Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU MAJALIWA AONGOZA MAZISHI YA MAREHEMU SAMWEL JOHN SITTA

$
0
0




 Mama Margareth Sitta ambaye ni Mjane wa marehemu Spika mstaafu,  Samuel Sitta akitupa udongo kwenye kaburi la mumewe katika kazishi yaliyofanyika Urambo, Tabora, Jumamosi Novemba 12, 2016.
 Bibi Kagoli Fundikira ambaye ni Mama Mzazi wa marehemu  Spika Mstaafu Samuel Sitta     akitupa udongo kwenye kaburi la mwanae katika mazishi yaliyofanyika Urambo, Tabora  
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mama Mary Majaliwa wakitupa udongo kwenye kaburi la Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta katika mazishi  yaliyofanyika Urambo.
 Mjane wa Marehemu Spika Mstaafu, Margareth Sitta, Mama Mzazi wa marehemu,  na watoto wa marehemu wakigusa jeneza na kushuhudia wakati mwili wa marehemu Samuel Sitta ulipokuwa ukiteremshwa kaburini katika mazishi yaliyofanyika urambo, Tabora.
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Job Ndugai akiweka shada la maua kwenye kaburi la Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta. 

Kwa picha zaidi BOFYA HAPA



Profesa Issa Shivji akizungumzia Mwaka mmoja wa Rais Magufuli

Wanawake wakutana kutathimini mwaka mmoja wa Serikali ya Rais Magufuli

$
0
0
Mwenyekiti wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Profesa Ruth Meena (katikati) akisoma tamko la wanawake kwa wanahabari kuelezea tathini ya mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya tano mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano huo. Wengine ni viongozi na wajumbe wa mkutano huo.

WANAWAKE kupitia Mfuko wa Wanawake Tanzania wamekutaka katika mkutano na kutoa tathimini ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli. Mkutano huo ulioshirikisha wanawake kutoka mikoa mbalimbali umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania, TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa mfuko huo, Profesa Ruth Meena aliipongeza Serikali ya Dk. Magufuli kwa mafanikio ilioanza kuonesha katika ukusanyaji na usimamizi wa mapato pamoja na mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa huku akiiomba Serikali kutambua pia kwa vitendo mchango wa wanawake katika ujenzi na maendeleo ya nchini. Aliyekuwa mgombea nafasi ya urais wa Chama cha ACT – Wazalendo, Anna Mghwira (kulia) ambye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho taifa akichangia mada katika mkutano wa wanawake ulioandaliwa na Mfuko wa Wanawake Tanzania. Baadhi ya washiriki katika mkutano huo wakijadiliana masuala anuai. Mkutano huo ulioshirikisha wanawake kutoka mikoa mbalimbali umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania, TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa WFT, Mary Rusimbi (kushoto) akichangia mada katika mkutano huo.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WAHITIMU CBE WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA AJIRA KWA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO VIDOGO.

$
0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amewataka wahitimu 1,811 wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) waliotunukiwa stahili zao katika Fani mbalimbali kwa mwaka 2016 kuchangamkia fursa za ajira zilizopo nchini kwa kuanzisha makampuni na viwanda vidogo vidogo vitakavyowawezesha kujiajiri na kuajiri wengine. 
 Akizungumza katika mahafali ya 51 ya chuo hicho jijini Dar es salaam Mhe.Mwijage amesema kuwa makampuni na viwanda vidogo vidogo watakavyoanzisha vitatumika kuzalisha bidhaa mbalimbali zenye ubora ambazo zitauzwa kote duniani hivyo kukuza uchumi wa nchi na kuwapatia ajira ya uhakika. 
 Amesema Serikali ya Tanzania inapenda kuwaona Wawekezaji wengi wa Kitanzania wakiingia na kuwekeza kwenye rasilimali mbalimbali zilizopo nchini Tanzania badala ya kuwaachia wageni kwa kuwa inao wasomi waliobobea kwenye fani ya biashara pamoja na ujasiriamali. 
 " Taifa letu limebarikiwa kuwa na fursa nyingi za kujiletea maendeleo, Serikali ingependa kuona wawekezaji wengi wa Kitanzania wakiwekeza kwenye rasilimali zilizopo kwa mfano tunayo gesi, madini, kilimo na na rasilimali nyinginezo nyingi" Amesisitiza Mhe.Mwijage. 
 Amefafanua kuwa Serikali itaendelaea kuwekeza kwenye Elimu ya Biashara kuwawezesha wananchi wengi zaidi kujiajiri na kuajiriwa katika sekta binafsi hasa Biashara.

