Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1413 | 1414 | (Page 1415) | 1416 | 1417 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Naibu waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo, amefanya ziara kwenye shule mbalimbali mjini Dodoma kuangalia maandalizi kwa ajili ya mtihani wa kidato cha nne unaoanza Leo nchini.

  Katika ziara yake kwenye Shule ya sekondari Jamhuri, Kiwanja cha ndege na Msalato, Jafo amewaonya walimu na wanafunzi hao nchini kuepukana na vitendo vya udanganyifu.

  Akizungumza na walimu na wanafunzi katika shule hizo, Jafo amesema katika mtihani huo hawatarajii kuwepo na udanganyifu kwa kuwa wamejifunza kupitia mtihani wa darasa la saba ambapo kumekuwepo na tabia ya walimu kujificha chooni ili kuwasaidia wanafunzi.
  Amesema shule zitakazofanya fanya hivyo zitakuwa zimepoteza thamani yake.

  Ameeleza hatarajii mitihani hiyo ifanyike kinyume na kuwataka walimu wasisubutu kufanya udanganyifu wowote na kuziingiza shule zao kwenye kashfa.Jafo ame sema mara nyingi mitihani hiyo inapofanyika kumekuwa na wizi wa mitihani na kutofuatwa kwa taratibu za mitihani.

  Akizungumza na wanafunzi, Jafo amewataka kujiepusha na vitendo hivyo kwa kuwa vitawafanya wafutiwe mitihani na kupoteza malengo yao kwenye maisha.

  Hata hivyo amewahakikishia walimu kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kuboresha mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia na kuwataka kuwajibika ipasavyo.  wanafunzi wa kidato cha nne wakimsikiliza naibu waziri Ofisi ya Rais Tamisemi selemani jafo mara baada ya kukagua maandalizi ya mtihani wa kidato cha nne unaofanyika Leo. 

  Naibu waziri ofisi ya Rais Tamisemi selemani jafo akiagana na wanafunzi wa  shule ya sekondari msalato mara baada ya kuzungumza nao.

  0 0
  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  KIKOSI cha vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys tayari kimeingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya siku saba hapa nyumbani kabla ya kwenda nchini Korea Kusini kushiriki michuano ya kimataifa iliyoandaliwa na chama cha soka nchini humo.

  Afisa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba kocha mkuu wa timu hiyo Bakali Shime tayari ameungana na timu baada ya kuwa kwenye mapumziko mafupi.

  Lucas amesema kwamba safari hiyo ni ahadi ya Raisi wa TFF,Jamali Malinzi ambapo awali alidai kuwa timu hiyo licha ya kushindwa kufuzu kwa fainali za vijana zitakazofanyika nchini Gaboni lakini kikosi kitaendelea kuwepo pamoja na kitajengwa kwani nia yao vijana hao sasa wataenda kuunda timu ya Ngorongoro Heroes.

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma.

  Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 48.3 kwa ajili ya kujenga Mahakama 40 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ili kuongeza ufanisi na kuharakisha hukumu za kesi katika ngazi mbalimbali nchini.

  Kutokana na fedha itakayotumika kujenga mahakama, shilingi bilioni 36 zinatokana na Bajeti ya mwaka huu wa fedha wakati shilingi bilioni 12.3 zilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.

  Hayo yamebainishwa leo mjini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dkt. Harisson Mwakyembe alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Iramba Mashariki Mhe. Allan Kiula aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama za Wilaya na uteuzi wa Mahakimu katika ngazi hiyo.

  Waziri Mwakyembe amesema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha Mahakama zinakuwepo kila wilaya ili kuwaondolea usumbufu wananchi, kurahisisha usikilizwaji wa kesi pamoja na kupunguza gharama kwa wananchi kutoka sehemu moja kwenda nyingine kufuata Mahakama zilipo.“Kwa mujibu wa Katiba ya Nchi, Sheria na Kanuni inaeleza kuwa kila Mahakama ina mipaka yake hivyo hatuwezi kubadilisha mahakama ya mwanzo kutumika kama ya wilaya” amesema Dkt. Mwakyembe.

  Ameongeza kuwa mpaka sasa bado kuna wilaya zinapata huduma ya Mahakama kupitia wilaya nyingine ambapo amewahakikishia Wabunge na wananchi kuwa Serikali itajenga mahakama 40 kwa mwaka huu wa fedha.

