Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

Wananchi wa Ruangwa waweka mikakati ya kuinua Elimu

0
0
Na Abdulaziz Video,Ruangwa

Jumla ya wanafunzi 212 Kati ya 449 wanaosoma kati ya darasa la tatu hadi la saba katika Shule za Msingi za Nandagala na Mkata Wilayani Ruangwa, Mkoani Lindi hawajui kusoma wala kuandika huku wengine 15 ambao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu huku wakiwa hawajui kusoma wala kuandika.

Hayo yamebainika katika kikao cha wadau wa Elimu Wilayani Ruangwa kilichokaa chini ya Mwenyekiti wake,Mkuu wa Wilaya hiyo Agness Hokororo Kupokea taarifa za hali ya Elimu na kutafuta Ufumbuzi wa chaongamoto zinakwamisha Elimu Wilayani humo kilichofanyika jana.

Wakichangia katika kikao hicho Baadhi ya Wadau wakiwemo Madiwani wa Halmshauri hiyo walieleza kuwa Mwamko Mdogo wa Wazazi na Uwezo mdogo wa Walimu katika Ufundishaji ikichangiwa na Upungufu mkubwa wa walimu pamoja na Mila na Desturi ni baadhi ya changamoto zinazokwamisha ukuaji wa Elimu Wilayani Humo.

Andrew Chikongwe,Diwani Kata ya Nandagala alisema kuwa tatizo lipo kwa walimu kwani wengi wao hawajitumi katika ufundishaji licha ya kuwepo kazini muda wote hali inayoonyesha kuwa wana mgomo baridi. “Pamoja walimu kuwepo kazini lipo tatizo la kutojituma katika ufundishaji hii inachangia sana watoto wetu wafanye vibaya”alisema Chikongweali.

Naye Juma Nampupanga ambaye ni Mfanyabiasharaalisema kuwa kutotilia mkazo wa elimu miongoni mwa wananchi ni kikwazo kikubwa kwa mafanikio ya watoto wetu kwani wananchi wengi wa wilaya ya Ruangwa hawana mwamko wa elimu kwani si kipaumbele cha hivyo kutofuatilia maendeleo ya watoto.

Ibrahimu Ndoro Diwani wa Kata ya Ruangwa aliitaka serikali kuwachulia hatua baadhi ya walimu wanaopangwa kufanya kazi katika Wilaya za mikoa ya kusini ambao mara wakisharipoti huwa wanaondolka kwa kisingizio cha kufuata familia zao na badala yake hawarudi tena na kufanya wilaya hizo kuendelea kuwa na upungufu wa waalimu.

Akizungumza kwenye mkutano huo mkuu wa wilaya hiyo Agnes Hokororo aliwataka wananchi na viongozi kushirikiana katika kuondoa changamoto mbalimbali zinzosababisha maendeleo mabaya ya elimu wilayani humo.

“Iwapo viongozi tutashirikiana maendeleo ya elimu wilwywni kwetu yatakuwa mazuri kwani suala la maendeleo ya elimu ni la kila mmoja wetu”alisema Hokororo
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa,Agness Hokororo(MB) Akiendesha kikao cha wadau wa Elimu wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.
Baadhi ya Wadau wa Elimu wilayani Ruangwa Mkoani Lindi,wakifatilia kikao hicho.

Mkataa kwao mtumwa

0
0
Kutokana na maombi ya wadau kibao ya kutaka kuona ngoma za asili za Tanzania sambamba na ngoma azipendazo ankal, Globu yako ya Jamii inatii amri hiyo ya wadau na kuanzia leo kutakuwa na ngoma zetu za kiasili. Tunaanza na Wachagga...

Lori la mafuta la kampuni ya Lake Oil lapata ajali mlima nyoka jijini mbeya leo.

