Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1411 | 1412 | (Page 1413) | 1414 | 1415 | .... | 3285 | newer

  0 0

    Hivi karibuni kumeibuka upotoshaji mkubwa kutoka kwa baadhi ya watu wenye nia ovu ya kutaka kuharibu taswira nzima ya Mshindi wa shindano la Miss Tanzania 2016,aliyevishwa taji hilo jana usiku ndani ya jiji la Mwanza,taarifa hizo ambazo zimekuwa zikisambazwa katika mitandao ya kijamii zikieleza upotoshaji wa taarifa mbalimbali za mlimbwende huyo zikiwemo na elimu yake.


  SEHEMU YA TAARIFA ILIYOKUWA IKIPOTOSHWA KATIKA MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII HII HAPA CHINI;

  MISS TANZANIA 2016
  🙊🙊🙊🙊🙊🙊
  JINA:Diana Edward Lukumai
  UMRI:Miaka 18
  ELIMU:Shahada(degree)
  Hii ina maana;
  Alianza Chuo akiwa na miaka 15
  Alianza Form one akiwa na miaka 9
  😂😂😂😂😂😂
  Ingawa sio mshabik wa haya mambo napenda nchukue hii nafasi kuwapongeza Wazazi wote kama wazazi wa Diana ambao watoto wao wameanza shule ya msingi wakiwa na miaka miwili


  HII NDIO TAARIFA SAHIHI YA MSHINDI WA SHINDANO LA MISS TANZANIA 2016,DIANA EDWARD LOY.

  Napenda kuujulisha Umma yafuatayo;

  1. Miss Tanzania 2016/2017 aliyeshinda taji jana jijini Mwanza, anaitwa Diana Edward Loy na siyo Diana Lukumai kama inavyotajwa mitandaoni.

  2. Mlimbwende huyo amemaliza kidato cha nne 2015 Shule ya Sekondari Arusha Day na si 2011 kama inavyotajwa mitandaoni kwa malengo ovu.

  3. Diana hajawahi kujiunga na Elimu ya Chuo Kikuu chochote Tanzania au duniani bali anatarajia kujiunga mwaka huu katika chuo cha IFM kusomea masula ya kodi ngazi ya stashahada (cheti) ingawa kulingana na ratiba zake na majukumu yake mapya ikiwemo kushiriki Miss world mapya huenda akaahirisha mwaka wake wa masomo.

  4. Tunawasihi watanzania kutumia vyema mitandao ya kijamii na si kufanya "Character assassination" lakini pia tunaheshimu haki yao ya msingi ya kuhoji masuala ya msingi kabisa kuhusu mtu ambaye ni Public figure na ataliwakilisha taifa katika anga za kimataifa.

  Tumuunge mkono mlimbwende wetu ili atuletee Taji la Dunia.

  Ahsanteni.

  Charles William
  Kaimu Ofisa Habari wake.
  (wilflow101@gmail.com).

  0 0

  Na Ally Daud-MAELEZO.

  MUSWADA wa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 umeonekana kuwa mlinzi kwa wanahabari nchini kwa kuwa na kipengele kinachowataka waajiri kuwapa bima na mifuko ya hifadhi ya jamii waajiriwa wake mara baada ya kuwaajiri kama wafanyakazi halali wa chombo husika.

  Hayo yamesemwa na Mwenyekiti na Mratibu wa kampeni ya Media Car Wash for Cancer Bw. Benjamin Thomson Kasenyenda wakati wa kutoa maoni kuhusu Muswada wa Sheria ya huduma za Habari ya 2016 hivi karibuni.

  “Hakika Muswada huu umekuja muda muafaka kwani tumepitia changamoto nyingi sana kama wanahabari ikiwa ni kupata ajali na kuugua mara kwa mara bila ya kuhudumiwa chochote na wamiliki wa vyombo husika vya habari hapa nchini” alisema Bw. Kasenyenda.

  Aidha Bw. Kasenyenda ambaye pia ni Mwanahabari mkongwe anayetumikia hii tasnia kwa muda mrefu amesema kuwa wanahabari wanatakiwa kuishukuru Serikali kwa kuleta huu muswada kwani una manufaa na ulinzi kwa wanahabari pindi wanapokuwa maeneo yao ya kazi .

