Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1410 | 1411 | (Page 1412) | 1413 | 1414 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Kumekuwa na mgogoro wa muda mrefu kijiji cha Mgubike kiasi cha wananchi kugawanyika katika makundi na familia zikiwa haziongei. Mgogoro ulikuwa kati ya mwenyekiti aliyepita wa kijiji Bwana Msafiri Pamagila na Mwenyekiti wa sasa Bi Lenatha Mbilinyi. 
  Mgogoro huo umekuwa unakwamisha shughuli za maendeleo kwa muda mrefu. Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela alifanikiwa kufuta tofauti zilizokuwepo kati ya makundi hayo mawili. Mzee maarufu alimshukuru Mkuu wa wilaya kwa kazi hiyo.

  0 0

   Mwanafunzi wa darasa la sita Shule ya Msingi Sombetini Jackson Mutalemwa akiuliza swali baada ya kupata elimu ya Ukatili dhidi ya watoto kutoka Ofisi ya Dawati la Jinsia na watoto mkoani hapa.
   Mkuu wa kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Arusha Mkaguzi wa Polisi Happyness Temu akisisitiza jambo kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Sombetini wakati anatoa elimu juu ya Ukatili dhidi ya Watoto kushoto kwake ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Evelyn Simalenga. 
   Wanafunzi wa Shule ya Msingi Sombetini iliyopo jijini Arusha wakishangilia mara baada ya kupata elimu ya Ukatili dhidi ya Watoto iliyotolewa na kitengo cha Dawati la Jinsia na watoto la mkoani hapa
  Askari Polisi kutoka kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Arusha Happy Mshana akiwaelezea wanafunzi wa shule ya Msingi Sombetini iliyopo jijini hapa aina za Ukatili dhidi ya Watoto. 
  Picha na habari na Rashid 
  Nchimbi wa Jeshi la Polisi, Arusha


  0 0


  0 0

  Aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa
   Makosa ya Jinai Bw. Diwani Athumani


  0 0

  Na Lulu Mussa-Tabora

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira hii leo ameendelea na ziara ya kikazi katika Mkoa wa Tabora akitokea Mkoani Kigoma.

  Akiwa Mkoani Tabora Waziri Makamba ametembelea Wilaya ya Kaliua na kukutana na changamoto kubwa ya Uharibifu wa Mazingira na Uvamizi wa Misitu unaofanywa na wananchi. Katika Kijiji cha Ufugala Wilaya ya Kaliua Waziri Makamba amefanya Mkutano wa hadhara kijijini hapo na kubaini kuwa Kitongoji hicho hakikufuata taratibu za kisheria katika kuanzishwa kwake na kimeanzishwa ndani ya Hifadhi.

  Akitoa maelezo ya Awali Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Bw. Abel Yeji Busalama amemueleza Waziri kuwa Kitongoji hicho kiko ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Kijiji ambapo jumla ya Vijiji 11 viamua kutenga eneo hilo kwa ajili ya Hifadhi.

  Bw. Busalama amesema kuwa wakazi hao wamekwisha amriwa kuondoka katika hifadhi hiyo na utekelezaji wake unaendelea.

  Akijibu hoja zilizowasilishwa na wakazi wa eneo hilo Waziri Makamba amesema kuwa wajibu wa Serikali ni kuhakikisha kuwa Sheria, tararibu na kanuni zinafuatwa bila kukiukwa. Waziri Makamba pia amesisitiza kuwa maamuzi ya matumizi bora ya ardhi yapo mikononi mwao. “Ndugu zangu ni nyinyi wenyewe mliamua kutenga eneo hili maalumu kwa hifadhi ya msitu wa kijiji na kufuata taratibu zote za kisheri katika kuusajili, maamuzi yenu ya awali yatabaki palepale mpaka mtakapofuata taratibu nyinginezo.” Makamba alisisitiza.

