Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110019 articles
Browse latest View live

nape atoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha bondia thomas mashali

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa pamoja na Chama cha Wanandondi nchini kufuatia kifo cha Bondia wa ngumi za kulipwa Bw. Christopher Fabian Mashale maarufu kama ‘Thomas Mashali’ (pichani) kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 31/10/2016.

Mhe. Nape Nnauye pamoja na watendaji wa Wizara wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha bondia huyo na kuongeza kuwa kifo hicho ni pigo  katika tasnia ya michezo nchini.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha bondia Thomas Mashali, sina maneno ya kuelezea masikitiko na huzuni niliyonayo, kwani kifo chake ni pigo katika tasnia ya masumbwi nchini” alisema Mhe.Nnauye.

Aidha, Waziri Nape Nnauye ameitaka jamii na wanamichezo kote nchini kuwa wavumilivu na watulivu wakati wote wa msiba na kumuombea marehemu makao mema kwa Mwenyezi Mungu.

Thomas Mashali alizaliwa Jijini Dar es Salaam tarehe 9 Septemba, 1989 na kuweza kushiriki katika baadhi ya michezo mbalimbali ya masumbwi ya kulipwa ambapo kati ya michezo 26 aliyowahi kucheza alishinda michezo 19, ambayo tisa ni ya Knock Out (KO), lakini pia alipoteza michezo mitano yaani KO minne na kutoka sare mchezo mmoja.

Bondia Thomas Mashali aliwahi kupigana na baadhi ya mabondia maarufu wa ndani na nje ya nchi wakiwemo Francis Cheka, Abdallah Paziwapazi, Ibrahim Tamba na wengineo.

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo


31 Oktoba, 2016


Olive Kiarie, mshiriki kutoka nchini Kenya ameibuka mshindi wa Maisha Plus East Africa 2016 na kujishindia kitita cha Tzshs. Milioni 30.

$
0
0
Winner“Kwanza napenda kumshukuru Mungu. Nimetoka Kenya kuja kutafuta hii pesa na nimeipata, hivyo namshukuru Mungu. Nawashukuru mabeste wangu wote, na wote walionipa sapoti. Asante pia Babu.” Alisema Olive huku akitoka machozi baada ya kutangazwa mshindi.880A9842Hii ni mara ya kwanza kwa taji hilo kwenda nje ya Tanzania ikiwa ni msimu wa tano toka mashindano haya yaanze mwaka 2009. Olive anakua msichana wa pili kujishindia taji hilo baada ya Bernick Kimiro aliyeshinda mwaka 2012. Kwa taarifa zaidi BOFYA HAPA

