Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1414 | 1415 | (Page 1416) | 1417 | 1418 | .... | 3284 | newer

  0 0
  0 0

  Mwenyekiti wa Ujumbe maalum wa wadau wa Ujenzi, Bi. Elizabeth Tagora (wa kwanza kulia), akijadiliana jambo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale (wa kwanza kushoto), wakati ujumbe huo ulipokagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la tatu la Abiria (Terminal III) katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA). 
  Mkurugenzi wa Mradi wa ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (TB III), Eng. Mohamedi Milanga akionesha wajumbe maalum wa wadau wa ujenzi eneo la kupumzikia abiria katika Jengo la Tatu la Abiria (TB III) waliokagua hatua za ujenzi wa jengo hilo. 
  Muonekano wa eneo zitakapokuwepo huduma za kibenki na Idara ya Uhamiaji katika Jengo la tatu la Abiria (TB III). 
  Muonekano wa juu wa Jengo la Tatu la Abiria (TB III) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA).


  0 0


  Na Saimeni Mgalula,Songwe

  MKUU wa wilaya ya momba Mkoani hapa,Juma Irando ametoa onyo kali kwa mganga mtawala wa kituo cha afya cha Tunduma Dr Kaogo na kumtaka kujirekebisha na kurekebisha mapungufu aliyobaini na kuwa tayari kuendana na kasi ya Sereikali ya awamu ya tano na kuamtaka kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

  Hayo aliyasema baada ya kwenda kutembelea kituo hicho cha afya jana na kubaini utaratibu mbovu wa utoaji huduma zakiafya baada ya kukaa katika kituo hicho kwa muda wa nusu saa bila ya kumuona hata muudumu mmoja akiwa mapokezi

  ''Viongozi niliongozana nao walilazimika kuwatafuta watoa huduma kwa dakika zaidi ya 45 baada ya kuwasuburi mapokezi kwa kipindi cha dakika 30 bila kupewa huduma pamoja na kuwepo kwa wagonjwa waliokuwa wakisuburi kusikilizwa eneo la mapokezi kwa kipindi kirefu''alisema.

  Hali iliyomlazimu Dc Irando kuwasiliana na Mganga mkuu wa Wilaya ya Momba aliyefahamika kwa jina moja Dr Felister na kumtaka ampe jina la mganga mtawala wa kituo na mganga wa zamu, ambao walipatikana baada ya dakika 30 kinyume na utaratibu.alisema


  0 0

  Chama Cha Mapinduzi kimewataka Watumishi wake kuelekeza nguvu zaidi katika kutekeleza ipasavyo majukumu yao kwa weledi na juhudi kubwa ili kukiletea ufanisi ndani ya Chama hicho.

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe. Vuai Ali Vuai, ametoa kauli hiyo, alipokuwa akifungua mafunzo maalum ya watumishi wa Chama na Jumuiya zake wa kada ya Udereva, Walinzi, Waangalizi wa Ofisi, Makarani wa Masjala na Wahudumu wa Chama hicho, kutoka Mikoa na Wilaya zote za Zanzibar. Mafunzo hayo ya takriban wiki moja yanafanyika Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui, Mjini Unguja.

  Amesema Chama Cha Mapinduzi kinaridhishwa na utendaji wa watumishi wa kada hizo, isipokuwa CCM kimeona kuna umuhimu wa kuandaa mafunzo maalum kwa watumishi hao, kwa lengo la kuwajengea uwezo na uelewa mpana zaidi katika kufanikisha majukumu yao na hivyo waendane na kasi ya Chama kwa sasa.

  Mhe. Vuai amesema Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuwapatia mafunzo watumishi wake wa kada mbali mbali kwa lengo sio tu la kuwaleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ndani ya Chama bali pia kuwajengea uwezo na kuwapa mbinu mbadala za kiutumishi.

  “Chama Cha Mapinduzi kitafanya kila linalowezeka kuhakikisha watumishi wake wa ngazi zote wanapatiwa mafunzo pamoja na kuwaendeleza kielimu, kwa madhumuni ya kunyanyua viwango vyao vya uelewa, na hivyo kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi”. Alidai Mhe. Vuai.

  Amesisitiza haja kwa wanafunzo hao juu ya umuhimu wa kuimarisha Chama na kudumisha suala zima la nidhamu pamoja na kuwepo kwa mawasiliano mazuri baina yao na Viongozi wao, ni dhahiri kutakijengea heshima kubwa chama hicho mbele ya jamii.

  Nao wanafunzo hao, wametumia mkutano huo kumpongeza kwa dhati Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kwa jinsi anavyotekeleza kwa kasi kubwa Ilani ya CCM ya mwaka 2015 - 2020 pamoja na kupambana vilivyo na suala zima la rushwa, wizi na ubadhirifu wa mali ya umma, kwa maslahi ya Taifa na wananchi wake.

  Wamempongeza pia Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, kwa kusimamia vyema Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 - 2020, kusimamia suala zima la amani na utulivu wa nchi, kuimarisha huduma za kijamii na miundombinu ya kiuchumi kwa maslahi ya Wananchi wa Zanzibar. 