  Aidha, Waziri Makamba ameahidi kuwasilisha suala hilo kwa Wizara ya Maliasili na Utalii na ile ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ili kupata ufumbuzi wa kudumu. “Nitaongea na Mawaziri wenzangu na kuleta timu ya wataalumu kupitia upya mipaka ya kijiji na kuifanyia kazi” Makamba alisisitiza.

  Kuhusu hifadhi ya Mazingira Waziri Makamba amewataka wakazi wa Ufulaga kuacha tabia ya kukata miti ya asili na kusisitiza kuwa uharibifu wa mazingira unabadilisha tabia za watu. “Wana Ufulaga, binadamu wakiharibu mazingira kwa kiasi kikubwa wanaanza wizi na udokozi na wanyama wataanza kuwinda watu kwa kukosa malisho” alisema Waziri Makamba.

  Waziri Makamba pia amefanya ziara katika Wilaya ya Urambo na kubaini changamoto kubwa ya uvamizi wa misitu na ukataji wa miti ya asili kwa ajili ya kuni za kukaushia tumbaku.

  Waziri ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutumia Sheria ya Mazingira namba 20 ya mwaka 2004 kifungu namba 196 (1) (a na b) kupiga marufuku ya matumizi ya majiko banifu ya kienyeji pia ukataji mkubwa wa miti ya asili kwa ajili ya biashara ya tumbaku. Katazo hilo litawahusu Wakulima na Vyama vya Msingi vyote vinavyojishughulisha na biashara ya tumbaku.

  Waziri Makamba anaendelea na ziara yake kwa kutembelea Wilaya za Nzega na Igunga.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akifafanua jambo kuhusu wananchi waliovamia msitu wa hifadhi ya Kijiji. Kushoto ni Bi. Veronica Nyasa mkazi wa eneo hilo ambae amesema yuko tayari kuondoka endapo atapatiwa sehemu mbadala.
  Uongozi wa Wilaya ya Kaliua wakimwonyesha Waziri Makamba magogo ya miti ya asili yanayotumiwa na wanachi katika kukaushia tumbaku kwa kutumia majiko ya kienyeji
  Pichani ni moja ya majiko ya kienyeji yanayotumia kuni/miti mingi katika kukaushia tumbaku. Waziri Makamba amewaagiza wakazi wa Kitongoji cha Mtakuja Magharibi kutumia majiko banifu ili kunusuru ukataji miti kwa wingi husnan ile ya asili.

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba amesema kuwa sheria ya Huduma za Habari itatungwa kulingana na maoni yaliyowasilishwa kutoka kwa baadhi ya wadau ili muswada huo usihairishwe kama miaka iliyopita.

  Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Mwenyekiti ya Kamati hiyo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya kamati hiyo baada ya kuongeza muda wa siku 10 kwa wadau ili waweze kuusoma kwa makini muswada huo.

  Serukamba amefafanua kuwa Muswada ukishasomwa kwa mara ya kwanza ni jukumu la wananchi kutoa maoni yao juu ya suala husika lakini kwa miaka takribani 23 wadau wa tasnia ya habari hawajaonesha nia ya utayari wa kutoa maoni yao na kuendelea kuiomba Serikali kuupeleka mbele mswada huo.

  “Kwa mwaka huu tena wadau hawa waliomba Muswada huu usogezwe mbele, lakini hatuwezi kuacha kutunga sheria kila siku kwa sababu ya baadhi ya wadau kutoleta maoni yao, tutaendelea kutunga sheria hii kulingana na maoni yaliyowasilishwa na baadhi ya wananchi na wadau”, alisema Serukamba.

  Amesema kuwa tangu mwaka 1993 huu ndiyo umekuwa mchezo unaofanywa na wadau wa tasnia hiyo ambapo kwa mwaka huu pia wadau hao walikuja na maoni lakini kwa makusudi waliamua kutoyatoa.

  Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa Oktoba 31 mwaka huu watakutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye kwa ajili ya kukubaliana juu ya vifungu ambavyo wamekuwa wakivijadili kwenye vikao vya kamati ili kuviweka kwenye Muswada tayari kwa kwenda kusomwa Bungeni.

  Aidha, amewataja baadhi ya wadau wa tasnia hiyo ambao wamekiri kupokea barua ya mwaliko wakuhudhuria kikao cha kamati hiyo kuwa ni Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Pili Mtambalike, Umoja wa Vyama vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na Baraza la Habari Tanzania (MCT).

  Amewashukuru wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa habari waliotoa maoni yao na amewatoa hofu kuwa muswada huo utatendewa haki na itatungwa sheria nzuri ambayo itarudisha heshima ya tasnia hiyo.

  Muswada huo ulisomwa bungeni kwa mara ya kwanza Septemba 16 mwaka huu na Waziri mwenye dhamana Mhe. Nape Nnauye ambapo baada ya hapo wananchi walitakiwa kuusoma na kutoa maoni yao.
  Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakiendelea na kazi ya kuchambua maoni yaliyotumwa na wadau wa habari ili kuboresha Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo mjini Dodoma.

  0 0


  NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO

  SERIKALI imewaagiza wakuu wa Mikoa na wilaya pamoja na wakurugenzi wote nchini kuweka programu kwa ajili ya kutenga maeneo maalumu yatakayotumika kwa ajili ya uwekezaji wa kujenga viwanda lengo la kuweza kuwakomboa vijana kupata soko la ajira ambalo litaweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.

  Hayo yalisemwa na Waziri wa viwanda biashara na uwekezaji Charles Mwijage wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa maonyesho ya 9 ya wajasiriamali mbali mbali kutoka mikoa mitano ya kanda ya mashariki yaliyofanyika katika viwanja vya Mwanakalenge Wilayani Bagamoyo.

  Mwijage alisema kwamba mikakati ya serikali ya awamu ya nne ni kuwa na nchi yenye viwanda vya aina mbali mbali ambavyo vitaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza wimbi la umasikini na kuwataka watendaji na viongozi kuchana na tabia ya kuuza maeneo kiholela.

  Aidha Mwijage alibainisha kwamba shirika la viwango Tanazania (TBS) pamoja na mamlaka ya chakula na TFDA kuhakikisha wanapunguza tozo za viwango na kutokwamisha vibali kwa wafanyabiashara wado wadogo na badala yake wawapatia fursa ya kuweza kuuza bidhaa zao kwa urahisi bila ya kuwa na masharti mengi.

  Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa shirika la viwanda vidogo vidogo (SIDO) Tanzania Profesa Syvester Mpanduji amesema kuwa kwa sasa wameshafanya maonyesha ya kitaifa 97 ya wajasiriamali ambayo yameweza kuwaingizia kiasi cha shilingi billion 16.8,na kuongeza lengo lao kubwa ni kuwawezesha kuwapatia mikopo pamoja na kuwajengea viwanda vidogo vidogo.

  Awali akisoma risala kwa niaba ya wajasiriamali wote walioshiriki katika maonyesho hayo Issa Njoka amesema kwamba serikali inapaswa kuhakikisha inawasaidia katika kuwaongezea mitaji sambamba na kuwasaidia kufanya maonyesho ya bidhaa wanazozitengeneza kuanzia ngazi za wilaya hadi Taifa ili waweze kutambulika zaidi.

  Maonyesho hayo ambayo yameandaliwa na shirika la viwanda vidodovidogo (SIDO) Mkoa wa Pwani yamewashirikisha wajasiriamali zaidi ya 200 kutoka mikoa mitano ya Dar es Salaam, morogoro, Lindi, Mtwara , pamoja na wenyeji Mkoa wa Pwani .
   Waziri wa viwanda biashara na uwekezaji Charles Mwijage akiwahutubia wajasiriamali walioshiriki katika  ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa  yaliyoendelea kufanyika katika viwanja vya mwanakalenge Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ambayo yameshirikishi jumla ya mikoa mitani ya kanda ya mashariki.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
   Waziri wa viwanda biashara na uwekezaji Charles Mwijage wa pili kulia akikata utepe na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikiro wakaati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa maonyesho ya wajasiriamali kanda ya mashariki yaliyofanyika kwenye viwanja vya mwanakalenge Wilayani Bagamoyo.
   Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Charles Mwijage akiangalia moja na biadhaa ambazo zimetengenezwa na wajasiriamali hao.

