Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 141 | 142 | (Page 143) | 144 | 145 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde kutoka mkoani Mtwara,inaeleza kuwa kumezuka vurugu kubwa kati ya wananchi na Jeshi la polisi hali iliyopelekea Jeshi hilo kulazimika kutumia mabomu ya machozi kwa ajili ya kuwatawanya wananchi hao.

  Chanzo cha vurugu hizo inadaiwa kuwa ni mara tu baada ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kusomwa Bungeni na kueleza kuwa mradi wa gesi Mtwara utatekelezwa bila kutaja faida za moja kwa moja kwa wananchi hao.

   Wananchi hao walianzisha vurugu leo huku wakiwa na kauli mbiu yao isemayo "Gesi haitoki hata kwa bomba la peni". Inaelezwa kuwa kuna kituo cha mafuta cha Total kimechomwa moto wakati wa vurugu hizo. Katika kukabiliana na vurugu hizo.

  Globu ya Jamii inaendelea kufuatilia tukio hilo na tutaendelea kupeana taarifa kadri zitakavyokuwa zikitufikia.

  0 0

  Mkutano unaozungumzia masuala ya uhuru na usalama wa mtandao kwa maendeleo ya Dunia umeaza leo mjini stockholm. Mkutano huo ambao umeandaliwa na Wizara ya mambo ya Nje ya Sweden umefunguliwa leo MEI 22, 2013 na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden Hon. Carl Bret.

  Mkutano huu muhimu ambao unakutanisha wataalamu wa masuala ya Internet na (policy makers) kutoka nchi zaidi ya Tisini na Tano(95) unazungumzia mambo muhimu kuhusiana na uhuru wa Mtandao ambao unahitaji kulindwa na kuheshimiwa na bila kusahau Usalama wa raia na maendeleo yao.

  Mkutano huu wa siku mbili utazungumzia changamoto zilizopo ikiwa na ukweli kwamba kuna baadhi ya serikali za baadhi ya nchi duniani zimekuwa zikitaka kuwa na (control) na maamuzi makubwa kuhusiana na uhuru wa Mtandao(Internet) kwa sababu zao binafsi kwa kisingizio cha usalama au kulinda usalama wa raia.

   Mkutano unajadili mambo ya usalama na sera maalumu ambazo zitakuwa zinakubalika zenye kuheshimu uhuru wa habari.
  Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden Hon. Carl Bret akifungua mkutano wa STOCKHOLM INTERNET FORUM ON INTERNET FREEDOM FOR GLOBAL DEVELOPMENT - SIF13.
  Bw. Wilfred Warioba akiwa na Fadi Chehadé, na Raisi na CEO wa (Internet Corporation for Assigned Names and Numbers, ICANN).
  Dr. Dorothy Okello form Makerere University and Founder of WOUGNET, Mr. Wilfred Warioba from Commission for Human Rights and Good Governance-Tanzania, Mr. John Ulanga, Executive Director, the Foundation for Civil Society.
  Kutoka kushoto Dr. Jabir Bakari, CEO wa e-Governance-Tanzania, Dr. Dorothy Okello form Makerere University and Founder of WOUGNET, Mr. Wilfred Warioba from Commission for Human Rights and Good Governance-Tanzania, Mr. John Ulanga, Executive Director, the Foundation for Civil Society.
  Kutoka kushoto Mr. John Ulanga, Executive Director, the Foundation for Civil Society Mr. Wilfred Warioba kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Dr. Jabir Bakari, CEO wa e-Governance-Tanzania.
  Bw. Warioba kutoka Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora, akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden Mhe. Carl Bildt.

  0 0

  Makamu wa Rais wa TBF Ndg. Phares Magesa akiwa na Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania Albert Sokaitis mara baada ya mazungumzo ya kupanga mikakati ya kuendeleza Michezo wa Kakapu Tanzania, VIJANA wengi watafaidika na Mpango huu wa mafunzo yatakayalenga kunyanyua kiwango Cha Michezo nchini kupitia Kocha huyu. Kutokana Na mpango huu baadhi ya vijana wetu watapata nafasi za kwenda kusoma na kucheza kikapu katika vyuo via Marekani, Vijana wetu muwe tayari... Chamsingi Ni kuwa Na Uwezo Mzuri wa Michezo na pia kuzingatia masomo (shule).