  0 0


  Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma

  Serikali imeainisha maeneo ya kipaumbele kwa mwaka 2017/2018 kulingana na mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka ujao wa fedha.
   

  Waziri wa Fedha na Mpiango Dkt. Philip Mpango amesema hayo leo Bungeni mjini Dodoma alipokuwa akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018.

  Dkt. Mpango amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na miradi ya kielelezo ya maendeleo ambayo inayolenga kufanikisha utekelezaji wa Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ni pamoja na miradi ya Makaa ya Mawe Mchuchuma, Mchuchuma Liganga, ujenzi wa reli ya kati kutoka Dar es salaam, Tabora hadi Kigoma yenye urefu wa km 1,251 kwa “Standard Gauge” pamoja na matawi yake ya Tabora kupitia Isaka hadi Mwanza yenye urefu wa km 379, Isaka hadi Rusumo km 371, Kaliua kupitia Mapanda hadi Karema km 321, Keza hadi Ruvubu km 36 na Uvinza hadi Kelelema kuelekea Musongati yenye urefu wa km 203.

  Miradi mingine ya kielelezo ni uboreshaji wa Shirika la Ndege TAanzania (ATC), ujenzi wa mitambo ya kusindika gesi mkoani Lindi, uanzishwaji wa Kanda Maalum za Kiuchumimkoani Tanga, Bagamoyo, Kigoma, Ruvuma, uanzishwaji wa kituo cha biashara cha Kurasini, kusomesha vijana katika stadi za mafuta na gesi, uhandisi na huduma za afya.

  Waziri Dkt. Mpango ameyataja maeneo mengine ya kipaumbele kuwa ni viwanda vya kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa kukuza uchumi wa viwanda, kufungamanisha maendeleo y uchumi na maendeleo ya watu, mazingira ya wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji, ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi pamoja na maeneo mengine muhimu kwa ukuaji wa uchumi na ustawi wa taifa.

  0 0  Foundation for civil society ambao ni asasi huru imetangaza kutumia utaratibu wa JUMANNE YA KUTOA (GIVINGTUESDAY) utaratibu ambao unatumika duniani kote kwa ajili ya kuhamasisha watu na jamii kuwa na moyo wa kujitolea kwa ajili ya wahitaji ambapo asasi hiyo imetangaza kuadhimisha siku hiyo hapa nchini kwa kuwasaidia watoto wenye ulemavu wanaosoma katika shule ya msingi Uhuru mchanganyiko ikiwa ni mara ya kwanza kwa Asasi hiyo kuadhimisha siku hiyo muhimu.
  Akizungumza na mtandao huu katika mahojiano maalum leo Martha Olotu ambaye ni Busness,Development and Partinaship Manager wa Asasi hiyo amesema kuwa FCS inalenga kutumia Utaratibu wa Jumanne ya Kutoa kwa namna ya kuhamasisha Moyo wa kujitolewa kwa wenye Uhitaji,ikiwa ni Jitihada za ulimwengu ambazo zilizinduliwa Rasmi Tangu mwaka 2012 na shirika la New York’s 92nd streat Y kwa ushirikiano na UN Foundation,Lengo likiwa ni kuweka siku maalum kwa ajili kuheshimu na kuadhimisha ukarimu katika kutoa,ambapo kwa sasa siku hii imekuwa ikiadhimishwa na nchi nyingi Duniani ikihusisha makampuni Binafsi,watu binafsi,familia na asasi za kiraia.  Akizungumzia maadhimisho hayo ambayo yatafanyika Tarehe 29 mwezi wa November Karin Rupia Ambaye Ni Resource Mobilization Executive Kutoka katika asasi hiyo amesema kuwa shirika hilo litakabidhi michango iliyotolewa, na kujiunga kufurahi na watoto kwenye shughuli kama kupima afya za watoto hao,kuchora na watoto,kucheza na watoto kusafisha watoto pamoja na kuwasomea watoto hao wa shule ya msingi Uhuru mchanganyiko.

  Kwa maelezo zaidi Juu ya siku hiyo unaweza kutizama HABARI24 TV kwenye Youtube account yetu hapo.

  0 0
 • 11/02/16--01:00: UTAALAMU WA PICHA ZA ANGANI

 • Ukihitaji huduma kama hii piga +255 714 472474

  0 0

   Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania chini ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wamempongeza Rais Magufuli kwa jitihada zake za kuwajali wanyonge hasa katika mambo yanayohusu elimu.

  Pongezi hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam na Katibu wa Shirikisho hilo Zenda Daniel wakati wa mkutano wao na waandishi wahabari kuhusu mambo sintofahamu ya juu ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini.

  Zenda alisema kuwa wao kama Shirikisho wanampongeza na kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kuwakwamu wanyonge

  “Sisi kama Shirikisho tunampongeza na kumuunga mkono mweshimiwa Rais Magufuli kwa juhudi zake za kuhakikisha wanyonge wanajikwamua kwakupata elimu bora”. Alisema Zenda.