  Mbali na hayo Mwanahabri huyo mkongwe nchini amesema kuwa wanahabari wanatakiwa kuusoma vizuri huo muswada na kutumia fursa hii kwa kutoa maoni yao ili upite na kuwa sheria nchini na wasicheze ngoma za wanasiasa ambao wanajinufaisha wao wenyewe bila kujali maslahi ya mwanahabari nchini.

  Kwa upande wa Mmiliki wa Blogu ya jamii inayojulikana kwa jina la Fullshangwe Bw. John Bukuku amesema kuwa wanaishukuru Serikali kwa kuleta muswada huu kwani kwa upande wa kipengele cha kuwapa bima waandishi wa habari itawafanya wawe salama Katika kazi zao wakati wowote na sehemu yoyote.

  “Naishukuru Serikali kwa kuleta muswada wa sheria ya habari hasa kwenye kipengele cha bima na mfuko wa hifadhi ya jamii kwani utakua ulinzi tosha kwa mwanahabari pindi atakapoumwa au kufariki itakuwa msaada mkubwa kwetu sisi wenyewe” alisema Bw. Bukuku.

  Naye Mwandishi wa habari wa gazeti la Majira anayeripotia Tanga Bw. Mashaka amesema kuwa wanahabari wasibweteke katika kutoa maoni kuhusu huu muswada kwani ndio kimbilio la haki zao kutoka kwa waajiri wao ili kufanya kazi zao kwa usalama na amani wawapo sehemu zao za kazi.

  “Kwakweli wanahabari umefika muda wetu wa kufanya kazi kwa usalama na haki kama muswada huu utapita kwani utatufanya tupate haki yetu ya msingi Katika kazi zetu hivyo tusibweteke kutoa maoni yetu ili tuupitishe huu muswada kwa maendeleo yetu wenye”alisema Bw. Mashaka.

  Muswada wa sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 kifungu cha 58(1) kinasema mwajiri ni lazima amwekee bima na mfuko wa hifadhi ya jamii mwajiriwa wake hivyo wanahabari wanatakiwa kutoa maoni yao kupitia cna@bunge.co.tz.

  0 0

  Na Alda Sadango-Afisa Habari
  Halmashauri ya Wilaya Handeni
  Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe amewataka Maafisa Tarafa, Maafisa Watendaji wa Kata, Watendaji wa Vijiji na Wenyeviti wa Vijiji kusimamia misingi ya utawala bora katika kutimiza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi. Mh Gondwe aliyazungumza hayo katika kikao kazi alichokiitisha mwishoni mwa iki Oktoba 28/2016. 

  Mh. Gondwe amewataka viongozi kusimamia rasilimali za umma ikiwemo misitu, ardhi na usimamizi wa suala zima la usafi na mazingira katika maeneo yao. Pia aliwakumbusha kusikiliza kero za wananchi kuanzia ngazi ya chini ikiwa na kushughulikia malalamiko yao kabla ya kufika ngazi ya Wilaya. Wananchi wanatakiwa kusikilizwa matatizo yao, pale ambapo ngazi za chini zimeshindwa basi ngazi ya Wilaya itashughulika kikamilifu.

  Mh. Gondwe amewaeleza Maafisa Watendaji na wenyeviti wa Vijiji kwamba kutokana na hali mbaya ya chakula suala la kulima ekari moja ya muhogo kwa kila kaya ni lazima sio jambo la hiari tena. Aidha amepiga marufuku kutumia mazao ya chakula katika kutengenezea pombe kwa sababu hali ya chakula kwa sasa katika Wilaya ya Handeni sio nzuri.” Ni marufuku mazao ya chakula kutumika katika kupikia pombe kwa sababu hatuna chakula cha kutosha” alisema.