  Akifafanua mgawanyiko wa Mahakama 40 zinazotarajiwa kujengwa nchini, Dkt. Mwakyembe amesema kuwa Serikali itajenga Mahakama Kuu nne, Mahakama za mikoa sita, Mahakama za Wilaya 14 na Mahakama za Mwanzo 16 katika wilaya mbalimbali nchini.

  Aidha, Mhe. Mwakyembe ametaja baadhi ya vigezo vinavyotumika kuanzisha Mahakama katika eneo lolote kuwa pamoja na uwepo wa hati ya kisheria ya kuwepo kwa wilaya, mkoa, kata na kijiji, umbali wa upatikanaji wa huduma za Mahakama, idadi ya wakazi wa eneo husika pamoja na uwepo wa huduma zingine za kipolisi na magereza.

  Ameongeza kuwa kutokana na changamoto hizo za kukosekana kwa mahakama katika maeneo ambayo yamekidhi vigezo ndiyo yaliyopelekea Serikali kujipanga kujenga Mahakama hizo ambapo ametoa rai kwa wananchi kuwa na subira wakati wakikusubiri kujengwa kwa Mahakama hizo. 

  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  SHIRIKISHO la mpira wa miguu  nchini TFF,limepokea mwaliko kutoka chama cha mpira wa miguu nchini Zimbabwe juu ya chama hicho kuhitaji kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya Tanzania Taifa Stars.

  Afisa habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba mara baada ya kupokea baraua hiyo shirikisho la soka hapa nchini limeridhia swala hilo na kwa sasa wakati wowote kuanzia sasa kocha mkuu wa timu ya Taifa Chars Boniphace Mkwasa ataanza program kwa ajili ya mechi hiyo inayotaraji kupigwa siku ya tarehe 13 mwezi huu.

   Kocha Mkwasa anatarajiwa kutangaza kikosi hivi karibuni na wataingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mechi hiyo ambayo ni muhimu sana kwao kwa ajili ya kupanda viwango vya FIFA.

  Awali timu hiyo ilitakiwa kucheza na Ethiopia katika kalenda ya FIFA ila iliweza kufutwa kutokana na hali ya usalama kuwa mbaya nchini humo.

  Kwa sasa Tanzania imeshuka katila viwango vya FIFA na kufika nafasi ya 142 kidunia.                        


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Kwanza wa Bunge la Umoja wa Afrika na Katibu Mkuu wa Mkutano wa Nne wa Beijing, Getrude Mongella, Ofisini kwake, bungeni mjini Dodoma Novemba 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Na Fatma Salum
  - MAELEZO

  Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 ambao unatazamiwa kuwasilishwa kwa mara ya kwanza bungeni katika kikao kilichoanza Novemba 1 mwaka huu umezua mjadala mkubwa na mpana miongoni mwa wadau wa sekta ya habari. 

  Mjadala wa muswada huu umekuwa ni mkubwa ukilinganisha na miswada mingine kwa sababu ukweli ni kwamba kila mtanzania ni mdau wa sekta hii ambayo wote tunaitegemea kwa kupata taarifa zinazoaminika ili kutusaidia kufanya maamuzi mbalimbali katika maisha yetu ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.

  Usahihi wa maamuzi yote makubwa tunayoyafanya mmoja mmoja au kwa pamoja kama jamii – iwe kuchagua vongozi, kuchagua kozi ya kusoma na mengineyo yanategemea sana taarifa tulizonazo.Ili tuweze kupata taarifa sahihi ni muhimu vyombo vya habari na waandishi watengenezewe mazingira mazuri ya kufanyia kazi, jambo ambalo ndiyo malengo ya sheria hii tarajiwa.
  Licha ya ukosoaji mkubwa unaofanyika, ukweli ni kwamba Muswada wa Vyombo vya Habari 2016, kama utapitishwa, utajenga mazingira mazuri ya tasnia hii na kuirudishia heshima inayostahili. Katika kupitia muswada huu nimeona faida nyingi za muswada, lakini kwenye makala hii nitataja faida tano kubwa.
  Heshima ya tasnia 
  Kwanza, muswada huu unairejeshea tasnia hii heshima yake iliyoipoteza siku nyingi kwa kuifanya fani hii iwe miongoni mwa fani za uweledi, kama zilivyo nyingine zikiwemo udaktari na uanasheria. 


