Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1405 | 1406 | (Page 1407) | 1408 | 1409 | .... | 3285 | newer

  0 0

   Sherehe za Mahafali ya tatu ya shule ya Mkuza Girls iliyopo Kibaha ambapo wanafunzi na Bodi ya shule wanapata picha ya pamoja na mgeni rasmi msaidizi wa Askofu Mchungaji  Chediel Lwiza 
   Mgeni rasmi Msaidizi wa Askofu Mchungaji Chediel Lwiza katika picha ya pamoja na pamoja na wajumbe wa bodi wa shule ya Mkuza
   Wajumbe wa Bodi wa Shule Mkuza wakiongozwa na Mwenyekiti wao  Mwanasheria Happy Mchaki na Bi Pamella Solomon walipokuwa wakitembelea miradi mbalimbali shulen hapo kabla ya mahafali kuanza
   Mjumbe wa bodi Bi. Pamella Solomon akitoa zawadi ya t-shirt kwa wahitimu 5 kama mchango wake wakati wa harambee ya kukarabati bweni shuleni hapo
  Wajumbe wa Bodi wakisikiliza kwa makini mmoja wa wanafunzi wa shuleni hapo akielezea 'acceleration of gravity' kabla ya kuanza kwa sherehe za mahafali ya kidato cha nne.

  0 0


  SIMU.TV: Naibu balozi wa Ufaransa ametembelea kampuni ya Africa Media Group na kujadili namna ya kueneza utamaduni wa kifaransa kupitia vipindi vinavyorushwa na Channel ten. https://youtu.be/PJYI6ityIFc

  SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amezindua mpango wa kunywa dawa za kinga ya magonjwa ya Mabusha, Matende Minyoo ya tumbo na Vikope. https://youtu.be/6V4EKRCJ8Us

  SIMU.TV: Wananchi katika vijiji vya Nadare na lubwa wilayani Longido wanalazimika kutembea kilometa 25 kufuata huduama za afya. https://youtu.be/-p983Efi8uQ

  SIMU.TV: Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom leo wamejitokeza kupima kwa hiyari na kupata ushauri wa magonjwa ya saratani. https://youtu.be/fWY8GAdjnnc

  SIMU.TV: Mkutano wa tano wa ushirikiano kati ya nchi za Afrika na Korea ya kusini umefanyika huko Korea ya Kusini ukijadili namna ya kuendeleza nchi za Afrika kupitia sekta ya kilimo na viwanda. https://youtu.be/P8DuKo5H4Vc

  SIMU.TV: Wizara ya viwanda biashara na uwekezaji ikishirikiana na mamlaka ya biashara TANTRADE imeandaa maonesho ya viwanda vilivyopo nchini ili kutangaza fursa zilizopo kwenye sekta hiyo. https://youtu.be/cHOIj7Qdvn0

  SIMU.TV: Wadau kutoka taasisi za kiserikali na asasi za kiraia wametakiwa kutoa mapendekezo ya kuandaa sera mpya ya uwezeshaji kwa wananchi. https://youtu.be/IZH2lkz1lyg

  SIMU.TV: Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga kesho inatarajia kuingia uwanjani kucheza na JKT Ruvu ikiwa ni mchezo wake wa kiporo. https://youtu.be/aDrXpfbO0cA

  SIMU.TV: Bondia kutoka nchini China amewasili nchini kwa ajili ya pambano lake dhidi ya mtanzania Dulla la kuwania ubingwa wa dunia wa WBO. https://youtu.be/lY-yilIGZXg

  SIMU.TV: Kutotiliwa mkazo kwa somo la sanaa na michezo shuleni kunasababisha kuzorotesha afya za wananfunzi pia kupoteza vipaji vya michezo kwa wanafunzi. https://youtu.be/uC05oW25_tc