  Ametoa tahadhari kwa viongozi na Watendaji kuwa makini na taasisi zisizo za kiserikali (NGO’s)zinapokuja kufanya huduma katika maeneo yetu, kwani taasisi nyingine zinakuwa hazina dhamira njema kwa wananchi kwani zimeonekana kufanya mambo ya kitapeli mfano baadhi yao zimekuwa zikichangisha fedha kwa wananchi bila kufuata utaratibu., ,”Viongozi wote na Maafisa Tarafa pale mnapoona kwenye maeneo yenu kuna taasisi zisizo za kiserikali zimekuja na hamuelewi mienendo yao tafadhali naomba mtoe taarifa mapema ili Uongozi wa Wilaya uweze kushughulikia mapema ” alisema.
   Mkuu wa Wilaya Mh. Godwin Gondwe akizungumza na viongozi watendaji na Maafisa Tarafa.
   Hapo ni mkurugenzi mtendaji akizungumza na viongozi watendaji na Maafisa Tarafa. 
   Mmoja wa Wenyeviti wa Vijiji akizungumza katika kikao kazi hicho.
   Afisa utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Abel Noel akitoa ufafanuzi wa misingi ya Utawala bora.
   Viongozi watendaji, Maafisa Tarafa waliofika katika kikao kazi cha DC.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0
  Rais Dkt John Pombe Magufuli             
   


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kesho tarehe 31 Oktoba, 2016 ataanza ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini Kenya kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.

  Rais Magufuli anatarajiwa kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi majira ya saa nne asubuhi na baadaye kupokelewa rasmi na mwenyeji wake Rais Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi ambako viongozi hao watafanya mazungumzo rasmi.

  Pamoja na kufanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais Magufuli atakwenda kutoa heshima katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta na pia anatarajiwa kuhudhuria dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta Ikulu Jijini Nairobi

  Katika ziara hii Rais Magufuli anatarajiwa kutembelea kiwanda cha maziwa cha  Eldovillekilichopo Karen Jijini Nairobi, na pia anatarajiwa kuzindua barabara mchepuko ya Southern By-pass iliyopo Jijini Nairobi.

  Barabara hiyo mchepuko ya Southern By-pass ni moja kati ya miradi mikubwa ya barabara nchini Kenya, inaunganisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi kwa barabara za juu na chini na imejengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika Jiji hilo.

  Rais Magufuli anatarajiwa kumaliza ziara yake tarehe 01 Novemba, 2016 na kurejea Jijini Dar es Salaam.


  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Nairobi
  30 Oktoba, 2016. 

  0 0


  0 0

   Golikipa wa Mbao FC, Emanuel Mseja akiruka kudaka mpira bila mafanikio uliokwenda moja kwa moja wavuni baada ya kurushwa na Mchezaji wa Yanga, Mbuyi Twite na kuiandikia timu yake bao la pili katika Mchezo uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam leo. Yanga imeshinda goli 3-0.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  MABINGWA watetezi wa ligi kuu Vodacom Tanzania Bara, Yanga wamefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Mbao Fc ya mkoani Mwanza na kufikisha alama 27 nyuma ya alama tano kwa mahasimu wao wa jadi Simba.

  Kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu sana kwa Yanga hasa baada ya Mbao kuonekana wako makini katika kuhakikisha hawaruhusu goli la mapema na mpaka zinafikia dakika 45 za kipindi cha kwanza timu hizo zilienda mapumziko 0-0.

  Kipindi cha Pili kilianza kwa kasi kwa Yanga kutafuta goli la dakika ya 53, mpira wa adhabu uliopigwa na Haruna Niyonzima na kumfanya golikipa wa Mbao kushindwa kuudaka na baada ya beki wa kimataifa wa Yanga toka nchini Togo, Vicent Bossou kuumalizia kwa kichwa na kuiandikia Yanga goli la kwanza.
  Dakika ya 55, Mkongo Mbuyi Twite anarusha mpira unaomponyoka golikipa wa Mbao, Emanuel Mseja na kuingia nyavuni na kuiandikia Yanga goli la pili na Amisi Tambwe akitumia madhaifu ya mabeki hao na kuiandikia Yanga goli la tatu na la ushindi.

  Mabadiliko ya Yanga yaliifanya safu ya ulinzi ya Mbao kuanza kucheza kwa umakini zaidi hasa baada ya kuingia Donald Ngoma na kutoka Obrey Chirwa, Deus Kaseke kutoka na kuingia Juma Mahadhi pamoja na Hassan Kessy na nafasi yake kuchukuliwa na Kiungo Thaban Kamosoku.

