Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

MUSWADA WA HABARI UTATOA FURSA KWA CHOMBO CHA HABARI KUOMBA RADHI PASIPO KUCHUKULIWA HATUA NA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA

$
0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO,Dar es Salaam.

SERIKALI imesema muswada wa sheria ya huduma ya habari utatoa fursa kwa vyombo vya habari kuiomba radhi jamii radhi kwa jamii pindi wanapoandika habari zenye upotoshaji na hawatochukuliwa hatua za kisheria kutoka katika mamlaka zinazohusika.

Akizungumza katika mwendelezo wa ziara yake katika vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas alisema hakuna haja ya waandishi wa habari kuuhofia muswada huo kipengele na badala yake wausome na kuelewa na kisha watoe maoni yao ili kuuboresha zaidi.

“Sifa moja ya taaluma ya habari ni kufuata maadili hivyo muswada umetoa fursa kwa mwanahabari kukanusha na kueleza ulichokosea hivyo mwandishi hatashtakiwa endepo akiona amekosea na kusahihisha ikiwemo kuomba radhi” alifafanua Mkurugenzi Abbas.

Kwa mujibu wa Abbas alisema kutakuwa na bodi maalumu itakayosimamia masuala ya maadili kwa waandishi wa habari nchini na hivyo kutoa fursa kwa waandishi hao kuhojiwa na kutoa ufafanuzi wa jambo husika.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akifanya mahojiano ya kipindi maalum cha heloo Tanzania kinachorushwa hewani na kituo cha redio Uhuru FM cha Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini humo. Kushoto ni mtangazaji wa kipindi hicho, Sheila Simba.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akibadlishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Redio Uhuru FM cha Jijini Dar es Salaam, Angel Akilimali ikiwa ni sehemu ya mwendelezo ya ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas (katikati) akizungumza na wahariri na waandishi wa gazeti la Uhuru wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo, Ramdhani Mkoma na kulia ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara Habari( MAELEZO), Jonas Kamaleki.


WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WANNE KUTOKA NCHI MBALIMBALI, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi wa Japan nchini, Ian Myles (wapili kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japan. Wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa Wizara hiyo, Haji Janabi, na kulia ni Msaidizi wa Balozi huyo, Pascale Julien. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi wa Norway hapa nchini, Hanne-Marie Kaarstad (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Nchemba ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Norway. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimsikiliza Balozi wa India hapa nchini, Sandeep Arya (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri huyo ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na India. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa India nchini, Sandeep Arya (kulia) mara baada ya Balozi huyo kumaliza mazungumzo na Waziri ambayo yalifanyika ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. Mazungumzo hayo yalikuwa na lengo la kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na India. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimsindikiza Balozi wa Rwanda, Eugene Kayihura (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo yao, yaliyofanyika ofisini kwa Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo. Lengo la mazungumzo hayo ni kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi jirani ya Rwanda na Tanzania. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MTENDAJI MKUU TEMESA AWATAKA WAFANYAKAZI WA MV TANGA KUZINGATIA USALAMA WA ABIRIA.

$
0
0

Na Theresia Mwami TEMESA TANGA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amewataka wafanyakazi wa kivuko cha Mv Tanga kuzingatia usalama wa abiria kwa kufata kanuni na Sheria za usafirishaji wa abiria kupitia vivuko.

Amesema hayo alipotembelea na kuongea na watumishi wa kivuko cha MV. Tanga kinachosafiri kati ya Pangani na Bweni na kuwasisitiza watumishi hao juu ya suala la usalama wa abiria na kuwa waaminifu katika ukusanyaji wa mapato ya kivuko hicho.

Ndugu zangu hapa tunabeba roho za watanzania wenzetu tuwe makini sana na kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo ili kuhakikisha usalama wa hawa abiria tunaowahudumia” Alisisitiza Dkt Mgwatu.

Kwa upande wake Meneja Msaidizi TEMESA Tanga Mhandisi Mahangaiko Ngoroma amemuahakikishaia Mtendaji Mkuu kuwa watazingatia taratibu na Sheria zilizopo ili kuhakikaisha usalama wa abiria wanaowahudumi kupitia kivuko cha Mv Tanga na vivuko vingine vilivyopo mkoani Tanga.

Aidha kwa upande wao watumishi wa Mv Tanga wamemwaomba Mtendaji Mkuu kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali zilizopo zikiwepo uhaba wa vifaa kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yuko katika ziara ya kikazi kutembelea vituo vilivyopo kanda ya Kaskazini kuangalia utendaji kazi wake na kuona changamoto zilizopo ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kwa maendeleo ya Wakala huyo.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (katikati) akitoa maelekezo ya kiutendaji kwa Meneja Msaidizi TEMESA Tanga Mhandisi Mahangaiko Ngoroma (kushoto) alipotembelea kituo hicho, kulia ni Mhasibu wa TEMESA Tanga Bw. Lusenga David. 
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto aliyesimama) akizungumza na watumishi wa TEMESA Tanga wakati alipotembelea kituo hicho kuangalia hali ya utendaji kazi, kulia ni Meneja Msaidizi TEMESA Tanga Mhandisi Mahangaiko Ngoroma.
Picha zote na Theresia Mwami TEMESA Tanga 

Mboni Masimba aja na Sauti ya Mwanamke

$
0
0
Mtangazaji wa Kipindi cha "The Mboni Show" kinachoruka kupitia kituo cha televisheni TBC1, Mboni Masimba ameandaa kongamano la kuwahamasisha wanawake aliloliita  Sauti ya Mwanamke lenye lengo la kuwapa uwezo wa kujikomboa kiuchumi.