  0 0

  Na Dotto Mwaibale

  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wazazi na walezi kuwaacha huru watoto wao kuendelea na masomo wayapendayo badala ya kuwachagulia.

  Mwito huo ameutoa katika mahafali ya 32 ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Jitegemee JKT Mgulani Dar es Salaam jana ambapo alikuwa mgeni rasmi.

  "Watoto wapewe uhuru wa kile wanachopenda kukisomea badala ya kuwachagulia kwa kufanya hivyo itawasaidia kupenda kazi watakayoifanya kutokana na masomo waliyosoma" alisema Makonda.

  Alisema hivi sasa kuna changamoto kubwa kwa watumishi kujiingiza katika vitendo vya ubadhirifu kutokana na kutokuwa wazalendo kutokana na kufanya kazi ambayo imetokana na masomo ambayo hawakuyapenda.

  Alisema kama mtoto anapenda kuwa mtaalamu wa kompyuta muache aendelee na masomo ya kompyuta badala ya kumlazimisha kuwa na taaluma nyingine.

  Mkuu wa Shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy alisema wahitimu hao wameandaliwa vizuri kwa ajili ya kufanya mtihani wao watakao uanza Jumanne wiki ijayo na kuwa wanategemea wote watafanya vizuri.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), akizungumza na wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT Mgulani katika mahafali ya 32 yaliyofanyika jana. Makonda alikuwa mgeni rasmi. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hiyo, Brigedia Generali Laurance Magere.
  RC Makonda akimkabidhi cheti Mwalimu Bora wa Shule hiyo, Grace Eliyatosha Moshi.
  RC Makonda akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Bora,  Samuel Ndebeto.
  Mkuu wa Mkoa Paul Makonda (katikati), akiwa meza kuu na viongozi mbalimbali. Kutoka kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Kigamboni, Luteni Kanali, Laurent Mgongolwa, Mkurugenzi wa Mipango ya Huduma Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Kanali Festus Mang'wela, Mkuu wa Shule ya Sekondari Jitegemee, Luteni Kanali, Robert Kessy, Mwenyekiti wa Bodi wa shule hiyo, Brigedia Generali mstaafu, Laurence Magere, Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, Hashim Komba na Mjumbe wa Bodi wa Shule hiyo, Sebastian Enosh.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
 • 10/29/16--23:20: Article 3


 • 0 0


  Mshindi wa Miss Tanzania 2016, Diana Edward akiwapungia Mkono wanachi mara baada ya kuvishwa taji la Miss Tanzania 2016.
  Tano bora.
  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura  akimkabidhi ufunguo Mshindi wa Miss Tanzania 2016, Diana Edward mara baada ya kuibuka Mshindi wa Miss Tanzania 2016.
  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura  akimpongeza Mshindi wa Miss Tanzania 2016, Diana Edward.
  Mshindi wa Miss Tanzania 2016, Diana Edward akiwa na washindi wanne wa kwanza katika kinyang'anyiro cha Miss Tanzania 2016 jiji Mwanza leo.
  Picha na Avila Kakingo, Grobu ya Jamii Mwanza.  0 0
  0 0


   Rais Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza kwa kazi nzuri Katibu Mkuu wa  Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi baada ya kukagua akikagua pembe za ndovu 50 zilizokamatwa katika operesheni maalum ya  ya kusaka majangili alipofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii (MPINGO HOUSE) jijini Dar es salaam leo Oktoba 29, 2016.