0
0
 Lori la kampuni ya Mafuta ya Lake Oil likiwa limepata ajali maeneo ya Mlima Nyoka-Mkoani Mbeya,Aidha katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha isipokuwa baadhi ya watu kadhaa walijeruhiwa.
 Baadhi ya Wakazi kutoka maeneo mbalimbali ya Mlima Nyoka ikiwemo jirani na mji maarufu wa kibiashara,Uyole jijini Mbeya wakiwa wamejumuika kwa pamoja wakigombea mafuta yaliyokuwa yakimwagika,mara baada ya Lori la Lake Oil kupata ajali.Picha kwa hisani ya Mbeya Yetu Blog.

Mazoezi ya uvutaji pumzi na mpiganaji Freddy Macha

0
0
FAIDA ZA MAZOEZI YA UVUTAJI PUMZI- Zoezi la Uso

abiria wa basi la tayassar wanusurika kifo kufuatia basi hilo kupata ajali leo.

0
0
 Basi la Tayassar likiwa limeacha njia jioni ya leo,lakini hakuna aliyepoteza maisha.
Pichani kama uonavyo ni basi la Tayassar ambalo abiria wake walinusurika kifo baada ya gari hilo kuacha njia kilometa chache kabla ya kufika njia panda Segera,kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa basi hilo lilipata pancha ghafla likiwa kwenye mteremko mkali,"lakini kudra za Mwenye Mungu dereva alijitahidi kwa uwezo wake na matokea yake basi hilo likaacha njia na kwenye kuvamia mtaro kama lionekavyo pichani,aidha katika mtafaruku huo hakuna aliyepoteza maisha zaidi wa tu wachache kupata mshtuko tu",alibainisha mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo.

JK ALIPOTEMBELEA BANDA LA NSSF KATIKA KILELE CHA WIKI YA MIFUKO YA JAMII DODOMA

0
0
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkrugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau wakati alipowasili kwenye maonesho ya Wiki ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii mjini Dodoma. 


Rais Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mkrugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk Ramadhan Dau alipotembelea banda la NSSF wakati wa kufunga maonesho ya Wiki ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii iliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma. Wa pili kushoto ni Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka. (Na Mpiga Picha Wetu)


 Rais Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifandji ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori wakati alipotembelea banda la NSSF katika maonesho ya Wiki ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii iliyofanyika mjini Dodoma
 Rais Jakaya kikwete akikaribishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shiorika la taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau alipowasili katika banda la NSSF. Kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifandji ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori.
 Mh. Rais Jakaya Kikwete akisoma jarida linaloonyesha kazi za NSSF.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau akifafanua jambo wakati wa mahojiano na waandishi wa habari.

DC NACHINGWEA AZINDUA KAMPENI YA KATA KWA KATA UTOAJI WA ELIMU YA AFYA YA JAMII CHF

0
0
Mkuu wilaya ya Nachingwea,Regina Chonjo akifungua Mpango wa Uhamasishaji kata kwa kata wilayani Humo kwa wanachama na Wanufaika wa mfuko wa bima ya taifa ya afya na Wa Afya ya Jamii CHF kushoto ni Kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya,Aborgast Kiwale NHIF/CHF Mkoa wa Lindi na Fortunata Kullaya,Msimamizi w Mwenyekiti wa halmashauri ya Nachingwea,Abdalah Chikawe.
Msimamizi wa mfuko wa Taifa wa Bima Ya Afya wa mkoa wa Lindi ya afya,Bi Fortunata Raymond Kullaya akikabidhi barua Kwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea barua ya kukubaliwa maombi ya hospital ya Wilaya kukubaliwa kukopa Vifaa Tiba KupitiaMfuko wa Bima ya Afya.
Baadhi ya Wanachama.

Na Abdulaziz Video,Nachingwea

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea,Regina Chonjo ameitaka halmashauri ya wilaya hiyo kuhamasisha vituo vya kutolea tiba Pamoja na Hospital ya Wilaya kuomba mikopo ya vifaa tiba kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya ili kuboresha Utoaji wa Huduma za Tiba ikienda sambamba na Upatikananji wa Dawa.