Katika  kongamano hilo litakalofanyika mkoani Mwanza Novemba 6, mwaka huu katika Hoteli ya Gold Crest,  wanawake mbalimbali waliofanikiwa kiujasiriamali, kibiashara na kielimu watakuwepo kuzungumza na wanawake  wa jiji hilo kwa kiingilio cha Sh40,000.

Masimba anasema kwa kiingilio hicho wanawake wa Mwanza
 watapata elimu, burudani pamoja na chakula.

"Atakuwepo Shekha Nasser ambaye ni mmiliki wa Shear Illusion na Mwanzilishi wa Manjano Foundation huyu amefanikiwa sana kwenye biashara, atakuwepo Mkandarasi Maida Waziri pamoja na Biubwa Ibrahim ambaye ana Kampuni ya  Namaingo Agri_Busness Agency inayowawezesha watu mbalimbali katika masuala ya kilimo," amefafanua Masimba.

Anaongeza kuwa pamoja na kupata elimu ya biashara na ujasiriamali, maarifa kuhusu maisha na nyumba yatatolewa na wawezeshaji maarufu Bi Chau na Bi Fatma.“Wanawake mnapokutana lazima mbadilishane ujuzi wa kila aina, hatutawaacha hivi hivi wanawake wa Mwanza, tumemuandaa Bi Chau na Bi Fatma kuwafunda yale mambo yetu,” anafafanua.

Shughuli yoyote ya wanawake bila burudani haiwezi kunoga ndiyo maana Masimba anawapeleka Mwanza, Isha Mashauzi na mchekeshaji Katarina Karatu kuifanya siku hiyo iwe nzuri.Masimba anasema sherehe itaendeshwa na mshereheshaji maarufu nchini Mc Zipompapompa.

“Tunaanzia Mwanza, lakini kongamano letu litakwenda nchini kote, tunataka kuwakomboa kifikra wanawake wa Kitanzania, Sauti ya Mwanamke ni  sauti ya jamii, ipewe nafasi,” anasema Masimba.

TRA YAFUNGUA OFISI MPYA KIMARA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Katika jitihada za kuboresha huduma kwa walipakodi na kuzifikisha huduma hizo kwa karibu zaidi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA) Bw. Alphayo Kidata amezindua ofisi mpya ya TRA katika eneo la Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam Tarehe 26 Oktoba 2016 itakayotoa huduma zote za kikodi ikiwemo usajili na uhakiki wa Namba za Utambulisho wa Mlipakodi –TIN, Usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani-VAT, Malipo ya Kodi za Magari, Kodi zote za Mapato zikiwemo Kodi za Makampuni, Watu Binafsi, Wafanyakazi (PAYE), Kuendeleza Ufundi Stadi – SDL, VAT, Ushuru wa Stampu na huduma nyingine za kikodi. 

Akizungumza na walipakodi waliofika katika ofisi hiyo kupata huduma wakati wa uzinduzi, Bw. Kidata aliwashukuru kwa mwitikio wao katika zoezi la uhakiki wa taarifa za TIN ambao utaisaidia Mamlaka kupata idadi sahihi ya walipakodi ili kuondoa walipakodi hewa ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za ulipaji kodi.

“Zoezi hili litaongeza ufanisi katika suala zima la usimamizi na ukusanyaji kodi kwa kiwango cha juu” Alisema Bw. Kidata

Kamishna Mkuu wa TRA aliwataka walipakodi hao wanaoishi maeneo ya karibu na ofisi hiyo mpya ya TRA iliyopo Kimara Mwisho kuendelea kujitokeza kwa wingi ili kupata huduma mbalimbali za kikodi ikiwemo uhakiki wa taarifa zao TIN kabla ya tarehe ya mwisho wa zoezi hilo kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambayo ni tarehe 30 Novemba 2016.

Aidha Kamishna wa Kodi za Ndani TRA Bw. Elijah Mwandumbya alisema TRA imejipanga kuhakikisha inaendelea kuboresha huduma zake na kuwafikia walipakodi kwa ukaribu zaidi ili kuondoa usumbufu na kuokoa muda wa upatikanaji wa huduma hizo.

“TRA kwa kuhakikisha walipakodi wanapata huduma iliyo bora imeanzisha vituo vingi vya kodi katika jiji la Dar es Salaam na nchi nzima ili walipakodi wapate huduma stahiki na ya haki na kuiwezesha Serikali kupata mapato yake kwa mendeleo ya Taifa letu” Alisema Bw. Mwandubya.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA) Bw. Alphayo Kidata – (Mwenye suti ya bluu katikati) pamoja na Kamishna wa Kodi za Ndani TRA Bw. Elijah Mwandumbya (Kushoto kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na walipakodi waliofika katika Ofisi Mpya ya TRA Kimara ili kuhakiki Namba zao za Utambulisho wa Mlipakodi –TIN. Ofisi hiyo imezinduliwa leo tarehe 26 Oktoba 2016 na Kamishna Mkuu wa TRA ili kuwafikia wananchi kwa karibu zaidi na kuboresha huduma mbalimbali za Kodi. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA) Bw. Alphayo Kidata akikata utepe kama ishara rasmi ya uzinduzi wa ofisi mpya ya TRA iliyoko Kimara Mwisho leo Tarehe 26 Oktoba 2016, Kushoto kwake ni Kamishna wa Kodi za Ndani TRA Bw. Elijah Mwandumbya pamoja na Wakurugenzi wengine wa TRA wakishuhudia tukio hilo 
Meneja wa TRA Kinondoni Bw. Wallace Mnkande (anayeongea kwa vitendo) akitoa maelezo ya kituo hicho kipya kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (aliyeketi) wakati wa uzinduzi wa ofisi hiyo. Wengine kutoka kulia ni Kamishna wa Kodi za Ndani TRA Bw. Elijah Mwandumbya, Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani Bw. Abdul Zuberi, Meneja wa Majengo Gerald Mwikuka, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Bw. Gerald Mwanilwa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Bw. Richard Kayombo. 
Meneja wa TRA Kinondoni Bw. Wallace Mnkande akimwonesha jambo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (kushoto kwake) alipotembelea ofisi ya TRA Kimara Mwisho wakati wa uzinduzi huo uliofanyika tarehe 26 Oktoba 2016 