 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akizungumza na wahitimu 1,811 wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) waliotunukiwa stahili zao katika Fani mbalimbali kwa mwaka 2016 wakati wa Mahafali ya 51 ya chuo jijini Dar es salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi ya CBE Prof.Mathew Luhanga akizungumza na wahitimu wa Chuo hicho wakati wa Mahafali ya 51 jijini Dar es salaam.
 Wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE wakivaa kofia zao mara baada ya kutunukiwa Shahada zao katika fani mbalimbali wakati wa mahafali ya 51 ya Chuo cha Elimu ya Biashara jijini Dar es salaam.
  Wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE wakivaa kofia zao mara baada ya kutunukiwa Shahada zao katika fani mbalimbali wakati wa mahafali ya 51 ya Chuo cha Elimu ya Biashara jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wahitimu wa CBE fani ya wakifurahia mara baada ya kutunukiwa Shahada zao mgeni Rasmi Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mijage. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

maendeleo ya ujenzi wa Markaz Shaafiyatul Azhariya ya Mbezi Salasala Dar es salaam

$
0
0
Alhamdullilah  Siku ya Ijumaa Tarehe 11/11/2016 tumekamilisha kwa sehemu kubwa Uzio wetu wa kulia upande wa kuchukua Udhu Kina Mama. Mungu akipenda litakalo fuata ni kuendeleza Ukuta wa Uzio Mbele ya Mihrab (Kibla ya Msikiti kama inavyo kuonyesha Picha 👇) .

Cement Imebaki mifuko Miwili .
Bajeti ya Ukuta huu wa Kibla ni kama ifuatavyo .
Cement Mifuko 50 @ 1 , 12000×50= 600,000/=
Lori kubwa la Mchanga Mende 300,000.
Nondo 15, @ 15500×15 = 232500.
Gharama za Kukodi Mbao 50,000
Jumla 1,182,500/=
Tafadhali  Toa Sadakatul Jaalia kwa Kumtolea Mzazi wako Ndugu yako na Allah atakupa zaidi .
Toa chochote ulicho nacho na huto jutia kwa ulicho kitoa duniani na kesho akhera . Tunapokea Vifaa .
Waweza wasilisha sadaka yako kupitia TIGO-PESA No 0715800772.
Na Mratibu Msimamizi , GHALIB N MONERO.




 Dua ya shukran kwa kukamilisha kwa sehemu kubwa Uzio  wa kulia upande wa kuchukua Udhu Kina Mama.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yakanusha taarifa kuwa Balozi Omar Ramadhan Mapuri amefariki dunia

$
0
0
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inapenda kukanusha taarifa kutoka Kwenye baadhi ya Mitandao ya Kijamii ikidai kwamba, Mhe. Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Balozi Omar Ramadhan Mapuri (pichani) amefariki dunia. 

Taarifa Rasmi ya Serikali kwamba taarifa hizo ni za uongo na hazina hata Chembe ya ukweli. Mhe. Kamishna Balozi Mapuri yupo hai na afya yake iko vizuri. 
Mheshimiwa Balozi Omar Ramadhan Mapuri ambae kwa sasa ni Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipata matibabu na baada ya kupata huduma kutoka kwa madaktari, Mheshimiwa Balozi Mapuri aliruhusiwa kurejea nyumbani siku ya Jumamosi Novemba 12 baada ya afya yake kuimarika. 

Serikali imesikitishwa na taarifa za uvumi na uzushi uliosambazwa jana na leo kwenye mitandao  ya kijamii, taarifa hizi sio za kweli na tunawaomba wananchi wazipuuze.

Aidha, Serikali inapenda kuvionya vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa za uongo kuhusu viongozi wa Serikali. 