Banda la Tanzania lang’ara maonyesho ya nchini Saud Arabia

$
0
0

Na Mwandishi Wetu, Saud Arabia
MAONYESHO ya biashara na Utalii yaliyoandaliwa nchini Saud Arabia katika Mji wake Mkuu wa Riyadh, yamefanyika wiki iliyopita huku Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikionekana kung’ara baada ya wageni wengi kupendezwa na bidhaa zilizokuwa zinaonyeshwa katika banda la Tanzania.
Katika maonyesho hayo ambayo bidhaa mbalimbali zilionyeshwa ukiwamo eneo maalum la mlima Kilimanjaro, nguo za Kitanzania na viatu pamoja na bidhaa nyingine muhimu zilizoonekana kuwapendeza wengi waliohudhuria maonyesho hayo.
Akizungumza katika maonyesho hayo, Balozi wa Tanzania nchini Saud Arabia, Mheshimiwa Hemed Mgaza, alisema kwamba wananchi wengi waliohudhuria maonyesho hayo walionekana kuvutiwa zaidi na nchi ya Tanzania kutokana na vivutio vyake.
Alisema hali hiyo imekuja kutokana na aina ya bidhaa zilizoonyeshwa pamoja na ubunifu wa kutangaza bidhaa zao na nchi kwa ujumla, wakiamini kuwa utachochea wageni wengi wa kutoka nchini hapa kwenda kutembelea nchini Tanzania kwa mambo mbalimbali.
“Binafsi nimefarijika mno kutokana na wenyeji kuandaa maonyesho haya na kutuaalika Watanzania ambao watumishi wa ofisi yangu pamoja na mimi mwenyewe wote tulihakikisha kwamba tunayatumia vizuri kutangaza nchi yetu Tanzania.
“Tumewahakikishia kwamba mbali na nchi yetu kujawa na vivutio vingi kutoka Tanzania Bara na Visiwani, lakini bado tumejawa na amani kiasi kwamba unapokuwa kwenye ardhi ya Tanzania huna sababu ya kuwa na wasiwasi wowote kwa sababu wananchi wake wanaishi kwa upendo,” alisema Balozi Mgaza.
Kwa mujibu wa Balozi Mgaza, maonyesho hayo kwenye ofisi yao waliyapa jina la Visit Tanzania the land Kilimanjaro, Serengeti and Zanzibar, ambapo pia walitangaza bidhaa za chai, kahawa, viatu vya kimasai, vinyago vya wanyama na nguo za utamaduni.


TEKNOLOJIA YA CCTV KUBORESHA USALAMA WA BENKI YA EXIM.

$
0
0
BENKI ya Exim Tanzania yatangaza uzinduzi wa chumba maalum kipya chenye kiwango cha juu cha kufuatilia kamera za ulinzi zilizopo katika matawi yote ya benki hiyo nchi nzima. 

Uzinduzi wa chumba hiki kipya kinaonyesha juhudi za benki hiyo katika matumizi ya teknolojia na uvumbuzi ili kuhakikisha kuwa benki yenye mazingira ya usalama sio tu kwa wateja bali kwa wafanyakazi pia. 

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha kuzuia hatari na uhakiki (Risk& Compliance) David Lusala amesema kuwa “Benki ya Exim imejikita katika kutengeneza mazingira ya usalama kwa wateja wake. Tuna timu nzima iliyopata mafunzo husika katika masuala ya usalama ambao wana jukumu la kuhakikisha shughuli zote zinarekodiwa na kusimamiwa ipasavyo. Kitu chochote kitakachoonekana kuwa hakiko sawa kitagundulika kwa haraka na hatua za haraka kuweza kuchukuliwa. Tungependa wateja wajue kuwa tutakuwa na taarifa za wakati pale ambapo kutatokea kitu chochote kibaya.” 

Katika kitengo cha kutoa taarifa kinachojulikana kama ‘whistle blow’ Lusala alitoa wito kwa wadau kufanya kazi kwa karibu na benki katika kutoa taarifa ya mambo yoyote ya hujuma. Hii inaenda sambamba na kampeni ya kuzuia udanganyifu iliyozinduliwa mwezi Agosti mwaka huu wakati wa maadhimisho ya miaka 19 ya benki. 

Kampeni ya kuzuia hujuma inalenga kutengeneza mazingira ya kutokuwa na udanganyifu katika sekta ya benki kwa kushirikisha umma kuweza kutoa taarifa za shughuli zozote za kihujuma katika benki. Umma unahimizwa kutoa taarifa hizo kupitia barua pepe eximbank@tip-offs.com au kupiga simu ya bure kupitia namba 0800 11 0050.

“Tunatambua umuhimu wa mchango wa wafanyakazi na wateja wa benki yetu, kampeni hii inalenga kujenga mazingira ya uwazi na usalama ili kuwapa fursa wadau wetu kuweza kutoa taarifa hizi bila woga,” ameongeza Lusala. 

Benki ya Exim Tanzania ni moja ya benki tano bora nchini, benki hii inaendelea kujivunia kuwa mwanzilishi katika uvumbuzi na teknolojia. Benki ya Exim Tanzania inahamasisha na kutumia teknolojia kuhakikisha ukuaji wa haraka na kuridhisha wateja.