Akifungua Mpango wa elimu kwa wanachama wa mfuko wa bima ya taifa ya afya na mfuko wa afya ya jamii,Mkuu wa wilaya hiyo alisisitiza kuwkutu kupitia maboresho ya mfuko katika Kuhudumia wanachama wake kunaendana na fursa za Upatikanaji wa huduma hivyo vituo vingi vinaweza kuboreka kihuduma ikiwa vifaa tiba vinakuwepo.

“Ningependa wilaya hii iwe kioo cha mafanikio ya utekelezaji wa sera ya mikopo ya vifaa tiba inayotolewa na mfuko huu na mkitumia fursa hizo tunaweza kuboresha huduma za matibabu kwa wanachama na jamii kwa Ujumla na Mkizingatia kuwa Mikopo ya NHIF inalipika kutokana na Huduma za wateja wao si vinginevyo;alimalizia uzinduzi huo na kuwapa fursa ya kutoa elimu hiyo kwa Kata zote 32 za wilaya hiyo.

Awali Bi Regina Chonjo Akizungumzia mpango huo wa elimu kwa wananchama na wadau wa mfuko huo,Aliitaka NHIF kwa kushirkiana na waajiri kuendelea na zoezi la kuwafikia wanachama hasa wale wanaoishi vijijini kwani unatoa fursa kwa wadau hao kutoa kero na kupokea maelekezo yenye ufafanuzi juu ya haki,wajibu za wanachama na maboresho ya kitita cha mafao.

‘Utaratibu wa kukutana na wanachama katika maeneo yao ya kazi ni utaratibu unaonyesha nia njema ya kuendeleza uwazi ,ushirikishwaji na uwajibikaji katika sekta ya afya na maendeleo ya mfuko Hivyo nashawishi asasi zote za umma kuwa na mfumo unaofanana na huu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kujali wateja wake”alisema Chonjo.

Kwa Upande wake Msimamizi wa Mfuko Huo Bi Fortunata Kullaya alieleza kuwa mpango huo ni moja ya mikakati ya mfuko huo kupata maoni ya wateja wao ikiwa pamoja na kutafuta namna ya kuboresha huduma ili kila mmoja apate Afya njema ambapo tayari mafunzo elekezi ya kata kwa kata katika mkoa wa Lindi yamefanyika katika wilaya za Liwale na Ruangwa

taarifa kwa umma


KIJIWE CHA UGHAIBUNI

TAARIFA YA CCM KWA VYOMBO VYA HABARI

0
0

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Moses Nnauye

Mei 19, 2013 Chama Cha Mapinduzi kilifanya kikao cha siku moja na wabunge wanaotokana na CCM, kikao hicho kilifanyika mjini Dodoma ambapo pamoja na viongozi wengine wa juu wa CCM kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Kikao hicho kilikuwa na lengo la wabunge wa CCM na viongozi wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM ambaye pia ni Rais na mtekelezaji mkuu wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kubadilishana uzoefu wa namna ilani ilivyotekelezwa hasa kwenye majimbo kwa kipindi cha nusu ya muhula wa miaka mitano. Baada ya kubadilishana mawazo uliwekwa mwelekeo wa namna bora ya kutekeleza ilani na ahadi mbalimbali kwa kipindi kilichobaki.

jamaa kapita Wrong way Mbele ya Mgambo

0
0
Mgambo wa Jiji la Dar wakiwa wameisimamisha Gari aina ya Canter iliyokuwa ikipita Mtaa wa Samora upande usioruhusiwa kupita magari.