Imetolewa na : 
Dk. Juma Mohammed Salum

Kny Mkurugenzi

Idara ya Habari MAELEZO


Zanzibar

KIVUKO CHA MAGOGONI CHAKUSANYA MILIONI 17 KWA SIKU

$
0
0
Na Theresia Mwami TEMESA

Kivuko cha Magogoni kinakusanya hadi jumla ya shilingi milioni 17 kwa siku za kazi kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa kutokana na kutoa huduma ya kusafirisha abiria, mizigo na magari kwa kutumia vivuko vya MV Magogoni na MV Kigamboni.

Takwimu hizo zimetolewa na Mkuu wa Kivuko cha Magogoni Mhandisi Lukombe King’ombe alipokuwa akitoa taarifa ya kivuko hicho kwa Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu alipotembelea kivuko hicho hivi karibuni.

Mhandisi King’ombe aliongeza kuwa kwa sasa wanakusanya mpaka milioni 17 kwa siku za Juma na kwa siku za mwisho wa wiki yaani Jumamosi na Jumapili kiasi hupungua kidogo kutokana na abiria wengi kutotumia kivuko hicho.

 Aidha Mkuu wa Kivuko cha Magogoni Mhandisi Kin’gombe alimueleza Dkt. Mgwatu kuwa hali ya makusanyo hivi sasa inaridhisha kwani abiria wengi wameanza kurudi kutumia kivuko hicho baada ya kujiridhisha kuwa  MV Magogoni imerudi kutoka kwenye ukarabati mkubwa na sasa inafanya kazi vizuri. 

Kwa upande wake Dkt. Mgwatu alimuagiza Mhandisi King’ombe kuhakikisha kuwa wanaziba mianya yote ya upotevu wa mapato kivukoni hapo ili kuhakikisha wanafikia lengo la kukusanya shilingi milioni 19 kwa siku ambayo ni agizo la Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa alipotembelea kivukoni hapo mapema mwezi Oktoba mwaka huu.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi TEMESA alitembelea na kukagua kivuko cha Magogoni ili kujiridhisha utendaji kazi wa kivuko hicho.
Mhandisi Lukombe King’ombe (kulia) akifafanua jambo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (wa pili kulia) alip tembelea chumba cha mifumo ya kuendeshea Kivuko cha MV. Magogoni.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Dk. Mussa Mgwatu (wa pili kulia) akikagua taarifa za mitambo ya kuongozea Kivuko cha MV Magogoni.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Dk. Mussa Mgwatu (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Kivuko Cha Magogoni Mhandisi Kingo’ombe Lukombe (Kulia), alipotembelea kivuko hicho.

Freddy Supreme Ndala Kasheba bado tunakukumbuka miaka 12 baada ya kifo chako

$
0
0
Hayati Freddy Supreme Ndala Kasheba enzi za uhai wake akitumbuiza maelfu kwa gitaa lake la nyuzi dazani kwenye onesho lililofanyika Bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam akiwa na Orchestra Safari Sound (OSS) "Wana Dukuduku" mwaka 1980.
Angekuwa hai nguli huyu wa muziki leo angekuwa ametimiza umri wa miaka 70 na siku 34. Lakini pamoja na hayo muziki wake bado ungali unapendwa miaka 12 baada ya kifo chake. 
Globu ya Jamii, ambayo alikuwa akiipa ushirikiano mkubwa wakati wote inampigia saluti Maestro Ndala Kasheba kwa kukumbusha habari zake mbalimbali tulizowahi kutoa. Kuzipitia BOFYA HAPA

WAKAZI WA UKONGA WAPAGAWA NA TAMASHA LA MZIKI MNENE CHINI YA VODACOM TANZANIA

$
0
0
 Msanii wa muziki wa Singeli  Tamimu Mshauri Salum akiwapagawisha mashabiki wa  muziki huo  kwenye  tamasha Mziki Mnene linalodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika viwanja vya Gonga Ukonga jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Baadhi ya wakaazi wa Ukonga jijini Dar es Salaam wakipagawa na mziki wa kizazi kipya wa Singeli wakati wa tamasha la Mziki Mnene lililofanyika katika viwanja vya Gonga na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania mwishoni mwa wiki.
Msanii chipukizi wa mziki wa Singeli mkazi wa Ukonga jijini Dar es Salaam,Aaron Chiwaz akiwapagawisha wakazi wa mji huo  kwenye  tamasha Mziki Mnene linalodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika viwanja vya Gonga Ukonga jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