  Pamoja na pongezi hizo Shirikisho hilo limeelezea masikitiko yake kwa kile kinachoendelea kuhusiana na suala ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu hadi kufikia hatua ya kultilia shaka uwepo wa baadhi ya watendaji wa Serikali kufanya hujuma ili kukwamisha azma ya Serikali kutoka mikopo kwa wate wanaostahili.

  Katika duku duku lao walionyesha miongozo miwili tofauti kuhusiana na vigezo vya wanaostahili kupewa mikopo, mmoja ukitolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia huku mwingine ukitolewa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ambapo walisema vigezo vilivyiwekwa kwenye miongozo hiyo vinakinzana.Zenda aliongeza kuwa hata pale wanaposema kigezo cha watoto uyatima kinapopaswa kutumika kumekuwa na changamoto kwani kuna baadhi ya wanachuo ambao wamethibitika kuwa ni yatima lakini hawajapewa mkopo hadi sasa.

  Aidha walitumia nafasi hiyo kutoa ushauri kwa Serikali kupitia Wizara husika kukaa pamoja na Bodi ya Mikopo ili kupitia upya vigezo vinavyotumika kuwapata wanafunzi wanaostahili mikopo hiyo.Kwa upande wake Katibu wa Hamasa wa Shirikisho hilo Nganwa Nzota alitoa angalizo kwa Bodi ya Mikopo kwa hatua yake ya uhakiki ambapo imelenga kuwaondoa wale wote watakao kuwa hawana sifa kulingana na vigezo vya sasa kuwa italeta mkanganyiko mkubwa utakasababisha watu waichukie Serikali yao.

  Alishauri kuwa zoezi la uhakiki liendelee lakini lisihusishe kuwaondolea mikopo wanufaika hao watakaobainika kutokidhi vigezo vya sasa kwani wao tayari wana mikataba nao na badala yake wajikite kuhakikisha wanakuwa makini kwa waombaji wapya.

  Katika Mkutano huo maalum uliohudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bwana Hamid S. Muhina Sherikisho hilo liliiomb Serikali ya Rais Dkt. Jonh Pombe Magufuli kupitia upya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu hili kuongeza ufanisi wake.

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu, Mh. James Kilaba
  Na Mwandishi Maalum, Hammamet, Tunisia.

  PAMOJA na maendeleo na faida mbalimbali za Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), masuala ya Usalama, faragha na imani katika matumizi bado yameendelea kuwa masuala ya kuwekwa maanani katika ngazi za kitaifa na kimataifa.

  Akihutubia kikao cha Mkutano wa Dunia wa Masuala ya Viwango Katika Mawasiliano (World Telecommunication Standardization Assembly – WTSA-16) mjini Jasmine Hammamet, nchini Tunisia hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Eng. James Kilaba amesema tekinolojia mpya ndani ya TEHAMA zina mchango mkubwa katika usalama (wa mitandao,mifumo, vifaa, data na wa watumiaji); faragha ( katika data na watumiaji) na Imani (kwenye mitandao,mifumo, vifaa, data na kwa watumiaji). 

  “Katika vikao kama hivi vya majadiliano kuhusu TEHAMA, wakati mwingi hatusahau kuzungumzia masuala ya huduma, vifaa na ukuaji wa watumiaji, mtandao na hata mapato. Leo tunazungumzia mchango wa teknolojia mpya katika usalama, faragha na Imani katika matumizi ya TEHAMA”, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA aliuambia mkutano huo.

  Eng. Kilaba ailisema kumekuwepo na mabadiliko ya teknolojia kutoka zilizotawaliwa kwa kiasi kikubwa na kuendeshwa kwenye mfumo wa intaneti kwa kutumia kompyuta binafsi zilizounganishwa kwa mfumo wa waya hadi tekinolojia zinazotumia vifaa ya mkononi vilivyounganishwa bila kutumia waya. Amesema hii imewezesha na kufanikisha mawasiliano zaidi na kwa kupitia mfumo wa intaneti kuifikia dunia iliyounganishwa na mfumo wa kompyuta.

  Eng Kilaba aliongeza kwamba mada kuu ya majadioiano katika mkutano huo ilikuwa ni huduma, vifaa, kukua na kuongezeka kwa watumiaji na kupanuka na kwa mifumo ya mawasiliano ambayo inawafika mbali zaidi na kuwafikia watu wengi zaidi.


  0 0
  0 0


  Na; Lucas Mboje, Jeshi la Magereza – Dar es Salaam

  KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja amekutana na Wawekezaji wa Kampuni ya CAMCE kutoka nchini China pamoja na Kampuni ya Wazawa ya KG CORPORATION na kumuahidi kushirikiana na Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza(Prisons Corporation Sole) katika kuwekeza katika miradi mbalimbali ya Kilimo cha kisasa, Madini na Viwanda vinavyoendeshwa na Shirika hilo.