Tamasha la Uhondo wa Zantel lazidi kupasua anga

$
0
0


Msanii maarufu wa muziki wa ‘singeli’ Rajabu Selemani ‘virusi mdudu’ (kushoto), akikonga nyoyo za wakazi wa kimara na maeneo ya jirani katika tamasha la Uhondo za Zantel katika viwanja vya Rhino, Kimara, Dar es Salaam juzi, ikiwa ni moja ya kampeni za kampuni ya simu za mkononi ya Zantel kuwa karibu na wateja wake ikiwajulisha bidhaa na huduma zao zilizopo sokoni.
Msanii maarufu wa muziki wa ‘singeli’ Rajabu Selemani ‘virusi mdudu’ (kushoto), akikonga nyoyo za wakazi wa kimara na maeneo ya jirani katika tamasha la Uhondo za Zantel katika viwanja vya Rhino, Kimara, Dar es Salaam juzi, ikiwa ni moja ya kampeni za kampuni ya simu za mkononi ya Zantel kuwa karibu na wateja wake ikiwajulisha bidhaa na huduma zao zilizopo sokoni.
Baadhi ya watu waliojitokeza katika tamasha la Uhondo wa Zantel wakiselebuka wakati mmoja wa wasanii waliopamba tamasha hilo akitumbuiza.

Tamasha la Uhondo wa Zantel linalodhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zantel limeendelea kukonga nyoyo za wakazi wa sehemu mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam mara hii ikiwa ni zamu ya wakazi wa Kimara na maeneo ya jirani kama inavyoonekana katika picha hizi hapa chini.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

$
0
0


UTOAJI WA MIKOPO KWA WANAFUNZI MWAKA 2016/2017
Baada ya kukamilisha zoezi la Uchambuzi wa maombi ya Mikopo 88,163 yaliyopokelewa hadi kufikia 11 Agosti, 2016. Jumla ya Wanafunzi wapya 20,183 wamepangiwa Mikopo. Upangaji huu umezingatia vigezo vilivyomo katika mwongozo wa  utoaji wa mikopo uliopitishwa na Bodi ya wakurgezi na kuidhinishwa na wizaya ya elimu sayannsi na teknoloji. Vigezo hivyo ni pamoja na
      I.        Vipaumbele vya  kitaifa vinavyoendana na Mpango  wa Maendeleo  wa Taifa wa Miaka mitano, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mafunzo ambayo yatazalisha wataalamu wanaokidhi mahitaji  ya kitaifa katika fani za kipaumbele ambazo ni;
·         Fani za Sayansi za Tiba na Afya,
·         Ualimu wa Sayansi na Hisabati,
·         Uhandisi wa  Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia,
·         Sayansi Asilia, na
·         Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu.
      i.        Uhitaji wa waombaji hususani wenye mahitaji  maalum kama vile ulemavu na uyatima
  1. Uhitaji wa waombaji wanaotoka katika familia zenye hali duni ya kimaisha
o    Wadahiliwa yatima waliopata mkopo                                                                    873
o    Wadahiliwa wenye ulemavu wa  viungo                                                                 118
o    Wadahiliwa  wahitaji wenye  mzazi mmoja                                                          3,448
o    Wadahiliwa wahitaji waliofadhiliwa na taasisis mbali mbali                                         87
o    Wadahiliwa wahitaji wanaosoma  kozi  za kipaumbele                                           6,159
o    Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi zingine                                                        9,867
Jumla                                                                                                         20,183

Kiasi cha Fedha zinazohitajika
Bajeti iliyoidhinishwa kwa ajili ya ukopeshaji kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 ni shilingi bilioni 483, kwa ajili ya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 25,717, na wanaoendelea na masomo wapatao 93, 295.
Hatua zinazofuata:
              I.        Wanufaika wote wanaopungukiwa na sifa watachunguzwa kwa ajili ya kurekebishiwa au kuondolewa katika unufaika wa mkopo
             II.        Waombaji waliwasilisha taarifa zenye upungufu, taarifa zao zitahakikiwa, na wakibainika kuwasilisha taarifa za uongo watachukuiwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kufutiwa mikopo yao
           III.        Wanufaika wote watatakiwa kuhuisha taarifa kwa kujaza dodoso. Taarifa za ziada za kiuchumi za wazazi au walezi wao zitatumika kutanua uhalisia. Wale watakaokutwa na hadhi zisizo stahili, watapoteza sifa za kuendelea kupata mikopo na kulazimika kurejesha kiasi watakachokuwa wamepokea tayari.

IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

PROF. MBARAWA AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI YA SHIRIKA LA POSTA

$
0
0
Na Daudi Manongi,MAELEZO

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Bodi teule ya Shirika la Posta kutumia fursa zilizopo ili kuongeza vyanzo vya mapato vya Shirika hilo.

Profesa Mbarawa ameyasema hayo wakati akizindua Bodi mpya ya wakurugenzi ya Shirika la Posta katika ukumbi wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano leo Jijini Dar es Salaam.

“Nashukuru kwa kuwa mmekubali uteuzi wangu,mmekuja katika shirika zuri na hivyo kama mtajipanga mtaweza kufanya mambo mengi makubwa,naitaji mtu anayeweza kutafta mapato na shirika hili la Posta lina vyanzo vingi lakini bado halijatumika vizuri na hivyo naomba mbadilishe mtazamo wa watu wetu ili msonge mbele” Alisema Prof Mbarawa.

Aidha Waziri Mbarawa ameitaka bodi iyo kuisimamia vizuri menejimenti ya Shirika la Posta ili ifanye kazi kwa ufanisi mkubwa na pia amemuagiza mwenyekiti wa bodi hiyo ya wakurugenzi kuwekeana mkakati wa mikataba ya kazi na malengo ili kupata matokeo mazuri na amesisitiza kuboreshwa kwa mahusiano kati ya watendaji wa juu na wafanyakazi wa chini.

Waziri Mbarawa ameagiza bodi iyo teule kusimamia huduma mpya ya Posta mlangoni na Huduma Center kwa uadilifu ili vilete tija kama ilivyokusudiwa na kuihakikishia bodi iyo kuwa serikali imejipanga kulipa Deni la kampuni iyo ili kupunguza mzigo wa utendaji wa shirika hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Luteni kanali Msaafu Haruni Kondo amemhakikishia waziri uyo kuwa wataisimamia vyema menejimenti ya Shirika hilo na kuhakikisha vyanzo vya mapato vinapatikana kama alivyoagiza kwani utekezaji wa majukumu ndio msingi wa maendeleo wa shirika hilo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikata utepe kwenye begi lilobeba vitendea kazi vya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora. 
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam. 


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam. 


HABARI ZIDI BOFYA HAPA

TANZANIA NA UGANDA WASAINI MKATABA WA UTEKELEZAJI UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa Tatu kushoto mstari wa Mbele) na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhandisi Irene Muloni (wa Pili kushoto mstari wa mbele) wakitoka katika eneo la Chongoleani mkoani Tanga baada ya kukagua sehemu itakayojengwa hifadhi ya mafuta pamoja na gati itakayotumika kupakia mafuta kwenye Meli mbalimbali baada ya kusafirishwa na Bomba la Mafuta kutoka nchini Uganda.
-----------------------------------------
Serikali ya Tanzania na Uganda  kwa pamoja wamesaini mkataba wa makubaliano ya namna ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa  bomba la mafuta ghafi unaotarajiwa  kuanza hivi karibuni  kutoka Ziwa Albat mpaka bandari ya Tanga.
Mkataba huo umesainiwa mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichodumu kwa siku tatu kati serikali ya Tanzania na Uganda kilichofanyika mkoani humo katika ukumbi wa hotel ya Tanga beach resort.
Makataba huo umesainiwa na waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo pamoja na waziri wa nishati na madini nchini Uganda Irene Muloni.
Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo Waziri wa nishati na madini nchini Tanzania Sospeter Muhongo alisema mkataba huo umegusa maeneo mbali mbali muhimu ikiwemo upatikanaji wa ardhi ,ulinzi pamoja na uwekezaji.
profesa Muhongo alisema Serikali ya  pande zote mbili  inashirikiana kwa ukaribu katika kuhakikiasha mradi huo unakamilika kwa wakati na kuanza kufanya kazi ifikapo mwaka 2020.
"Mradi upo na kasi ya utekelezaji inatendeka lengo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 mradi umekamilika na hivyo basi kwa sasa ni wakati wa kila mtu kuwa tayari kwaajili ya mradi huu"alisema Muhongo
Kwa upande wake Waziri wa nishati na madini nchini Uganda Irene Muloni alisema amefurahi kuona namna ambavyo wananchi wa  nchi zote mbili walivyokuwa na shauku ya kuupokea mradi huo.
"Jana nimetembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Tanga ikiwemo bandari pamoja sehemu ambayo bomba la mafuta litapita na nimeona ni jinsi gani wananchi wameufurahia mradi huu hivyo ni wakati sasa wa kufanya kazi na wananchi wa Tanzania na Uganda wajiandae"alisema Muloni

Tume ya Ushindani (FCC) yatoa msaada wa mabati 5,743 kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera leo

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstafu Salim Kijuu akiishukuru Tume ya Ushindani (FCC) kwa kutoa msaada wa bandali 360 zenye jumla ya  mabati 5,743 yenye thamani ya TZS 86.145m/- kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani humo ofisini kwa Mkuu wa Mkoa mjini Bukoba leo.
 Kamishna wa Tume ya Ushindani (FCC)Bw. Fadhili Manongi akiongea machache kabla ya kukabidhi msaada huo wa mabati.
Tume ya Ushindani (FCC) leo  akikabidhi  msaada wa bandali 360 za mabati 5,743 zenye thamani ya TZS 86.145m/- kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Maj. Gen (Rtd) Salim Kijuu. Kamishna wa Tume Bw. Fadhili Manongi (kulia) alikabidhi kwa niaba ya Tume ofisini kwa Mkuu wa Mkoa, mjini Bukoba leo.