  0 0

  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akizungunza na waandishi wa habari, leo katika ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Amezungumzia masuala mbalimbali yaliyojiri kwenye kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichomalizika jana. (Picha na Bashir Nkoromo).


  0 0


  Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limemteua mwamuzi kutoka Afrika Kusini kuchezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na wenyeji Morocco (Lions of the Atlas).

  Mechi hiyo ya kundi C itachezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech, Morocco kwenye Uwanja wa Grand kuanzia saa 3 kamili usiku kwa saa za Morocco. Mwamuzi atakayechezesha mechi hiyo ni Fraser Daniel Bennett.

  Bennett atasaidiwa na Thusi Zakhele Siwela pia wa Afrika Kusini, wakati mwamuzi msaidizi namba mbili atakuwa ni Marwa Range kutoka Kenya. Mwamuzi wa akiba (fourth official) ni Lwandile Mfiki wa Afrika Kusini.

  Kamishna wa mechi hiyo ni Robert Mangollo-M’voulou wa Gabon wakati mtathimini wa waamuzi (referee assessor) ni Charles Masembe kutoka Uganda.

  Taifa Stars ambayo iko chini ya Kocha Kim Poulsen, na ikidhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari iko kambini katika hoteli ya Tansoma ikiendelea kujinoa kwa ajili ya mechi hiyo ambapo kabla itajipima na Sudan (Nile Crocodiles) Juni 2 mwaka huu jijini Addis Ababa, Ethiopia.

  Ratiba ya mazoezi kwa timu hiyo ni kama ifuatavyo;

  Mei 22                 Saa 10 jioni                             Uwanja wa Karume
  Mei 23                 Saa 1 asubuhi na Saa 10 jioni   Uwanja wa Karume
  Mei 23                 Saa 10 jioni                             Uwanja wa Karume


  Mei 25                 Saa 1 asubuhi na Saa 10 jioni     Uwanja wa Karume
  Mei 26                 Saa 3 asubuhi                            Uwanja wa Karume

  0 0


  0 0


  0 0
 • 05/22/13--08:16: kutoka bungeni dodoma leo
 • Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof. Sospeter Muhongo akilionyesha bunge moja ya michoro ya miradi mbalimbali ya umeme wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti Bungeni leo.
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Mathias Chikawe akiangalia moja ya michoro ya mradi wa umeme wakati bajeti ya Nishati na Madini ikiwasilishwa Bungeni leo.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Simba Chawene akizungumza jambo na mbunge wa Mtwara mjini mhe. Hasnain Murji.
  Mbunge wa Peramiho Mhe. Jenista Muhagama akizungumza na Mhe. Ally Kessy (Mb. Mpanda Kaskazini) katika kikao cha bunge leo.
  Mbunge wa Ubungo Mhe. John Mnyika akisoma hotuba ya Kambi ya Upinzani Bungeni ya Nishati na Madini leo.
  Mbunge wa Same Mashariki Mhe. Anne Kilango Malechela akichangia hoja katika hotuba ya bajeti ya Nishati na Madini.PICHA NA ZAWADI MSALLA-MAELEZO.

  0 0


    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali, yatakayofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yamefunguliwa leo. Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR
  Baadhi ya washiriki  wa maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya kufungua rasmi maonyesho hayo ya siku tatu katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Maofisa wa mfuko wa PPF, kutoka (kushoto) ni Meneja wa Kanda ya Ilala, Evans Musiba, Meneja Uhusiano, Lulu Mengele na Ofisa Masoko, Sereki Michael, wakati alipotembelea katika banda la maonyesho la PPF, leo kwenye maonyesho ya Nane ya Vyuo Vikuu kutoka nchi mbalimbali yanayofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi alianza ziara yake Same kwa kufika ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Same Mwalimu Herman Kapufi kujitambulisha.
  Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi na ujumbe wake wakipitia baadhi ya kurasa katika kitabu hicho.
  Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Donat Mnyagatwa(aliyenyoosha mkono) akimuonyesha Katibu Mkuu Bi. Maimuna Tarishi (suti nyeusi) eneo lenye mgogoro wa mpaka katika Hifadhi ya Mkomazi. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Malikale Donatius Kamambaa; Kaimu Mkurugenzi wa Mipango wa TANAPA Dk. Ezekiel Dembe na Mkurugenzi wa Utumishi Wizara ya Maliasili na Utalii Said Msambachi.
  Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Donat Mnyagatwa akitoa Taarifa ya Hifadhi ya Mkomazi kwa Katibu Mkuu Maliasili na Utalii pamoja na ujumbe wake.
  Watumishi wa Hifadhi ya Taifa Mkomazi wakiwa makini kumsikiliza Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi alipowatembelea.
  Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi (wa pili kulia) akizungumza na watumishi wa Hifadhi ya Mkomazi. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Malikale Donatius Kamamba, Mkuu wa Hifadhi ya Mkomazi Donat Mnyagatwa na Mkurugenzi wa Utumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Said Msambachi.
  Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi katika picha ya pamoja na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.
  Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi akiangalia mbwa mwitu waliohifadhiwa katika uzio maalum kwa ajili ya kuwalinda Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.Picha zote na mdau Pascal Shelutete.