  0 0

  Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

  Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni jambazi alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na askari Polisi kisha kufariki dunia wakati akipelekwa katika hospitali ya Monduli kwa ajili ya matibabu.

  Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo alipoongea na waandishi wa habari leo mchana ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Naibu  Kamishna (DCP) Charles Mkumbo alisema tukio hilo lilitokea muda saa 07:00 Usiku maeneo ya Makuyuni barabara ya Arusha-Makuyuni wilayani Monduli.

  Kamanda Mkumbo alisema jambazi huyo akiwa na wenzake wapatao 29 walikuwa na bunduki ambayo bado haijafahamika pamoja na silaha za jadi mapanga na marungu ambapo waliweka mawe barabarani na kulisimamisha gari aina ya Fusso lenye namba za usajili T. 871 BUZ ambalo lilikuwa lina mzigo likitokea Moshi kuelekea mkoani Singida.

  ‘’Mara baada ya kulisimamisha gari hilo wakaanza kumpora abiria mmojawapo aliyejulikana kwa jina la Victor Pius (46) Mfanyabiashara, mkazi wa Majengo Moshi ambapo walichukua simu mbili aina ya Nokia na Samsung pamoja na fedha taslimu Tsh 50,000/=’’.

  “Wakati wanaendelea na tukio hilo askari Polisi waliokuwa High Way Patrol walipata taarifa za tukio hilo ambapo walikwenda kwa haraka na mara baada ya majambazi hao kuwaona walianza kufyatua risasi hovyo na Polisi kuanza kujibu mapigo na kufanikiwa kumjeruhi mmojawao na kuwakamata wengine kumi na mbili papo hapo wakiwa na mapanga sita na marungu manne huku wengine akiwemo na yule mwenye bunduki wakikimbia”. Alifafanua Kamanda Mkumbo.

  Kamanda Mkumbo alitoa wito kwa wananchi wa mkoa huu kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu ili zifanyiwe kazi kwa haraka, huku akitoa onyo kwa majambazi wanaopenda kujipatia kipato bila kuvuja jasho kwani Jeshi hilo limejiandaa vizuri.

  0 0  Mwenyekiti wa Kamati ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Jimbo la Konde Mh. Omar Seif Abeid wa Pili kutoka Kushoto akizungumza katika Kikao ilichowakutanisha Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Uongozi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

  Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Mjini Zanzibar.

  Wa kwanza kutoka kushoto ni Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Mohammed Aboud Mohammed, wa kwanza kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Nd. Joseph Abdulla Meza, Naibu Katibu Mkuu Ahmad Kassim Haji na Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti - OMPR - Nd. Ameir Ussi.Picha na – OPMR – ZNZ.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta leo tarehe 01 Novemba, 2016 wamezindua barabara ya Southern By-pass iliyojengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Nairobi nchini Kenya.

  Sherehe ya uzinduzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 28 na inayounganisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi imefanyika katika eneo la Karen nje kidogo ya Jiji la Nairobi.

  Akizungumza katika sherehe hiyo Rais Magufuli amempongeza Rais Kenyatta na Serikali yake kwa kujenga barabara hiyo ambayo sio tu itawasaidia wananchi wa Kenya bali pia itawasaidia wananchi wa Afrika Mashariki wanaotumia barabara zinazopitia Nairobi.

  Rais Magufuli pia ameishukuru Serikali ya China kupitia benki yake ya Exim ambayo imetoa mkopo wa kujenga barabara hiyo, kwa kuendelea kuziamini nchi za Afrika Mashariki na kuzikopesha mikopo inayosaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara. 

  "Wananchi wanahitaji maendeleo na haya ndio maendeleo, barabara hii itasaidia kuinua uchumi na itasaidia masuala ya kijamii" amesema Rais Magufuli.

  Dkt. Magufuli amesema viongozi wa Afrika Mashariki wameamua kufanya kazi ya kuharakisha maendeleo na kuinua maisha ya wananchi, na kwamba ili kufanikisha hilo wamedhamiria kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara zinazounganisha nchi wanachama na kujenga vituo vya pamoja vya utoaji wa huduma za mpakani (One Stop Border Post).