Kagera Earth Quake Re-construction

TANZANIA DIASPORA CONFERENCE UK 2016, COVENTRY

$
0
0
RE: TANZANIA DIASPORA CONFERENCE –COVENTRY, UK 2016.
YOU  ARE  ALL  WELCOME  TO  ATTEND  THE   TANZANIA  DIASPORA  CONFERENCE   ORGANISED  BY  NEWDEAL  AFRICA  UNDER  THE  THEME  DEVELOPMENT  AND  INNOVATION
THE   EVENT  WILL  TAKE  PLACE  ON  THE  201TH  10  2016  AT  THE  SCHOOL OF  ENGINEERING  COVENTRY  UNIVERSITY TIME FROM 10 AM
THE  EVENT  AIMS  TO  BRING  MOST TANZANIANS  AND  FRIENDS  OF  TANZANIA  LIVING  IN  THE  UK TOGETHER...

WASAJILI WA NDOA MKOANI SINGIDA WAKABIDHIWA LESENI ZA KUFANYA SHUGHULI HIZO

$
0
0
TAASISI isiyokuwa ya Kiserikali ya JAMAAT ANSWARU SUNNA TANZANIA (JASUTA) Mkoa wa Singida imepinga vikali Propoganda zinazoenezwa na baadhi ya watu wa ndani na nje ya nchi wa kukiuka utaratibu wa maumbile  kwa kutaka kuhalalisha kuwepo kwa ndoa za jinsia moja nchini,na kuapa kwamba haitajihusisha na usajili wa ndoa za aina hiyo. 
Hayo yamo katika risala ya Jumuiya hiyo iliyosomwa na Shabani Ramadhani Nkhomee kwenye hafla fupi ya kuwakabidhi leseni wasajili wa ndoa  21 wa JASUTA Mkoa wa Singida,hafla iliyofanyika kwenye kituo cha walimu Nyerere, mjini Singida. 
“Nabii Luti (amani iwe juu yake ) watu wake waliangamizwa kwa kukiuka utaratibu wa maumbile Propoganda zilizopo za kuhalalisha ndoa za jinsia moja”alisema Nkhomee. 
Aidha Nkhomee alisisitiza kuwa taasisi ya JASUTA inapinga vikali na kwa nguvu zote Propoganda zinazoenezwa na baadhi ya watu wa ndani na nje ya nchi wa kukiuka utaratibu wa maumbile kwa kutaka kuhalalisha kuwepo kwa ndoa za jinsia moja. 
“Sisi tunapinga kwa nguvu zote Propoganda hizo na tunasema wazi kuwa hatutahusika kusajili ndoa hizo na tunaendelea kupinga hatua zote za kuhalalisha ndoa za jinsia moja kadri tuwezevyo”alisisitiza.
  
Akikabidhi leseni hizo kwa wasajili wa Taasisi hiyo,Mkuu wa wilaya ya Singida,Eliasi Tarimo aliweka wazi kwamba serikali haipo tayari kuunga mkono ndoa za jinsia moja.
 Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya alibainisha kuwa kwa mujibu wa sheria na kwa mujibu wa mila za kitanzania,vitendo hivyo havina nafasi katika jamii ya Tanzani,kwani utaratibu huo ni mgeni kwa watanzania.
 
Kwa upande wake katibu wa JASUTA Mkoa wa Singida,Yahaya Mohamedi alisema katika siku za nyuma si kwamba wasajili hao walikuwa hawajishughulishi na shughuli za kuozesha na si kwamba ndoa walizokuwa wakizisimamia hazikusihi,hapana bali ndoa hizo zilisihi kabisa. 
Lakini kaatibu huyo alifafanua kuwa kutokana na kuishi katika utaratibu wa kiutawala ni vema zaidi sote tukaingia katika utaratibu wa kiutawala utakaoirahisishia serikali katika kutekelza majukumu yake. 
Hafla ya kuwakabidhi leseni wasajili 21 wa JASUTA Mkoa wa Singida,ilihudhuriwa pia na baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini na Taasisi zingine za dini ya Kiislamu zilizopo mjini Singida.
  Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Eliasi Tarimo akimkabidhi mmoja wa wasajili wa ndoa wa Manispaa ya Singida leseni ya usaajili wa ndoa. Hafla hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kituo cha Walimu cha Nyerere,mjini Singida.
  Mmoja wa wasajili wa ndoa,Maalim Mayogho akimshukuru mkuu wa wilaya ya Singida kwa niaba ya wasajili 21 waliokabidhiwa leseni za ndoa kwenye hafla iliyohudhuriwa na waumini wasiopungua mia moja.
 Baadhi ya wasajili wa ndoa wa wilaya ya Singida waliohudhuria hafla ya kupokea leseni za ndoa.
 Mkuu wa wilaya ya Singida, Mhe. Elias Taraimo( wa pili  kulia) wakati wa hafla hiyo ya  kukabidhi leseni za wasajili wa ndoa wa wilaya hiyo ili waweze kufanya shughuli hizo kwa kufuata sharia,kanuni na taratibu zilizowekwa.
Katibu wa Mkoa wa JASUTA,Bwana Yahaya Mohamedi (wa kwanza kutoka kulia) akisikiliza hotuba ya mkuu wa wilaya ya Singida( hayupo pichani),Bwana Eliasi Tarimo aliyotoa kwa wasajili wa ndoa wa wilaya ya Singida,kwenye hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kituo cha walimu cha Nyerere,mjini Singida.(Picha Na Jumbe Ismailly)

YANGA YAENDELEA KUTOA DOZI LIGI KUU, YAICHAPA JKT RUVU 4-0 UWANJA WA UHURU LEO.