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya MOI akifungua rasmi sherehe za kuadhimisha siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi Duniani,ambapo alisema wanakazi kubwa ya kutoa matibabu kwa watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubongo na mifupa na mpaka sasa watoto takribani 202 wameshafanyiwa upasuaji na zoezi linaendelea Nchi nzima.
  Mwenyekiti wa chama cha wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi Bw. Hakim ambaye nae mtoto wake anamatatizo kama hayo akielezea  kuwa kuna umuhimu wa kutoa elimu kwa kuwa watu wengi wanahusisha tatizo hilo na imani potofu, aliongeza kuwa watoto waliofanyiwa upasuaji mkoa wa Mbeya ni 18, Morogoro 12, Mwanza 50, na Izazi 14. na wamefanikiwa kuokoa Maisha ya watoto 185 katika mikoa 16 Tanzania.
  Meneja wa Nakiete akitoa neno wakati wa Maadhimisho hayo
  Mmoja wa wazazi akiwa na Mwanae mwenye tatizo la Kichwa kikubwa
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Moi (Kushoto) akipokea Msaada kutoka Duka la madawa la Nakiete.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO-Dar es Salaam 
  SERIKALI imesema hakutokuwa na matumizi mabaya ya mamlaka anayopewa Waziri anayesimamia tasnia ya habari katika muswada wa sheria ya huduma ya habari isipokuwa kwa masuala yatakayohatarisha usalama wa Taifa.
  Imesema Serikali haiwazuii waandishi wa habari kukosoa sera, matamko na ahadi mbalimbali zinazotolewa na Viongozi wa kitaifa pindi wanaposhindwa kutekeleza maagizo wanayoyatoa kwa wananchi.

  Akizungumza katika mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Hassan Abbas alisema muswada huo unatoa fursa kwa chombo cha habari kupeleka malalamiko yake mahakamani pindi inapotokea kutokubaliana na hatua itakayoweza kuchuliwa na Waziri mwenye dhamana ya habari.
  Kwa mujibu wa Abbasi alisema yapo masuala kadhaa yanayopaswa kuchuliwa hatua za haraka za maamuzi ikiwemo suala la uchochezi, uasi wa kikundi fulani cha watu kinachotaka kuigombanisha Serikali na wananchi.
  Aliongeza kuwa hata katika mikataba ya kimataifa ikiwemo kifungu cha 19 mkataba wa geneva wa mwaka 1966 umeeleza kuhusu haki ya kupata habari na taarifa ingawa upo ukomo katika masuala kadhaa ikiwemo suala la usalama wa taifa.


  Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas (mwenye suti) akizungumza katika ya kipindi mahojiano maalum cha 360 kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha CLOUD wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam na kuelezea maudhui mbalimbali yaliyopo katikamuswada ya sheria ya huduma ya Habari. Wengine ni Watangazaji wa Kituo hicho, Babbie Kabae (kushoto) na Hassan Ngoma. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Redio cha Times FM cha Jijini Dar es Salaam, Rehure Nyaulawa akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas kuhusu utendaji kazi wa gari la urushaji matangazo ya nje. Katika ziara hiyo Msemaji huyo wa Serikali alizungumzia maudhui mbalimbali yaliyopo katika muswada wa sheria ya huduma ya habari. 
  Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya Uhariri ya Kituo cha Redio cha Times FM cha Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari Jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo Msemaji huyo wa Serikali alizungumzia maudhui mbalimbali yaliyopo katika muswada wa sheria ya huduma ya habari. (PICHA NA ISMAIL NGAYONGA) .
  0 0