  0 0

  Kocha wa JKT Mlale Edga Msabila akihojiwa na Ruvuma TV on Line baada ya mpira kumalizika na kutoka sale ya moja moja  na Coast Union ya Tanga katika mchezo uliochezwa uwanja wa MAJI MAJI uliopo miji Songea Mkoani Ruvuma

  0 0

   Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,wakimsikiza kwa makini Bw. Robert Mwaisambo Mkazi wa Morogoro, alipofika kununua simu katika gulio la Smart phone liliondandaliwa na kampuni hiyo katika viwanja vya sabasaba,Mkoani humo mwishoni mwa wiki
  Wakala wa Vodacom Tanzania,Abdalla Magala akimfafanulia jambo Alen  Anatory Mkazi wa Morogoro, kuhusiana na simu aliyonunua katika gulio la Smart phone liliondandaliwa na kampuni hiyo na kufanyika katika viwanja vya sabasaba,Mkoani humo mwishoni mwa wiki.


  0 0


  Na Theresia Mwami TEMESA iringa

  Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA) imeanzisha program ya kubaini vipuri bandia kwa ajili ya kuboresha huduma za matengenezo ya magari na mashine mbalimbali.

  Agizo hilo limetolewa na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt.Mussa Mgwatu alipotembelea karakana ya TEMESA mkoani Iringa kujionea jinsi karakana hiyo inayotumia kutumia mfumo huo wa kubaini vipuri bandia.

  Dkt Mgwatu ameongeza kuwa mfumo huu umekuja wakati sahihi kwani kwa sasa kumekuwa na uingizwaji wa vipuri bandia ambao umesababisha hasara kwa wamiliki wa vifaa vinavyotumia vipuri kutoka nje ya Tanzania.

  “Ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia inabidi tuwe na mfumo ambao utatusaidia kutambua vipuri bandia kwani vinakwamisha sana utendaji kazi wetu” alisema Dkt Mgwatu.

  Akieleza jinsi mfumo huo unavyofanya kazi, Meneja wa TEMESA Iringa Mhandisi Ian Makule alisema kuwa kwa kuingiza taarifa za namba ya gari husika kwenye program ya kompyuta, unaweza kubaini kama kipuri kinachokusudiwa ni halisi kabla ya kukiagiza.

  Mhandisi Makule aliongeza kuwa kama namba na jina la kipuri zitakuwa sahihi kwenye kasha lake lakini kipuri chenyewe sio halisi, kitaweza kutambuliwa kwa kutumia programu ya ‘barcode scanner’.

  Dkt. Mussa Mgwatu ameziagiza karakana zote za TEMESA nchini kuanza kutumia programu ya kompyuta katika kuagizia vipuri toka kwa wazabuni ili kuondokana na lawama zinaotokea wakati wa kutengeneza na kukarabati magari ya Serikali na mitambo mbalimbali.

  Soko la vipuri vya magari, kama yalivyo masoko ya vifaa vingine, limeingiliwa kwa kasi na uwepo wa vipuri bandia (Non genuine parts) katika kukabiliana na tatizo hili TEMESA imeamua kuanzisha mfumo wa kubaini vipuri bandia.
   Meneja wa TEMESA Iringa Mhandisi Ian Makule (Kulia) akimuonesha Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto) stoo ya vifaa kwa ajili ya ukarabati mdogo wa magari.Picha zote na Theresia Mwami TEMESA Iringa. 
   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (kulia) akisikiliza taarifa ya kituo cha TEMESA Iringa kutoka kwa Meneja wa kituo hicho Mhandisi Ian Makule. 