$
0
0
TIMU ya soka ya Yanga imefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 4-0 dhidi ya JKT Ruvu na kufikisha jumla ya alama 24 na kuendelea kusalia katika nafasi ya pili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Yanga walioanza kuona goli la JKT Ruvu dakika ya sita ya mchezo kupitia kwa Obrey Chirwa lakini umakini mbovu wa safu ya washambualiaji ulifanya wakose magoli mengi na mpaka kumalizika kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza Yanga walitoka mbele kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kulisakama lango la JKT Ruvu na katika dakika ya 63 Amisi Tambwe aliyeingia kuchukua nafasi ya Donald Ngoma aliiandikia Yanga goli la pili na dakika ya 83 Simon Msuva kwa kutumia udhaifu wa golikipa Said Kipao aliyekuwa mwiba kwa safu ya ushambuliaji wa Yanga akaweka kimiani goli la tatu.

Safu ya ushambuliaji ya JKT Ruvu wanashindwa kuwa makini ambapo wanashindwa kufanya mashambulizi ya uhakika na mabeki wa Yanga kuweza kusahihisha makosa yao.

Dakika ya 90, Amisi Tambwe anaiandikia Yanga goli la nne na kupeleka kilio zaidi kwa JKT Ruvu na mpaka dakika 90 zinamalizika Yanga wanatoka mbele kwa goli 4-0.

Yanga imecheza leo chini ya Kocha Juma Mwambusi baada ya Aliyekuwa kocha mkuu Hans Van De Pluijm kujiuzulu jana jioni.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Amis Tambwe akishangilia mara baada ya kupatia timu yake bao la pili, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu, uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo na kuifanya timu ya Yanga kuondoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 4-0. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Amisi Tambwe akiachia mkwaju mkali uliotinga moja kwa moja wavuni na kupatia timu yake bao la pili, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu, uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo na kuifanya timu ya Yanga kuondoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 4-0.
Mchezaji wa Yanga, Donald Ngoma akiwania Mpira na Beki wa Timu ya JKT Ruvu, Nurdin Mohamed katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa leo katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 4-0.

DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI JUMATANO OKTOBA 26, 2016


MAKALA YA SHERIA: MALI YA MIRATHI YA MTOTO MDOGO NA ASIYE NA AKILI TIMAMU HUTUNZWA NA NANI

$
0
0
Na  Bashir  Yakub.
Mtu  anapokufa  huacha  warithi  wa  namna  mbalimbali.  Yumkini  ndani  mwake  waweza  kuwamo  watoto  wenye  umri  mdogo na  hata  vichaa.  Umri  mdogo  twaweza  kuuhesabu  kuanzia   mwaka  0  mpaka 18. Aidha wakubwa ambao  wamezidi  miaka 18  hao nafasi  yao   inajulikana   ikiwa  marehemu  ameacha  mali.

Mali  zao  watakabidhiwa  kwa  utaratibu  maalum  ulioratibiwa  na  sheria.  Swali  litakuwa  kwa watoto wadogo  ambao  hawawezi  kukabidhiwa, tutahitaji  kujua  sheria  inasemaje.
Hapa  kuna  mazingira  ya aina  mbili kwanza, ni  pale marehemu  anapoacha  warithi  watoto  tu  na  hakuna  mkubwa  hata  mmoja  na  pili ni  pale anapoacha  warithi wakubwa  na  watoto.

Pia  kwa  ufupi  tutaangalia   sheria  inavyosema  kuhusu  mali  za  mrithi  ambaye  hana  akili  timamu. Hii  nayo  tutaangalia  mazingira  yote,  mazingira  anapokuwa  na  warithi  wenzake  na  mazingira  anapokuwa  mrithi  pekee.

1.MTOTO  MDOGO.
Sura  ya  352 kifungu  cha  23 Sheria  ya  mirathi  kinasema  kuwa  urithi  au  hati  ya  kusimamia  mirathi  haiwezi  kutolewa  kwa  mtoto mdogo.

Tukiachana  na hilo tujue  kuwa  ikiwa mtoto  mdogo  si  mrithi  pekee  isipokuwa  wapo  ndugu  zake  wengine  ambao  ni  warithi  basi  mmoja  wao  muadilifu  atateuliwa  kusimamia  mirathi  yote ikiwemo  ya  mtoto  mdogo. Msimamizi  huyo  atakuwa  na  wajibu  wa  kuhakikisha  anatunza  mali  ya  mtoto/watoto  hao  mpaka  wanakua  na  kuwa  na uwezo  wa  kutunza  mali  zao  binafsi.

Pili ni  pale  ambapo  mtoto/watoto  wadogo  ndio  warithi  pekee   wa  mali yaani  hakuna  mkubwa  kati  yao.  Ikiwa  hilo  litatokea  basi   mlezi  wa  watoto anaweza  kuomba  mahakamani  kusimamia  mirathi hadi  watakapokua.