  0 0

  Baadhi ya vijana wakiuliza maswali toka kwa wataalamu wa COSTECH juu ya Kazi na Mchango wa COSTECH katika elimu ya juu,Sayansi na Teknolojia katika Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es salaam.
  Mfanyakazi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia,Frank Makalla(kushoto) akimuelezea mwanafunzi wa elimu ya Juu kuhusu jinsi COSTECH inavyohusika kuishauri serikali juu ya Mambo yote yanayohusu sayansi,Teknolojia na Ubunifu nchini.

  Moja ya mwanafunzi aliyemaliza kidato cha Sita akipewa ufafanuzi kuhusu Sheria No 7 ya Bunge ya Mwaka 1986 iliyoiunda COSTECH na kulilithi lililokuwa Baraza la Taifa la Utafiti mwaka 1972.

  0 0

  On Sunday 26 May, the Big Brother launch show will come alive when multiple award winning musicians from Nigeria, Kenya and South Africa take centre stage. The big night will also see 28 new housemates being revealed to audiences in over 50 African countries for season 8 of Big Brother Africa, The Chase.

  With the live show screening from 19:00 CAT on AfricaMagic, AfricaMagic Entertainment, AfricaMagic World as well as on DStv channel 197 and 198. Audiences can look forward to sassy and upbeat tunes from Kenya’s very own award winner, STL.

  Boasting hit songs such as "Take My Time" , "Hula Hoop", "Bad as I Wanna Be", the singer, songwriter and rapper, also recipient of awards from the Kisima Awards, Clops Awards and Jeermaan Awards, promises to deliver an unforgettable and lasting performance with her distinct pop, soul and rap sound.

  Hailing from Nigeria, musical heavy weights Don Jazzy, D’ Prince and Wande Coal are also set to grab audiences with their energetic and charming personas. Multi award-winning record producer, singer-songwriter and musician Don Jazzy, will join stars in their own right, D’ Prince and Wande Coal on stage for their collaborative performance.

  These chart topping hit makers from Mavin Records are also best known for songs such as “I like What I See”, “Bumper 2 Bumper” and “Who Born the Maga”. The continent can expect a sensational performance that will ignite the Big Brother live show stage.

  Last but not least, one of South Africa’s leading Afro Pop music groups, Mafikizolo will also serenade audiences with their soulful and rhythmic tunes on the big launch night.

  With several albums and awards under their belt, the duo has brought fans far and wide, dance-floor filler hits such as ”Sibongile”, “Ndihamba Nawe”, “Nisixoshelani” and most recently “Khona”. Their performance on the Big Brother stage is sure to evoke dance moves, reminding audiences why the chart topping group remains pioneers in their field with musical experience spanning over 15 years.

  The line-up will also include a slot for some comic relief from Kenyan stand-up comedian Daniel Ndambuki, popularly known as Churchill. The highly talented entertainer has also become a household name with his TV show called “Churchill Live”.

  In Addition to the live screening of the launch show, the good news is that the show will also concurrently be streamed live to audiences across Africa on the Big Brother website, www.bigbrotherafrica.com. All you need to access the live stream is a personal computer and internet connection.

  With less than a week to go, be sure not to miss the jam packed, highly anticipated Brother Africa The Chase live launch show. Thereafter Africa’s biggest reality series will be screened live for 91 days, 24/7 on DStv channels 197 and 198 while GOtv audiences will be able to see highlights on AfricaMagic World.

  0 0

  MTANZANIA mwenzetu marehemu Shaaban Robert anaandika;
  ” Wasadikika wana desturi ya kutafuta fimbo baada ya kuumwa na nyoka. Tumekwisha umwa na nyoka kwa matendo yetu mabaya ya zamani.