  Afisa Mtendaji wa Kata ya Mburahati Jijini Dar es salaam ametakiwa kusimamia kwa uaminifu mapato ya soko Mburahati ili kuimarisha mapato ya Manispaa hiyo ambayo yataimarisha uboreshaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi.
  Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati alipofanya ziara sokoni hapo kwa lengo la kujionea hali halisi ya soko pamoja na hali ya ukusanyaji wa mapato.
  Sambamba na agizo hilo pia Mkurugenzi amemtaka Afisa Mtendaji huyo kwa kushirikiana na kamati ya soko Kuandaa orodha ya majina ya walipaji wote pamoja na kiasi wamachotakiwa kulipa, kutolewa namba pamoja na kuwepo na orodha ya kiasi kinachotakiwa kukusanywa kutoka katika maduka hayo, Kutoa mapendekezo mapya ya viwango vya tozo, na kuwepo na jina la kila mmiliki wa meza sokoni hapo na kiasi cha ushuru anacholipa.
  MD Kayombo ametoa siku tano kwa Afisa Mtendaji huyo kwa kumtaka Kuwasilisha orodha ya watu wote wanaodaiwa tozo na kodi katika soko na vibanda pamoja na muda wanaodaiwa sambamba na Kutengeneza data base ya wafanyabiashara wote katika soko hilo.
  Pamoja na ukaguzi huo Mkurugenzi alipata maelezo juu ya ukusanyaji mapato katika soko la Mburahati lililopo pembeni ya jengo la soko linalojengwa. Akisomewa taarifa ya soko hilo na katibu wa soko Ndg Fikiri Pazi alisema kuwa wenye meza hulipa kiasi cha shs 200 kwa siku na wenye vibanda (maduka)hulipa shs21000 kwa mwezi viwango ambavyo wamekuwa wakilipa tangu kuanza kwa soko hilo mwaka 1982.
  Mkurugenzi hakuridhika na viwango hivyo kwa ni ni viwango vilivyopitwa na wakati kutokana na hilo ameagiza tozo hizo ziangaliwe upya na walete mapendekezo ya viwango vipya ambapo menejimenti ya Manispaa itavipitia na kulinganisha na mapendekezo ya viwango vya menejimenti na kisha kufanya maamuzi ya viwango vipya.

  0 0


  0 0

  Mhe. Mohammed Haji Hamza, Balozi wa Tanzania nchini Misri akiwakaribisha wageni waliohudhuria katika ufunguzi wa kongamano la biashara kati ya Tanzania na misri lililofanyika katika miji ya Cairo na Alexandria kuanzia tarehe 17 hadi 19 Oktoba 2016. Kongamano hili lililowakutanisha wafanyabiashara kutoka nchi hizi mbili lilifunguliwa na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Mhe Balozi Amina Salim Ali. 

  Kongamano hilo lilihudhuriwa na washiriki kutoka sekta mbalimbali zinahusika na uwekezaji, biashara, ujenzi, usafirishaji, elimu, afya, viwanda, uhandisi ,kilimo na utalii. Kongano hilo liligharmiwa na kuratibiwa kwa ushirikiano kati ya Ubalozi wa Tanzania nchini Misri, Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri, Jumuiya za Wafanyabiashara wa Misri na makampuni binafsi ya biashara ya Misri. Katika kongamano hilo washiriki wa Tanzania pamoja na kutoa mada zilizohusu fursa za biashara na uwekezaji nchini Tanzania na hasa katika sekta ya viwanda na utalii pia walipata fursa ya kushiriki katika mazungumzo ya ana kwa ana ya kibiashara.

  Siku ya pili ya kongamano hili washiriki kutoka Tanzania walipata nafasi ya kutembelea sehemu mbalimbali za uzalishaji na huduma zikiwemo: kijiji cha teknolojia cha Cairo, viwanda vya utengezaji madawa, vifaa tiba na rangi za ujenzi mjini Cairo pamoja na viwanda vya nguo, vifaa vya ujezi na samani za chuma katika miji wa Tenth Ramadhani . 

   Siku ya tatu ya kongamano hilo baadhi ya washiriki kutoka Tanzania walitembelea vyuo vikuu vya Alexandria na chuo kikuu cha kiarabu cha sayansi, teknolojia na usafiri wa bahari mjini Alexandria na kuwa na mazungumzo ya ushirikiano na viongozi wa vyuo vikuu hivyo. 

  Ujumbe wa Tanzania pia ulipata nafasi ya kutembelea kiwanda cha kutengenezea manukato kilichopo nje kidogo ya jiji la Akexandria. Akiwa jijini Cairo, Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika kongamano hilo alipata nafasi ya kukutana na Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Misri, Rais na Mtendaji Mkuu wa Afri exim bank na Katibu Mkuu wa Wakala wa Ushirikiano na Maendeleo wa Misri.
  Vingozi mbalimbali walioshiriki kwenye ufunguzi wa konganano la kibiashara mjini Cairo siku ya tarehe 17 Oktoba 2016 wakisimama wakati wa Nyimbo za Taifa za Tanzania na Misri zilipopigwa. Wa kwanza kutokea kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda wa Misri. Wa pili ni Katibu Mkuu wa Wakala wa Ushirikiano na Maendeleo wa Misri, watatu ni Mhe Balozi Amina Salim Ali, Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar, akifuatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Misri, Mhe. Mohamed Haji Hamza , watano ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar na wa sita ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Biashara ya Misri. Waliosimama mbele ya meza kuu ni Mabalozi kutoka nchi za SADC waliopo mjini Cairo. 
  Balozi Amina Salum Ali, Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Zanzibar akifuatilia neno la ukaribisho kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Misri, Mhe. Mohammed Haji Hamza .