Taasisi  ya  udhamini  ( trust  cooperation)  pia  yaweza  kuomba  au  kupewa  bila  kuomba  jukumu  la kusimamia  mali  za watoto  hadi  watakapokua. Hii  ni  kutoka  kifungu  cha 22 cha  sheria  ya  mirathi.  Yeyote  atakayeteuliwa  kati  yao  atakuwa na  wajibu  mkubwa wa  kuhakikisha  anatunza  mali  za  watoto  kwa  kadri  mahakama itakavyoelekeza.

Wakati  mwingine  wanaweza  kujitokeza  walezi   wengi  kila mmoja  akitaka  kusimamia  mali  za  watoto.  Ikiwa  itakuwa  hivyo  basi  suala  hilo  litapelekwa  mahakamani  na  mahakama  itaamua  nani  anafaa  kusimamia  mali  hizo  kwa  kuzingatia  zaidi  mustakabali  wa  baadae  ya  hao  watoto.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS OKTOBA 27

WAZIRI MAKAMBA AKAMILISHA ZIARA KATIKA MKOA WA KATAVI

$
0
0
 Bibi Josephine Rupia, Mkuu wa Idara ya Maliasili Halmashauri ya Mpanda akitoa maelezo ya Mto Katuma kupoteza mwelekeo wa kutiririsha maji katika mkondo wake kama ilivyokuwa hapo awali. Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akihutubia wananchi wa kijiji cha Kabage kilichopo Mkoani Katavi na kuwasisitizia umuhimu wa Hifadhi ya Mazingira

Mmiliki wa Kiwanda cha kutengeneza chumvi cha Nyanza Mining akitoa maelezo kwa Waziri Makamba juu uzalishaji wa chumvi hiyo kwa kutumia nishati ya jua.



TAARIFA YA ZIARA YA MHE. JANUARY MAKAMBA KATIKA MKOA WA KATAVI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na  Mazingira  Mhe January Makamba hii leo ameendelea na ziara yake katika Mkoa wa Katavi kwa kutembelea kijiji cha Kabege ambapo aliangalia mradi Mkubwa wa Umwagiliaji wa Mwamkulu katika Manispaa ya Mpanda ambao kwa sasa umesitisha kutoa huduma zake kwa kukosekana kwa maji ya kutosha katika Mto Katuma.


Katika kikao cha Majumuisho ya Ziara yake ya siku mbili katika Mkoa wa Katavi, Waziri Makamba ameutaka uongozi wa Mkoa huo kudhibiti yafuatayo:

1.    Ongezeko la watu na mifugo ambayo kwa kiasi kikubwa inachangia uharibifu wa mazingira.

2.    Kusitisha uchepushaji kwa Mto Katuma ambapo taarifa ya Mkoa ilieleza kuna jumla ya mabanio 40 ambayo yanatumiwa na watu kuchepusha maji kwa ajili ya manufaa yao binafsi.

3.    Uchimbaji hatari wa Madini usiofuata taratibu

4.    Kuhuisha sheria ndogo ndogo za mazingira katika ngazi mbalimbali za Serikali za mitaa

5.    Kuanisha maeneo maalumu ambayo yatatangazwa katika Gazeti la Serikali kama mazingira nyeti ili kuyapa ulinzi zaidi

6.    Kusimamia uondoshwaji wa wavamizi katika Vyanzo vya maji

7.    Kufanyika kwa sensa ya mifugo ili kujua Mkoa una mifugo kiasi gani na kubuni namna bora ya kuhumudimia mifugo hiyo bila kuathiri mazingira

8.    ameahidi kuaanda andiko maalumu la Mradi wa Ziwa Katuma

9.    Mmiliki wa Jema Sitalike Project kutafutwa popote alipo, leseni yake ya madini isitishwe, apigwe faini na kurekebisha eneo alilokuwa akitumia awali kwa shughuli za uchenjuaji wa dhahabu.

10.  Waziri Makamba meagiza Watendaji kata na Vijiji kutotoa vibali vya uchimbaji wa madini bila kufuata utaratimu wa Wizara ya Nishati na Madini


Mara baada ya Majumuisho Waziri Makamba alipata fursa ya kuongea na wanakijiji cha Kabage na kusisitiza yafutayo:

1.    Wananchi kutunza mazingira kwa kutofanya kilimo cha kuhamahama, Ukataji Ovyo wa Miti na Uchomaji wa misitu.

2.    kuwakumbusha wananchi kuwa rasilimali ya maji ni ya watu wote hivyo isiwanufaishe watu wachache

3.    Serikali inaangalia namna bora ya kurudisha Mto Katuma katika njia yake ya awali ambayo ilipotea baada ya kutokea kwa mafuriko mwaka 1998

4.    Kuundwa kwa jumuiya za watumia maji na kuzingatia Sheria ya Mazingira ya kutofanya shughuli zozote za kibinadamu ndani ya mita sitini za chanzo cha maji

5.    Kuundwa kwa Kamati ya Mazingira katika Kijiji hicho

6.    Kuondokana na Makazi holela kwa kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Waziri Makamba amewasili Katika Mkoa wa Kigoma na kutembelea kiwanda cha Nyanza Mines na kuwapongeza kwa kuzalisha chumvi kwa kutumia nishati ya jua ambapo awali kiwanda hicho kilifungiwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutokana na uharibifu wa Mazingira kwa kutumia magogo mengi mwaka 2015. Kiwanda hicho kwa sasa kinazalisha tani 20,000-25,000 ndani ya miezi mitatu.