Deputy Permanent Secretary hold talks with UK' Royal College of Defence Studies

0
0
Ambassador Rajab Gamaha, Deputy Minister of Foreign Affairs and International Co-operation holding talks earlier today with Mr. Jeremy Jarvis, Senior Directing Staff of the Royal College of Defence Studies based in the UK together with the delegation of about twenty people in the Ministry in Dar es Salaam. Ambassador Rajabu Gamaha explains Tanzania's current state and its regional integration with neighboring countries during their meeting today in the Ministry, in Dar es Salaam. Mr. Jeremy Jarvis, Senior Directing Staff of the Royal College of Defence Studies express his appreciation of the Tanzania Government's hospitality during their Study Tour Visit which encompasses Defence Studies students of post graduate programme in international strategic studies, which focuses on the themes of security, stability and prosperity. Other in the photo are Ambassador Dora Msechu (2nd right), Director of the Department of Europe and Americas in the Ministry. Defence Studies stu.
Ambassador Rajabu Gamaha explains Tanzania's current state and its regional integration with neighboring countries during their meeting today in the Ministry, in Dar es Salaam.
Mr. Jeremy Jarvis, Senior Directing Staff of the Royal College of Defence Studies express his appreciation of the Tanzania Government's hospitality during their Study Tour Visit which encompasses Defence Studies students of post graduate programme in international strategic studies, which focuses on the themes of security, stability and prosperity.  Other in the photo are Ambassador Dora Msechu (2nd right), Director of the Department of Europe and Americas in the Ministry.  
Defence Studies students that included Mr. Stephen Shelley (left), Directing Staff of the Royal and Colonel Jonathan Calder-Smith(2nd left) of the British Army, Captain Masashi Kondo (3rd right), Japan Maritime Self-Defence Force and Mr. Teemu Pentilla (2nd right), from the Ministry of Defence, Finland. 
Ambassador Rajabu Gamaha expresses Tanzania's historical prosperity in security and stability in the region and within the country.  
Delegation from the UK' Royal College of Defence Studies during their meeting today with the Deputy Permanent Secretary in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation in Dar es Salaam.  Also in the photo are British High Commissioner Dianna Melrose (2nd right) in the United Republic of Tanzania and Mr. Jeremy Jarvis (right), Senior Directing Staff of the UK' Royal College of Defence Studies.  
Members of the Tanzania Defence Force also were in attendance during the meeting.All photos by Tagie Daisy Mwakawago of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation 

JK AONGOZA KIKAO CHA CCM DODOMA LEO

0
0
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wajumbe, wakati wa Kikao Cha Kamati Kuu (CC) ya CCM, kilichofanyika leo May 21, 2013, kwenye ukumbi wa Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kufungua kikao cha Kamati Kuu (CC) ya CCM, leo Mei 21, 2013, kwenye ukumbi wa Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk. Ali Mohamed Shein na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, wakiwa mkutano wa Kamati hiyo, leo Mei 21, 2013, kwenye ukumbi wa Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.Picha na Bashir Nkoromo.

WANANCHI WAJIHADHARI NA UNUNUZI WA MAJI FEKI JIJINI DAR

0
0
Wananchi wakifuatilia mzozo baina ya mfanyabiashara wa maji na mteja wake baada ya kubainika kwamba amemuuzia maji bandia.Mfanyabiashara huyo ametambulika kwa jina la Kagira Mhisho mwenye umri wa miaka 15 inaseemekana kuwa amekuwa akifanya biashara hiyo kwa kutumia maji kutoka sokoni kariakoo kwa takribani miaka mitatu sasa.Ninvyema wananchi wakajihadhari na maji yanayouzwa njiani kwani baadhi ya wafanyabiashara wasiowaaminifu huokota chupa zilizokwisha tumika na kuzitumia.Ninashauri vyombo husika katika ukaguzi na kujali afya za walaji kuingilia kati ili kuepusha wananchi kupata maradhi mbalimbali.
Mfanyabiashara wa maji aliyetambulika kwa jina la Kigira Mhisho(15) akimwaga maji baada ya kubainika kuwa anauza maji bandia.(PICHA NA Frank Shija - MAELEZO)