SAFARI YA KUTOKA TABORA, DODOMA HADI DAR KWA BOMBADIER Q400 YA ATCL

$
0
0
Viongozi wa serikali, Vyama vya siasa na wabunge wakisafiri kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam kwa ndege mpya ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ya Bombardier, Novemba 13, 2016. Wote walikwenda Urambo Tabora kumzika Spika Mstafu Samuel Sitta Novemba 12, 2016. Kutoka kulia ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mama Mary Majaliwa , Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Sheikh Shariff Majini

$
0
0
 Sheikh Shariff Majini anawatangazia akina mama wote kuwa anaendelea na DUA kila siku kasoro siku ya IJUMAA na Dua ya pamoja ya watu wote ni kila Jumapili kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa saba mchana. nyumbani kwake Mabibo Mwisho. Sheikh anawakaribisha sana kwa ajili ya kupata DUA ambayo ni silaha tosha kwa kila mwanadamu. Dua ni bure kabisa.
Kwa mawasiliano ya Sheikh piga 0715-581552
 Sheikh Shariff Majini akiukaribisha uongozi wa mkoa wa BAKWATA
 Kinama waliojitokeza kupata mawaidha na DUA toka kwa Sheikh Shariff Majini 

Sheikh Shariff Majini akimuombea DUA mtoto mchanga

Tanzania Kupata Bilioni 12 Za TradeMark East Africa Kusaidia Wafanyabiashara Wanawake

$
0
0
Mkurugenzi wa TradeMark  Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga akifungua Mkutano wa Chama cha Wafanya Biashara Wanawake wa Tanzania (TWCC) jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
 Tanzania itafaidika na msaada wa Dola za Marekani Milioni 5,300,000 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 12 za Kitanzania, zitakazotolewa na Taasisi ya TradMark, East Afrika, kuwajengea uwezo wafanyabiashara wanawake wa Tanzania, kuyafikia masoko ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, hata nje ya Afrika na kwa kuanzia, TradeMark,  itaanzisha madawati ya jinsia kwenye mipaka mitatu ya Holili, Kabanga na Mutukula. 
Ahadi ya fedha hizo, imetolewa na Mkurugenzi wa TradeMark  Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga (pichani), wakati akifungua Mkutano wa Chama cha Wafanya Biashara Wanawake wa Tanzania, TWCC,  kujadili vikwazo kwa wafanyabiashara wanawake mipakani, uliofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. 
Ulanga amesema  fedha hizo zitatolewa na TradeMark East Africa, kupitia mradi wake wa “Women in Trade”  uliolenga kuwajengea uwezo kuhimili ushindani wa kibiashara na kukabiliana na vikwazo vya kibiashara kwa wafanyabiasha wanawake Tanzania kuwawezesha kufanya biashara ya kimataifa ikiwemo kuwezesha bidhaa zao kuyafikia masoko ya nchi za Afrika Mashariki na soko la kimataifa. 
Bwana Ulanga amesema, TradeMark East Africa ni taasisi inayoongoza katika kuleta usawa wa kijinsia katika biashara, kwa sababu utafiti umeonyesha kuwa asilimia 70% ya wanaofanya biashara za mipakani ni wanawake na wanakabiliwa na vikwazo vingi vya kibiashara vikiwemo vikwazo vya kijiografia, vikwazo vya kijinsia, vikwazo vya kisheria, vikwazo vya kimtazamo, hivyo TradeMark imeandaa mpango kamambe wa miaka sita wa kuwajengea uwezo, atakaogharimu shilingi bilioni 12, kati ya hizo, Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania, TWCC, kitapatiwa shilingi milioni 500. 
Akishukuru kwa msaada huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC), Bibi Jaquiline Mneney Maleko, ameishukuru TradeMark kwa msaada huo, na kuahidi utatumika vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa. 
TradeMark East Africa (TMEA) ni shirika lisilo la kiserikali, la maendeleo kwa lengo la kuongezeka ustawi wa kiuchumi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa njia ya biashara. TMEA inafanya kazi kwa karibu na taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), serikali za kitaifa, sekta binafsi na asasi za kiraia.
 TMEA inachangia ukuaji wa biashara Afrika Mashariki kwa kufungua fursa za kiuchumi kupitia:
• Kuongezeka kwa fursa za upatikanaji  wa  masoko;
• Kuboresha mazingira ya biashara; na
• Kuboresha biashara ya ushindani. 
Kuongezeka kwa kiwango cha biashara kuchangia  ukuaji wa uchumi, na kupunguza umaskini na hatimaye kuongezeka ustawi.