  Akizungumza na Wawekezaji hao leo asbuhi Ofisini kwake (Jumatano, Novemba 2, 2016) alisema kwamba Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Uzalishaji mali lina fursa nyingi za miradi ya uwekezaji kwenye sekta nyingi kama vile Kilimo, Viwanda na Madini ambapo aliwahahakishia ushirikiano wa kutosha kwenye uwekezaji wao

  Wawekezaji hao tayari wamefanya mazungumzo na Viongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo wanatarajia kuiingia Makubaliano (MoU) na Jeshi la Magereza kwa ajili ya miradi mbalimbali ikiwemo ya Kilimo cha kisasa katika Gereza Idete lililopo Mkoani Morogoro pamoja na Mradi wa Ngo’mbe wa nyama Gereza Ubena, Mkoani Pwani.

  Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Kampuni ya CAMCE kutoka nchini China Bw. Lane Lei alisema amefurahishwa na ziara waliyofanya nchini na wapo tayari kuwekeza hapa Tanzania.

  Naye, Mwakilishi wa Kampuni ya Wazawa ya KG CORPORATION Bw. Dan Ngowi ambayo inashughulikia na masuala ya Kilimo cha mazao ya chakula na nyama alisema watawekeza kwenye kilimo hususan cha umwagiliaji na watajenga Kiwanda kwa ajili ya usindikaji.

  Shirika la Uzalishaji mali la Magereza(Prisons Corporation Sole) lina jumla ya Miradi 23, kati ya hiyo miradi 15 ni ya kilimo na mifugo na 8 ni ya viwanda vidogo vidogo, pia zipo shughuli za mradi wa Kikosi cha Ujenzi zinazosimamiwa na Shirika hilo.

  Mkakati wa Jeshi la Magereza hivi sasa ni kuendelea kuboresha maeneo mbalimbali pamoja na kuchangamkia fursa zilizopo ikiwemo uwekezaji wa ubia kwenye miradi yake ili kuhakikisha kuwa linafikia ufanisi unaotarajiwa katika utekelezaji wa majukumu yake.

  Kamishna Jenerali wa Mgereza – CGP John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wawekezaji wa masuala ya Kilimo cha kisasa mara baada ya mazungumzo Ofisini kwake leo Novemba 2, 2016, Makao Makuu ya Magereza(kulia) ni Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Kampuni ya CAMCE kutoka nchini China Bw. Lane Lei(kushoto) ni Mwakilishi wa Kampuni ya Wazawa ya KG CORPORATION Bw. Dan Ngowi

  0 0

  Na Ramadhani Ali-Maelezo Zanzibar .

  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka matarajio makubwa kwa Bodi ya Hospitali ya Mnazi mmoja katika kufanikisha azma ya kuwa Taasisi yenye mfumo wa kujitegemea baada ya Baraza la Wawakilishi kupitisha Sheria ya kuanzishwa taasisi hiyo.

  Amesema Bodi hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti mzoefu wa masuala ya Afya Zanzibar Dkt. Abdulwakil Idrissa Abdulwakil inahitaji mashirikiano ya karibu ya wafanyakazi wa Hospitali hiyo na wananchi katika Kuleta mabadiliko hayo.

  Waziri Mahmoud ameeleza hayo Ofisini kwake Mnazimmoja alipokuwa akizindua Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Mnazi mmoja ambayo lengo lake kuu ni kuifanya Hospitali hiyo kufikia kuwa ya rufaa inayoshughulikia maradhi maalum yaliyoshindikana katika vituo vya afya na Hospitali za kawaida.

  “Tunawataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kuvitumia vituo vya afya vilivyo karibu nao, vinavyofikia 142, na kuiacha taasisi mpya ya Mnazi mmoja kushughulia magonjwa makubwa,”alisisitiza Waziri wa Afya.

  Ameitaka Bodi kuishauri Serikali njia bora za kuchangia matibabu katika maeneo maalum kwa vile Sera ya Serikali bado ni kuendelea kutoa matibabu bila malipo kwa wananchi.Waziri wa Afya amewaeleza wajumbe wa Bodi hiyo kuwa Hospitali ya Mnazi mmoja inarasilimali kubwa ya kuaminiwa na wananchi wengi wa Zanzibar na linapotokea tatizo lolote huwa ni la nchi nzima hivyo suala la kuongeza ufanisi lina umuhimu mkubwa.

  Amesema hivi karibuni Hospitali hiyo itafunga majengo mengine mawili mapya ambayo yanavifaa vya kisasa hivyo wafanyakazi watapaswa kuwa waangalifu na kuacha kufanyakazi kwa mazoea.Amewataka viongozi wa sehemu zote za Hospitali ya Mnazimmoja kuwasimamia wafanyakazi walio chini yao na kuiunga mkono Bodi katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili Hospitali hiyo.

  Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Abdulwakil Idrissa Abdulwakil amesema jukumu walilopewa na Serikali ni kubwa lakini kwa kutumia utaalamu wa wajumbe wa Bodi hiyo watajitahidi kuhakikisha malengo yaliyowekwa ya kuifanya Hospitali ya Mnazimmoja kuwa ya kujitegemea linafikiwa.Hata hivyo amewaomba viongozi wa Wizara na wafanyakazi wa Hospitali ya Mnazimmoja kuwapa ushirikiano na watakuwa tayari kupokea ushauri utakaosaidia kufikia malengo yaliyopangwa.

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Juma Malik Akili amewaeleza wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mnazi mmoja kuwa Wizara itaendelea kusimamia sera lakini Bodi ndio yenye jukumu la kushauri maendeleo ya taaisi hiyo.
  Waziri wa Afya Zanzibar Mahmuod Thabit Kombo akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mnazimmoja katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
  Waziri wa Afya Zanzibar Mahmuod Thabit Kombo katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mnazi baada ya kuizindua rasmi Bodi hiyo, wa kwanza (kushoto) Katibu Mkuu Wizara ya Afya Jama Malik Akili na (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Abdulwakil Idrissa Abdulwakil.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0

  Na Theresia Mwami TEMESA Lindi

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amepongeza utaratibu unaotumika katika kituo cha TEMESA Lindi na karakana zake kwa kuratibu vizuri kazi za kila siku.

  “Nawapongeza sana kwa utendaji wenu wa kazi kwa kuweka utaratibu wa kufuatilia kila kazi inayofanywa na wafanyakazi wa kituo” alisema Dkt. Mgwatu.Dkt Mgwatu amemuagiza Meneja wa TEMESA Mkoa wa Lindi Mhandisi Greyson Maleko kuhakikisha kuwa magari yote ya Serikali mkoani Lindi yanafanyiwa matengenezo katika karakana ya TEMESA iliyopo mkoani humo.

  Dkt. Mgwatu amemtaka Meneja huyo kuhakikisha anakusanya madeni yote wanayodai kwenye Taasisi, Halmashauri na Idara mbalimbali za Serikali kutokana na matengenezo ya magari na mitambo, sambamba na kulipa madeni yote wanayodaiwa na wazabuni kwa kipindi cha Julai-Septemba, 2016.

  Kwa upande wake Meneja wa TEMESA Lindi alisema kuwa changamoto kubwa inayokabili kituo hicho ni uwepo wa madeni makubwa wanayodai kwenye Taasisi na Halmashauri mbali mbali za serikali zilizopo Mkoani Lindi kutokana na matengenezo ya magari na mitambo lakini wanajitaidi kuendelea kufanya kazi kwa ustadi na kujituma.

  Katika hatua nyingine Dkt. Mgwatu alitembelea eneo litakalojengwa gati kwa ajili ya kivuko kutoka Lindi hadi Kitunda.Dkt. Mgwatu yupo katika ziara ya kikazi kutembelea mikoa ya Lindi na Mtwara ili kujionea hali ya Vituo katika mikoa hiyo pamoja na utendaji kazi wake.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme – TEMESA Dkt Mussa Mgwatu (kulia) akiongea na Meneja wa TEMESA Lindi Mhandisi Grayson Maleko (kushoto) alipotembelea kituoni hapo.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme – TEMESA Dkt Mussa Mgwatu (katikati) akiongea na Mafundi wa TEMESA Lindi walioko kwenye mafunzo ya vitendo, alipotembelea kituoni hapo.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto w) akiongea na watumishi wa Karakana ya TEMESA Lindi, alipotembelea kituoni hapo mapema.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu akiangalia eneo litakalojengwa gati kwa ajili ya Kivuko cha Lindi Kitundamkoani Lindi.Picha Zote na Theresia Mwami TEMESA Lindi


  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF), limemteua Jonesia Rukyaaa – Mwamuzi wa soka kutoka Tanzania kuwa miongoni mwa waamuzi wa kati 10 watakaochezesha mechi za Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake zitakazofanyika kwa wiki mbili kuanzia Novemba 19, mwaka huu.

  Kwa uteuzi huo, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), amempigia simu Jonesia kumpongeza kwa hatua hiyo ambayo ni sehemu kubwa ya mafanikio ya soka la Tanzania kufanya vema katika medani za kimataifa.

  Rais Malinzi amesema kwamba Mwamuzi Jonesia ameliletea heshima taifa la Tanzania kwa kujijengea heshima ya kuaminika mbele ya Kamati ya Ufundi ya CAF – Waratibu na Waandaaji wa fainali hizo zitakazofanyika Cemaroon ambako mechi za mechi ya mwisho ya fainali itafanyika Desemba 3, mwaka huu.

  “Namtakia kila la kheri, naamini kwamba Jonesia atafanya vema. Nina uhakika kwamba hii ndiyo njia yake pekee ya kufanikiwa zaidi kwani ipo siku atateuliwa kuchezesha hata fainali za Kombe la Dunia,” yalikuwa ni maneno ya Malinzi akimwelezea Jonesia kwenye simu leo mchana.