Serikali kuanzisha sera na Sheria ya usalama wa bidhaa nchini

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Bi. Joyce Mapunjo, akifungua warsha ya kujadili mpango wa ukaguzi wa bidhaa kabla ya kuingizwa nchini (PVoC) uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Bureau Veritas, Bw. Jean-Michel Marnoto (katikati), akifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Warsha ya kujadili mpango wa ukaguzi wa bidhaa kabla ya kuingizwa nchini (PVoC) uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mratibu wa Bureau Veritas, Bw. Michael Maryogo na wa tatu ni Meneja wa Bureau Veritas Tanzania, Bw. Cedric Serre.
Baadhi ya wadau wakifanya usajili kabla ya kuingia kwenye warsha ya kujadili mpango wa ukaguzi wa bidhaa kabla ya kuingizwa nchini (PVoC) uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulifunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Bi. Joyce Mapunjo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Bi. Joyce Mapunjo, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua warsha ya siku moja iliyojadili mpango wa usalama na ubora wa bidhaa nchini (PVoC) pamoja nae ni Meneja wa Bureau Veritas Tanzania, Bw. Cedric Serre.
Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa umakini hotuba ya ufunguzi wa Warsha ya kujadili Mpango wa Ukaguzi wa Bidhaa kabla ya kuingizwa nchini (PVoC) uliofanyika kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.

MAMA SALMA AKUTANA NA DR JEROME PAULSON KUTOKA MAREKANI NA VIONGOZI WA CHAMA CHA MADAKTARI WA WATOTO NCHINI

0
0
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkaribisha kwa mazungumzo Daktari bingwa wa watoto Jerome Paulson, Mkurugenzi wa Afya ya watoto na Mazingira kutoka Chidren's National Medical Center ya huko Washington nchini Marekani aliyemtembelea Mama Salma kwenye ofisi ya WAMA jijini Dar es Salaam tarehe 21.5.2013. Dr. Jerome amekuja Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa Madaktari Bingwa wa watoto hapa nchini kuhusu afya ya mtoto na mazingira kufuatia makubaliano aliyoyafanya na Mama Salma wakati alipotembelea taasisi hiyo huko Washington mwaka 2012.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Daktari Bingwa wa watoto Jerome Paulson aliyeambatana na Mkewe pamoja na viongozi wa Chama cha Madaktari wa watoto hapa Tanzania (Paediatrc Association of Tanzania-PAT). Kutoka kushoto ni Dr. Augustino Masawe akifuatiwa na Rais wa Chama cha Madaktari wa watoto nchini (PAT) Dr. Rodrick Kisenge, Mrs Jerome na kwa nyuma ni Dr. Francis Furia,Mjumbe na Dr. Hadija Mwamtemi, Mwekahazina wa chama hicho.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Daktari Bingwa wa Watoto Jerome Paulson kutoka Marekani na Viongozi wa Chama cha Madaktari wa Watoto hapa Tanzania kwenye ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, tarehe 21.5.2013. PICHA NA JOHN LUKUWI

TAARIFA KUTOKA TFF LEO

0
0

14 RCL KUUMANA RAUNDI YA PILI WIKIENDI
Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kuwania nafasi tatu za kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao inaingia raundi ya pili wikiendi hii kwa kukutanisha timu 14 zilizofanikiwa kusonga mbele.

Timu zitakazocheza raundi hiyo kwa mtindo wa nyumbani na ugenini ni Abajalo ya Dar es Salaam itakayokuwa mwenyeji Kariakoo ya Lindi katika mechi itakayochezwa Jumamosi (Mei 25 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

Siku hiyo hiyo Uwanja wa Azam ulioko Chamazi utatumika kwa mechi kati ya Friends Rangers ya Dar es Salaam na African Sports ya Tanga wakati Jumapili (Mei 26 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Machava FC ya Kilimanjaro na Mpwapwa Stars ya Dodoma itakayochezwa Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

Stand United ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Magic Pressure ya Singida katika mechi itakayochezwa Jumapili (Mei 26 mwaka huu) Uwanja wa Namfua mjini Singida wakati Polisi Jamii ya Mara na Biharamulo FC ya Kagera zitaumana siku hiyo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.

Mjini Kigoma kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Saigon FC na Katavi Warriors ya Katavi. Nayo Kimondo SC ya Mbeya itakuwa mgeni wa Njombe Mji ya Njombe katika mechi itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Sabasaba.