  Kwa upande wake Rais Kenyatta amesema kujengwa kwa barabara hiyo kumesaidia kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Nairobi na pia kutaboresha shughuli za maendeleo ya wananchi.

  Mhe. Kenyatta amemshukuru Rais Magufuli kwa kuungana nae kuzindua barabara hiyo na amesema Kenya itaongeza juhudi katika utekelezaji mradi wa ujenzi wa barabara zinazounganisha Kenya na Tanzania zikiwemo barabara ya Malindi kupitia Saadani hadi Bagamoyo nchini Tanzania na barabara ya Voi - Taveta- Holili-Arusha.Sherehe za uzinduzi wa barabara ya Southern By-pass zimehudhuriwa na Naibu Rais wa Kenya Mhe. William Ruto.

  Kabla ya kuzindua barabara hiyo Rais Magufuli ametembelea kiwanda kidogo cha kusindika maziwa cha Eldoville kilichopo katika eneo la Karen ambacho kinamilikiwa na familia ya mkulima Bw. James Karuga.

  Familia hiyo ilianzisha kiwanda cha kusindika maziwa mwaka 1985 kwa uzalishaji wa chini ya lita 1,000 kwa siku na hivi sasa imefikia uzalishaji wa lita 5,000 kwa siku na inatarajia kuongeza uzalishaji hadi lita 70,000 katika mwaka mmoja ujao baada ya kuongeza kiwanda cha pili.


  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Nairobi.


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, wakiweka jiwa la msingi kuashiria ufunguzi wa barabara ya kupunguza msongamano ya Nairobi Southern Bypass nchini Kenya.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Naibu Rais wa Kenya William Rutto pamoja na viongozi wengine, wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya kupunguza msongamano ya Nairobi Southern Bypass nchini Kenya.

  Sehemu ya barabara hiyo ya Nairobi Southern Bypass nchini Kenya.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakicheza wimbo pamoja na kikundi cha kwaya katika eneo la Karen mara baada ya kufungua barabara hiyo ya Nairobi Southern Bypass nchini Kenya.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Bi. Lucy Karuga kuhusu usindikaji wa mazao ya chakula katika kiwanda cha Maziwa cha Eldoville katika eneo la Karen nchini Kenya.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia usindikaji wa Samli katika kiwanda hicho cha maziwa cha Eldoville nchini Kenya. PICHA NA IKULU .


  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewasaa watumishi wa Umma wa Mkoa wa Dar es Salaam kuchangamkia fursa ya nyumba zinazojengwa na Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) na kuacha kufikiria akistaafu atajenga nyumba sehemu zipi.

  Makonda aliyasema hayo wakati alipotembelea miradi ya nyumba za watumishi wa umma za Bunju B pamoja na Magomeni Kota inayotekelezwa na TBA, amesema kuwa kujengwa kwa nyumba hizo kutafanya watumishi kufanya kazi kwa uhakika kutokana na mazingira ya kustaafu yamewekewa msingi na serikali ya kupatikana kwa nyumba.

  Amesema watumishi wa umma wamekuwa wakifanya kazi kwa muda mwingi wakifikiria nyumba kutokana na kipato chake hawezi kujenga nyumba hivyo kuwepo kwa nyumba zilizojengwa na TBA zitawaondolea machungu ya kufikiria suala la nyumba.

  Aidha amesema kuwa Mradi wa Magomeni Kota ameshaanza kutekelezwa kutokana na ahadi aliyoitoa Rais Dk. John Magufuli kuona wananchi waliondolewa katika Kota hizo wananufaika na nyumba zitazojengwa.

  Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Elius Mwakalinga amesema kuwa watanzania wawaamini wamedhamiria kujenga kila mkoa kwa kuanzia nyumba 10 ili watumishi waweze kupata makazi.

  Amesema kuwa ndani ya mwaka mmoja watakuwa wamemaliza mradi wa Ujenzi wa Magomeni Kota utakuwa umekamilika kutokana na kujipanga ili kuweza wananchi waanze kuishi katika nyumba hizo.