  Jonesia anafanya idadi ya waamuzi watakaochezesha mchezo huo kutoka nchi za Afrika Mashariki kuwa watano kwani wengine kwa mujibu wa orodha ya CAF ni Salma Mukansanga (Rwanda), Lydia Tafesse (Ethiopia), Carolyne Wanjala (Kenya) na Suan Ratunga (Burundi).

  Waamuzi wengine ni Maria Packuita wa Mauritius, Gladys Lengwe (Zambia), Akhona Zennith Makalima (Afrika Kusini), Jeanne Ekoumou (Cameroon) na Aissata Amegee (Togo). Katika orodha hiyo pia yumo Mary Njoroge wa Kenya ambaye mwamuzi wa pembeni pekee.

  Katika fainali hizo, timu shiriki ni Cameroon, Afrika Kusini, Misri na Zimbabwe zipo kundi A wakati Nigeria, Ghana, Kenya na Mali zimo kundi B.

  Jonesia ambaye jana Jumanne alirejea kutoka Cameroon kwenye kozi ya uamuzi ngazi ya juu, kesho Alhamisi anatarajiwa kuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara pale Mtibwa Sugar ya Morogoro itakapokaribishwa na Mwadui kwenye Uwanja wa Mwadui. Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Mbao Fc na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

  0 0


  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imependa kuwatakia kheri na mafanikio watoto wote wa kidato cha nne walioanza kufanya mtihani wa Taifa wa kuhitimu elimu ya Sekondari kuanzia tarehe 01 Novemba, 2016. Wizara yenye dhamana ya maendeleo ya watoto inawaomba watoto wanaotahiniwa kutambua kuwa, muda wa kufanya mtihani ni fursa adhimu kwao, hivyo ni lazima kuutumia kwa umakini mkubwa kwa ajili ya mustakabali wa maisha yao binafsi, familia na taifa kwa ujumla.

  Wizara inawaasa kuwa waangalifu muda wote wa kutahiniwa, wazingatie kanuni na taratibu stahiki, na pia kuepuka kuandika mambo ambayo yasiyotakiwa katika karatasi za mtihani. Kipindi cha kufanya mtihani ni kifupi ukilinganisha na muda wa miaka minne ambayo watoto hawa wamekaa madarasani wakiwa katika masomo; hivyo watoto wanahimizwa kujiepusha na vishawishi vyovyote ikiwemo vitendo vya udanganyifu katika chumba cha mtihani ambavyo vinaweza kusababisha kubatilishwa kwa matokeo yenu na hivyo kukatisha ndoto zenu. Ni matarajio ya Wizara kuwa wote mtamaliza mitihani yenu vizuri na kwa amani na utulivu.  Wakati watoto wetu wakiendelea kufanya mitihani yao, Wizara inawakumbusha wazazi na walezi kutambua kuwa mnaowajibu wa kuweka mazingira ya kuwasaidia kukumbuka yote waliyojifunza kipindi chote cha masomo yao na kuwa tayari kujibu mitihani yao wakiwa wameandaliwa kisaikolojia ili kuhitimu vizuri. Aidha Serikali haitarajii kusikia au kuona mzazi au mlezi yeyote akijaribu kutengeneza mazingira ya kuharibu ndoto ya mtoto yeyote hasa watoto wa kike kwa kupanga kuwaozesha mara tu wanapomaliza mitihani ya Taifa ya kidato cha Nne.  Wizara inaamini kuwa wazazi na walezi watakuwa makini kuandaa mazingira ya watoto kufikia ndoto zao kielimu, na kuwaepusha watoto wa kike na janga la ndoa za utotoni, hadi watakapofikia umri stahiki. Wizara inasisitiza kwamba atakayethubutu kukatisha ndoto ya mtoto wa kike kwa kumwozesha chini ya umri wa miaka 18, Serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya mzazi na mlezi huyo ili kulinda haki na masilahi ya mtoto kulingana na sheria, taratibu na kanuni zinazomlinda mtoto.  Wizara inatoa rai kwa wazazi, walezi, makondakta na jamii kwa ujumla, kuwapa ushirikiano madhubuti watoto wetu katika kipindi hiki cha mitihani yao ili waweze kuhitimu vizuri mitihani yao. Watahiniwa ni hawa ni vijana wetu wanaotarajiwa kuendeleza taifa letu, hivyo tuwajengee mazingira murua ya kupata haki ya elimu ili kuwa na vijana mahiri na wenye weledi wakiwa na stadi na maarifa ya kubeba majukumu ya Taifa katika harakati za kuelekea uchumi wa kati,
  MARGARET S. MUSSAI 

  KAIMU MKURUGENZI WA MAENDELEO YA WATOTO 
  WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO 

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
  MWANDAMIZI wa masuala ya usalama barabarani , Lawrence Kilimwiko amewataka waandishi wa habari  kutumia kalamu zao kuelimisha umma juu ya usalama bora na namna ya kukabiliana nazo.