Mechi za marudiano zitachezwa kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu wakati timu zitakazofuzu kucheza raundi ya tatu zitacheza mechi za kwanza kati ya Juni 8 na 9 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitakuwa kati ya Juni 15 na 16 mwaka huu.

LIUNDA KUTATHMINI WAAMUZI MECHI YA FIFA
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limemteua Leslie Liunda wa Tanzania kuwa mtathmini wa waamuzi (referee assessor) katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia.

Mechi hiyo ya Kundi B, Kanda ya Afrika kati ya Cape Verde na Equatorial Guinea itafanyika Juni 8 mwaka huu saa 10.30 jioni kwenye Uwanja wa Verzea mjini Praia.

Waamuzi wa mechi hiyo ambao watatoka Angola ni Martins De Carvalho Helder, Dos Santos Jerson Emiliano, Da Silva Lemos Julio na Muachihuissa Caxala Antonio. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Diarra Massa Momoye wa Mauritania.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

FLAVIANA MATATA ASHIRIKI MISA YA WALIOKUFA KATIKA AJALI YA MELI YA MV BUKOBA

0
0
 Flaviana Matata akiwa na Baba yake mzazi (suti nyeusi) katika Misa ya  maombelezo  Ajali ya MV Bukoba ambapo Flaviana alimpoteza Mama yake mzazi, Igoma,Mwanza leo

 Flaviana Matata akiwasha mshumaa ikiwa ni ishara ya kuomboleza katika Makaburi ya Igoma Mwanza walikozikwa baadhi wananchi walopoteza maisha yao miaka 17 iliyopita.
 Flaviana Matata akiwa ofisini kwa Bw. Projest Samson Kaija ambaye ni General Manager wa Marine Services Company ltd ambao hushirikiana nae kila mwaka katika maombolezo ya Ajali hii ambapo mwaka jana aliwapa msaada wa maboya ya kujiokoa
Flaviana Matata akiwa na marafiki na baadhi ya waombolezaji waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo. Picha na Shamim Mwasha

MAKAMANDA wa polisi wa Mikoa ya Kikanda, wamekutana Jijini Mbeya, kujadili hali ya uhalifu na kuweka mikakati

0
0
NA MBEYA YETU
MAKAMANDA wa polisi wa Mikoa ya Kikanda, wamekutana leo Jijini Mbeya, kujadili hali ya uhalifu ikiwa na kuweka mikakati itakayosaidia kuwabana askari watakaobainika kukiuka sheria na taratibu za kazi. Mkutano huo unafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, lengo kuu likiwa ni kujadili hali ya usalama na uhalifu wa maeneo katika Mikoa ya Morogoro, Iringa, Ruvuma, Njombe na Mbeya . 
Akizungumzia mikakati hiyo, Mwenyekiti wa Mkutano Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ndugu Faustine Shilogile alisema katika kikao hicho agenda kuu itakuwa ni kujadili matukio ya uhalifu wa unyang’anyi wa kutumia silaha, matukio ya ajali pamoja na kujadili nidhamu kwa watendaji wa jeshi hilo. 