TMEA ina makao yake makuu mjini Nairobi nchini Kenya, na ina  matawi katika miji ya Arusha, Bujumbura, Dar es Salaam, Juba, Kampala na Kigali.
Ili kujua zaidi kuhusu TMEA, tafadhali tembelea tovuti TMEA katika www.www.trademarkea.com

Mwisho

 Mkurugenzi wa TradeMark  Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga akifafanua jambo wakati akifungua Mkutano wa Chama cha Wafanya Biashara Wanawake wa Tanzania  (TWCC)
Mkurugenzi wa TradeMark  Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga wakati akifungua Mkutano wa Chama cha Wafanya Biashara Wanawake wa Tanzania (TWCC)

WAZIRI WA MICHEZO ARIDHISHWA NA UKARABATI UWANJA WA NYAMAGANA JIJINI MWANZA. KAMPUNI YA MAFUTA MOIL YAONESHA NIA YA KUWEKA MAJUKWAA

$
0
0
Itakumbukwa kwamba nyasi bandia kwa ajili ya uwanja huu zilikwama bandarini kwa muda mrefu baada ya TFF kutakiwa kulipiwa kodi ya zaidi ya shilingi Milioni 32 hali ambayo ilisababisha utekelezaji wake kusuasua.
Waziri Nape Nhauye amesema Serikali itaendelea kuboresha viwanja mbalimbali nchini ikiwemo kushirikiana na makampuni mbalimbali ili kukarabati viwanja vilivyopo ili Tanzania iwe sehemu bora hata kwa mataifa mengine kufika kwa ajili ya mazoezi na michezo mbalimbali hususani ya mpira wa miguu.
Altaf Hiran Mansoor ambaye ni mdau wa michezo Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, amesema kampuni hiyo iko tayari kuchangia ukarabati wa uwanja huo ikiwemo ujenzi wa majukwaa.
Uwanja mkongwe wa Nyamagana sasa unang'aa kwa viwango vingine, ambapo Waziri Nape amesema anashawishika kuandaa mechi ya kirafiki kati ya timu za Simba na Yanga zinazoundwa na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itakayochezewa kwenye uwanja huo.
Itakumbukwa kwamba Mwaka 1974 timu za Simba na Yanga zilikutana kwenye uwanja wa Nyamagana, kwenye Fainali ya Ligi ya Taifa ya Soka ambapo Yanga iliichapa Simba bao 2-1.

LUKUVI AONGOZA MAZISHI YA MZEE JOSEPH MUNGAI MUNGAI HUKO MAFINGA WILAYA YA MUFINDI, IRINGA

$
0
0
Familia ya Marehemu  Joseph  Mungai ikiwa  imeshikana mkono ishara ya  upendo wakati wa mazishi ya baba yao mjini Mafinga  wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa.
Waziri  mkuu mstaafu Mhe. Frederick Sumaye  akitoa  salama zake kwa  niaba ya mwenyekiti wa Taifa wa  Chadema katika mazishi ya Mzee Joseph Mungai huko Mafinga  wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa.
Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo  ya makazi Mhe. Wiliam Lukuvi akiteta jambo na mbunge wa  Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu wakati wa mazishi ya marehemu Mungai.