  0 0

   Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wenzake wa Fedha kutoka nchi 54 za Kiafrika, wanaohudhuria Mkutano wa 5 wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea na nchi za Afrika (KOAFEC), unaofanyika Jijini Seoul, Korea Kusini.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika anayeiwakilisha Tanzania (AfDB) Dkt. Nyamajeje Weggoro (katikati) wakimsikiliza kwa makini Raisi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kabla ya kuanza kwa mkutano unaojadili namna kilimo na mapinduzi ya viwanda vinavyoweza kuibadili Afrika Kiuchumi na Kijamii wakati wa Mkutano wa 5 wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea na nchi za Afrika (KOAFEC) unaofanyika Jijini Seoul, Korea Kusini. 
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango  (Mb) (katikati) akiwa na Mawaziri wenzake kutoka nchi za Kenya, Uganda na Ethiopia (wengine hawako Pichani) wakionesha kwa waandishi wa habari (hawako pichani pia) nyaraka za makubaliano ya uteuzi wa mradi utakao fadhiliwa kwa pamoja kati ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Serikali ya Korea, wenye thamani ya dola Milioni 50 za Marekani sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 100.18 zitakazotumika kujenga njia ya usafirishaji umeme kwa njia ya gridi ya Taifa, yenye msongo wa kV 400 katika ukanda wa kaskazini Magharibi kwa upande wa Tanzania itakayoanzia mkoani Mbeya, Nyakanazi hadi Mkoani Kigoma. wakati wa Mkutano wa 5 wa ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na nchi za Kiafrika, unaoendelea Jijini Seoul Korea Kusini.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kushoto, na Mwenyekiti ambaye pia ni Rais wa Benki ya EXIM ya Korea Kusini, Lee Duk-Hoon, wakitia saini  Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za marekani milioni 90.092 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 194 za Tanzania, kwa ajili ya mradi wa Upanuzi wa Miundombinu ya mfumo wa maji taka Jijini Dar es salaam, wakati wa Mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea na nchi za Afrika, unaoendelea Jijini Seoul, Korea Kusini


  Baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania na Korea walioshuhudia utiawaji saini wa mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za marekani milioni 90.092 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 194 za Tanzania, kwa ajili ya mradi wa Upanuzi wa Miundombinu ya mfumo wa maji taka Jijini Dar es salaam, wakati wa Mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea na nchi za Afrika (KOAFEC), unaoendelea Jijini Seoul, Korea Kusini.
  Picha zote na Benny Mwaipaja-Wizara ya Fedha na Mipango)


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa Rwekaza Mukandala (kulia kwake) kuelekea kwenye ukumbi wa Nkurumah baada ya kuwasili kwenye Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuhutubia kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 55 ya Chuo hicho Oktoba 25, 2016. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ally Happy, kushoto ni Rais wa Jumuiya ya Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Jaji Joseph Warioba na wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinoloji, Dkt. Leonard Akwilapo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa Rwekaza Mukandala baada ya kwasili kwenye ukumbi wa Nkurumah chuoni hapo kuhutubia kwenye kilelele cha Maadhimisho ya Miaka 55 ya Chuo hicho Oktoba 25, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia kwenye kilele cha Maadhiisho ya miaka 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwenye ukumbi wa Nkurumah jijini Dar es salaam Oktoba 25, 2016.
  Baadhi ya waliohudhuria kwenye kilele cha Maadhimisho ya miaka 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye ukmbi wa Nkuruma jijini Dar es salaam Oktoba 25, 2016.