  0 0

  NA VICTOR MASANGU

  MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo Mohamed Mwanga amesema kuwa atahakikisha anazisimamia  na kuzivalia njunga ipasavyo fedha  amabzo zinazotolewa na halmashauri kwa ajili ya kuweza kuwasadia vijana na wakinamama lengo ikiwa ni kuona zinatumika katika vikundi mbali lli  kuweza kukuza uchumi na kuleta chachu ya kimaendeleo.
  Mwanga ameyasema hayo jana wakati alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha redio cha Jijini Dar es Salaam kuhusina na changamoto  mbali mbali zilizopo katika utendaji wa kazi pamoja na mikakati kabambe  aliyoiweka katika kuwahudumia wananchi wake wa Bagamoyo.
  Alisema kwamba halmashauri zinanapaswa kutenga kiasi cha asilimia kumi cha makusanyo ya mapato yake ambapo vijana wanatakiwa kupatiwa asilimia tano na kwa upande wa wakinaamama wanatakiwa wapatiwe asilimia tano kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao za ujasiriamali.

  “Mimi kama mkuuwa Wilaya ya Bagamoyo mikakati yangi ni kuhakikisha kwamba fedha hizo ambazo ni asilimia kumi zinawafikia walengwa wote bila ya kuwa na ubaguzi, hivyuo nitazisimamia na kuona ni jinsi gani zinaweza kuleta mabadiliko chanya kwa vijana pamoja na wakinamama ambao watapatiwa fedha hizo,”alisema Mwanga.

  Aidha mkuu huyo alisema kwamba ana imani kwamba eendapo halmashauri ikilitilia mkazo suala hilo la kuhakikisha kiais hicho cha asilimia kumi kinatolewa katika kila bajeti kutaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa kuviwezesha vikundi vya aina mbali mbali ili viweze kuendesha biashara zao na kukuza mitaji waliyonayo.
  Pia alifafanua kuwa fedha hizo zinatolewa kwa uataratibu maalumu ambapo inatakiwa vijana au wakinamama kuunda vikundi vyao na kuvisajili ili pindi fedha hizo zinapotolewa ziweze kuwafikia walengwa kwa wakati na kuweza kuwanufaisha kwa kiais  kikubwa katika kuendeleza biashara zao ambazo wanakuwa wanazifanya ziweze kukua zaidi.
   “Katika Wilaya yangu ya Bagamoyo kwa sasa nina halmashauri mbili, ambapo kuna halshauri ya bagamoyo, pamoja na halmashauri ya mji mdogo chalinze, kwa hivyo zote hizi zinatakiwa kutenga asilimi hiyo kumi kwa ajili ya kuviwezesha vikundi hivyo nbila ya kuwa na upendeleo wa aiana yoyote,”aliongeza Mwanga.
  Alisema kwamba kwa sasa kuna fedha ambazo tayari zimeshatolewa na halmashauri  kwa ajii ya kuvisaidia vikundi hivyo vya wakinamama na vijana, ambapo katika halmashauri ya bagamoyo kumeshatolewa kiasi cha shilingi milioni 120 na kuongeza kuwa fedha hizo zitakuwa zinatolewa kwa mzunguko ii ziweze kuwafikia walengwe wote.

  Katika hatua nyingine Mwanga alitoa wito kwa vijana na wakinamama ambao watapata fursa ya kupatiwa fedha hizo kuhakikisha kuwa  wanazitumia vizuri katika kuendeshea biashara zao ili kuweza kukuza mitaji yao na kuondokana na kuwa tegemezi.

  0 0

  Rais wa Korea Kusini, Park Geun-hye amemtunuku nishani ya heshima aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Bw.Henry Clemens kwa kutambua juhudi zake katika kuleta maendeleo katika vijiji vya Mfuru Mwambao na Njianne kupitia mfumo Saemaul Undong (SMU) yaani kijiji kipya cha maendeleo.

  SMU ni mfumo uliotumika Korea katika kujiletea maendeleo mpaka sasa kufika katika orodha ya nchi tajiri duniani. Mfumo huo unasisitiza swala la wananchi wenyewe kufanya kazi kwa kujitolea kwa ajili ya maendenelo yao wenyewe.Bw. Clemens ambaye ni mwenyekiti wa SMU Tanzania alisema wazo hilo alilipokea mwaka 2009 akiwa Mkuu wa wilaya ya Mkuranga na kulifanyia kazi katika vijiji viwili na kuleta matokeo mazuri.