Kampuni ya Bayport yasherehekea miaka 10 ya kuanzishwa kwake pamoja na watoto wa KCVC

$
0
0


Mgeni rasmi, Mke wa Rais Mstaafu Mama Anna Mkapa, akiongea na wafanyakazi wa Bayport, waandishi wa habari na walimu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Kibaha Children Village Center (KCVC), wakati wakusherehekea miaka 10 ya Bayport ambayo ilifanyika katika kituo hicho juzi, Kibaha mkoani Pwani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport, John Mbaga, akiongea na wafanyakaziwa Bayport, waandishi wa habari na walimuwakituo cha kuleleawatotoyatima cha Kibaha Children Village Center (KCVC), wakati wakusherehekeamiaka 10 ya Bayport ambayoilifanyikakatikakituohichojuzi, KibahamkoaniPwani.

Baadhi ya wafanyakazi wa Bayport Tanzania wakiwa valisha fulana watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Kibaha Children Village Center, wakati wafanyakazi hao walipokwenda kusherehekea miaka 10 ya kampuni hiyo.

Wafanyakazi wa bayport wakiwa katika picha ya pamoja naviongozi, watoto yatimanawatotowawafanyakaziwa Bayport Tanzania, wakati wa kusherehekea miaka 10 ya Bayport ambayo ilifanyika katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Kibaha Children Village Center (KCVC), wengine pichani (Kuliakwa Mama Mkapa) ni MkurugenziMtendajiwa Bayport John Mbaga na Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano NgulaCheyo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

HAMJAMBO HAPO.......

MBUNGE VITI MAALUM CCM IRINGA AFANYA ZIARA KWA AKINA MAMA WA MADUMA

$
0
0
MBUNGE wa viti maalum CCM  mkoa wa Iringa, Rose Tweve ametembelea kikundi cha akina mama wa kata ya Maduma Wilaya ya Mufindi na kuwapongeza kwa juhudi zao wanazozifanya katika shughuli za ujasiriamali.

Tweve akiwa katika kata hiyo aliweza kuwapatia wakina mama hao pesa taslimu milioni moja kwa ajili ya kujiendeleza zaidi kibiashara na kuacha kuwa tegemezi .

Akizungumza na wakina mama hao, Tweve ameweka wazi mpango wake wa kuwasaidia wanawake wote wanaoanzisha vikoba au vikundi kwa ajili ya ujasiriamali zaidi wajitume zaidi kuhakikisha wanakuza mitaji yao.

Katika ziara hiyo, Mbunge huyo aliongoza na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Mufindi na wao waliweza kuchangia Laki tano kwa wakina mama hao.

Tweve amesema kuwa wakati wa kampeni za mwaka jana pamoja na ilani ya chama cha Mapinduzi aliwaahidi wakina mama wa Iringa kuwa ataungana nao katika kuwasaidia kujiinua kiuchumi na kupambana na umaskini kwa Kuanzisha mfuko wa wanawake ambao umeshaanza kufanya kazi.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Rose Tweve akipokea zawadi ya kikapu kutoka kwa akina mama hao wa Maduma alipoenda kuwatembelea na kuangalia namna wanavyojishughulisha katika biashara zao za ujasiriamali.
Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Iringa, Rose Tweve akimkabidhi moja ya akina mama wa Maduma fedha taslimu kiasi cha milioni moja kwa ajili ya kuendeleza mitaji yao ya biashara.