  0 0

  Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) Jamila Mahmoud akitoa elimu kwa wanafunzi wa darasa la walemavu wa akili liliopo Skuli ya Jang’ombe juu ya kuelewa viashiria vya udhalilishaji wa kijinsia
  Baadhi ya walemavu wa akili wa Skuli ya Jang’ombe wakionyesha kazi walizofanya wakati wa mafunzo yaliyotolewa na Viongozi wa ZAFELA kuhusu kuelewa viashiria vya udhalilishaji wa kijinsia.
  Mratibu wa ZAFELA Saada Salum Issa akifuatilia kazi walizowapa walemavu wa akili wa Skuli ya Jang’obe wakati walipofika kutoa elimu ya kutambua viashiria vya udhalilishaji wa kijinsia.

  0 0

    Mfalme Mohammed  VI wa Morocco akibusu Masahaf kabla ya kumkabidhi Waziri Mkuu Kasim Majaliwa katika hafla fupi ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa msikiti kwenye eneo la BAKWATA Kinondoni jijini Dar es salaam Oktoba 25, 2016.  Kulia ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Abukary Zubeir. Jumla ya Masahaf 10000 zilikabidhiwa na Mfalme huyo
   Mfalme Mohammed  VI wa Morocco na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakishuhudia wakati Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir (kulia)  akitia saini Makubaliano ya ujenzi wa Msikiti kwenye eneo la BAKWATA, Kinondoni jijini Dar es salaam Oktoba 25, 2016
   Mfalme Mohammed  VI wa Morocco na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakishuhudia wakati Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir (kulia)  akitia saini Makubaliano ya ujenzi wa Msikiti kwenye eneo la BAKWATA, Kinondoni jijini Dar es salaam Oktoba 25, 2016
  Mfalme   Mohammed VI wa Morocco,  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa , Rais Mstaafu Alhaj  Ali Hassan Mwinyi na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Bilal wakiwa katika hafla fupi ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa msiki uliofnywa na Mfalme Mohammed wa Morocco kwenye  eneo la BAKWATA, Kinondoni jijini Dar es salam Oktoba 25, 2016.  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0


   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika foleni akisuburi zamu yake ya kupiga kura leo katika kituo cha hospitali ya kijiji cha Msoga kata ya Msoga wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani Oktoba 25,2015  
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ambaye pia nu mgombea wa Urais akipiga kura yake katika kituo cha Skuli ya Msingi ya Bungi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kaskazini Unguja

  Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipiga kura yake kijijini Chato mkoani Geita leo.

  0 0
  0 0

   
   Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu (katikati) akimuonesha namba ya simu Afisa mwandamizi wa  Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini,Bakari Maggid (kushoto)ili aihakiki ambapo Bw. Venansi Deo, Mkazi wa Kahama aliibuka mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 100/- kupitia droo kubwa ya  promosheni ya ”kamata mpunga” inayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544.Aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neno”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali.Kulia ni Meneja Msimamizi wa masuala ya Usalama wa kampuni hiyo, James Wawenje.
    Afisa mwandamizi wa  Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini,Bakari Maggid(kushoto) na  Meneja Msimamizi wa masuala ya Usalama wa Vodacom Tanzania, James Wawenje wakimshuhudia Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)baada ya kumtangaza Bw. Venansi Deo,Mkazi wa Kahama kuwa mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 100/-kupitia droo kubwa ya “Kamata Mpunga”inayoendeshwa na kampuni hiyo na kuwawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno“GO”kwenda namba 15544.Aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neno”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali.


  0 0

  Ziafuatazo ni picha za hafla mchapalo (Cocktail Party) ya kukata na shoka ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa tangu ulipoanzishwa iliyofanyika nyumbani kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali mashuhuri kutoka taasisi mbalimbali za serikali, binafsi pamoja na mabalozi wa nchi mbalimbali.
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa katika hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya umoja huo tangu kuanzishwa kwake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) kuzungumza na wageni waalikwa.
  Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika nyumbani kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) jijini Dar es Salaam.
  Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu (kulia) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.
  Picha juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Shamimu Nyaki-WHUSM. 

  Ubalozi wa China nchini umeipatia Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo vifaa vya ofisi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 ikiwa ni kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Serikali hizo mbili.

  Hatua hiyo imekuja ikiwa na lengo la kusaidia katika kukuza na kuendeleza sekta ya sanaa ambayo katika mpango wa miaka mitano ya maendeleo ya Serikiali inatakiwa kuongeza ajira pamoja na pato la taifa kupitia kazi mbalimbali za sanaa.

  Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo leo Jijini Dar es Salaam Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu aliushukuru Ubalozi huo kwa mchango wao wa kuhakikisha sekta ya sanaa inakuwa na kuleta mabadiliko nchini.

  “Tunashukuru Ubalozi wa China kwa kutupatia vifaa hivi ambavyo vitasaidia sana utendaji katika Sekta ya Sanaa ambayo inaendelea kukua kwa kasi hapa chini na kusaidia kuimarisha ushirikiano mzuri baina ya Serikali yetu na China”Alisema Bw. Petro Lyatuu.
  Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu akipokea Luninga kutoka kwa Mshauri wa masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China hapa nchini Bw Gao Wei wakati wa makabidhiano ya. Vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 kutoka Ubalozi wa China nchini kwa ajili ya maendeleo ya Sekta ya Sanaa leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara hiyo , kulia ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Bibi Leah Kihimbi. 

  . Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya Vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 kutoka Ubalozi wa China nchini kwa ajili ya maendeleo ya Sekta ya Sanaa leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara hiyo ,kushoto ni Mshauri wa masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China Bw.Gao Wei, na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Bibi Leah Kihimbi.  

  Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu (Katikati ) akimshukuru Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China Bw Gao Wei kutokana na msaada wa Vifaa walivyotoa kwa Wizara kwa ajili maendeleo ya Sekta ya Sanaa leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara hiyo, kulia ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa wa Wizara Bibi Leah Kihimbi. 
  Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi Leah Kihimbi (Kulia) akitoa neno la Shukrani kwa Ubalozi wa China hapa nchini baada ya kupokea Vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 kutoka Ubalozi wa China nchini kwa ajili ya maendeleo ya Sekta ya Sanaa leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara hiyo ,katikati ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Petro Lyatuu, na kulia ni Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China Bw. Gao Wei. 


  0 0

  Na Mashaka Mhando, Tanga .

  MTANDAO wa kijamii wa Wana muziki na wadau wa muziki wa dansi nchini (Kavasha), wamechanga fedha zilizowezesha mwanamuziki George Gama kupata kadi ya bima ya afya.

  Mtandao huo kupitia simu za mikononi imewezesha kumkatia bima ya afya kupitia Chama cha mtandao wa Wana muziki nchini ambao ni wakala wa NHIF kama kundi chini ya mwanamuziki nguli John Kitime ambaye ni kiongozi wa mtandao huo na amepewa kadi hiyo na mfuko wa bima ya afya wanaita NHIF .

  Kiongozi wa kundi la mtandaoni linalojumuisha wadau wa muziki na Wanamuziki wa dansi (Kavasha) Fredy Paschal alisema wao kama kundi wameweza kuchanga fedha kiasi cha Zaidi ya sh 76,800/= zilizowezesha mwanamuziki huyo wa zamani wa bendi mbalimbali ikiwemo Twanga Pepeta, kupata kadi hiyo aliyokabidhiwa na Katibu wa Kavasha John Shekwavi aliembatana na Mwanamuziki Tabu Mambosasa ambae ni Mweka Hazina wa kundi hilo .

  Alisema sababu ya wao kuchangia gharama ya kadi hiyo kuwa ni utaratibu wa kundi kusaidiana baina ya wanachama, kusaidia kuinua muziki wa dansi na kusaidi wanamuziki hapa nchini.

  Paschal aka FP alisema mwanamuziki huyo ni wa kwanza kwa utaratibu huo na kwamba hivi sasa mwanamuziki wa zamani wa bendi ya UDA jazz Mikidadi Seif na mkewe watafatia baada ya kiasi kinachohitajika kuwa tayari kimeshachangwa.

  "Huyu (Gama) ni mwanamuziki wa kwanza kupata bima lakini kuna maandalizi ya kadi ya Bima ya mwanamuziki wa zamani wa UDA JAZZ Ndugu Mikidadi Seif na mkewe Bi Zulfa zipo kwenye maandalizi ya awali kupitia kundi la PSPF ambavyo vyote ni michango ya wanachama wa kundi la Kavasha, "alisema Paschal.