  Nyoka mwenyewe amekwishakimbia. Hapatikani kwa kujilipiza kisasi, lakini, sumu yake imebakia katika jeraha tulilolipata. Sasa, shauri lililo jema ni kuzuia sumu hii isienee miilini mwetu ikaleta kifo.
  Maovu yana hatari kubwa kukaa kati yetu. Tumedumu nayo kwa muda mrefu. Hayakutuletea faida ila hasara, huzuni na kilio siku zote.”- Shaaban Bin Robert.


   Ndugu zangu,
  Yanayotokea Mtwara yanatuletea mashaka kama taifa.  Linalohitajika sasa si tamko la Serikali tu, bali, tamko letu Watanzania kwenye mioyo yetu, kwamba, pamoja na haki yetu ya kimsingi ya kudai  haki, lakini, lililo la hekima na busara ni kutumia njia mujarab za kuitafuta haki hiyo. 

  Na njia hiyo haiwezi kuwa ni matumizi ya nguvu ikiwamo kufanya vurugu. Hivyo, kufanya maovu ikiwamo kutoa roho za wenzetu na uharibifu wa mali, iwe imefanywa na wananchi au Serikali.

   Kama Watanzania huu ni wakati wa kufikiri kama taifa. Hii ni Nchi Yetu. Huu si wakati wa kufikiri kwa mitazamo ya kiitikadi au kiimani. 

  Yanayotokea Mtwara yana madhara kwa nchi nzima, na yakiachwa bila kupatiwa ufumbuzi  wa haraka, yatatawanya sumu mahala pengine pia.
   Ni wakati wa Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Chama Tawala, Viongozi wa Vyama Vya Upinzani , Viongozi wa kidini na kwa kuwashirikisha wazee wa Mtwara, kutoa matamko yatakayosisitiza umuhimu wa kutumia majadiliano  katika kupata ufumbuzi wa tatizo lililopo.

   Tukumbuke, kuwa nchi yetu ina mipaka, hivyo basi, ina maadui pia. Tusipotanguliza hekima na busara, yumkini tunaweza kutoa nafasi kwa maadui kutugombanisha zaidi. Na hivyo  ikawa hasara zaidi kwetu , na faida kwa wengine.

   Hakika,tunaweza kuyamaliza yetu kwa mazungumzo. Tuianze kazi hiyo sasa.

   Maggid Mjengwa,
  Iringa.

  0 0

  Balozi wa Tanzania BENELUX na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai yenye rangi ya taifa) akiendesha Mkutano wa Wadau wa Ushikirikiano kwa Manufaa ya Wote (Smart Partnership) wa Brussels. Kushoto kwa Balozi Kamala ni mhe. Alhaji Muhammad Mumuni Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pacific. Kulia ni Dr Smith Mihela Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Ushirkiano kwa Manufaa ya Wote. Mkutano umefanyika leo Brussels.

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli(Wanne kushoto),Waziri wa Fedha Mgimwa(kushoto),Mwakilishi wa Balozi wa Japan Bwana Kazuyoshi Matsunaga(Wapili kushoto),Mwakilishi mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) Bi.Tonia Kandiero(Wapili kulia) pamoja na mbunge wa Isimani William Lukuvi wakikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa Barabara ya Dodoma Iringa sehemu ya Migori-Fufu Escarpment na Migori Iringa leo mchana.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akiwahutubia wananchi waliohudhuria uzinduzi wa ujenzi wa Babarabara ya Dodoma Iringa leo mchana.
  Baadhi ya Wananchi walihudhuria uzinduzi wa ujenzi wa Barabara ya Dodoma Iringa eneo la Migori leo mchana(picha na Freddy Maro)

  0 0

  JESHI la Polisi Mkoani Morogoro limefanya msako mkali katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Morogoro na wilaya ngingine za Mkoa huo na kufanikiwa kuwatia mbaroni watu zaidi ya 33 wakituhumiwa kufanya makosa ya uharifu na utengenezaji wa pombe haramu ya gongo na usafisishaji wa bangi.