5THEAC UNIVERSITY STUDENTS’ DEBATE ON REGIONAL INTEGRATION ONGOING AT THE KIGALI INDEPENDENT UNIVERSITY

$
0
0
 Intense Debate is underway: The 5th EAC University students’ debate, themed “Youth Participation in Electoral Democracy,” is taking place from 31st October to 3rd November 2016 at the Kigali Independent University in Kigali, Rwanda. The debate has brought together various participants including University students as well as lecturers, academia, policy makers, media, youth leaders and high school students from Uganda, Kenya, United Republic of Tanzania, and Rwanda, the host country. 
The EAC University Students’ Debate Model is an interactive and representational style of debating aimed at educating, discussing and making resolutions among the Youth in East African to nurture a bond of “Eastafricaness” with a distinct East African identity.

Rwanda’s Minister of Trade, Industry and EAC Affairs, Hon. Francois Kanimba in a group photo with the debaters. For full story CLICK HERE

Mwanamitindo Ceccyleyer Godfrey anaomba kura yako

$
0
0
Ceccyleyer Godfrey ni msichana wa miaka 18, Ni Mwanamitindo wa kitanzania na ni mshiriki pekee anaeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Miss Teen - Heritage yatakayo fanyika huko nchini Sri Lanka. anaomba kura yako moja kila siku kupitia site maalumu ya shindano hilo ambayo ni hii: 


ili kumuwezesha kuipeperusha vyema Bendera yetu ya Tanzania. Kumbuka. kura moja kila siku. 
Asante.

BENCHMARK WITH THE BEST IN THE WORLD, EAC PARTNER STATES URGED

$
0
0
 Former EAC Secretary General, Hon. Amanya Mushega, gives the keynote address at the opening of the EAC-EU-IMF Conference on EAC integration in Arusha.
 The Head of the EU Delegation to Tanzania, Hon. Roeland Van de Geer addressing delegates at the EAC-EU-IMF Conference on regional integration in East Africa.
 IMF African Department Director, Mr. Abebe Aemro Selassie, speaks at the opening of the EAC-EU-IMF Conference on EAC Integration in Arusha, Tanzania.
EAC Deputy Secretary General (Finance and Administration), Hon. Jesca Eriyo, making her remarks during the official opening of the EAC-EU-IMF Conference on EAC integration.
--------------------------------
East African Community Partner States have been challenged to benchmark themselves with the world’s most advanced economies if they are to grow their economies. 
Hon. Amanya Mushega, a former EAC Secretary General, said the EAC needs to revisit and do away with the standard way of judging itself by Sub-Saharan African standards. 
“India, Singapore and South Africa, just to mention but a few refused to treat themselves that way. They aimed high, looked at the way the USA, Japan, Germany, UK and the USSR developed their human resources, copied them with the view to competing with them and not fellow third world countries and the results are out,” said Hon. Mushega. 
“Our problem of remaining poor and beggars is not lack money or natural resources, it is our mindset. We have put the bar too low. We are not going to be competing with Gambia or Haiti but with Korea, Japan and China, first for our own EAC market and secondly, for the world market,” he added.  
Hon. Mushega called for heavy investment by the Partner States in human resource development, and urged the Community to compare the number and quality of local skills with those countries that have prospered rather than the comfort zone of Sub-Saharan Africa.

Michigan Tanzania Independence Party

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0

SIMU.TV: Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wameiomba kamati ya bunge huduma na maendeleo ya jamii kuwapa muda wa kuupitia muswada wa habari na kutoa maoni yao kabla ya kupitishwa na bunge. https://youtu.be/7r6qScPR0Yw

SIMU.TV: Makamu wa rais Samia Suluhu Hassani amepiga marufuku uharibifu wa mazingira unaoendelea sehemu mbalimbali nchini unaoweza kupelekea nchi kuwa jangwa. https://youtu.be/9pGimrqPpzU

SIMU.TV: Uharibifu mkubwa wa mazingira pamoja na uchomaji wa misitu ovyo umetajwa kuwa changamoto inayopelekea mabadiliko ya nchi maeneo mbalimbali. https://youtu.be/RKbzEUXEIeI