  Baada ya ushindi huo, Yanga wanakwea pipa hadi Jijini Mbeya kwenda kuvaana na Mbeya City Novemba 02, na kumaliza na Prison Novemba 06  kabla ya kurejea tena Dar es salaam kuvaana na Ruvu Shooting Novemba 11.
   Hassan Kessy wa Yanga, akitafuta namna ya kuitona Ngome ya Timu ya Mbao FC, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo katika Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda goli 3-0.


  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizindua kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO).

  Na Peter Daffi, Dodoma

  Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deo Ndejembi ameanzisha kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO) yenye dhamira ya kuwasaidia wananchi kuondokana na hali yanjaa ambayo ni kadhia kubwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo sambamba na Taifa kwa ujumla.

  Kuanzishwa kwa Kampeni ya Okoa njaa Wilaya ya Kongwa imejili wakati Mkuu huyo wa Wilaya ya Kongwa Akizungumza na Wakuuwa Idara na vitengo, Madiwani wa Kata zote zilizopo Wilayani humo, Watendaji wa Kata, Maafisa Tarafa, Waratibu Elimu Kata, Wenyeviti wa Vijiji vyote 87 vya Wilaya ya Kongwa na watendaji wao, pamoja na wadau waalikwa na Kilimo.
  Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizungumza mara baada ya kuzindua kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO).

  Akizindua kampeni hiyo Dc Ndejembi alisema kuwa Kampeni hiyo imezinduliwa Mwezi Octoba kwa ajili ya msimu wa mwaka 2016/2017 na inatarajiwa kuwa kampeni Endelevu katika kipindi cha Miaka mitano.

  Ameeleza kuwa huu ni mkakati maalumu katika Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma ili kukabiliana na hali ya Ukame ambayo ni tatizo sugu katika maeneo mengi nchini.

  Kutokana na hayo DC Ndejembi ameagiza kuwa na kilimo cha Mtama zaidi kuliko Mahindi. Kwani Wilaya ya Kongwa ina Kaya 59141, na kila kaya kama ikilima Heka mbili (2) za Mtama, Mavuno itakuwa Tani 71000, za Mtama sawa na 83% ya hitaji la chakula Wilayani Kongwa.
  Ofisa Kilimo Mkoa wa Dodoma Bi Aziza Mumba akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Okoa Njaa Wilayani Kongwa.


  0 0


  Basi lenye namba za usajili T990 AQF la kampuni ya Safari Njema liililokuwa likitokea Dodoma kuja jijini Dar, limeteketea kwa Moto maeneo ya Kimara Stop Over-Suka,mara baada ya kugongana na Lori lililokuwa limebeba shehena ya mifuko ya Cement (namba zake za usajili hazikujulikana mara moja),jioni ya leo,Inaelezwa kuwa mali zote zilikowemo katika basi vimeteketea kabisa kwa moto,hali ya abiria waliokuwemo ndani ya basi hilo tutawaleta taarifa kamili itakayotolewa na Jeshi la Polisi.

  UPDATES 
  Jeshi la Polisi limeeleza kuwa mtu mmoja amefariki Dunia katika ajali hiyo na wengine 16 wamejeruhiwa na baadae  kukimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.
   Pichani Lori kama lionekavyo likiwa nyuma ya basi baada ya kugongana kusababisha mlipuko mkubwa wa moto na kupelekea magari yote mawili kuwaka moto . 
  Baadhi ya Wakazi wa eneo la Kimara Stop Over na Kimara Suka wakielekea kushuhudia eneo la ajali kati ya basi la Safari Njema na Lori lililokuwa limebeba shehena kubwa ya mifuko ya Cement.
   Baadhi ya mashuhuda wakishuhudia tukio hilo lilivyokuwa
   Gari la zima moto likiwa eneo la tukio kuuzima moto huo.
   Baadhi ya Vijana wasio waaminifu walivamia eneo hilo la ajali na kuanza kuondoka na mifuko ya Cement iliyokuwa imebebwa na Lori hilo.

  0 0

  Na Vero Ignatus, RSA Arusha. 