  Mwakalinga amesema katika mradi wa Bunju B wametumika kati sh.Bilioni 13 hadi 14 katika kitalu cha 19 wameweza kujenga nyumba 219 na mradi mwingine watajenga nyumba 300 kwa viwango tofauti kutokana na vipato vya wafanyakazi.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikagua mradi nyumba zilizojengwa na TBA katika eneo la Bunju B katika ziara aliyoifanya leo jijini Dar es Salaam.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Elius Mwakalinga akimpa maelezo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda juu ya mradi wa nyumba za watumishi wa umma Bunju B leo jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea miradi inayotekelezwa na TBA leo jijini Dar es Salaam.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Elius Mwakalinga akizungumza na waandishi wa habari juu ya miradi inayotekelezwa na TBA ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma.

  0 0

  Msuluhishi wa kisheria wa sakata la madai ya Simba dhidi ya Young Africans hali kadhalika Mchezaji Hassan Hamisi Ramadhani maarufu kama Hassan Kessy, Wakili Msomi, Mzee Said El-Maamry anatarajiwa kukutana na pande zinazopingana Alhamisi Novemba 3, mwaka huu ili kufikia mwafaka wa mwadai hayo.

  Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji iliagiza pande za Simba na Young Africans kumaliza suala hilo mapema mwezi uliopita, lakini kwa sababu zilizo nje ya TFF na Kamati yake walishindwa kufanya hivyo kupewa barua ya wito kuitwa kikaoni Oktoba 29, mwaka huu.

  Hata hivyo, msuluhishi huyo alishindwa kuendelea na kikao hicho baada ya taarifa kutoka Young Africans kusema kwamba mmoja wa Wawakilishi wake, Wakili Msomi Alex Mgongolwa kuwa safarini Iringa alikokwenda kwa sababu ya matatizo ya kifamilia. Ilielezwa kuwa Mgongolwa ambaye ni Mwanasheria wa Young Africans, alifiwa hivyo kuomba kupangiwa siku nyingine.

  Kutokana na hali hiyo, E-Maamry amepanga sasa kukutana nna viongozi na/ au Wawakilishi wa pande zote mbili Alhamisi saa 11.00 jioni kwenye ofisi za TFF ili kuketi chini ya kuangalia namna ya kumaliza madai ya Simba iliyowasilisha mashauri mawili ambako moja ni dhidi ya Young Africans ilihali jingine ni dhidi ya mchezaji Hassan Kessy.

  Mzee El-Maamry amesema: “Ili kutenda haki, lazima tutoe nafasi kwa pande zote kusikiliszwa. Ni vema Mwanasheria wa Young Africans akasubiriwa.”

  Kamati ya TFF inasuburi makubaliano hayo, na ikitokea imeshindikana, suala hilo litarudi kwenye Kamati hiyo kwa ajili ya uamuzi wa mwisho kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria zinazoongoza mpira wa miguu.

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama akizungumza bungeni mjini Dodoma Novemba 1, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Tarime, Ester Matiko bungeni mjini Dodoma Novemba 1, 2016.
  Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, bungeni mjini Dodoma Novemba 1, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 1, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 1, 2016.


  0 0


  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt Hamisi Kigwangalla akiongea kuhusu upatikanaji wa dawa na vifaa tiba leo mjini Dodoma.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Suleimani Jafo akijibu swali la Mbunge wa Kwela Mhe. Ignas Malocha (hayupo pichani) aliyehitaji kujua ni lini kituo hicho cha afya kitapewa hadhi ya kuwa Hospitali ya Wilaya,

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kukarabati kituo cha afya cha Laela kilichopo mkoani Rukwa ili kikidhi vigezo vya kuwa Hospitali ya Wilaya ikiwa ni moja ya jitihada za kupunguza adha ya wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya zilipo.

  Hayo yamesemwa leo mjini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Suleimani Jafo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kwela Mhe. Ignas Malocha aliyehitaji kujua ni lini kituo hicho cha afya kitapewa hadhi ya kuwa Hospitali ya Wilaya.


  Mhe. Jafo amesema kuwa ni uamuzi wa muda mrefu wa Serikali kuiweka Hospitali hiyo kuwa ya Wilaya na ndiyo sababu ya kufanya jitihada za kukiongezea uwezo kituo hicho kwa kujenga wodi nyingi pamoja na kutoa kibali cha kuajiri watumishi wapya kwani kwa sasa kituo hicho kina upungufu wa watumishi .