SIMU.TV: Halmashauri ya manispaa ya Ilala kesho inaanza rasmi kuwaondoa wafanyabiashara wanaofanya biashara kando kando ya barabara za magari yaendayo haraka. https://youtu.be/xFMSVW58DJE

SIMU.TV: Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam linalitafuta kundi la matapeli lililotumia jina la mkuu wa mkoa Paul Makonda kutapeli kampuni ya Kichina https://youtu.be/Vn9x9rVQ7Ug

SIMU.TV: Rais wa Korea ya Kusini amemtunuku nishani ya heshima aliyekua mkuu wa wilaya ya Mkuranga Henry Clemence kwa kutambua jihada zake katika kuleta maendeleo kwa kutumia mfumo wa SMU. https://youtu.be/v0tPp8mNcS0

SIMU.TV: Mafundi wanaotumia saruji ya Rhino kuzalisha matofali jijini Mbeya wameiomba kampuni hiyo kujenga kiwanda katika mkoa wa Mbeya. https://youtu.be/R55Bdry3MiU

SIMU.TV: Vijana wa mkoa wa Dar es  Salaam wametakiwa kujiunga na programu ya jiandalie ajira ili waweze kupata mafunzo ya ujasiriamali kwa ajili ya kuanzisha biashara zao. https://youtu.be/vNk5FoBUUts

SIMU.TV: Maziko ya bondia wa ngumi za kulipwa Thomas Mashali yatafanyika siku ya Jumatano tarehe mbili Novemba katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. https://youtu.be/22oxZi-8yus

SIMU.TV: Tamasha kubwa la utamaduni maarufu kama Cha kale Dhahabu linatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam December 30 katika uwanja wa Uhuru. https://youtu.be/TZXsRDxGnzk

SIMU.TV: Msanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya Rajabu Said ameibuka mshindi katika shindalo la Club Raha Leo Show. https://youtu.be/0Vx2jIoYovY

MBUNGE VITI MAALUM MKOA WA IRINGA AFANYA ZIARA KATA YA MADUMA

$
0
0
MBUNGE wa viti maalumu mkoa wa Iringa, Mhe. Rose Tweve ametembelea kikundi cha akina mama wa kata ya Maduma Wilaya ya Mufindi na kuwapongeza kwa juhudi zao wanazozifanya katika shughuli za ujasiriamali.
Tweve akiwa katika kata hiyo aliweza kuwapatia wakina mama hao pesa taslimu milioni moja kwa ajili ya kujiendeleza zaidi kibiashara na kuacha kuwa tegemezi .
Akizungumza na wakina mama hao, Mhe. Tweve ameweka wazi mpango wake wa kuwasaidia wanawake wote wanaoanzisha vikoba au vikundi kwa ajili ya ujasiriamali zaidi wajitume zaidi kuhakikisha wanakuza mitaji yao.
Katika ziara hiyo, Mbunge huyo aliongozana na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Mufindi na wao waliweza kuchangia Laki tano kwa wakina mama hao.
Mhe. Tweve amesema kuwa wakati wa kampeni aliwaahidi wakina mama wa Iringa kuwa ataungana nao katika kuwasaidia kujiinua kiuchumi na kupambana na umaskini kwa Kuanzisha mfuko wa wanawake ambao umeshaanza kufanya kazi.
 Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Rose Tweve akipokea zawadi ya kikapu kutoka kwa akina mama hao wa Maduma alipoenda kuwatembelea na kuangalia namna wanavyojishughulisha katika biashara zao za ujasiriamali.

 Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Iringa, Rose Tweve akimkabidhi moja ya akina mama wa Maduma fedha taslimu kiasi cha milioni moja kwa ajili ya kuendeleza mitaji yao ya biashara.