  Mabalozi wa usalama wa barabarani (Road Safety Ambassadors - Arusha) wamesherehekea sikukuu ya kuzaliwa ya Kamanda Mohammed Mpinga jijini Arusha.  Hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Milestone Park -Sakina , imeandaliwa na kamati ya (RSA -Arusha) chini ya mwenyekiti wa mkoa Bi. Stella Rutaguza na kuhudhuriwa na wajumbe wa( RSA - Arusha)  "Kwakweli mmenistua jamani sikutegemea kama mmeniandalia jambo kubwa kama hili ,nilijua nakuja kukutana tu na mabalozi ili kufahamiana na kuongelea maswala yetu ya usalama barabarani "alisema Mpinga. 

  DCP Mpinga mbaye yupo kikazi jijini Arusha alikutana na mabalozi wa usalama barabarani,kwa lengo la kuongelea na kujadili maswala ya usalama barabarani na mabalozi hao,ambao kazi yao kubwa ni kuelimisha jamii,kukemea na kuripoti matukio yanayoathiri usalama barabarani,na kushawishi mabadiliko ya tabia ,sheria na sera. 

  Amezungumzia changamoto iliyopo kwa sasa kwa utoaji wa risiti pale dereva anapotakiwa kulipa faini kutokana na makosa yanayofanyika barabarani,amesema kuwa mfumo huo wa kieletroniki tayari umeshaanza kutumika jijini Dar-es-salaam na hivi karibuni mfumo huo utaanza kutumika katika mikoa sita iliyopewa kipaumbela kabla ya mwaka huu kumalizika.
  Kamanda Mohamed Mpinga akipokea "Birthday Surprise Cake " kutoka kwa Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bi. Stella Rutaguza katika hafla ya Sikukuu ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016. PICHA NA GADIOLA EMANUEL
  Kamanda Mohamed Mpinga akikagua "Birthday Surprise Cake " aliyopewa na Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bi. Stella Rutaguza katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
  Katibu wa RSA - Arusha Bw. Gadiola Emanuel akigonga Cheers na Kamanda Mohamed Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
  Kamanda Mohamed Mpinga akipata picha ya pamoja na Mabalozi katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.  0 0
  0 0

   Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi,Mwanasha Tumbo katikati akiongozwa na Diwani wa Kata ya Potwe, Rashid Mdachi na Mwenyekiti wa Serikali ya  Kijiji cha Zeneti wakitembelea Jengo jipya la Zanahati ya Zeneti iliyojengwa kwa ushirikiana baina ya Halmashauri, Wananchi na Shirika la World Vision na Mbunge wa Jimbo hilo ambalo limegharimu kiasi cha milioni 35.2
   Kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Muheza,Mathew Mganga akimuongozwa Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat, Mhandisi Mwanasha Tumbo aliyetembelea zahanati ya Zeneti kuona jinsi inayoendelea na ujenzi wake kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Zeneti
   Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat, Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akiingia kwenye vyumba vya zahanati mpya ya Zeneti kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza,Lwiza Mlelwa.


  0 0

  Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Kampuni ya Clarkson Insurance Brokers inayojishughulisha na masuala ya bima Bw. Godfrey Simbeye ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF akionyesha zawadi aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa Kampuni ya Clarkson Insurance Brokers Justin Lambert mara baada ya uzinduzi wa kampuni hiyo uliofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.

  Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Kampuni ya Clarkson Insurance Brokers inayojishughulisha na masuala ya bima Bw. Godfrey Simbeye ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF akizungumza wakati alipozindua Kampuni ya bima ya Clarkson Insurance Brokers kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande Othman akizungumza na Balozi Mstaafu Peter Kalaghe wakati wa uzinduzi wa kampuni ya Clarkson Insurance Brokers inayojishughulisha na masuala ya bima katika uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Parkal Randall ambayo ni Kampuni Tanzu ya Clarkson Insurance Brokers Bw. Coutts Otolo.


  0 0

  Na Lulu Mussa TABORA 

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. Jauary Makamba amempongeza Bw. Leordard Kushoka kwa kubuni kiwanda kinachotengeza nishati mbadala rafiki kwa mazingira.

  Akiwa Mkoani Tabora, Waziri Makamba alipata fursa ya kutembelea kiwanda hicho na kusema kuwa Serikali inathamini sana ubunifu na uvumbuzi hasa unao okoa mazingira. “Bwana Kushoka mimi nakupongeza sana, niliona jitihada zako kupitia kipindi cha televisheni na kuamua kukuita na kukusaidia” alisisitiza Waziri Makamba.