  Akitolea ufafanuzi juu ya masuala ya usalama barabarani, Kilimwiko amesema kuwa waandishi wengi wa habari wanaripoti habari za ajali kama matukio na kushindwa kufuatilia hasa baada ya kumaliza kuandika hawafanyi ufuatiliaji wa majeruhi.

  Kilimwiko amesema kwa ajali za barabarani zimekuwa janga la afya hasa baada ya takribani watu milioni 50 wanaathirika na ajali hizo na wengine kupoteza maisha  na kundi kubwa linaloathirika ni vijana na inakadiriwa kufika mwaka 2030 ajali za barabarani zitachukua namba 5 katika janga la vifo duniani.

  Kutokana na ajali hizo, zimesababisha kupeleka mzigo mkubwa kwa sekta ya afya na kupelekea kuongeza gharama za serikali na kuchangia umasikini kutokana na nguvumali ya taifa kuangamiakwa ajali za barabarani.

  Uchunguzi uliofanyika kupitia Shirika la Afya Duniani(WHO) kupitai usalam barabarani  wamegundua kuwa asilimia 95 za  ajali zinatokana na matumizi mabya ya barabara na kuhamasisha waandishi wa habari kusaidia na kuchochea mabadiliko ya sera za sheria za Usalama barabarani.

  Kilimwiko amesema nchi kama Afrika Kusini ina sheria ambayo dereva yoyote haruhusiwi kutumia simu wakati anaendesha chombo cha moto na atakapokamatwa basi atapigwa faini na hili linatakiwa kufanyika hata nchini kwetu na hilo litasaidia kupunguza ajali.
   Mwandamizi wa masuala ya Usalama Barabarani, Lawrence Kilimwiko akizungumza na waandishi wa habari juu ya masuala ya Usalama barabarani na jinsi ya kuelimisha jamii kuhusiana na sera za usalama bwa barabara katika semina elekezi kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA).
  Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa makini kumsikiliza mwandamizi wa masuala ya usalama barabarani Lawrence Kilimwiko.Picha na Zainab Nyamka,


  0 0

  Na Ally Daud-MAELEZO. 

  MAMLAKA ya mapato nchini (TRA) imetakiwa kuwa makini na wafanyabiashara wanaoingiza nguo nchini bila ya kulipa kodi kwa kuwa hawalipii biashara zao kwa kila mzigo unaoingia hivyo kuchangia kuleta hasara ukusanyaji wa pato la taifa. 

  Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage wakati wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya ujasiriamali kwa wanawake yaliyofanyika jijini Dar es salaam yakiwa na lengo la kukuza na kuwezesha wanawake kujitegemea kiuchumi na kukuza maendeleo ya taifa kupitia viwanda. 

  “Napenda kuwaambia TRA wawe makini wafanyabiashara wanaoingiza nguo nchini bila ya kulipa kodi kwa kuwa hawalipii biashara zao kwa kila mzigo unaoingia hivyo kuchangia kuleta hasara katika pato la taifa kwa kupoteza takribani shilingi bilioni 319 kutokana ukwepaji wa kodi za nguo zinazoingia nchini” alisema Waziri Mwijage. 

  Aidha Waziri Mwijage amesema kuwa kwa kufanya hivyo TRA itaweza kukusanya mapato mengi zaidi na kukuza uchumi wa nchi kupitia ukusanyaji wa kodi kwa wafanyabiashara na wanaostahili kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi. 

  Mbali na hayo Waziri Mwijage amesema kuwa wanawake wajasiriamali wanatakiwa kuwa wabunifu na sio kuiga ubunifu wa mtu mwingine kwa asilimia kubwa ili kuweza kujiletea masoko ya bidhaa zao ndani na nje ya nchi ili kujipatia soko la kimataifa. 

  Kwa upande wa Mwenyekiti wa MOWE Bi. Elihaika Mrema amesema kuwa maonyesho hayo yamewalenga wanawake wajasiriamali kuonyesha na kuuza bidhaa zao ambazo zimetokana na ubunifu wao kwa maendeleo ya mwanammke na Tanzania kwa ujumla ili kukuza pato la taifa. 

  “Wanawake wajasiriamali wanatakiwa wawe wabunifu katika kubuni biashara mbalimbali za kujikwamua na uchumi ili kuacha kutegemea wanaume kwa asilimia kubwa na kuendesha jamii kubwa ya Tanzania” alisema Bi. Elihaika.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kulia akisalimiana na Meneja wa huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA Bw. Gabriel Mwangosi katikati alipotembelea banda lao wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya biashara na wajasiliamari wanawake jijini Dar es salaam,kushoto ni Meneja wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi Bi. Valentina Baltazar.
  Afisa Elimu Mkuu kwa mlipa kodi wa TRA Bi. Rose Mahendeka akiwapa maelekezo wateja waliotembelea banda hilo wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya biashara na wajasiliamari wanawake jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kushoto akipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni inayotengeneza batiki na unyonyaji wa maji taka Genevive Investment Bi. Jane Mwaituka kulia alipotembelea banda lao wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya biashara na wajasiliamari wanawake jijini Dar es salaam.Picha Na Ally Daud- MAELEZO.