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA TAMASHA LA MAZINGIRA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI KATIKA UKUMBI WA NKURUMAH HALL CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepiga marufuku uharibifu mkubwa wa mazingira unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini ambao unaweza kusababisha nchi kugeuka jangwa.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Makamu wa Rais ameonya kuwa jukumu la kuhifadhi mazingira sio la Serikali peke yake bali ni kila mwananchi na wadau wa mazingira kwa ujumla, hivyo wananchi ni muhimu kwa umoja wao wakaongeza jitihada za kupanda miti katika maeneo yao ili kukabiliana na hali tete ya uhabifu wa mazingira nchini.

“Uharibifu wa mazingira usimame leo na marekebisho ya uharibifu tulioufanya uanze leo na hili ni jukumu la kila Mtanzania”Makamu wa Rais pia ametoa wito maalum kwa viongozi wa ngazi zote nchini kuchukua hatua katika kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji katika maeneo yao ili visitoweke.

Makamu wa Rais ametahadharisha kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yameanza kuleta athari si kwa Tanzania na dunia kwa ujumla hivyo jitihada za makusudi zinahitajika ili kuhakikisha changamoto zinazojitokeza kwa sasa zinakabiliwa ipasavyo.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya mabadiliko ya Tabia ya nchi,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Pius Yanda amesema mkutano huo wa siku TANO utakuwa na jukumu kubwa la kujadili kwa kina namna bora ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikikata utepe kuashiria kuzindia kitabu cha Pastoralism and Climate Change in East Africa kwenye Tamasha la Mazingira na Mabadiliko ya Tabia Nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza viongozi wengine kuonyesha juu kitabu cha Pastoralism and Climate Change in East Africa kuashiria kimezinduliwa rasmi kwenye Tamasha la Mazingira na Mabadiliko ya Tabia Nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Wajumbe walihudhuria mkutano wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye ukumbi wa Nkurumah Hall,tayari kufungua mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Waliokosa mikopo sasa HESLB ruksa kukata rufaa

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza siku 90 kuanzia leo (Jumatatu, Oktoba 31, 2016) kwa waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017 kukata rufaa kwa njia ya mtandao ikiwa hawajaridhsihwa na matokeo ya upangaji uliotangazwa hivi karibuni. 

Serikali imetenga Tshs 483 bilioni kwa ajili ya kutoa mikopo kwa jumla wanafunzi 119,012 – kati yao, wanafunzi 93,295 ni wanaondelea na masomo na wanafunzi 25,717 ni wa mwaka wa kwanza. Hadi sasa, jumla ya wanafunzi 20,183 wa mwaka wa kwanza wameshapata mikopo. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (Jumatatu, Oktoba 31, 2016) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru, Bodi imeanza kupokea rufaa hizo kwa njia ya mtandao (Online Loan Application and Management System) kuanzia leo (Oktoba 31, 2016) hadi Januari 31, 2017. 

“Wanachotakiwa kufanya wanafunzi ni kuingia katika mtandao wetu wa http://olas.heslb.go.tz na kujaza fomu, kuichapa na kuiwasilisha kwa Afisa Mikopo wa chuo chake ambaye atawasilisha kwetu fomu zote za chuo chake kwa barua kwa ajili ya sisi kuzifanyia kazi,” amesema Bw. Badru.

*ANGALIZO: Ada ya Maombi ya Tshs 10,000/- iliyopaswa kulipwa na waombaji mikopo kwa MPesa kwa ajili ya malipo ya Rufaa (HESLB) imefutwa.Taratibu nyingine zinabaki palepale 


FURSIKA: Welcome Tanzanian innovators, entrepreneurs, developers, and solution providers!