  Katika kuthamini mchango wa Kiwanda hicho cha “Kuja na Kushoka” Ofisi ya Makamu wa Rais imemsaidia Bw. Kushoka kupata haki miliki ya Kiwanda hicho.

  Awali Bw. Leonard Kushoka, Mkurugenzi wa Kuja na Kushoka Tools Manufacture Group amesema kuwa kiwanda chake kimefanikiwa kutoa ajira kwa vijana 13 na kufanikiwa kubuni teknolojia mbalimbali rafiki kwa mazingira ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kuwafikia vijana zaidi ya 50 katika Wilaya za Tabora Manispaa, Urambo, Kaliua, Mlele pia Katavi na kufanikiwa kuwafundisha utengenezaji wa Majiko banifu yanayopunguza matumizi ya kuni na mkaa kwa asilimia 50.

  Pia Kiwanda hicho kimefanikiwa kubuni mashine ambayo ina uwezo mkubwa wa kuzalisha kilo 160 kwa saa kwa kutumia dizeli lita 5 na kuzalisha wastani wa Kilo 1000 za mkaa mbadala na pia Kiwanda hicho kimefanikiwa kubuni mtambo kwa kukaushia tumbaku kwa kutumia taka kavu au mabaki yote ya mazao kama maganda ya karanga, randa za mbao, magunzi ya mahindi na masuke ya mpunga.

  Bw. Kushoka amesema kuwa “Mtambo huu umetoa matokeo mazuri katika ukaushaji wa tumbaku kwani wastani wa matumizi ya taka kilo 3 hukausha kilo moja ya tumbaku kwa kutumia mabani ya kisasa” Bw. Kushoka amemuomba Waziri kuisaidia Kampuni hiyo kupata mafunzo mbalimbali ya namna bora zaidi ya kubuni na kuendeleza uzalishaji wa nishati mbadala hasa katika nchi zinazofanya vizuri zaidi.

  ‘Kuja na Kushoka” ilianzishwa rasmi mwaka 2000 na kupata usajili mwaka 2013 na kupewa hati (TMC/CO/CBO/48).

  Waziri Makamba akiwa katika Mkoa wa Tabora pia amepata fursa ya kutembelea Wilaya ya Nzega na Igunga, akihitimisha ziara yake ya Mikoa 10 hapa nchini yenye changamoto za kimazingira.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akipata maelezo kutoka kwa Bw. Leonard Kushoka wa pili kulia katika hatua mbalimbali za uzalishaji wa nishati mbadala. 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akiangalia mkaa uliokamilika baada ya uzalishaji, mkaa ambao ni rafiki kwa mazingira. 

  0 0

   Kamanda Mohamed Mpinga akipokea "Birthday Surprise Cake " kutoka kwa Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bi. Stella Rutaguza katika hafla ya Sikukuu ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016. PICHA NA GADIOLA EMANUEL.
    Kamanda Mohamed Mpinga akipokea Chupa ya Shampeni kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bw. Bakari Msangi katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
   Katibu wa RSA - Arusha Bw. Gadiola Emanuel akigonga Cheers na Kamanda Mohamed Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.


  0 0  0 0

      Kaimu Mkurugenzi  Huduma kwa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF ramadhani Mkeyenge akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dodoma kuhusu miradi iliyotekelezwa  na LAPF katika maeneo mbali mbali nchini. 

   Maabara ya Kompyuta katika Chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo 
   Baadhi ya Maofisa wa LAPF pamoja na waandishi wa Habari wakitembelea mradi wa mabweni katika Chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo nje kidogo ya manisapaa ya Dododma. LAPF imetumia bilioni 39 kujenga baadhi ya majengo na miundimbinu katika chuo hicho. 

    Mradi wa Mabweni katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). LAPF imetumia bilioni 22 kujenga majengo na miundimbinu katika Chuo cha Elimu ya Tiba na Afya chuoni hapo kwa awamu ya kwanza ya mradi huo. 
  Moja ya Vyumba vya madarasa katika Chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo (Sehemu ya mradi wa LAPF). Darasa hili lina uwezo wa kuchukua wanafunzi 520 kwa wakati mmoja. 