  Alisema utaratibu wa kundi hilo la Kavasha ni kuwa ni kuwasaidia mwanachama wao ingawa wamekuwa pia wakiwasaidia wanamuziki hasa wasio na misaada ikiwemo fedha za matibabu kupitia michango kwa wanamuziki kadhaa na wanachama pia pamoja na msaada wa mazishi.

  Paschal alisema Malengo ya kavasha ni kuwahamasisha wanamuziki wajiunge na makundi rasmi kama mtandao wa wanamuziki, mifuko ya hifadhi ya jamii kama PSPF , NSSF pamoja na vikundi vya mtandaoni kama Kavasha group Tz ili kujiwekea akiba na pia kujirasimisha kwa ajili ya kurahisisha mambo mbalimbali ya kimaisha.

  "Katoa wito kwa niaba ya kundi la Kavasha Group Tz kuwa linashauri familia ya muziki wa dansi nchini ni waimarishe Umoja na mshikamano ambavyo vitawafanya iwe rahisi kushirikiana na kuwa na nguvu moja katika masuala mbalimbali,"alisema Paschal.

  Gama kwa sasa hana bendi amepumzika kutokana na maradhi ila aliwahi kupita bendi za Mchinga sound, Double M. Sound, Twanga Pepeta na nyinginezo.
  Katika George Gama, pembeni kulia katibu wa Kavasha John Shekwavi na kushoto Mweka Hazina Tabu Mambosasa.

  0 0

  NA VICTOR  MASANGU, RUFIJI.

  BAADHI ya wakinamama wajawazito wanaoishi katika vijiji vya  Mbunju na Mbambe vilivyopo kata ya Mkongo. Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani kwa sasa wanakabiliwa na changamoto ya muda mrefu ya kujifungulia wakiwa  njiani kutokana na kuwepo kwa umbali mrefu kutoka makazi wanayoishi hadi kufika katika zahanati au  kituo cha afya kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

  Wakinamama hao wametoa kilio chao wakati walipotembelewa na mbunge wa jimbo la Rufiji ikiwa ni moja ya ziara yake ya kikazi yenye  lengo la kuweza kusikiliza changamoto  mbali mbali zinazowakabili wananchi wake  pamoja na  kero zao  ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi na kuweka mikakati ya kuleta chachu ya maendeleo.

  Zarau Kiambwe  Tabia Athumani,pamoja na Suzan Masela  ni miongoni mwa wakinamama hao wanaokabiliwa na changamoto hiyo,walisema  wakati mwingine wanapata wakati mgumu hususan nyakati za usiku kutokana na kukosa usafiri hivyo kuwalazimu kujifungulia njiani hali ambayo inahatarisha uhai wa kupopteza maisha yao ukizingatia na gharama za usafiri wa piki piki ni kubwa hivyo wanashindwa kuzimudu kutoka na kutokuwa na kipato chochote.

  Aidha wakinamama hao wamemuomba Mbunge wa jimbo hilo la Rufiji kwa kushirikianana serikali ya awamu ya tano kuliingilia kati suala hilo ili kuweza kuwasaidia wananchi kwa  kuwajengeaa  zahanati pamoja na vituo vya afya vilivyvyo karibu na maeneo wanayoishi ili kuweza kupata huduma ya matibatu kwa urahisi bila ya  usumbufu.

   Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mbunju na Mbambe wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuwatembelea kwa ajili ya kuweza kubaini changamoto mbali mbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.(PICHA NA VICTOR MASANGU).
   Mbunge wa jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akizungumza na baadhi ya wanakijiji hicho kwa ajili ya kuweza kujadili kero zinazowakabili.
   Mbunge wa Rufiji akifurahia jambo baada ya mzee maarufu kijijini hapo kumpa pongezi za dhati kwa kuhudi zake anazozifanya katika kuwataumikia wananchi wa jimbo hilo.

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohamed Mchengerwa akifungua kongamano la siku mbili la kitaifa la msaada wa kisheria kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani linalofanyika mjini Dodoma.

  KITENDO cha jeshi la polisi kuwaweka ndani mahabusu zaidi ya saa 24 bila kuwapeleka mahakamani au kuwapa dhamana ni ukiukwaji wa sheria na uvunjifu wa ,katiba ya nchi.Hayo yalisemwana leo Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohamed Mchengerwa alipokuwa akifungua kongamano la siku mbili la kitaifa la msaada wa kisheria kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani.