Mbunge wa Mikumi Mhe. Joseph Haule akitoa heshima zake za mwisho.
Kwa taarifa zaidi BOFYA HAPA


Jamii yaaswa kufanya kazi kwa uaudilifu ili kujijengea heshima katika jamii

$
0
0
 Mhadhama Kardinali Polycarp Pengo na Dkt. Fredrick Kigady wakifuatilia historia fupi ya Tuzo ya BENEMERENTI ambayo upewa mtu aliyetoa mchango wake mkubwa katika kutumikia jamii pamoja na kanisa wakati wa hafla ya kumkabidhi tuzo hiyo Dkt. Kigadya mapema wikiendi hii Jijini Dar es Salaam.   
 
 Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa akizungumza katika hafla fupi ya kumkabidhi tuzo na kumvisha nishani Dkt. Fredrick Kigadye aliyotunukiwa na Baba Mtakatifu Papa. Francis  mapema wikiendi hii. Kushoto ni Mhadhama Kardina Polycarp Pengo, Dkt Fredrick Kigadye na Mkewe.
 Muadhama Kardinali Polycarp Pengo akimkabidhi hati yenye ujumbe maalumu kutoka kwa Baba Mtakatifu Papa. Francis Dkt. Fredrick Kigadye wakati wa hafla ya kumkabidhi tuzo aliyetunukiwa kufuatia mchango wake mkubwa katika kulitumikia Kanisa Katoliki kupitia Idara ya Afya chini ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) mapema wikiendi hii. Kulia ni Mke wa Dkt. Kigadye akishuhudia tukio hilo.
 Muadhama Kardinali Polycarp Pengo akimvisha nishani ya heshima ijulikanyao kwa jina la  Benemerenti (Anayestahili) Dkt. Fredrick Kigadye aliyetunukiwa tuzo hiyo na Baba Mtakatifu Papa Francisco kufuatia mchango wake mkubwa katika kulitumikia Katisa Katoliki kupitia Idara ya Afya chini ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) jana Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mke wa Dkt. Kagadye akishuhudia tukio hilo.
Dkt. Fredrick Kigadye akitoa neno la shukrani kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kwa kutambua mchango wake katika jamii na kanisa kwa ujumla. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

NEWS ALERT: TAIFA STARS YAFUNGWA 0-3 NA ZIMABWE JIJINI HARARE LEO

$
0
0
Mbwana Samata akijaribu bahati yake langoni mwa Zimbabwe. katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe leo. Tanzania ilifungwa mabao 3-0.
  Mshambuliaji wsa Taifa Stars, Elius Maguri akichuana na beki wa Zimbabwe, Hadebe Teenage 
  Mshambuliaji wsa Taifa Stars, Elius Maguri akichuana na beki wa Zimbabwe, Hadebe Teenage katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe leo. 

Beki Michael Aidan wa Tanzania akijiandaa kumtoka mchezaji wa Zimbabwe, Danny Phiri katika mchezo huo.

Serikali haitatoa Vibali vya kununua Jasi/Makaa ya Mawe Nje ya nchi - Prof. Muhongo

$
0
0

 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa Tatu kulia) akiwa  katika mgodi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka uliopo kata ya Ruanda mkoani Ruvuma ambapo  aliambatana na watendaji mbalimbali kutoka viwanda vya simenti vinavyotumia makaa ya mawe, Chama cha Wamiliki wa Malori (TATOA), Wazalishaji wa Makaa ya Mawe, Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na viongozi kutoka  Mkoa wa Ruvuma.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa tatu kushoto) akipata maelezo kuhusu briketi za makaa ya mawe zinazotengenezwa na kikundi cha Wanawake cha Mbarawala kwa  ajili ya kupikia. Kikundi  kinafadhiliwa na kampuni ya TANCOAL inayomiliki Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka ulipo mkoani Ruvuma.  Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mbinga Cosmas Nsheye, wa pili kushoto ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje. Anayetoa maelezo ni Meneja Uendeshaji wa Kikundi hicho, Hajiri Kapinga.Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