  0 0
 • 11/02/16--09:38: MATUKIO BUNGENI DODOMA LEO
 • Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema akijadiliana jambo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
   Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Bulembo (CCM), akichangia hoja kuhusu mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2016/2017 bungeni Dodoma, hasa jinsi ya kuwawezesha vijana nchini
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akijibu maswali ya wabunge.
   Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lisu (Chadema), akichangia hoja bungeni, ambapo alihoji watu wasio husika kuwaweka kwenye makumbusho ya mashujaa nchini.


  0 0


  Na Bakari Madjeshi,Globu ya Jamii 

  Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekanusha taarifa ya kutoa Zabuni kwa Kampuni ambazo hazina vigezo kupata zabuni hizo. 

  Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam,Naibu Meya wa Halmashauri hiyo,Mussa Kafana amesema kumekuwepo na taarifa ikidai kuwa Halmashauri hiyo imetoa zabuni kwa Kampuni ambazo hazina sifa. 

  "Tumeona tutoe ufafanuzi kwamba hatujatoa zabuni kwa Kampuni ambayo haina sifa,Mfano Kenya Airport ambayo mpaka leo mkataba wake haujasainiwa,"amesema Kafana 

  Amesema baadhi ya mikataba haijasainiwa kutokana na Kampuni hizo kutotimiza vigezo na masharti vinavyotakiwa kama zabuni inavyoeleza. 

  Kafana ameeleza kuwa Mikataba haijasainiwa kutokana na Kitabu cha Zabuni kinaonyesha kuwa Halmashauri ya Jiji kitu gani inataka ikiwa ni pamoja na kutimiza Masharti hayo ya Halmashauri ya Jiji. Pia amesema Mzabuni anatakiwa kuleta dhamana ya Asilimia 10 ya kile kiwango alichobidi katika kuomba zabuni,hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa Kitabu cha Zabuni katika sura ya 41 Kifungu cha kwanza,

  Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,Mussa Kafana akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu kuwepo kwa taarifa ambayo inadai kuwa Halmashauri hiyo imetoa zabuni kwa Kampuni ambazo hazina sifa.

  0 0


  SIMU.TV: Baadhi ya wabunge wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania wasema mpango wa maendeleo wa 2017/2018 hauendani na maisha halisi ya kiuchumi iliyopo. https://youtu.be/edp2ikv8PSA

  SIMU.TV: Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema leo ameongoza zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wadogo wanaopanga bidhaa kando kando ya  barabara za mwendo kasi. https://youtu.be/wrBYOxEA6co

  SIMU.TV: Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinatarajia kuanza kutumia hati ya pamoja ya kusafiria kwa raia wa nchi hizi kuanzia Januari mwaka 2017. https://youtu.be/YGbQQxxmkiE

  SIMU.TV: Serikali imekemea tabia ya baadhi ya wafanyakazi wake kutotekeleza majukumu yao kikamilifu ukilinganisha na wafanyakazi wa makampuni binafsi. https://youtu.be/RoDpF_kWu-M

  SIMU.TV: Halmashauri ya manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam imekifunga kituo cha mabasi cha Mbagala baada ya kugundulika kuendeshwa kinyume na sheria. https://youtu.be/jjSTD9pYoyY 

  SIMU.TV: Mtoto Lengai Godi mwenye miaka mitatu amelazwa katika idara ya Mifupa MOI hospitali ya taifa ya Muhimbili baada ya kushambuliwa na baba yake mkubwa kufuatia ugomvi wa kifamilia. https://youtu.be/KJcaXl4CZ64

  SIMU.TV: Kampuni ya Vodacom Tanzania imezindua simu mpya yenye uwezo mkubwa wa kuunganisha mtandao wa kasi ya 4G. https://youtu.be/NGcO6ahgkPg

  SIMU.TV: Shirika la nyumba la taifa NHC limepata mkopo wa zaidi ya shilingi bilioni 60 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya nyumba za makazi na mahoteli. https://youtu.be/v7gP4SuDRyE

  SIMU.TV: Mamia ya waombolezaji wamejitokeza kwenye maziko ya bondia wa Thomas Mashali yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. https://youtu.be/ofbCU98jgeo

  SIMU.TV: Klabu ya Simba imeendelea kuongeza kasi ya kulifukizia kombe la ligi kuu Tanzania bara baada ya kuifunga Stand United  bao moja kwa bila. https://youtu.be/hsHZlhfwwSs

  SIMU.TV: Makocha wa timu za wanawake zinazoshiriki ligi kuu ya wananwake nchini wameomba wadu kujitokeza kuzisaidia vifaa timu hizo. https://youtu.be/DxfhB-us8uI

older | 1 | .... | 1414 | 1415 | (Page 1416) | 1417 | 1418 | .... | 3284 | newer