$
0
0
Welcome Tanzanian innovators, entrepreneurs, developers, and solution providers! We need your help to show how data and the use of data can make a change in people’s lives! Are you interested? Join the challenge!
The Data for Local Impact (DLI) Innovation Challenge will award grants to Tanzanians (both individuals and organizations) who have creative ideas about how to use or combine data - including open data - in new ways to gain insights or empower people through access to life-changing information. The DLI Innovation Challenge also aims to engage, support, and connect Tanzanian innovators, developers, and solution providers to each other and to opportunities to make a difference in people’s lives.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 31.10.2016

RAIS DKT MAGUFULI AWASILI NCHINI KENYA,APOKELEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS UHURU KENYATTA

$
0
0

Rais Dkt John Pombe Magufuli, akilakiwa na Mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta alipokaribishwa Ikulu, Nairobi nchini Kenya leo. Rais Magufuli yupo nchini Kenya kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais Dkt John Pombe Magufuli (kulia) akiwa na Mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta wakipokea salamu za kijeshi, katika viwanja vya Ikulu ya Kenya, Jijini Nairobi leo.
Rais Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride la Jeshi la Kenya, alipowasili Ikulu jijini Nairobi leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na ujumbe wake katika mazungumzo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na ujumbe wake katika Ikulu ya Nairobi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mbalimbali wa Kenya mara baada ya kumaliza  mazungumzo yao na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

matembezi ya hisani ya amref health africa tanzania

RIDHIWANI:NITAHAKIKISHA NATATUA KERO ZA WANANCHI KWA WAKATI

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akifurahia jambo  na moja wa vijana wa Skauti eneo la Visakazi alipotembelea jimboni humo.

Mwenyekiti wa Chama cha CCM Tawi la Visakazi akieleza baadhi ya malalamiko ya wananchi mbele ya  Mbunge wao Ridhiwani Kikwete hayupo pichani kwenye ofisi ya chama hicho katika mkutano.


Mbunge Ridhiwani Kikwete wa pili upande kushoto  ashiriki katika mazishi  Mama mzazi wa Diwani wa zamani Kata ya Bwilingu Ndg.Rashidi Shomari Lugazo na wa kwanza upande wa kulia ni Sheikh Hussein wa Bwilingu akitoa neno la Mawaidha katika msiba
-------
Wananchi katika jimbo la Chalinze mkoani Pwani, wamekiri kuona mwanga kwa jinsi viongozi wanavyotatua matatizo yao, kufuatia kuongezeka kwa ushirikishwaji wa wananchi katika kutoa kero zao mbele za viongozi na kujadiliana utatuzi wake kwa pamoja.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa mkutano kati ya wananchi wa kitongoji cha Visakazi kata ya Ubena Chalinze na Mbunge wa Chalinze RIDHIWANI KIKWETE, ambapo sehemu kubwa ya wananchi waliohojiwa wameonyesha kukubali kwamba mikutano ya majadiliano mara kwa mara kati ya viongozi na wananchi huongeza ufanisi katika utendaji. 

Naye Mbunge wa Chalinze kwa upande wake amebainisha kuwa mikutano hiyo ni sehemu ya utaratibu wa kiuongozi ambao amejiwekea katika kuhakikisha anatatua kero za wananchi wake kwa wakati muafaka na kwa kiwango kinachotakiwa.

Wakati wa mkutano huo, wananchi hao wameshukuru kwa kazi kubwa ambazo tayari zimefanyika katika jimbo hilo ikiwemo uimarishaji wa huduma za  afya, elimu na pamoja na mambo mengine ya kijamii.

“Mbunge huyu amekuja na staili kama ya wakati wa mzee wake wananchi tunapewa nafasi tunasema hata yetu binafsi naamini hii itasaidia sana na utakuwa karibu na wananchi wako", alisema Bi Semeni Masound, 

Aidha  wameelezea kuridhishwa na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa katika kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

katika hatua nyingine Mbunge Ridhiwani ameshiriki katika mazishi ya Mama mzazi wa Diwani wa zamani Kata ya Bwilingu Ndg.Rashidi Shomari Lugazo.

Mbunge huyo ataendelea na ziara ya kutembelea wananchi tarehe 5 novemba.

Viewing all 110019 articles
Browse latest View live




Latest Images