VOA SWAHILI: Ziara ya Baraza la Usalama la UN huko DRC

KUTOKA MAKTABA: Rais mwinyi na kamati ya Saidia Taifa Stars ishinde na wanahabari mwaka 1994, Mwalimu na timu ya Taifa mwaka 1964

$
0
0
Rais Ali Hassan Mwinyi katika picha ya pamoja na kamati ya Saidi Taifa Stars Ishinde aliyoikaribisha Ikulu jijini Dar es salaam kwa kazi nzuri waliyofanya ya kuwezesha Taifa Stars kunyakua ubingwa wa Challenge Cup ya  Afrika Mashariki mwaka 1994. Toka wakati huo Tanzania haijashinda tena kombe hilo.
Waliosimama mbele toka kulia ni Ankal, Brigedia Moses Nnauye, Mwenyekiti wa chama cha soka (FAT) Alhaj Muhidin Ndolanga, Mhe. Rais, Profesa Philemon Sarungi (wakati huo waziri wa afya), Mwenyekiti wa kamati Mzee Reginald Mengi, Mbunge wa Dodoma Mhe. Kuwayawaya S. Kuwayawaya, na mwanahabari Richard Mwaikenda. 
Nyuma kutoka kulia ni Joseph Senga, Stephen Rweikiza, Deus Mhagale, Kanali Ali Mwanakatwe, Richard Ndassa, Japhet Sanga, Godfrey Lutego, nyuma yao ni Evarist Mwitumba, James Nhende, Meja Jenerali Makame Rashid na nyuma yake ni mwanahabari Edmund Msangi na mwandishi jina limenitoka.
Picha ya chini ni Mwalimu Julius Nyerere akiwa na kikosi cha Timu yetu ya Taifa iliyoshinda kombe la Gossage mwaka 1964 alipowakaribisha Ikulu jijini Dar es salaam kuwapongeza.  
Gossage Cup ni mashindano yaliyoshirikisha timu za taifa za Kenya, Uganda, Tanganyika na  zanzibar. Mechi ya kwanza ilipigwa kati ya kenya na uganda mwaka 1926 ambapo kenya waliibuka washindi kwa bao 3-1 kwa aggregate baada ya kurudiana walipotoka sare mechi ya kwanza. Tanganyika ilishiriki kuanzia mwaka1945 na Zanzibar toka mwaka 1926. Michuano hiyo ilikuwa inadhaminiwa na kampuni ya kutengeneza sabuni ya Gossage, iliyokuwa inamilikwa na ndugu wa kiingereza walioitwa Level Brothers. Tanganyika ilikuja kutwaa kombe hilo mwaka 1964.


Mwaka 1967 jina la michuano hiyo ilibadilika na kuitwa East and Central African Challenge Cup  kabla ya kubadilika kuwa Baraza la vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati Council  of East and Central African Football Associations (CECAFA) ambapo Tanzania ndio walishinda huo mwaka 1994.


WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDANI DIS WATEMBELEA KITUO CHA UWEKEZAJI NCHINI KUJIFUNZA

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford Tandari (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita wa Shule ya Sekondari ya Dar es salaam Independent (DIS), wanaosomea masomo ya biashara ambao walitembelea kituo hicho hivi karibuni ili kujifunza maswala mbali mbali yanayohusu uwekezaji. wengine pichani ni wafanyakazi wa kituo hicho.
Afisa Uhamasishaji na Uwekezaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Latifa Kigoda akifafanua jambo kwa baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita wa Shule ya Sekondari ya Dar es salaam Independent (DIS), wanaosomea masomo ya biashara ambao walitembelea kituo hicho ili kujifunza maswala mbali mbali yanayohusu uwekezaji.
 Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Pendo Gondwe akifafanua jambo kwa baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita wa Shule ya Sekondari ya Dar es salaam Independent (DIS), wanaosomea masomo ya biashara ambao walitembelea kituo hicho ili kujifunza maswala mbali mbali yanayohusu uwekezaji.
Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Pendo Gondwe akiwaonyesha wanafunzi hao, moja ya vyeti vinayotolewa na TIC kwa muwekezaji anayekamilisha taratibu zote za kuwekeza nchini.

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images