  Askari Polisi wakiongozwa na Makamada kuanzia mei mosi mwaka huu hadi Mei 22, walifanya msako huo walianzisha msako huo katika maeneo ya Kata ya Lukobe, Kingolwira na maeneo mengine na kufanikiwa kukamata pombe haramu ya gongo lita 600, mitambo 22 , vyombo vya kupikia 124 , madumu 60 na magunia manene ya bangi.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilongike , alisema hayo Mei 22, mwaka huu alipozungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake na kuwaonesha vitu hiyo vilivyowekewa eneo la viwanja vya Ofisi ya Polisi Mkoa.

  Hata hivyo alisema katika opareshani hiyo , Polisi imefanikisha kukamatwa kwa meno vipande 320 vya Kiboko na meingine mawili ya Nyati katika Wilaya ya Kilombero.

  Katika hatua nyingine Polisi imefanikiwa kumtia mbaroni askari wa zamani mwenye cheo cha Koplo Usu Omari Abdallah ambaye alifukuzwa a uaskari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) Kikosi cha Ruvu, Mkoani Pwani baada ya kukutwa akiwa na sare ya Jeshi hilo.

  Hatua ya kukamatwa kwake ilitokana na taarifa ya raima mwema na kwamba mtuhumwa alikuwa akiishi eneo la Msamvu , Manispaa ya Morogoro

  Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, askari hiyo wa zamani wa JWTZ licha ya kufukuzwa kazi aliendelea kubaki na sare za Jeshi hilo ‘ combati’ kinyume na sheria za Majeshi na kuitumia katika kufanya uharifu wa kutampeli wananchi.

  Hata hivyo Kamaanda huyo wa Mkoa , alisema Opereshani hiyo ni endelevu na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano ili kutokomeza mambo hayo ya kiharifu mkoani Morogoro.
  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilongile ( mwenye fimbo) akiangalia mifuko ya mbolea iliyobadirishwa kwa baadhi kuwekwa mbolea Minjingu katika mifuko ya mbolea yenye nembo ya aina ya CAN baada ya kuikamata hivi karibuni katika ghala la mfanyabiashara wa Duka la Pembejeo za kilimo eneo la Nane Nane , Mjini Morogoro.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilongile akiwaonesha Waandishi wa Habari ( hawapo pichani) baadhi ya vitu vya aina mbalimbali ikiwemo mitambo ya kupinga pombe haramu ya gongo, mapipa , madumu na mifuko ya mbolea iliyochakachuliwa, viroba vya bangi na sare moja ya JWTZ ,ambayo kwa pamoja vilikamatwa na Polisi wakati wa oparesheni iliyioanza Mei mosi mwaka huu hadi Mei 22, mwaka huu mkoani Morogoro.
  Baadhi ya Askaari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro walioshiriki oparesheni ya ukamataji wa mitambo na mapipa ya gongo.Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii,Morogoro.

  0 0

  Ujumbe wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) uko nchini Rwanda kubadilishana ujuzi na uzoefu na Rwanda kuhusu utekelezaji wa mradi wa kurahisisha na kuwezesha biashara (Trade Facilitation) kwa kutumia TEHAMA - Electronic Single Window System. Muda mfupi ujao TPA itaanza utekelezaji wa mradi huo kwa niaba ya wadau wote wa sekta ya usafirishaji, Forodha, wafanyaniashara na wadau wote wa Tanzania. Ujumbe huo wa Tanzania unaongozwa na Mkuu wa mradi na Kaimu Mkurugenzi wa idara ya TEHAMA-TPA Ndg. Phares Magesa wa kwanza kushoto, wengine ni Mathayo Ntandu, Jesse Shali na Kilian Chale ambao ni maofisa wakuu TPA.

  0 0


  Menejimenti ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unapenda kuutaarifu umma wa Watanzania kuwa tangazo la nafasi za ajira ambalo limewekwa katika mtandao www.eastafricajobscarieer.comni  batili. Mtandao huo ulichapisha tangazo hilo bila ridhaa ya Menejimenti ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya hauna mkataba wowote wa kibiashara na mtandao huo.

  Aidha, tangazo hilo ni nakala ya tangazo la ajira ambalo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ulilitangaza katika magazeti ya Mwananchi, Nipashe, na Daily News tarehe 07, 10 na 14 Februari, 2012 na mchakato wa kujaza nafasi zilizotangazwa ulishakamilika.

  Menejimenti ya Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya inawaomba radhi wote ambao wamepata usumbufu kutokana na tangazo hilo.

  Limetolewa na:
   Mkurugenzi Mkuu,
  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,
  S.L.P. 11360,
  DAR ES SALAAM.