  “Ni kinyume cha sheria kuweka watu ndani zaidi ya muda uliwekwa kisheria. Lakini watanzania wengi hawajua hili…hii inatokana na uelewa finyu wa naswala ya kisheria,” alisema Mchemgerwa, wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo liloandaliwa na Shirika la Legal Services Facility (LSF).
  Alisema wapo watu ambao wanakutana na matatizo mbalimbali pamoja na kuwekwa ndani bila ya makosa kutokana na kutokujua sheria.

  Mchengerwa alisema watu wengi hawajui kama kuna dhamana ya polisi ambapo mtuhumiwa hatakiwi kukaa mahabusu zaidi ya saa 24 bila kupelekwa mahakamani au kupewa dhamana.Katika kongamano hilo,Mchengerwa alisema watoa msaada wa kisheria wanatakiwa kutoa msaada huo katika kila wilaya hususani maeneo ya mjini na vijijini.

  "Wapo watu ambao wako gerezani na hawana kosa lakini kutokana na tatizo la uelewa mdogo wa kisheria wamekuwa wakifungwa.
  Abdullkarim Saidi, mmoja watoa msaada wa kisheria kutoka Zanzibar akizungumza kwa niaba ya wasaidizi wa kisheria wa visiwani Zanzibar.

  "Jamii bado haijui kama kuna dhamana ya polisi pia ni kosa la kisheria kumweka mahabusu mtuhumiwa zaidi ya saa24 bila kumpeleka mahakamani au kumpatia dhamana"alieleza.

  Aliwataja wasaidizi wa kisheria kama nguzo muhimu ya kuwasaidia kuelemisha watanzania kuhusu maswala haya ya kisheria na jinsi ya kupata haki zao pindi wanapopatwa na matatizo mbalimbali ya kisheria.

  Kwa upande wake mmoja wa watoa msaada wa kisheria kutoka Zanzibar, Abdullkarim Saidi alisema licha ya kazi kubwa wanayofanya ya kutoa msaada wa kisheria, wasaidizi wa kisheria nchini bado wanakabiliwa na changamoto nyingi.
  Washiriki wa Kongamano la Kitaifa la Wasaidizi wa Kisheria walioshiriki kongamano hilo linalomalizika mjini Dodoma leo.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


    Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO. Geita 


  Shirika la Plan International limetoa rai kwa Serikali kuanzisha Idara ya Kazi katika maeneo ya migodi ili ishirikiane na wachimbaji wa madini kuhakikisha tatizo la ajira kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 18 linakoma.

  Hayo yamesemwa leo mkoani Geita na Mratibu wa Mradi wa Uondoaji Ajira Hatarishi na Vitendo vya Ukatili kwa Watoto wa shirika hilo, Maxmillian Kitigwa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya changamoto zinazoukabili mradi huo.

  Kitigwa amesema kuwa katika Mkoa huo kuna changamoto nyingi zinazowakabili watoto lakini kukosekana kwa Idara ya Kazi katika maeneo ya migodi kunasababisha uvunjwaji mkubwa wa haki za watoto kwa kuwa watoto wengi wanakimbilia kufanya shughuli mbalimbali katika maeneo hayo ili kujipatia kipato.

  ”Sasa hivi Geita imeshakuwa Mkoa, na mkoa huu umezungukwa na migodi mikubwa hivyo Serikali inatakiwa kuweka Idara ya Kazi katika sehemu hizi ili kuzuia ajira za watoto pamoja na kukomesha unyanyaswaji unaofanywa kwa baadhi ya watu wanaofanya kazi huko”, alisema Kitigwa.
  Meneja wa Miradi wa Shirika la Plan International - Geita, Gratian Kweyamba akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya malengo ya Mradi wa Uondoaji Ajira Hatarishi na Vitendo vya Ukatili kwa Watoto, kulia ni Mratibu wa Mradi huo, Maxmillian Kitigwa. Mradi huu wa miaka mitatu unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), unaratibiwa na Shirika la Plan International na kutekelezwa katika Wilaya 3 za Mkoa wa Geita.


older | 1 | .... | 1405 | 1406 | (Page 1407) | 1408 | 1409 | .... | 3285 | newer