari wafanyakazi wa hospitali hiyo. 
 Leo wafanyakazi wa hospitali hiyo walikuwa wakipimwa kisukari na uzito pamoja na kupatiwa ushauri jinsi ya kupunguza uzito kwa wale waliobainika kuwa na uzito mkubwa. Wafaanyakazi waliojitokeza leo ni madaktari, wafanyakazi kurugenzi za utawala, wauguzi na wanafanyakazi mbalimbali wa hospitali hiyo. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo Profesa Lawurence Museru alikuwa mstari wa mbele katika kuwashawishi wafanyakazi kupima kisukari. 
 Naye Mkuu wa Kitengo cha Kisukari, Dk Mohamed J. Mohamed amesema Muhimbili imeona kuna umuhimu wa kupima kisukari kwa wafanyakazi wake kutokana na kubanwa na shughuli mbalimbali na hivyo mara nyingi wamekuwa wakikosa nafasi ya kupata huduma za afya. 
 “Tumeona ipo haja ya kutoa huduma hii kwani kuwa mfanyakazi wa Muhimbili haimaanishi kwamba upo salama kiafya hivyo tunafanya hivi ili wapate nafasi ya kupia kisukari,” amesema Dk Mohamed.
 Dk Elias Mwandwani akimpima kisukari mmoja wa wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Leo.
 Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akiwa amevaa beji ikiwa ni ishara ya kuwamasisha wafanyakazi wa hospitali hiyo kupima kisukari leo
 Juma Selemani akipima uzito Leo kabla ya kupima kisukari  katika Hospitali  hiyo leo.
 Dk Faraja Chiwanga wa Muhimbili akimpima kisukari Juma Selemani katika hospitali hiyo Leo.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni, ‘Kuwa Makini na Kisukari Pima Kujikinga.’ Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU WA AFRIKA KUSINI THABO MBEKI IKULU

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mwenyeji wake Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

WASANII 202 WA MIKOA YA KANDA YA ZIWA WAJIUNGA NA PPF JIJINI MWANZA.

$
0
0
WASANI  202 wa mikoa ya kanda ya ziwa wajiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF kupitia mfumo wa uchangiaji wa hiyari wa Wote Scheme jijini Mwanza wakati wa warsha fupi ya kuwajengea uwezo wa sanii  iliyofanyika katika ofisi ya mkuu wa Mkoa  jijini Mwanza.

Akizungumza wakati wa kuwakabidhi kadi za uanachama wasanii hao Meneja wa PPF Kanda ya ziwa, Meshack Bandawe amesema wasanii mbali mbali wamejiunga katika mfumo ‘Wote Scheme’moja kwa moja   katika  Mfuko huo ambapo watapata mafao yanayotolewa na PPF 
moja kwa moja katika mfumo wa Wote Scheme ambapo mtaweza kupata huduma ya matibabu baada ya kuchangia miezi 3, 
 faida ni kupata mikopo ya biashara,  pamoja na mafao ya uzeeni.

Amewaasa wananchi wote wa mikoa ya kanda ya ziwa ambao hawapo katika sekta rasmi kama madereva wa Tax, wajasiliamali, wakulima, wavuvi, wafanyabiashara na madereva wa bodaboda wajiunge na mfuko wa PPF ili waweze kunufaika na mafao mbali mbali.

Wasanii hao ni kutoka Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Tabora na  Geita, pamoja na kupata elimu kutoka PPF vilevile washiriki walipata fursa ya kujengewa  uwezo wa kuhariri kutengeneza Miswada ya filamu pamoja na umuhimu wa kujiunga na mifuko ya uchangiaji wa hiari kwa ajili ya manufaa yao wenyewe pamoja na familia zao.  

Kwa upande wa wasanii wamefurahia sana mfumo wa Wote scheme kwani umekuja wakati sahihi ambapo Mfumo huu wa PPF utawasadia kwa kuwezesha kupata mikopo ya maendeleo na Bima ya afya, hivyo kuwafanya kuendelea na maisha yao.
Meneja wa PPF Kanda ya ziwa, Meshack Bandawe akimkabidhi mfano wa kadi ya uanachama wa Mfuko wa PPF, Msanii wa Filamu jijini Mwanza, Mwanaharusi Hela ambapo zaidi ya wasanii 202 walipojiunga na  na mfuko wa PPF mwishoni mwa wiki katika warsha ya kuwajengea uwezo wasanii wa mikoa ya kanda ya ziwa jijini Mwanza leo.
Meneja wa PPF Kanda ya ziwa, Meshack Bandawe akizungumza na baadhi ya wasanii  wa mikoa ya kanda ya ziwa mara baada ya kuwakabidhi kadi za uanachama mara baada ya kujiunga na mfuko huo mwishoni mwa wiki.
 Meneja wa PPF Kanda ya ziwa, Meshack Bandawe pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa PPF akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii waliojiunga na  PPF kupitia mfumo wa Wote Scheme.
 Msanii wa filamu  Mwanaharusi Hela akizungumza jinsi alivyofurahishwa na  mfumo wa wote scheme kupitia PPF ambapo utamnufaisha kwa kupata huduma ya afya  na mkopo wa maendeleo.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images