Amesema Wahalifu wamekuwa na tabia ya kuhama hama mara wanapofanya tukio, hawakai sehemu moja hivyo mkutano huu utasaidia kwa wajumbe kubadilishana na kupeana uzoefu wa kazi,’alisema Aidha, amefafanua kuwa jeshi la polisi hivi sasa kupitia baadhi ya askari limekuwa likikumbwa na matukio ya ukiukwaji wa maadili kwa kukutwa na tuhuma mbalimbali za uhalifu. 
Kwa upande wake, Kamanda wa polisi wa mkoa wa mbeya, Ndugu Diwani Athumani ambaye ni mwenyeji wa Mkutano huo , alisema kikao hicho kinatarajia kutoka na mikakati itakayosaidi kupunguza wimbi la uhalifu pamoja na ajali barabarani. 
Amesema mara nyingi Wahalifu wamekuwa wakitumia njia nyingi kufanya uhalifu na kukimbilia mikoa ya jirani hivyo mkutano huu ambao unahudhuriwa na Makamanda pamoja na wakuu wa upelezi utasaidia kuwabaini ikiwa na kusambaratisha mtandao uliopo Mkutano huo ni watatu baada ya mkutano wa kwanza kufanyika Mkoani Iringa na wa pili ulifanyika Mkoani Morogoro na kwamba wajumbe wanatarajia kutoka na maadhimio mapya.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa mbeya, Ndugu Diwani Athumani ambaye ni mwenyeji wa Mkutano huo , amesema kikao hicho kinatarajia kutoka na mikakati itakayosaidi kupunguza wimbi la uhalifu pamoja na ajali barabarani.
Mwenyekiti wa Mkutano  Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ndugu Faustine Shilogile amesema katika kikao hicho agenda kuu itakuwa ni kujadili matukio ya uhalifu wa unyang’anyi wa kutumia silaha, matukio ya ajali pamoja na kujadili nidhamu kwa watendaji wa jeshi hilo.
Baadhi ya maafisa wa jeshi hila la Polisi wakiwa makini kusikiliza mwenyekiti wao katika kikao hicho
Baadhi ya makamanda wa polisi wakiwa maetulia kwa umakini kumsikiliza mwenyekiti wa kikao hicho
Picha ya pamoja

IGP MWEMA AWANOA MAKAMANDA

0
0

 Na Frank Geofray, Jeshi la Polisi
 Maofisa na askari Polisi kote nchini  wametakiwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuwa suala hilo siyo la hiari bali ni la lazima kulingana na kanuni pamoja na taratibu za ufanyaji wa kazi za Polisi.
 
 Hayo yalisemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema, wakati wa kikao cha kikazi kilicho wakutanisha maofisa wa Polisi Makao makuu, Kanda maalumu ya Dar es Salaam na Vikosi vya Jeshi hilo chenye lengo la kuwajengea uwezo na kupeana mafunzo yatakayosaidia kufanya kazi kwa weledi zaidi ili kuweza kukabiliana na vitendo vya uhalifu wa aina mpya unaojitokeza hapa nchini katika sura mbalimbali.
 
Aidha, IGP Mwema alisema, kila ofisa na askari polisi anapaswa kutekeleza kwa vitendo utoaji wa huduma bora ndani na nje, ikiwa na maana kwa askari wenyewe na kwa wananchi, ili kuendana na maboresho yanayoendelea ndani ya Jeshi hilo na kuweza kukabiliana na vitendo vya vurugu na matishio mengine ya kihalifu na wahalifu yanayojitokeza hapa nchini.
 
Aliwatataka Makamanda na maofisa wa polisi wote kuendelea kuwa karibu na wananchi ili kujua kero za kiusalama zinazowakabili na kwa pamoja kuweza kuzitafutia ufumbuzi ili kuondoa hofu ya uhalifu kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa jambo ambalo litaendelea kuimarisha hali ya usalama hapa nchini.
 
Aidha Mwema, amesema Jeshi la Polisi halitasita kuwachukulia hatua kali baadhi ya watu wanaotumia mwamvuli wa siasa au dini kama kisingizio cha  kufanya ama kuchochea vurugu hapa nchini kwa kuwa vurugu hizo ni kosa la jinai kama yalivyo makosa mengine ya jinai.
 
“Hakikisheni mnawakamata wale wote wanaofanya vitendo vya vurugu kwa visingizio vya siasa kwa kuwa siasa zao zinaishia pale tu wanapokuwa wamefanya vitendo vya vurugu ambavyo ni kosa la jinai na sisi hatuwezi kuwafumbia macho” Alisema Mwema.
 
IGP Mwema alisema Jeshi la Polisi litaendelea kufanya kazi zake kwa kufuata kanuni, maadili na taratibu zinazoliongoza katika kuhakikisha amani na usalama vinadumu hapa nchini na kusisitiza kuwa askari wa Jeshi la polisi si wanachama wa chama chochote cha siasa japokuwa wanaruhusiwa kupiga kura.

Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images