  “kumekuwa na maendeleo makubwa mara baada ya kutoa mafunzo kwa wanakijiji juu ya thamani ya ardhi na umuhimu wa kufanya kazi kwa ushirikiano,” alisema Bw. Clemens.Alisema uzalishaji wa mazao kama mhogo, papai na nazi umeongezeka kwa asilimia kubwa kutokana na ushirikiano wa wanavijiji wa Mfuru Mwambao na Njia nne.
  Mwenyekiti wa Saemaul Undong Tanzania(SMU), Bw.Henry Clemens akikambidhi zawadi kwa niaba ya wanakijiji wa Njianne, wilayani Mkuranga Balozi wa Korea Kusini Nchini Bw.Song Geum-young alipotembelea katika kijiji hicho kujionea maendeleo waliofikia kwa kupitia dhana ya Saemaul Undong yaani kijiji kipya cha maendeleo ambayo ndio dhana iliyowafanya wao kupiga hatua kiuchumi mpaka kufikia katika prodha ya nchi tajiri Duniani. Katikati ni mwasisi wa SMU Mchungaji Joshua Lee
  Mwenyekiti wa Saemaul Undong Tanzania,(Mkuu wa Wilaya Mstaafu wa Mkuranga) Bw.Henry Clemens akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) medani ya heshima na cheti alichokabidhiwa na Rais wa Korea kusini Park Geun-hye kwa kutambua mchango wake wa kuviendeleza vijiji vya Mfuru mwambao na Njia nne vilivyopo Wilaya ya Mkuranga kupitia mfumo wa saemaul undong( kijiji kipya cha maendeleo).
  Balozi wa Korea Kusini Nchini Tanzania Bw.Song Geum-young akipiga picha daraja linalounganisha kijiji cha Njia nne na Nyamihimbo wakati waziara yake katika kijiji hicho na kujionea maendeleo waliofikia kwa kupitia dhana ya Saemaul Undong yaani kijiji kipya cha maendeleo ambayo ndio dhana iliyowafanya wao kupiga hatua kiuchumi mpaka kufikia katika prodha ya nchi tajiri Duniani. Kulia ni Mbunge mstaafu wa Mbinga Magharibi Bw.Gaudence Kayombo. Kushoto ni mwasisi wa SMU Tanzania,Mchungaji Joshua Lee. Wapili kushoto Mwenyekiti wa Saemaul Undong Tanzania Bw.Henry Clemens

  0 0

  Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Geita 

  Shirika la Misaada na Maendeleo ya Jamii (CODERT) limejipanga kuwasaidia jumla ya wananchi 7000 wanaoishi katika mazingira magumu Mkoani Geita ili waweze kujikwamua kutoka katika lindi la umasikini linalowakabili. 

  Shirika hilo ni moja ya mashirika yanayoshirikiana na Shirika la Plan International katika kutekeleza Mradi wa Uondoaji Ajira Hatarishi na Vitendo vya Ukatili kwa Watoto unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) na kuratibiwa na shirika la plan International kwa kuwapatia wananchi hao vifaa pamoja na elimu ya ujasiriamali.

  Hayo yamesemwa leo Mkoani Geita na Msimamizi wa Miradi wa shirika hilo, Edward Saramba alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu njia wanazozitumia kuwainua wazazi na vijana wa mkoa huo ili waache kuwapeleka watoto walio na umri chini ya miaka 18 kufanya kazi katika maeneo ya migodi.