KAMPUNI YA GAZETI LA DIRA YAIOMBA RADHI JESHI LA WANACHI TANZANIA (JWTZ).

$
0
0





UONGOZI wa kampuni ya DIRA NEWSPAPER COMPANY LTD wachapishaji wa gazeti DIRA YA MTANZANIA unamwomba radhi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa nchi na jeshi la wananchi wa Tanzania kwa ujumla kwa habari iliyochapishwa kwa bahati mbaya katika gazeti letu; toleo Na.424 la Juni,20-26 ,2016 iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho “KIFARU CHA KIVITA CHA JWTZ CHAIBWA”.

Tunapenda kueleza kwa masikitiko kuwa habari hiyo ilichapishwa kwa bahati mbaya baada ya mtayarishaji wa kurasa (graphic designer) kuipanga habari ambayo ilikuwa haijakamilika kiuchunguzi na kuiacha iliyotakiwa ichapishwe siku hiyo.

Tunapenda JWTZ na watanzania wote kwa ujumla kuwa wafahamu kuwa gazeti la DIRA YA MTANZANIA halikulenga kuchafua Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kama ambavyo baadhi ya watu walivyofikiria.

Tunafahamu mchango mkubwa wa jeshi la wananchi wa Tanzania kwa taifa letu na namna jeshi hilo linavyoshirikiana kwa kiasi kikubwa na vyombo vya habari hasa utoaji wa taarifa mbalimbali na kamwe jeshi hili tokea kuanzishwa kwake halijawahi kukwaruzana na vyombo vya habari jambo ambalo ni heshima kubwa kwetu na taifa kwa ujumla.

Hivyo uongozi wa gazeti hili umeonelea kuomba radhi kwa Mkuu wa majeshi (CDF), askari wote wa JWTZ na watanzania wote walioshitushwa na habari hiyo na hasa mkuu wa kikosi cha 83 KJ cha Kiluvya mkoani Pwani ambaye kikosi chake kilitajwa kama chanzo cha habari hiyo.

Na tunaomba ifahamike kuwa tumeomba radhi kwa ridhaa yetu na tunaamini kuwa “kuomba radhi” ni kitendo cha kiungwana kwa utamaduni wa waafrika na hasa watanzania tuliokulia katika misingi ya amani, upendo na utulivu na pia tunaamini kuomba kwetu radhi kutazidisha mahusiano mema na ya karibu kati yetu na JWTZ.

Tunatanguliza shukrani zetu.

Musiba Esaba Meneja utawala na Fedha.

TAASISI YA TEKNOLOJIA DAR ES SALAAM: KUANZA KWA MUHULA/MWAKA WA MASOMO 2016/17

$
0
0
Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) anawatangazia kuwa Muhula wa kwanza wa Mwaka wa Masomo 2016/2017 utaanza rasmi tarehe 7/11/2016.  Wanafunzi wote wa Mwaka wa kwanza (OD & BEng / BTech) wanatakiwa kuripoti chuoni kuanzia siku ya Jumamosi tarehe 29/10/2016 kwa usajili na “Orientation Week” itakayofanyika kwa wiki moja kuanzia tarehe 31/10/2016. Aidha, mambo yafuatayo ni muhimu sana kuzingatiwa kwa wanafunzi wote kuelekea ufunguzi wa Chuo.

1.Usajili utafanyika kwa wiki mbili tu na mwanafunzi ambaye hatakamilisha usajili wake kwa muda huo hataruhusiwa kuingia darasani.

2.Ili mwanafunzi akamilishe usajili ni lazima alipe Ada na kuwasilisha Bank pay in slip wakati anasajiliwa.

3.Wanafunzi wa Stashahada wenye ufadhili binafsi (Private sponsored Students) watakaopata nafasi ya  Malazi katika mabweni ya Taasisi watalazimika kulipa jumla ya Tshs 990,000/- kwa mwaka na watahudumiwa kwa utaratibu maalum watakaoelekezwa baada ya kukamilisha malipo hayo.

4.Kila mwanafunzi wa mwaka wa kwanza atahitajika kuwasilisha vyeti halisi wakati wa usajili kinyume cha hapo hatasajiliwa kama mwanafunzi wa DIT.

5.Sheria zote za udahili na mitihani zitazingatiwa kama zilivyochapishwa katika Prospectus ya Taasisi kwa Wanafunzi wote wanaoendelea yaani mwaka wa Pili hadi wa Nne na KWA WANAFUNZI WAPYA WANAONZA MWAKA WA KWANZA 2016/2017 kuna nyongeza kwenye sheria hizo kwamba; Mwanafunzi atakayeshindwa  kufaulu CA (Continous Assessment) hatapewa nafasi ya mtihani wa Marudio yaani Supplementary Exam na badala yake atalazimika kuirudia hiyo “module” upya katika mwaka wa kimasomo unaofuata. 

6.Akaunti zifuatazo zitatumika kwa malipo.
Ada na gharama nyingine:  A/C. No. 0150408417800 – CRDB
Chakula na Malazi; Bima ya Afya (NHIF); DITSO Fees zilipwe zote kupitia 
A/C No. 011103005481 – NBC LTD Tawi lolote kabla ya Usajili.

7.Malipo ya Ada ni lazima yalipwe kwa angalau 50% kabla ya kujisajili.

Ofisi ya Uhusiano,
Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam,
S.L.P 2958,
Dar es Salaam.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images