  0 0


  Jana hapa London kulikuwa na kampeni ya kuchangisha mfuko wa kusaidia watoto wenye magonjwa ya kansa
  Shughuli hiyo iliandaliwa na Mama Balozi Mrs Joyce Kallaghe na kuhudhuriwa na watu wengi sana yakiwemo makampuni mbali mbali makubwa UK ambapo Serengeti Freight WAZEE WA KAZI walikuwa wadhamini wa hafla hiyo.
  Wazee wa kazi wakiwa  pamoja na Mheshimiwa Balozi  
  Kulikuwa na mnada na bahati nasibu ambapo vitu bali mbali vilinadiwa kutunisha mfuko
  Chris Lukosi alijishindia zawadi ya miwani ya Gold 
  Dada mtanzania alijishindia tiketi ya VIP kwenda kumuona Alicia Keyys pale O2 arena
  Mheshimiwa Balozi akiwa na muandaaji wa shughuli mama Balozi

  0 0

  Rais Jakaya Kikwete akiongea na wachezaji wa timu ya mpira ya Taifa, Taifa Stars leo Ikulu jijini Dar es salaam alipokutana nao kuwapa hamasa waweze kupata ushindi katika mchezo wao dhidi ya Moroco utakaochezwa Juni 7, na michezo mingine ikiwa ni hatua ya kuiwezesha timu hiyo kukata tiketi ya kushiriki mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014.
  Rais Jakaya Kikwete akiwaaga wachezaji wa Timu ya Taifa Stars mara baada ya kukutana nao leo Ikulu Jijini Dar es salaam kuwahamasisha washinde mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Moroco utakaofanyika June 7 ikiwa ni sehemu ya Taifa Stars kutafuta ticketi ya kucheza mashindano ya Kombe la Dunia.
  Meneja wa Timu ya Taifa Stars Bw. Mukebesi akiteta jambo na Kepteni wa Timu ya Taifa Stars Juma Kaseja Ikulu jijini Dar es salaam walipokutana na Rais Jakaya Kikwete.
  Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya Pamoja na wachezaji wa Timu ya Taifa , Taifa Stars, viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
  Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Taifa , Taifa Stars Ikulu jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

  Na. Veronica Kazimoto –MAELEZO.

  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amekutana na timu ya Taifa (Taifa stars) kwa lengo la kuitia moyo katika mechi ijayo kati yake na timu ya Moroco ikiwa ni harakati za Tanzania kutafuta tiketi ya kucheza fainali za kombe la Dunia kwa mara ya kwanza mwaka 2014.

  Rais Kikwete ameiambia timu hiyo kuwa ina uwezo mkubwa wa kusonga mbele kutokana na uwezo mkubwa waliouonesha katika mchezo wao dhidi ya Gambia ambapo walifanikiwa kupata ushindi wa bao 2-0.

  “Maadamu mara ya kwanza mliwashinda Gambia, hakikisheni pia mnapata ushindi dhidi ya Moroco, mkishinda tunafurahi sana na mkishindwa tunanyong’onyea sana,” amesema Rais Kikwete.

  Aidha amempongeza kocha wa timu hiyo Kim Poulsen pamoja na Kamati ya Taifa ya ushindi ya Taifa stars kwa kuisaidia timu hiyo kiasi cha shilingi milioni 30 ikiwa ni mkakati wa kuiongezea nguvu kwa hatua iliyofikia na kuwataka wachezaji kujituma ili kuwafurahisha watanzania ambao hivi sasa wanaipenda timu yao ya Taifa.

  Nae Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fenera Mukangara amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo nchini ili kuondoa changamoto zinazoikabili timu hiyo.

  Kwa upande wake Kocha Poulsen, amemshukuru Rais Kikwete kwa kuwakaribisha na kuwatia moyo ambapo ameahidi kuifundisha vizuri timu hiyo ili kuhakikisha kuwa wanapata ushindi.

  Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake kaptaini wa timu hiyo Juma Kaseja amemshukuru Rais Kikwete na kuahidi kujituma kwenye mazoezi na hatimaye kuibuka washindi kwenye mechi zijazo.

  Taifa stars ambayo inakamata nafasi ya pili katika kundi C inatarajia kucheza ugenini na Morocco mnamo Juni 7 mwaka huu.

older | 1 | .... | 141 | 142 | (Page 143) | 144 | 145 | .... | 3278 | newer