  0 0

  Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii asubuhi hii, inaeleza kuwa Bondia maarufu nchini, Thomas Mashali amekutwa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo na mwili wake kukutwa maeneo ya Tabata, Jijini Dar es salaam. akithibitisha kutokea kwa kifo cha mwanamasumbwi huyo, Bondia Abdallah Pazi (Dullah Mbabe) amesema Mashali amefikwa na umauti huo usiku wa kumkia leo kwa kudaiwa kupigwa mpaka kuuawa na watu wasiojulikana kwa tuhuma za wizi. tutaendelea kujuzana taarifa zaidi za msiba huu wa Mwanamasumbwi huyu nguli hapa nchini, endelea kutembelea Libeneke la Globu ya Jamii.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mhe. Gabriel Daqarro wakitoa Maagizo kwa watendaji wa serikali na taasisi kuwapa kipaumbele cha kwanza wazee wakati akiongea na wazee wa Halmashauri ya jiji la Arusha leo jijini Arusha. Picha zote na Mahmoud Ahmad, Arusha

  Katikati Ni mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro na kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Arusha David Mwaiposa na kushoto ni mwenyekiti wa baraza la wazee wilaya Arusha Mhina Sezua wakati wa mkutano na mkuu huyo wa wilaya kubaini changamto mbali mbali wanazokumbana nazo wazee wilayani hapa

  Meza kuu wakifuatilia hoja mbali mbali zilizokuwa zinatolewa na wazee leo jijini Arusha

  Sehemu ya wazee waliohudhuria mkutano huo wakiwa wanamsikiliza mkuu wa wilaya Gabriel Daqarro

  Katibu wa wazee akiongea katika mkutano huo.
  Kwa taarifa kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Timu ya taifa ya michezo ya kabbadi nchini tanzania inatarajiwa kushiriki kombe la dunia la michezo ya kabaddi yatakayoanza rasmi novemba mwaka huu katika jimbo la punjab.

  Hayo yamebainishwa na balozi wa india nchini Tanzania Mh. Sandeep Arya wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini dar es salaam na kueleza kuwa mchezo huo utashirikisha jumla ya watu 34 kati yao ikiwa ni timu ya wanawake na timu ya wanaume pamoja na makocha wa nne.

  "Tunafuraha kwa nchi ya tanzania kupata washiriki watakaoenda nchini india kushiriki kombe hilo la dunia la kabadi wanaume wakiwa kumi na tano na wanawake kumi na tatu wakiongozwa na makapteni wao.

  Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi idara ya maendeleo ya michezo,Alex NKenyenge ameongeza kuwa serikali ya Tanzania itazidi kutoa ushirikiano na nchi hiyo hususani katika michezo ya jadi huku akizitaka timu hizo kufanya vizuri katika michuano hiyo ili kuipeperusha bendera ya Tanzania."Michezo isiishie hapa hasa hii ya jadi bali ipewe kipaumbele zaidi iweze kufika mbali na hvyo viongozi wasing'ang'anie michezo iliyozoeleka"aliongeza kaimu mkurugenzi .

  Kabaddi ni mchezo maarufu katika jimbo la punjab na mikoa mingine ya india ambapo hii ni mara ya sita kufanyika kwa kombe la dunia la mchezo huo ambapo kwa mwaka huu timu 13 kutoka sehemu mbalimbali za dunia zitashiriki ambazo ni Tanzania,USA,England,Kenya,India,Mexico n.k.

  Balozi wa India nchini Tanzania Sandeep Arya akizungumza na waandishi wa habar juu ya Mashindano hayo yatakayo fanyika nchini India mapema leo jijini Dar es salaam.
  Kaimu mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Alex Nkenyenge akizungumza na waandishi wa habar kuhusiana na Michuano hiyo leo jijini.

  Timu ya Wachezaji wa Mchezo wa Kabaddi wakiwa katika Picha ya pamoja na Balozi wa India Nchini Bw Sandeep Arya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Alex Mkenyenge leo jijini Dar.

  0 0older | 1 | .... | 1411 | 1412 | (Page 1413) | 1414 | 1415 | .... | 3285 | newer