  Amefafanua kuwa hadi sasa kuna baadhi ya majengo ambayo tayari yameshakamilika ambayo ni jengo la upasuaji wa dharura, wodi ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji pamoja na wodi ya mama wajawazito.

  “Kwa sasa kituo cha afya cha Laela hakina miundombinu inayokidhi sifa za kuwa Hospitali ya Wilaya ila kutokana na kupanuka kwa Mji huo na kuongezeka kwa watu wanaohitaji huduma katika kituo hicho tumeamua kukiboresha ili kifikie hadhi ya kuwa Hospitali ya Wilaya”, amesema Jafo.

  Ameongeza kuwa kwa sasa huduma za rufaa kwa wagonjwa wanaohudumiwa katika kituo hicho zinatolewa kupitia magari ya kawaida ya Halmashauri kutokana na ukosefu wa gari la kubebea wagonjwa lakini Wizara ina matarajio ya kutenga fedha ya kununulia gari hilo katika Bajeti ya mwaka 2017/2018.

  Aidha, Mhe. Jafo amethibitisha kuwa kituo hicho kimetengewa jumla ya shilingi 9,358,100 katika Bajeti ya fedha ya mwaka huu ambayo itagharamia kununua dawa na vifaa tiba vitakavyorahisisha upatikanaji wa matibabu kwa wananchi wa eneo hilo.

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt Hamisi Kigwangalla amesema kuwa Wizara hiyo inaendelea kuipitia mikataba ya makampuni binafsi ili kuangalia namna ya kushirikiana nao katika kusaidia upatikanaji wa vifaa tiba katika Hospitali na vituo vya afya nchini.

  0 0


  0 0


  0 0

  Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma
  Watumishi wa Umma 1,663 kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa, na Mamlaka za Serikali za Mitaa wamechukuliwa hatua za kinidhamu baada ya kubainika kusababisha watumishi hewa 19,629 hadi Oktoba 25, 2016.
  Waziri ya Nchi, Ofisi ya Rais, anayeshughulikia Utumishi na Utawala Bora Angella Kairuki amesema hayo leo Bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mainda Hamad Abdallah (Mbunge wa Viti Maalum) alilohoji hatua zilizochukuliwa na Serikali dhidi ya watumishi wanarudisha nyuma maendeleo ya nchi.
  Akifafanua idadi hiyo, Waziri Kairuki amesema kuwa idadi ya watumishi waliochukuliwa hatua za kinidhamu kutoka Wizara mbalimbali ni 16, Idara zinazijitegemea na Wakala za Serikali watumishi tisa, Sekretarieti za Mikoa watumishi sita na Mamlaka za Serikali za Mitaa watumishi 1,632.
  Waziri Kairuki amesema kuwa watumishi hao wameisabishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh. bilioni 19, huku Halmashauri ya Kinondoni ikiwa na watumishi hewa 107 ambao waligharimu Serikali sh. bilioni 1.29, Kishapu watumishi 73 wamesababisha hasara ya kwa kugharimu sh. milioni 543 na kuonya kuwa waajiri waendelee kuchukua hatua za haraka na kudhibiti uwepo wa watumishi hewa ili kuipunguzia Serikali kuingia hasara kubwa badala ya kuwahudumia wananchi.  
  Aidha, Waziri Kairuki amesema kuwa jumla ya watumishi 638 wamefunguliwa mashtaka polisi, watumishi 50 wanafanyiwa uchunguzi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na watumishi 975 mashtaka yao yamefikishwa kwenye Mamlaka zao za kinidhamu.

  0 0


  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitelemka kwenye ndege baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nairobi, Kenya,  alikokuwa katika ziara ya Kiserikali ya siku mbili leo Jumanne Novemba 1, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan  baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nairobi, Kenya,  alikokuwa katika ziara ya Kiserikali ya siku mbili leo Jumanne Novemba 1, 2016 

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi  baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nairobi, Kenya,  alikokuwa katika ziara ya Kiserikali ya siku mbili leo Jumanne Novemba 1, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea  na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan  baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nairobi, Kenya,  alikokuwa katika ziara ya Kiserikali ya siku mbili leo Jumanne Novemba 1, 2016 


  0 0


older | 1 | .... | 1413 | 1414 | (Page 1415) | 1416 | 1417 | .... | 3283 | newer