  Saramba amesema kuwa mradi huo unaoratibiwa na shirika la Plan International umewasaidia wananchi wa mkoani Geita kuinua maisha yao kwa kuwasaidia kuunda vikundi vya kuweka na kukopa pamoja na kuwapatia vifaa mbalimbali vinavyowawezesha kujipatia vipato ambavyo vinawasaidia kuendesha maisha yao ya kila siku. 
  Mmoja wa wananchi waliosaidiwa kupata mradi wa kuku kupitia Mradi wa Uondoaji wa Ajira Hatarishi na Vitendo vya Ukatili kwa Watoto unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), unaratibiwa na Shirika la Plan International na kutekelezwa katika Wilaya 3 za Mkoa wa Geita, Shabani Masanja akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mradi huo ulivyomsaidia. 
  Msimamizi wa Miradi wa Shirika la Misaada na Maendeleo ya Jamii (CODERT), Edward Saramba alipokuwa akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu njia wanazozitumia kuwainua wazazi na vijana wa Mkoa wa Geita ili waache kuwapeleka watoto walio na umri chini ya miaka 18 kufanya kazi katika maeneo ya migodi.


  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii

  Waziri wa elimu, sayansi Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema wananchi wa Mkuranga wamejitoa katika kupata Mandeleo.

    Profesa Ndalichako wakati kufunga kambi ya kufyatua tofali 45000 kwa ajili ujenzi wa mabweni matano na nyumba tano za walimu katika shule ya sekondari Nassibugani iliyopo kata ya msonga wilaya Mkuranga.

  Amesema kuwa wananchi wamejitoa kuhakikisha watoto wanapata elimu bora inayoendana na mazingira. Amesema kuwa nia yake nikuona mkuranga kunapatikana mapinduzi ya Elimu.

  Amesema vijana 53 wameamua kumuunga mkono kutokana na kuona njia inaonekana ya kujitoa na kwao katika kusaidia maendeleo ya Taifa.

  Amesema ujenzi wa mabweni hayo itakuwa suluhu kwa wasichana  kufanya vizuri.Amesena jitihada zinaendelea kutatua baadhi ya changamoto za Elimu kwa kushirikiana na wananchi.Katika ufungaji wa kambi hiyo Mbunge wa Mkuranga ,Abdallah Ulega amesema nia yake ni kuona maendeleo yanapatikana yenye tija.

  Waliohudhuria ufungaji ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, Mkuu wa Wilaya, Filberto Sanga na viongozi mbalimbali.
   


  Waziri wa Elimu, sayansi Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako  sambamba na viongozi wengie wa wilaya ya Mkuranfa wakishiriki kufyatulia tofali,wakati wa hafla fupi ya kufunga kambi ya kufyatua tofali 45000 kwa ajili ujenzi wa mabweni matano na nyumba tano za walimu katika shule ya sekondari Nassibugani iliyopo kata ya msonga wilaya Mkuranga. 

   Pichani kushoto ni Waziri wa Elimu, sayansi Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako  pamoja na Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega wakishriki kwa pamoja kuchanganya mchanga wa kufyatulia tofali,wakati wa hafla fupi ya kufunga kambi ya kufyatua tofali 45000 kwa ajili ujenzi wa mabweni matano na nyumba tano za walimu katika shule ya sekondari Nassibugani iliyopo kata ya msonga wilaya Mkuranga. 

   Waziri wa elimu, sayansi Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wananchi wa Mkuranga wakati wa kufunga kambi ya kufyatua tofali 45000 kwa ajili ujenzi wa mabweni matano na nyumba tano za walimu katika shule ya sekondari Nassibugani iliyopo kata ya msonga wilaya Mkuranga.

  Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega 
  akizungumza na wananchi wake wakati wa kufunga kambi ya kufyatua tofali 45000 kwa ajili ujenzi wa mabweni matano na nyumba tano za walimu katika shule ya sekondari Nassibugani iliyopo kata ya msonga wilaya Mkuranga.

older | 1 | .... | 1410 | 1411 | (Page 1412) | 1413 | 1414 | .... | 3270 | newer